Imeandikwa…Yakobo 5:13-14

Marko 6:13 “Wakatoa pepo wengi, wakapaka ,afuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza

Yakobo 5:13 “Mtu wa Kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi. Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana, hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa

Bwana Yesu asifiwe, nimekuwa na swali hili muda mrefu kuhusu mafuta tunayopakwa kanisani. Napenda kujifunza zaidi katika hili kutokana na sura tajwa hapo juu. Inaonekana Yesu na wanafunzi wake waliwapaka wagonjwa  mafuta na katika Yakobo 5:14 imeeleza vizuri kwamba  “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana, hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa

Sasa swali langu ni  Je, kama mafuta ni kwa ajili ya wagonjwa mbona ufunuo wa mafuta umekuwa kwa kasi? mtu yeyote anapakwa, na watumishi wengine wanauza mafuta haya ya upako?

Na katika Yakobo 5:13 kuhusu kuombewa, vipi kuhusu kuombewa kwa njia ya simu? kushika redio na Televisheni? Maana Imeandikwa. “Mtu kwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee

Mungu awabariki!

Advertisements

2 thoughts on “Imeandikwa…Yakobo 5:13-14

  1. Hii ndio sababu tunahitaji kujazwa na Roho Mtakatifu na kujifunza Kumjua zaidi, na hatimaye kumfanya wa karibu kuliko chochote au yeyote. Ni Roho wa Mungu peke yake anayeyajua mambo ya Mungu kwa ufasaha na kwa ukubwa usioelezeka ndio maana kila siku kuna ufunuo mpya kwa wale wanaompa nafasi ya kwanza.
    Kabla ya kusoma neno la Mungu tunamhitaji Roho mtakatifu katika akili na fahamu zetu ili tusiyachukue mambo ya Mungu kwa akili za mwilini na kuyatafsiri kwa akili za mwilini (Rumi 2:12 “Nia=Akili”)

  2. Kuna maigizo mengi kwa watu wa Mungu. Mungu atufunulie Mapenzi yake. Aturehemu!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s