Nini maana ya Rastafari? na wanaamini nini?

Kuna watu wanampenda Bob Marley ama wanasema wanafuata nyayo au kuiga mfano wake, lakini ziko habari kwamba Bob Marley kabla hajafa alimpokea Bwana Yesu na kubatizwa kuwa muumini wa Orthodox na siyo Haile Selassie.

Alipokuwa katika mahojiano Askofu aliyembatiza Marley, Abuna Yesehaq wa kanisa la Ethiopia Orthodox, alisema Marley alikuwa mtoto wa Mungu tofauti na watu walivyomuona.

Aliendelea kusema “Ugonjwa wake wa kansa ulikuwa sababu kubwa ya yeye yeye kumpokea Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Watu wengi walidhani alibatizwa kwa sababu alijua angekufa, lakini haikuwa hivyo, alibatizwa kwasababu hakuwa na msukumo kutoka kwa yeyote na alipobatizwa aliikumbatia familia yake na kulia kwa nusu saa.”

Marley alibatizwa tarehe 4 Novemba 1980 na alifariki  21 May 1981 akiwa na miaka 36.

Tukiachana na habari ya Robert Nesta Marley au Bob Marley, Kuna dini ya marastafari na washirika wake tunao mitaani ambapo kwa asilimia kubwa ni vijana, Je dini hii ya marasta wanaamini nini? na rasta zinahusiana vipi na kuvuta bangi?

Advertisements

30 thoughts on “Nini maana ya Rastafari? na wanaamini nini?

 1. Nadhani tatizo la wengi tumeathiriwa na miungu ya kigeni iliyotutenga na nguvu ya roho itokayo katka tunda la uumbaji la BWANA na kuziamini mno sanamu na madhabahu zilizofanywa kwa kazi ya mikono ya wanadam.Tukilijua Jina la BWANA tusingebaki tukiupinga na kuutukana MCHE ALIOUPANDA BWANA KWA MKONO WAKE WA KUUME,ZABURI 80:15,16.na katika hili tutambue imeandikwa kuwa hakuna atakayemwona BWANA asipokua na HUO UTAKATIFU..BALI WAOGA NA WASIOAMINI makazi yao ni katika lile ziwa la moto.

 2. Kila mtu Aheshimu imani ya mwenzie kama tunavyo heshimu c marasta imani za watu wote bila ubaguzi lakini nyi wakristo/waislam mnabagua sana viumbe vya mungu lkn c marasta Jah hatufundish ivyo kila mtu ni saw a kwa Jah

 3. kila MTU anapaswa kuamini Dini ya mwenzie naomba ufafanuzi. kuhusu hayati Bob Marley alikuwa na watoto wangapi

 4. Amani…..nimefurahia mada….am in transition to rasta livity, came across this in ‘the quest” of a type….(((smile)))…hope hear n learn more…byeJahmen

 5. I&I greeting the name of Hailless Sellas I
  Mimefutahishwa sana na majibu ya marasta kwa kweli mmejibu na maswali ambayo nilitaka kujua
  Je Peter Making tosh alikuwa na watoto, Kama ndio wangapi.
  Jha Rastafar I &I

 6. ulishawahi kujiuliza kwanini ukimtendea vema uliejua ni mwehu hushukuru na kuomba ubalikiwe?ukimuuliza anapoishi hutaja jina geni,jina lake pia ni geni,na lugha anayotumia ni ngeni hata yeye haijui lakini anajua anachoongea hapokei pesa ila chakula na kwanini kiwe kile kilichoacha viumbe hai?mpaka ahakikishe inzi wakitua hawafi maana mwanadamu ahaminiki.usizungumzie kitu husichokijua,usizungumzie rastafari kwa kufanya maamuzi,kuwa ni hivi ni vile.YAHU kaandika amri zake vichwani mwetu na sheria zake mioyoni mwetu,kila mtu atumie ufahamu na maarifa aliyopewa na YAHU kupata utambuzi,sio unakurupuka tu na thiologia za kizungu.

 7. Kama ni msomaji wa angano njipya utaona jinsi watu walivyopata shida katika kuyafafanua mafundisho ya YESU hata wale mitume kumi na wawili ambao yesu aliwachagua. Sitopenda kupinga mawazo ya wezangu hapo juu kuhusu wanachoamini ila nisingependa kupita tu bila kuchagia lolote katika mada hii. Biblia ni mjumuiko wa vitabu vilivyo andikwa na ROHO WA MUNGU kupita mikono ya mitume na manabii. Na wengi walitoa maoni hapo juu nimeona wametumia baadhi ya maandiko yalioko katika Bibilia ili kutia uzito hoja zoao lakini ningependa kuwaambia jambo moja tu wakoritho wa kwanza 2:10-11 inasema hivi “lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roha huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. 11 Maana ninai katika binadamu ajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyoandani yake? vivyo hivyo mambo ya mungu hakuna ayafaumuye ila Roho wa mungu”. Kikubwa ambacho nilicho taka kuwaambi wenzangu kuwa si kwamba hadi uwe umesoma sana elimu ya kidunia au umesoma sana BIBILIA ndipo uwe na uwezo wa kufanua kuelewa bibilia hapana niswala la kuongozwa na Roho wa MUNGU katika kuyafafaua maandiko tatizo la watu wengi wamesaau kuwa mambo ya mungu ni mambo yanayofafanuliwa na Mungu mwenyewe kupitia Roho wake. Hebu mkumbuke Nikodemo katika yohana3:1-10. yesu alipomuuliza wewe si mwalimu wa israeli na mambo haya huyafaamu (Yohana3;10) . Sikwamba nikudemu hakuwa msomi hapana YESU anamtaja kuwa mwalimu wa israeli na alikuwa mwalimu wa sheria kwa kipindi hicho. lakini hakuwa na ufahamu wowote juu ya mambo ya kimungu hdi alipoamua kumuuliza Yesu. Na si nikodemo pekeyake hata wanafunzi wa YESU walipata shida katika kuyatambua mafundisho ya YESU kwa wakati ule. lakini YESU aliwambia hivi katika Yohana 14:26 “lakini huyo msaidizi, huyo Roho mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Namkumbuke kuwa wanafunzi wa yesu walianza kuwa na uelewa wa maandiko baada tu ya kushukiwa na roho mtakatifu kamailivyo ahadi ya YESU kwao. hivyo swala si kusoma bibilia tu swala ni kuongozwa na roho wa mungu katika kuyafafanua maandiko matakatifu.. Napia ningetoa tu taadhari kuwa shetani humjaribu pia mtu kupitia haya maandiko matakatifu ukitaka kujua juu ya hili kasome majaribu ambayo Yesu alijaribiwa na shetani kunajaribu litokanalo na maandiko matakatifu.( Matayo Mt 4:1-11). asateni na mbarikiwe.

 8. Rasta ni maisha yetu ya kila siku.Kuwa rasta ni kujinyenyekeza mbele ya Mwenyezi Mungu na kuzifuata amri zake kumi.Pia urasta ni kuwa wazalendo na watetezi wa bara la Afrika na Tamaduni zake hasa zile tamaduni nzuri.mfano ulaji wa vyakula vya asili ambavyo ni bora kuliko vile vya viwandani ambavyo vimetiwa kemikali ambazo sii nzuri katika mwili wa binadamu,kuthamini lugha zetu,mavazi na yale yote yanayo utambulisha utamaduni wetu.Kuwa makini na mifumo yote ya kiutawala na kuipinga ile kandamizi kwa maslahi ya Waafrika wote.Kuishi katika maisha ya Amani na Upendo, na pia kufanya kazi kwa bidii katika dhana ya kujitegemea.Yapo mengi mazuri katika Rasta ila kwa sababu ya mfumo wa kibepari wengi wameaminishwa kuwa Rasta ni uhuni.Kama mchangiaji mmoja hapo juu alivyosema ni vyema kufanya utafiti kwanza kuliko kutumia mihemko na kujihesabia haki.JAH bless Africa!

 9. Rasta ni imani kama imani nyingine Rasta siyo lazima avute bangi ni muamifu ni muadilifu ni mbunifu utetea haki za wanao onewa na kwa kila kiumbe lile jani la mche ni nembo kama nembo nyingine na niasili haujatengenezwa na mwanadamu hauna mchanganyiko asili ni jadi yao utumia vitu vya asili na jadi chakula mboga za majani na za kienyeji dawa uvaaji kujipamba shanga magome nk. ila kwa hayote Amani Upendo na Eshima ndiyo msingi JAH tutangulie.

 10. I&I. Dada Rosemary kidogo naona sijakuelewa. Yesu Kristo hakuja duniani kuanzisha DINI wala DHEHEBU….Hapa ndipo penye TATIZO na TATIZO ni kuijua kweli. Basi hatuna budi kwa dhati kumwomba muumba wetu muumba wa mbingu ardhi na vilivyomo. Yeye pekee aliye mtakatifu daima aliye mwanzo na mwisho atufundishe iliyo kweli. kwa maana ametukumbuka kwa neema tu. Eeee Jihova nakwita Jah nifundishe iliyo kweli katika machafuko haya ya utitri wa manabii na machukizo ya kidini. Jah bless

 11. I&I Ras tafari I. ja bless. mimi ni mwafrika Rasta. nimebatizwa Baptist. ninaufahamu ukristo na wakristo nafahamu tabia za kikristo na tabia za wakristo. kikubwa ni imani, kuzingatia misingi ya imani bila ya kukengeuka kwa sababu ya shida za kidunia. kupiga kelele, kujisifu na kuwaaminisha watu kuwa wewe ni mkristo sio ukristo bali kuwa ndani ya misingi ya kikristo ( ameni ) wengi tumekuwa tukijiuliza ukristo ulianza lini na hasa ni kwa sababu ya nani..???…kuwa mkristo sio tiketi ya kuishi katika utakatifu wa milele wa mwenyezi mungu Jihova Elishadai, bali kuitambua iliyo kweli. jah ras tafara i kuwa rasta ni kuachana na maovu na machukizo mbele ya jamii. kuyaacha machukizo kwako mwenyewe kuishi kwa amani na upendo kufuata amri kumi na amri nyinginezo katika agano la kale zinazo sisitiza utakaso wa roho nafsi na mwili. too much is humful hili linaeleweka ukila ukavimbiwa utapata madhara. ukinywa maji, juisi au kimiminika ckinginecho kupita mahitaji ya mwili hali kadhalika utakuwa umesumbua mfumo wa mwili na akili. ulaji na unywaji wa namna hii ukiwa endelevu bilashaka ndugu zangu mnaelewa ni nini matokeo yake. matumizi ya bange kwa sisi waafrika yamekuwepo tangu karne na karne hata kabla ya ujio wa wazungu bila ubishi babu zako na bibi zako wanaifahamu vema. matumizi kulzidi mahitaji kwa mwanadamu ni dhambi. sina sababu toshelezi kupinga kwamba bangi ikitumika kuliko mahitaji ya mtumiaji ni hatari kama kula chakula na kuvimbiwa. Mimi ni rasta sivuti bangi,sigara wala pombe na wala sili kwa kuvimbiwa,simlazimishi mtu kuamini ninachoamini mimi bali napenda mtu aelewe ninacho kiamini. Jah ras tafari I ninakila sababu ya kuwaheshimu walionitangulia mimi mtu mweusi waliokuwa na busara na maono yaliyo saidia mimi na kizazi nilichomo kujitambua, nina kila sababu ya kutunza tamaduni niliyo achiwa kwa manufaa ya kizazi kijacho…BOMBOCLAT BABILON…….Babilon still alive africans be ware.
  tukijituma tunaweza……. Ras tafari I……Rastofa

 12. nimefurai sana kuona mada kama hii kwangu mimi nikitazama kwa jicho latatu naweza nikasema rastafari ni utakatifu rastafari ni maisha ya kila siku ya mwanadam inayompendeza mungu rastafari ni zaidi ya nyama rastafari nizaidi ya bangi kuna kitu nataka niseme apo kuhusu bangi kwangu mimi bangi sio ki levi wala kuvuta bangi sio dhambi tuangaliye mwozoni ilitumika kama nini mwazoni ilitumika kama sehemu ya ibada ya yindu inchini india mimi siwalaumu watu wanao sema bangi ni mbaya mwanzo 1:2 inasema nayo nchi ili kuwa ukiwa tena utupu yani inamaanisha nchin ilikuwa haina kitu chochote ukisoma katika isaya 66:2 inasema maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote vitu hivi vyote vikapata kutokea asema bwana jah rastafari king of king amani na upendo

 13. Watu wasipende kupotosha maana, Rastafari kama imani iko chini ya Ethiopian Orthodox na kama unajua kiutendaji ETHIOPIAN ORTHODOX ni Afro-Christian yaani mchanganyiko wa mambo ya kikristo na kiafrika ndani yake. Bob Marley kubatizwa na kanisa la Ethiopian Othodox siyo kitu kigeni kwani Rasta wote wanabatizwa katika makanisa yao ambayo yako chini ya Ethiopian Othodox.

  Pili Rastfari ni imani inayoamini juu ya misingi sita ya imani ambayo ni
  KUMTAMBUA HAILE SELASSIE KAMA KIONGOZI WAO AU WENGINE WANAENDA MBALI ZAIDI NA KUMCHUKULIA KAMA MFANO WA MUNGU KATIKA DUNIA

  PILI, KUUCHUKIA MFUMO WOWOTE WA KUNYONYANA NA KUKANDAMIZANA

  TATU, KUONA FAHARI KWA NGOZI NYEUSI SABABU RASTA ILIANZISHWA MAALUMU KWA AJILI YA WATU WA JAMII YA WAAFRIKA

  NNE, KUITAMBUA AFRIKA (ETHIOOPIA) KUWA NDIYO PARADISO YAO

  TANO, KUICHUKIA NA KULETA USUMBUFU KWA SERIKALI YOYOTE ISIYOJALI MASLAHI YA WANANCHI WAKE

  SITA, KULIPA VISASI KWA WANYONYAJI WOTE IKIWEPO KUPINGA VILE AMBAVYO WANYONYAJI WANAVITAKA IKIWEPO UZAZI WA MPANGO NA MATUMIZI YA NJIA ZA KISASA ZA UZAZI WA MPANGO

  Tunawaomba watu wetu wasipotoke zaidi juu ya Rastafari, ilianzishwa na Marcus Garvey ikiwa na maana nzuri tu na Mfalme Haile Selassie I ndiye mhimili wa imani kwa sababau hata jina Rastafari linatokana na jina la awali la Haile Selassie I yaani RAS TAFARI MAKONNEN, hivyo Mtu Rasta au Rastaman ni wafuasi wa Haile Selassie I katika matendo na katika imani. Ikiwa Haile Selassie I alikuwa mkristo wa imani chini ya Ethiopian Othodox basi Rastafari wote pia ni wafuasi wa Ethiopian Othodox, mfumo wanaotumia Ethiopian Othodox kanisani ndiyo huo huo unaotumika na kamanisa yote ya Rastafari duniani kote.

  Ndugu wasichanganye, Bob alikuwa mristo wa Ethiopian Othodox kama walivyo Rastafari wengine. Rastafari wote kama walivyo waumini wa makanisa ya OTHODOX wanapinga mifumo ya kidini iliyo ya kinyonyaji kama KATOLIKI na makanisa mengine ya kikristo.

  Amani na Upendo

 14. TUJIKOMBOE KIFIKRA ILI TUWEZE KUFIKIRA KWA UPANA.LAITI UTU WA MWANADAMU NI KWA JINSI GANI UNAVYOWEZA KUFIKIRI DHIDI YA MWANADAMU MWINGINE,VIUMBE WENGINE NA MAZINGIRA YANAYOKUZUNGUKA. EINSTEN ALISEMA”
  KILA KIUMBE NI MWENYE HEKIMA ILA UKITAKA KUHUMUKUMU SAMAKI KWA ZOEZI LA KUKWEA MTI KWA KUMFANANISHA NA VIUMBE KAMA TUMBILI UTAMFANYA AJIONE YEYE NI JUHA KWA MAISHA YAKE YOTE”. TUJIFUNZE KUJITAMBUA KWA TUNAYOAMINI NA KUAMINISHWA TUNAYAJUA

 15. Unajua kila kitu kinapita katika hatua mbalimabli za maendeleo hadi kukubalika kwake. Rastafari ilianzishwa na MARCUS GARVEY baada ya kutoa unabii wake juu ya RAS TAFARI mbaye baadae alikuja kujulikana kama HAILE SELASSIE I. Rastafari wanaishi ndani ya misingi sita ambayo ni:-

  1. Kumtambua Haile Selassie I kama mwenye mamlaka na kiongozi pekee wa watu weusi
  2. Chuki kwa unyonyaji
  3. Fahari ya ngozi nyeusi
  4. Fidia kwa wanyonyaji
  5. Kupinga serikali ya ubaguzi (babylon system)
  6. Kuitambua Afrika kuwa paradiso ya kweli

  katika kukamilika kwa imani hii, imepita katika mikono ya viongozi na vyombo mbalimbali ambavyo kwa pamoja vimeifanya kukam ilika hadi kufikia hatua iliyofikia. moja ya viongozi hao ni mwalimu wa kwanza LEONARD HOWELL mashirika na vyombo kama EWFI nk.

  Kuhusu bangi, kama wewe ni mtu wa kusoma biblia na makala mbalimbali ya kihistoria utajua wazi kuwa BANGI NI KITU CHA KIHISTORIA katika mambo ya uabudu. Kwanza tafuta asili ya majina ya mti huu kama BANGI, GANJA au GANJIKA, HEMP, CANNABIS, SENSAMILA na ukishajua kwanini mti huu unaitwa hivyo halafu rejea katika maandiko ya BIBLIA TAKATIFU juu ya MTI WA UHAI unaopatikana katika kitabu cha MWANZO, UFUNUO nk. hapo utajua kwa nini RASTA wanautumia mti wa BANGI kuwa ndiyo mti MTAKATIFU?

  kwa maalezo zaidi naomba utafute kitabu changu kiitwacho IMANI NA UTAMADUNI WA RASTAFARI chenye cover la mtu Rasta aliye ndani ya ramani ya AFRIKA katika sura ya saba inatiwa KAYA ndiyo utajua kilicho ndani yake. pia kuna sala ya kuwashia kaya inayosaliwa “GLORY TO THE FATHER AND TO THE MAKER OF IRATION, ATA IT WERE IN THE IGINING, NOW AND FOREVER BE WORLD WITHOUT END, SELAH. Amani kwetu kaka zangu.

 16. Mubelwa,

  Maelezo ya Urastafari ukiyapata kutoka kwa walio katika imani hiyo ni bora kuliko ya wale walioikimbia! Basi maelezo ya Paul (ras seaga) nayaona ni toshelevu katika kukueleza imani hiyo ni nini.

  Kuhusu bangi, faida zake ulizoziorodhesha kimatibabu, ziko kama zilivyo na pengine zikaongezeka kulingana na maendeleo ya utafiti (ule Ujuzi wa mema na mabaya). Pia ni vizuri ukafahamu kuwa dawa zooote, potentially ni SUMU, ndio maana hutolewa chini ya uangalizi maalumu. Hasara za matumizi ya bangi pia ziko wazi kitabibu na kijamii. Athari zake hazilingani baina ya watumiaji, lakini msukumo mkubwa wa watumiaji wote pamoja na Marastafari, ni ile AHUENI wanayoipata ambayo haijalishi wewe ni Rasta au sio! Kwa kifupi ni kiburudisho!! Kwa vile ni kiburudisho cha mwilini, yaani kinapotumiwa, kemikali zake zinapoingia ingia katika mfumo wa mwili, huathiri mifumo ya kufikiri na utendaji mwingine wa viungo na kukusababishia kuondoka katika uhalisia wa hali iliyopo na kukuingiza katika ulimwengu wa kufikirika au ‘Cloud Nine’, na kwa wengine huwaongezea nguvu ya kufanya kazi, hamu ya kula kupita kiasi, nk. Kuna wengine pia walioizoea, huwalazimu kupata bangi kwanza ndipo waweze kufikiri sawa sawa ili kukabiliana na hali iliyo mbele yao! Na wengine huwatia ukichaa!!!

  Basi matumizi yooote ya bangi nje ya kitabibu ni kwa burudani, unaweza ukajidanganya kuwa ni IMANI, lakini huo ndio ukichaa wenyewe. Kinachotusitisha kuwaona hivyo watumiaji ni kule kutokuzijua kwetu level za ukichaa tu. Wengi wa hao tungewaita “machizi maarifa” yaani huyo ni chizi unayeweza kukaa naye hata miaka kumi usimjue kuwa ni chizi ukadhani ni wa dini ya Rasta!!

  Ushauri wangu kwa Marastafari wote: Badala ya kuhangaika na bangi kila siku, NJOONI kwa Kristo, yeye ni BANGI mtakayoivuta MARA MOJA tu, na MTABURUDIKA maisha yenu yooote! NJOONI mpate “Amani ya Mungu ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”

  Kuhusu dhambi, yeyote asiye mwamini Kristo, atafia dhambini!!! Yoh 8:24

  Barikiwa!

 17. Amani, Heshima na Upendo kwenu.
  Ni muda mrefu sasa tangu niungane nanyi. Na naamini wengine mlishanisaha na wengine ni wapya mmejiunga baada ya mimi kupotezwa na shughuli.
  KWENU NYOTE…….SHALOM.

  Nakumbuka wakati fulani tulikuwa na mjadala wa DINI hapa nami nikauliza NI WANGAPI AMBAO WALIKUWA WAISLAMU NA SASA WAMEKUWA WAKRISTO AMBAO WANAWEZA KUELEZA KINAGAUBAGA KUHUSU PANDE ZOE MBILI?
  Sikubahatika kumpata.
  Swali ni kuwa NI WANGAPI WALIKUWA AMA WAMESHAKUWA MARASTA NA SASA WAMEUACHA WAJE KUTUELEZA?
  Ukweli ni kuwa wengi wenu mnaoamini katika dini inayokataza kuhukumu mnatumua hukumu kama kithibitisho cha imani yenu.
  Mimi nimekulia seminary na kuishi na maRasta. Na hakuna ubishi kuwa maRasta wanajua wazungumzalo kuliko ‘BLA BLA” ninazoziona zikiandikwa hapa kuwashutumu.
  Wanasoma na kuitafakari Biblia kuliko waigizaji wengi wa ulokole.
  Wengi wa Marasta ni waumini wa kweli japo ni wachache ukilinganisha na waKristo wengi ambao asilimia kubwa yao ni waigizaji.
  MaRasta wengi wako na imani inayofanana ukilinganisha na uKristo ambao niliofunzwa Tanzania sio ninaofunzwa hapa Marekani.
  Mmepewa namba hapo. Nendeni mkajifunze kuhusu uRasta kisha mrejee kwenye mada hii. Aliyeuliza kuhusu kuvuta bangi, NAPENDA MNIELEZE KWANINI MNATAKA SUALA LA UVUTAJI BANGI LIWE ISSUE WAKATI HAKUNA ALIYEWEZA KUTHIBITISHA KUWA KUVUTA BANGI NI DHAMBI (kwenye mada hii https://strictlygospel.wordpress.com/2010/06/01/uvutaji-wa-sigara-na-bangi-ni-dhambi/) ambapo moja ya maelezo yangu nilisema “Labda hapa niulize kuwa BANGI (ambayo hutumika katika tiba za hospitali)inapojumuishwa kwenye matibabu mengine inakuwa DHAMBI ama ni dhambi kama itatumiwa na mtu mmoja mmoja bila uangalizi ama ushauri wa Daktari?
  Labda nijazie maelezo kidogo juu ya kile kizungumzwacho kuhusu BANGI ama CANNABIS ambayo mtoa maoni mwingine kaeleza athari zake. Hii ni post ya BBC na ntaweka link hapo chini usome mwenyewe post nzima kujua pande zote za shilingi.
  “For instance, cannabis appears to be able to help reduce the side effects of chemotherapy treatment given to cancer patients.

  The drugs used to treat cancer are among the most powerful, and most toxic, chemicals used in medicine. They produce unpleasant side effects, such as days or weeks of vomiting and nausea after each treatment.

  Cannabis is an anti-emetic, a drug that relieves nausea and allows patients to eat and live normally.

  Extracts also seem to benefit patients suffering from multiple sclerosis, stopping muscle spasms, and reducing tremors.

  In the USA, the Food and Drug Administration has approved the oral use of dronabinol, a cannabis derivative, for people with Aids.

  There is evidence that cannabis may stimulate the appetites of Aids patients with wasting disease.

  It may also help relieve the pain of menstrual cramps and childbirth.

  Campaigners claim the drug is useful in treating depression and other mood disorders.

  Cannabis analogues have been shown to prevent seizures in epileptic patients when given in combination with prescription drugs.

  The drug can also help in the treatment of patients suffering from glaucoma, one of the commonest causes of blindness, by reducing fluid pressure in the eye.

  Claims have also been made for its use in treating asthma, strokes, Parkinson’s Disease, Alzheimer’s Disease, alcoholism and insomnia.”

  Waweza kusoma post nzima kwenye hii link ambamo PIA WAMEZUNGUMZIA WASIWASI WAO KUHUSU ATHARI ZA BANGI (http://news.bbc.co.uk/2/hi/health/227926.stm)

  Sasa swali langu ni kuwa KAMA NI KWELI KUNA BAADHI YA FAIDA KIMATIBABU, JE BANGI HIYO ISITUMIKE HUKO HOSPITALINI KWA KUWA UMEIWEKA KWENYE KUNDI LA “VILEVI”? Ama ikitumika Hospitalini ni sahihi na si dhambi ila ikitumiwa na mtu asiye mtabibu ni dhambi?

  Ni swali ninalojiuliza kama ambavyo nilishawahi kutuma swali kuuliza kama MTU ANAYEFANYA KAZI YA KUNYONGA WATU WALIOHUKUMIWA NA MAHAKAMA ANAKUWA AMETENDA DHAMBI AMA LA?????

  Kwa maana nyingine, ningependa kujua kama DHAMBI yaweza kutokuwa dhambi ikifanywa na fulani ama mwenye mamlaka fulani. Kama sivyo, basi hawa wale watumiao bangi kwenye matibabu (na najua inatumika kihalali) wana dhambi.”

  Sheria ama ustaarabu wa kiandishi unasema NO RESEARCH, NO RIGHT TO SAY.
  Nasubiri wale wenye uelewa kuhusu RASTAFARIANISM watueleze hapa na sio wale waliokaririshwa na wachungaji wasiojua na ambao hata hawashirikiani na maRasta.

 18. Paul nimependa maelezo yako hasa kuonesha kuwa watu wasiwe mabox kudhani wanachojua ni sahihi kuliko wengine na inaweza kuwa ni kukosa upendo kwakuwa dini zote ni mafundisho na tamaduni zetu. Binafsi sio rasta na ni mkatoliki lakini naheshimu kila imani ya mtu ikiwamo uislam na rastas.

  Ikumbukwe kuwa Rastafarians na hata waislam wana mkili Kristo ila mapokeo na mafundisho yanatofautiana.

  Mwalimu wangu wa saikoloji alinifundisha kuwa always think outside the box. Sio kwakuwa uko ndani ya box uamini kuwa this is the only best box ever na all i know about this box is conclusive. Tujifunze na kuamini kuwa dini zote zina uhalali sawa na tuhubiri ukristu wetu vizuri ili uvutie walio nje waingie kuliko kuamini kuwa wenzetu hawana dini na wahuni ila sisi ndio tuna dini. Tambua wingi wa madhehebu unatokana na wingi wa uelewa tofauti.

  TUmsifu Yesu kristu

 19. Asante kwa kuwek hili somo la rastafari,lakini nasikitika kwa watu weng kuchangia kwa kuona ni dini ya kihuni,wapend ni lazima tukubali kila neno linahitaji mtu kufundishwa mfano ni lazima ufundishwe matoleo ndio utaanz kutoa sadaka,zaka au fungula kumi hata rastafari dini ambayo haijulikan sana hapa tanzania ni lazima mtu ueleweshwe ndio unaweza kuwa na ufahamu,mfano waislamu wanashangazwa wakristo wanaposema kuna mungu mwana,roho na baba kutokana kutokuwa na uelewa.ni kweli rastafari ni dini na political movement iliyosambaa sana 1920-30 si dini tu lakini ni namna ya maisha pia,fikiri ni wakristo wangapi ambao wanajaza mabaa ya pombe ambayo rasta tunaita ‘a soap of evil’ wakristo wa leo ndio vinara kufungua bar, unagundua watu wengi wanafkiri dini ni kwenda kanisani tu hapani ni uwanja mpana ndio maan marasta tunaamini hadi the way you live,tunaamini emperial haile selassie I ni chaguo la jah baada ya yesu ,zab 68,zephaniah 3:3,mwanzo 1,zab 87:4-6,1 kings 10-13 pili tunamwamini marcus mosiah garvey kama yohana mbatizaji ezekiel 28:25,revelation5.5 tunamwamini yesu pia rasta ni dini yenye historia ya sisi weusi chimbuko lake ethiopia zaburi 68.31 , kuliko dini nyingine ambazo zimeletwa hasa na weupe ambao leo hii wanaoneka kushuka kiimani kuliko sisi tulioletewa unajua sisi watu weusi tinachangamoto kubwa ya kujikomboa ndio maana wengi leo tunapuuza dini hizi kama rasta,na kuishi maisha ya kibabylon .Kuhusu bangi watu wengi tunadanganywa na babylon kuhusu bangi ,mungu alisema tutumie majani matunda na asali na si nyama ambayo unaipend rasta tunatumia miti,mizizi na majani kuliko maisha ya vyakula hatari tunavyovijua,bangi ni moja ya majani ambayo mungu aliumba ili wanadamu tutumie soma mwanzo 1,11-29 revelation22.2,zaburi104.14 umewahi fikiria bangi na sigara kipi ni hatari?basi nakwambia tu sigara ni kitu hatari ambacho kimeundwa na wanadamu babylon ili wapate pesa kwa takwimu sigara ina chemicals hatari zaidi ya 30 mfano methano,cooper,ddt,swamp gas,rocket fuel,rat poison,carbon monoxide na ile hatari zaidi nicoten wapendwa hebu fikir sumu zote hizi zinaingia kwenye mwili ambao ni hekalu la mungu,mfano nchi yetu inapata faida,hisa na kodi kubwa kutokana na sigara,pombe kuliko madini yetu ambayo ni asilimia mbili kwenye bajeti ya nchi unaona haiwezekani serikar iruhusu bangi ambayo ni natural haina adition ya chemical yoyote,chakula chochote ikitumia vibayo unaathirika wapo walokufa kwa mkate unaoujua wewe hata bangi ukitumia vibaya ina madhara vijana wengi wanatumia kama kujifrahisha tu lakini bangi kwa rasta si kitu cha kujifrahisha tu ambayo ni dawa rasta tunaamini kama ni moja ya sakrament ya mungu rejea biblia,kuhusu nyama ipo wazi mungu wakati anaumba dunia hakusema adam ale nyama haya ni matokeo ya anguko la dhambi mfano wote tunajua nyama tunazokula sasa si nyama ni matatizo tu nyama za sasa zimejaa sumu za kila aina kutokana na maisha ya kibabylon,mungu aliumba kuku aliwe baada ya miezi tisa sisi wa leo tumefanya briding process kuku anakuwa baada ya miezi 3 wapendwa rasta si hivyo tunavyo fikiri na kudanganya na imani yenye upana wake nimejaribu kudokeza tu lakini ukitaka mafundisho zaidi nione 0712461679 ras seaga,kuhusu iman ni jambo la kiroho hasa kuliko mwili sis marasta tunaamini amri kuu ambayo ni upendo,umoja,kutofanya ubaguzi wowote kama dini za babylon ambazo tangia dunia inaanza hakuna alipotokea papa mwenye ngozi nyeusi(kiongozi wenu mkuu vatikan itali) rasta tupo tofauti kabisa na imani kama hizi za kimwili zaidi,,, amen I and I bress

 20. Utafiti wangu ni kwamba, vijana wengi wanafuata dini ya urasta hawajui undani wake nini pamoja na kuhusudu bangi. nami nataka kujua kuhusu dini yao na wakifa wanaenda wapi?

 21. @ Massanja, mwanzilishi wa dini ya Yesu Kristo yu hai, kwanini wewe unaamini ktk wafu basi, je wanakusikia, watakuokoa?

 22. Dini yoyote haisimami bila imani. Halafu dini yoyote, mwanzilishi lazima awe ameshakufa. hii ina maana kuwa, hatuna budi kutembea na kuishi kwa imani kwa kuwa hakuna mwalimu mwanzilishi aliye hai wa kuweza kuweka bayana ya imani husika. Hii inapelekea watu kuishi tu kwa mapokeo na hofu zinazopandikizwa na wale wanaoturithisha: kwa ufupi, ndio maana tunaishi kwa imani pasi na uhuru kamili. Kutokana na nilichokisema, kwa mada kama hii, tutaishia kulumbana kila mmoja akiwambia ngozi upande wake bila ya kuwa na muafaka. la msingi ni kuijua kweli, na kweli yenyewe ni kuishi sasa na kutafuta maana haswa ya uwepo wetu.

 23. Maana:Rastafali, RAsta, ni jamii au kundi la Watu weusi Wajamaica, waliochukuliwa utumwa,ni kikundi miongoni mwa vikundi vya kupigania uhuru (Pan-African Movement)

  ila walimuamini na kuimuabudu sana Mfalme wao wa Mwisho wa Ethiopia Haile Selassie I, waliamini ndiye Yesu aliyekuja mara yapili, na ni Mchaguliwa maalumu wa Mungu kwajili ya Dunia.

  Wenyewe hawana kanisa maalumu na kiongozi wa dini maalumu.

  ni miongoni mwa dini ndogo ya Kijamaika iliyojitawanya duniani kote yenye waumini kama 700,000 hivi.

  WANAAMINI kujitegemea na kuwa binafsi, kwa kundi au mtu, kuhurumia kila kiumbe cha Mungu (ndo maana hawali nyama) ila mambo wanayoyafanya ni KUVUTA BANGI, MIZIKI YA REGGAE, kufuga nywele ndefu nk. Kuvuta Bangi ni tabia yao tu kwani wanaamini inawapa nguvu na kujiamini katika jamii, kwa mtazamo wangu Rastafari sio dini ya Kweli.

  By Godfrey Gerald Kitangala

 24. Ninakushukuru ndugu kwa mada hii na hususani kwa maswali yako haya, “Je dini hii ya marasta wanaamini nini? na rasta zinahusiana vipi na kuvuta bangi?”. Lakini hata na dini zetu siye tusiye marasta tuna ambayo tunayafanya sawa na haya ya watu wa imani za kirasta. mimi nakumbusha tu wakati tunajadili ni kwa nini imani ya marasta inahusishwa na bangi, basi na sisi itakuwa vyema tukajadili na yal4e yakwetu na kwa nini.

  Jambo jingine ni kuwa, sidhani kama kuna haja ya kusimamia alichoamua marehemu Bob Marley. sidhani kama maamuzi yake yatasababisha tuamini kuwa dini ya marasta si sahihi balli ukristo, uislamu na dini nyingine ndizo sahihi.

  Ikumbukwe tu kuwa sijazua watu kujadili ni kwa nini rasta zinahusishwa na bangi. labda mawazo yangu yanaweza kufanya mjadala huu ukajadiliwa kwa mapana zaidi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s