Madaktari na Serikali!

Picha na rnw

Ni habari ya kusikitisha kusikia madaktari wanaendelea kugoma, na pia inasikitisha mvutano walionao na serikali pasipo kusawazisha na huduma ikaendelea kwa wagonjwa ili kujali afya ya Wananchi kwanza.

Ni maombi yetu, Mungu awape busara Kamati ya kudumu ya Bunge inayohusika na masuala ya huduma za jamii pamoja na madaktari katika mazungumzo mnayotarajia kufanya.

Pia poleni wote mliodhurika na mgomo huu!!

Advertisements

3 thoughts on “Madaktari na Serikali!

  1. Sometime Majibu ya Mungu kugeuza Nchi hii yanaweza yasiendane saaaana na uzoefu wetu, ufahamu tulionao, njia tunazozijua na thoughts ambazo tungedhani Bwana angepitia ua kuzitumia. Ni kweli tuendelee kuomba but tuombee nini? swali hilo muhimu kwakua Biblia inadokeza tunaomba hatupati kwa kua tunaomba vibaya! Ivyo tunamuomba Mungu adili na madaktari kivip na adili na serikali kivipi, that is critically important, Mimi nafahamu kua madaktari wana utumishi ambao wanadamu wengine hatuuwezi, Kuna namna fulani nature yao ya kibinadamu wa kawaida ife ili wafanye wanayoyafanya, not normal! ivi umeshapata picha utatoka kuchana-chana mtu chumba cha upasuaji au unatoka kutreat maiti chumba cha maiti, halafu saa 7 imefika, unanawa mikono kula lunch then unarudi job hiyo hiyo? au amelazwa mtu anafanya kila kitu hapo kitandani, then nesi anakujakuclear mambo yote au donda kubwa la kansa kulidress kila siku then ukanywe chai? Jesus Christ,nawapenda madaktari na wafanyakazi wote wa tiba za wanadamu mahositalini, ni mwito mkuu na Mungu anawaheshimu, basi tu serikalini ni wanadamu wanamuitaji Mungu haraka sana kuliona hilo, pesa ipo nyingi tu nchi hii kama ikielekezwa ktk mambo yenye tija.

  2. Bwana Yesu apewe sifa wapendwa, wakati kama huu ni sawa na maafa yametokea katika taifa ambapo hata viongozi wote wa serikali wanatakiwa kushughulikia jambo hili mpaka suluhisho lipatikane. Kama tu wakati ambapo huduma ziko kawaida ukienda hospitali za serikali unashtuka je sasa ambapo Madaktari wamegoma itakuwaje?? Kwa mawazo yangu naishauri serikali na viongozi wetu waliangalie jambo hili kwa jicho la tofauti. Pale Misri, wiki iliyopita kulitokea maafa katika uwanja wa mpira na wabunge walikuwa nyumbani kwao, lakini kwa kuona umuhimu wa jambo hili waliitwa haraka kuja kutafuta suluhisho sasa Viongozi wetu wako wapi jamani?? Mbona wengine wako ziarani mikoani kwani wanaokufa si wapiga kura wao?? Nawaombeni viongozi wetu wasitishe mambo mengine yote na wadili na jambo hili. Pia madaktari naomba muwatumie wawakilishi wenu ili wao wakutane na serikali wakati ninyi mnaendelea na kazi na Mungu awabariki na ashughulikie maslahi yenu kwa njia ya Kimungu. Amen!!!

  3. BWANA YESU ASIFIWE!Kwakweli tuendelee kuomba serekali iacheugumu wa mioyo na kuanza kuona umuhimu wa afya za watu zilivyo muhimu waache siasa watu wanakufa!tuombe ile hofu wanayokuwanayo wakati wauchaguzi ya kuhakikisha wanashinda irudi ileile kwa kujali uhai wa wananchi wanapoteza maisha!nihatari kweli hizi ni nyakati za hatari!afya za watu zinatumika vibaya kisiasa zaidi!BWANA YESU atusaidie AMEN!
    Frederick Marandu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s