TB Joshua atabiri kifo cha Rais Afrika?

Nabii maarufu kutoka Afrika TB Joshua amezua gumzo katika nchi za Africa baada ya utabiri wake alioutoa kanisani kwake mwanzoni mwezi huu, akiongea sehemu ya utabiri huo alisema “God loves us, you should pray for one African head of state, when I say President… again the sickness that is likely to take life; sudden death, it could be sickness being in the body for a long time but God showed me the country and the place but I’m not here to say anything like that.”

“When it’s too close and there is nothing I can do about it, I’ll mention it clear; the place, the country and the person so that they can see what they can do to rescue him. Okay, it is very close. Jesus loves us. Wave your hand, wave your hand,” 

TB Joshua amekuwa akitabiri mambo mengi na kutokea ikiwemo, Ushindi wa Raisi wa Ghana John Atta Mills, Michael Jackson, utabiri wa mpira wa miguu, matetemeko ya ardhi nk pia wana siasa maarufu wamefika kanisani kwake akiwemo mke wa zamani wa afrika kusini Winnie Mandela na Waziri mkuu Tanzania aliyejiuzuru, Edward Lowassa.

Advertisements

57 thoughts on “TB Joshua atabiri kifo cha Rais Afrika?

 1. Poleni sana wachangiaji wa mada aliyoianzisha ndugu yetu kuhusu T B Joshua(Mtumishi wa Mungu) japo yeye anapinga bila hata kuonyesha maandiko,siamini kama hata yeye anayajua maandiko vyema ila mafundisho ya dini yake.
  WAGALATIA 4;16 ”NIMEKUWA ADUI YENU KWA SABABU NAWAAMBIA YALIYO KWELI?” hicho ndicho ninachokiona kwako wewe unayepinga NENO la MUNGU analofundisha TB Joshua. kwani mbali na ishara zinazotokea ni mwalimu mzuri wa imani,kama wewe unaamini huwezi kumwona Mungu mpaka mtu ahubiriwe kuhusu ubatizo wa maji bado kiroho hujakua, Yule mwizi pale msalabani alitangaziwa uzima wa milele na Yesu alibatizwa kwa maji yapi? Au Yesu alivunja amri ipi alipomwambia ,”YESU AKAMWAMBIA,AMIN,NAKUAMBIA,LEO HIVI UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI.” LUKA 23;43.
  Nikukumbushe tena Yesu alipopaa hakuacha maji,alipoona huzuni ya wanafunzi wake aliwaambia hatawaacha yatima,nitwaletea msaidizi naye ni Roho Mtakatifu. Soma LUKA 24:49 NA TAZAMA,NAWALETEA JUU YENU AHADI YA BABA YANGU,LAKINII KAENI HUMU MJINI,HATA MVIKWE UWEZO UTAKAO JUU” hichi ndicho ndg yangu TB Joshua alichopewa uwezo kutoka juu, wewe kama unaangalia vya duniani maji na majengo utabaki hapa hapa.
  Paulo alipokutana na wanafunzi kule Efeso aliwauliza je,mlipokea Roho Mtakatifu? Tena akawauliza mlibatizwa kwa ubatizo gani? Hayo yote yako ktk MATENDO 19:2-6 Sasa mstari wa sita haswaaa, ”NA PAULO,ALIPOKWISHA KUWEKA MKONO YAKE JUU YAO,ROHO MTAKATIFU AKAJA JUU YAO;WAKAANZA KUNENA KWA LUGHA,NA KUTABIRI”
  Ndg yangu unayempinga mtumishi wa Mungu sielewi wewe unalitafakari vipi neno la Mungu,kwa akili zako mwenyewe? Au kwa msaada wa Roho Mtakatifu,neno hilo mwishoni linasema na KUTABIRI” Unaelewa maana ya kutabiri? hakuna mpaka wa kutabiri kwa roho wa Mungu,atatabiri juu ya kila kitu chini ya mbingu hiyo ni kazi ya Mungu na sii TB Joshua,yeye ni chombo tu na muda wake ukifika atapita atainuliwa mwingine.
  NAKUSHAURI UMWONE MUNGU KWA WATU AMBAO KUPITIA MTUMISHI WAKE WAMEPATA UPONYAJI,MIMI NI SHAHIDI NA NDG ZETU WAMEPOKEA UPONYAJI AMBAO HOSPILI ZETU WALISHINDWA LAKINI MUNGU ANAYEFUNULIWA KWETU KUPITIA NABII WA SASA AMEWAPONYA. TUBU ILI USIINGIE KWENYE MTEGO WA KUWASEMA VIBAYA WATUMISHI WA MUNGU,HAPO HUPAMBANI NA TB JOSHUA ILA MUNGU. TUBU!!!!!!!!!!!!

 2. Kazi ya Mungu inayofanywa katika njia ya Kiungu inajitetea yenyewe. Ni gharama ilioje kutetea njia isiyokuhusu! Ukiijua kweli hauhitaji kutumia nguvu. Utukufu wa mbegu upo kwenye tunda. Nguvu ya tunda haiiachi asili ya mbegu. Wenye ufahamu hutumia uhalisia wa nguvu ya kweli iliyoumbika ndani yao inayofanya waiishi hiyo kweli. kwa hiyo umahiri wa pingamizi wa kazi unayoitilia shaka ni taswira ya pingamizi yenye mizizi dhaifu isiyoweza kusimamia mchakato wa makuzi chanya. Ni busara kutambua kwamba mipaka dhaifu katika fikra za ndani husababisha vizuizi vya mabadiliko ya nje.

  BJMWAKA

 3. Haya, wote mliochangia mada bila kuomba muongozo wa Roho ya Shauri, Mutharika katangulia ghafla aliwa madarakani. Mtatafuna kauli zenu??

 4. Lwembe, hata mimi nina mashaka sana na huyu mtunishi TB Joshua. sitaki kusema mengi l;akini ukweli ni kwamba nina mashaka naye. Tunahitaji sana Mungu atupe macho ya rohoni ili tutambue mitego ya mwovu.

 5. Ndugu yangu JOHN HAULE,
  pole kwa kazi ya BWANA. Naomba usinishangae kwa kukurudisha nyuma, nia yangu si kwamba mjadala huu uanze upya, hapana. Kwakawaida hupenda kurudia comment mbalimbali za nyuma ili kujifunza na kupitia maandiko polepole. Kilichonifanya nisimame kwenye post yako ya tarehe Saturday,February 25,2012 at 12:22 pm. nikutokana na mshituko mdogo nilioupata baada ya kuona na kukisoma ulicho kiandika siku hiyo niliyoitaja hapo juu. Napenda hoja hiyo POTOFU Isipite bila kupingwa! Sababu zangu kwa ujumla ni kama ifuatavyo; Nukuu ulivyoandika……. “Tito3:9,10 Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe…….” Mwisho wa kunukuu. Alichokisema Mwdishi katika nukuu yako iliyo katika kitabu hicho cha Tito, si sawa na ulivyoeleza, kwasababu, Mwandishi alikuwa akiwaambia watu waliokuwa katika imani na fundisho “moja” ambalo watu wale walikwisha fundishwa na kukubali kuwa fundisho hilo lilikuwa sahihi – watu au wanafunzi kama hao hujulikakana kama watu “wa imani moja” Sasa, iwapo mtu au watu wakitokea katika kundi hilo, wakanena kinyume na mafundisho tajwa,…….waonywe, walejezwe, wakemewe nk. Na kama kwa vyovyote ikaonekana juhudi zote za kimalejezo zimeshindwa, wakabidhiwe kwa shetani – YAANI KANISA LIACHANE NAO!- Mfano mmoja katika hilo, ile Roma ya kale wale wote waliokuwa wakatoriki na kisha wakaanza mafundisho nje ya Ukatoriki waliitwa ” Wazushi” watu kama hao walifukuzwa kutoka katika Katoriki au kuuawa. Sasa, kama hivyo ndivyo, Lwembe utamfukuzaje toka kwenye kundi asilokuwemo? Pia ulisema nanukuu “…….1Tim6: 2,3 Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa……Maaandiko yanatanabaisha kuwa mwanafunzi mmoja Mtume Paul alimkabidhi shetani apate kufundishwa……..” Hapo LWEMBE huwezi KUMKABIDHI kwa Shetani kwa sababu; Lwembe ANATOFAUTIANA na wewe katika “kuamini” juu ya kile kilichokuwa mezani kikijadiliwa (Utatu Mtakatifu) Lwembe haamini juu ya (UTATU MTAKATIFU) lakini wewe unaamini juu ya hilo, hivyo ninyi nyote mnatokana na makundi mawili yenye imani tofauti. Mtu hatiwi hatiani kwa tofauti ya kimtazamo, bali kwa kuvunja makubaliano! Nukuu yako ifuatayo inakubaliana nami (Kumbuka Wewe na Lwembe,hamtokani na mwalimu mmoja). Ona umeandika hivi; “…..Wapendwa amani ya Kristo iamue mioyoni mwetu,kuingia magoti kumwombea huyu mpendwa Lwembe au kumkabidhi shetani.Mtu aliyempokea Bwana Yesu amehuisha hawezi kuwa kama huyu Mpendwa maana kama ukiangalia maandiko “1Tim6:3″Utaona bayana kuwa ana wazimu wa kuwazia habari ya maswali na mashindano ya maneno kwa nia ya kuleta husuda na shuku mbaya nk ili watu wanajisike tupungukiwe na utukufu wa Bwana……”mwisho wa kunukuu, – na hiyo ndiyo iliyokuwa “kesi” ambayo ikawafikisha hapo mlipofika! – Kwa hiyo, utaweza kuona kuwa wewe na Lwembe hamtokani na “FUNDISHO NA IMANI MOJA” Kwa maana hiyo kati yenu wote hakuwepo mpotoshaji…….ila kila Mtu kati yenu anaamini na kujua kivyake! Kilichokuwa kinatakiwa pale nikuletwa Neno la Biblia MBAYO WOTE MNAIKUBALI KUITETEA Ili tuone kama umo mstari unaotuacha bila SHAKA YOYOTE kuwa Mungu ni UTATU ama LA! Sasa, kwa kuwa hamtokani na “fungu” moja la imani – ingawa wote mnadai ni WAKRISTO lakini kila mmoja kati yenu ameaminishwa tofauti na mwenziwe kimafundisho. Kwa hiyo wewe hunahaki hata kidogo ya kumkabidhisha Lwembe kwa shetani! Kwa maelezo mafupi niliyoyatoa hapo juu, USISHANGAE iwapo naye SHETANI ANASHANGAA kwa kumpelekea ZIGO lisilo lake. Kwa uchche niliona si vema ukaaminiwa kuwa ulikuwa pamoja na Paulo kwa kumhukumu Lwembe! Ni hayo tu. UBARIKIWE.

 6. Wapendwa mnao changia, hebu muwe macho kidogo, yawezekana kabisa huyu CK Lwembe amekuja kuwatia najisi kama John Haule anavyosema. Nimeiona michango yake na jinsi anavyopingana nanyi kama inavyoonekana pia katika mjadala huu. Basi jihadharini ili isije ikawa kwa kuyakataa kwenu yanayojishuhudia kwa maandiko kama ninayoyaona hapa katika mjadala huu yakawaingiza katika unajisi wa kuyakataa maandiko ambayo ndiye Roho Mtakatifu, ambako ni kumkufuru!

  Mbarikiwe nyote.

 7. Ndugu Chubwa,

  Labda utusaidie mawazo, Biblia tunayosoma imeonyesha wazi Watumishi wa Mungu wakitofautiana mawazo……wakibishana …… na hata wakitengana…na Biblia tunayosoma inasema tusiziamini kila Roho na tuzichunguze……Biblia tunayosoma inasema kuna watumishi waliovaa mavazi ya Kondoo kumbe ndani ni Mbwa Mwitu……..Biblia tunayosoma inasema Miujiza sio kigezo cha mwisho kwamba fulani ni mtumishi wa Mungu……!Mtumishi wa Mungu anajulikana kwa kuangalia wigo mpana wa huduma yake ulivyojikita katika Maandiko na ushuhuda wa maisha yake….ndani na nje ya kanisa….. sio miujiza tu…..sio mahubiri tu…sio ukubwa wa ministry tu…..na hata tukitumia wigo huo mpana wa Maandiko bado hata hivyo kuna wengi watumishi wa uongo tutashindwa kuwatambua mpaka Bwana atakapowakataa mwishoni……na hii itakuwa baada ya hao “watumishi” kudanganya wengi duniani……sasa kwa vile bado tupo duniani…tunaweza kabisa kuwaangalia hao watumishi ili kujiepusha kudanganywa…. iwe kwa miujiza yao au mafundisho yao……mimi naamini Maandiko yametupa uhuru huo…….!Mradi tu tuutumie kwa uhuru ulioko katika Maandiko…….

  Kwa mtazamo wako tufanyaje…? Kwangu mimi blog hii inatoa nafasi ya kuleta mawazo yetu ma mitazamo yetu mbali mbali……kila mtu akija na mawazo yake kwa kadri ya ufahamu wake….kwa wengine inaweza kuwa ni chakula kugumu……….lakini hata Biblia ndivyo ilivyo kuna sehemu ni chakula Kigumu kisichoeleweka……lakini hatuachi kuisoma……..tusipopata mawazo tofauti tofauti na hata mitazamo tofauti tofauti na nadhani tutakua na ufinyu wa kuelewa……Labda tusaidie wapi tuchore mstari……?

 8. Ndugu zangu kuamini au kutokuamini kazi ya TB Joshua na manabii wengine haikupi credit yoyote katika ufalme wa Mungu. Neno la Mungu linposema zijaribuni Roho haina maana ukisha ijaribu basi uanze kuhukumu. “Wisdom is the decision you make from the knowledge you have” Wakristo tusitumie nguvu nying kurumbana katika vitu ambavyo vinahitaji hekima ya Mungu. Uelewa wetu tumepishana katika mambo tofautitofauti, hata katika neno la Mungu sio kwamba wote tunalingana uelewa. Halafu mkiwa mnatumia Bog hii ya SG kumbukeni tunatakiwa kilakitu kilenge Injili (Uweza wa Mungu uletao wokovu). Ukiwa uanajadili lenga kuujenga ufalme wa Mungu na sio kuona kuwa huyu hajui lolote na wewe ndio unajua. Neno la Mungu linasema ujidhaniae umesimama angalia usianguke, pia ukifkiri umelijua neno bado hujalijua. Tusilete malumbano ya utaalamu wa maandiko hapa au kuwa na roho sana na roho kidogo, haya mambo hayapo katika UKRISTO WA KWELI. Shetani asije akajitwalia sifa katika malumbano yasiyo jenga na zaidi ni kubomoa. Tunatamani kuona blog hii inakuwa tofauti na blog zingine katika mtizamo wa content, tunokua tunajadiliana kuhusiana kitu flani tunaonyesha tumekuwa kiufahamu nankimtizamo.Mimi siwahukumu kuwa mmejadiliana vibaya lakini haijawa katika mfumo mzuri sana. inahitajika tuboreshe namna unavyo toa hoja bila kuofend wengine. Hii blog sio ya dhehebu fulani, kwani changamoto kubwa ya wakristo ni madhehebu, na haya ndio yanatuletea shida ya kuona kunamadhehebu yanayojua sana na yasiojua sana. hiyo inaleta impact hadi katika maish ya kawaida ya wakristo mitaani. Huu mjadala unaweza kukupa picha halisi ya wakristo mitaani. Namna hii hatutaweza kuwaleta watu kwa Yesu, watabaki wanashangaa tu mbona wanapingana wao kwa wao?

  Kimsingi kama unaona kunashida flani ndani yako kuhusiana na mtumishi flani jitahidi Roho Mtakatifu akupe hekima ya kuzungumza juu ya huyo mtumishi au unyamaze kwasababu sio lazima eti Roho mtakatifu akikuonesha kitu ni lazima ukiseme. Kunawakati anaweza akakuambia au asikuambie. Alafu kama unakuwa haunaimani na kituflani au jambo flani sio lazima ulilete hapa SG. Jaribu kujadilianana na watuunaoishinao physically and then ukiona linatija kwa jumuiya (Public) lilete.Tunahitaji kujadiliana mambo ya Kuujenga ufalme wa Mungu au vipi wana SG? Tutumie hekima tunapokua tunajadiliana Mambo kama haya haswa katika internet. Tunahitaji SG iwe chumvi ya ulimwengu kama sisi tulivyo tunaotumia hii blog. Mtu avutiwe na hoja tunazochangia mpaka aone kuwa mkristo ni kuwa na hekima na busara.

  mimi ni mgeni Tuu jamani lakini tuko pamoja kabisaaaaaaa.
  “Ufalme wa mung kwanza”.

 9. Wapenzi wa Bwana Yesu Mbarikiwe…

  Sihitaji kusema sana kuhusu mtumishi wa Mungu Joshua kwa kuwa nimemuona na kumsikia katika TV (Emmanuel) kwa kutumika kwake sina shaka nae hata kidogo. Na kwa hakika ni Mtumishi wa Mungu.

  Kuhusu taarifa alizotangaza kwa dunia kuhusu kifo cha kiongozi wa Africa, kama ujumbe ni wa Mungu tuombe rehema kwa Mungu haya yasitokee kwa kiongozi yeyote wa Afrika. Watu wanahitaji kuomba au kusema kitu Kwa Bwana ili Mungu asamehe – Hayo yanawezekana.

  Lakini pia kama hayakutokea tutashukuru na kushangilia kwamba Mungu ametukumbuka na kupokea maombi yetu. Mimi sioni tatizo katika suala hili kwa kuwa kwa Mungu chochote chaweza kutokea “Ndiyo au Hapana”.

  Hapa nataka kusema kwamba ikitokea huyo kiongozi kafariki basi tutakuwa tumepokea taarifa ambayo tumeifanyia kazi kwa kuomba kwanza au kufanya sala kwanza. Kwa hali hii tuone nini kitatokea.

  Waana wa Mungu, watumishi wa Mungu tusiwanenee mabaya, kuwakashifu au kuwatukana kwa kuwa Mungu amewachagua. Tuombee huduma zao kwa kuwa pia mjaribu (shetani) huja kwa level zao za utumishi tuwaombee. Ikitokea kweli kiongozi kafariki wakati tumetoa kauli kali, DHAMIRA zetu zitaumia,lakini isipotokea HEKIMA zetu zitainuliwa.

  Mbarikiwe nyote

  Mzee Makunzo. 0754060996

 10. Na sie tusiojua neno la Mungu ngoja tu-shut up kama ilivyoshauriwa, ila mjadala huu haujengi kanisa lolote lile.

 11. John Bethania,

  Tafakari haya maandiko

  “Tito3:9,10 Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.”

  ‘1Tim6: 2,3 Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
  AMEJIVUNA; wala hafahamu neno lo lote; bali ana WAZIMU wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na SHUKU MBAYA; ”

  Maaandiko yanatanabaisha kuwa mwanafunzi mmoja Mtume Paul alimkabidhi shetani apate kufundishwa.

  Wapendwa amani ya Kristo iamue mioyoni mwetu,kuingia magoti kumwombea huyu mpendwa Lwembe au kumkabidhi shetani.Mtu aliyempokea Bwana Yesu amehuisha hawezi kuwa kama huyu Mpendwa maana kama ukiangalia maandiko “1Tim6:3″Utaona bayana kuwa ana wazimu wa kuwazia habari ya maswali na mashindano ya maneno kwa nia ya kuleta husuda na shuku mbaya nk ili watu wanajisike tupungukiwe na utukufu wa Bwana,Hilo ndio kazi aliyopewa kufanya na shetani kwa kujua au kutokujua.na ndio maana tangu ajiunge hapa anazunguka kama simba aungurumae hili apate kumeza mtu,anapinga kila kitu kwa kujadili kwa jazba na kebehi,Hili kwa hila TUNAJISIKE,
  Sifa kwa JEHOVA kwa njia ya Kristo ametufanya kuwa wana wake,Basi hatukosi kujua hila zake shetani na wajumbe wake.

  Lakini maandiko yanasemaje…

  2lkor6:2 -9
  “Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;
  katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote. ”

  Wapendwa TAHADHARI neema isije tupungukia.

  Gal5:8 Chachu kidogo huchachua donge zima.

  Amen

 12. Nakubaliana nawe KASULE!. Wenyehekima husema mwenye neno hana neno, na Shetani anasifa kuu mbili, cha kwanza KIBURI nacha pili UONGO, Biblia husema, HASIRA haitendi haki ya Mungu! Shetani huwajaza watu kiburi, hujiona wanajua sana hivyo wanaacha kumsikiliza Roho mtakatifu awafundishe na ndipo majigambo hingia na uongo unachukua nafasi gafla!

 13. Nimesoma comments za Watu wengi, nimegundua kuwa watu wengi wanaongea kwa Jazba bila kuwa na relevant references from the Bible. Hii inatokana na kutosoma na kutafakari Biblia. Tunatakiwa tujadili kwa amani na kwa upendo na kwa kusaidiana.
  Kila mtu aheshimu mawazo ya mwenzake. Tuache kuhukumiana. Bado tunajifunza, na bado tuko safarini, hakuna aliyefika.

  Nawapenda wote.

 14. Mtumishi Christopher asante umeamua vema kabisa, acha tumwache TB Joshua afanye alilotumwa kufanya maana Mungu amempa hizo nguvu na hayo anayofanya yanajulikana wa jinsi ya rohoni maana mtu akiwa nje ya rohoni ni vigumu sana kuyatambua haya kwa sababu rohoni ni mbali sana, wanafika huko waliojaaliwa na yeye. Basi na wewe Usiulegeze mkono wako katika kufanya kazi ya Mungu. Maana utawapa wengi kushinda nawe utapokea taji yako usipozimia roho.

 15. Kutokana na michango yenu, naomba niulize maswali haya tu na plz naomba majibu kwa kua mtu wa kweli mbele za Mungu na Roho Mt hawezi kushindwa kusema kitu alichonacho au anachojua kwa hakika, na pia kujibu kutatupa nafasi kujua tunachangia mada na watu wa Spiritual status ya level gani hivyo kuchukuliana au kuacha wafu wawazike wafu wenzao kama si kutowapa chakula cha watoto ma-dogs ua kuchezea lulu ktkk ya mapigs!

  1. Nani kati yanu ameokoka?kumpokea Bwana Yesu personally kama Bwana na mwokozi wa maisha yake? (You once had personal spiritual experience of receiving Jesus Christ in your heart for it is a remarkable experience which is so real and lasts endlessly)
  2. Nani kati yenu husikiaga sauti ya Roho Mtakatifu? (Personal experience of Holy Spirit readings/voice in your daily walk and engagements with/in God)
  3. Zipi njia nyingine ambazo Mungu hukuongozaga?
  4. Je Wakati mambo yanakua critical and confusing thas is vitu vinafanana mfano Mtumishi wa kweli na mtumishi feki, karama zinafanana yaani za man-made, devo na za Mungu, umepata kazi mbili kwa mkupuo, umepata nafasi za kusoma mbili nje, kujua msichana au mvulana fulani ni mke/mme wako Mungu aliyekupa, na mambo yafananayo kama hayo yawe ya kiroho au kimwili, waga unatumia njia gani kuamua ili uwe ktk mapenzi ya Mungu yaliyosahihi?
  5. Kukitokea mashindano Kati ya team ya Man U na Chelsea au Simba na Yanga au Zambia na Tanzania au Brazil na Afganistan,Libya,Saudia, Mungu ata support timu gani?

  NB:Kwa yeyote makini Spiritually will know why nimeuliza maswali haya! Unaweza jibu kimoyomoyo but haitasaidia mjadala huu betterr publically

  Barikiweni enyi nyote.

 16. Ndugu Christopher,

  Swali uliloliuliza kuwa, “Hivi Yesu akija leo Tanzania kwa mwili kama wa kwetu nani atakubali kuwa ni yeye?” ni la msingi sana. Kumjua Yesu itategemeana na jinsi unavyomfahamu, kama ulitambulishwa kwake kupitia Maandiko, basi utamtambua kulingana na hayo characteristically, maana vyote hutambulika kwa jinsi hiyo; na kama ulitambulishwa kwake kulingana na mafundisho ya kundi lolote lile, utamtambua hivyo;labda yeye ni nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu nk. kama ambavyo wengi wetu leo hii kama ulivyozishuhudia shuhuda nyingi pamoja na ya kwako katika post hii, wanaamini kuwa Yesu amekuja katika huduma ya nabii TB Joshua!!!!

  Pia kuhusu kuwaleta wangapi kwa Yesu au umewapotosha wangapi, huwezi kulikwepa hilo, Hata Yesu mwenyewe amekuambia ni bora uwe Baridi au Moto atakuelewa, kuliko kuwa vuguvugu kama unavyojaribu kuwa wewe lakini imeshindikana na mwishowe umeabudu pamoja na TB Joshua! Hakuna middle ground!! Lazima useme uko upande gani, hata ukijaribu kujificha haiwezekani kwa siku ya Leo; Chagueni mtamfuata nani Yesu aitwaye Neno la Mungu au Manabii wenu na vipawa vilivyo nje ya Neno la Mungu???

  Ubarikiwe!!

 17. Baada ya kusoma comments za watu wawili wa mwisho nimesikia faraja. Hivi Yesu akija leo Tanzania kwa mwili kama wa kwetu nani atakubali kuwa ni yeye? Nani aliyeamini habari zake? nani aliyetega sikio lake na kusikia habari zake? Jamani mambo kama hayana faida kwetu tuyaache tusije tukajikwaa kwa midomo yetu. Mimi binafsi nawapenda watu wote hata kama hawaamini, pia nawapenda sana wanaomtumikia mungu kwa bidii kama TB Joshua. Nampenda maana akili zake sio lengevu pia mikono yake ni imara pia. Nawapenda hata wale waliotolea comment kwa kumponda mtumishi huyu maana wanataka kujujifunza kitu kutoka kwa watu. Mungu fungua macho yetu ya rohoni na masikio ili tujue siku zetu za hapa duniani. je ukiondoka leo umepotosha wangapi na umeleta wangapi kwa Yesu. Mungu awabariki.

 18. Ndugu yangu John Bethania,

  Ninakushukuru kwa maoni yako na jinsi ulivyojikosha damu yangu kutoka mikononi mwako!

  Kinacho nishangaza zaidi kuhusu kauli zako ni ule ukigeugeu. Kama wewe unanikataza mimi kuyatumia Maandiko katika kukikagua kipawa cha nabii T.B. Joshua, iweje tena wewe utumie Maandiko hayo hayo kunipima mimi na mwishowe kunipachika kosa la kumkufuru Roho Mtakatifu? Isome tena para ya mwisho ya post yako.

  Kuhusu unabii kutimia, lile giza, ni sawa hilo lilitimia wakati wa Kristo, bali unabii wakati mwingine husimama sehemu zaidi ya moja katika kutimia kwake. Ile nuru iliyowazukia wakati ule, manabii wa uongo wameshughulika nayo sana kuifisha na sasa dunia imegubikwa tena na giza totoro la kiroho kupitia huduma za kinabii kama hii ya TB Joshua. Labda nikupe mfano wa unabii kutimia mara mbili; tazama unabii uliotolewa na Yoeli 2:28-32 huo unatimia katika Mdo 2:16 na tena unatimia Azusa! Hili ili kujihakikishia jaribu kumuuliza mwalimu Mwakasege maana ndani ya Biblia halimo!!

  Kuhusu kunishawishi kuwategemea watumishi, nadhani ufahamu wako wa jambo alilolifanya Mungu utakuwa ni mdogo sana. Hakuna mtumishi anayekuja na mawazo yake mwenyewe, watumishi huleta wazo la aliyewatuma. Mimi ninaishi katika wakati ambao yule aliyewatuma hao watumishi, nami amenipa vigezo vya kuwatambua watumishi wake halali na hao waliojiingiza katika imani kwa siri, watu walioandikiwa Hukumu. Kwa hiyo, uoga wako haunihusu mimi, wewe kama ulikwisha iuza roho yako kwa hao mawakala, wafuate wakurudishie, kama wamezipeleka HQ yao, basi tulia hapo kwa manabii wako, maana hakuna jinsi ya kukusaidia!

  Nimeona umeniletea nukuu nyingi ukijaribu kuziunganisha ili ziseme kisichokuwepo. Unaniambia pale Mwz 1:26, Mungu alikuwa anaongea na Yesu na Roho Mt, pia kwa kuhakiksha hilo nisome Mithali 8:22. Nikadhani hapo ndipo yameandikwa hayo lakini sikuyaona! Wenzako mlionao kwa manabii hao walikwisha kuja na vifungu hivyo, nikawaomba wanioneshe katika Maandiko ni wapi Mungu ametuonesha alipowaumba Malaika ili tuelewe iwapo waliumbwa baada ya Adamu ili jambo hilo liaminike hivyo wanavyotaka! Hawana jibu, wanatumia akili zao kupambanua mambo ya Mungu. Kwanini mnang’angania kuwa alikuwa akiongea na zile nafsi za utatu na si kundi la malaika wake wanaomzunguka???

  Yohana 1:1-14 haizungumzii Utatu. Inakubidi ujishushe kidogo ili uweze kuelewa Yohana anatuambia nini. Umejaribu kuiunga na Mwz 1:3 na kuleta hitimisho kutokana na maelezo yako kuwa:” Yaani Mungu akamwamuru Yesu kuumba.” Kwa kifupi unatuambia Yesu AKAAMRIWA! Mimi nadhani wewe ungeendelea kukaa chini ya manabii wako uwatumikie, badala ya kujiingiza katika mambo usiyoyajua! Waachie manabii wako mambo haya au nenda kwao wakupe tafsiri ya Utatu halafu ndio uje kwenye blogu. Kwa taarifa yako hizo nafsi Tatu za huyo Mungu wenu, zina mamlaka sawa na zina heshimiana kuliko mnavyoheshimiana na manabii wenu, maana ninyi licha ya ukiri wenu wa wokovu, manabii wenu mnawaogopa kuliko Maandiko!! Kwa hiyo kulingana na Utatu hakuna anayeweza kumuamuru mwenziwe!!!. Pia ningependa kujua kutoka kwako, huyu unayesema ‘Mungu’ akamwamuru Yesu, ni yupi kati ya hizo nafsi tatu? Je, huyo ndiye huyo anayeitwa Mungu katika kila sehemu alipotajwa katika Biblia? Maana huyo anaonekana ndiye kiongozi wa hao wenzi wake kulingana na maudhui ya utendaji wake, jambo ambalo ni kinyume na utatu! Roho wa Mungu na Roho wa Kristo na Roho Mtakatifu, je, ni roho tatu tofauti? Nimezisika kauli nyingi na pia kwa maelezo ya Utatu (ambayo wewe huyajui) zikianisha juu ya Mungu katika namna ya Mungu Baba, jambo ambalo ni sawa ki Biblia, lakini sina uhakika na hili la MUNGU MWANA na pia MUNGU ROHO MTAKATIFU; kwa vile unaonekana una ujuzi wa maandiko, nisaidie katika hilo unioneshe mambo hayo yalipo katika Biblia.

  Kuhusu Siri aliyokuja nayo nabii Joshua, nilitegemea wewe unayo lakini naona tena unaniongoza niende kwa “Mwalimu Mwakasege” ukiwa umekianza cheo chake kwa ‘M’ kubwa kinyume na fundisho la Kristo aliyesema tusimwite mtu ‘Mwalimu’. Huyo ni mwalimu Mwakasege, hizo ndizo heshima mnazofunzwa chini ya manabii!

  Kwa kifupi hata Balaamu alimtumikia Mungu, kwani alitabiri kuzaliwa kwa Kristo na mambo mengine mengi licha ya kuwa mchawi, lakini Musa ndiye aliyemuua! Basi huyo Musa kwa mafundisho yako hatauona Ufalme wa Mungu! Bethania, acha kutumia akili kama akina John Haule. Mapenzi ya mioyo yenu hayawezi kuyabadili mapenzi ya Mungu. Mungu anaangalia Neno lake na si mafundisho hayo mnayopewa na walimu wenu. Kusoma unajua, sasa unashindwa nini kujibu swali moja kwa moja unapoulizwa uonesha ni wapi Maandiko yanasema, “Roho Mtakatifu alishirikiana na Baba na Mwana kuumba ulimwengu”?? Unaleta porojo za ‘Mwz1:26”, hicho ndicho kifungu kinachoonesha kuumbwa kwa ulimwengu? Mkiambiwa roho zenu zimefungiwa kwenye mashimo, na sasa mmekuwa misukule ya hizo huduma za kinabii mnang’aka!!!

  Jamani mlio katika uhuru wa Neno la Mungu, waombeeni hawa ndugu zetu waliochukuliwa misukule roho zao na hizi huduma lukuki za kinabii zilizo nje ya Neno la Mungu, zirudishwe ili waweze kuyaona tena ya ROHONI, maana sasa hivi hawana wanaloliona isipokuwa kusifu na kuabudu huduma hizo!!!

  Bwana atujalie Roho wa Maombi!

 19. Watu wote mjue kuwa mtumishi wa Mungu akiamua kuomba jambo lolote linakuwa kwa namna nyingine mtumishi wa Mungu anayo hatima ya maisha ya watu. kwa maana anayo imani inayomwezesha kuamuru vitu navyo vikamtii. watu wasimnukuu vibaya hajataja nchi wala jina la Rais yeye amesema Rais wa nchi mojawapo ya afrika.

  Mfano wa kwanza
  Mtumishi wa Mungu alitabiri kuwapo chakula mtu mmoja akampinga alipompinga aliambiwa kuwa atakiona chakula lakini hatakula mara chakula kikatokea alipokuwa anakimbilia kukichukua chakula hicho alianguka na wemgine waliokuwa wanakimbilia chakula hicho walimkanyaga na akafa.

  Mfano wa pili
  TB Joshua alipoona kuwa Timu ya mpira ya Zambia wamefika Final alijawa na huruma na kumwomba mungu ili awafute machozi kutokana na kupoteza timu nzima katika mechi kama hiyo miaka kama kumi iliyopita, Hivyo akatabiri akiwa na uhakika kuwa maombi yake yamejibiwa na ndivyo ilivyokuwa. tazama you tube pale anaposema kuwa timu pinzani watapata nafasi lakini mchezaji akiwa amebaki peke yake na goalkeeper atakosa kufunga na ndivyo ilivyokuwa.

 20. New post on The TB Joshua Blog

  WHAT TB JOSHUA ACTUALLY SAID REGARDING AN AFRICAN HEAD OF STATE
  by thetbjoshuafanclub
  There have been numerous reports flying round the internet and various news media in many African countries for the last few days about what Prophet TB Joshua said on Sunday 5th February about an African president. Different time-frames and false dates, including ‘2 months’ ’60 days’ ‘February 16th’ and ‘April 16th’ have been mentioned. This is to certify and clarify once and for all what Prophet TB Joshua actually said on that day.
  Prophet TB Joshua DID NOT prophesy that an African president would die in 60 days or two months time. He DID NOT mention any specific date or time-frame.
  DO NOT misquote him. DO NOT spread rumours and attribute them to Prophet TB Joshua. Prophet TB Joshua speaks forth only what he hears from God Almighty and it is not to be misquoted, mistreated or misused for one’s own benefit. “You shall not add to the word which I command you, nor take from it, that you may keep the commandments of the Lord your God which I command you” (Deuteronomy 4:2).
  PROPHECIES revealed by God Almighty through Prophet TB Joshua are broadcast LIVE on Emmanuel TV during the Sunday Live Services At The SCOAN.
  IF YOU DIDN’T SEE IT FOR YOURSELF ON EMMANUEL TV, IT DIDN’T HAPPEN!
  THIS is what Prophet TB Joshua prophesied regarding an African head of state:
  “We should pray for one African head of state, president, against sickness that will likely take life. It is a sickness for a long time – being kept in the body for a long time. God showed me the country and the place but I’m not here to say anything like that. I am still praying to God to deliver the president concerned.”
  He did not say more than that. He only said that we should pray for his life to be saved. He did not say that the prophecy was unchangeable. He did not give his name; he did not say when the leader would die; he did not say that the leader must die; he did not give the name of the country the leader was from. He only said that we should pray for him.
  Please let people around you, your friends and colleagues and all who care to listen know what TB Joshua actually said. What a prophet says is not meant for speculation; it is rather a sober encouragement for us all to continue to give ourselves to prayer. We may know that we need God but we may not know how much we really need Him. thetbjoshuafanclub | February 9, 2012 at 2:02 pm | Tags: abdoulaye wade, africa, african, african head of state, african president, angola, Cameroon, congo, death, Denis Sassou Nguesso, Eduardo Dos Santos, Emmanuel TV, kenya, lies, Michael Sata, mugabe, mwai Kibaki, Pastor TB Joshua, Paul Biya, predict, Prophecy, prophesy, Prophet TB Joshua, rumour, SCOAN, sickness, synagogue church of all nations, TB Joshua, The Synagogue Church Of All Nations, Zambia, Z|imbabwe | Categories: Prophecy | URL: http://wp.me/pxw1c-1bK
  Comment See all comments

  Unsubscribe or change your email settings at Manage Subscriptions.
  Trouble clicking? Copy and paste this URL into your browser:
  http://thetbjoshuafanclub.wordpress.com/2012/02/09/what-tb-joshua-actually-said-regarding-an-african-head-of-state/
  Be carefull of what your saying you will destroy your hollynes iam advising you take tame to pray for the sevants of GOD this is my advice as frederick if you dont beliave them just ask GOD only not neighbers you meight ask the wrong persson.
  Be blessed

  Frederick D Marandu

 21. Mimi ninaamini kwamba STRCTLY GOSPEL wameanzisha blog hii ili sisi tupate ujifunza kutoka kwa wenzetu wengi waliojaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu wetu na si mahali pa kumkufuru Roho mtakatifu. Mbarikiwe sana STRCTLY GOSPEL. Napenda kusema machache juu ya comments za ndugu yetu Lwembe juu ya mtumishi wa Mungu aliye hai T.B.Joshua. Kuna maneno aliyoyatumia katika kujenga hoja zake naomba ninukuu machache tu mfano;
  (1) “Katika wakati huu ambapo dunia imegubikwa na giza, nalo giza nene juu ya watu; akiibuka mtu mwenye kipawa kama hicho na kuyatabiri mambo ya jinsi hiyo, basi katika giza kama hilo, mwanga wa simu ya tochi huonekana jua la mchana kwa walio gizani!!”

  kwa maneno hayo ndugu Lwembe bado hajaelewa kuwa Nuru (Yesu) alikwisha kuja Soma Isaya 9:2 kweli kabla ya Yesu kuja dunia ilikuwa katika giza lakini sasaYesu anang’ara sana dunani ila watu wamependa giza kuliko nuru, ndiyo sababu vita dhidi ya wakristo ni kubwa sana duniani. Na wewe Lwembe unapigwa vita pasipo kujua na hao wanaoupinga ukristo maana wanakufanya umkane kristo pasipo kujua; hata sasa kwa maneno yako unamkana Kristo. Ndugu yangu Lwembe kumbuka hakuna siku utakuja kumwona Yesu au Mungu mahali na wakati wowote ila utawaona watumishi wake kama viunganisho kati yako na Mungu/Yesu. Hivyo kama huwaamini watumishi waliotumwa na Mungu maana yake huna imani na Mungu aliyewatuma.

  (2) Sentensi ya kwanza kabisa katika ‘Statement of Faith’ yake inasema hivi:“The Holy Spirit worked with the Father and the Son to create the world.” Tafsiri ya karibu ya kauli hiyo kuhusu wanacho amini ni, “Roho Mtakatifu alishirikiana na Baba na Mwana kuumba ulimwengu.”

  Ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 1:26 neno linasema “….na tufanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu….” Hivi Mungu alikuwa anazungumza na nani kule mbinguni? Lwembe huoni kuwa kulikuwa na kikao huko mbinguni wakijadili juu ya uumbaji wa mtu? (ajabu ee?) kwa taarifa yako Mungu alikuwa anaongea na Yesu (soma Mithali 8:22…) na Roho Mtakatifu (roho ya Mungu). Lwembe hebu soma maandiko kwa taratibu na kwa kutafakari. Soma taratibu Yohana 1:1 Hapo mwanzo alikuwako Neno (Neno hapa ni noun – person); Neno(Yesu) alikuwako kwa Mungu; Neno alikuwa Mungu; huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. mstari wa 14: Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu; huyo ndiye Yesu. Vitu vyote vilifanyika kwa huyo (Yesu) yaani Yesu ndiye aliyeviumba vyote. Soma Mwanzo 1:3 Mungu akasema Iwe (noun yaani Iwe ni Person yaani Yesu ) ikawa nuru.Yaani Mungu akamwamuru Yesu kuumba. Soma pia Mithali 8:30 Ndipo nilipokuwa naye kama stadi wa kazi (wa kuumba). Tafakari hayo utaelewa.

  (3) Kwa kifupi huyu ni nabii wa Utatu!
  Ndugu Lwembe hapa hujui unachosema maana yaonekana una ugomvi na utatu wa Mungu. Hebu tia ufahamu juu ya Mungu ili upate kumjua Mungu ndugu yangu. Mtu anayemjua Mungu hawezi kutamka neno ulilotamka hapa. Unaongea maneno mengi mno ndugu yangu! Soma kitabu cha Koheleth 5:2 ili uchukue tahadhari wakati wa kunena mbele za Mungu.

  (4) Nimejaribu kuitafuta Huduma ya Nabii TB Joshua katika ule ‘Mwongozo’ ili nijue amekuja katika Roho gani na kuifanya Huduma ipi ambayo Mungu amemfunulia Siri yake, sijaiona!

  Ikiwa kama umeshindwa kuelewa huduma ya T.B. Joshua imekuja katika roho gani basi hutaelewa hata huduma Samwel ailikuja kwa roho gani maana yeye alikuwa anajiita mimi ndimi mwonaji wa israeli! Soma 1Samwel 9:18 Je? Hujui kuwa Yohana alikuja kwa roho ya Eliya? Luka 1:17. Fungua ufahamu wako Lwembe hebu jaribu kuwaona waalimu wa Biblia watakufunza siri zilizofichika za ufalme wa Mungu. Sasa hivi Mwalimu Mwakasege anafundisha semina ya neno pale Biafra tafadhali hudhuria na ujaribu kuuliza maswali upate uelewa wa mungu.

  (5) Anaye Roho wa Utambuzi tu anayeweza kukamata mambo ya mwilini kama vifo vya wanaulimwengu, mipira na mambo ya namna hiyo na si ya ROHONI.

  Katika statement zote ulizotoa ndugu yangu Lwembe hii ndiyo fungakazi maana ndiyo mbaya kuliko zote kwakuwa umeufunga mlango ambao hutakuja kuufungua (siku moja utakuja kukumbuka hili nitakalosema). Kwa nini? Hii ndiyo dhambi isiyosamehewa yaani ni dhambi ya milele. Yaani “Umemkufuru Roho Mtakatifu.” Ni kweli kabisa soma Marko 3:28-30. Dhambi hii ninakuhakikishia kuwa haisamehewi kwa sababu umesema T.B.Joshua (yeye aliyetumwa na Mungu) ana pepo. Soma vizuri andiko hilo ambalo alilitamka Yesu mwenyewe. Je? Mpaka hapo ndugu Lwembe huoni umejihukumu mwenyewe? Unaonaje? Nafasi yako katika ufalme wa Mungu bado ipo? Weka kwenye mzani hayo unayoongea uone kama nafasi yako katika ufalme wa Mungu bado ipo!! upo hapo?!!

  (6) Kwa hiyo kipawa chochote lazima ukikague kulingana na Maandiko, maana wengine wamepewa hivyo ili wapate kuwapoteza watu!!

  Na wakweli hili umeongea sawa kabisa maana wewe ni mmoja wa watu wanaowapoteza watu kwa ujuzi wa kuongea bila kutafakari. Maana tayari umewashawishi wengine kuamini kuwa unachosema ni sahihi juu ya Mungu kumbe sivyo. Akina Mtemani katika kitabu cha Ayubu waliongea maneno mengi mazuri ya hekima na busara sana tena yote ni ya kweli. Lakini Mungu mwishoni anapata hasira juu yao anasema hawakuongea yaliyo sawa juu ya Mungu na mtumishi wake Ayubu. Lwembe fikiri umemsababisha ndugu John Haule aseme “Neema mimi ni mmoja wa ambao amani ya moyo wangu haijamkubali TB Joshua” yaani hata kama angekuwa sio mtumishi wa Mungu mtu anathubutu kusema hamkubali mwanadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu? Lwembe kama watu wengi wamepotea kupitia comments zako huoni wewe hukumu yako itakuwa kubwa zadi?
  Ndugu Lwembe si vema sisi tunyamaze maana tutadaiwa damu yako mikononi mwetu. Ezekieli 33:7-9 Wako watu wengi sana duniani hata hapa Tanzania wanaoteseka kwa magonjwa na taabu nyingine nyingi kwa sababu waliwanena vibaya watumishi wa Mungu na hata kumkufuru roho mtakatifu. Wengine waliwanena atumishi vibaya pasipokujua lakini waliingia hatiani; Soma Walawi 5:17. Na kisha wewe Lwembe huwezi kukagua kipawa cha mtu kupitia maandiko uliyokariri maana mambo ya rohoni hujulikana wa jinsi ya rohoni kwa sababu yaliyo ndani ya mtu anayeyaelewa ni Mungu. Maana waweza kusema amepotoka kumbe yeye ameambiwa na Mungu afanye hayo anayoyafanya. Naomba niishie hapo.

 22. Ndungu Nduta,

  Naona utatuita kwa majina ya kila namna!…Ulianza kusema anayempinga Nabii Joshua ni wa mwilini……nikakuuliza Je anayesema Nabii Joshua ni nabii wa Mungu ndie mtu wa Rohoni? Ukawa Kimya…mara ukasema yoyote anayempinga Nabii Joshua anautata….nikakuuliza Je anayemuunga Mkono Nabii Joshua yeye ndiye njia zake ndio nyoofu? Ukawa kimya pia….. Sasa unasema kuwa tunaompinga Nabii Joshua tunajishirikisha mambo ya ajabu ajabu….! Naona kabisa huna mahali pa kusimamia isipokua ushabiki tu dhidi ya huyu Cultic figure wa Nigeria…..Simamia maandiko ndugu yangu ndio mahali Imara……acha hisia ….ushabiki….upambe…….! Mambo ya Kiroho hayaendi hivyo!

  Toka awali ujumbe wangu umekuwa ule ule na haubadiliki na kamwe hautabadilika kama wewe kila mara unavyobadilika! …… Msimamo wangu umekuwa wazi…….hatuipimi kazi ya Mungu kwa miujiza….Hivyo ndivyo Biblia inavyosema ….Hivyo ndivyo Paulo anavyosema…..Hivyo ndivyo Maandiko ya Agano jipya yanavyosema….sio mimi Orbi….Yesu tunayemwamini alitenda Miujiza….anatenda Miujiza…na ndiye huyo huyo alisema wengi watakuja kwa njia ya Miujiza na kupoteza wengi….! Na ndiye huyo huyo kwa kuptia mtumishi wake Paulo alisema “tuzipime/tusiamini kila roho”…….. Nimekupa nukuu nyingi mno…..labda nikupe tena nukuu hii…..”KWA MAANA WATAONDOKA MAKRISTO WA UONGO NA MANABII WA UONGO WATATOA ISHARA NA MAAJABU WAPATE KUWADANGANYA KAMA YAMKINI HATA HAO WATEULE…….BALI NINYI JIHADHARINI NIMEKWISHA KUWAONYA MBELE”

  Nadhani aya hii haiko katika Biblia yako…….! Sioni unachukua tahadhari yoyote…bali kadri unavyoandika unaonyesha fanaticism yako ilivyo kubwa dhidi ya huyo cultic leader wa Nigera….unavyooandika unaonekana wazi “ameku-Posses”……hebu angalia nukuu yako hii……..

  “T.B. JOSHUA NI NABII WA NGUVU ………. Huo ndio msimamamo wangu na ninawaaacha nyie msiomkubali T.B. Joshua mwendelee na kile mnachokiona chema. Ila mimi sikubaliani nanyi mpaka kesho.”

  Ndugu Nduta na wewe umekuwa Nabii….? angalia nukuu yako hii tena………

  “Wapingaji wote hamna lolote la mnalolisema. Ninathubutu kusema ukiroho wenu ni FEKI.”

  Sasa ndugu yetu Nduta wewe ndio Mhimili wa Imani……una futi kamba ya kupimia kiroho cha watu…….. Na kigezo chako cha kuwa feki kiroho ni kumkataa Nabii Joshua? Dalili mojawapo ya imani potofu ni jinsi ambavo zinaua uwezo wa kufikiri kwa wafuasi wake……maandiko yako yanaonyesha wazi mno…..uko tayari kumfia Nabii huyu wa Nigeria…….. Na hili ndilo tatizo la Imani nyingi za Kinabii na mitume…. zinaua uwezo wa kufikiri….zinazaa chuki na hasira kwa yoyote anayejaribu kwenda kinyume chake…na kuja na vitisho vingi…..! ilikuwa hivyo kwa Jim Jones……ilikuwa hivyo kwa Bob Koresh…..kwa akina Kibwetere……. waamini walionywa mno…….lakini kama vile mpiga filimbi wa Hamelin…… kamba ya miujiza ilikuwa ni tanzi zito lililote maangamizi makubwa kwa wafuasi wa manabii hawa………….na hata hapa Tanzania unaona ushabiki wala sio Maandiko yakiwasukuma waumini kwa Manabii na Mitume….kisa miujiza…..kisa wingi wa watu……kisa Baraka……..na Babu wa Loliondo alithibitisha wazi wazi kuwa Maneno ya Yesu yalikuwa sahihi kabisa na yatabakia kuwa sahihi leo….. ….njia rahisi mno ya ……..”KUWAPOTEZA HATA WATEULE”…..ni miujiza! Hakuna kitu kingine…!

  Sina muda zaidi tena wa kuandika katika Mada hii……nimeandika vya kutosha mno….na ujumbe wako umekuweka wazi mno pia ….na imeonyesha wazi Imani yako imejengwa juu ya nini………Na kama wewe mwenyewe Ulivyothubutu kusema wanaompinga Nabii huyu wa Nigeria Kiroho chao ni Feki…nami Kwa Ujasiri Kabisa namalizia kwa maneno ya Bwana wetu Kristo……..BALI NINYI JIHADHARINI NIMEKWISHA KUWAONYA MBELE” (Marko 13:23)

  Ubarikiwe ndugu yangu Nduta.

 23. Wapendwa,

  Nimesoma majibu ya CK Kwembe na nimerudia kufanya tathmini ya majibu na hoja za wote wanompinga T. B. Joshua.

  Doctrinal statement inayonukuliwa ni kwa lengo la kuzua ubishi tu. Lipo kundi moja la kidini ambalo kazi yake ni kuweka mada za kuwa -kandia watumishi wa Mungu.

  Ukiingia kwenye mtandao (Internet) na ku-search utagundua kila mtumishi mkubwa wa Mungu amepakaziwa hivyo hivyo. Kuanzia Reinhard Bonke, Benny Hinn, T.D. Jakes, Joel Osteen, Kenneth Copeland, Oral Robert, Keneth E. Haggin na wengine wengi.

  Wote wameitwa “False Prophets” yaani Manabii wa uongo.

  Sasa hii Tabia ya kuwapakazia watumishi wa Mungu “Manabii wa uongo” inatekelezwa na Free Masons na Devil Worshipers (Waabudu Shetani) na dini zingine kengeufu ambao wamevaa vazi la kondoo (Nikiwa na maana kuwa wanajifanya nao ni wakristo waliookoka wakati si kweli).

  Hakuna mtu aliyeokoka kiukweli ambaye anapinga miujiza halali.

  Hakuna mtumishi wa Mungu wa ukweli anayepinga miujiza ya Yesu.

  Watu pekee wanaopinga na kukataa matendo makuu ya Yesu ni wapinzani kutoka makundi niliyoyataja hapo juu na watu wenye nia mbaya.

  Yesu ni mtenda miujiza. Manabii kama Elia na Elisha walitenda matendo makuu. Mitume na wainjilisti walitenda matendo makuu.

  Yesu alisema hata kazi kuu kuliko alizozifanya zitatendeka na Kanisa.

  Kingine ni Wivu kuna watu ambao kwa kuwa Mungu hawatumii wao kutenda hiyo miujiza basi wanaingiwa na wivu na kuanza kukandia.

  Kwa hapa ninaona wengi wawanaopinga watakuwa ni KWENYE KUNDI LA WAKENGEUFU.

  iSIJE KUWA NYIE MNAOPINGA NDIO FREE MASON HUKU MNAMPAKAZIA T.B. JOSHUA KUWA YEYE NDIO FREEMASON.

  FREE MASON HAWAWEZI KUFANYA MIUJIZA. HAWAWEZI KUPONYA WAGONJWA!

  DINI ZA KIHINDI HAZINA MIUJIZA YOYOTE WALICHONACHO WAO NI UGANGA , MAZINGAOMBWE NA USHIRIKINA.

  NENO LA MUNGU LINAAMBATANA NA MIUJIZA. 1 wakorintho 12:1 na kuendelea inaongelea karama za roho mtakatifu alivyogawanya. Wengine wamepewa kutenda matendo ya miujiza lakini kwa manufaa ya kanisa lote.

  Kwa hiyo siyo lazima wote watende miujiza lakini wapo ambao Roho amewapa kipawa na sisi tunafurahi pamoja na wao na kumshukuru Mungu.

  Injili mnayotaka kutuletea sisi ambayo mnapinga Mungu kujidhihirisha kwa nguvu ni INJILI POROJO!

  KUHUSU MICHEZO. MICHEZO SIYO DHAMBI. SASA NASHINDWA KUELEWA UKRISTO WENU UMEKALIA WAPI.

  LAZIMA MTAKUWA MNAJISHIRIKISHA MAMBO YA AJABU AJABU AMBAYO YATADHIHIRIKA HUKO MBELE TUENDAKO.

  AHSANTENI

 24. Ndg Zangu nimewasoma wote nimejua kila mtu anahisia zake. Lakini mimi nionavyo ni kwamba hatujaambiwa “kuhukumu” Pia tumezuiwa kunyosha vidole kwa wale wanaojiita watumishi wa mungu. Mkata majani ya ng’ombe ni sawa na mfanyakazi wa ofisini kwa sababu wote wanapokea shekeli ili walishe matumbo yao. Kwa hiyo basi si wote wanahuduma za kuponya ingawa neno linakiri kwamba tukiweka mikono juu ya wagonjwa watapata afya je leo makanisani watu wanapona? Je Yesu akija leo akaanza kuhubiri ufalme wa mungu na kufanya miujiza wangapi watakubali huduma yake? Kuzaliwa kwake walitia mashaka kwa kuwa mji aliozaliwa haukuwa na hadhi je leo akija Tanzania Wazungu watasema ndio yeye? na akitokea somalia je nyie watoa hoja hamtasema maharamia ya kisomalia? najaribu kuwafikirisha ili msije mkawa sasa na wale waliomwua yesu siku zile bila wao kutambua. Funga mdomo wako waache wafanye lakini kila mtu atapata sawasawa na kipimo anachotumia. amina mungu awabariki.

 25. Ndugu zangu,

  Tuweni wenye ujasiri,

  Neno la Mungu ni Upanga ukatao kuwili, pia ni moto ulao! Iwapo mnayo haja ya kweli ya kulitafakari Neno la Mungu, basi njooni mkiwa na ufahamu kamili wa hilo, vinginevyo mnajishirikisha wenyewe katika HUKUMU yenu! Napenda kumsahihisha kidogo ndugu yangu Orbi katika kauli yake inyoonesha moyo wake wa huruma, kwamba “Kumwita Nabii Joshua Ni Free Mason HATA Nabii wa Uongo hakuna kufuru ya aina yoyote….hata kama kweli si Nabii wa Uongo…..! Unaingia tu katika kigezo cha kukosa ufahamu wa huyo nabii ….Na tukitumia Maandiko tutasema Hujui Utatendalo…..wala haingii katika category ya laana…….!” Katika hili ‘wasiojua watendalo’ walikuwa ni Wayahudi tu, maana wao walipofushwa. Sisi tuna macho yote na NURU yote, kisingizio cha kutokujua, kwetu hakipo. Kwetu sisi; ‘Kweli yako, iwe Kweli na Hapana yako, iwe Hapana!’

  Kwa hiyo, tunaposema huyu si nabii wa Mungu, tunasema hivyo tukiwa na ufahamu kamili, na kwa sababu ni mambo yanayomhusu Mungu, tunaepuka kutumia vigezo vya mwilini, tunaviruka hivyo kwanza, tunaipima Huduma hiyo katika vigezo vya rohoni na kisha kuitolea uamuzi. Na kama tutasimama Hukumuni kwa hilo, tutajitetea kwa kuyarejea Maandiko na si kwa ushuhuda wa kupewa utajiri wa mali au kuponywa upofu katika huduma hiyo! Hayo ni mambo ya mwilini yalikuwa kigezo kwa Wafarisayo waliokuwa wa mwilini, Haki yetu sisi inapaswa izidi ile ya Wafarisayo!

  Pia, kwa wanaofanya ushawishi wa kuwaongoza watu kwenda kwenye Huduma hiyo, tunaamini nao pia wanafanya hivyo wakiwa na ufahamu kamili kuwa roho wanazo zishawishi zikafanye Ibada huko, iwapo zitawalilia siku ya Hukumu, nao wako tayari kujibu mashtaka ya USHAWISHI wao dhidi ya Neno la Mungu. Kama wanategemea nukuu kama ya Yoh 9:25 ili kuikimbia Hukumu, basi hao yaonesha wamebaki mwilini, hawana uwezo wa kuyapokea makuu zaidi kama ya Mt 24:24. Nao pengine kwa makusudi ya utajiri na mambo mengine ya mwilini, kama nilivyoyaona kwa kiwango kikubwa katika post za ndugu Ndutta, wamejiaminisha katika mambo hayo nao wanajipa ahueni katika vifungu vya Biblia wanavyo vinukuu out of context! Hebu fikiria mkristo anayejaribu kumhusiha Mungu na mipira iliyojaa uchawi na mambo ya jinsi hiyo, halafu anaminin kabisa kuwa mitume wale 11 ilikuwa timu ya mpira!! acheni kuwachanganya watu!!! Dunia ina mambo yake mengi sana, nayo mapepo ya michezo tunafahamu yanacho kifanya; yanakuondoa uweponi mwa Mungu ndio maana tunaona utetezi wa jinsi hii kuhusu michezo, mtapotea nayo hiyo. Jitengeni na ulimwengu!!!!

  Katika maelezo yangu ya awali niliwawekeeni ‘Statement of Faith’ ya Huduma hiyo inayosema, ““Roho Mtakatifu alishirikiana na Baba na Mwana kuumba ulimwengu” Ndipo nikawaomba nyote mnaofanya ushawishi wa kuitukuza Huduma hiyo kuwa ni ya Mungu, tuonesheni ni wapi katika Maandiko yapo maneno hayo!??? Badala ya kutudhihirishia hilo mnajaribu kufanya hila ya kuleta ugomvi wa maneno na kuleta nukuu za uponyo ili kupotosha mada ionekane tunamzungumzia mtu badala ya issue. Uponyo si kigezo cha kujiprostrate kwa kila Huduma, kama wachawi wanaweza kukutia nyembe tumboni na mganga wa kienyeji akakutapisha kwa matambiko, basi hao nao siku moja utawasujudia maana siku hizi wanakupa na mistari ya Biblia ukasome, tena wachawi wenyewe ni wa kiwango cha Balaam! Hata hiyo picha iliyowekwa hapa katika post hii inamaliza maelezo yote kama hujapofushwa macho ya kiroho; Tazama mshumaa huo!!!! Kama unajionea sawa tu, ndio hivyo; ulipojiprostrate roho yako kwa huduma hiyo, ndipo roho yako ilipofungiwa humo, kwa hiyo huna tena uwezo wa kuelewa chochote zaidi ya KUSIFU na KUABUDU katika roho ya SYNAGOGUE CHURCH; mkiendelea na rituals na enchantments, kama picha ya ‘Nabii wa Kizazi’ inavyojieleza!!!!!!!!

  Acheni porojo za vijiwe vya kidini, hamkatazwi kwenda huko na kwingine kokote wanakowahubiria hizo ‘Injili za Vipodozi’ bali hakikisheni angalau mnaupata utajiri wenyewe au mnatimiziwa hayo mnayoyaendea huko, kuliko kufanya ushabiki ambao gharama yake utailipia sawa na wale walioiendea huduma hiyo, wakapokea na wakapigwa mhuri wa upotevu!

  Nimemuona ndugu yangu Haggai anatuasa tumuombe Roho Mtakatifu atuoneshe! Hivi ndugu yangu, hebu jaribu kukumbuka ni mhudumu gani aliyewahi kukiri kuwa hajawahi kuongea na Roho Mtakatifu?? Kwa ushauri wako huo, hata mkifanya maombi ya pamoja wana SG wote, mimi ambaye sikuwa nanyi Roho Mtakatifu alipowashukia na mkaanza kunena kwa lugha, na kupewa jibu kuwa ‘Huyo ni nabii wangu’ unadhani nitawaamini? Siwezi! Nitaishia kuwaambia huyo hakuwa yeye Roho Mt., labda mseme kawatuma mkamwambie aibadili ile ‘Statement of Faith’ yao!!! Pia unapaswa kuiamini Biblia yako inachokisema, huyo ndiye Roho Mtakatifu; “Maneno haya niyasemayo ni Roho na Uzima” Usipoiamini Biblia yako, on that instance mapepo ya kidini yanakuvaa, sijui utajichomoaje humo, nawe Roho wa Mungu mwenye kukulinda ulimuacha na kufuata miujiza ya kichawi!!

  Umeambiwa watakuja mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo. Basi ukiwaona kondoo hao waliokuja, jaribu kuwachunguza kwa siri haswa sehemu za miguu, ukiuona ukucha umeitoboa ile ngozi ya kondoo na kujitokeza japo kiduchu, usingoje kuona mkia wake utakuwa umechelewa, KIMBIAAAAAAAA!!!!!

  Nadhani nifunge kwa kuirudia kauli ya Edwin:
  Barikiweni enyi nyote mtakaopenda kubarikiwa, aaaaaaaaaaaaaaamen!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 26. Wapendwa,

  Ninachoona mimi hapa ni ukiroho wa uongo tu. Kila anayepinga miujiza halali kama ya T.B. Joshua ni mwongo tu wakawaida.

  Mungu aliyeumba ulimwengu anajua tutakuwa na michezo na burudani halali.

  Yesu alihudhuria harusi na alikuwa na wakati wa kuburudika na kuongea na watu wa kawaida na kushiriki maisha ya kawaida (Social).

  Manake mimi nashangaa HAO WANAOMPINGA T.B. JOSHUA WANAPINGA MAMBO YA MICHEZO HALAFU WANAHAMIA KUPINGA MIUJIZA.

  WAPINGAJI WENGINE WANADAI ETI HAWANA MSUKUMO WA KUMWANGALIA T.B. JOSHUA.

  KWA HIYO INAONEKANA WAO WANAPINGA KILA KITU KITAKACHOTOKANA NA T.B. JOSHUA

  WANANIKUMBUSHA WALIOKUWA WANAMSHITAKI YESU, MARA WADAI ANAPOTOSHA WATU, MARA WADAI ANAKATAZA WATU KUTOA KODI KWA KAISARI, MARA ANAJIFANANISHA NA MUNGU? MARA YESU ANADAI KUWA ANAWEZA KUBOMOA HEKALU HILI NA KUJENGA NDAINI YA SIKU TATU.Mathayo 26.61

  Wapingaji wote hamna lolote la mnalolisema. Ninathubutu kusema ukiroho wenu ni FEKI.

  Mungu ameahidi injili inayoambatana na Nguvu na Ishara.

  Mungu anaweza kuonyesha vitu vinavyokuja (future) na hakuna yeyote atakayempangia Mungu mambo anayotaka kuyaonyesha watu wake.

  Wanaopinga michezo mimi nawaambia hicho ni kiroho FEKI.

  T.B. JOSHUA NI NABII WA NGUVU NA MUNGU AMBARIKI. Huo ndio msimamamo wangu na ninawaaacha nyie msiomkubali T.B. Joshua mwendelee na kile mnachokiona chema. Ila mimi sikubaliani nanyi mpaka kesho.

  Marko 14:56-59

  KWA MAANA WNGI WALIMSHUHUDIA UONGO, WALAKINI USHUHUDA WAO HAKUPATANA. HATA WENGINE WAKASIMAMA WAKAMSHUHUDIA UONGO WAKISEMA. SISI TULIMSIKIA AKISEMA, MIMI NITALIVUNJA HEKALU HILI LILILOFANYIKA KWA MIKONO NA KATIKA SIKU TATU NITALIJENGA JINGINE LISILOFANYIKA KWA MIKONO. WALA HATA HIVI USHUHUDA WAO HAUKUATANA.

  AHSANTENI
  Mbarikiwe

 27. Seriously speaking, katika wote mliaochangia kuhusu Tb…. ni mtu mmoja tu ambaye ana hoja ya msingi ya KiMungu na kibiblia…naye ni Orbi. Wengine manafosi ”king”…ni longolongo tu na material ushabiki!. Kwa Mtu aliyemzima ndani kuleeeeeeee….vyumba vya ndani walio wa rohoni watajua na refer nini…. watajua tu Orbi ameongea Biblically but the rest physically. Yaani Orbi ametumia Neno la Mungu KWA USAHIHI- in the real context as intended by Holy Spirit the author of the Word. Any body can use and quote the Words lakini si kwa usahihi

  Mambo ya kudauti kuhusu huduma hii yako kibao tu wala msimsingizie Roho Mt wala
  kumpa assignment awafunuliwe wakati issue zenye utata zinoonekana live! nyie wapendwa acheni kukomplicate some time.

  Kubase miujiza kama kigezo cha kupima ya rohoni ni kufilisika kiroho na spiritual babish kabisa, ni zero sum game kupima mtu wa Mungu kwa miracle performance kwakua hata iyo babu yangu unyamwezini anaperform ya kutisha. Wachawi ktk Biblia waliperform sana tu ishara na miujiza=read your Bible from old-new testament!

  Utabiri kuhusu timu kushinda mashindano, sijui president kudead, mara sijui ndege itapinduka, kwa mtu niliyeookoka kama mimi na nayejua Neno na navyo fahamu priorities za Mungu ni zipi na Bwana Yesu mpaka akaacha mbingu na kukubali kuacha Uuungu wake na kufa kwa ukatili vile unaozidi ukatili wa ualikaida na ualishabaab, usitegeme ni weeeeseeeeeeeke eti Bwana amesema. Why hasitabiri huyo presidaa kuokoko ua ndege kusave au mengine yenye tija in the Kingdom of God na sadaka ya Yesu msalabani? These maunabii are just mbwembweism, hamna lolote.

  Na embu niwaambieni watu wa Mungu humu, Mungu is so clever and protective wa kazi yake na watu wake mpaka ameturuhusu kupima kila roho….note.. kila roho….meaning kila mtu, mtumishi awe mkuuuuuuuuuubwa au mdooooooooogo, anapimwa tu kabla ya kuumeza unabii wake.,wakristu wa leo au watoto ktk mambo ya Mungu na Neno mtu akitabiri tu, akatoa unabii tu, akasema ameooneshwa tu, wanamiminikia huko, wanameza bila kutumia haki yao ya msingi ya kucheki kwanza kwa Biblia na pia na Roho mt ambaye huongeaga-kwa wenye dini hilo walilijui.

  Mwisho wengine tunaosoma humu tunajua Neno na Mungu na Roho Mt na tumeokoka kweli kweli, so plz anayechangia mada awe deep na Mungu na ufahamu wa mambo ya mbinguni na ya rohoni na ya Neno kama Orbi, otherwise ukichangia tu nakwa tunaojua tukisoma tu what you say, unaona utoto mwingiiiii wa mambo ya Rohoni na Neno na udini kibao wa mhuusika-ni aibu

  Barikiweni enyi nyote mtakaopenda kubarikiwa, aaaaaaaaaaaaaaaaaaamen.

 28. Kaazi kweli kweli,hapa duniani kazi tunayo.Itafika wakati kila mtu ataanza kusali nyumbani kwake kwa kukosa Imani na Watumishi…. Amani ya Mungu na iamue moyoni mwangu. Amani ya Mungu ikiamua mioyoni mwetu (Wafilipi 4:7) sidhani kwamba mtu awaye yote anaweza kumshawishi mtu kwa maneno ya ufundi wa aina yoyote kuamini kile anacho amini yeye. Ndio maana kukawa na madhehebu mengi sana ni kutokana na mitazamo tofauti tofauti iliyojengwa na watumishi. Kibinafsi ninawiwa sana na watumishi ambao wanatwanga injili kwa kwenda mbele badala ya kuanza kulumbana na mitazamo ya kimadhehebu. (1 Wakorintho 3: 4-5) ” Kwa maana mtu anaposema” Mimi ni wa Paulo,” lakini mwingine anasema ”mimi ni wa Apolo,” je,ninyi si wanadamu tu? 5. Basi Apolo ni nani ? Ndiyo,Paulo ni nani? Wahudumu ambao kupitia wao mlikuja kuwa waamini,kama vile Bwana alivyompa kila mmoja.6. Mimi nilipanda,Apolo akatia maji,lakini Mungu akaendelea kuikuza.

  Sioni tatizo kwa TB.J,tena mara nyingi sana nimemsikia akiwashauri waumini wa makanisa mengine ambao wamekuja kufunguliwa katika kanisa lake kutokuhama kwenye huduma walizokuwapo awali… Kila mtu ana Roho Mtakatifu ndani yake,ni vizuri kumuuliza yeye kuliko kupima kwa akili za kibinadamu. Nakumbuka kuna siku nilikuwa jirani na mtumishi fulani nikiwa ninasoma gazeti ukurasa wa michezo.Katika ukurasa huo kulikuwa na matokeo ya Mechi ya yanga na simba.Yule mtumishi tulikuwa naye katika gari akaniambia maneno yafuatayo ” NAMSHANGAA SANA MUNGU KABLA HUU MPIRA HAUJACHEZWA ALINIAMBIA MATOKEO”.akaendelea kusema ” HUWA NASHANGAA SANA KWA NINI MUNGU ANANIAMBIA HATA VITU KAMA HIVI.. Nachoona hapa kila mtu anapokea kwa jinsi yeye alivyomuwekea Mipaka Mungu.Kuna watu wanaend Makanisani lakini hawaamini kama kuna kunena kwa Lugha . Lakini pamoja na kutoamini kwao haimaanishi kuwa kunena kwa Lugha hakupo.. Tusimuwekee Mungu mipaka.

 29. Ndugu Nduta,

  Unasema tunaopinga tunapinga tusichokijua….Je wewe unayetetea unatetea unachokijua? Au unatetea unachoona kwenye screen kwa dakika chache? Unajua kinachofanyika behind the scene? Unajua TB Joshua anakiri nini? Kwako miujiza ndio kilele cha imani? Nenda India utawakuta kina Sai Baba uone Miungu yao ikitenda miujiza na kuwapoteza mamilioni ya Wahindi!

  Biblia yangu nayosoma inaonyesha Wateule watapotezwa kwa Miujiza….sio kama ulivyosema kwa Nabii Tito kuwaambia watu wavute sigara …..! Hebu rejea tena mafundisho ya Yesu……Kuponya na Miujiza si ISHARA TU ya kuwa Mungu yu pamoja na Mtenda mijuiza! Rudia tena Biblia yako upya ……”Na manabii wengi wa Uongo watatokea na kudanganya wengi” …….”NA MANABII WA UONGO NAO WATATOA ISHARA KUBWA NA MAAJABU WAPATE KUWAPOTEZA YUMKINI WATEULE” Haya ni maneno ya Yesu! Sio yangu wala ya Paulo! Wateule hawatapotezwa na kuambiwa wavute sigara….au Pombe si dhambi……..au waende wakazini! Wateule huwa wameishavuka ufahamu huu wa msingi wa kuishi maisha ya Kikristo!

  Kumbuka kuwa Roho ya udanganyifu na upotevu haitatoka NJE YA KANISA……bali ndani ya Kanisa….Kama Paulo alivyolionya kanisa la Kwanza…….” NAJUA MIMI BAADA YA KUONDOKA KWANGU MBWA MWITU WAKALI WATAINGIA KWENU ( watakua kama wakristo kwa kila kitu) WASILIHURUMIE KUNDI. NA KATIKA NINYI WENYEWE ( ndani ya kanisa, ndani ya imani) WATAINUKA WATU……(Matendo 20: 29-30)

  Hivyo ndugu yangu Nduta….huyo Nabii anayetabiri Mipira ya Miguu …..mara kiongozi fulani atakufa….Je hujiulizi kuwa mbona Rumi kulikuwa na michezo mingi wakati wa Paulo…….Je uliona tabiri za aina hiyo kwa Paulo?

  Narudia tena….Miujiza si Ishara tu kuwa anayeifanya anatembea na Mungu…..! Huo ni uchanga wa kutoijua Imani hii….! Simwangalii mtumishi yoyote anayesema wa Bwana kwa miujiza tu! Uhuru huo kanipa Yesu Mwenyewe kwa kupitia maneno yake……! Kuna Yesu wa Biblia na kuna Yesu mwingine….kuna Injili iliyo wazi katika Maandiko na kuna Injili nyingine…….Paulo kafundisha hivyo……..! Hivyo nina Uhuru kabisa kwa kumtilia mashaka mtenda miujiza huyu wa Nigeria…..!

  Mungu atusaidie siku hizi za mwisho….zilizojaa roho za ukengeufu kwa ajili ya kuwapoteza hata wateule…….!

 30. Wapendwa,

  Kwa wale wasiofahamu manabii wa uongo, Manabii wa uongo ni kama

  1. Wale wanaosema Yesu anarudi tarehe fulani na unabii wao hautimiii

  2. Nabii wa uongo ni kama yule Nabii Tito anayefundisha watu kuvuta sigara na kunywa pombe na kuoa wake wengi

  3. Nabii wa uongo ni wale ambao wanaombea watu wafe kila kukicha ni kuuwa huyu au yule.

  4. Nabii wa uongo ni yule ambaye hapendi kuona watu wanabarikiwa au wanaponywa au wanaokolewa au chochote chema kikitokea kwa wana wa Mungu

  Neno la Mungu linasema kila kipawa chema hutoka kwa Mungu Yakobo 1:17 Kila kutoa
  kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeuka geuka.

  Mithali 10:22 BARAKA YA BWANA HUTAJIRISHA WALA HACHANGANYI HUZUNI NAYO (THE BLESSING OF THE LORD MAKES RICH AND ADDS NO SORROW TO IT)

  YOHANA 10:10 NALIKUWA WAWE NA UZIMA KISHA WAWE NAO TELE

  AHSANTE

 31. Wapendwa,

  2 Petro 2:9,10,11 Inaongelea watu wenye kudharau mamlaka, wenye ushupavu, wenye kujikinai HAWATETEMEKI WAKIYATUKANA MATUKUFU.

  Kwa ujumla sura hii nzima inaongelea watu (manabii na walimu wa uongo pia) ambao wanadharau wapakwa mafuta na wakikufuru juu ya mambo wasiyoyajua. mstari wa 10 unasema kwa kiingereza (self-willed, they are not afraid to speak evil of dignitaries; …).

  T.B. Joshua ametumika na Mungu kutuponya wengi. Amefungua watu wenye vifungo wengi.

  Mimi naruda tena SIWEZI KUKUBALIANA NA MTU YEYOTE ANAYEPINGA MATENDO MAKUU YA MUNGU AMBAYO YAKO DHAHIRI NA WAZI KABISA.

  NINASIMAMA KINYUME NA WOTE WANAOPINGA KAZI YA MUNGU KUBWA NA YENYE UTUKUFU KAMA HII YA T.B. JOSHUA.

  NA BILA KIFICHO NINAMASHAKA MAKUBWA NA WOTE WANAOMPINGA T.B. JOSHUA. KWA SABABU SIJUI NI INJILI GANI WANAYOIHUBIRI WAO.

  MTUME PAULO ANASEMA INJILI YETU HAIKUJA KWA MANENO MATUPU BALI KWA NGUVU 1 wakoritho 2:4, NA NENO LANGU NA KUHUBIRI KWANGU HAKUKUWA KWA MANENO YA HEKIMA YENYE KUSHAWISHI AKILI ZA WATU BALI KWA DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU

  1 Wakorintho 4:20 Mtume Paulo anaendelea kusema: MAANA UFALME WA MUNGU HAUWI KATIKA NENO, BALI KATIKA NGUVU.

  Mtume Paulo alikuwa anakemea walimu na manabii wa uongo waliokuwa wanapingana na naye kwa maneno matupu tu.

  Yesu alisema ikiwa natoa pepo basi ufalme wa Mungu umewadia Luka 11:20,

  Mimi nasema hakuna FREEMASON ANAYEWEZA KUFANYA MIUJIZA. Vile vile hata hao mnaopinga T.B. Joshua hamna uwezo wa kufanya muujiza wowote na ninatia Mashaka kama mnafanya kazi ya Mungu.

  Ubingwa wenu ni kupinga msichokijua.

  YOHANA MBATIZAJI ALIPOINGIWA NA WASIWASI YESU ALIWATUMA WANAFUNZI WA YOHANA WALIOKUJA KUTAFITI UKWELI, AKAWAAMBIA WAKAMWABIE YOHANA WALIYOYAONA KWA MACHO YAO: Luka 7:20 “VIPOFU WANAPATA KUONA,VIWETE WANATEMBEA, WENYA UKOMA WANATAKASKA, VIZIWI WANASIKIA, WAFU WANAFUFULIWA, MASIKINI WANAHUBIRIWA HABARI NJEMA.

  Tatizo la wapingaji wote huwa hawana chochote cha kuonyesha walichofanya wao

  Mbarikiwe

 32. Daniel
  kabla sijafungua hii post TB Joshua muda mchache tu uliopita,nilikuwa natafakari siku moja huko nyuma Mwl wangu wa kiroho alipokuwa ananifundisha namna za ushuhuda kupitia andiko hili Yoh 9:25,”NALIKUWA SIONI SASA NINAONA” nalikuwa namuona na kumsikia tena nikiwa nimezama ktk tafakari,kwani kabla ya hapo nIlikuwa nimeshuhudia kanisa matendo makuu aliyonifanyia Bwana Yesu kwa urefu na namna isiyo faa

  Barikiwa Daniel

 33. Bila shaka watu waliofunguliwa matatizo yao kwa watumishi mbalimbali ambao watu wanakuwa na Mashaka nao ukiwauliza swali kuhusu mtumishi huyo jibu litakuwa kama la huyu ndugu hapa chini ambaye Mafarisayo walitaka kumlazimisha kuamini kuwa Yesu hakuwa mwana wa Mungu.
  – ( YOHANA 9: 25-27)

  25. Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona.

  26. Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani?

  27. Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?

 34. Wapendwa,

  Kwa kweli naachwa mdomo wazi na comment za watu wengi kuhusu mada hii. Hebu ngoja niendelee kumjifunza kila mmoja anaye comment kuhusu hili. Kwa wanaompinga na wanamkubali T.B.JOSHUA, la muhimu la kujiuliza ni kweli wote mnaongozwa na Roho Mtakatifu katika jambo hili? Tumeshindwa kweli kukaa chini na kumuomba huyu Roho Mtakatifu aonaye sirini na afundishaye sirini kwa umoja wetu kama mwili wa Kristo ili atufunulie kuhusu “nabii” huyu?

  Kwa nini tunataka kujeruhiana wenyewe kwa wenyewe wakati tunaye Roho Mtakatifu? Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa kila aliye kinyume yetu si wa ufalme wa Mungu, lakini aliye upande wetu ni mwenzetu. Na hili lilitokana na wanafunzi wake kulalamika kwake kwamba wamewakuta watu wengine wasiowajua wakitoa pepo na kuponya magonjwa. Pia akasema pepo hawezi kumtoa pepo mwenzake, ingawa anaweza kutabiri na kuona mtu aliye wa upande wa Mungu na kusema wazi kama alivyofanya yule kijakazi wa kike katika Matendo 16:16 na yale mapepo yaliyowararua watoto wa Skewa kwenye Matendo 19:11-16.

  Lakini kamwe pepo hawezi kumtoa pepo mwenzake kwenye mwili wa mwanadamu. Kumbuka pia Yesu aliwaonyo wanafunzi wake kwamba wasifurahi sana kwa kuwa pepo wanawatii bali wafurahi kwa kuwa majina yao yameandikwa mbinguni. Hapa Yesu alikuwa anajaribu kuwaambia wanafunzi wake kwamba kumtoa pepo ni kazi rahisi sana, lakini ku-mantain jina lako liendelee kuandikwa kwenye kile kitabu cha uzima ndio kazi kubwa!

  Sasa mimi nawaomba, sisi wote kama Wana SG, ambao tumeokolewa kwa Neema ya Mungu na tumejazwa na Roho Mtakatifu, na Roho wa Mungu anakaa ndani yetu na anaongea nasi kwenye mambo mengi sana pale tunapoomba kwake atujulishe juu ya mambo hayo, kwa nini tusikae chini kila mmoja wetu na kwa umoja wetu (hata kama hatupo pamoja)tuombe kufunuliwa na Roho juu ya nabii huyu!

  Kama wengine walivyosema mambo ya rohoni hujulikana na watu walio na Roho wa Mungu, kwa akili na ufahamu wetu wa kawaida kamwe hatuwezi kuyajua haya. Pia huwezi kuwa mtu wa rohoni kama husomi na kuweka kila kitu katika kipimo sahihi cha neno la Mungu. Miujiza pekee haiwezi kutuhakikishia kuwa huyu ni nabii wa uongo au nabii wa kweli, mpaka hapo neno la Mungu litakapokuwa limesimama juu ya miujiza yote (kama ilivyokuwa kwa waganga na wachawi wa Farao wakati wa mapigo kumi katika nchi ya Misri, nguvu ya Mungu ilisimama na wachawi wote wakatimua mbio na kumwacha Musa akitamba na Mungu wake), ndipo tutakapokuwa na uhakika kwamba miujiza hii inatoka kwa Mungu.

  Nawaombeni tena, punguzeni jazba na maneno makali juu ya T.B. Joshua na juu yenu wenyewe kwa wenyewe, maana hata Haruni na Miriamu walilalama hivi hivi juu ya Musa kuhusu ndoa yake na Mungu aonaye na kusikia sirini akawasikia na wote tunajua yaliyompata Miriamu, bahati yake Haruni vazi la Ukuhani lilimlinda. Lakini kwa upande mwingine Nabii Nathani hakumuonei aibu Mfalme Daudi kumwambia ukweli juu ya dhambi aliyoifanya kwa mtumishi wake Uria kwa kuzini na mke wake pamoja na kwamba Daudi alikuwa mpakwa mafuta wa Bwana. Hivyo hii inaondoa kabisa ile dhana inayojengeka kwa kasi sasa ndani ya watu wa Mungu kwamba tusiwaseme vibaya watumishi wa Mungu, alimradi tunachokisema tuwe na uhakika nacho katika vigezo vyote vya neno la Mungu au kile ambacho Roho Mtakatifu amekifunua kwetu.

  Ufunuo wowote anaopewa na Mungu, mtu wa Mungu hupewa pia hekima ya kuufikisha ufunuo huo. Kama hakuna hekima ya namna ya kuufikisha ufunuo huo, basi ufunuo huo huleta uharibifu zaidi kuliko kujenga mwili wa Kristo na ni afadhali kunyamaza kimya kuliko kuufikisha ufunuo huo; na hili ndilo ninaloliona linataka kufika hapo juu ya Nabii T.B. Joshua.

  Naomba tufunikwe na neema na hekima ya Mungu ipitayo akili zetu pale tunapolijadili jambo hili.

  Baraka kwenu nyote.

 35. Ndugu Nduta,

  Naomba uandike ukiwa objective…….nikiwa na maana tumia Maandiko kujenga hoja zako…..hasa kwa sababu tunayoyaandika yanahusiana na Imani ya Kikristo….na mwamuzi wa mwisho huwa ni NENO LA MUNGU.Lakini pia kama umeshindwa kutumia Maandiko basi tumia hata hekima ya kutoa na kujenga hoja………!

  Hebu angalia ulichoandika

  “…..KITU KIMOJA NINACHOKIELEWA MIMI NI KUWA KILA MTU AMBAYE NI “MPINGAJI SANA” UKIMFUATILIA MAISHA YAKE AU MAISHA YA WAPINGAJI KWA UJUMLA HUWA YAMEJAA “UTATA”.

  Unatumia kigezo gani kusema hayo……Je experience yako ndio mwamuzi? Je anayekubali kila kitu ndio wa Rohoni? Utasemaje Kuhusu Biblia inayotuonya kwa maandiko mengi tusikubali kila Roho?Utasemaje maneno ya Yesu aliyotuonya na Manabii wa Uongo? Utasemaje juu ya Paulo ….hasa ukisoma 1Thesalonians “Maana ile siri ya kuasi hata sasa inatenda kazi “….au aliposema …”MAANA WATU KAMA HAWA NI MITUME WA UONGO …….WANAOJIGEUZA WAWE MITUME WA KRISTO…..WALA SI AJABU MAANA SHETANI MWENYEWE HUJIGEUZA AWE MFANO WA MALAIKA WA NURU…..” 2COR 11 :13-14…… Wewe na Maneno ya Mungu nani tumsikilize? Au utasema pia maisha ya PAULO yamejaa utata? Na kwa nukuu yako hapo juu ina maana maisha ya watu ambao unakutana nao katika Mtandao na kupinga unachokiamini wewe wana maisha ya utata? ……..wewe Ni nabii…? Naomba mtetee Nabii Joshua kwa hoja za Maandiko wala sio hisia……..!

  Je kama wanaopinga wana maisha ya Utata…..Je wanaokubali kila kitu kinachosemwa mimbarini……wana maisha yaliyonyooka? Waberoya walichunguza Lile neno waliloambiwa na Paulo….na wakaitwa Waungwana…..sembuse sisi kuchunguza unabii wa Nabii anayetabiri mambo ya Ligi ya Kombe la Africa……na ambako katika “Sinagogi” lake kuna Maandiko ya “Allah U Akbar” yakiwa pamoja na msalaba? kumbuka pia Kanisa ni kusanyiko la Waumini…Je tuko katika Kipindi cha Sinagogi…..? Rudia kitabu cha Matendo ya Mitume na historia ya Kanisa….jinsi Imani ya Kristo ilivyojitenga na Kuabudu katika Masinagogi….! Isije ikawa Nabii huyu ndiye yale Maandiko tunayoonywa katika Ufunuo……”Nao sio bali ni Sinagogi la Shetani”Ufu 2:9

  Na kwa kukuelimisha Kumwita Nabii Joshua Ni Free Mason HATA Nabii wa Uongo hakuna kufuru ya aina yoyote….hata kama kweli si Nabii wa Uongo…..! Unaingia tu katika kigezo cha kukosa ufahamu wa huyo nabii ….Na tukitumia Maandiko tutasema Hujui Utatendalo…..wala hiingii katika category ya laana…….! Kama Kweli ni Nabii yeye Ni Nabii wa Mungu…..Hebu nipe Andiko la kuthibisha kwamba Nikimwita Nabii Joshua Nabii wa Uongo nitakuwa NAKUFURU…..!? Rudia Biblia yako vizuri wapi Laana inapatika ndani ya Biblia……..au rudia maneno ya Yesu mwenyewe kuhusu laana……!

  Kwa taarifa yako tu, wengi tulipinga kuhusu Nabii wa Mizizi Ambilikile na tukaambiwa na wengi ni wapingaji wa Kila kitu……Tunalofanya ni kulionya Kanisa la Kristo…..kutomeza kila kitu kinachokuja kwa jina la Kristo katika siku hizi za Mwisho…….Hilo ndilo linalotusukuma baadhi yetu……..na kama Hatutaeleweka naamini Mungu ataelewa Nia zetu….na kutusamehe pale tunapokosea!UBARIKIWE.

 36. Ndugu zangu,

  Naomba niongezee kwa kusema kuwa kuna “walokole” wengi sana ambao wanajifanya wa kiroho hata kuliko Mungu mwenyewe.

  Yaani ukifurahia michezo eti wao wanakuona una kasoro. Ukivaa vizuri wanakuona una kasoro. Hebu tuache ukiroho wa uongo na kweli.

  Mungu aliyetuumba na kutuweka hapa duniani anajua tutafurahia mambo mazuri kama michezo. Mungu alikuwa anamtembelea wakati wa kupunga Adam na hawa na ku” enjoy fellowship”. yaani kuwa na maongezi mazuri tu.

  Ulokole wa kuhukumu kila kitu unachokiona ndio matokeo yake. Sasa mnahukumu mpaka watumishi wa Mungu. Hata akina “Kora” na akina “Miriamu” walikuwa na hoja “nzuri” tu lakini Mungu alipoingilia kati waliumbuka.

  Sasa mimi sipendi vitisho na siviungi mkono lakini angalizo tu : Ni vizuri kuwa makini na matumishi juu ya Mambo tusiyoyajua vizuri.

  Na mkumbuke kwamba hamna vigezo vyovyote vya kumpinga T. B. Joshua ZAIDI YA KUONGOZWA NA HISIA TU. “ETI MIMI SIJAWAHI KUWA NA MSUKUMO” AU ETI MAMBO YA MPIRA YANA UMUHIMUGANI” YAANI NI MAONI TU YANAYOTOKANA NA KIWANGO CHA UELEWA WENU.

  KITU KIMOJA NINACHOKIELEWA MIMI NI KUWA KILA MTU AMBAYE NI “MPINGAJI SANA” UKIMFUATILIA MAISHA YAKE AU MAISHA YA WAPINGAJI KWA UJUMLA HUWA YAMEJAA “UTATA”.

  WENGI WA WAPINGAJI HUWA HAWANA MAISHA YA KUMTUKUMZA MUNGU KWA LOLOTE UKIOONDOA KUHUKUMU NA KUJIONA KUWA WAO NI WA KIROHO ZAIDI. LAKINI UKICHUNGUZA UTAONA HAKUNA CHA UKIROHO WOWOTE BADALA YAKE KUNA UTATA KIBAO TU.

  SIYO LAZIMA KUMKUBALI T.B.JOSHUA LAKINI KUMWITA KUWA NI NABII WA UONGO NA NI FREE MASON NI KUFURU KWA SABABU HAINA UKWELI WOWOTE ILA NI UELEWA BINAFSI TU.

  LA KUKUMBUKA TU NI KUWA UKITENDA KOSA ETI KWA KUWA HUELEWI HIYO HAITOSHI KUKUFANYA USIWE NA HATIA. KWA KIPIMO HICHO HICHO MKITUMIACHO NDICHO KITAKACHOTUMIKA KUWAHUKUMU NA MAMBO YENU.

  AHSANTE

 37. Wapendwa,

  Mimi naomba mtu mmoja kati ya hao wanaompinga T. B. joshua wananiembie ni wapi au lini ambapo FREEMASON walifanya muujiza wowote?

  Huyu ndugu yangu wa NEW HOPE MINISTRY (Huduma ya Matumaini Mapya). Ni matumaini gani unayowaletea watu huku ukipinga nguvu za Mungu.

  2 Timotheo 3:5 Inasema siku za mwisho zitakuwako nyakati za hatari…Kutakuwako na watu wenye MFANO WA UTAUWA . LAKINI WAKIKANA NGUVU ZAKE, HAO NAO UJIEPUSHE NAO.

  uliona wapi mfuasi wa kristo akipinga utendaji wa Nguvu za Mungu?

  Mungu amesema ishara zitafuatana na hao waaminio. Marko 16:15

  Mbarikiwe

 38. no comment, sijawai kumsikiliza TB Joshua, sijawai kuwa na msukumo wa kumsikiliza, sijui chochote kuhusu yeye.

 39. DADA NEEMA MARTIN,
  Hongera kwa “kufumbuliwa macho” = “KUFUMBWA MACHO ZAIDI”.

  Kwanza kabla sijaendelea naomba ujibu swali hili “IBADA YENYE UTULIVU WA KIMUNGU” NDIO NINI?

  Na kama kweli hiyo ibada ipo, je “IBADA ISIYO NA UTULIVU” NDIO INAKUWAJE?

  Swali la pili; Je tangu uangalie mahubiri na mafundisho kwenye hiyo tv UMEWAHI KUAMBIWA NA ROHO WA MUNGU kuwa hapo “sipo”. Alipokuambia ulihoji ni kwanini? Kama la; NI KWANINI UKUBALI KUFUMBULIWA MACHO NA MTU WAKATI NI KAZI YA ROHO WA MUNGU HIYO? -Siri za rohoni azijua ROHO wala si MTU. 2COR…

  Nasubiri majibu toka kwako dada.

 40. Ndugu Nduta na Mrs N.R.O

  Unawaita waompinga Nabii Joshua ni kuwa ni ni wakristo wa mwilini… na Mrs N.R.O anasema kumpinga Nabii Joshua ni ufarisayo! Je kukubali kazi ya Nabii Joshua inakufanya uwe mkristo wa Rohoni? Na ni kweli kumpinga Nabii huyu wa Nigeria ni kuwa Mfarisayo? Utasemaje kuhusu maneno ya Mungu kuwa tuzichunguze kila roho? Kusema simkubali Nabii Joshua kama Nabii wa Mungu hakunifanyi niwe wa mwilini na kumkubali hainifanyi pia niwe wa rohoni! Wala hakunigeuzi na kuwa Farisayo!

  Mimi nina maswali mengi dhidi ya Nabii Joshua…Lakini siamini kabisa yanaweza kuniondolea Neema ya Wokovu toka Kwa kristo! Kwani nina Maandiko mengi mno ya kuiuliza kazi yake…..kama vile vile wanaomtetea walivyo na maandiko pia ya kuitetea kazi yake….!

  Kwangu mimi sioni mantiki ya Kutabiri matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu kumfanya huyu Jamaa awe ni Nabii wa Mungu……wangapi wametabiri matokeo ya mpira miguu na ikawa….Je hii inawafanya wawe manabii….au kwa kuwa yeye anatumia jina la Yesu? Juzi juzi Nigeria wameuawa Wakristo zaidi 125….Nabii Joshua alikuwa kimya! Kwa hiyo kwa Mungu mpira wa miguu ni wathamani kuliko mamia ya wakristo waliouawa katika Ibada? Mpira wa miguu una faida gani katika utukufu wa Jina la Kristo?

  Kutabiri vitu vikawa kweli hata viwe vya Kimungu havifanya mtu huyo akawa na ujumbe toka kwa Mungu……hiyo ni ABC ya msingi katika Imani yetu…! Angalia Matendo 16:16 yule binti aliyekua na roho ya uaguzi…..alimfuata Paulo siku nyingi na kusema kweli kabisa juu ya Paulo……! Lakini alikuwa na pepo mchafu…..!! Kwa nini mimi sasa nisiwe na mashaka na na huyu Nabii?

  Kuna maswali mengi mno dhidi ya Nabii Joshua…..sikubaliani kwa sehemu na critics za ndugu Lwembe dhidi ya Nabii Joshua…Lakini kwangu mimi msingi mzima wa Imani ya Nabii TB Joshua unazaa maswali mengi mno……! Kama tukiyaangaza hapa tutawakwaza wengi…… !

  Kinachonisikitisha sana kwa Wapendwa wa leo ni miujiza kuwa Kigezo kikuu cha utendaji wa Mungu! Kumbukeni kwamba Yesu alikuja ulimwenguni kufanya zaidi ya Miujiza! Alifundisha pia! Tunapomwangalia Yesu wa Biblia tunamwangalia kwa miujiza yake na mafundisho yake pia! Huwezi kuvitenganisha! Na tunapowaangalia watumishi wowote wanaodai wana ujumbe toka kwa Yesu, hatuwaangalia kwa Miujiza tu……tunaangalia hata kwa kile wanacho kikiri na kukifundisha! Kwa kigezo hicho Nabii TB Joshua analeta utata mwingi katika mwili wa Kristo……..

  Na kumbukeni pia ni Yesu Mtenda miujiza aliyetuonya kuhusu Watenda miujiza ambao wanaweza kuwapoteza hata Wateule!

 41. Ndugu yangu Emma na wengineo,

  Kwanza napenda ieleweke kuwa tunachokizungumzia hapa ni huduma na si mtu binafsi. Ndipo huduma ya TB Joshua nimeifananisha na huduma ya Balaam yule nabii. Nafahamu kuwa wengi wamekwazika katika hilo, lakini bado wanalo jukumu kama watu wazima la kuyakagua hayo niliyoyasema katika Maandiko kwanza, ndipo waje na maelezo yao yenye kunikosoa au chochote kile wanachotaka kukisema. Mimi nimewawekea hapo “Statement of Faith” au ‘Ukiri’ wa huduma hiyo ambao sijauona ushahidi wake katika Biblia. Kama ninyi mmeona sehemu yoyote ile katika Biblia inayowaambia kuwa “Roho Mtakatifu alishirikiana na Baba na Mwana kuumba ulimwengu” mlipaswa kutuonesha hilo badala ya kutuletea hisia zenu zituongoze katika kuwafuata hao manabii wenu!!!

  Balaam alikuwa nabii. Kwa taarifa yenu, nabii ni mtu anayeweza kuwasiliana na Mungu. Hiki ni kipawa ambacho mtu huzaliwa nacho. Vipawa havina majuto. Kwa hiyo kipawa chochote lazima ukikague kulingana na Maandiko, maana wengine wamepewa hivyo ili wapate kuwapoteza watu!!

  Wengi wetu hupenda sana kumshirikisha Roho Mtakatifu katika mambo yetu na semi zetu ili kuwajengea hofu watu wote walio kinyume nasi! Huyo Roho Mtakatifu mnayedai anawaongoza, sijui ni yupi! Kwani huwezi kujazwa Roho Mtakatifu nje ya Neno la Mungu! Kazi ya Roho Mtakatifu ni kukuongoza kulitii Neno la Mungu. Neno la Mungu ndilo Roho Mtakatifu! Sasa, iweje wewe ujipachikie maneno yako kama huo ‘Ukiri wa Imani’ ambao hauomo katika Biblia halafu umsingizie Roho Mtakatifu? Kwanza kule kuwa na ukiri wa jinsi hiyo peke yake huonesha kuwa unalo Fundisho lako nje ya kile Roho Mtakatifu alichokiweka!

  Huo “Muunganiko na Roho wa Bwana” utaupata wapi nawe ukiwa uko nje ya Neno lake? Ubatizo unaokuleta katika muunganiko huo unaukataa, sasa utajiunganishaje, kwa nguvu?? Huwezi kujazwa Roho Mtakatifu nje ya Ubatizo wa Jina la Bwana Yesu Kristo kama walivyofundisha mitume (Mdo 2:38). Yeyote anayefundisha ubatizo tofauti na huo, Biblia inasema amelaaniwa, sasa kama aliyelaaniwa hujazwa Roho Mtakatifu, hilo ningependa kujifunza kutoka kwenu!!

  Jamani, acheni kutembea huku mmefunga macho, mnajiridhisha kwa uongo mkitegemea utageuka uwe ukweli!!! Nabii akiinuliwa leo hii, atakuja na Ujumbe ambao utakuwa sawa sawa na Neno la Mungu kama lilivyo katika Biblia, tena ni lazima Huduma yake iwe imenenwa humo kimbele!

  Mnauza Haki yenu ya mzaliwa wa kwanza katika Kristo kwa vimiujiza na mafanikio ya kimwili kama Esau (Mwz 25:33-34), mtakuja kuijutia maana hamtarudishiwa tena.
  Jihadharini na Roho za Dini, huu ndio wakati wake, zimeachiliwa hizo zitudanganye kwa miujiza na mambo makubwa makubwa, lakini yote si ya ki Maandiko!!!!!

  Ole wetu!!!

 42. Wapendwa,

  Kwa wale wanaomtetea Nabii Joshua na hata wanaompinga kigezo kinatakiwa kuwa katika maneno ya Mungu tu….

  Lakini mnaposema ni “Nabii wa kizazi hiki” au “Ni baraka ya Ulimwengu wote hasa ni baraka ya Afrika” Maneno haya yanasimama katika lipi hasa?

  Ni baraka zipi TB Joshua ameleta Afrika? Tuache baraka za kimwili…zipi baraka za Kiroho ambazo unaweza kusema Afrika imepata toka kwa Nabii huyu? Acha Afrika tu…turudi Nigeria nyumbani kwake ….!! Nimepata neema ya kutembea West Africa…….kama kuna nchi inayokupa picha halisi kuwa mwafrika ana matatizo makubwa na kukuliza machozi ni Nigeria…..!!

  Hivyo kigezo cha kumpinga na kumkubali kiwe katika wigo Maandiko tu…na wala sio hizo sifa za kishabiki……….

 43. Neema mimi ni mmoja wa ambao amani ya moyo wangu haijamkubali TB Joshua,Tuache unafiki wanayo ibada inayoeleweka pamoja na mafundisho yanoyoeleweka,na wala sina haja ya kumnenea mabaya kwakua moyo wangu hamjamkubal TB Joshuai,kila mtu Mungu amempa mtumishi wake kwa jinsi ya aina yake ili apate kupokea,Ndiposa utakuta mpendwa anashuhudia kwamba akihutubu mtumishi fulani uwa ninapokea na huyu mwingine wala sipokei.Mtume Paul alihubiri injili ya wasiotahilriwa(mataifa)Mtume Petro injili ya waliotairiwa(Wayahudi)kwahiyo usiongozwe mambo ya mwilini kuamua mambo ya rohoni,Wasio watumishi wake Bwana awajua na jiinsi atakavyowashughulikia.
  Neema na Amani ya Mungu na Bwana Yesu iongezwe kwako.

  Amen

 44. LWEMBE ASANTE SANA KWA KUNIFUNGUA MACHO HATA MIMI NILIKUWA NA MASHAKA SANA NA HUYO MTUMISHI T.B KANISA LAKE HALINA MAFUNDISHO NA HALIISHI WATU WENYE MAPEPO HAKUNA SIKU IBADA INAUTULIVU WA MAFUNDISHO YA KIMUNGU YANAYOELEWEKA. NASEMA HIVYO KWANI NIMEKUWA NIKIANGALIA KWENYE TV SIJASIMULIWA .

 45. jamani wewe kaka c.k.lwembe huwa nasoma sana comments zako kwenye mada tofauti tofauti.sijawahi kuona unaandika jambo zuri siku zote wewe ni kuponda tu. yaani natamani sana ningekuona na nifahamu unasali wapi kwasababu ninachokiona mimi wewe ni mfarisayo mambo leo.unakariri maandiko tu na wala hutafakari kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. nakushauri ubadilike kaa chini muombe Mungu wa mbinguni akufungue kutoka eneo hilo. na jambo usilolielewa hebu muulize Roho mtakatifu vyema na ukiona pia kama majibu yanachelewa kaa kimya.

  MNISAMEHE WANA SG KWA MANENO MAKALI UKWELI NI KWAMBA MIMI NAUCHUKIA SANA HUU UFARISAYO MAMBO LEO NDIO MAANA NIKAAMUA KUONGEA NA HUYU KAKA KWA KUTUMIA MANENO HAYO.

  T.B.JOSHUA(PROPHET) NIMEMSIKILIZA NA KUWATCH CHANNEL YAKE KWA MUDA NA NINAKIRI KWAMBA NI NABII WA KIZAZI HIKI.CHA MSINGI ALIYESIKIA PROPHECY HIYO ATAKE ACTION.MTI WENYE MATUNDA NDIO UNAOPIGWA MAWE NA PENYE MIZOGA NDIPO WANAPOKUTANIKA TAI.

  MBARIKIWE

 46. Mimi Nashangaa jinsi ambavyo “wakristo” wakimwili jinsi wanavyomheshimu na kumwogopa shetani. Wanaona kila zuri na jema limetoka kwa shetani.

  Tangu lini Free Mason wakatenda miujiza? Huu ni wivu tu.

  Mungu ametupa wa Afrika Nabii wa kipekee badala ya kumshukuru Mungu, tunaishia kumkufuru Mungu.

  Wenzetu wazungu Mungu akiwabariki na chochote wanakienzi.

  T.B. Joshua ni baraka ya ulimwengu wote na zaidi sana baraka ya Afrika.

  Kinachotakiwa huyu kiongozi wa Afrika achukue unabii huu na autendee kazi. kama ni kumwomba Mungu amponye au kujiandaa na kutengeneza mambo yake ili aende mahali pema.

  Mbarikiwe

 47. Ni kweli ni bora kukaa kimya “kama huna muunganiko na Roho wa Bwana” kwa unaloongea juu ya mtumishi yeyote wa Mungu.

  Ndugu na rafiki Lwembe; Kusema eti “Kwa kifupi huyu ni nabii wa Utatu! Hana jambo lolote lile linalo mhusu Mungu la kutuletea kwa ajili ya kuyajua matakwa au mapenzi ya Mungu juu yetu kwa siku ya leo. Anaye Roho wa Utambuzi tu anayeweza kukamata mambo ya mwilini kama vifo vya wanaulimwengu, mipira na mambo ya namna hiyo na si ya ROHONI.” Ni maneno ambayo siamini yanaweza kutoka kwa “MKRISTO MWENYE ROHO WA KRISTO”.

  Nije kwa ndugu na rafiki mwingine “New Hope Ministry”; Japo ni kama umeuliza swali but ni vyema tukajifunza zaidi kwa habari tusikiazo zikirandaranda, kuandikwa, kusemwa…kuliko kuzikomalia kama vile sisi ndio tumezihakiki. Kwani wewe wakianza kusema unavyopanda kwa kasi katika huduma kuwa una “ufundi uashi huru” sisi/mimi niamini tu bila kujadili na kuhojiana yeye atufundishaye “siri” na kutupa kujua kweli?

 48. Dada Janeth,

  Ubarikiwe!

  Pole sana kwa kuishangaa sana hiyo kauli yangu! Pia kwa kutokunielewa vyema!

  Hayo yote ni kweli, kwa mtu unayemuheshimu na kumpenda, haswa katika anga za kiungu, kauli kama hiyo niliyoitoa kumhusu, ni lazima ikuleta katika hali hiyo. Hata hivyo, katika kauli yangu sikumlenga TB Joshua kama yeye binafsi, bali Ofisi yake ya Unabii. Hiyo ofisi yake, ndiyo niliyojaribu kuileta katika kipimo cha Maandiko ili tuitazame ni nini.

  Biblia, kulingana na Amos 3:7 inatuambia Mungu hafanyi jambo lolote hapa duniani bila ya kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake! Basi nabii ni mtumishi wa Mungu, hivyo huja na ujumbe aliopewa na Mungu, huo ambao Mungu amemfunulia. Basi unaweza kulipima wewe mwenyewe moyoni mwako jambo hili, iwapo Siri aliyokuwa nayo Mungu ambayo anataka kuifanya katika siku na wakati huu ni kuipa Zambia ushindi wa mpira wa miguu katika hizo fainali ya AFCON! Sijui hilo linasaidia nini katika kuufikia Ufalme wa Mungu!? Tazama Matendo 16:16

  Wengi wetu hatuifahamu kwa undani Ofisi ya Unabii, mara nyingi huichanganya na huduma ya watabiri. Kwetu sisi mtabiri hubaki kuwa hivyo iwapo atakuwa ni mpagani au muisilamu (kama marehemu Sheikh Yahaya) au wa dini nyingine yoyote ile isipokuwa ukristo. Mtabiri huyo akiwa ni mkristo, basi sisi moja kwa moja humtambua huyo kama Nabii, haijalishi Neno linasema nini; hata hao watabiri wenyewe hujitambulisha kama manabii!

  Jambo jingine la msingi ni kwamba kwa siku ya leo, Mpango mzima wa Ukombozi, yaani ile ‘Blue Print’ au ‘Mwongozo’ tulikwisha kabidhiwa, ambayo ni Biblia. Kwa hiyo jambo lolote linalotokea, linalohusiana na Mungu, tunayo fursa ya kulikagua kwanza na kujiridhisha, kisha kuamua kuambatana nalo au kulikataa. Naye Mungu huyaheshimu maamuzi yetu hata kama yatakuwa ni kinyume na Neno lake, ambavyo ni sawa na kumkataa Yeye.

  Fursa hiyo ndiyo niliyoitumia. Nimejaribu kuitafuta Huduma ya Nabii TB Joshua katika ule ‘Mwongozo’ ili nijue amekuja katika Roho gani na kuifanya Huduma ipi ambayo Mungu amemfunulia Siri yake, sijaiona! Kama ulipata fursa ya kusoma post ya “Kazi ya Manabii ni Ipi?” siku za nyuma, huko nadhani mambo haya ya manabii yalifikiwa kwa kiwango kikubwa sana, humo unaweza kupata mwanga zaidi wa Ofisi hii ya Manabii kwa vile wote hawa ni sawa, haijalishi anatoka nchi gani, kwani hawayafanyi hayo kwa mapenzi yao bali huyafanya kulingana na Roho anayewatuma. Huyo Roho ndiye tunayepaswa kumchunguza iwapo ni yule aliyeuandika ule Mwongozo tuliopewa au la!

  Kwa vile sijaiona Huduma hiyo katika Maandiko, nilipoitazama nikaiona ni sawa tu na huduma nyinginezo za manabii wa kidhehebu waliotapakaa dunia nzima, kama inavyojieleza Statement of Faith yake. Ni kutoka kigezo hicho, ndipo nikaitazama Huduma hiyo tena katika Maandiko na kuiona ni mojawapo ya zile huduma tulizoambiwa zitatufikia (Mt 24:24). Nazo Huduma hizo ndio hizi zimetufikia!

  Nalo Neno la Mungu halitanguki, basi lazima wawepo wa kudanganywa kama Maandiko yanenavyo. Nayo hali hiyo itaendelea kama tunavyopashwa habari yake katika 2Tim 3:13.

  Basi dada yangu Janeth, Ishara na Miujiza huambatana na Ujumbe au Sauti ya Mungu ikitueleza Siri yake ambayo itatuingiza katika Ufalme wake. Ukiona Ishara na Miujiza inaishia kuuza Maji ya Upako na kumuongezea umaarufu mtumishi bila ujumbe wowote ule kimaandiko, kama huduma hii ya TB Joshua, KIMBIAAAAAAAA

  Bwana akutie nguvu!

 49. TB Joshua ni miongoni mwa watumishi wanaotembea katika ulimwengu wa miujiza katika kizazi hiki, lakini kunatetesi kwamba TB Joshua ni miongoni mwa wanachama wa Free Masons hivi ni kweli?

 50. Ck Lwembe; Huo ni ufahamu wako, na ninakushauri utake kujifunza kwa Roho Mtakatifu kwani ungelizama kwake angelikuthibitishia kuwa hata unayeemwita “Baalam” ni mtumishi wake, Bila ya Roho Mtakatifu kuanza na wewe chochote unaanza nacho katika elimu ya Kristo ni sifuri sio ubatizo wala maji yake! Mungu atusaidie kwa Roho Mtakatifu tuchunge kile tunasema kuhusu watumishi wengine na huduma walizoitiwa. Sisi ni mwili mmoja (Kanisa=Mwili wa Kristo) ila viungo mbalimbali.

 51. Duh! nimetoka kapa, sijakuelewa vyema mt. Lwembe! Namuheshimu na ninampenda nabii TB Joshua.

 52. Baalam mwingine, katika wakati wetu!

  Huyu ni mtabiri mwenye kipawa cha unabii! Katika wakati huu ambapo dunia imegubikwa na giza, nalo giza nene juu ya watu; akiibuka mtu mwenye kipawa kama hicho na kuyatabiri mambo ya jinsi hiyo, basi katika giza kama hilo, mwanga wa simu ya tochi huonekana jua la mchana kwa walio gizani!!

  Ili kumjua kama ni nabii wa kweli au la, chunguza mhimili wake ni nini? Je, ni Mungu gani anayemtumikia? Sentensi ya kwanza kabisa katika ‘Statement of Faith’ yake inasema hivi:
  “The Holy Spirit worked with the Father and the Son to create the world.” Tafsiri ya karibu ya kauli hiyo kuhusu wanacho amini ni, “Roho Mtakatifu alishirikiana na Baba na Mwana kuumba ulimwengu.”

  Licha ya kwamba hajautaja Utatu, maelezo hayo machache aliyoyatoa, katika dhana hayana tofauti na Utatu. Amekwepa kuweka wazi mambo mengi ya imani. Kama Ubatizo, ameuacha ukining’inia katika namna ya ‘tunaamini katika ubatizo wa maji na ubatizo wa Roho Mtakatifu…” msisitizo zaidi ukiwa katika ubatizo wa Roho Mt. maana huo huhusishwa na miujiza.

  Kwa kifupi huyu ni nabii wa Utatu! Hana jambo lolote lile linalo mhusu Mungu la kutuletea kwa ajili ya kuyajua matakwa au mapenzi ya Mungu juu yetu kwa siku ya leo. Anaye Roho wa Utambuzi tu anayeweza kukamata mambo ya mwilini kama vifo vya wanaulimwengu, mipira na mambo ya namna hiyo na si ya ROHONI.
  Jihadharini na mambo ya manabii, msije mkapigwa mihuri ya upotevu!!!

  Bwana atuepushe na ulaghai wa kiroho ulioivamia dunia!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s