Umetenda Mema – Kambua

 Kambua

Kambua ni muimbaji wa nyimbo za Injili  mwenye jina kubwa nchini Kenya, alianza kuimba na kupenda nyimbo za Injili alipokuwa mdogo na watu wengi waliona kilichokuwa ndani yake, baadaye mwaka 2005 akaenda kusomea Muziki nchini  Canada chuo cha Kikristo, Calgary. Na katika maisha yake chuoni, alijiunga na band ya chuo Legacy Youth Conference (LYC). Anasema alipokuwa Canada, hawezi kusahau alipochaguliwa kuimba na Angelique Kidjo kwenye tamasha moja.

Kambua ambaye mama yake ni mchungaji, mbali na nyimbo zake kupigwa redioni na kuonekana kwenye TV pia na tuzo alizopokea haachi kusema kwamba maisha yake ameyatoka kwa Bwana Yesu na kusoma Neno lake mara nyingi.

Muimbaji huyu amekuwa akifanya huduma aliyonayo kwa kushirikiana na waimbaji wengine na kuuinua muziki wa Injili kwa kuiwakilisha nchi ya Kenya na hata Afrika mashariki.

Ametamani kuwa sauti ya wanawake na watoto katika kujenga maendeleo ya nchi zinazoendelea, mbali na shughuli za jamii na uimbaji Kambua pia ni mtangazaji wa Citizen TV, kipindi cha Rauka.

Moja ya wimbo wake unaochezwa kwenye redio na TV za Afrika mashariki

One thought on “Umetenda Mema – Kambua

  1. Bwana Yesu asifiwe!
    Hongera sana mtumishi wa Mungu, Kambua kwa kujaliwa kipaji cha uimbaji na kukitumia vizuri.Kwa kweli tunashukuru sana kwa sababu tunazidi kubarikiwa na nyimbo zako.Mungu akubariki.Amen.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s