Askofu Moses Kulola

Moses Kulola, niliyezaliwa 1928 katika familia ya watoto kumi, ambapo watano tuko hai hadi sasa, nilijiandikisha katika shule yangu ya kwanza mnamo mwaka 1939. Shule hiyo ilikuwa inaitwa Ligsha Sukuma, ikiwa ni shule ya Misheni. Baada ya kumaliza hapo Ligsha Sukuma Mission School nikajiunga katika Idara ya  Uchoraji wa Majengo mnamo mwaka 1949. Na mwaka 1950 nikabatizwa katika Kanisa la AIM Makongoro, mjini Mwanza..

Nimemuoa Elizabeth na Mungu alitujalia kupata watoto 10, ambapo kwa sasa saba (7) bado wako hai.  Nilianza kazi za Umisionari mnamo mwaka 1950, ingawa nilikuwa nimesikia wito huo mwaka ule wa 1949!

Mwaka 1959 niliajiriwa serikalini. Lakini pamoja na kuajiriwa huko mimi niliendelea na kuhubiri Injili katika Miji na Vijiji. Utumishi wangu kama mwajiriwa wa Serikali ulikwisha mwaka 1962 baada ya kuwa nimekabidhi nguvu, mwili na nafsi yangu katika kazi ya Mungu! Ilipofika mwaka 1964 niliamua kusoma na nikajiunga katika  Chuo cha Theolojia na kuhitimu katika kiwango cha Diploma mamo mwaka ule wa 1966.

Baada kupata Diploma hiyo sikuishia hapo bali niliendelea kusoma kwa Njia ya Posta na kupata Vyeti vingi sana kutoka Sehemu mbali mbali duniani.

Nilitumika miaka miwili kama mchungaji, 1961-1962, katika kanisa hilo la AIM na baada ya hapo nikawa muumini wa Kipentekoste. Halafu nikatumika katika kanisa la TACR kuanzia 1966 hadi 1991 ambapo nilijisikia kuanzisha Evangelistic Assemblie of God, maarufu kama EAGT. EAGT ni kanisa ambalo limefanikiwa kukua kwa kasi kubwa nchini hasaTanzania, Zambia naMalawi ambapo jumla yake ni kama makanisa 4,000 yakiwa ni makanisa makubwa na madogo, na mimi Moses Kulola nikiwa ndiye Askofu Mkuu na Msaidi wangu akiwa Askofu Mwaisabira.

Faustine Munishi(malebo) Moses Kulola,Emmanuel Mwasota.

Si kazi rahisi kuendesha makanisa elfu nne (4,000) na ndiyo maana ilibidi kugawanya katika maeneo 34 ya kiutendaji, kukiwa na Kanda Tano ili kurahisisha kazi hiyo ya Mungu. Kila eneo na Kanda kuna mwangalizi wake.

–Imetafsiriwa na Strictly Gospel kutoka Emmanuel Mabisa Blog–

Advertisements

26 thoughts on “Askofu Moses Kulola

 1. Wachangiaji mbona mnataka tu kujua kipindi cha matengano, vurugu nk. Waliyo kwaruzana yalisha pita na bila shaka wakamwomba Mungu msamaha, yakaisha .Sasa ninyi mnaotaka aanze kueleza chanzo,awataje waliosigana hapo mwanzo nao waanze kujitetea.Je, hamuoni ya kuwa huko ni kufufua tatizo naomba msing’ang’anie kufufua mgogoro uliokwisha kufa,kwa kisingizio cha kutaka historia kwani maisha mnayoishi kila siku hayawafundishj?. Amani iwe pamoja nanyi nyote.Amina.

 2. nashangaa kuona watu mna leta ushabiki na kwenye mambo ya KIMUNGU jaman injiri sio siasa, bali ni uweza wa MUNGU uletao wokovu.

 3. Ni vizuri ingewekwa wazi kwa nini alianzisha EAGT na jinsi alivyopigana. Haina maana ya kufanya kizazi hiki kiwachukie waliotaka upigwe hadi kufa NO ila ili kujenga maisha ya watu kiroho wajue jinsi mzee alivyopambana na bado katika yote alitangaza msamaha ili Jina la YESU liinuliwe na jina la kulola liandikwe mbinguni. Jamani Mungu akupe miaka zaidi mzee wetu, Tunajivunia kuwa na Kulola kwa hakika. Mungu atusaidie tupigane vita vya imani na kumtangaza Kristo kama mzee wetu alivotuonyesha mfano mzuri.

 4. hapo sijaelewa historia ya mosses kulola kwani hajazungumzia suala la yeye kutoka tanzania assemblies of God(tag) kwani yeye alikuwa minjilst mkubwa wakutegemewa pamoja na askofu lazaro wa tag,naomba majibu kwa wanaofahamu,be blcd by mighty God

 5. Nice History, Hata ukilala kazi ya Bwana umefanya nasi tumeiona na tunaendelea kuiona.

 6. ningependa kupokea dvd au cd za mafundisho na mahubiri ya mzee bishop Moses KULOLA

 7. nice song dear SARAH K.uzidi kubarilikiwa na MUNGU wetu . uzidi kuomba MUNGU ili aendelee kukubariki ili tupate nyimbo za mafuta kama hizi.Asante sister tena tunabarikiwa kupitiya wewe. tunakuombea pia

 8. NAMUOMBA MUNGU AINUWE WA2 WATAKAO HUBR KWEL S KWA HLA ILA WA2 WAIJUE KWEL NA WAWE HURU KWEL WASINDELEE KUWA WATUMWA WA ZAMBI MUNGU AWABARK WA2MISH WA MUNGU TUNAOMBA ZAID USHUHUDA WA HUYO MZEE WE2 KULOLA IL WA2 WAJFUNZE ZAID, CHANGAMOTO ALZO KUTANA NAZO VKUND ALVYO SAL NA JNS MUNGU ALVYO M2MIA KWA SEHEMU MBALIMBALI NA SABABU YA MGAWANYKO HUO ME NAZAN YEYE ANAJUA ZAID MAANA ALKUWEPO IL TUELEWE NA MIGANYKO INAYO INDELEA IKIWEZEKANA IKOMESHWE KTK MAKANISA MBALMBAL

 9. Kanisa la TAG liliingia kwenye mgogoro mwaka 1982 mpaka 1986 mwishoni ndipo walipogawana waumini kati ya Moses Kulola na Emanuel Lazaro wa TAG wakati huo ,chanzo sijui ila nakumbuka mimi nilikuwa mwana sunday school wakati mgawanyiko huo unatokea .Askofu mkuu alikuwa Moses Kulola-(MWANZA) na makamu alikuwa Moses Mwamwenda -(MBEYA-Songwe Viwandani) kwa mara ya kwanza nilimuona Moses Kulola 1983 Mwanjelwa mbeya nikiwa na umri wa miaka 9.Ninakumbukumbuku kidogo hata baadhi ya viongozi wa majimbo nawakumbuka,-Kameta (mbeya mjini) Mwaisabila (mwanjelwa) Kadukungonde Huyu bila shaka alikuwa Katibu,alikuja na pikipiki kanisani Songwe ili kusuhuhisha mgogoro huu na liondoka bila kuelewana na makamu wa askofu Moses Mwamwenda. Nimesema hivyo ilikusisistiza kuwa taarifa zilizopo zinahitaji kina zaidi ,TAG ilikuwepo kabla ya EAGT na Moses kulola Alikuwa na askofu wa mwanzo kabisa wa TAG-Muulizeni yeye mwenyewe kabla hamjaweka habari zake kwenye blog .Hbari hizi hazitoshi kumuulezea mtu kama Moses Kulola kijujuujuu!

 10. Mimi kama mmoja wa wanae kiroho na kihuduma,Niliposoma historia hiyo hapo juu,niliona kama ni fupi mno,Mimi nilianza kumsikia Mtumishi wa Mungu miaka hiyo ya 80 na nikamuona kwa macho 1986 akihubili Kitete,mimi nikiwa kwenye kama ya maombi ya mkutano wake, Kanisa likiwa BADO linaitwa TAG,na ndio mwaka alioniombea nakunitabilia kuhusu ukubwa na uzito wa huduma yangu,tukiwa naye wawili kwa mzee Kapela.Nilipo ona vile Mungu alivyokuwa akimtumia,nilipata picha mala moja ya Moses wa Biblia kwani niliyo yaona ilikuwa ni mala ya kwanza kuona vile Mungu anavyo weza kuponya na kuokoa kwa nguvu za pekee.Nilifuatilia sana historia ya huyu mzee kwa undani tangu hapo,nikapata kuona wazi vile Mungu navyoweza kumchagua mtu na kumtumia kwa kaisi cha kutetemesha milima.Kama walivyosema wenzangu hapo juu,nasisitiza kwamba kujitokeze watu wangwana sana wenye busara na walio jawa na Roho wa Mungu,ilikuandika historia nzima ya mzee huyu,na pia kupata tasfiri nzuri na yakiroho,ya yale yaliyotokea mika hiyo ya 1986,,punde Kanisa lilipo ingia kwenye mgogolo hadi kugawanyika.TAG na EAGT.Na ikumbukwe kuwa kipindi hicho magawanyiko yalitokea siyo tu TAG,lakini hata Kanisa la Pentecoste Tanzania ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora,lilivyogawanyika miaka hiyo hiyo,na kutoea Makanisa mengi hum,Haya yote lazima yatafsiriwe na watu wa kiroho,bila kuona tu negatives ndani yake.Ninatumai tutawekea maanani jambo hii mhimu na kwa faida ya Kanisa na vizazi vijavyo…

 11. Namshukuru Mungu kwa ajili ya mtumishi M.Kulola. Kama ilivyo wazi Historia ya Mitume wa Yesu: Magumu waliyopitia, walivyovumilia na kudumu katika imani n.k . Kupitia historia hiyo Wakristu wa leo tunapata mwogozo wa imani zetu. Hivyo basi nashauri Mtumishi Moses Kulola aiandikie jumuiya ya Wakristu waliopo na wajao kwa mapana na marefu juu ya huduma yake na alivyowezeshwa na Mungu kuipanua hadi kuwepo kwa EAGT. Nasema hivyo kwa kutaadharisha upotoshaji unaoweza kujitokeza hapo baadae kutoka kwa watu wasiokuwa na hofu ya Mungu juu ya huduma ya Askofu Moses Kulola.

 12. Cha msingi kama wachangiaji wengine wenye Upendo wa Mungu walivyosema, kuna haja sana wasifu wa huyu mzee wetu urekebishwe na mambo yote yenye utata yawekwe wazi. Kwa mfano mimi sielewi nini kirefu cha AIM au TACR kweli hapa naachwa gizani. Nilitegemea neno Tanzania Assembies of God liwepo lakini sijaona. Mimi nliye mtoto wa kiroho wa baba yangu Mzee Kulola nikamuulize nani anipe historia sahihi isiyo na utata ya kanisa langu tangu lilivyoanza hapa Tanzania hadi sasa? Nawapenda wote TAG na EAGT

 13. Kusema kweli Mzee Kulola ni mtumishi aliyetumiwa na Mungu kuleta mapinduzi ya Kiroho maishani mwangu.Siwezi kusahau Easter Crusade ya tarehe 13.04.1991 pale Mnazi mmoja, Dar wakati nikiwa mwnafunzi DIT.
  ninachotaka kusema hapa wapendwa ni kwamba kuna haja kumwomba sana Mungu atujalie hekima tufahamu adui yetu ni shetani aliyelipasua kanisa hata likagawanyika. Hali hii imezaa chuki, kudharauliana, kuwasema vibaya watumishi wa Mungu na pia watumishi kutokuwa wawazi kwa kutetea upande wao. Tuwe waangalifu

 14. napenda mafundisho yake. elimu yake ya dunia kuhusu vyeti na phd kwangu si muhimu sana bali jinsi anavyotafsiri maneno ya Mungu toka Biblia takatifu

 15. Naamini kuwa wote hamjabo kwa jina la Bwana Yesu kristo. Nimefuatilia michango mingi iliyotolewa kuhusu Mzee Moses kulola; Kimsingi sijaelewa ni nini hasa kinachotakiwa wapendwa wakijue juu ya Mzee wetu huyu Kulola! Maana nijuavyo mimi, wasifu wa mtu ni historia fupi ya maisha ya mhusika, ambapo hueleza tu kwa kifupi lini na wapi alizaliwa na mpaka alipofikia. Na kama labda watu wanataka kujua historia ya Mtu Fulani na Huduma yake hilo litakuwa nijambo lingine. Histori Ni kusanyiko la matukio mbalimbali Na huandikwa Kwa madhumuni maalumu, huhitaji ushahidi wa kimaelezo, kimaandishi na hata wa kimazingira, Historia huandikwa kwa kutumia “questioner”. Historia handikwa na watu au mhusika mwenyewe na shahidi hubakia kuwa mhusika kama yupo hai. Sasa labda tujue kwanza tunatakaje, Wasifu wa Mtu kama mtu mwenyewe au Historia ya EAGT ambayo mwanzilishi wake ni Mzee Moses Kulola? Mbarikiwe wote.

 16. Nashukuru kwa michango, nami nakubaliana katika kuweka kumbukumbu sahihi za Mtumishi wa Mungu Askofu Moses Kulola, katika ushuhuda wake hapo juu ameeleza kwa ufupi ni vizuri angeweka kitabu ambacho watu watakirejea (reference) kwa sababu kauli kama nilipata “vyeti vingi sana” watu wangependa kujua nyanja ambazo amepita kwa sababu hivi sasa ametunukiwa PhD.

  Kanisa la EAGT limetokana na kupanuka kazi ya Mungu ndani ya Kanisa la TAG ni vizuri akaeleza maono yake yaliyompelekea kuanzisha kazi hii ya EAGT katika aina ya machafuko makubwa yaliyotokea wakati wa mpito wake, ni Mungu ndiye aliruhusu kwa kusudi lake? haya ni masuala ya msingi aweze kutupatia ushuhuda wake. Amen

 17. Mimi ninachokishangaa siku zote ktk haya madhehebu ni jinsi yanavyoanzishwa kwa njia za hila na akili za kibinadamu hafu baadae yanakuwa na UPAKO ULIOJAA NGUVU ZA MUNGU(ila sina uhakika sana na hizi nguvu maana ni vigumu kuzipima kwa akili na upeo wetu tuliopewa wa kuchambua moja kwa moja lip ni sahihi na lip sio) sijui hapa pakoje wakati Mungu HAKUHUSISHWA wakati wa mafarakano na wakati wa kuanzisha kikundi(kanisa ) jipya.

 18. Ndg Jerome na wengine
  Shalom
  kuwa na huduma tofauti haimaniishi kanisa tofauti, kanisa liliisha wekwa na Yesu kwa msingi wake wa mitume na msingi mkuu au jiwe la pembeni au nguzo inayoshikilia ni Yesu mwenyewe, kuwa na tofauti za kufanya watu waanzishe huduma au majina mengine sio kuanzisha kanisa.
  Katika matendo ya mitume kulitokea kutokuelewana kati ya Paulo na Barnaba
  Matendo ya mitume 15: 39 -40 Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kipro. Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana….ndugu kutofautiana sio ajabu ila tu tunapaswa kusameheana na kusonga mbele.
  siwezi kuweka mistari hiyo yote kwa sasa lakini mwanzo wa kanisa pia ktk kitabu cha matendo tunaona kulikuwa na makusanyiko ktk nyumba tofauti tofauti wakiabudu kwa pamoja mradi tu walisimama ktk misingi ya mwanzilishi Yesu Kristo.
  Enzi za kuwa na hekalu moja tu ambalo wote tunapaswa kukusanyika kuabudu zilipita Yesu aliposema hatutaabudu huku wala kule, tutamwabudu Baba ktk Roho na kweli hiyo ndio ibada halisi, hayo majengo, watumishi, kanuni na mengineyo hayatutengi mradi tunaamini ktk Roho na kweli.
  Binafsi nikiwa safarini ninaabudu ktk nyumba yoyote mradi ndio kanisa lililopo hapo na linasimama ktk misingi ya Biblia, wakati sisi tunagombea fito za nyumba yetu hii (Kanisa) kuna watu hawaruhusiwi au hawapelekewi hata hiyo injili tu ili wampokee Yesu, nimekaa Pemba miezi miwili nikiabudu ktk chumba changu pekee maana sikupata kumjua Mkristo yoyote ktk wilaya niliyokuwa. Ni Tanzania hihi wapendwa hebu tuihubiri injili na tusiwapigie kelele wanaoanzisha huduma kuwafikia wengine. Tusonge mbele.

 19. Kutokana na Umaarufu wa Kiutumishi alioufanya Mwinjilisti Moses Kulola, hiki kilichoandikwa hapa ni maelezo machache mno kuwa ndiyo HISTORIA YOTE ya mtumishi huyo wa Mungu! Kwa hiyo mi naamini yako mengi saana ya huduma aliyopitia na matatizo na changamoto za kiutumishi ambayo yanaweza patikana SEHEMU nyingine na siyo katika maneno haya MACHACHE! Suala la MUHIMU ninaloshauri ni kuwa INABIDI WATUMISHI WA MUNGU WA HAPA TANZANIA WAANZE UTARATIBU WA KUANDIKA VITABU VYA MAPITO YAO WANAYOPITIA!

 20. hii ni hatari jamani mtu kujisikia kuanzisha dhehebu…jamani jamani tuachane na mazoea katika kumtumikia MUNGU,,,,,,MUNGU aseme nawe kama ni wewe kuanzisha kitu chake… Kulola nilitegemea labda EAGT imetokana na Mungu mwenyewe kumbe ni wewe tu ulijisikia kuianzisha……..,,,,,,,,hii ni hatari wapendwa tuweni macho

 21. Godfrey,

  Ni vigumu mno kuipotosha historia……na si kwamba hakuna walioandika…labda kwa lugha ya Kiswahili….lakini unaweza kusoma nini kilitokea katika Matengano ndani ya TAG na kuzaa EAGT……unaweza kusoma vitabu ….na hata pia kwenye Journal ya Tanzania Law report yenye maamuzi toka kwa Judge Chipeta ambayo kwa hakika yalisababisha EAGT kuzaliwa…..soma baadhi ya vitabu…….

  1. Church and State in Tanzania: aspect of changing relationship 1961-1994 by Frieer Ludwig

  2. African Pentecostalism: An Introduction by Ogbu Okulu

  3. Questioning the Secular State: The worldwide of politics and religion by David Westerlund.

  Hivyo kama Mzee Kulola kama yeye hataandika chochote kinachohusu kipindi kilichosababisha kuzaliwa EAGT, wengine waliokuwepo kipindi hicho walioona na kushuhudia wataandika, Kwani Mzee Kulola hakuwa peke yake, na kwa yeye kutoandika itamfanya Mzee Kulola kuonekana kuwa anaficha kitu, Hivyo ni vyema akaandika historia yake pasipo kuiacha sehemu hii muhimu, ambayo kwa mtazamo wangu ni muhimu sana kama ikawekwa wazi kwa ajili ya kuelewa na kujifunza. Historia inafundisha kwamba…usipojifunza kutoka kwenye Historia kuna uwezekano wa kurudia makosa…..!

 22. Yoote haya ya Kolola hakuna gumu alilopitia ?kama unandika kana kwamba hayupo kimsingi hitusaiidiikutudanganya mfuate muulizi magumu na mabaya anayooyaona ktk huduma ili nasi tujifunze na ikiwezekana tumuulize maswali
  Na hili kanisa lina mwanzo Duniani na sio Tanzania aseme kweli iliimueke yeye na sisi huru

 23. Nafikiri ni vyema apatikeni mtu wa kufanya article ya maisha ya huyu mzee akiwa bado hai maana ni ukweli wazi kwamba baada ya kuondoka kwake, wapotoshaji nao watataka kujipatia fedha na umaarufu kutoka kwenye hili na ni vizuri hali hii ikadhibitiwa mapema. Huyu ni mtumishi mkubwa sana wa Mungu na ambaye ametumiwa kufanya reformation kubwa kwenye jamii yake, historia yake inastahili kutunzwa vyema.

 24. Tunashukuru mno waliotuletea tafsri hii ya Wasifu ya Mzee Mosses Kulola…..Lakini mbona ameiandika historia hiyo kwa kuacha kipindi cha toka 1966-1991 yaani alipoanzisha EAGT…?EAGT haikuanzishwa toka hewani…….. Hofu yangu ni kwamba asipoandika yeye mwenyewe kuhusu historia yake na yalitokea hadi kuanzishwa EAGT, wengine wataandika na wanaweza kuandika tofauti na Ukweli ambao Mzee Kulola angelipenda waelewe…..ana nafasi nzuri mno akiwa hai kuweka records straight from his own perspective …..na kutoka kwake na waliotutangulia tunaweza kujifunza, ama kwa makosa yaliyofanyika au kwa mazuri waliyotenda……Kama tunavyojifunza kwa mazuri na makosa waloyofanya watu wa Mungu wengine kwenye wasifu wao….maandiko Matakatifu……. kama akina Musa….Daudi……Petro…..Naamini akiweka wazi wasifu wake hasa katika kipindi kigumu cha huduma yake itasaidia wengi……Hasa katika kipindi hilki ambacho wengi tuko kwenye maombi tukiuomba tena Mungu atuinuliwe tena Mtu au watu watakaoleta uamsho Tanzania……..

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s