Wanafunzi waliookoka wanafeli mitihani?

Bwana Yesu Asifiwe watumishi, mimi nina swali kidogo linanitatiza hivi huku kufeli kwa wanafunzi wengi waliookoka je ni kusudi la Mungu? Kwa sababu watumishi hawa wamekuwa wakifanya kweli kazi ya Mungu lakini mwishoni hufeli masomo yao nashindwa kuelewa kipi ni kipi!!

Christopher

Advertisements

14 thoughts on “Wanafunzi waliookoka wanafeli mitihani?

 1. Nimevutika kuchangangia mada hii, kwa vile mie ni mwalimu na nimeokoka, kuna mwanafunzi mmoja aliandika kwenye karatasi yake ya mtihani ” mungu ibariki kazi ya mikono yangu” na majibu aliyoyaandika kwenye mtihani hakustahili hata 10 chimi ya 100, nikajiuliza kweli mungu anabariki kazi ya mtu isiyokuwa na matunda.
  Yesu alipokuwa na njaa, aliuona mti uliokuwa na dalili ya kuwa na matunda, lakini alipousogelea aliona hakuna matnda yoyote, akasema mti ukatwe kwa nini unaiharibu ardhi, sababu ulitegemewa kuwa na matunda na haukuwa na matunda, wanafunzi wakamwambia acha tuutilie mbolea, tuupalilie tuone kama mwakani hatutapata kitu, tutaukata, sijui kilichotokea, nadhani kama hakukuwa na matunda ulikatwa. Unasemaje mpendwa, ambaye huzingatii masomo, na unategemea mungu akubariki, itawezekana?
  Nampenda mhubiri mmoja wa Marekani Joyce Mayer, anasema fanya unachoweza, na mungu atafanya pale ambapo huwezi, soma, jifunze kwa bidii, kisha omba upendeleo na mazingira ya kukuwezesha kufaulu na sio vinginevyo.

  Wanafunzi darasani pia wanatofautiana kiuwezo wa akili, kuna wenye IQ kubwa, ambao wanaweza kuingia tu darasani, kumsikiliza mwalimu na wakajibu mitihani yao vizuri na wakapata alama nzuri sana, na kuna wale ambao IQ zao sio kubwa sana, ili wafaulu inabidi watie bidii kwa kweli, wasikilize kwa makini darasani, usome vitabu mara 3 na uende discussion ndio uipate concepts zifundishwazo, ili wafaulu mitihani yao.

  Kama wewe ni mpendwa na unaujua uwezo wako wa akili, muombe roho mt akupe ujasiri wa kuwaambia wapendwa wenzako wanaotaka kila mara ufanye shughuli zitazokupa muda mdogo wa kusoma, wakuelewe tatizo lako ni lipi na unahitaji msaada gani toka kwao, wa kuelewa tatizo lako, kukuombea na kukupa muda wa kushgughulikia masuala ya shule.

  faida ya kujibidiisha kimasomo ni hii, wazungu wanasema at the end of the day, usipojisghulisha na shughuli zilizokuleta shuleni, ukifeli, utarudi nyumbani, uhakika wa kupata kazi nzuri ya kukuwezesha kuwa na maisha mazuri wewe na familia yako, unaukata,
  so be careful, huo sio mpango wa mungu ufeli mtihani.
  Blessings
  Greta

 2. Nianze kwa kukataa kuwa ni mapenzi ya Mungu waliookoka wafeli mitihani.halafu nitafafanua
  baadaye ni kwa nini wanajibidiisha kwa Mungu na kufeli.

  kwa nini wanafeli.
  1.kuvunja kiburi ndani ya mtu kuwa ana akili sana,hii nitatolea mfano wangu mwenyewe baada ya kuwa nashika nafasi za juu darasani toka shule za msingi na sekondari,ikizingatiwa nilisoma shule zenye ushindani mkubwa sana darasani na ni mara chache kukuta ziko out ya kumi bora kwenye matokeo kitaifa(kibaha na Tabora boys).nilifikiri ninaakili sana.nikiwa kidato cha tano niliokoka bado niliendelea kuwa juu masomoni,lakini ktk hali isiyoya kawaida mtihani wangu wa mwisho kwenye somo ambalo nilikuwa nakuwa wa kwanza mpaka kumaliza form six ndo nilipata alama za chini kabisa. kwa nini nilifanya vibaya.
  a.ili Mungu anidhihirishie pasipo yeye hakuna mtu anayeweza kujiona yeye ana akili sana,ili utukufu ubaki kwake daima.
  b.nilikuwa ndo nafanya mtihani unaonielekeza nitakwenda kusomea kazi ipi chuo kikuu,kumbe kozi niliyoiazimia siyo ile aliyoniitia Mungu,kuliko ningeenda kupoteza miaka yangu ya bure nisiifanye hiyo kazi.baadaye nilikwenda kusoma mambo mengine tofauti ambayo yananifanya nalipwa pesa nyingi hata ninge kuwa na elimu ya juu sana kwenye kozi niliyotaka kuisoma mwanzo nisingezipata,hivyo Mungu anaamua kukufelisha ili uelekee njia anayoitaka.

  2.sababu nyingine ni majaribu ya Mungu kabla ya kuwainua zaidi, kumbuka Mungu anapotupitisha kwenye majaribu ni kutaka kuyajua yaliyomo moyoni mwetu hasa baada ya kuonekana Mungu ametuacha ili atutendee mema mwisho wetu mfano nina rafiki yangu aliyepata div.0.form six alimtumikia Mungu kwa uaminifu lakini sasa ni afisa mkubwa sana magereza pamoja na ziro.

  mimi baada ya kushindwa kufanya vizuri sana form six tofauti na matarajio yangu maana nilipata div.two na nilitaka one, chuo nilipokwenda nilitumia muda mwingi kumuomba Mungu aniinue kwenye masomo tofauti na mwanzo nilipojiona ninauwezo wa kusoma mwenyewe,pia nilikuwa kiongozi wa maombi wakati mwingi tulitumia muda mwingi kuwaombe wanafunzi wenye mapepo na huduma zingine lakini ndo nilikuwa best academic kwa muda wote wa miaka minne wa kozi niliyokuwa nasoma.

  3.kutokusoma kwa bidii na kumsikiliza Rohomt.anapokuongoza neno linasema utakapoisikiliza kwa bidii sauti yangu na kutii ndipo utafanikiwa sana,wakati mwingi wakati nikisoma chuo Roho aliniongoza kusoma sehemu zilizokuja kwenye mitihani,wakati moja alinizuia nisisome nilikuwa naenda kufanya mtihani mmoja nilianza kukemea nilijua ni hila za shetani lakini baadaye nikaamua kulala siku hiyo nilipokwenda kwenye mtihani ulikuwa rahisi Mungu hakuona sababu ya mimi kukesha.

  4.watu wengi wana ombea kazi ya Mungu bila kuombea masomo yao mpaka Mungu awahakikishie kuwa watafanya vizuri,mie kabla ya mhula kuanza nilikuwa naombea masomo yangu na hapo nilimuomba Mungu kama nataka kuwa wa kwanza ananionyesha hata kabla haujaanza,yeye hutangaza mwisho wa jambo tangu mwanzo.wakati moja nilikwenda nchi ya nje kwa masomo nilikuwa najiandaa kufanya presentation,Mungu alinionyesha usiku vitu vya kupresent na kweli ilifana mno.

  Maneno ya Mungu yako wazi kuwa tutakuwa vichwa ukiyatendea kazi lazima yatimie na pia neno linasema yeye ana nguvu katika uwezo wa fahamu.

 3. Nadhani aliyetoa mada ailikuwa na nia njema ya kufundisha na kukumbusha mambo fulani ambayo kimsingi ni ya kuyatilia mkazo kwenye imani zetu kwa Kristo,
  naamini Mungu ni muweza wa yote na yeyey ni baba wa kila jambo, hivyo kama tutamtumikia kwa uaminifu hata mwisho hakika atatuvisha taji.
  Kuna tofauti ya Mtu kusema ameokoka na mambo yake binafsi anayoyafanya. Sitaki kuhukumu ila wengi wetu tunachukua fellowship au mikusanyiko ya waamini kama mahali pa kuficha uovu na maovu badala ya kuwa mahali pa kutakaswa na yale maovu. sasa kinachotukitukuta ni kuwa, hatufanyi Utumishi wetu kwa uaminifu, kutokana na sababu hiyo wengi tunalipwa sawa na matendo yetu na huduma zetu tuwapo vyuoni.
  Aidha, mimi naamini Mkristo anayemtumikia Mungu anajua Mungu wetu ni wa Utaratibu na anaamini kuheshimu Mungu na kuheshimu Mamlaka zilizowekwa. Vyuo navyo ni Mamlaka iliyowekwa na mitihani ile ni ya Mamlaka, sasa kama huwezi kuheshimu utaratibu ambao Mungu amekupeleka pale kwa makusudui ya Utukufu wake, elewa utakuwa hujamheshimu Mungu wako huo ndio uwazi.
  Nawashauri wanafunzi wa vyuo waliookoka kuelewa kuwa Uwepo wao huko ni Utumishi tosha, ambao una makusudi ya kuutukuza UFALME WA MUNGU. Cha msingi ni kutobweteka na kuwa watu wa kudumu kuomba Ulinzi na Maarifa ya kukabiliana na changamoto za masomo, waelewe kuwa Ibilisi naye yupo karibu akiwatafuta ili wafeli mitihani yao kwa maudhui ya kurudisha Nyuma kazi ya Mungu.

 4. Ni kweli waliookoka wanafeli na kama ni swala la ushahidi lipo kabisa.
  Kitu cha msingi ambacho watu wengi hawajui au wanakichukulia kimakosa ni pale wanapochukulia kuwa as so long mtu ameokoka basi atashinda na atakuwa kichwa kwa kila, kitu ambacho si kweli na hii inatokana na sababu nying ambazo zinahitaji makala kuiandika.
  Wapendwa watashinda sana kwenye mambo ya kiroho kama ulivo wito wao, ila kwa maswala ya elimu na maswala ya kilimwengu watafanikiwa kwa wastani tu. Na endapo mtu atajaribu kuendana nayo yote kwa usawa lazima kuna sehemu moja atashindwa.

 5. Napinga kuwa waliokoka wanafeli chuo kikuu na sijui umefanyia wapi utafiti wako na umetumia njia gani kufanya utafiti maana mbona wapo wengi ambao wameokoka na wamemaliza vizuri.

 6. SABABU ZA KUFELI KWA WAPENDWA ZIPO NYINGI KAMA ZILIVOAINISHWA HAPO JUU! ILA NAPENDA KUENDELEZA ORODHA HIYO KUTOKANA NA UZOEFU NILIONAO

  SABABU YA(1): Wapendwa wengi wanapotoshwa na mistari mbalimbali ya biblia inayotumika vibaya kuhalalisha au kutohalalisha juhudi zao za masomo.

  SABABU YA(2): Kufaulu kwa mwanafunzi kunategemea vitu vingi ila baaadhi ya vitu hivyo ni asili ya uwezo wa uwelewa wa mtu huyo na juhudi binafsi.

  SABABU YA(3): Kushindwa kubalansi na kupata utofauti kati ya Elimu ya Mungu na Elimu Dunia

 7. Kanuni ya kawaida ya kufaulu mitihani ni kusoma. Unaposoma mkabidhi Mungu masomo yako kama ambavyo mfanyakazi, mkulima, nk anapaswa kumkabidhi Mungu shughuli zake hizo. Mengine mwachie Mungu atakupigania. Sijapata kusikia ushuhuda kuwa mtu alikuwa anamtumikia Mungu, hasomi kabisa, halafu akafaulu mitihani yake. Kama yupo, na ajitokeze sasa. Cha msingi wengine wameshakitaja: balance.

 8. Sisi tuliosoma kidogo mambo ya ufundi,kanuni mojawapo ya sayansi inasema, MLINGANYO UNAPASWA ULETE JIBU SIFURI! Nimekuelewa vizuri MLIGO,watu wengi kwa uvivu katika kuwajibika na jambo,hulalia kuliko laini,na huko walikolalia hawatekelezi yahusuyo huko kwa uaminifu,matokeo kotekote wanakosa!

 9. Wewe umenikumbusha kitu cha zamani sana Ya kuwa mtu AKIOKOKA anakuwa MASKINI !
  Sasa ukweli nikuwa ianategemea SANA MAWAZO YA MUHUSIKA

  Akiwaza sana kwenda mbinguni na kufikia hatua ya kutofanya KAZI lazima awe maskini !
  Sasa wanafunzi pia wapo SIO.Masaa 24 anaweza wokovu na vipindi vya masomo anasahau LAZIMA MAVUNO APATE.Maana kila mtu apandacho atavuna !Na hii ni dhambi maana uafanyia mchezo gharama zinazolipwa na wazazi/walezi.Usitegemee sana kuuna ufalme wa MUNGU

 10. Mimi sioni kama wanafunzi waliokoka wanatatizo lolote wasifanikiwe kitaaluma.Ninacho jua anaye mtumikia Mungu aliye hai atapiganiwa katika masomo pia.Vinginevyo sio yule Mungu wa Israel ambaye hapingani na Neno lake.Pia ninacho jua kingine ni swala balance ya mambo yote mawili yaani Mungu-masomo.Mizani ikiegemea upande mmoja lazima utapata matokeo hasi.Ninayo mifano ya watu ‘wanaobalance’ mambo yao na wanaongoza madarasani kwao hata sasa!

 11. ila simaanishi na wale waliokuwa chuo wachukulie hiki kitu vibaya, kama mpo chuo msiache kumtumkia Mungu kaa vizuri na Mungu katika maombi na kumuuliza uelekeo anaotaka uende au kuufuata usije ukaingia mwenyewe mwenyewe, Na mimi Niliweka nadhiri, nikamwambia Mungu utakaponisaidia kumaliza degree yangu ya sheria vizuri na kufaulu vizuri basi hii Degree nitakupa wewe, na kweli Degree yangu ya sheria nimempa Mungu siyo ya Kwangu kwasababu hiyo siweze kuitumia kufanya kazi yoyote ambayo mimi ninajisikia lazima niende katika pattern ambayo Mungu anaitaka, Kuna wakati nilianza kuwa na self ambitions bila kuangalia kusudi na mapemzi ya Mungu, nikawa katika taasisi kama TRA makao makuu Dar idara ya sheria, nikaondoka hapo, nikawa katika Shirika la Umeme Tanzania( Tanesco) makao makuu Dar, nikaondoka hapo, kuna watu wakanitumia e-mail wakawa wanataka nifanye nao kazi na wakaniambia na mshahara ambao ulikuwa unafikia shillingi milioni mbili kwa mwezi, nikaa na Mungu na Roho Mtakatifu akanisemesha nisichukue hiyo kazi kwasababu kuna mambo yamefichika katika hiyo kazi, wale watu walikuwa na nia tofauti. Kuna wakati napigiwa simu na kuulizwa na maafisa rasilimali watu ktoka katika shirika la Umeme( Tanesco) wakaniuliza kama nina kazi, na mimi huwa kuna kitu ninawambia, kabla sijaokoka nilikuwa na ambitions nyingi kwa kweli ambazo kwa kweli ningezitekeleza tu kwa gharama yoyote, nilikuwa ambatious kuja kufanya kazi umoja wa mataifa UN, na nilitengeneza connection kubwa sana, na watu nje ya Tanzania, nikapewa na nafasi ya kusoma masomo ya BA katika uhusiano wa kimataifa na mambo ya diplomasia katika chuo kikuu kimoja Swiss,Geneva, na wazazi walikuwa tayari kunisomesha kwa gharama yoyote, nilihadiwa kusoma katika vyuo vikuu kenya, kwa hiyo nikiwa ambitious person, lakini kwa kweli nimeliona kusudi la Mungu juu yangu na picha yake ipo wazi kabisa mbele zangu, ninakimbia mbio zote kuelekea katika hilo kusudi, ndani ya hilo kusudi nimeona mambo mazuri sana na mpango mzuri sana wa Mungu juu yangu. Ninajua Mungu ataniinua sana kuelekea juu sana. Nitakuja kuwa mhimili na nguzo Muhimu ya ufalme wa Mungu katika taifa la Tanzania. Kwahiyo ninawatia moyo wanafunzi, wakae katika kusoma kwa bidii na zaidi sana wautafute ufalme wa Mbinguni na haki yake. Watu wengi sana lile andiko linalosema “mtakuwa vichwa wala hamtakuwa mikia” wamelichukua vibaya, anaposema mtakuwa vichwa hana maana ya kuwa best na kuwa na akili academically, kwasababu wapo wasomi Tanzania, maprofesa wa uchumi na wengine wamebobea katika masuala ya utawala wa Fedha, lakini nchi inaonekana kama imekosa kitu fulani na inahitaji sana kitu fulani. Nchi imeshindwa kusogea, anaposema matakuwa vichwa ina maana mtakuwa viongozi, mtakuwa creators, mtakuwa innovators, mtakuwa inventors wenye hekima na maarifa katika mambo mbalimbali. katika uchumi,katika mipango na utekelezaji wake, mkia kazi yake ni kufuata, kichwa kinaongoza, Kazi yetu kama vichwa ni kuonyesha direction na utekelezaji wa mambo mbalimbali, mipango ya miaka kumi inayokuja, miaka miaka 15 inayokuja, sisi ni kuonyesha direction, kuna na mambo mapya na kanuni mpya zitokazo katika hazina ya maarifa na hekima, ujuzi na ufahamu ambao Mungu ametupa katika mambo yote, Soma habari za Daniel wakati yupo babeli, tena sisi ni zaidi ya Daniel kwa kuwa tuna Yesu Kristo ambaye hazina zote za maarifa, ujuzi, hekima na ufahamu wote upo ndani yake na sisi tupo ndani ya Yesu.

 12. Ninakumbuka wakati niko Chuo kikuu miaka ya 2005, kwa kweli nilikuwa natumia muda wangu hasa katika kuhubiri kwa wanafunzi wa shule za secondary, kila mara nilikuwa napata mialiko, mara nyingine kwenye makanisa, muda niwapo chuo nilikuwa napita bweni hadi bweni kwa wavulana na wasichana, kila mlango nikishudia habari za Yesu, niliutumia muda wangu kwa maombi, kila ijumaa tulikuwa na maombi kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi na mbili alfajiri. Nilikuwa na maombi yangu mwenyewe kila siku kwa muda usio pungua masaa mawili, asubuhi, mchana na jioni mahali pa utulivu sana katika Chuo kikuu nilichokuwa nasoma, nilienda katika vijiji vya kuhubiri injili na kulala huko huko.

  Kwa kweli Mungu alionekana kwa jinsi ya pekee sana, Nakumbuka mwaka 2006 Mwalimu Christopher Mwakasege alikuwa na semina ya siku nne pale Iringa mjini, na mimi nilikuwa katika timu ya kuombea semina, kuna wakati nilikuwa nakosa vipindi chuoni kwasababu nina zamu ya kuombea semina. Kwa kweli wakati ule Mungu alionekana sana pale chuoni, kupitia watu tuliokoka katika fellowship mbalimbali. Na tulipomaliza na kuondoka chuo mwaka 2008 kwa kweli tuliacha alama isiyofutika na kumbukumbu isiyosahaulika yaani ” legacy” hii ni kwasababu tu tuliamua kulitumikia kusudi la Mungu pale chuoni na Mungu alionekana pia katika masomo yetu na kututetea, lakini pia tulikuwa na bidii ya kusoma na kujituma sana darasani, tukaweza kuacha legacy. Mwaka jana nilienda pale chuoni kwa mara ya kwanza toka nimalize, nikakutana na wachungaji wa KKKT waliokuwa wanasomea masomo ya Theology kwa miaka 5 ambao niliwacha wakiendelea na masomo, wakaniambia kiyu hiki ” hatujui kama ulikuwa ni mpango wa Mungu kuwainua na kuwaleta chuoni na kisha mkaondoka kwasababu mlifanya kazi wakati mpo, mmeondoka na kuna kitu pia kimeondoka. Nilisikitika sana kwa maneno yale, kwasababu wakati tumeondoka tuliendelea kusikia habari zetu zikitajwa na wanafunzi ambao walikuja badala yetu, nikajiuliza hii legacy tuliyoiacha imeishia wapi? na kwa kweli Mungu aliniambia na kutathmini kazi niliyoifanya na mahali ambao upungufu ulikuwapo, Hata sasa kwa kweli ninamuomba sana Mungu mahali pale ninapoelekea katika kusudi lake kubwa ambalo nimekwisha kuliona niweze kutumika kwa kiwango cha juu sana, na hii itaniwezesha kuacha alama au legacy kwa vizazi vingi vinavyokuja.

 13. Una uhakika? Kwani waliofika na kumaliza vyuo vikuu ni wapagani peke yake? Na je hivi wapagani wanafaulu tu hakuna wanaofeli? Mpokee Yesu mapema kaka Yohana 8:44, Waebrania 12:14

 14. Kama hujisomei huwezi kupasi hata kama umeokoka.

  Hii ni kanuni ya Mungu.

  Kuna majira na makusudi katika kila jambo duniani. Mungu ameweka majira ya kusoma na majira ya kazi ya Mungu. KWa lugha nyingine Zingatia “major” na “minors” Yaani majira ya mambo ya msingi (Priorities) na mambo ya ziada “Extra curricular activities”. Kwa kuwa unapokuwa chuoni ni majira ya kutafuta elimu hii ndio “Major” yako. Kazi ya Mungu kwa wakati huu ni “extra curricular”. Ni vizuri kutumia muda wako mwingi kusoma na muda mchache kwa ajili ya huduma.

  Hosea 4: 6
  my people are destroyed from lack of knowledge.

  Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s