Mungu anaangalia Moyo tu?

Kuna makusanyiko ya ibada mbalimbali wanajali mavazi au mwonekano wa nje wa muumini na kama anaonekana tofauti anazuiwa kuingia kanisani, na makusanyiko mengine hawajali. Mfano tuliwahi kujadili suala la mavazi ya akina dada, wakaka waliookoka kuvaa cheni na kutoboa masikio na kuonekana haina madhara kwa mkristo.

Siku hizi fasheni ya kuvaa miwani ya jua, kuvaa kofia na tumia simu kwenye kusanyiko la ibada inaonekana ipo baadhi ya sehemu, Je Mungu anajali haya? Anaangalia Moyo tu?

Advertisements

16 thoughts on “Mungu anaangalia Moyo tu?

 1. Nakubaliana na mengi ambayo watu wa Mungu wametoa. Na kwangu napenda kusema tu ya kwamba “nikivaa gunia/hariri/suti maridadi na viatu vya kiitalia au kimasai kwa ajili ajili ya utukufu wa Mungu na wala si kumkwaza au kumpendeza mtu – tena iwe mahali pake, wakati wake na staha yake, basi hapa Mungu ataangalia vyote “mwili na roho”. Sioni vibaya mtu akijipodoa kwa ajili ya utukufu wa Mungu aonekane kuhukumiwa kwa hilo maana hata Esther, Daudi, Sulemani na wengine walifanya hivyo.
  Miwani ya jua ni kwa ajili ya jua na kama mtu ataivaa kanisani kwa kuwa ana shida ya macho kwa ajili mwanga mkali hapa sioni kosa lake.
  Tusiwe wepesi wa kuwahukumu wengine kwa kuyaona yale ya nje tu. Maana hata nywele za bandia sasa ni mtindo kwa akina mama hata wale waliookoka. Lakini nasema watu wajipambe kwa utukufu wa Mungu. Na kama ni kwa utukufu wa Mungu basi kuna mipaka yake.

 2. Shalom!
  Hekima ya Ki-Mungu yapaswa kutumika katika mambo yote ili tumpendeze Mungu na wanadamu (Luka 2:52). Hatupaswi kuwa makwazo kwa wengine. Jambo lolote ambalo si agizo la Mungu na watu wanalilalamikia maana yake ni kwamba jambo hilo lina makwazo kwa wanaolilalamikia.Iwapo tunakuwa kwazo kwa watu wa Mungu ni kwa nini hukumu isituangukie, maana neno la Mungu limekataza tusiwe kwazo kwa watu wake 2Kor 6:3.

  Matendo ya nje ni ishara ya yale uliyonayo rohoni. Ni matunda yanayoonekana machoni yakifafanua ulichokibeba katika moyo wako. Hakuna mwanadamu awezaye kuujua moyo wa mwanadamu bali atautafsiri moyo wa huyo mwanadamu kwa yale anayoyaona katika mwili wake. Soma Lk 6:43-45 “Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa KILA MTI HUTAMBULIKANA KWA MATUNDA YAKE……….mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu.” Mungu haangalii moyo tu bali na matendo ya nje pia ndiyo sababu hata mfalme wa ninawi alijivika nguo za magunia na kuketi katika majivu ili Mungu asiwaangamize ikiwa ni ishara ya nje ya toba.

  Tena neno la Mungu linatuonya tusifuatishe namna ya dunia hii. Ndugu wapendwa kila jamii inao utaratibu uliokubalika, hivyo hivyo kwa mataifa na kanisa pia. Tukiingiza utaratibu usiokubalika ndani ya kanisa twaweza kudhani kuwa tumesimama kumbe tayari tu maajenti wa shetani.

 3. Mungu anaangalia moyo zaidi maana huko ndiko zitokako chemchem za uzima na za kifo

 4. Shalom!!

  1 Wakorintho 10;23-24
  “Vitu vyote ni halali,” lakini si vitu vyote vilivyo na faida. ‘‘Vitu vyote ni halali,’’ lakini si vyote vinavyojenga. Mtu ye yote asitafute yaliyo yake mwenyewe, bali kila mtu atafute yale yanayowafaa wengine

  Kuna baadhi ya vitu tunatakiwa kuvifanya kwa upendo ili imani za watu zisirudi nyuma, mavazi, ukisasa ambao haumtukuzi Mungu tunatakiwa kuviacha kwa ajili ya usalama na kupunguza makwazo kwa wengine.

  Mbarikiwe

 5. M nionavyo maswala haya ya mavazi na mitazamo ya nje ya moyo(utu wa ndani wa mtu), yanatakiwa kutazamwa na kupatiwa ufumbuzi kwa njia mahsusi zenye mtazamo mpana wa mambo(kibiblia na kistaha-desturi&tamaduni) pia hekima zaidi itumike kuliko jazba na hisia za mtu binafsi.
  Kwa namna hii tunaweza kupata angalau picha ya nini ni sahihi na nini kifanyike.

  UKWELI NI KWAMBA HI MADA NI PANA-KIUCHAMBUZI NA INAHITAJI BUSARA NYINGI KULIKO SHUTUMA. SOMO LAKE LIPO NA NI PANA SANA, Ila atakiwaye kujifunza ni yule mwenye kupenda kujifunza mengi na asiwe na mipaka isiyo ya lazima.

  THANKX!

 6. BIBLIA INANAMBIA “ALAANIWE MTU AVAAE MAVAZI YAMPASAYO MWANAMME NA NA MWANAMME AVAAE MAVAZI YAMPASAYO MWANAMKE”
  Mambo mengine sidhani kama hata kama tutayatatua kwa mijadala tu ila inabidi tutumie akili pia. Mfano ofisi tu hasa za serikali zinakuwa na taratibu zake kwani nyingine kuna baadhi ya mavazi hayaruhusiwi kwa watumishi wake na nyingine urembo wa ajabu ajabu hauruhusiwi na nyingine wamezuia kabisa matumizi ya simu,hiyo yote nikwaajili ya kuleta nidhamu za ofisi. Je kwanini kwenye nyumba za ibada tufanye kawida? UTANDAWAZI UTATUKOSEHA MBINGU kama tuspokumbuka kuwa “WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.Neno la MUNGU hlibadiliki jamani

 7. MUNGU wetu apewesifa watumishi wa Bwana kama neneo la MUNGUlisemavyo usiwe kikwazo mbele za mwenzako mimi ninahisi kulingana na tamaduni zetu na mila zetu si vizuri kufanya hivyo kwenye hema ya kuabudia tena watu waniga praise za nje au watu waliokoka nje wale wenzetu tunatofautiana kimila na hali ya hewa kwa sababu hiyo hutakiwa kuvaa nguo zinazoleta joto plz tufuate protocal za MUNGU mbarikiwe

 8. Kudai kuwa Mungu huangalia moyo tu na sio mwili , je; kwani huo moyo uko wapi ? si ni ndani ya huo mwili? pili ; hiyo ni dalili kwamba mtu anaetetea hoja hiyo amekwisha mzimisha Roho tayari, kwa sababu alipuuzia sauti ya Roho kumuonya kwa makusudi, mwisho Roho hukaa kimya na kumwacha aendelee kujidanganya.Ni matokeo ya kutokumtii RM.

 9. Mungu anaangalia moyo lakini kweli kama mtu unamtafuta Mungu lazima uwe na uchaji kwani hata kanisani kama uko na shida ya ukweli kofia, simu na hayo mengine hayasaidii kwani unakua muhitaji kwa mungu kwani yote ya dunia si kitu. Na ndiyo maana imeandikwa turarue miyoyo yetu na siyo mavazi. tuombe neema ya mungu ituongoze na roho wake ili tuweze kutenda yale yanayompendeza

 10. Maandiko yanabainisha wazi wazi kuwa vinavyoujaza moyo wa mtu ndivyo vimtokavyo. Vinamtoka vipi? Kupitia maneno na matendo yake. Mti mwema hauwezi kutoa matunda (maneno na matendo) maovu. Hali kadhalika mti mwovu hauwezi kutoa matunda mema. Kwa ufupi, Mungu japo anaangalia moyo, anatuonya tuachane na matendo ya mwili kwa kuwa, mwisho wa siku, hayo ya mwili yanabainisha kile kilichojaa moyoni mwa anayeyafanya.

 11. ukweli ni kwamba kama kwenye hazina ya moyo wa mtu kumejaa kumpendeza Mungu,kuna vitu vingine mtu hawezi kuvifanya kwani atajua tu kisichofaa wakati mwingine inakuwa ni sababu ya tofauti ya mahali na mahali,night dress iwe mahali pake, evening dress iwe mahali pake(kwa mfano tu).
  tusisahau pia 2Cor 6:3a inasema wazi,”Tusiwe kwazo la namna yoyote katika jambo lolote,…… ili utumishi wetu usilaumiwe;

 12. Ni utoto au ukaidi eti kusema Mungu anaangalia moyo tu,halafu ukaufanyia mwili kama utakavyo,labada tukubali tu kwamba kwa sasa dunia imeingia kanisani kwa nguvu kiasi kwamba tumechanganyikiwa hatujui lipi linalompendeza Mungu,badala ya kanisa kuivuta dunia dunia ndiyo inalivuta kanisa,tuliookoka lazima tuwe tofauti na dunia kwa vyovyote vile

 13. naungana na wewe dada Magreth. kweli Mungu anaangalia vyote (moyo na mwili. kila tukifanyacho kiwe ni kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu. ni lazima tuwe barua inayosomeka vyema kwa jamii.

 14. BWANA ASIFIWE!Nadhani kama kweli mtu ana nia ya kumuabudu MUNGU hatakuwa na madoido ya ajabu ajabu ktk ibada kwahakika ukija na miwani ya jua tena yamadoido doido na ukavaa kofia ya kushangaza watu kadhaa hasa watoto badala ya kutafakari kilicho mleta ibadani atakuwa akishangaa maajabu yako na tafakari inaondoka,japo niliwahi kugundua wakatifulani nikiwa mjini palikuwepo na madadafulani wao kawaida yao ilikuwa kuchelewa ibada na huingia ibadani na viatu vyenye kelele halafu huanza na kutafuna big g (chingam)sasa huwa wengine ni stail yao ya kiajent wapoteze tafakari ya neno kwa walegwa na wengine nikutojua ukuu wa MUNGU!na kudhani wako ktk fashio show,lakini kama kweli unajiandaa uende ktk ibada mwenyewe utaona tu kwamba vazihili lina stahili, na ndani ya ibada hakuna hatajua na wewe siongonjwa wa macho! miwani ya giza yanini kamahuna hilawewe!?hebu wacha waliokuja kuabudu kwakumaanisha waabudu MUNGU wao wanayemjua uthamani wake.na kama hujui anzakujiuliza je nina wezakuwa miongoni mwa watu wanao poteza tafakari / utulivu ktk ibada au namamimi nisehemu ya ibada (nipokuabudu)
  barikiwa
  by frederick

 15. Shalom watu wa Mungu. Ninavyofahamu Mungu haangalii moyo tu bali pia mwili na ndio maana kwenye 1 Cor 6:19-20 anasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu hovyo tunapaswa kuilinda miili yetu pia…na sio kaufanya tufanyavyo kwa kusema Mungu anaangalia moyo.

  Barikiwa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s