Mbinguni na peponi ni wapi?

Bwana Yesu Asifiwwe ndugu zangu, mimi ninaomba msaada wa ufafanuzi wa andiko la (2 Wakorintho 12:1-5) Je mtu huyo anayemwongelea Mtume Paulo ni nani?  na anaposema ( kwamba alikuwa katika mwili sijui, kwamba alikuwa ndani ya mwili sijui; Mungu ajua )” ana maanisha nini? Je kuna mbingu ngapi? maana hapa anasema akanyakuliwa mpaka mbingu ya 3, je kuna ya 1,2 3 na kuendelea? Pia anasema alinyakuliwa mpaka Mbingu ya 3 na mstari wa 4 anasema alinyakuliwa mpaka peponi je sehemu hizi mbili ni sawa au zina tofauti gani? Naomba msaada wenu.

Judicate

Advertisements

8 thoughts on “Mbinguni na peponi ni wapi?

 1. Ukweli ni upi hasa;
  Jua ndo linalozunguka Dunia au Dunia ndo huzunguka Jua?

 2. ndugu zangu Bwana Yesu asifiwe,napenda kuchangia kidogo katika andiko hilo,nikweli kwamba mtu huyo alikuwa ni Paulo mwenyewe na hakupenda kujisifu kwani alijua haipendezi katika bwana,pia kuhusu swala la mbingu ni kwamba,ukiisoma biblia utaona Mungu anahusika na wanadamu kwa mambo ya dunia tu,hakuwahi kumwagiza binadamu popote kuchunguza nini amefanya ktk anga zingine,kazi aliyotupatia ni kutangaza injili watu waokolewe,habari ya sayansi na Mungu ni tofauti sana kwani sayansi hujaribu kupingana na neno la Bwana,ndugu zangu napenda mjue kuwa paulo alikuwa ktk maono na alipelekwa na roho mtakatifu,hivyo utaona kuwa tunatakiwa tuongozwe na Roho Mtakatifu ktk kulijua Neno na sio sayansi,wanadamu tumekuwa tukitumia akili zetu wenyewe kulisoma neno na hata roho mtakatifu ameacha tuende tujuavyo.Mungu hachunguzwi kama wanasayansi wafanyavyo wakidhani ukiijua sana sayansi umempata la huo ni upofu,hebu mwone Yesu anamwambia Petro ktk Mathayo kuwa damu na nyama havikukufunulia hayn bali Roho mt. ubarikiwe.

 3. Mpendwa,

  Ukweli ni kwamba Mbinguni na peponi ni maneno yenye maana sawa. Yanatumika kumaanisha kitu kimoja.

  Ukisoma Kamusi ya kiswahili au ya kiingereza utaona kwamba neno “Paradise”= Paradiso kwa kiswahili au Heavens = Mbinguni yote yana maana moja tu ya: Mahali penye raha, starehe, burudani na amani tupu.

  Wakristo wengi wamejaribu kutaka kutofautisha maneno haya. Lakini ukitafakari kwa undani bila ya uvivu wala mazoea utakuta kwamba ukisema, “Peponi” au “Mbinguni” au “Paradiso” ni maneno yenye kuwa na maana (Context) moja.

  Paulo pia aliyatumia kumaanisha maana moja tu. Swala la kuna mbingu ngapi? Limekuwa likiulizwa sana hasa kwa kurejea maandiko uliyotolea mfano.

  Mimi kwa uelewa wangu, nadhani wengi wanachanganya mambo ya kiroho na kimwili. Watu wanataka watu waamini kwamba anga linaloonekana kwa macho yetu, eti eneo lenye mawingu, nyota na sayari ndilo mbingu ya kwanza. Wengine wanasema mbingu ya pili ni mahala wakaapo Ibilisi na Mapepo. Na kwamba eti baada ya hapo inafuata mbingu za mbingu yaani akaapo Kristo na Mungu Baba.

  Mtazamo huo mimi huwa siukubali hata kidogo. Hoja zangu ni kwamba Mbingu ni ENEO LA KIROHO na wala siyo eneo linalogusika(Not tangible air space). It is a spiritual world yaani ni ulimwengu wa roho.

  Kuna watu wengine husema kwamba kuzimu ni ndani ya tumbo la dunia. Kwamba watu waovu wafapo huelekea katika tumbo la dunia hii ambapo kuna mateso na moto. Huu nao ni uongo kwa mtazamo wangu. Ukweli ni kwamba Kuzimu nako ni ulimwengu wa roho na wala siyo chini ya ardhi kama wasemavyo wengine.

  Hapo kale hata wakati wa Mtume Paulo, bado watu waliamini kwamba dunia iko kama meza na siyo duara hadi karne nyingi zilipopita ndipo ikagundulika kwamba dunia ni mduara na inalizunguka Jua na kujizungusha kwenye mhimili wake ili kupata usiku na mchana na majira ya mwaka.

  Kutokana na hali hiyo, watu walidhania kwamba kuna mbingu ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne, ya tano hadi ya saba, nk. Lakini ukweli nionao mimi yote haya yanamaanisha picha moja tu.

  Tunaposema Mungu yuko Mbinguni na Shetani yuko kuzimu haya yote ni maneno ambayo huwezi kuyathibitisha haraka haraka endapo utaulizwa mbinguni ni wapi na Kuzimu iko wapi. Wengi husema mbinguni ni Juu na Kuzimu ni Chini. Kwa fikra hizi wengi huendelea kuwa na fikra potofu na kuacha kufikiria kwa upana zaidi. Ukiulizwa Mbinguni ni wapi ukasema ni juu bado watu watabaki na maswali, je ukiwa kwenye Mwezi neno “JUU” litatafsiriwa vipi? Je ukienda kwenye sayari ya Jupter au Mars, JUU ni wapi? Kusema ukweli JUU inakuwa ni DUNIANI unapokuwa huko kwani DUNIA unaiona iko JUU. Sasa JUU ni wapi na Kuzimu ni wapi?

  Watu wanapaswa kuelewa upya kwamba, MBINGU ni mahali ambapo huwezi kupaonesha kwa kusonta kidole chako na kusema, “Mbinguni ni kuleeee” kwa kuonesha kidole juu mawinguni kwa hoja kwamba hata Yesu Kristo alipaa Juu. “Yesu alipopaa Juu” haimaanishi kwamba mbinguni ni JUU yaani anga tunaloona juu yetu. MBINGU ni ulimwenguu mwingine kabisa ambao hauko katika Mfumo wa dunia hii (Solar System). Mbinguni ni Ulimwengu wenye mfumo wake binafsi kabisa (Heavens/Paradise is unseen Non-Solar System World). Tunaposema “Solar System” huu ndio mfumo unaokamilisha mfummo wa maisha ya mwanadamu duniani kwani sayari zote zilizopo zimewekwa na Mungu kumsaidia mwanadama aishi kwa furaha.

  Kwa hiyo, wapendwa wasitake kuamini kwamba Mungu yuko katika Mfumo wa dunia hii(God does not live in this terrestrial world and its solar systems) wala shetani makazi yake hayako katika Mfumo wa dunia hii. Yuko ulimwengu wa roho ambao hakuna mwanadam awezaye kuwatembelea katika mwili huu hata kama angeondoka katika mfumo wa dunia hii (Out of this seen solar system galaxy).

  Nawaomba wapendwa wasomapo maandiko yoyote yahusuyo Mbingu ya kwanza, ya pili, ya tatu, nk waelewe katika upana wa elimu hii na siyo katika fikra za kibinadamu kama tulivyozoea.

  Eee Mungu tunaomba kuelewa siyo Neno lako tu, bali na elimu ya anga pia.

  Mr. Milinga.

 4. Kumbuka andiko linasema yapata miaka 14, kipindi Paulo anaandika kitabu cha wakorintho ni mwaka wa 55 A.D hivyo ilishapita zaidi ya miaka 20 hivyo tukisema ni Yesu itakuwa sio sahihi, wengi wanasema ni paulo na ndio maana anasema sio kama anajisifu. Hakupenda ajitaje moja kwa moja ili isionekane ana jivuna, na ieleweke haya yalikuwa ni maono wala sio kitu phisically. Peponi ni mahali pa mapumziko kabla ya kuingia mbinguni ambapo ni mbingu ya pili na mbingu ya tatu ndio huko aliko Kristo. Mbingu ya kwanza ni hili anga tunaloliona kwa macho yetu. Barikiwa.

 5. Ndugu Judicate,Yesu atukuzwe sana.
  1. Paulo alikuwa anajibu swali juu ya Yesu.Maana,watu walidhani kuwa Yesu ni mwanadamu wa kawaida.Hivyo,mtume Paulo alijaribu kutetea hoja ya Yesu ambaye alikuja katika umbo la mwanadamu.Yesu ndiye Mungu,John(Yohana8:58) na angekuja kama alivyo,tungemwogopa;Kutoka19:17-21 utaona jinsi gani watu waliogopa kukutana na Mungu ila,Musa tu ndo aliweza.
  2. Zipo mbingu tatu,soma ufunuo21:1-2.
  a;ya kwanza,ndoo hii tuliyomo.
  b;ya pili,ni sehemu ya mapumziko kwa walio watakatifu,Peponi.watakatifu wakilala,hawaendi mbinguni kwa Yesu moja kwa moja.wanaenda peponi;mbingu ya pili.
  c;ya tatu,ndo huko alipo Yesu.na hakuna mbingu zaidi ya ile aliyomo Yesu(Mfalme wa wafalme).
  3. Peponi ni sehemu ya mapumziko kwa watakatifu.Na,kuzimu ni pa shetani.mahali alipofungiwa pamoja na wafuasi wake na wanaotenda dhambi hapa duniani.Na baada ya siku ile ya hukumu ndo watatupwa jehanamu(moto wa milele na milele).
  Nadhani,kwa hayo utapata uelewa kuhusu hayo maswali uliyo nayo Judicate.Ubarikiwe!.
  by Precious.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s