Tumsifu Yesu Kristo!

Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Mimi ni mama mwenye Familia ya watoto wawili ninaomba mnisaide kuniombea familia yangu imeingiwa na mfadhaiko mkubwa mtoto wa kwanza kati ya hawa wawili anakunywa sana pombe hata siku nyingine kushindwa kwenda kazini. hajaoa bado. na anavuta sigara sana, vilevile hawa wote wawili hawana mwammko kabisa wa kumfuata Yesu, hawaendi kanisani siku za jumapili, nimelazimisha hawaelewi inaniuma sana; jamani mwenyewe sina mume, ninatamani sana ningepata mume ili niweze kufunga ndoa niishi maisha ya kumpendeza Mungu badala ya kuhangaika na waume za watu hili linanisikitisha sana na kuniudhi mno lakini sina bahati hiyo ya kumpata mume wa kwangu mwenyewe.

Mimi ni mtumishi ninafanya kazi ya kuajiriwa; lakini ofisi ninayofanyia kazi,ina majungu kupita kiasi watu ni waongo sana, wasengenyaji, wana wivu kupindukia washirikina pia wamo, wengi wao hawapendani, kwa kweli; yote haya yanahitaji msaada wa Mungu tu, watu wameonywa lakini hawakubali kujirekebisha, tafadhalini wakristo wenzangu wanamaombi tusaidieni, tunahitaji msaada wa maombi. ninaomba maombi yenu ili kuweza kuokoa familia yangu na kazi yangu.

Stella

Advertisements

6 thoughts on “Tumsifu Yesu Kristo!

 1. Ndugu Stella,pole sana.Yesu anapenda watu walio wazi na wanaotokea kuichukia dhambi(shetani).Nakushauri uombe rehema kila siku.Juu yako we-mwenyewe na juu ya watoto wako.Pia,tafuta kanisa la kiroho likusaidie kukufundisha maombi mbalimbali ili,uvunje minyororo ya pombe,sigara na giza(kukosa mwamuko wa kumfuata Yesu).
  Ukijifunza kuomba itakusaidi kuvunja hata roho za mizimu na urithishwaji wa tabia chafu toka kwa mababu. Precious.

 2. Bwana Yesu asifiwe. Dada pole kwa mapito unayopitia. Napenda kukushauri kuwa, umpe Yesu maisha ili uweze kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Ikatae roho ya uzinzi inayokufuatilia maana kupenda waume za watu sio jambo la kawaida ila ni kazi ya shetani,ikatae hiyo roho omba rehema kwa Mungu na matatizo mengine Mungu atafanya njia. soma Luk18:27,Rum 10:13

 3. Tumsifu Yesu Kristo Milele Amen!

  Kwako Stella

  Ipo njia ionekayo ni nzuri machoni pa mwanadamu lakini mwisho wake ni mauti!

  Kwanza kile kitendo cha KUYACHUKIA unayoyafanya ni NEEMa ya MUNGU kupitia Roho wake anavyotaka uchukue hatua ya kumuabisha shetani. najua katika hari uliyonayo kuna ndoto MUNGU anazokuonyesha lakini bado umekuwa mzito kuamka toka usingizini, kwani shetani amekufunga(unamacho hauoni una masikio hausikii(rohoni)) anakuonyesha uzuri wa dhambi unazofanya mfn anakufikirisha na kukutia hofu kuwa ukiwaacha hao waume za watu hutapata pesa na marupurupu mengine,pia anakuletea raha ya dhambi ya kuzini wakati ni raha ya muda mfupi tu,ndiyo maana kila ukifanya tendo hilo dhimira yako inakushitaki mbele za MUNGU kwani umeisi amri yake ya 6 usizini, tazama yote hayo yamekuwa chukizo mbele ya MUNGU ila anakuvumilia kwa maana ameweka USHINDI MBELE YAKO,angalia dhambi yako ilivyo laana hadi kwa watoto wako nao wamekuwa waasi,usipochukua hatua zilizopo katika Warumi 10:9….UTATESWA SANA kama tulivyoteswa wengine hadi tukakata shauri ndiyo mambo yamekuwa kama ahadi ya MUNGU.

  hiyo laana ya dhambi yako mzazi itaenda hadi kizazi chako cha nne Kutoka 20.2. usipochukua HATUA za kuvunja minyororo/nira alizokufunga ibirisi, MUNGU anataka kukutumia kwa ajiri ya wengi. ULIPOSEMA Tumsifu Yesu Kristo najua wewe ni muumini wa katoliki. sasa Vunja ukuta/nira/kiambata cha udini simama katika NENO la MUNGU yaani BIBLIA chukua hatua ya kuanza kumkaribia Mungu(okoka) ili upate kulitimiza KUSUDI la MUNGU kwenye maisha yako hata hapo kwa hao wafanyakazi wako wenzio wasengenyaji,washirikina nk BWANA atakupa ujasiri wa KUwabadilisha

  Atakubadilisha wewe na familia yako soma Kumb la torati 28;1….. ila kwanza tengeneza maisha yako wewe, patana na MUNGU wako kwanza, zamani hizi ni zile za mwisho soma 2timotheo 3.1-6 ndipo utakapo yaona hayo yanayotendeka katika maisha yako. UKIKUBALI na KUTII utakula mema ya nchi ila ukiasi na kuziendea njia zako unazoziona ni nzuri machoni pako utangamizwa kwa UPANGA.

  kwa maana lazima utoke kwenye maisha yako uliyoyazoea ndipo YESU Kristo aje akae ndani yako kama wanisreil walivyo tazama nyoka wa shaba ndipo Israel ya sasa(wewe) sharti uutazame Msalaba Mwambie YESU UMETENDA KWA WENGI,NITENDEE NA MIMI BWANA,NIPATE KUTANGAZA MATENDO YAKO YALIYO MAKUU ILI KILA ULIMU NA FAHAMU ZOTE ZIPATE KUMTII YEYE

  NENO LA MUNGU NI HABARI NJEMA KWA WAAMINIO,KWA USIYE AMINI KWAKE NI HUKUMU YA MAUTI

  Habari za watoto wako, ukiokoka BWANA atashughulika nao, kwani hautajisumbua kwa lolote bali utajisumbua kwa kuomba na kusali

  Mwl. Mwangomo N

  0717 450 300

 4. Amen, Pole sana kwa matatizo yanayokuzunguka dada Stella, sina hakika kama umempa Yesu maisha yako kwani maelezo yako unataka pia upate mume wa kukuoa ili uachane na waume wa muda, Kitu cha kwanza mpe Bwana Yesu maisha yako kisha upate mahali sahihi pa kumwabudu mungu wako na ukae na Mchungaji akupe ushauri kuhusu mapito unayopitia. Tambua ukiwa ndani ye Yesu yeye ni mfariji na mtia moyo na hakika watoto wako watafika mahali watakuwa watoto wazuri. Maombi pamoja na kufunga ndiyo yanaweza kung’oa milima-Mt 17:14-21. Na pia fahamu kuwa yote yawezekana kwake yeye aaminiye. Mk 9:23, na imani ya kungoa milima imo ndani ya watakatifu yaani watu waliomwamini Kristo Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao. Usikate tamaa tupo pamoja na pia tutakukumbuka katika maombi, Ubarikiwe na Bwana Yesu, Amen.

 5. Pole sana dada Stella. Mungu wetu anasema ‘njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha’. Hapo hakufafanua ni mzigo wa namna (ina maana ni mzigo wa namna yoyote ile). Hebu kuwa na IMANI juu ya Mungu wako na zidisha Maombi.
  “Ombeni bila kukoma” – 1The 5:17

  Na hakikisha unajitahidi kutokumtenda dhambi Mungu wako, mana hata sikiliza Maombi yako, hata kama Unaomba sana usiku na mchana.

  Na nakushauri ufanye Maombi ya kufunga, ni mazuri sana kwa Mungu kujibu haraka maombi yako.

 6. BWANA YESU asifiwe!Dada Stella pole sana jibu la tatizo ulilonalo ni uamue kumpa Yesu maisha yako yeye anasema tumtwishe fadhaa zetu zote!tafuta kanisa karibu yako linalo hubiri habari za wokovu na uokoke ukulie kiroho hapo huku ukiendelea kusikia Neno nalo Neno litakuweka huru, pia unaweza ukauliza huduma zinazo shughulika na kufunguliwa uongee na watumishi juu ya tatizo lako utafunguliwa. Mara nyingine mtu huwa na pepo mahaba na huyo huweza hata kuua mwinzi wa mhusika ili azidi kumyumbisha akikuacha upate mwenzi huwa ni mwenzi wa utata utata ama mwenzi wa mtu au mzee zaidi yako nivituko mtindo mmoja hata husambaratisha ndoa na familia ama pia ikawa ni roho ya kifamilia lakini kwa ujumla ukae na watumishi wenye huduma hiyo uongee nao muhojiane utajua shida ilipo na ufanyiwe maombezi na kufuguliwa(delivarance)kwa mambo hayo ni maombi na kufunguliwa ktk kifungo hicho!inabidi kufunguka na mapepo yanayo kufanya upende waume wa watu yatoke uwe huru na jua bila kufunguliwa ukiombewa kwa mtandao ni rahisi kujikuta unarudia hukohuko!na unaweza ukafunguliwa wewe na familia yako ikaanza kufunguka, mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru kweli kweli!

  Barikiwa,

  Frederick

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s