Dk. Mwakyembe atoa ushuhuda kanisani!

Mwakyembe akiwa na Askofu Gwajima

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu atoke India kwa ajili ya matibabu. Dk. Mwakyembe alionekana jana kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa muujiza wa kupona ugonjwa uliokuwa unamsumbua na kusema nguvu za mafisadi zimeshindwa kummaliza.

Alisema kuwa hivi sasa anatarajia kuzunguka kwenye makanisa mbalimbali nchini kutangaza shetani alivyopanga kummaliza lakini Mungu akamsaidia.

Nimepanga kuzunguka kwenye makanisa kumzomea shetani kwamba ameshindwa na kuwashukuru watu wa Mungu kwa maombi yao,” alisema.

Picha na Kapingaz Blog

Dk. Mwakyembe alisindikizwa na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; mbunge wa Kahama James Lembeli (CCM); na Aloyce Kimaro, aliyekuwa mbunge wa Vunjo.

Wabunge hao wote waliongea kuhusu utumishi wao na kuongeza juhudi katika kupambana na kuitetea nchi ya Tanzania pasipo kuogopa.

Advertisements

17 thoughts on “Dk. Mwakyembe atoa ushuhuda kanisani!

 1. MUNGU WA MBINGUNI AENDELEE KUKUTUNZA DR. MWAKYEMBE, HAUTAKUFA BALI UTAISHI SIKU ZOTE NA UTAUSIMULIA MATENDO MAKUU YA MUNGU. TUNAMSHUKURU SANA MUNGU KWA AJILI YAKO. DAMU YA YESU KRISTO INENAYO MEMA IKANENE MEMA JUU YAKO NA KATIKA KILA HATUA UTAKAYOPITA, HEKIMA IZIDIYO IKUFUNIKE NA SHETANI ATAKAPOKUONA AJUE KUWA YUKO MUNG ANAYETUWAZIA MAWAZO YA AMANI KUTUPA TUMAINI SIKU ZETU ZA MWISHO

 2. Nafurahi kumuona Mheshimiwa kagundua kuwa uhai wake upo mikononi mwa Mungu n no one can temper with it,hilo tosha limemfanya kuwa righteous mbele za Mungu na kumfanya shetani aishiwe nguvu ya kuendelea na his dirty plan. Mhe endelea kujikita kwa Yesu zaidi.In Him, life is abanduntly and secured coz He came so that we can have life n life in abandunce.Wen u have God in ur side,mtu wala shetani asikutishe coz watapanga njama na zitawanasa wenyewe coz it is written NO EVIL CAN TOUCH THE SONS N DAUGHTERS OF THE MOST HIGH GOD coz we are operating in the Most high realm where evil is powerless.Mungu akutunze na kukulinda na akufundishe kumjua zaidi

 3. kumshukuru Mungu ni jambo ambalo Mungu analipenda mno, Dr Mwakyembe amelitambua hilo, kwa maana imeandikwa mshukuruni Bwana kwa kila jambo. Mungu akubariki sana Dr na tunazidi kukuombea uweze kupata nguvu zaidi na kurudi kazini. Cha muhimu ni kumshikilia Yesu na kumtegemea kwa kila kitu. barikiwa.

 4. Mhesshimiwa Dr. Mwakyembe, umefanya jambo kubwa la kumnyamazisha shetani, Ayubu alisema maneno ya maana sana wakati anapitia changamoto alisema Ayubu 23:10. “But he knoweth the way that I take, when he hath tried me I shall come forth like Gold” Dr. for this testimony the challenges has been your stepping stone to your destiny. Congrats!!!!

 5. Mungu aendelee kukuponya na hongera sana kwa kutokwenda kwa babu wa loliondo ungeenda kwa babu wa loliondo labda tungesha kusahau maana babu wa loliondo ni mshirikina aliyejificha sana,mpaka uwe na macho ya kiroho vinginevyo utabugia tu kikombe.

 6. Mungu wetu ni Mungu aliye karibu,anaesikia wakati wote…shetani umeona aibu zsako???Asate Mungu kwa kujibu maombi yetu,na ijulikane leo kuwa wewe upo,adui azidi kuaibika katika jina takatifu la Yesu wetu..tunazidi kuwaombea sana viongoz wetu na wabaya wote waache njia zao mbaya wamrudie Mungu kabla hajawaumbua hadharani

 7. Dr Mwakyembe, pole sana. Lakini usijute kwa yaliyokupata, hatuelewi kwa nini ilikutokea hivyo, huenda ni kusudi la Mungu kwa kupitia kwako ili jina lake liinuliwe. Jipe moyo, mwangalie YESU pale msalabani hii ni saa yoko anakwenda kukuinua sasa. AMEN

 8. MUNGU wetu wa mbinguni anastahili sifa na utukufu naye hana mpinzani
  Dr Mwakyembe nasi tunamshukuru MUNGU pamoja nawe na tunakuombea. Amini tu kwani YESU wetu hashindwi jambo lolote

 9. Hawa wachache wenye nia njema ni wengi kuliko wengi wachafu, kwa nini? Wako upande mwamuzi, Mungu.

 10. Mungu akubariki sana Mheshimiwa.God is alwaysgood and faithful to his People..viongozi wengine waige kwako ndipo taifa letu litakapoinuliwa.

 11. mimi naanini Mungu anayo kila jibu la jaribu kwenye maisha yetu, Mhe alijaribiwa ila Mungu amemtetea baada ya kujishusha na kumtumainia. Ni jambo la fahari kumshukuru na kushuhudia ukuu wa Mungu.
  Ombi langu kwa wote, tusimame imara tukiwaombea viongozi wetu hasa Mhe Samweli Sitta kwa kuwa wanaonyesha utumishi wao kwa Jamii na Mungu. na sisi kama wakristo wenye kujua nini maana ya vita vilivyopo kati ya Nuru na Giza tunao wajibu wa kuwaweka mikononi mwa Jehovah na sio kuendelea kushabikia siasa.

  Mungu akuepushie kila ovu lililopangwa kwako Dr Mwakyembe na Mhe Sitta, hakika kazi yenu inalitangaza vyema jina la Kristo

 12. hapo muheshimiwa umechagua lililo jema!.NA WENGINE WAFUATE NYAYO ZAKO,kwa sababu hata wangekutoa msukule kwa ufisadi tungekurudisha tuuu!..AMEN

 13. Ninamjibia! ni ushirikina mtupu, wako wapi waliopata tiba kwake ?, wasimame washuhudie tuone.

 14. Marandu, umemtaja babu wa Loliondo. Kwani alichokuwa anakifanya kilikuwa ni ushirikina?

 15. BWANA YESU Asifiwe!hivi ndivyo ilitakiwa viongozi wawe mstari wambele kushukuru MUNGU na kuomba ndivyotaifa litabarikiwa,Sio kama wakatiule hadi tulionekana wa kwanza duniani kwa ushirikina!Inawezekana sisi na viongozi tuendeleze maombi na kubadilika badala ya kuabudu ushirikina kama wakatiule babu loliondo alipandisha chati nchi yetu tukaonekana niwashirikina zaidi duniani,wacha sasa turudi magotini hadi tuwe wa kwanza duniani kwa maombi viongozi wapate nyazifa kwa maombi!sio ngozi na mifupa ya albino ule niuongo wa shetanitu!Natumia mdahuu kushauri viongozi watakao kuwa wa kwanza ktk maombi kuombewa lazima wapate nafasi wanazo hitaji bila kupingwa hakuna linalo mshinda MUNGU! kwake yote yana wezekana!wote tuige mfano huo wa mwakyembe!
  mbarikiwe
  na Frederick Marandu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s