Kumradhi!

Bwana Yesu asifiwe Watembeleaji SG na Familia ya SG! Kuna wengi wanaotuma mail, simu kuhusu mjadala huu na ule kuwahusu watumishi wa Mungu Nabii TB Joshua na Mtume na Nabii Josephat Mwingira. Tunaomba ieleweke kwamba nia na lengo letu sio KUBOMOA ila ni kufundishana, kuonyana ili KUJENGA mwili wa Kristo.

Hivyo basi kutokana na maoni mbali mbali, tunajifunza kutoka kwa watumishi wanaotuma maoni yao hapa na kuna ambao wengine tunafahamu huduma zao wanazozifanya na kuwaona wakifundisha sehemu mbalimbali pamoja na magazetini Mfano: CK Lwembe ambaye wamemlalamikia sana.

Hii inatufanya kufahamiana, uwezo wetu katika kumjua Mungu pamoja na kupokea changamoto na naamini kuna ambao Roho Mtakatifu anasema nao kupitia maoni ya mada mbali mbali zinazojadiliwa hapa…kuna ambao Mungu anawatumia hapa vyema, kazi yenu si bure, kuna mbegu inapandwa kwa mtu.

Msimamo wa Strictly Gospel ni Neno la Mungu. Nasi tutajitahidi kukaa hapo. Kama Mtu atakuja kwa nia ya kuharibu. Hatutaruhusu maoni yake. Yapo maoni tunayoyazuia, yanaoonekana hewani ni kwa kujifunza, Mtu asipotaka kujifunza. Tafadhali unaweza kujadili kwenye blogs nyingine zisizo na mipaka ya Neno la Mungu.

Tunaomba radhi kwa makwazo yoyote mliyoyapata.

Mungu awabariki na karibuni tena!

Advertisements

24 thoughts on “Kumradhi!

 1. Nawatakia siku njema wale wote wenye Mapenzi Mema na SG na Hata wale wasiyona mapenzi mema na SG kwakuwa wanashiriki mahali hapa basi kwaku shiriki kwao tu Kwa Neema ya Mungu ipo siku watabadilishwa Na Mungu mwenyewe, watakuwa na Mapenzi mema na SG Wanzilishi SG, hakika Maono yao Haya ni Mazuri na ni makubwa sana kwa mtazamo wa ki-Roho zaidi na hayo maono ndiyo yaliyotukutanisha hapa hapa, na tunaendele kuwepo na kwakuwa maandiko matakatifu yanasema wakutanapo watu wawili watatu kwa jina langu na mimi nipo pamoja nao Mathayo 18:20 Ninaamini sana juu ya kukutana kwa jina la bwana kumbe watu wanaweza kukutana maalufu Mungu asiwe katikati yao,ila kwa jina lake ndipo anakubali kuwa katikati yake kwakuwa Tupo hapa kwa jina la Mungu ninaamini blog hii, muovu hana Nafasi wala Mamlaka ya kuiba kuharibu wala kuivuruga kwa namna yeyote wala kwakuwa Mungu anaifahamu na watu wanaipenda na wanaiombea Mungu usiku na Mchana ili iwepo hapa hivyo Ushindi ni mkubwa kuliko kushindwa na Hatupo tayari kujifunze kwa aliyeshinwa kwakuwa tutapata sababu ya sisi kushindwa pia, kusonga Mbele ni vizuri kujuwa ni wangapi hawawezi na kuwafahamu ila kujifunza kutoka kwao ni Hatari kwakuwa Aliyeshindwa anasababu nyingi Mno za kushindwa kwake, Hawa wanaotupatia changamoto ni kama kipindi cha baridi kabla ya Mvua kunyesha changamoto ni Daraja la kule tuendako zinatuandaa kutufikisha katika kusherekea ushindi, kwakuwa yale unayoyaweza wengine inawezekana wanayashindwa kufanya na hiyo ndiyo maana halisi ya mafanikio ni kufanya kile mwinine atatamani kukifanya na akikiweza mtashangilia kwa pamoja ila akishindwa utashangilia peke yako wakati yeye anahudhunika, wapendwa usikubali kupimwa kwa kuwa umeshindwa mara ngapi bali kubali kupimwa umeweza Mara ngapi, NA TAMANI SANA KUJIFUNZA KWA WALE WOTE WALIOWEZA neno kushindwa ni chumba cha giza ambako huwezi kufanya lolote la Maendeleo yako , Mungu awabariki sana, Ninamshukuru Mungu kwa kuniruhusu kupita katika SG Mahali ambako kuko na changamoto nyingi sana, Mimi ninafurahishwa sana na hizo changamoto maana ninatambuwa yakuwa ninahitaji changamoto ili Mungu atukuzwa kupitia hizo changamoto mimi, ninayo maoni mengi ila kwa leo, ninaomba niishie hapa ninashukuru kwa wote
  Ni Mtumishi wa Mungu, toka Mwanza-Geita huduma ninayo simamia Calivary Assemblies of God, Kwa ushahuri Maombezi masaa 24 siku 7 za juma karibu ni bure piga simu, 0756 809 209, 0654 29 42 19

 2. Let’s not entertain men, we must not quench the Holy Spirity. ”(1)Wengi watakuja kwa jina langu”(jina la YESU); (2)”Jihadharini na manabii wa uongo”; (3)”Mtawajua kwa matunda yao”; (4)Jilindeni nafsi zenu”. (5)”LAKINI SAA INAKUJA, NAYO SASA IPO, AMBAYO WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI”-Yohana4:23-24. TUFUATILIE VIZURI MAANDIKO HAYA NA TUWE MAKINI. MARANATHA.

 3. Ndugu yangu Sam,

  Labda kutumia kwangu neno Orthodox kwenye zile mada zilizopita kulieleweka na kutoa tafsiri nyingine ambayo sikuwa na maana nayo………..nililitumia kwa maana hii tu…..

  or·tho·dox   [awr-thuh-doks]
  adjective

  1
  customary or conventional, as a means or method; established.
  2
  sound or correct in opinion or doctrine, especially theological or religious doctrine.
  3.
  conforming to the Christian faith as represented in the creeds of the early church.

  Sikuwa kabisa na maana ya Kidhehebu….Kanisa fulani……! Samahani sana kama sikueleweka….

  UBARIKIWE.

 4. Ndugu yangu Orbi!

  Ahsante sana kwa maoni yako ambayo naamini yatatusaidia wengi sana tunao pita katika blogu hii. Ninaweza kusema kwa uhakika, kuwa kwa maoni yako, kama sote tutafika hapo, tutakuwa tumefika kwenye ‘common ground’. Kutokea hapo, sasa twaweza kuyaendea majadiliaono katika uelewa mpana unaoruhusu kujifunza kwa uhuru mkubwa uliojikita katika upendo, ahsante sana!!

  Nikirudi kwenye lile suala la IMANI tunalolizungumzia, kumekuwa na reference nyingi tofauti tofauti kama zilivyojitokeza kwenye michango katika mada zinazoendelea, pamoja na michango yako, zinazotuelekeza kwenye “kanisa la kwanza”; “kanisa la Orthodoxy”; “kanisa la mitume” na “kanisa katoliki”. Hebu nipanue uelewa kuhusu mambo haya , which is which?

  Ahsante sana ndugu Orbi
  Mungu wetu atufunue ufahamu!

 5. Ndg. Yangu John Paul,
  1. Wapendwa, nawasalimuni wote katika jina la Bwana wetu Yesu kristo. Nilitaka kuamini kuwa Ndg. Yangu John paul upo sawa na ninavyowaza, uliposema kwamba, nanukuu….” Mi naamini kabisa kuwa lengo la SG ni kuwakutanisha watu hapa ili baada ya mijadala TUWEZE KUTAMBUA IMANI SAHIHI NA KUIFUATA. Haitakuwa na maana kabisa kama kila baada ya mjadala kila mtu atabakia NA IMANI YAKE! Sasa maana ya kukutana hapa itakuwa ni nini? Haitakuwa ni kupoteza muda?” mwisho wa kunukuu. Baadaye kidogo nilipoendelea mbele katika maelezo yako, ulinitia moyo sana uliposema, nanukuu……..” Hata mimi sitakuwa na sabababu ya KUJADILIANA NA WATU HAPA halafu baadaye NIRUDIE KULE KULE NILIKOKUWA. Bali naamini hapa ni mahali pa KUJIFUNZA. Tunajifunza kwa kadri ya Neno la Mungu, ili mtu akiona IMANI yake iliposimama si SALAMA, basi AIGEUKIE IMANI SAHIHI” mwisho wakunukuu. Nilipoendele kusoma maelezo yako kusema kweli, ulinivunja moyo, maana niliona kama unaugeuza Mpira kushambulia goli unalolilinda, katika usemi ufuatao, nanukuu…..” Kwa hiyo naamini ni HAKI kabisa ya blog KUFUTA baadhi ya maoni ya watu yanayopotosha. Hata nami ikitokea NINAPOTOSHA niko tayari tu KUFUNGIWA kuliko nipotoshe lengo na kusudi la blog!” Sasa maswali yangu ni hivi, UTAJUAJE UKWELI KAMA HAKUNA UPOTOSHAJI? NA UTAUIJUAJE IMANI YA KWELI KAMA HAKUNA IMANI POTOFU ? Ni hivi, kila mtu ana MALI Isipokuwa inapokuja kupimwa thamani yake, viyohivyo kila mtu ana IMANI yake, isipokuwa ikipimwa kwa kigezo cha Neno la Mungu ndipo hujulikana THANI YAKE – yaani kama ifuatwe ama la! Mara zote ushindi upo kwa mshindi, na bila mashindano hakuna mshindi! Haupo mjadala ukaitwa mjadala kama hauna pande mbili zenye mawazo mawili kinzani! Mungu alimuacha shetani hai, ili awapate wafuasi wa kweli chini ya mjadala mkali wa WALIOUPANDE WA SHETANI na WALIOUPANDE Wa MUNGU. Nionavyo mimi, blog iwe katikati ili kuwaongoza watu wasiende NJE ya mjadara au maada iliyopo mezani, na maada zote ziwe zinatokana na BIBLIA na wachangiaji wajiepushe lugha kali, dharau, majivuno, ushabiki wa kimadhehebu, kiburi wote wasimamie misingi ya BIBLIA, maana blog yenyewe ni ya KI- KRISTO. KUWAFUTA waliyo na mawazo yasiyokubaliwa na WENGI, kwa maelezo kuwa ni WAPOTOSHAJI ni woga usio na sababu, kwanza mpotoshaji atampotosha nani, iwapo wote Tutayapima yasemwayo kwa mjibu wa Neno la Mungu na kwa uongozi wa Roho mtakatifu? Ulisema pia ,….“ Hata nami ikitokea NINAPOTOSHA niko tayari tu KUFUNGIWA kuliko nipotoshe lengo na kusudi la blog!” Sijakuelewa, kwanini kaka John unafikiri ipo siku unaweza kupotosha na ufutwe kwa upotoshaji? – wakati huo utakuwa unampotosha nani?, ikiwa ulisema pia kuwa,…. “Tunajifunza kwa kadri ya Neno la Mungu, ili mtu akiona IMANI yake iliposimama si SALAMA, basi AIGEUKIE IMANI SAHIHI” mwisho wa nukuu. Mimi nakubaliana na Ndg Sam, aliposema……”Lakini, definition ya IMANI ndiyo inayoleta changamoto ya majadiliano baina ya pande zinazo kinzana licha ya wote kudhani tuko katika Imani moja. Tofauti na hilo, SG inaweza kujikuta imejiegemeza katika tafsiri ya Imani fulani, hivyo KUIUA blog!” mwisho wa nukuu. Na pia nakubaliana na Ndg. Yangu Orbi, aliposema……” definition ya Imani ilisumbua kanisa la Kwanza…..imesumbua kanisa la Kristo karne na karne………hata madhehebu tuliyo nayo leo ni matokeo ya “definition ya Imani”….hivyo tusiogope kuleta majadiliano yanayokinzana….hatutakuwa wa kwanza…….Nia ya kila mmoja iwe ni kuujenga na kuutea mwili wa Kristo na Neno lake…..” mwisho wa nukuu. Nionavyo kama SG itaifanya Blog iegemee maoni ya Imani ya upande fulani tu, na kudhani kuwa changamoto zinazotolewa ni upotoshaji basi, Blog lazima IFE, Maana HAKUNA MJADALA usio na mawazo mawili KINZANI!
  Mbarikiwe wote.

 6. Sam,

  Umenifurahisha na kunipa changamoto kwa nukuu yako hii……

  “Lakini, definition ya IMANI ndiyo inayoleta changamoto ya majadaliano baina ya pande zinazokinzana licha ya wote kudhani tuko kwenye imani moja”

  Nakubaliana na wewe….definition ya Imani ilisumbua kanisa la Kwanza…..imesumbua kanisa la Kristo karne na karne………hata madhehebu tuliyo nayo leo ni matokeo ya “definition ya Imani”….hivyo tusiogope kuleta majadiliano yanayokinzana….hatutakuwa wa kwanza…….Nia ya kila mmoja iwe ni kuujenga na kuutea mwili wa Kristo na Neno lake…..asante mno kwa nukuu yako.

  Naamini timu ya Strictly Gospel imekuelewa.

  UBARIKIWE

 7. John Paul, ooh, umekwenda mbali sana!

  Nilikuwa nazungumzia ile ‘Kumradhi’ na ile mijadala iliyopelekea hiyo kumradhi, pamoja na response zake. Kama umeipitia vizuri, unaweza kuona nilichokisema kuhusu ‘mijadala isiyogusa MIHIMILI ya IMANI zetu’. Yaani ufike mpaka kwenye kukwazika, ndio unaweza kuona sababu iliyonifanya nishauri hivyo ili angalau wote tuwe na Amani!

  Blog ipo, na itaendelea kuwepo kulingana na MAONO yake iwapo itabakia hapo. Leo, kati ya washirika wake, wako ambao wanakwazika kwa mijadala kama hii iliyokuwepo na pia wapo ambao wamenufaika kwa namna moja au nyingine. Tena hatua iliyopo blog leo, kadiri tunavyosonga mbele katika wakati, tunaweza kutegemea ukomavu zaidi huko mbele kiasi kwamba mijadala kama hii iliyowakwaza watu leo, ikawa changamoto zaidi kwetu sote na hivyo kutujenga katika IMANI ya kumjua zaidi KRISTO! Kama Maandiko yanenavyo, “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.“ Basi tegemeo letu kuu ndilo hilo, nayo blog inachotufanyia ni kuwa catalyst katika hiyo HUDUMA ya BABA, hiyo inayotuvuta kwenda kwa Kristo!

  Kwa hiyo nadhani ni vizuri tuwe katika ufahamu wa kuijua mipaka ya Mungu na nguvu zake, na ile ya kibinadamu ambayo kwayo wakati mwingine twaweza kulitolea maamuzi jambo fulani tukiongozwa na makwazo yetu. Nikikunukuu katika usemi wako, “Si mahali pa watu kuja hapa na IMANI tofauti, huku zingine ZIKIWA SI SALAMA, halafu wakimaliza KUJADILIANA MIJADALA YA KAWAIDA, warudie IMANI ZAO. Hapo hapatakuwa na maana yoyote ya kujadiliana.” Lakini, definition ya IMANI ndiyo inayoleta changamoto ya majadiliano baina ya pande zinazo kinzana licha ya wote kudhani tuko katika Imani moja. Tofauti na hilo, SG inaweza kujikuta imejiegemeza katika tafsiri ya Imani fulani, hivyo KUIUA blog!

  Basi mwelekeo halisi wa blog unapashwa kuwa ule walioanza nao, ambao kubaki katika huo, sote twapashwa kuwaombea ili blog hii iendelee kuwa ni blog pekee inayoweza kukupa fursa ya kuweza kuyajadili yale mambo makuu makuu mbali na kanuni za ‘mahema’ na usimamizi wao, nasi tuzoelee hali hiyo na kuyachukulia hayo katika umbali huo, ndipo tutayaona manufaa yake!

  Ubarikiwe John Paul na woote!

 8. Sam,

  Mimi nimeguswa na Maneno yako uliyoandikwa hivi:

  “Lakini tukiwafanya SG kuwa wametubia makwazo yetu, moja kwa moja tutakuwa TUMEIUA BLOGU! Tunapaswa kuwapongeza na kuwatia MOYO na kwamba uhuru wa kujadili wasije wakauondoa bali wajaribu kutuwekea mijadala ya kawaida isiyogusa MIHIMILI ya IMANI zetu.”

  Na kutoka hapo ninachukua hili:

  “……bali wajaribu kutuwekea mijadala ya kawaida isiyogusa MIHIMILI ya IMANI zetu.”

  Mi naamini kabisa kuwa lengo la SG ni kuwakutanisha watu hapa ili baada ya mijadala TUWEZE KUTAMBUA IMANI SAHIHI NA KUIFUATA. Haitakuwa na maana kabisa kama kila baada ya mjadala kila mtu atabakia NA IMANI YAKE! Sasa maana ya kukutana hapa itakuwa ni nini? Haitakuwa ni kupoteza muda?

  Suala la IMANI ndiyo kila kitu katika maisha ya mtu! Ninaamini Waendesha blog hii wako na IMANI wanayoiamini. Na ninatumaini kabisa walianzisha blog hii katika misingi ya IMANI hiyo. Na kutokana na kusoma na kuangalia jinsi ilivyoandikwa hapo juu, kulia, unaweza kuona kuwa IMANI inayoendesha blog hii ni IMANI KATIKA YESU KRISTO. Ni blog ya Injili. Blog kwa ajili ya kueneza Habari za Yesu Kristo.

  Sasa tukisema wawe wanaweka “mijadala ya kawaida” na “isiyogusa IMANI zetu” hapo tutaifanya blog hii nayo kuwa YA KAWAIDA. Yaani isiyohusiana na mambo ya IMANI.

  Nijuavyo mimi blgo za “mijadala ya kawaida” ziko nyingi sana. Ndiyo maana blog hii IKAJIKITA KATIKA MISINGI YA NENO LA MUNGU ili watu kupitia hapa WAWEZE KUIFAHAMU INJILI NA KUMWAMINI YESU KRISTO, na baadaye waweze kumuona Mungu.

  Si mahali pa watu kuja hapa na IMANI tofauti, huku zingine ZIKIWA SI SALAMA, halafu wakimaliza KUJADILIANA MIJADALA YA KAWAIDA, warudie IMANI ZAO. Hapo hapatakuwa na maana yoyote ya kujadiliana. Hata mimi sitakuwa na sabababu ya KUJADILIANA NA WATU HAPA halafu baadaye NIRUDIE KULE KULE NILIKOKUWA. Bali naamini hapa ni mahali pa KUJIFUNZA. Tunajifunza kwa kadri ya Neno la Mungu, ili mtu akiona IMANI yake iliposimama si SALAMA, basi AIGEUKIE IMANI SAHIHI, imani ya KUMWAMINI YESU KRISTO. Na kwa njia hiyo lengo la Blog litakuwa limefanikiwa.

  Hayo ndiyo maoni yangu. Kwa kuwa SI VEMA blog ikakosa mweleleo,. Yaani kila mtu aandike tu anavyojua mwenyewe. Hapana. Ni lazima kuwa na MODERATION ya COMMENTS kwa ajili ya kuweka uelekeo. Kwa hiyo naamini ni HAKI kabisa ya blog KUFUTA baadhi ya maoni ya watu yanayopotosha. Hata nami ikitokea NINAPOTOSHA niko tayari tu KUFUNGIWA kuliko nipotoshe lengo na kusudi la blog!

  Nashauri kuwa tunapojadiliana hapa tujadiliane kwa lengo la KUJIFUNZA NA KUCHUKULIA HATUA YALE TUJIFUNZAYO! Na kama italazimika kubadilia IMANI basi itakuwa ni vema ikiwa badiliko hilo LITAMSOGEZA MTU KARIBU ZAIDI NA MUNGU.

  Sina muda mzuri wa kukaa kwenye kompyuta, kwa hiyo inawezekana ukaniuliza kitu halafu nikachelewa kukujibu.

  Mungu atusaidie!

 9. Ndugu Sam,

  Tatizo la wengi wanaompinga T.B.Joshua ni kwamba wanafahamu zaidi waganga wa kienyeji na utendaji wa shetani lakini hawana ufahamu wa Mungu na utendaji wa Roho mtakatifu.

  Kwa hiyo kipimo chao ni Shetani (yaani shetani ndiyo “standard” yao au kwa lugha nyingine Shentani ndiyo BenchMark)

  Kwa hiyo kila kinachofanyika wanakipima kwa kutumia ufahamu wao wa mambo ya shetani na jinsi wanavyo mheshimu shetani.

  Kama nilivyowahi kusema huku nyuma watu wengi wanamheshimu na kumtambua shetani zaidi (they have confidence in the power of satan and are believers in the “supremacy of satan”)

  Waefeso 1:17 Mungu amemketisha yesu mkono wa Kuume na amemketisha juu sana ya falme, mamlaka, usutani na juu ya kila jina litajwalo katika ulimwengu huu na ujao pia.

  Ahsante

 10. Ndugu Nduta, hivi hujawahi kusikia waganga wanaokamata wachawi? kama wakina Manyanyau.

  Mungu atusaidie!!

 11. Bwana Yesu asifiwe wapendwa.
  Napenda kutoa pongezi zangu kwa wenye SG, nimefurahishwa na jinsi walivyoingilia yale machache ambayo pengine yalionekana au yalitaka kuwa kikwazo kwa watu na wadau wa blog hii kwa ujumla. Kwa kifupi nilivyojua mimi hapa tupo kujifunza na kwamba tunamsikiliza roho mtakatifu bila ushabiki wowote, kupitia michango na maoni mbalimbali yawe mafundisho kwetu,tuzijue mbivu na mbichi zilizoifunika Dunia hii. KILICHOKUJA KUNISHANGAZA NILIONA WATU HAWaNA HAJA TENA YA KUANGALIA BIBLIA KAMA KIONGOZI, badala yake kushutumiana na kubambikana majina na matamshi ya kejeli kujiona wajuzi na kwamba wao ndio wenye Neno la Mungu na kwamba ati Ndugu zao wengine wakawaona ni wapotoshaji na kutaka hukumu itolewe ya kuwaangamiza “wapotoshaji” hao! Neno la Mungu linasema, Kanisa la Bwana Yesu Kristo KAMWE MILANGO YA KUZIMU HAITALIANGUSHA! Sasa sijajua watu kwanini hawaliamini Neno la MUNGU na hata kutolisikiliza, wamefunikwa hofu na woga wakutoangusha Hadhi zao za kimadhehebu! Kwa Neno hilo tu, mimi Napata ujasiri wa kusema kuwa watu wengi ni washabiki au wapenzi wa Ukristo, bila kutaka KUJIPELELEZA kama ni wakristo kweli. Mfano mpenzi au shabiki wa Timu Fulani ya mpira, huishangilia na hata kutokula timu husika ikfungwa! Shabiki au mpenzi,huvaa sale sawa na timu husika, hukaa upande uleule wa timu husika na hushangilia kwa bidii zote na kwamba huiiita ati ile timu aliyoko ni YAKE! Sasa ona, Mtu huyu kwa kweli hana kadi ya chama na hata pengine anayo hailipii, tatizo huja wanapotakiwa WANACHAMA HAI TU, Ili ladba waingie katika chumba cha mkutano wa timu husika, ndipo washabiki na wapenzi hao hubaki wameduwaa na hawana la kufanya! Kamwe huwezi kujua nyeusi kama nyeupe haipo, wala huwezi kulijua giza kama nuru haipo! NDPO INAPOKUJA MAANA YAKUWA NGANO IACHWE IKUE NA MAGUGU PAMOJA – Hadi mvunaji aje! Lazima upande mmoja utoe hoja za udadisi na upande mwingine utoe hoja za ufumbuzi, hapo ndiyo mjadala hukolea lakini yote lazima msingi wake uwe ni NENO LA MUNGU na Roho mtakatifu aachwe atumike kama mwalimu na si vinginevyo! Asanteni wana SG, ila UOGA NI DHAMBI. Mbarikiwe wote.

 12. Wapendwa,

  Kama mliangalia ibada ya Synagogue leo Machi, 11. Mtakuwa mmemuona kiongozi wa New Hope Ministry ya Nigeria akienda kufanyiwa deliverance na kukiri yeye mwenyewe kuwa ni mganga wa kienyeji (Spiritualist) na kuwa alianzisha makanisa ili kuficha ukweli unaomhusu kwani alikuwa anatumia nguvu za giza huku akijiita ni Nabii.

  Sasa sijui kuna uhusiano gani na New Hope Ministry niliyoisoma hapa kwenye blog yetu ya SG.

  Mimi ninaamini kabisa kuwa wengi wanaopinga huduma ya TB Joshua ni kutokana na kiwango kidogo cha uelewa wa Mungu na utendaji wake. Wengine waliobakia ni masuala ya wivu wa kihuduma tu,
  Kundi la mwisho ni la wale ambao wanatatizo la kimadhehebu.tunafahamu lile dhehebu kongwe la kiroho ni wapinzani wa huduma “independent” (Nond denominational)

  Tangu lini mtoto wa darasa la kwanza akawa na ujuzi wa kumkosoa mtu wa sekondari? Ndivyo ilivyo kwa wengi hapa watakapopata roho ya hekima na ufunuo (efeso1:17) wataelewa lakini cha kusikitisha ni kuwa watakuwa wamepotosha wengi.

  Kiwango cha T.B. Joshua ni kikubwa , kitu kinachopelekea wengi kuchanganyikiwa.

  Mimi binafsi nimeshafika kwenye kanisa la Synagogue church of all nations na nilibarikiwa sana.Ninamshukuru Mungu kuwa nimepata fursa ya kutembelea mataifa mbalimbali na huduma kubwa mbali mbali za kiroho ulaya na usa.

  Huduma ya TB. Joshua ni baraka ya Afrika.

  AMPOKEAYE NABII KWA KUWA NI NABII ANAPOKEA THAWABU YA YULE NABII. Mathayo 10.41

  NA AMPOKEAYE MJUMBE ANAMPOKEA ALIYEMTUMA.Yohana 13:20

  NATOA POLE KWA WALE WANAOSEMA “HAKUNA CREDIT” KUMPOKEA NA KUMKUBALI NABII.

  MBARIKIWE.

 13. Shalom SG. Binafsi naomba niwapongeze walioanzisha blog hii, nimejifunza mengi kutoka kwa wachangiaji mbali mbali. Mpaka sasa ninawajua wenye hekima na wanaoandika kupotosha.Changamoto zinazojadiliwa hapa, naomba zisikome ziwepo, watu wafunguliwe macho, tujifunze kwa wanaojua zaidi. Mungu awatie nguvu wote. Amen

 14. Wana SG

  Mbarikiwe!

  Wandugu, mbona tunashindwa kuelewana katika majadiliano? Kwanini tunapenda nafasi za juu? Jamani tusome maoni, tuyatafakari, tuiangalie mijadala inatutaka tuchangie nini halafu ndio tuandike kulingana na mijadala, vinginevyo tunaishia kuyageuza mambo na kuyapeleka kusikotakiwa!

  Angalia hii “KUMRADHI” ya SG, naona wengi wanafikiri eti SG wameomba MSAMAHA! Kumradhi maana yake ‘EXCUSE ME’ ua ‘PARDON ME’ yaani kimatumizi, ni ule usemi unaotumika mtu anapoingilia kati mazungumzo ya watu wawili au zaidi na kuhitaji myasimamishe kidogo mumsikilize yeye. Hicho ndicho walichofanya SG.

  Wamesema imewabidi wafanye hivyo baada kupigiwa simu na barua pepe wakilalamikiwa kuhusu mijadala hiyo waliyoitaja.

  Pia wameweka wazi Msimamo wao, ambao tunatakiwa kuuelewa kama sharti la kujumuika nao na wapendwa wengine, kuwa wao wanasimama katika Neno la Mungu na si dhehebu lolote. Tukilijua hili tutegemee mijadala motomoto, hapo ndio tutaweza kujifunza mengi na kufahamiana vizuri na KUPENDANA licha ya tofauti za mitazamo yetu!

  Lakini kutokana na hizo simu na barua, ndipo wakajua kuwa kuna wapendwa wengine ambao wamekwazika kwa mijadala hiyo. Nao wakiwa ni wasimamizi wa mijadala hiyo, hekima ikiwa imewatawala, wakaingilia kati ili kuwa upande wa waliokwazika angalau kuwapa nafasi ya kuyakulia mambo hayo. Ndio hiyo kumradhi!!

  Lakini tukiwafanya SG kuwa wametubia makwazo yetu, moja kwa moja tutakuwa TUMEIUA BLOGU! Tunapaswa kuwapongeza na kuwatia MOYO na kwamba uhuru wa kujadili wasije wakauondoa bali wajaribu kutuwekea mijadala ya kawaida isiyogusa MIHIMILI ya IMANI zetu.

  Mungu wetu na atupe uvumilivu!

 15. Bwana Yesu asifiwe!

  Maoni yangu mimi ni haya:

  Ninashukuru Mungu kwa kuwa SG wameona tatizo hilo na kuamua kuliweka wazi ili kila aliyeumizwa na hali iliyotokea aweze kutambua kuwa kuna mtu amejali na kisha ameomba msamaha! Ingewezekana kabisa kufuta maoni au kuzuia mengine kimya kimya tu, pasipo kuweka wazi tatizo lililopo. Sasa hatua hii ya kuliainisha tatizo kisha kuomba msamaha mi naona ni hatua ya juu katika ukristo! Si wakristo wengi anaweza akakosea kisha akajitathmini na kugundua halafu aombe msamaha. Ndiyo maana hata makanisani mwetu kuna migogoro mingi sana itokanayo na watu KUANGUKA KATIKA MAKOSA lakini mtu huyo anaendelea kufanya shingo ngumu pasipo kuomba msamaha na kubadili mwenendo!

  Kwa hiyo, jambo hili la kuomba msamaha, au kuomba radhi kama lilivyoandikwa, mi naona ni jambo linalostahili pongezi, Naamini kabisa moyo huu ungekuwemo kwa wingi katika mwili wa Kristo, tusingekuwa na majeraha mengi kama ilivyo leo, katika makanisa, makwaya, vikundi vya maombi nk. Kwa hiyo mi binafsi napongeza hatua hiyo!

  Sasa ushauri wangu ni kuwa Kwa kuwa SG wameshaomba msamaha baada ya kuliona tatizo lilipo, basi ni jukumu letu sasa KUSAMEHE, KUONDOKA HAPO, TUENDELEE MBELE! Maana tukiendelea kulaumu na kuendelea kutahadharisha, kwa jambo ambalo tayari lilishagundulika, hiyo ni SAWA NA KUMPIGA MTU MAHALI PENYE JERAHA! Mfano mtu kaanguka kwa pikipiki kisha wewe ukafika na kuanza kumpiga pale pale alipoumia, kwa lengo la kumkanya! SG wameomba msahama. Hakuna kuomba msahama kusiko na gharama na gharama ni maumivu! Kwa hiyo twatakiwa sasa tuwatie moyo na kukubali kuwasamehe na ninatumaini kabisa nao wamepata changamoto mpya ambayo itafanya kuwe na umakini zaidi katika kusimamia mijadala!

  Maana inawezekana hapa tena pakawa na mtego mwingine, kila mtu akitamani amalizie hapo maumivu yoote aliyoyapata kutokana na mambo yaliyotokea na hivyo tukajikuta tunazunguka hapoa hapo. Mi nashauri kuwa yale tuliyo nayo ya kuwashauri tuyafanye hivyo kwa upendo lakini yale ya kulaumu yasiendelee kuandikwa maana hiyo haitusaidii tena kwa kuwa ugonjwa umeshajulikana na dawa tayari wameshaijua. Bali tuendelee mbele kwa moyo ule ule uliokuwepo mwanzo na pia tuendelee kuwaombea maana SIYO KAZI RAHISI kupambanua maoni yoote yanayoingia ili kuweza kupembua mchanga toka katika mchele. Tuwaombee ili Msaada tokwa kwa Mungu uwe juu yao! Ili waifanye kazi hiyo kwa usahihi, pamoja na Kristo mwenyewe!

  Ninawashukuru ndugu walioandika kukubali maoni yangu kwenye mijadala. Pia namshukuru ndugu aliyeandika kuwa nami huwa nakosea, na ametoa mfano hai, mahali ambapo nilikosea na nikagundua kuwa nimekosea na sababu iliyonikosesha niliiandika, nikaomba msamaha kisha kubadili msimamo. Ninaamini kabisa tukienda kwa moyo wa ushirikiano namna hii hakuna kitakachoharibika! Na Mungu atusaidie kuwa na tabia ya kujichunguzam na mara mtu ukiona ulipokosea, basi unageuka haraka na safari inaendelea. Siyo lazima hadi ufukuzwe na Moderator! Hiyo haiwezi kuwa hali nzuri!

  Mungu atusaidie tunapoendelea kujifunza katika mijadala mbali mbali, kuombeana pamoja na kuulizana na kujibiana maswali kadha wa kadha yanayohusu safari hii ya Mbinguni!

  Mungu atusaidie!

 16. nashukuru sana kwa post hii. ila SG nimeshindwa kuelewa neno moja hapo kwamba mnamtetea ndugu C.K.Lwembe kwa sababu mnamfahamu au mlikuwa na maana ipi? la pili ninachoona mimi hapa ni kwamba watu waliotajwa direct kwamba wana mapungufu fulani wanachokifanya ni kujitetea zaidi.
  ukweli ni kwamba hata mimi nashindwa kuielewa blogu hii jinsi siku zinavyokwenda. imekuwa sio ya kujifunza tena ila ni ya kuzodoa watumishi wa Mungu.
  take care.

 17. SG,Amani ya Kristo iwe juu yenu
  Wapendwa ….
  Nina shauri,
  Tumeifikia huzuni ya Mungu iliyotopelekea tutubu(toba) ,hakuna haja kurejea na kujitetea yale manyonge tuliofanya tusameheane na kusahau,Tumetenda dhambi tumepungukiwa na Utukufu wa Mungu,Bwana Aturehemu.
  Habari ya kupatana ……
  ‘Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Mathayo18: 19-20
  Yatupasa kufkia kimo hiki cha Malaki3:16-18
  “Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.”
  SG,Moderator shika zamu yako sawasawa, kuna watoto wachanga wa kiroho hapa,
  Imeandikwa
  “Bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari. Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!’ Mathayo18:6-7
  Nami ninawaomba radhi wale wote ambao nimewakwaza kwa maandiko yangu.
  Bwana ni mwingi wa Rehema,Aturehemu.
  Barikiwa,

 18. Ndugu Akongamimi, naona umeenda mbali sana mpendwa kwa kauli yako. Mimi nakushauri neno la Mungu ndilo liwe KWELI yako ya mwisho ya kuingalia na siyo mwanadamu amesema au hajasema nini? Kuhusu ndugu John Paul ni kweli hutoa maoni ya kujenga lakini kuna wakati naye huwa anakosea mfano ktk ule mjadala wa Talaka vs Kuachana kama ulikuwa unaufuatilia! Naye alilitambua hilo na kubatilisha maoni hayo!

  Ubarikiwe!

 19. Wapendwa katika Kristo!

  Napenda kuwashukuru nyote mlio katika blogu hii, kwa ushirikiano na pia uvumilivu wenu katika yote. Ninafahamu kuwa wengi wamekwazika na michango yangu katika mada mbili tatu nilizochangia, ambazo maudhui yake yalijikita zaidi katika changamoto za ki IMANI. Jambo la msingi ambalo ninawaomba wana SG na wengine wetu tunaopita katika blogu hii tulifahamu, ni kwamba tunazo tofauti nyingi katika Imani yetu ya Kikristo. Ufahamu huu utatupa fursa nzuri ya kujifunza yale ambayo hatuyafahamu na pia kutupa uelewa zaidi wa Imani yetu.

  Pia kutokana na makwazo yaliyowapata, wana SG wengi walijifikisha katika kuamini kuwa mimi nimevamia blogu hii ili nieneze sumu, au kwamba natafuta waumini au nimekuja kubomoa na mambo ya jinsi hiyo. Lakini napenda niwaeleze kuwa sijawa na nia kama hizo wakati wowote ule. Msukumo wangu siku zote umekuwa KURUDI pale MWANZO, kanisa la Mitume! Ni katika theme hiyo, nimekuwa nikiandika, hata SG wakanikaribisha in good faith, nijiunge nao ili kuleta changamoto hiyo ya ki Imani, na si kwamba labda hawa ndugu walioachiwa kuindesha blogu hii wametoka nje ya ONO kwa kunikaribisha au wameniita au chochote kile wanachowazia, ilmradi kuwafanya tu kuwa wamepotoka, hilo si kweli! Naambatanisha Email niliyotumiwa kuhusu jambo hilo. Nimeondoa na. ya simu ya aliyenitumia ambayo atakayeitaka naamini anaweza kuipata kwao SG:

  “Bwana Yesu Asifiwe ndugu,
  Napenda kukukaribisha kwenye blog ya injili, ikiwa una lolote ungependa kusema katika blog hii unakaribishwa http://www.strictlygospel.wordpress.com pia ikiwa ungependa kufundisha au kufundishwa lolote lihusulo Injili wakaribishwa pia. Uwe huru Strictly Gospel haina udini wala sio dhehebu fulani. Lengo letu ni kuwafanya watu hasa wanaoenda katika internet na kuangalia/ kujifunza yasiyofaa waache na kujifunza yale yaletayo uzima. Lengo letu ni kubadilisha KIZAZI hiki!

  Strictly Gospel ni zaidi ya BLOG! Utasikia mengi kuhusu sisi muda unavyozidi kusonga. Jumuika nasi tubarikiwe pamoja!

  Nakutakia Baraka za Mungu na akutunze.

  Mary Damian
  http://www.strictlygospel.wordpress.com
  Monday, October 6, 2008. 9:20 AM”

  Pia subira ni jambo la msingi sana katika kujifunza, haswa pale inapozuka changamoto, maana changamoto huleta mtikisiko. Kuna wana SG walionilalamikia kuwa sisomi michango ya wachangiaji wengine, hilo pia si kweli. Majibu yangu yote yalitokana na kile kilichoandikwa. Nadhani jazba zilitawala sana kwa upande wao ndio maana wamekuwa ni wenye kulalamika, kulaani na kushikilia mambo ambayo si ya kweli licha ya kuyakanusha. Kwa mfano nimekanusha zaidi ya mara moja kuwa mimi sihusiki na imani ya ‘JESUS ONLY’ au “JINA LA YESU TU”, lakini bado naona wanaendelea kunihusisha na dhehebu hilo, aidha kwa kuongozwa vibaya au kwa makusudi ya kuwafikisha watu katika ufahamu wanaoutaka wao. Sehemu nyingine katika michango yangu, niliongelea kuhusu tafsiri katika Biblia ya Kiswahili kuwa kuna sehemu hazikutafsiriwa vizuri nikitegemea kuwa itatufaidia sote; lakini jambo hilo ambalo si la ki imani likageuzwa kuwa hivyo nk! Kuwaambia watu ukweli unaoufahamu ni jambo jema hata kama utakuwa umekosea basi uwe radhi kusahihishwa na pia kuwaomba radhi wengine. Nadhani katika hili, naungana na mchangiaji aliyesema ameona ukomavu kwa ndugu John Paul, hilo ni kweli!!

  Nafahamu kukwazika kunakoambatana na jambo lililo kinyume na Imani yeyote ile linapojitokeza. Lakini kukwazika, nadhani kunaweza kutafsirika kama udhaifu kwetu kibinafsi katika kile tunachokiamini. Hebu niwapeni mfano mdogo unaouhusika na jambo la jinsi hiyo. Siku moja jioni, nikiwa nimeongozana na rafiki yangu, ambaye ni muislam, tulipita karibu ya msikiti wa Mtambani, Kinondoni. Hapo kulikuwa na muhadhara uliokuwa ukiendelea, mtoa mada alikuwa akizungumzia jinsi Biblia ilivyogoshiwa na hivyo haipaswi kuaminiwa kabisa! Lakini nyuma alitangulia kutangaza kuwa wao Waislamu, wamepewa vitabu vinne vya kuwaongoza; Quran, Injili, Torati na Zaburi. Rafiki yangu, katika mzaha, akawa ananichalenji katika hayo. Ukimya wangu ukamfurahisha. Ndipo nikamuuliza, hao wanamzungumzia Mungu yupi? Akanishangaa, lakini nikaendelea, je, ni Mungu huyu aliyeziumba mbingu na nchi ambavyo kwa kuvisoma mwenendo wake wanasayansi wanaweza kutabiri kupatwa kwa jua labda miaka miwili kabla ya kutokea na ikawa hivyo? Akasema NDIYE MUNGU huyo!! Nikamuuliza, umemsikia na kumuelewa huyo mhadhiri kuhusu vitabu vinne mlivyopewa mvifuate? Akasema amemsikia na ANAFAHAMU HIVYO! Basi nikamwambia, nitamlipa shs. Laki moja ya usumbufu, aniletee vitabu hivyo. Akalikubali hilo si katika mzaha tena, bali akiamini atavipata!!! Baada ya mwezi mmoja nilimuuliza ile laki niitumie? Akakiri kuwa havipo na hajawahi kuliwazia hilo hivyo. Ndipo nikamwambia, iwapo huyo Mungu ameshindwa kuvitunza vitabu alivyowaambia viwaongoze, utamwaminije kumpa roho yako??? Aliniambia hilo ni tatizo, lakini hawezi kuondoka katika Uislamu! Nikamuuliza vipi kuhusu wale wahadhiri na maelfu wanaowashabikia wakiyaamini mambo hayo? Akaniambia haifai hata kuwashtua!!!

  Basi ndugu zangu ni vizuri kuzielewa tofauti zetu. Maana km, kanisa Katoliki kwa ukubwa wake duniani, limesambaa karibu kila kona ya dunia, lakini linaongozwa kwa ROHO MMOJA NA FUNDISHO MOJA. Sasa twapaswa tujiulize katika ujumla wetu kulikoni katika tofauti zetu kimafundisho, je, ni ROHO MMOJA anayetuongoza kutofautiana??

  Nawaombeeni nyote Rehema ya Mungu iwafunike hata kutuleta kuwa kundi moja chini ya mchungaji (fundisho) mmoja!

 20. John Paul pekee ndiyo msema kweli katika blog hii. Asipotoa maoni basi mimi huwa nachukia sana.

 21. Wana Strictly Gospel,

  Kwa vile sitakuwepo kwenye Blog kwa muda labda niweke yangu, Kwanza wenye Maono Strictly Gospel wao ndio wa mwisho wenye kuamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe…hata mimi nimewahi kusimamishwa kuchangia……maoni yangu yamewekwa kapuni….Lakini sikuona vyema kulalamika….na nimekuwa na mahusiano mema na wenye maono ya Blog hii….kwani naamini mawazo yangu kama mwanadamu yanaweza kuwa biased……na uelewa wangu wa KWELI HII YA INJILI unaweza kuwa na mipaka……! Hivyo si lazima mawazo yangu yakubalike na yaeleweke……ila kila niandikapo najitahidi mno kufanya kile nachokiandika kifikishe kile nachoakiamini……

  Wengine wamenilaumu kuwaita wengine ni cults……..ni kweli inawezekana nimefanya hivyo……lakini kwa kutumia Maandiko……historia ya kile wanachokifundisha……..na wala sitanyamaza….kusema kutokana na ufahamu wangu wa Maandiko kwamba Lwembe anafundisha kinyume cha Biblia….Imani ya Jesus only si ngeni kabisa Tanzania….si ngeni katika ulimwengu wa Cults…zilizozaliwa katika Kipindi cha uamsho wa Pentekoste miaka ya 1906……wafuasi wa “nabii Branham” nimeanza kuwafahamu toka miaka ya 1980….na wamewatoa wengi katika imani hai ya Kristo…..Lwembe na akina Mabinza sio wa Kwanza………!

  Wengine wamenilaumu kuhusu mtazamo wangu kuhusu Nabii Mwingira…../naomba wasome tena posts zangu …….nilichokifanya na nachoendelea kufanya nikuonya Waamini wanapoanza kujenga tegemeo la “kumwabudu” nabii Mwingira…nilionya kuwa hawamsaidii Nabii wala Ministry ya Efatha……nilionya kabla hajaingia kwenye matatizo anayopitia sasa…….! Mimi si nabii….lakini kwa ufahamu wa kawaida tu na macho ya mwilini ungeweza kuona kama sifa hizo wanazomwagia Mwingira zikamwingia tu…..basi tutegemee lolote…..Nabii anahitaji wasaidizi wa kumuonya na wala si kumuombea tu…..yeye ni binadamu na wala si malaika….! Amevaa mwili wa damu na nyama……! Nimeona Ministry kubwa kuzidi ya Mtume Mwingira zikianguka….! zenye utajiri….zenye wingi wa watu…….Labda kwa wenye nafasi wasome kitabu cha “I WAS WRONG” Jim Baker….Ministry hii ilikuwa kubwa Marekani….! Utajiri wake ulikuwa mkubwa nadhani zaidi ya serikali ya Tanzania……Lakini iko wapi leo…..?

  Kuhusu TB Joshua….nilichopost ni mtazamo wangu tu…..nimekaa WEST Africa……nafahamu huduma nyingi za Nigeria……kwa hiyo nilichokiandika kuhusu Nabii huyo ni mtazamo wangu…….! Si lazima wote waamini kama navoamini mimi……!Na siwalaumu kabisa wale ambao kwa ufahamu wao Nabii huyu ni kutoka kwa Bwana……!

  Kwa hiyo wapendwa naamini kabisa kila mtu anafunuliwa Neema hii ya Wokovu kwa Kujenga….lengo langu kila napokaa kwenye Keyboard ni kujenga……Nakubaliana kabisa inawezekana kabisa kuna wadhaifu wa Imani…..wenye nguvu….(Rom 13:1 na Rom 14:1) Lakini itabidi tuchukuliane katika kuinena Kweli……..!

 22. STRICTLY GOSPEL MKO KWENYE MTEGO MBAYA SANA. KUNA POST YANGU MMEITOA ILIYOKUWA INALALAMIKA KWA NINI MASWALI HAYAJIBIWI? MIMI NIMESHANGAA. MIJADALA YA KIKRISTO ISIPOKUWA NA MODERETOR INA HATARI YA KUTENGENEZA UZUSHI MWINGI SANA. UKIWAANGALIA LWEMBE, ORBI NA WENGINEO UTAGUNDUA WANASHAMBULIANA BADALA YA KUFUNDISHANA. WOTE WANAKIMBILIA KUMSHTAKI MWENZAKE KWAMBA NI CULT. OMBI LANGU NI KWAMBA MASWALI YANAYOULIZWA YAJIBIWE, UTATA UJE KUPITIA MAANDIKO NA FAFANUZI ZA KIMAANDIKO ZIPANULIWE MFANO LUGHA ILIYOTUMIKA, TAFSIRI YA WAKATI HUO, MLINGANISHO KATI YA LUGHA NA LUGHA, MAZINGIRA YA WAKATI NENO LINAANDIKWA,CHANGAMOTO ZILIZOTOKEA WAKATI WA KUTAFSIRI HATA KUTOA NAFASI KWA TAFSIRI POTOFU. MIMI NAAMINI MAMBO HAYO NDIYO YANAJENGA MJADALA. MUNGU AWABARIKI

 23. SG ,angalizo….
  Chunguza/Tujichunguzeni, Hasa nyie ambao mmeachiwa/kuchaguliwa kuongoza SG,Je? Bado mnaenenda ktk kusudi la Mungu na la Mbeba maono wa hii Blog Mary Damian.Angalia Lugha za hao watumishi mnaosema mnawajua kama zajenga maono au zabomoa hayo maono Kuandika kwenye gazeti/kufundisha kwenye mahema sio hoja ya msingi,haijalishi hata kama mko nao hema mmoja.SG ni mlango tu unaweza kutumiwa na Mungu au shetani kuleta habari za falme zao,Leo SG inapitisha habari za ufalme wa Mungu kesho inaweza ikapitisha habari za ufalme wa shetani na viongozi ni walewale,SG ni mlango tu,Tunatazama roho gani hipo nyuma ya SG,Bila shaka tunaiona.Kwa mafundisho ya aina hii.una haja ya kuwaambia wapendwa wahamie blog zingine kwani tayari umeshawapoteza ,Angalia kule kwenye forum zinapita siku hakuna mchango,Msipoangalia hiyo itakuja hata huku,wasomaji ni walewale
  Mnategemea mkiitisha mkesha watu waje kukesha!!!???
  Kumbe sisi ni Barua,Ndugu zetu wasio na wokovu wakitusoma hapa wavutie nasi amani iingie mioyoni mwao kisha wamkabidhi Bwana maisha yao,Lakini wakiona tunawazungumza au tunashindana kama farasi mwitu ambaye hamjui mjomba wala mama teke tu na hawezi kula wakati huohuo anataka kubweka lazima aache kula hili abweke,hawatarudi kufungua hii blog tena,imeandikwa pasipo maono watu upotea.
  Chachu kidogo uchachua donge zima.
  Wakati naandika hii Comment, Naomba Bwana awape ujasiri wa kuliweka hili bandiko kwenye Blog,.Najua yatakuwa mapenzi machungu kwenu lakini Yatupasa kuwa kama mmoja wa wale manabii wakubwa aliye ambiwa na Bwana unaona nini akajibu naona rungu,akaambiwa chukua nenda njiani mtu akipita mwambie akupige nalo kichwani,akaja mtu wa kwanza akakataa kumpiga,Yule nabii akamwambia sikia neno la Bwana hapo mbele utakutana na simba naye atakurarua na ikawa hivyo lile neno likatimia.WANA WA SG MWAONA NINI?.
  Bwana Aturehemu,
  Amen.

 24. Shalooom wapendwa
  kwanza nawashukuru wote kwa kuvumiliana ktk mijadala hii
  Mungu azidi kutupa uvumilivu na saburi kwani ktk hayo tunaweza kumsikiliza hadi mwisho mtu anawaza nini, anaamini nini na hivyo kuweza kumuonya na wengine wenye imani na mawazo kama yake kujifunza
  Napenda kumrudishia Mungu utukufu kwani kama Yesu alivyotuahidi atatupa msaidizi “ambaye atatufundisha yote atakayoyasikia kwake….” ni kweli anaendelea kutufundisha kila siku kupitia neno lake na watumishi mbalimbali kama hapa SG.
  Namrudishia Mungu utukufu kwa kumtumia Orbi na kina Haggai kutufunua macho nini wanachoamini wenzetu kina ndg Lwembe, binafsi nilishindwa hata kuchangia kitu maana hata mistari inayoelezea Mungu ktk utatu wake ni mingi mno kiasi nilishindwa kuelewa mtu anakuwaje anasoma Biblia hii ninayoitumia na asielewe isipokuwa kwa makusudi maalumu aidha kwa kulishwa sumu ya imani potofu.
  Nachukua nafasi hii kumuomba kaka Lwembe pamoja na kuchangia ajenge tabia ya kuisoma michango ya wenzie na kupitia Biblia wanapoitaja mistari kwa moyo wa kufundishika na sio kupinga tu labda Mungu ana makusudi yake ktk kukuleta hapa, ktk mjadala wa manabii wa Tanzania aliouanzisha ndugu Orbi niliona michango mingi ya hawa watu lakini haikuwa imejikita ktk neno la Mungu. Ni vizuri kuzikagua hizi roho hata mimi kama mimi ninafaidika sana hapa na kujikagua kama niko sahihi kupitia michango yenu hivyo tuzidi sana kumruhusu Roho mtakatifu atuongoze. Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s