Je Mungu ana mtu aliyemchagua awe mwenzi wako?

Vijana wengi wamekuwa na maswali kuhusu wenzi watakaowapata..kama Mungu amemchagua mtu kwa ajili yako, Je utamtafutaje huyo mwenzi wako? Au utabaki umkisubiri Mungu amlete kwenye maisha yako? 

Advertisements

12 thoughts on “Je Mungu ana mtu aliyemchagua awe mwenzi wako?

 1. Mlio oana tayari uwanja wenu huuu!! Mwageni shuhuda kwa vijana. Jitokezeni ili kunusuru vijana walio okoka.

  Mungu wetu habadiliki ila wanadamu sisi tunabadililka, Mungu amemuwekea kila mtu mwenzi wa kufanana nae lakini niwa kufanana tabia. Je tabia yako ikibadilika unafikili Mungu bado atamleta yule mwenzi mzuri kwako? kwavyovyote vile wewe utakuwa umesha kengeuka na uko nje ya mpango wa Mungu.

  Kikubwa ni kudumu katika mapenzi ya Mungu huku tukilitazama kusudi lake bila ya kuweka vigezo vinavyo badilika.

  Chako ni chako lakini pia unaweza kukipoteza kutokana na tabia yako na mwenendo wako.

  There is somebody for you!!! keep waiting and praying.

 2. Swali la vijana ni la msingi sana na lina majibu yake. Nataka kukumbusha ndg msomaji habari hii,Mungu alipo muumba mwanadamu ambaye ni Adamu maana ndiye alitangulia kuumbwa kabla ya Eva alisema, “BWANA Mungu akasema,Si vema mtu huyo awe peke yake,nitamfanyia mtu wa kufanana naye” Kwa hiyo ni kweli yuko wa kufanana na wewe na ili Umtambue,Yuko Roho Mtakatifu atakuongoza usiende kwa pupa yeye anajua.

 3. Hapo huwa pana ugumu wake ila Mungu atusaidie kwa kweli ili tusonge mbele katika maisha ya ushindi.

 4. Mungu anakuonesha mtu sahihi suala la kuchagua ni la kwako.Watu wengi sana wanaweza kuwa watu sahihi kwako lakini Mungu ametengeneza kanuni ya mke mmoja mume mmoja. Maana yake kati ya hao wengi wanaoweza kukufaa unatakiwa uchague mmoja tu. .

  Na mara nyingi Mungu anatumia mashauri yetu (our desires) kutupa vitu tunavyotaka alimradi hayo mashauri yetu yawe katika mapenzi yake.

  Yakobo alipewa Rahel kwa sababu alikuwa anampenda kwa vile alikuwa na macho mazuri kuliko dadake Leah (acording to Yakobo) na Mungu hakuona kuwa hiyo ni tamaa mbaya maana yeye ndiye kayaumba hayo macho aliyoyazimikia Yakobo.

  Wapendwa, ningependa kusema kuwa hakuna mtu ambaye yuko “smart” katika kujua vitu vizuri kuliko Mungu,kama unajua ktk akili yako jinsi mwanamke au mwanamume mzuri alivyo basi Mungu anajua hivyo na zaidi.Halaf kwa nini suala la kuchaguliwa na Mungu linakuja kwa habari ya ndoa tu, si atuchagulie hata magari,mavazi,taaluma,n.k!!!!

  Kama Mungu hutuchagulia wenzi hata kama hatuwataki basi yeye sio Baba mzuri mwenye kuwapa zawadi nzuri watoto wake.Kama nataka mwanamke mfupi,mweusi,mwenye macho madogo na miguu ya upinde kwa nini anichagulie mrefu,mweupe, mwenye macho makubwa na Miguu ya bia? sintamfurahia,akinikosea nitamwambia “asingekuwa Mungu kunilazimisha nisingekuoa” duh!!

  Nini huwa kinafanyika basi:Ikitokea umempenda au umependwa na mtu Roho mtakaifu hukushauri kwa kukutia moyo kuwa ni mtu sahihi au kwa kukuonya kuwa huyo si mtu sahihi kwako. Hapo ndipo wengi huwa tunachemsha hasa katika kuelewa ule ushauri wa onyo. Samsoni alishauriwa na wazazi wake kwa habari ya Delila lakini akawagomea;tunajua nini kilimtokea mwishoni.

  Namaliza hivi; sijawahi kuona kwenye biblia mahali Mungu alimchagulia mtu yeyote mwenzi.Na hata kama angekuwa amekuchagulia haina maana kuwa huwezi kukutana na changamoto za ndoa,zenyewe ziko palepale lazima upambane nazo, ulichaguliwa au ulichagua.

 5. Bwana asifiwe na mimi napenda kuwatia moyo wenzangu kuwa tusifanye haraka kukimbilia wenzi amboa Mungu hajatuchagulia kuepuka mateso kwani si mpango wa Mungu ndio maana unakuta mtu anatelekezwa na watoto halafu unahangaika kwa hiyo tusubiri tu mwenzi mema kwani ahadi za Bwana zimewekwa kwa ajili yetu vijana tusiwe na haraka,

 6. Isaya 34:16 “Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome, hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo ,hapana mmoja atakayemkosa mwenzake, kwa maana kinywa chake kimeamuru na roho yake imewakusanya”

  Cha msingi ni subira na kumngoja Bwana kwa wakati ambaye ataamuru…………..
  vijana tusiwe na haraka

 7. MPENDWA NAAMINI HAUJAMBO, KWA KIFUPI MUNGU HAMCHAGULII MTU MWENZA,UNACHAGUA WEWE MWENYEWE, KWA KUTUMIA VIGEZO AMBAVYO YEYE – MUNGU AMEVIWEKA KATIKA NENO LAKE. UKISHA KUCHAGUA, UNAPASWA KUSUBILI MUNGU AKUPE!(AKUKABIDHI)

 8. HAYA,
  NI KWELI KWAMBA WAKATI MUNGU ANARUHUSU MTU AZALIWE, MTU MUME AU MKE, NA BIBLIA INA SEMA KWAMBA, MUNGU AZIJUWA HITAJI ZETU KABLA HATUJA ZIELEZA
  SO, NAWEZA KU SEMA KWAMBA MUNGU MPANGO WAKE JUU YA MWANADAMU NI MPANGO WA AMANI NA SIYO WA LAANA, KWA HIYO MUNGU ANA MTU ALIYE MCHAGUA KUA MWENZI WAKO

  ROLAND

 9. katika hili sijui kama ntakuwa kimwili zaidi ama kimaandiko zaidi ila katika biblia inasema Mungu anawajua walio wake na Mungu anasema atuita sote twende kwake na anasema anawanyeshea mvua walio wake na wasio wake! nataka kusema kwamba mwombe Mungu na pia usome na nyakati

 10. Kwa kujibu swali, naamini Mungu alikwisha mchagua mwenzi wako, kama alivyofanya kwa Isaka, (Mwanzo 24) Ila kila kitu kina wakati wake.
  Sio jambo gumu kwa Mungu, yeye anaweza kukutanisha na mwenzi wako kwa njia yoyote ile. Hana mipaka, na pia kuna njia nyingi anazoweza kutumia ili umjue kuwa huyo ndie. Kila mtu aliyekuwa akimuomba Mungu juu ya mwenza na akampata atakuwa na ushuhuda tofauti na mwingine jinsi gani Mungu alimjibu! Wengine huambiwa live ndani ya mioyo yao huyo ndie. Wengine husikia amani baada ya kumuona kaka au dada fulani, wengine huoteshwa ndoto, wengine huona ishara, unabii, wengine huweka vigezo, nk

  Ndugu mlio ktk ndoa karibuni kutoa shuhuda jinsi Mungu alivyofanya kwenu.

 11. Wapendwa tunahitaji sana Neema ya Mungu katika hili.
  Hii ni changamoto kubwa sana kwetu sisi vijana.
  Wakati mwingine nahisi kama mambo hayaendi kabisa.

 12. NIKWELI KUWA MUNGU ANAMPANGO MZURI KATIKA MAISHA YA VIJANA KWA KUWAPATIA WENZI WAO LAKINI VIJANA WENGI AKIWEMO MIMI HATUJUI JINSI GANI TUTAWAPATA WALE AMBAO MUNGU MWENYEWE AMEWACHAGUA KWA AJILI YETU. JE TUTA WATAMBUAJE? KWA ISHARA ZIPI? NINA OMBA MUNGU ATUPE MACHO YA ROHONI ILITUWEZE KUWAONA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s