Mtu asipozaliwa kwa Maji na kwa Roho!

Mimi nimeokoka January mwaka huu nimekuwa na maswali kuhusu maana ya TOBA, na nini maana ya ubatizo wa TOBA? na pia kuna mstari kwenye Biblia nikisoma siuelewi vizuri kuhusu ubatizo, unatoka Yohana 3:5 ‘Yesu akajibu Amin Amin nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.’

Hellen Charles

Advertisements

39 thoughts on “Mtu asipozaliwa kwa Maji na kwa Roho!

 1. Baraka Charles,

  Nashukuru kwa maelezo yako hapo juu.

  Sasa unaweza kujibu maswali yangu tafadhali?

  Asante.

 2. Seleli,

  Ni busara na pia kuna faida kubwa sana, ukikaa kimya na kujifunza linapozungumziwa jambo usilolijua, kuliko kuyakurupukia mambo yanayokuzidi kimo!!!

  Kwa muda niliokuona hapa SG, nilitegemea kuwa angalau utakuwa umejifunza kitu fulani, na hivyo ufahamu wako kuongezeka kidogo kwa at least hata mambo ya kawaida; lakini nakuona haujasaidiwa lolote lile, yaani HUNA uwezo wa kujifunza zaidi ya kumimic usiyoyajua!!!

  Kama UBATIZO unaoagizwa ktk Mdo 2:38 ndio huo wanaoutimiza “Jesus Only” basi wao wako sahihi kuliko wewe usiyekijua hata unachokiamini! Na kama wewe kwa UJINGA unaweza ukatangaza kwamba mwanzilishi wa UBATIZO huo ambaye ni RM ndani ya Petro na mitume, yuko TENGE, basi nakuombea kwa Mungu aikubali dhabihu yako ya dhambi kwa Ujinga, asikuhesabie kufuru!!

  Kwa kukuondoa UJINGA uliouzoelea, “Jesus Only” wanabatiza kama jina lao linavyoitwa, “kwa jina la Yesu Pekee” jambo ambalo si la ki Maandiko na hivyo halina faida ya kiungu zaidi ya kukufungia ndani ya jela ya kidhehebu kama wewe ulivyo!!!

  Usiwe mwepesi wa kuyaongelea usiyoyajua, jaribu kuchukua wasaa kuyatafiti kabla ya kuyashobokea, utakuja tukana na visivyotukanika kwa kupenda sifa!!!

  Bwana na akupe HOFU YAKE!!!

 3. Lwembe,

  Acha kuambukiza doctrine mfu iyo ya ”Jesus Only”, wamekuajili au umo uko umekabwa kama Siyi na dude la M23 Commandementali….si useme tu uko kazini hapa! Ishu ya kubatizwa kwa Jina la Yesu tu…ni extremes za Mwanzilishi wa dini/imani yenu( wwe soma yao, akina Jesus Only) je wewe u mmoja wao?

  Ishu ya ubatizo mbona haina shida kuelewa, why una..complicate kwa kuback up madude yenu uko kwa faith yenu tenge jamaa yangu?

  Press on

 4. Raymond,
  Ubatizo wa kweli, ni huo walioutimiza mitume, maji mengi, kwa jjna la Bwana Yesu Kristo! Hakuna ubatizo nje ya huo!!! Kwa siku za nyuma zile za giza la Maandiko, ubatizo wa kidhehebu ulifaa. Kwa ubatizo huo tulihesabiwa Haki na tukaendelea Kutakaswa, tukakomea hapo HATUKUJAZWA RM!!!! Bali kwa leo Neno kamili limefunuliwa, isome Biblia yako kwa leo iko wazi; jitahidi ubatizwe kama Mdo 2:38 inavyoagiza ili uondolewe dhambi zako na upokee vipawa HALISI vya RM na hatimaye UJAZWE!!!

  Ubarikiwe!!

 5. Kuzaliwa mara ya pili ni moja ya kuepka dhambi ya asili na adhabu zake.

 6. isingelikuwa rahisi kwani ingekuwa kama analazimisha watu wamjue,pia mwone paulo alipo pelekwa juu ktk maono hata yeye hakutaka kujitamka wazi na hataleo kunawatu wanadai hakuwa Paulo.jambo muhimu hapa ni kwamba sio mara ya kwanza Mungu kuuvaa mwili,kumbuka alipokwenda Sodoma aliuvaa mwili na akaongea na Ibrahimu na akaishi nae kwa siku nzima,kama pia alivyo kaa na mitume wakati wa kuwakomboa wanadamu,na kule alikwenda kumkomboa Rutu,tazama wakati wa mateso ya Abednego Meshack,pia Mungu aliuvaa mwili na akawa nao kwa muda mle ktk tanuru ya moto,sasa leo kuvaa mwili tena kama mwana aliyezaliwa tayari kawa mwingine,sasa tafakari jina hili Math,1:23 sasa utaona siomwana na wanadamu ni Mungu original,msikie Paulo amjuavyo Tit,2:13,ni Mungu mkuu,sasa kama sio Mungu hata mitume ni waongo,pia mwone mwenyewe ajiitavyo Ufu.1:7:8 sasa hata yeye Alfa na Omega nimwongo?kaka omba pia Yesu akufunulie hili,Amen.

 7. Baraka,
  Umesema kuwa Baba, Mwana, Roho mtakatifu ni sifa.
  Una uhakika kuwa neno baba sio jina bali ni sifa, kwa mujibu wa mwalimu wako aliyekufundisha aina za maneno?

  Na kama Yesu aliposema kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt. alikuwa na maana ya kusema ‘kwa jina la Yesu’ unadhani kwa nini hakusema tu kwa jina la Yesu moja kwa moja?

  Naomba majibu ndugu Baraka!

 8. wapendwa ktk bwana,taabu kubwa inayolipata kanisa leo ni kungangania mapokeo ya dini,sasa ona mitume wangebatizaje kwa jina la Baba na Mwana naRoho mt, wakati wameshafunguka macho ya Rohoni wanatambua kuwa Yesu ndiye Mungu?Yoh,14:8:9, taabu ni kwa kizazi hiki ambacho kinadhania kuwa mitume walikosea kumbe wao ni vipofu,neno linasema tumejengwa juu ya misingi 2 mitume na manabii,kama hamtafuata imani nayale waliyo fanya mkidhania walikosea hapo mmepotea,mnafuata misingi ya Utatu kama nafsi,kweli shetani kawafumba macho.Utatu ni sifa za Mungu sionafsi,sasa ona kweli Baba ni jina? au Mwana ni jina? au Roho mt,nijina?hapana,jina ni moja tu Yesu kristo.mfano,mimi ninaitwa Baraka,wanangu hawataniita Baraka bali Baba,na sasa watu waseme jinalangu ni baba?hasha pia mwana pia ni sifa sijina,kafanyika hivyo atukomboe Yoh.1:14 sasa nikama mwana,lakini ni yeye yule,pia Roho mt,sijina bali sifa,Mw.1:2 sasa Mungu ni Roho yuleyule.sasa nafsi tatu mnazitoa wapi?wapendwa Mungu ni yeye Yesukristo na ubatizo ni kwajina lake tu.

  pia kuzaliwa mara ya 2 sio kubatizwa kwa maji,mafundisho mengi yamewapofusha waamini macho hawajui na wanapotea.sikiliza ndugu kubatizwa hatua ya kutakaswa pia kutimiza kweli yote,lakini kuzaliwa mara 2 ndoubatizo wa Roho mt.ambao Yohana aliwaambia watu waungoje,kwa maana haukuwepo bado Yoh,3:16,sasa kama huo ubatizo wa maji ungelikuwa ndo kuzaliwa mara 2 yohana asingeliwaambia wasubiri mwingine.Mdo.11:15:18,haleluyaaa,unaona huohapo ubatizo wa Yesu na hapo mtu anakuwa amezaliwa mara ya 2,sikunena kwa lugha bali kuipoakea nguvu ya Bwana,unakuwa kiumbe kipya cha kiroho yakale yanapita unakuwa mwili wa Kristo,haleluyaaa,achana na mafundisho duni,Yesu ni yeyeyule jana leo na hata milele,wengi wamebatizwa kwa maji wakajua wamezaliwa mara 2 nawapa pole,wengine wananena kwa lugha wanadhani ndowamempata Yesu,angalia maisha yako unayo ishi yawe kielelezo cha wokovu wako,haleluyaa,kama hujaelewa mwombe sana Mungu akufungue macho,amen.

 9. Ndg Golanga,

  Ni kweli maneno haya mawili, KUOKOKA na KUONGOKA, yamekuwa yakitatiza kidogo kutokana kuyachanganya kwetu katika maana pale tunapoyaleta kuwa katika maana moja. Basi kwa kadiri ya Maandiko, hebu sote tuyatazame kwa pamoja ili tuyaone yanavyojifunua:

  1: Mk 16:15-16 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA; asiyeamini, atahukumiwa.” (msisitizo ni wangu).

  2: Rum 10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA.”

  Kulingana na maelezo tunayoyaona katika vifungu hivi, haswa kile kifungu cha Mk 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”, hapa ndipo NGUVU ya kuokoa (ule upako) ilipopandikizwa ndani ya mitume, nguvu hiyo ilichipua siku ya Pentekoste. Hii ndiyo siku ambayo Injili ilianza kuhubiriwa, wakiitimiza hiyo Mk 16:15!

  Kwahiyo mtu yeyote yule aliyeipokea Injili aliyohubiriwa, akaiamini, huyo ameokoka! Kuokoka ndiyo hatua ya kwanza anayoipitia mkristo. Hii ni kule ‘KUHESABIWA HAKI’, kwa imani, pale ulipoiamini Injili uliyohubiriwa, nao udhihirisho wa huko kuamini, hukamilika kwa ubatizo. Nao ubatizo huo, kwa siku ya leo, hutimizwa katika maji mengi, kwa jina la Bwana Yesu Kristo, kama ilivyo amriwa katika Biblia ili kupata Ondoleo la dhambi, Mdo 2:38! Kuna kati ya makundi yetu ya kikristo ambao hupenda kukomea katika kifungu hicho cha Rum 10:9, wakiona kubatizwa si lazima ili mradi wamemkiri Kristo kuwa ni Bwana, lakini huko ni kushindwa kuitimiza haki yote, maana iwapo ukiri wao ungekuwa ni wa rohoni, basi Roho wa Mungu angewaongoza wakabatizwe kama ilivyokuwa kwa nyumba ya Kornelio!

  Hatua inayofuata katika mtiririko huo, yaani baada ya kuwa sasa umeokoka, ni ile iliyoainishwa katika Mt 28:20 “…na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi”. Hii ndiyo hatua ya pili anayopitia mkristo. Anapaswa kuketishwa chini na kufundishwa yampasayo katika maisha yake mapya. Neno analofundishwa HUMTAKASA. Neno hilo huziondoa tabia mbaya na madhaifu yake na kuvitupa huko nje! Hatua hii ndiyo UTAKASO.

  Katika hatua zote hizi mbili, mkristo bado anaweza KUPOTEA! Anaweza kupotea kwa sababu anakuwa bado hajakamilika. Yuda alizifikia hatua zote mbili na akapotea!! Hatua hii ya pili ni ya muhimu zaidi kwani mafundisho haya ndiyo yawezayo kumtakasa mkristo na kumfikisha katika kipeo cha Utakatifu au yakambakiza katika kiwango cha dini, kutegemeana na usahihi wake.

  Katika hatua hizi mbili tunaweza kusema kuwa pale ulipoipokea Injili, mbegu ya Golanga wa kiroho ndipo ilipopandwa, na imeendelea kukua kama mtoto akuavyo katika tumbo la mama!

  Hatua ya Tatu na ya mwisho ni kukamilika kuumbika kwa huyo Golanga wa kiroho kutokana na kulishwa chakula sahihi chenye virutubisho vyote vya kiroho, lile neno lisilo goshiwa. Hapa ndipo Mungu humtia muhuri mkristo kwa kumjaza Roho wake Mtakatifu, yaani ule Ubatizo wa Roho Mt. ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa hatua zile mbili za awali, kwamba kwako wewe sasa, ile kazi ya Ukombozi IMEKAMILIKA! Huku ndiko KUONGOKA, yaani nawe sasa uko kamili na tayari kwa kazi ya kuwasaidia wengine kama tunavyomuona Kristo anapomuelekeza Petro kuhusu jambo hilo, Luka 22:32 “Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.” Katika hatua hii ndipo Golanga wa kiroho anapozaliwa, ni huyo pekee anayeweza kuwasaidia ndugu zake, akiwa mezaliwa mara ya pili, kwa Roho wa Mungu. Huyu ni kiumbe kipya, cha kiroho si kimwili tena! Huyu ndiye mwenye uwezo wa kuwasiliana na Mungu na kayaelewa maagizo yote anayopewa!

  Basi ndugu yangu ngoja niishie hapa, huenda wapendwa wengine wakawa na maelezo mazuri na yenye kufaa zaidi, nasi sote tukapata fursa ya kuendelea kujifunza.

  Ubarikiwe!

 10. ck, naomba unisaidie ufafanuzi kati ya haya maneno kuongoka na kuokoka, maana yamekua yakinitatiza.

 11. Ndg Innocent,

  Ubatizo wa “Jina la Baba na Mwana na la Roho Mtakatifu” kwa siku ya leo unakuingiza katika dhehebu lenu tu. Yaani jambo ambalo Mungu kwa ile Neema aliyotukirimia, ubatizo huo unakufanya uokoke, na jina lako kuingizwa katika Kitabu cha Uzima! Yaani safari yako itakwamia katika stage ya pili, kwani kwa huo ubatizo wa “jina la Baba na la…” uliHesabiwa Haki, ambako ndiko huko KUOKOKA, na ulipodumu kanisani kwenu UKATAKASWA kwa lile Neno ulilofundishwa, ambalo kwalo unaendelea kuhukumiwa! Kwa kukwamia kwako katika hatua hii ya pili, ya Utakaso, inayoambatana na Hukumu, wewe HAUTAKUWEMO katika ule UFUFUO wa KWANZA, huo unaowahusu watakaonyakuliwa, maana wewe unao msamaha tu wa dhambi kama wale watakatifu wa Agano la Kale. Hawa pia kama wewe hawakuzaliwa mara ya pili, kwani ile Damu, ule Uzima uliomo ndani ya ile Damu, ulikuwa bado haujatolewa kwao hivyo iliwabidi wausubiri huo mpaka Damu hiyo itakapomwagika kwa ajili yao kuwasafisha na hivyo kupata kibali.

  Sasa sisi pia, kwa bahati mbaya, walimu wetu wa dini, hao walioirukia kazi kabla ya KUONGOKA, wametutangulia mbele na kutuzuia kuingia Patakatifu pa Patakatifu, huko iliko hiyo Damu iondoayo Dhambi, ambayo ndio huo Ubatizo kwa “Jina la Bwana Yesu Kristo” huo uletao ONDOLEO la Dhambi!!! Mdo 2:38 Huko ndiko kusafishwa kikamilifu ili Roho Mtakatifu aweze kuja kukaa humo ilimokwisha kuondolewa dhambi, apate kukukuza hata upate kupewa Mamlaka, huku ndiko KUONGOKA, maana sasa unaweza kuwaimarisha ndugu zako; na si kama hawa walimu wetu ambao wameishia katika Utakaso tu, halafu kwa vipawa wakasema wamehitimu na kujing’ang’aniza utumishi nje ya Mapenzi ya Mungu; yaani wakimtendea Mungu kazi pasipo Mapenzi yake!!!

  Basi ndugu Innocent, Mungu ni Mwaminifu kwa yote, Wokovu na Hukumu, hebu na tutembeeni pasi kufumba macho!

 12. Jamani Mungu awabaliki sana. Nimefalijika sana kwa michango yenu mubakiwe. Samahani sana mimi ni mkristo nimebatiza. Nina swali kuhusu ubatizo swali lenyewe ni hili : katika matayo 28:19 panase hivi ( Kwendeni basi mukawafanye mataifa wote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na la mwana na la roho mtagatifu. Mimi katika kusoma kwangu sikuona sehemu hata moja kwenye mitume walipo batiza hivo. Matendo 2: 38 petro akawambia tubuni mukabatizwe kilb mmoja kwa jina lake yesu. Sehemu nyigine matendo 19:5 waliposikia maneno haya wakabatizwa katika jina la yesu matendo 10: 48 akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo… Hakuna hata sehemu moja walio batiza kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu. swali je walimwasi yesu kutogutimiza maagizo yake? Mukitaka tuma ku email yangu. Thanks to all and my God bless u all.

 13. kuokoka n kumpokea bwana yesu kama bwana na mwokoz utawezaje kuokoka hlo n swl la kujjbu. kuokoka maana yake n ntatoa mfano m2 mmoja alkuwa aksafr kwenda zanzbar alpokuwa kwenye bot mawmb yalipga bot na wa2 weng wakafa kwa bahat zur altokea kjana mmoja mwenye nguvu za ajabu akaogelea mbaka alpo yule m2 alpo akamshka mkono na kumuokoa ktk bahar nadhan aliye okolewa atamshuru sana yule kjana ikiwezekana watakuwa marafk wakubwa.m2 anapo kuwa ameokaka inamaana alkuwa ktk kufa kama n zamb au magonjwa nk.kuokaka s kuombewa sala ya toba au kutubu na kuishia hapo.nlazma ugeuzwe nia na mwenendo wa kale maana umezaliwa mara ya pli. il uokoke n lazma kuz2bu zamb zako na kwa kuongozwa na m2 mithal 28:13 neno lnasema m2 asfche uovu bal aungame sala ya toba s kutubu bal n sala n maomb yalio ktk mpangilio tofaut na dua na maomb 1tim 2;1-2hivyo n lazma m2 kutubu yeye kama yeye sala ya toba unaweza kuifanya kla cku na s kutubu ukisha ku2bu mungu anasamehe na kufuta kabsa isaya 4325-26 mungu anasema mkumbushe zle zamb zako apate kukupa hk yako.wapendwa 2yaelewe maandko.matendo.matendo 2;37petro anasema tubun mkabatzwe hakuwaombea sala ya toba alafu wabatzwe matendo 17;30-31 mungu anaagza kla mmoja atubu.nn maana ya kutubu kutubu n kukubal kuwa umefanya lle kosa na kuomba msamaha kama n mzz unatubu kwa yesu me n mzz naomba unsamehe i zamb kwa toba unai2bu c kusema me n mwenye zamb yesu nsamehe.hata mtoto akkosa hawez kusema baba nmefanya kosa nsamehe baba ataulza kosa lp?ndpo amsamehe.cha kwanza umwamin yesu la pl tubu la ubatizo huwez kutubu na huku umwamin yesu au kubatzwa na huku huja2 wala huamin.wa2 weng wanashndwa kuupata ushnd wa zamb kwa sababu hajazliwa kutokana na mungu 1yohana 3;8-9 m2 aliye zaliwa mara ya pl hawez kutenda wala shetan kugusa ovyo bal huushnda ulmwengu kwa sababu mungu u ndan yake kama neno linavyo sema mungu anakaa ndan ye2. c kwamba zamb hazta kufuta ztakuata lakn inakupa kuzshnda maan mungu u ndan yako akikuwezesha kam ahayupo utashndwa ila yesu n mshnd bwana apewe sfa nas pia 2 washnd kwa sababu 2mezaliwa na yeye ak2osha makosa ye2 yote hoo!damu ya yesu n ya ajabu imeniweka huru nai2kuza na kuisfu hiyo damu.baada ya kuzpitia hzo hatua 3 kuamin kutubu kubatzwa iwe kwa roho au kwa maj inawezekana ukajaa roho kabla ya hata ya kubatzwa kwa maj sasa unaendelea kuusifu msalaba na damu ya yesu ndivyo uzd kupata ushind na zaid ya ushnd mtangaze yesu kwa aw2 wote wapate kumjua.kufanya yote uliyo agzwa. ushnd wa zamb upo nna uhakika na hl nnalo Lsema mwiln mwangu nmepgwa chapa ZA YESU AMAN YA AJABU KUTOKA KWA YESU NA USHND WA ZAMB KTK YEYE.BWANA APEWE SFA

 14. Neno la Mungu ni pana sana. Wakati tunalisoma, kwanza tuanze na maombi ya kupewa uwezo wa kuyaelewa maandiko. Pili, wakati tunasoma tunahitaji kutafakari kwa kusoma kifungu kizima na hata kufuatilia rejea zake. Tena, kama kuna hoja ya kutafakari kwa kushirikiana haipendezi kutoa maoni tu kwa ajili ya msimamo wa kidhehebu. Neno linajitosheleza lenyewe na linajitafsiri kwa kadiri unavyozidi kuwa karibu nalo.

 15. SHALOM WAPENDWA.
  Mungu awabariki sana, kuna vitu tunavipata ni vipya ktk masikio yetu.

  PRECIOUS, naomba namba yako ya simu nina jambo nikuulize nakereketwa nalo.
  AMEN.

 16. Ndugu Masanjila,

  Ni Biblia ipi hiyo inayofundisha kuwa mtu anayejazwa Roho Mtakatifu matokeo yake ni Kunena kwa Lugha….tu?”…? Hata Yesu alisema mtapokea Nguvu………matokeo ya Mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu ni Nguvu anayopata ya kumtetea KRISTO….KUMUHUBIRI KRISTO….KUWA TAYARI KUMFIA KRISTO……Hivyo ndivyo navyoona ndani ya Maandiko……….Je Maandiko haya hayako ndani ya Biblia yako…….

  1. Matendo 4:8- 13 Ndipo Petro AKIJAA Roho Mtakatifu Akawaambia……..walipoona UJASIRI WA PETRO……

  (Hakuna kunena lugha yoyote hapa……bali Ujasiri wa kutangaza Kristo)

  2. Matendo 4:31 Hata walipokwisha Kumwomba Mungu mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”

  (Hii inazidi kuthibitisha maneno ya Yesu ya Kupokea Nguvu……sio lugha wala kunena….)

  3. Matendo 7:55 ” Lakini yeye (Stephano) AKIJAA ROHO MTAKATIFU AKAKAZA MACHO…….AKASEMA…….

  (Stephano alipojazwa Roho Mtakatifu…..alipata Nguvu….Ujasiri….hakuna Lugha au kunena lugha mpya……)

  4. Paulo alipojazwa Roho Mtakatifu Magamba yalimtoka ( Matendo 17:39)

  Matokea ya Kujazwa Roho Mtakatifu sio Kunena kwa Lugha…..bali ni ujasiri/Nguvu ya kushuhudia Kristo……

  5. Kunena Kwa Lugha katika Matendo ya Mitume kuliambata na NGUVU /UJASIRI wa kunena Habari za Mungu na ili kuwafikia kundi la watu waliojazana Yerusalem Roho Mtakatifu aliwawezesha MITUME Kunena kwa Lugha INAYOELEWEKA……..Kila mtu alisikia Matendo ya Mungu kwa Lugha yake Mwenyewe……..!

  6. Matendo 2:41- 42 Lile kundi la watu elfu lililopokea Neno la Mungu kwa Mahubiri ya Petro…….lilibatizwa na kuendelea na mafundisho ya Mitume pasipo kunena kwa Lugha…..Je Petro alisahau kuwafanyia ubatizo huo….!

  6. Lugha “ISIYOELEWEKA” INAYOONGIZWA na Roho Mtakatifu kama itazungumzwa mahali ambapo pana Kundi la Watu (waumini) Ni LAZIMA IWE NA TAFSRI……..Hivyo ndivyo anavyosema Paulo katika Kitabu cha Corintho…..

  7. Paulo anataka TUNENE KWA LUGHA KAKINI HALAZAMISHI Kunena kwa Lugha…….anasema tutake sana Karama za Rohoni…..ambazo ziko nyingi…….

  8.Paulo anasema anayehutubu ni MKUU kuliko anenaye Kwa Lugha…..

  Nachoshauri ndugu Masanjila jaribu mno kuyapa Maandiko ya pande zote nafasi……

 17. Yeyote anayejazwa Roho Mtakatifu lazima matokeo yake huwa ni kunena kwa lugha,asiyenena kwa lugha,jibu ni rahisi tu kwamba hajajazwa Roho mtakatifu na kunena kwa lugha kuna tafsiri mbili kuu nionazo mimi (1)Kuongea lugha yoyote ambayo hukuwahi kujifunza,na hata unapoiongea unakuwa huielewi,lakini pia inaweza kuwa ni lugha ya watu wa kabila au taifa lingine,ila wewe huielewi (Mdo 2;4-13) (2)1 Kor 14;2)Kuongea lugha ambayo,hakuna anayeielewa,ni lugha haieleweki katika nchi yoyo duniani,hata wewe mwenyewe unakuwa huielewi,lakini ni Roho Mtakatifu anapeleka taarifa zako kwa mambo yako ya sirini.

 18. Kutubu ni kubadili mtazamo ulionao.Ni kuachana na dhambi,Nikujikana na kuubeba msalaba wa Yesu. kutubu ni pamoja na kugeuka na kuachana na dhambi kwasababu, Biblia inasema watendao dhambi hawakufanana na Mungu.Kubatizwa kwa Roho ni kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu ambazo bila hizo huwezi kumpendeza Kristo.Ndiomaana katika matendo ya mitume18,19,Paulo anawauliza,Mlipookoka mliupokea na ubatizo wa Roho Mtakatifu?Hiini kuwajulisha kuwa kila anayeokoka ni lazima apokee na ahadi ya Roho Mtakatifu ili aishi akiwa na uhakika wa kufika kwa Kristo kwasababu waongozwao naRohowa Mungu hao ndio wana wa MUNGU.

 19. Jamani tusiwe wajuzi kuliko Yesu,usiongeze wala kupunguza neno,ni kuzaliwa mara ya pili wala siyo mara tatu,maana hata imani potofu huanza hivyo hivyo.Pia ubatizo ni kwa ajili ya waliotubu tu ila ambao hawawezi kutubu ubatizo kwao ni batili Mathayo 3;11 Nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba,ubatizo wa maji ni ishara kwamba mtu huyu alitubu au alimkiri Yesu kwa kinywa chake.

 20. Naomba nikujibu kidogo Preciuos,Kubatiza kwa Jina la Baba,na Mwana na Roho Mtakatifu ni agizo tena limetolewa kwa kinywa cha Yesu mwenyewe Mathayo 28;19- hatubatizi kwa jina la Yesu pekee kamwe.Kubaiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu inaonyesha ni jinsi gani unaamini utatu mtakatifu,kwa sababu unapookoka hawa wote UTATU MTAKATIFU unakaa kwako.Kama unatamka baba wa herufi ndogo basi ujue unatamka shetani ila kama unajua unachotamka kwamba ni ‘Baba’ni herufi kubwa unajua unaemtaka kwamba ni MUNGU Muumba mbingu na nchi,lakini zaidi sana maisha unayoishi katikadhamiri yako ndiko kwenye jibu hata kama ukijifanya unatamka Mungu muumba mbingu na nchi,haitasaidia walahaitakuwa kinga kwako kwamba unaamaaniha MUNGU MKUU ORIGINAL GOD,maisha yako yako ndiyo yanayotamka jina kuu wala si kinywa chako pekee,sawa precious na wote ?

 21. Thanx a lot john, na mungu akaubariki sana maana umeufanya ubongo wangu kupokea kitu kizuri sana na moyo wangu kufurahi maana hicho kitu kilikuwa kinaniumiza kichwa sana na kinaninyima raha, Litukuzwe jina la bwana maana amekutumia kufungua kifungo cha mawazo yangu, mungu akubariki sana, Amen

 22. John Mtangoo,kama hujawahi kuona maji mengi ktk biblia,je mbona wapo wanaobatiza watoto wadogo ingawa haionyeshi popote kwamba watoto walibatizwa ila walibarikiwa tu,maana watoto hawahukumiwi adhabu hata wakifa ,maana biblia yasema ‘aaminie na kubatizwa’je mtoto mdogo aweza kuamini?.Unaposema toba ndiyo halisi si toba pekee ila chochote kilichoagizwa ktk biblia ni cha muhimu neno lasema ‘kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao,na kwa kuwaongoza,na kwa kuwaadibisha ktk haki. Wapo waliobatizwa kwa maji mengi pia hukengeuka lakini pia waliotubu toba halisi hukengeuka.Unaposema TOBA HALISI ndio ya msingi,Mungu asingeagiza agiza uwepo ubatizo,na kama hujafundishwa maana ya ubatizo na ukajua faida yake bora usibatizwe kwanza mpaka ujue maana yake na faida yake,ndio maana NINAPINGA VIKALI watoto wadogo kubatizwa,maanaikiwa wakubwa tu hawajui maana na faiday ubatizo sembese watoto wadogo,hata KUOKOKA watu hawapaswi kuokoka ikiwa hawajui maana yake,ili wasije ingia ktk dhambi mara mbili.Kwa kuuona ubatizo si kitu halisi kama TOBA ndiko kuliko sababisha watu wakachukulia kirahisi kwa kubatiza kichwani tu,na wakasema UBATIZO unaondoa dhambi ya asili,ingawa si kweli maana tunaona hata watoto bado hukasirika ingawa inasemwa dhambi ya asili imeondolewa kwa kubatiza,elewa kwamba dhambi inaanza kuhesabiwa mara baada ya mtu kujua mema na mabaya,mtoto kamwe hahesabiwi hukumu.Ndani ya ubatizo tunatimiza haki yote.Elewa kwamba mtu anapobatizwa si jambo la kimwili tu ila na roho yake inapata kitu,ndio maan ukuija ktk ubatizo wa watu wanaoamini ujazo wa Roho Mtakatifu,baadhi ya watu hujazwa Roho mtakatifu{Mathayo 3;16-},wengine huponywa magonjwa,wengine mapepo hulipuka na kukimbia {Yohana 1;26-}Ukiona watu wanabatizwa halafu hakuna ishara hizo basi anza kuwa na mashaka na mahali ulipo.HAPO JUU NIMEONYESHA BAADHI YA MAANDIKO YANAYOONYESHA NI NINI MAANAYA KUBATIZA KWA MAJI MENGI, BIBILIA IMETUMIA NENO “KUZIKWA PAMOJA NA KRISTO KATIKA UBATIZO “RUMI6;4-,WAKOLOSAI 2;12,NA NIKAONYESHA JINSI AMBAVYO WOTE WALIOBATIZWA WALIBATIZWA KWENYE ENEO LILILOKUWA NA MAJI MENGI RUMI 8;38,MATHAYO 3;16. NIPIGIE KWA MAELEZO ZAIDI 0756 038556 na Mungu awabariki nyote.

 23. John Bethania,
  Congratulations!! Very elaborative points, May God Bless you abundantly! Sifa na utukufu zibaki Kwake Yeye awezaye kuwatumia watu kama John katika kuifunua siri hii ya wokovu.

 24. Hellen umeuliza swali ambalo linawatatiza wengi hasa maana ya kuokoka au kuzaliwa mara yapili au kumpokea yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako. Tatizo linatokana na neno hilohilo ambalo Yesu alimwambia mzee Nikodemo. Yesu alipoona Nikodemo haelewi anachomwambia akasema Yohana 3:8 “upepo huvuma upendako na sauti yake waisikia lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Kadhalika na hali yake mtu aliyezaliwa kwa roho (aliyeokoka)”. Na ndivyo ilivyo kwako Hellen maana unaamini tu kuwa umeokoka lakini haieleweki ni nini hasa kimekutokea. Kuokoka sio kuacha dhambi maana wako wapagani hawatendi dhambi wanaishi maisha ya kupendeza tu wakati mwingine kuliko hata waliookoka. Kuacha dhambi kunatakiwa kuwe ni matokeo ya kuokoka. Kwahiyo kuacha dhambi sio kuokoka. Kuokoka ni nini basi? Ni mabadiliko ya kiroho (spiritual transformation) yanayompata mtu anapookoka au kuzaliwa mara ya pili. Nini maana ya neno la Yesu la Yohana 3:5? Kwa lugha nyepesi kabisa (layman’s language) ili mtu auone ufalme wa Mungu sharti azaliwe mara tatu:
  (i) Kuzaliwa kwa mwili (mst.wa 6a ) sababu kilichozaliwa kwa mwili ni mwili yaani mtu huzaliwa kwa mwili anapotoka tumboni mwa mama yake;
  (ii) Kuzaliwa kwa maji (mst wa 5b) Mtu asipozaliwa kwa Maji na… sasa huo ndio ubatizo wa maji na;
  (iii) Kuzaliwa kwa roho (mst wa 6b ) mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho maana kinachozaliwa kwa roho ni roho sio mwili tena.

  Hellen wewe ulikwisha kuzaliwa kwa mwili (kutoka tumboni) na hata kwa maji (ubatizo). Lakini unapoongozwa sala ya toba (haijalishi ni mlokole gani aliyekuongoza) ndipo unapozaliwa mara ya pili au unapookoka au unapompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Kwahiyo tunapozungumza juu ya ubatizo ambao utamfanya mtu aingie mbinguni tunazungumza juu ya ubatizo wa kuzailwa mara ya pili yaani kuzaliwa mara ya kwanza kwa maji (ubatizo wa Maji) na kisha wa pili kwa roho (kuokoka). Huo ndio ubatizo unaoongelewa katika mstari wa 5.
  Hata hivyo bado si rahisi kuelewa maana ya kuzaliwa mara ya pili au kuokoka. Mzee Nikodemo akamwuliza Yesu “itawezekanaje mtu mzima kuzaliwa mara ya pili? je atarudi tumboni mwa mama yake azaliwe upya? Ni ngumu kuelewa kwa sababu unapookoka saa ile unabakia kuwa yuleyule wa zamani hakuna kinachobadilika sanasana wengine huona furaha sana ndani ya mioyo yao furaha ambayo huwa inafika mahali inatoweka. Kuokoka ni kama Yesu alivyosema katika mstari wa 8 kama vile upepo usivyoeleweka unakotoka wala uendako. Hii ni kwasababu kuokoka ni mchakato wa kiroho (spiritual process) ambao hatuuoni kimwili au hata kihisia. Kwakuwa ni mchakato kuna hatua tano za msingi ili kuokoka.
  (i) Kujitambua kuwa wewe ni mwenye dhambi (Warum 3:23) tafakari sana juu ya maisha yako yaliyopita ili uone jinsi ambavyo maisha yako hayakumpendeza Mungu kisha anza kujenga hasira ya kuichukia dhambi maana imekuchelewesha kwa mengi.
  (ii) Kutafakari kuwa Yesu alikufa wa ajili ya dhambi zangu hivyo sina sababu ya kuendelea kuishi katika dhambi (Yohana 3:16;Warumi 8:1)
  (iii) Kutubu dhambi. Kutubu dhambi nao ni mchakato ambao una hatua tatu kuu.
  (a) Kuisikitikia dhambi kama Daudi alivyosema katika Zaburi 38:18 “Kwa maana nitaungama uovu wangu na kuisikitikia dhambi yangu”. Kuisikitikia dhambi vipi? Fikiri umemtukana mama yako je utakuwa na amani moyoni mwako? Si zaidi sana tunapomkosea Mungu ambaye ni mkuu kuliko mama zetu? Tunahitaji tuumbe hasira ya kuchukia na kusikitikia dhambi tulizofanya
  (b) Kukiri dhambi zako kwa kinywa chako. Huku ndio kuongozwa sala ya toba. Ni vizuri kukiri dhambi zako mbele za watu kwa sababu dhambi (ambayo pia ni roho) ina tabia ya kuona aibu. Yaani ni lazima kuiaibisha dhambi mbele za miungu (wanadamu) kwa kukiri mbele zao. Kusema kweli hapa ndipo mtu anapopokea wokovu. Warumi 10:9-10 . Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako……..utaokoka. Tunapomwamini tunakuwa na haki ila tunapomkiri kwa vinywa vyetu ndipo tunaokoka.
  (c) Kuacha dhambi usirudie tena (theoretical). Maana yake dhamiria moyoni mwako kuacha dhambi yaani kasirikia maisha yako ya zamani ambayo yalikuwa hayampendezi Mungu. Ni kazi kubwa sana maana mwili ni uleule, marafiki na ndugu ni walewale, mazingira unayoishi ni yaleyale, hali ya maisha ni ileile, na hata Tanzania ni ileile nk. Hakuna kinachobadilika ila moyoni.
  (iv) Umpokee Yesu ndani ya moyo wako kwa njia ya Roho Mtakatifu. Baada ya kumpokea Yesu moyoni kwa kawaida mtu huwa mwenye furaha ya ajabu sana ndani ya moyo wake sababu Roho Mtakatifu huwa ameingia ndani yake. Mpaka hapo unahesabika kuwa umeokoka na jina lako limeandikwa katika kitabu cha uzima wa milele. Lakini kuna hatua moja bado ya msingi sana ambayo na yenyewe inakuhitaji utumie muda mrefu sana kutembea humo. Ni hii;
  (v) Kufanyika kiumbe kipya yaani kuutupa utu wa kale na kufanyika upya. (2Wakorintho 5:17). Huu nao ni mchakato unaohitaji maelezo ya peke yake maana unaeleza namna ya kuukulia wokovu na sio kubweteka. Maana yake sio kwamba kwakuwa mtu ameongozwa sala ya toba tayari amefanyika kiumbe kipya la hasha, kuna hatua zaidi za kuchukua ili mtu awe kiumbe kipya na ya kale yawe yamekwisha kupita. Ya kale yamepita ni yapi hayo? Maana kama mtu alikuwa mwongo sio kwamba uongo umekwisha, mawazo ya kutamani bado yapo, kama alikuwa msengenyaji usengenyaji bado haujatoka na ndiyo maana wapo walokole wasengenyaji maana bado hawajawa viumbe vipya. Soma Wagalata 5:19…. tabia hizo ziko na walokole wengi kwa sababu ni kazi kubwa sana kufanyika kiumbe kipya. Kimsingi toba ni kuokoka kila siku.

 25. Safi sana Noel!.Ubatizo ni lazima!.jamani, tuangalie ‘MIFANO’ Yesu aliyotupa kwa vile alivyofanya,ndipo na sisi tutaishi sawasawa katika wokovu.maana,Yeye ndiye Mungu,Bwana na Mwokozi.tukishaelewa kila ‘step’ ya maisha yake,tutaushinda ulimwengu huu! Ubatizo ni kufa pamoja na kufufuka na Yesu,colossians2:12.ndugu,Mtangoo.ubatizo wa kweli,ni katika jina la YESU wa Nazareth(jina lipitalo majina yote).’Wapentecost’,tumepewa jina lakini hatujui kulitumia.tunabatiza kwa jina la baba,mwana na roho?!
  Je,baba yupi?maana,hata shetani ni baba wa dunia hii ya uovu,baba wa uongo! Specify!.
  Mwana,ndo nani? Mwili(Kristo)-ndo ulizaliwa na Yusuph na Maria.ila,Yesu;hakuzaliwa.alishuka pale Kristo alipomwendea Yohana mbatizaji,kubatizwa.
  Roho,Ipi? Hata shetani ni roho!
  Kabla ya Yesu kuleta ufalme wake,ilikuwa hairuhusiwi kutaja jina lake bure.Ila,baada ya Yeye kuja,akatupatia jina lake,tupate kulitumia.ndo hayo mamlaka tuliyopewa.ndo nguvu,ushindi,uzima.jina la Yesu ni kila kitu kwetu.Ubatizo katika jina la Yesu,ndio ubatizo wa kweli,wenye nguvu,mamlaka,ushindi,mafanikio n.k
  Hili ni somo kubwa sana na linahitaji muda wa kukaa chini na kufafanua vyema tukitumia Neno la Mungu(Yesu wa Nazareth).
  Ila kwa hayo,ningeshauri kila mtu afunue Biblia na kuangalia nini kile mitume walifanya.Jinsi gani walibatiza.
  Toba;kuachana na dhambi na kumfuata Yesu maana,Yeye ni mtakatifu pia,hupendezwa sana na watakatifu.Ubatizo wa toba:ubatizo wa ondoleo la dhambi.Huu ndo ule alioutumia Yohana mbatizaji.Kwa mengi zaidi,njoo ‘House of Prayer church’-Boko Magengeni.Mbarikiwe wapendwa!.
  Ujumbe:tupende sana kupata changamoto especially,kutoka katika Neno la Mungu,tutakuwa kiroho na kiufahamu zaidi!.

 26. kubatizwa kwa maji mengi ni lazima,maandiko yaonyesha waziwazi kwa kubatiza maana yake nikuzikwa na Yesu Wakolosai 2;12 ‘Mkazikwa pamoja nae katika ubatizo’Rumi6;4- Basi tulizikwa pamoja nae kwa njia ya ubatizo neno kuzikwa linaeleweka kwamba tunapozika huwa hatuziki kichwa pekee bali mwili wote, Mdo 8;36 ‘wakafika mahali penye maji’ Rumi 8;38’wakatelemka wote majini’Math 3;6 ‘akawabatiza atika mto jordani’Math 3;16-akapanda kutoka majini’ katikahaya maandiko yanonyesha jinsi ambavyo maji mengi yalitumika ktk kubatiz na ubatizaji wenyewe ulivyokuwa wa kutumbukizwa mtu mzima mzima

 27. Mwanangu,

  Nakupa ushauri huu. Mwone Mchungaji wako aliyekubatiza, atakupa mafundisho mazuri kuhusiana na swali uliloliuliza katitika mtandao. Cha muhimu ni pongezikwa uamzi huu mzito kuhusiana na hatua ya usindiya kubatizwa amani ya Bwana iwe nawe.

  Makunzo (Songea) 0754060996

 28. Mungu awabariki wote mliyoshiriki kunisaidia kuelewa na aendelee kuwatia nguvu, Kwa hiy dada Martha mtu ukiokoka na kumkiri Yesu kuwa bwana na mwokozi tayari unakuwa umebatizwa kwa maji na kwa roho mtakatifu, naamini nilivyoelewa ndivyo ulivyoelezea. Asante

 29. 1. sijawahi kuona mstari kwenye bibilia unataja maji “MENGI”. mistari yote ninayoifahamu inataja maji. kama kuna mtu anamstari unaosema neno “MENGI” nauomba tafadhali.
  2.kubatizwa kwa maji ni ishara ya nje ambayo inaendana na kukiri. haya yote huwa ni kwa ajili ya muonekano wa nje. Muonekano wa ndani ndio TOBA HALISI. Toba halisi ni kuishi sawasawa na neno la Mungu. JOSHUA 1:8 na wakolosai 2:16.
  3. Maji hayajawahi kuondoa dhambi. kama huamini uliza kuna watu wamebatizwa hadi mara kumi lakini dhambi iko pale pale iwe ni kuiba au kusengenya. kama huamini jiulize kwa nini viongozi wetu wakuu wa dini ambao wanatuletea mafundisho ya maji hawapendani? wanatukanana kwenye tv, wanakashfiana wao kwa wao kwa sababu macho yao yamepofuliwa na maji (ambali sio fundisho kuu) badala ya NENO LA MUNGU. ukijali sana mafundisho ya maji utasahau kuhusu neno la Mungu. Mimi nakwambia toba ya kweli na KUSOMA,KUYATAFAKARI NA KUTENDA SAWASAWA NA NENO LA MUNGU. HUU NDIO UBATIZO WA ROHO NA MOTO.

 30. asanteni sana na Mungu awabariki wote mlioshiriki kunisaidia kuelewa japo kwa ufupi lakini imenipa changamoto ya kuendelea kuelewa zaidi, lakini nilichokuwa namaanisha zaidi na hichi ndicho kinachonifanya nisielewe utofauti uko wapi, kuna mfanya kazi mwenzangu ameokoka akaniuliza je baada ya kuokoka umebatizwa kwa maji mengi? nikamwambia hapana, kwani haitoshi kuongozwa sala ya toba na kukiri mwenyewe kuwa nimempokea Ykuwa Bwana na Mwokozi wangu na kuenenda sawasawa na mapenzi yake na kufanyika kuwa Mwana wa Mungu hadi nibatizwe kwa maji mengi?, ndipo akaniambia kuwa nisipo batizwa kwa maji mengi nitakuwa bado sijafanya kitu kwenye kuuona ufalme wa Mungu, akanipa baadhi ya mistari ambayo ipo kwenye biblia inasema kuhusu ubatizo, nikaisoma lakini nimeshindwa kuelewa vizuri, Mungu awabariki sana na mzidi kuniombea.

 31. KUZALIWA KWA MAJI NA ROHO KUNAMAANISHA: UBATIZO SI MAJI MATUPU TU BALI NI MAJI KATIKA NENO LA KRISTO. NA KUZALIWA MARA YA PILI KUNAMAANISHA KUFANYWA UPYA ROHO YAKO YAANI KUONDOA DHAMBI YA KWANZA AMBAYO KILA BINADAMU HUZALIWA NAYO {DHAMBI YA ADAMU NA EVA KULA TUNDA BUSTANINI EDENI] HIVYO KWA KUBATIZWA TUNAKUA TUMEZALIWA UPYA ROHO ZETU.

 32. Shalom. kwa uelewa wangu, kwamujibu wa Yohana 3:5, kwanza ubatizo unaotambulika kibiblia (wa maji) ni ule wa maji mengi. na utakapobatizwa kwa maji mengi means utakuwa umetimiza haki yote. na utakapobatizwa kwa maji mengi baada ya kukata shauri la kuokoka, unakuwa umebatizwa kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. maana yake ni kwamba, huwezi kubatizwa kama hujamwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mokozi wako, halafu kisha ukamkiri kwa kinywa chako hadi kuitwa/kusema nimeokoka. baada ya hayo, ndipo inabidi utimize haki yote kwa kubatizwa kwa maji mengi kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. sasa, kama umeokoka na umebatizwa kwa maji mengi, usirubuniwe kubatizwa kwa maji mengi na mtu yoyote. maana utamkufuru Roho Mtakatifu. kwani unapoamini na kuokoka, utabatizwa kwa maji mengi huku Roho mtakatifu akihusika kwa 100%.

 33. Precious,

  Mafundisho ya’ Ubatizo wa toba” yanafundishwa sana na watu wenye misimamo ya “Oneness Pentecostalism” ambao baada ya kukujia kwa “ubatizo wa toba” watakujia tena na “Ubatizo wa jina la Yesu tu” kwanza huanzia mbali sana kwa kuuleza “Utatu” kwa tafsiri ambao inayalazimisha maandiko yaseme wanachotaka yaseme…….na kutokea hapo utafundishwa mafundisho mengi ambayo ni ya kufuata sheria tu (legalistc) .hivyo labda ningoje wale wanaofundisha “ubatizo wa toba” waje na maelezo yao….tuone kama yanakwenda sambamba na maana ya ubatizo kama ulivyojifunua kwenye maneno ya Mungu……..andiko hilo moja…Yoh 3:5 haliwezi kuwa ndilo la msingi kujenga hoja au fundisho la “ubatizo wa toba” Inabidi uangalie maandiko yote kuhusu ubatizo ndani ya Biblia ndio uje na fundisho….! Mstari mmoja tu haujengi fundisho (Doctrine) Hii ni kanuni ya msingi mno katika kuyaelewa maneno ya Mungu.

  UBARIKIWE.

 34. Precious,

  Mimi nadhani toba ya Kweli haijalishi umeongozwa na mtu….hasa baada ya kulisikia Neno la Mungu na Kusema sasa nifanyeje (Matendo 2:37) Au umeifanya peke yako….La Msingi Toba hiyo itazaa matunda (Matunda yapasayo toba) Kuacha maovu na kuamua kumfuata Kristo……!

  Labda tungemsaidia muuliza mada maana ya Toba….na Ubatizo wa toba…..

 35. kuzaliwa mara ya pili,ni kuachana na dhambi zote na kumfuata Yesu! bytheway,ni dhambi kuongozwa sala ya toba.mtu akiamua kuokoka,atubu mwenyewe kwa kinywa chake yale aliyomkosea Yesu.Pia,maneno yale yatoke rohoni mwake mwenyewe kama Zachayo.alipoamua kutubu,alikiri makosa yake mbele ya watu na Yesu bila kuongozwa namtu yeyote kutubu.ina maana,walokole wengi,hatujaokoka sawasawa sababu,tumeongozwa kutubu! a challenge-Precious.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s