Tuyatamani sana mapenzi ya Mungu!

Mapenzi ya Mungu ni nini Kwako? Watu wengi wanatamani mapenzi ya Mungu yatimizwe kwao, lakini wanahangaika kwasababu hawajui mapenzi ya Mungu.

 1. Mungu anamakusudi makubwa kwenye maisha yako!

  Tumeumbwa na Mungu, kwa sura yake, na kwa mapenzi yake. Kama alivyofanya kwa Isaya tangu tumboni mwa mama yake (Isaya 49:1) Yeremia (Yeremia 1:5) na Paulo (Wagalatia 1:15) kwa kusudi maalum, basi pia Mungu ana kusudi maalum na maisha yako.

  Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho -Yeremia 29:11

  Biblia inasema mapenzi ya Mungu ni “mazuri” ya kumpendeza na ukamilifu-Warumi 12:2

 2. Kitu muhimu sana Mungu anachotaka kwetu ni, tuwe na mahusiano na Yeye kupitia Mwanaye, Yesu Kristo. 

  Hili ni zuri na lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu, ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli- 1 Timotheo 2:3-4

 3. Mungu anataka tuwe wanafunzi wa Bwana Yesu 

  Hii ina maanisha kwamba wakristo tuyatafute mapenzi ya Mungu kila siku, bila kujali gharama yake.

  Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate- Luka 9:23

 4. Biblia (kama Neno la Mungu) Itatusaidia kuyajua mapenzi ya Mungu.

  Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu- Zaburi 119:105

 5. Mungu ameahidi kutupa hekima kama tukimuomba (maombi) Amini atakupatia 

  Wakati mwingine tunahitaji kuomba Hekima tuyatambue mapenzi ya Mungu kwetu

  Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei: naye atapewa- Yakobo 1:5

  Katika Wafilipi 4:6, Mungu anatuambia tunaweza kuomba jambo lolote.

 6. Mungu ametupa Roho Mtakatifu kama kiongozi.

  …Atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote- Yohana 16:13a

 7. Fuata ushauri wa watumishi wa Mungu, au watu wa Mungu ambao Mungu amekukutanisha nao kwenye maisha yako.

  Mara nyingi ushauri wa wazazi, mchungaji, kiongozi wa vijana, mwalimu au yeyote mtu mzima anaweza kukushauri na kusaidika kuamua nini Mungu anataka ufanye.

  Njia ya mpumbavu imenyooka machoni pake mwenyewe, Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri- Mithali 12:15

  Pasipo mashauri makusudi hubatilika, Bali kwa wingi wa washauri huthibitika- Mithali 16:22

 8. Neno la Mungu linasema kuna Amani inayopatikana tunapomhusisha Mungu kwenye maisha yetu

  Unapochagua njia mbili ambazo zote ulikuwa ukiomba, wakati mwingine njia mojawapo itakupa amani kamili, hiyo njia yawezekana ni mpango wa Mungu.

  Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima- Isaya 32:17

 9. Inabidi tuweke tumaini letu kwa Mungu, Mapenzi yake yatimizwe kwetu. 

  Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe- Mithali 3:5-6

  Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu, ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu- Wafilipi 1:6

 10. Mungu amempa kila mmoja wetu karama na uwezo tutumie kwenye kazi yake. 

  Siku zote Mungu anawezesha nguvu ya kufanya yale anayokuwezesha kufanya. Kama hauna kipaji fulani, usilazimishe, Mungu hajakuita kufanya hicho kitu. (Soma Warumi 12:6-8, 1 Wakorintho 12:1-11 na Waefeso 4:11-13 kwa karama za rohoni na maelezo yake)

  Kumbuka kwamba mapenzi ya Mungu ni makubwa kwetu sote, Ili Yeye Atukuzwe, Ainuliwe “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” 1 Wakorintho 10:31, Injili na ufalme wa Mungu ukatangazwe kwa wote. Mwanzo 50:20 na Wafilipi 1:12.

  Mungu Awabariki.
Advertisements

One thought on “Tuyatamani sana mapenzi ya Mungu!

 1. Praise God!Somo zuri na fupi linavutia kusomeka linaelimisha na kukumbusha,Pia itasaidia wapo watu wengi wanatamani wawe kama fulani bila kukumbuka vipawa nitofauti pengine chako ni bora kuliko huyo fulani! nimegundua somo likiwa refu sana!wengi hawasomi barikiwa!
  Frederick Marandu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s