Glorious Celebration Band

Band nzuri inayovuma kwa sasa nchini Tanzania, kwa uchezaji wao wa staha na sauti zenye kusikika vyema. Kiongozi wa  Glorious Celebration Band Emmanuel Mabisa, aliongea nasi machache kuhusu kazi yao na malengo waliyonayo katika kuujenga mwili wa Kristo.

“Maono yetu ni kufanya huduma mashuleni na vyuoni kwa ajili ya kuwahubiria Vijana Habari njema za Kristo, na pia kufanya matamasha makubwa mbali mbali”

Alkadhalika kundi hili linaundwa na waimbaji mahiri wanaosikika kwenye soko la muziki wa injili na wengine chipukizi wanasikika. Band hii inalelewa na msimamizi mkuu Bishop Mwakang’ata wa Full victory Gospel Church ya Chang’ombe Temeke, Dar es salaam.

Waimbaji wengine wanaounda kundi hilo ni Angel Bernard ambaye ndiye mweka hazima, Chaka Mtunguja Katibu wao, Jesca Honore, Nice Marandu, Davina, Risper, Ima Malisa, Emmanuel Materu, Emmanuel Gripa, Daniel Kibambe, Arone Botto, David Silomba, Ester Peter, Paul Mwakanyamale na Mercy Denis.

Kwa sasa wanajiandaa kurekodi Live Dvd mapema mwezi wa sita mwaka 2012! Hapo awali wamerekodi video ya album yao ya kwanza NIGUSE, unaweza kufarijika kwa kusikia wimbo huu wa NIGUSE,

Mpaka sasa wametimiza mwaka mmoja tangu wameanzisha bendi yao na wametoka na album ya NIGUSE….hata hivyo kama watu walivyozoea kila Ijumaa kuwaona THE ATRIUMS HOTEL, kwa sasa itakuwa wanamtukuza Mungu kila ijumaa ya mwisho wa mwezi, viwanja vile vile.

Tanzania tunajivunia kuwa na waimbaji kama hawa!

19 thoughts on “Glorious Celebration Band

 1. ilke ur song very much kiac kwamba naamka nauckilza every day UMENIFANYA IBADA. GOD BLESS U.

 2. yan nikiamka asubuhi lazim walau nisikie saut zenu guyz,pia nimefurahi rafik yang daniel anam2mikia mungu 2mepoteana mda mrefu once u see this comment u can contact me through this no 0715222734,nawapenda ts susan phocus

 3. Mungu awabarik kwa huduma yenu nzur inayogusa moyo wa Mungu, napenda sana wimbo wa unaweza Yesu, eeh Roho, juu ya mataifa na nakupenda Yesu, lakn jitahidin kuwa barua inayosomeka vema kwa watu ili watu waendelee kumjua Mungu kupitia nyimbo zenu (2timotheo 2:15).nawapenda sana

 4. Mungu awabariki kwa kutenda kazi yake..! Bless you..!
  ..
  Nyimbo za “Mawazo”, “Ee Roho” na “Unaweza Yesu” zinanibariki kwa namna ya pekee..!

 5. from university of dodoma (udom) were i heard of u at first i was really blessed and i am still blessed. goodlucky

 6. i like the way u sing i am blessed abundantly,may the almighty God show u a real way to go in ur ministry.p’se come and visit us at muhimbili fellowship of evangelical students(MUFES) at Muhimbili university..blessings

 7. Mungu awatienguvu kwa kufanya kazi zenye ubora na roho mtakatifu akiwemo.tunategemea mazuri kutoka kwenu mbarikiwe sn.

 8. Mimi kwa kweli nawapenda sana hawa Jamaa.Nilipoiona kazi yao nilishindwa kujizuia nikanunua copy 3 moja yangu 2za ndugu zangu.Na ninahitaji kuwapa mualiko wafike Kanisani kwetu Cha kujiuliza watakuja maana watu wakisifiwa tu ndio huwa inakuwa taabu ILA kazi yao mm naipa tena BIG UP

 9. my first time 2 see u guys i was in A town and i was really blessed and give a challenge that i need more practice
  i pray for you guys that god guide you all the ways every way

  A wish u all the best

  love you!!!!!!!!

 10. gloriuos niliwapenda siku ya kwanza niliposikia wimbo wa niguse na nilipo kuja kuona video ndo nikaelewa kwanini niliguswa na nyinyi sana,,,nawapenda sana ndugu zangu nawaombea kwa MUNGU mzidi kudumu katika huduma ya huimbaji nitaendelea kumpinga shetani kwa ajili yenu kwasababu sitaweza kuvumulia nikimwona anatakuvuruga chochote kile MUNGU ameweka ndani yenu.. YESU manaye mwinua na kumwmbia awapiganie na kuwatia nguvu kila siku,,,..

  nawatakia kila lakheri na MNGU AWENANYI DAIMA.

 11. glourious Mungu awabariki muwe na uimbaji wa kumuinua Mungu zaidi kuliko mambo mengine…!

 12. hakika Mungu awatie nguvu katika kazi hii.msikubali shetani akawateke,ombeni sana mungu awajaze nguvu.Jackson Mndeme niko Mkwawa university.Vijana hawa wananibariki sana.

 13. nawafahamu DANI KIBAMBE baba yake alikuwa ni LEGEND wa muziki wa injili (Mungu amrehemu aliko), namfahamu Emma Mabisa (mkurugenzi) tokea zamani sana, Angel Benard na Jesca Honore kwa kuwataja wachache JAMANI HII NI ZAIDI YA BAND! hawa niwatumishi na pia wanajua wanafanya nini. I WISH ningekuwa DAR!
  USHAURI
  Band imejaa watumishi mashuhuri. Kumbukeni lusifa alikuwa mashuhuri mbinguni msije mkategwa. Pili nashauri kuwe na program ya kuinua waimbaji wachanga ili uwepo wa Band uwe wa kudumu maana siku zote aliyekuja na umaarufu wake ni tofauti na aliyetengenezewa hapo. Tatu MSICHOKE KUOMBA!
  MUNGU AZIDI KUWASIMAMISHA

 14. Amina! Mungu awatangulie katika Utumishi wenu. La msingi ni kutambua kuwa utumishi wa Mungu, mbali na gharama zinazohitaji pesa kutatuliwa, pia kuna gharama za kiroho. Inabidi kujikana mambo mengi, kujikana vile unavyotaka kuwa kwa ajili ya kazi ya Mungu!

  Mtangulizeni Mungu zaidi na mtamani kuwa Mfano Mwema hata kwa vizazi vijavyo. Muwe na nia moja, ya utumishi na mambo mengine ya kibinafsi yasipate nafasi ya kuingilia kikundi chenu!

  Mungu awabariki na kuwapa afya na mafunuo mapya kwa kazi yake!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s