Chanzo Cha Matatizo ni shetani!

Mara nyingi watu hawajui kama ni Mungu au ni shetani anayesababisha mambo mabaya yatokee.Huwa wanasema sawa pengine Bwana anajaribu kunifundisha kitu fulani!

Ninakumbuka niliwahi kumsikiliza mwinjilisti mmoja miaka mingi iliyopita. alikuwa akihudumu kwenye hema moja kubwa yenye uwezo wa kuketisha watu 20,000 lakini alipoiweka hema yake ilipigwa na kimbunga (Tufani)  na kuangushwa chini.katika mkutano huo watu walitoa sadaka maalumu ili kumsaidia kupata hema nyingine alisema kitu kimoja kidogo tu ambacho kingeweza kuniangusha chini, SIJUI KAMA NI MUNGU AU NI SHETANI AMBAYE AMEIANGUSHA HEMA YANGU.

Mungu hana muda wa kuiangusha hema ya injili! Mungu anapenda kuyasimamisha, Mtu mmoja alisema Mungu alihusika.

Mungu wetu si Mungu wa Dunia hii  2 WAKORINTHO 4:3-4   Inamwita shetani mungu wa Dunia hii  na majanga yanayoipata Dunia siku za leo yanatokana na kuanguka kwa mwanadamu na laana iliyokuwa juu ya Dunia.

Na kwa sababu watu hawaelewi kitu hiki, Ndio maana wanamsingizia Mungu kwa mambo yanayotokea kama AJALI,GHARIKA,TUFANI,MATETEMEKO YA ARDHI, MAFURIKO, MAGONJWA NA VIFO.

Mungu hahusiki katika kuleta mambo haya, wala siye  anayeyaanzisha. Bwana Yesu alikemea mambo mabaya  kama haya ili kumbariki mwanadamu. Yesu alisimama kwenye merikebu na kukemea dhoruba akasema ” NYAMAZA KIMYA”  kama tunavyo soma  ktk Yohana 14:10 Mungu aliyekuwa ndani ya Yesu ndiye  aliyefanya kazi hiyo. Ikiwa ni Mungu aliyesababisha dhoruba basi angekuwa anajipinga kwa kuiamuru itulie.

Ndivyo ilivyokuwa katika uponyaji ambao Yesu alifanya … BABA ALIYE NDANI YANGU NDIYE ANAYEZITENDA KAZI HIZI. Uponyaji wote, miujiza yote kazi alizofanya Yesu ni Mungu aliyezifanya.

Ikiwa MUNGU ndiye mwanzilishi wa magonjwa na maumivu, halafu akaponyesha watu  kupitia Yesu, Basi ingeonyesha kama Mungu anapingana na nafsi yake.

Haiwezi kuwa hivyo kwa sababu YESU alisema   ” NA UFALME UKIFITINIKA JUU YA NAFSI YAKE, UFALME HUO HAUWEZI KUSIMAMA.  NA NYUMBA IKIFITINIKA   JUU YA NAFSI YAKE, NYUMBA HIYO HAIWEZI KUSIMAMA”   Marko 3:24-25

KUPAMBANUA CHANZO

Ni rahisi kugundua mambo yanatokea wapi. BWANA YESU Kristo mwenyewe alitofautisha kazi zake na kazi za shetani  YOHANA 10:10 “Mwivi haji ili aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele”

Katika tukio lingine  ambapo mwanafunzi mmoja alimwambia “UTUONYESHE BABA” YESU AKAJIBU ALIYENIONA MIMI AMEMUONA BABA”  Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake  YOHANA 14:9-10

Kama tukisikiliza Neno la Mungu litatusaidia kuondoa kabisa kuchanganyikiwa kunakosababishwa na kutoelewa ni wapi matatizo yanakotokea.

Wengi wetu, hata hivyo tunashidwa kusoma Neno la Mungu kwa undani kwa sababu tumegubikwa na mawazo ya kidini tuliyofundishwa tangu tulipokuwa watoto.  Tumesikia mambo yasiyotokana na maandiko yakihubiriwa na kusemwa katika maisha yetu yote .

Ukikubali kuingia katika Neno la Mungu mawazo yako yatanyooshwa. Fikiri kulingana na neno la Mungu linavyosema   hata kama ulifundishwa maana tofati ya neno hilo na watu wengine,  JIULIZE WEWE MWENYEWE JE NENO LA MUNGU LINASEMAJE.

Mf. mtu akipanda juu ya nyumba na kuvunjika mguu hawezi kusema ni Mungu aliyenisukuma nikaanguka chini au ni Mungu aliyenivunja mguu. HAPANA  Mungu aliweka sheria ya mvutano ktk Dunia  na mtu huyo alipovunjika akavuna matokeo yake.

Ni kweli kwamba Mungu ndiye aliyeweka nguvu ya uvutano. Lakini hakutarajia yule mtu avunjike mguu wake. Hakuwa anatarajia kuanguka kwake. Huyu mtu alianguka kwa bahati mbaya au kwa kutokujali!

Sasa wakati mambo fulani yanapotokea katika maisha kama vile MAGONJWA, MISIBA,nk na watu wakasema ”’ Mungu ndiye aliyefanya haya,  wanakosea . Si Mungu aliyesababisha. Yametendeka kwa sababu mwanadamu alitenda dhambi.

Siyo lazima iwe yule aliyepata matatizo hayo NDIYE ALIYETENDA DHAMBI.

LAKINI ADAMU ALITENDA DHAMBI—–NA KILA MWANADAMU AKARITHI MATOKEO MABAYA YA DHAMBI YAKE.

Malkia Pamela

Advertisements

6 thoughts on “Chanzo Cha Matatizo ni shetani!

 1. Wapendwa

  Matatizo husababishwa na watu watatu na hutegemeana na aina matatizo:

  1. Shetani

  2. Mungu

  3. Mwanadam

  Wote hawa husababisha matatizo kulingana na sababu au nyakati.

  Tuanze na Shetani:

  Huyu aweza kusababisha matatizo kama vile: Kupagaa mwanadamu kwa mapepo, kuleta magonjwa yasiyopona kabisaa hata ufanyeje, Kuua mtu kwa ajali au njia yoyote ya mauaji, kuchochea tamaa ya macho na kiburi cha mali na uzima.

  Upande wa Mungu:

  Mungu anaweza kusababisha tatizo fulani litokee ili utukufu wake ujidhihishe mbele za wanadamu. Mfano ni pale alipoufanya moyo wa Farao kuwa mugumu kule Misri. Mfano mwingine ni pale alipoleta gharika wakati wa Nuhu. Dunia nzima iliangamia.

  Upande wa mwanadamu:

  Mwanadamu aweza kusababisaha matatizo na yakamrudia yeye mwenyewe akaanza kulaumu Mungu au Shetani lakini kusema ukweli aliyesababisha ni yeye.

  Mfano: Kama umekata miti yote na nyumba yako haijazungukwa na miti kisha kimbunga kikaja kikaezua nyumba yako, wakijilaumu ni wewe siyo Mungu wala ibilisi.

  Kama umezaa watoto wengi kuliko uwezo wako wa kuwatunza na kuwalisha kisha wakashindwa kupata mahitaji ya msingi maishani mwao wakawa vibaka na malaya, wewe ndiye uliyesababisha wawe hivyo.

  Kama umekula sana chakula hadi ukavimbewa tumbo na kuanza kuharisha au kutapika wewe ndiye ujilaumu.

  Kama umelala bila kufunga milango kisha wezi wakaja kuiba kwako kirahisi, aliyesababisha tatizo hilo siyo shetani wala Mungu, ni wewe.

  Milinga.

 2. @John, Mungu hakuumba wala hatendi mambo mabaya kama unavyodai wewe, kwa sababu Mungu Yeye mwenyewe anasema humwazia kila mmoja mambo mema, na kila jambo analotenda ni kwa faida yetu na kuhakikisha kuwa tunakoelekea ni pema. Kwa sababu Mungu ni haki, ameweka sheria rahisi na kuonya kwamba kila jambo lina matunda/madhara yake, kwa mfano ukila chakula kichafu tarajia kuumwa tumbo. Mitihani “tests” anayotupa Mungu ni kwa ajilia ya kutuimarisha na ina milango ya kutokea.

  Kanuni ya Mungu ni rahisi: Kitu chochote hata kama ni chema usipozingatia kanuni za matumizi yake mwisho wake utaishia kwenye ubaya. Mungu amempa uwezo kila mtu kujua kwamba kila jambo analofanya linaweza kumfanya aishie wapi.

  Tofauti ya matendo ya Mungu na shetani ni kama mashariki na magharibi. Umetoa mfano wa Mungu kumfanya mtu kuwa kipofu, nia Yake sio kumpofusha bali ni kumfanya amrudie, na tena atamfungua tena. Shetani anafanya mambo ya kuangamiza, hapa duniani, halafu bado anataka na mbinguni usiingie.

  Mungu halipi mabaya kwa mabaya, Kisasi anachoongelea Mungu sio cha kibinadamu, bali kwa mfano huwageuza maadui kuwa baraka, marafiki au kugeuza nguvu yao ya uharibifu na kuifanya izae matunda wasiyoyatarajia – hicho ndicho kisasi chenyewe, sio kisasi cha uharibifu. Mungu anaweza kufanya hivyo kwa kila mtu bila kujali matendo yake, LAKINI “ameguarantee” kufanya hivyo kwa wale wanaomtegemea. Kama Mungu angekuwa anaangamiza kila anayetenda mabaya, basi dunia ingekuwa haina mtu hata mmoja maana wote tumetenda maovu.

  Wewe ikiwa humtii wala kumtegemea Mungu, maana yake “umedeclare” kwamba “you are responsible for your behaviour”. Mungu ni mwenye haki, kwa sababu umeamua kutegemea nguvu na akili zako anakupa uhuru. Hapo sasa shetani “anatake advantage”, kwa sababu ana uhakika sasa huna nguvu ya kukulinda, kwa hiyo anakuchezea atakavyo, piga magonjwa, kukuletea ajali, etc.,. Yaani kimsingi unakuwa “potential victim” wa matatizo lukuki. Unakuwa unaenda kwa mwendo wa kubahatisha. Shetani anakuwa anakurushia mtego mmoja baada ya mwingine ili akupate, na wewe kwa sababu una akili wakati mwingine unashtuka unagundua hapa ni shetani, akishaona hivyo anabadilisha mbinu haraka.

  Shetani “hutransform” hata yale mambo machache mazuri unayotenda ili matokeo yake yawe ubaya.

  Maisha ya mkristo yanalindwa na Mungu, halafu bado anakupa uwezo wa kuepuka mitego ya shetani, yaani mkristo anakuwa na “remote sensor”, shetani anapoandaa mtego wa kumwangamiza anaushtukia mapema.

  Mungu hawezi kuleta kwa mfano ajali ya basi ili kuangamiza watu kwa ajili ya kumfundisha mtu mmoja au kumfanya huyo mtu amwabudu, kinachotokea ni watu kukiuka kanuni za kawaida za maisha. Mfano gari bovu, mwendo kasi mkubwa, dereva amelewa. Kwa mambo kama hayo ajali inaweza kutokea. Mungu anaweza kuokoa hata kama uwezekano wa kupona haupo ili kuonyesha ukuu wake au kwa sababu zake mwenyewe, au anaweza asihusike na kufanya jambo lolote lakini “physics” ya tatizo lenyewe ikafanya wengine wapone.

  Hakuna kitu anachofurahia shetani kama yeye kusababisha tatizo halafu akafanikiwa kuwapumbaza watu waone kwamba huo ni mpango wa Mungu, “that is the most powerful and successful Satanic strategy”. Kwa hali hiyo ataendelea kutandika tu.

  Mungu awabariki.

 3. Asante dada Vaileth inaonekana umeelewa nilichosema, kwa nyongeza soma Zaburi 78:34, 49; 1Samweli 2:6-7, 10; Kumbukumbu 32:39 utaona jinsi Mungu anavyotenda kazi chini ya jua. Ni kweli kabisa watu watakaokuonea mtakatifu wa Mungu yeye huwa anateta nao ndiyo maana akasema kisasi ni cha Mungu yaani wewe hutakiwi kulipiza kisasi kwa anayekuonea ila wewe samehe ili yeye (Mungu) atete naye. Kwanini Mungu analeta mabaya kwa mtu? Kila mwanadamu ameumbwa kwa kusudi fulani duniani.Na kusudi kubwa ni kumtolea Mungu ibada. Watu kwa mabilioni yao wanaabudu miungu mingine na hata walokole wana miungu yao. Wengine mungu wao ni tumbo (neno linasema), wengine wamewafanya watoto wao ndiyo miungu (soma habari za nabii Eli jinsi alivyokwenda kubaya baada ya kushindwa kuwaonya watoto wake). Wengine kazi imekuwa ndiyo mungu wao (wako bize hawafanyi ibada), Mungu anahitaji ibada kutoka kwa wanadamu. Katika hali hiyo tutegemee nini? Ndipo Mungu hushusha mapigo mbalimbali (kila mtu kwa pigo lake) wengina magonjwa, ajali, mafarakano katika ndoa, familia, majirani, kazini, mitaani nk. Na hapo Mungu hatafuti watu ila anatafuta mtu mmoja atakayemwabudu. Fikiri Mungu yuko tayari kumfanya mtu awe kipofu ali mradi amgeukie na kumwabudu (mtume Paulo). Na hapo tunajifunza kuwa Mungu aweza kuhakikisha basi linapinduka na kuua watu wengi lakini nia yake ni mtu mmoja anatafutwa amfanyie ibada. Mtu mmoja anapotubu huwa furaha kubwa huko mbinguni. Anafanyaje? Kama ilivyo katika barabara zetu serikali imeweka Traffic Police ili kuhakikisha watumiaji wa barabara wanatimiza sheria za barabara, ndivyo ilivyo katika barabara ya kwenda mbinguni, Mungu ameweka traffic wake ili kuhakikisha kuwa waendao katika njia hiyo wanafuata sheria za barabara ya kwenda mbinguini na hao si wengine ila ni mapepo. Kwanini mapepo? ili ukivunja sheria hapohapo yanakupiga kwa magonjwa, ajali nk. maana yameagizwa na mwenye bararbara. Na katika njia hiyo haijalishi mtu ameokoka au la, watu wote walioumbwa kwa mfano wa Mungu ni wasafiri na wapitaji wote wanaelekea kumoja (kunako hukumu ya Mungu). Mtu anapogundua ya kuwa yeye ni mvunja sheria ya barabara ya kwenda mbinguni ndipo anatubu kisha pepo linafukuzwa maana yeye amesamehewa au ameachiliwa nakosa lake. Pepo hamkamati mtu asiye na kosa hata siku moja.
  Lakini nikuambie dada Vaileth, Zaburi ya 35 siyo nzuri maana inatumiwa sana na watu walioumizwa mioyo yao na wenzao na hivyo wangependa Mungu awapige adui zao haraka sana. Mungu huwa hafanyi hivyo ila yeye huangalia sana nani mwenye haki kati ya wewe na adui yako. Lakini je utajuaje adui yako ametumwa na Mungu ili akutikise kusudi Mungu apate kupima imani yako wewe au kukurudisha unapopotea njia au kukutahadharisha kuwa kesho kuna jambo baya linaenda kukupata? Isaya 54:16 na 41:25 anamwinua mtu, yaani anamtuma mtua je akufanyie mabaya ili wewe ushituke kwanini rafiki yangu amenifanyia hivi? Selemani akasema katika Mhubiri 7:14 “…..siku ya mabaya ufikiri” usikurupuke kugombana na mtu aliyekuumiza wala usimlaani moyoni mwako maana hujui nani amemtuma kufanya hayo. Kwa hiyo Zaburi hiyo uitumie kwa ufahamu sana maana inaweza ikakugeuka kwakuwa ukimpiga aliyetumwa maana yake unampiga aliyemtuma. Na kama ni Mungu ndiye aliyemtuma maana yake utakuwa unampiga Mungu na hakuna aliyewahi kupigana na Mungu akashinda. ZAIDI KUMBUKA KUWA MUNGU NDIYE ALIYEUMBA SHETANI NA SHETANI HAJAWAHI KUUMBA UBAYA ILA AMEPEWA TU. YEYE MUNGU AMEUMBA VITU VYOTE VYEMA NA VIBAYA LAKINI KWAKE VYOTE NI VYEMA MAANA ANAVITUMIA. Ubarikiwe sana.

 4. Bwana Yesu asifiwe,
  Naendelea kujifunza kutoka kwenu wapendwa. Nikisoma Zaburi 35 yote naona kuna matatizo mtu anayoweza kuyapata mfano: Tunapoomba kuwa Bwana teta nao wanaoteta nami ni kwamba Mungu anahusika katika tatizo litakompata yule mtesi wangu na akiisha liruhusu anatoa nafasi ya mtu kutubu na kuomba rehema kisha anaponywa.

  Bado najifunza barikiwa.

 5. Ndugu Malkia soma;
  Mhubiri 7:13-14; Isaya 45:7; Ayubu 1:21; Ayubu 2:10. Mikononi mwa Mungu mna yote mema na mabaya! Niambie kama shetani ana nguvu za kwenda kumnyang’anya Mungu mabaya aliyoshika mikononi mwake? Shetani huwa anatumwa tu na Mungu kwenda kufanya (soma habari za Ahabu, Nabii Mikaya na pepo aliyetumwa na Mungu kwenda kumdanganya Ahabu katika 2Nyakati 18:19-22 ….. Soma kuanzia mstari wa kwanza utapata picha kamili ninayokueleza.) Na yeye (shetani) ni mtumishi wa Mungu kama wewe ulivyo mtumishi wa Mungu (Zaburi 119:91). KUMBUKA BIBLIA NI MSITU UKITUMBUKIA HUMO NA USIPOKUWA MWANGALIFU ITAKUMEZA USIFIKE ULIKOKUSUDIA KUFIKA. Ubarikiwe sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s