Ni lazima kuzungumza kwa Lugha Mpya?

Bwana Yesu asifiwe wapendwa? jamani naomba mnisaidie kuna swali linanipa shida: Hivi kuna ukweli kwamba mtu aliyempokea Roho Mtakatifu ni LAZIMA AZUNGUMZE KWA LUGHA MPYA?

Je, akifanya ishara nyingine za Roho Mtakatifu na kuwa na matunda ya vipawa vya Roho Mtakatifu,LAKINI KAMA HANENI KWA LUGHA,huyo hana Roho Mtakatifu?

MERERE,Cuthbert

Advertisements

172 thoughts on “Ni lazima kuzungumza kwa Lugha Mpya?

 1. Bravo, Lwembe!

  Huo ufafanuzi mdogo wa kihistoria unamaana kubwa katika kuuleta ukweli wa uhalisia wa suala la kunena kwa lugha katika madhehebu mbalimbali leo.

  Nilishangazwa sana na msabato Siyi kusema ata nao wananena kwa lugha alhali siku zote wamekuwa wakipinga kwa kusema suala hilo liliishia kanisa la kwanza.

  Na hiinayo nimeipenda zaidi ” wakiwa wamejichepusha ktk mafunuo ya vitabu vya kinabii kama Daniel nk, wakijaribu kuvifunua nje ya wakati na hivyo kuishia kujichanganya na sasa wakijiingiza zaidi ktk Uongo ili kukabiliana na Changamoto za Injili kadiri inavyopanda ktk Hatua zake, tunapokusogelea Kuja kwa Bwana”

  Kwa sababu tangu niko mdogo wasabato walikuwa wanaongea sana habari za mnyama na suala zima la mpinga kristo wakisema kuwa mpinga kristo ni papa, na walikuwa wana vitabu fulani vimechorwa picha za ajabu ajabu za hao wanayama waliosemwa katika vitabu vya kinabii nya Daniel na Ufunuo.

  Siku hizi hawasisitizi sana mambo hayo, inaonekana wamegundua kuwa mpinga kristo siyo papa tena. Sasa hivi wamejikita zaidi kwenye lishe za asili.

  Mungu awasaidie waikubali kazi ya Roho mtakatifu, ili wapone!

  Bless!

 2. Siyi,

  Kanisa la Kristo hilo lililoanza siku ya Pentekoste huko Yerusalemu, likiwa na madhihirisho ya Nguvu za Mungu katika maana ya Vipawa na mwenendo, likimdhihirisha Kristo, ilifikia wakati LIKAFA, pamoja na Madhihirisho yake!!!

  Nikakuambia kuwa Katoliki ndio waliolifisha Kanisa hilo na wao kuwa ndio “Kanisa”!! Haya makanisa yooote unayoyaona leo hii pamoja na ninyi Wasabato, katika maana ya madhehebu, chimbuko lao ni Katoliki. Nikakuambia kuwa Ufufuo wa lile Kanisa la Kristo, katika maana ya hao walioitwa watoke katikati yao, umeanza na Martin Luther kwa Neno la KUHESABIWA HAKI KWA IMANI. Hii ndio sehemu ya Neno waliyopewa hao waliouitikia wito wa Luther, yaani hao Wakatoliki waliotoka.

  Kwahiyo kwa macho ya kawaida, katika siku hizo kulikuwa na wakristo aina mbili; moja ikiendelea na jitihada za mwili, hao waliokataa wito wa Luther, na kundi jingine likiwa limeondokana na jitihada hizo, hao walioHesabiwa Haki kwa Imani. Basi unapaswa uelewe kuwa ukiisha likataa Neno la Mungu uliloletewa katika wakati wako, hakuna namna unayoweza kulipokea tena huko mbele, yaani Kiroho UNAFIA HAPO! Wakatoliki walifia hapo katika siku za hilo Neno, hawawezi kupokea chochote tena, wanaendelea na Mafundisho yao yakiwashusha ktk ngazi za Kuzimu!

  Kwahiyo Hao waliolipokea Neno la Luther ndio waliokuwa Kanisa la Kristo kwa kulitii Neno hilo tu. Mambo mengine Mungu hakuyatazama, kwa mfano pombe na sigara, waliendelea nazo bila hukumu yoyote ile mioyoni mwao. Baada ya umbali fulani Mungu aliwapandisha kiwango kwa kuwaletea Neno la UTAKASO. Sasa si kwamba ni Neno jipya, la hasha yote yamo humo humo ktk Biblia yako, bali huwa yamefungwa mpaka aje Roho ayafungue! Kwahiyo Roho alilifungua kwanza Neno lake la Kuhesabiwa Haki, dunia nzima ikaingia ktk kipindi hicho ktk umbali huo, huwezi ukazidi hapo kwani hicho ndicho kiwango cha Roho kwa Kanisa. baada ya hapo ndipo juu ya Kuhesabiwa Haki, Kanisa likaingizwa katika Utakaso. Walutheri waliolipokea Neno hilo wakaingizwa ktk Hatua hiyo mpya, waliolikataa Neno hilo wakafia hapo, mpaka kesho wanaendelea na sigara zao na pombe kama wanavyoendelea Wakatoliki na ibada zao za sanamu.

  Wasabato wamezaliwa ktk kipindi hiki kutoka ktk wa Methodist, wakiwa wamejichepusha ktk mafunuo ya vitabu vya kinabii kama Daniel nk, wakijaribu kuvifunua nje ya wakati na hivyo kuishia kujichanganya na sasa wakijiingiza zaidi ktk Uongo ili kukabiliana na Changamoto za Injili kadiri inavyopanda ktk Hatua zake, tunapokusogelea Kuja kwa Bwana. Katika Hatua hizi mbili hakukuwepo Kunena kwa Lugha kwa dhehebu lolote lile wala Kanisa kama kusanyiko!!! Sio jambo la Kunena tu bali Hata uponyaji wa kiungu HAUKUWEPO ukiacha wale individuals waliokitembea na Mungu, lakini si makusanyiko kama leo ilivyo!

  Hatua ya Tatu ya Kanisa la Kristo ni hapo alipowachukua hao aliowatakasa, hao waliojisitiri katika Neno, hawakufuata mafunuo wasiyopangiwa, hao ndio akawashushia PENTEKOSTE nyingine!!!! Akawakamilisha kwa Ubatizo wa RM na kuvirejesha vipawa vyake Kanisani, wakanena kwa Lugha!!! Makundi mengine yaliyozaliwa katika Hatua hii ya Utakaso na kujichepusha njia yakafia hapo katika kiwango cha Utakaso. Ni watu wazuri sana, wakristo wasiojichafua kwa mambo ya mwili, lakini kiroho wamefia hapo mpaka siku ya Ufufuo wa Hukumu maana wote hawa walioiishi Hatua ya Mbele ya Neno lililowazaa, kisha hawakulipokea Neno la kuwapeleka Mbele ambalo humo ndani yake ndimo mna Nguvu ya Ufufuo, hao wanabaki kuwa wafu licha ya kwamba wanatembea!

  Ndio kusema Makatoliki aliyebaki katika Ukatoliki, licha ya kulisikia Neno la Kuhesabiwa Haki kwa Imani, huyo ni mfu, maana ndani yake HANA Neno la kumfufua anyakuliwe! Naye Mlutheri aliyelipokea Neno la Kuhesabiwa Haki, akaliishi hilo, huyo ATAFUFULIWA kwa Neno hilo, ni Bibi Arusi wa Kristo aliyeposwa kwa Neno hilo! Lakini Mlutheri aliyelisikia Neno la Utakaso kisha akalikataa, akajibakisha ktk Neno la Kuhesabiwa Haki ambalo ule Uzima uliokuwamo ndani ya Neno hilo, umetoka na kujikusanya katika Neno la Utakaso, huyo naye atakuwa AMEFIA hapo, akiwa hana ndani yake Nguvu ya kumfufua! Pia aliyelipokea Neno la Utakaso atafufuliwa kwa Neno hilo maana ndani yake ndimo ilimo ile Nguvu ya UFUFUO.

  Lakini huyo aliyetakaswa kisha akalikataa Neno la Ubatizo wa RM, hilo lenye kuambatana na vipawa vya Kunena kwa Lugha, Uponyaji nk, huyu pia anafia hapo, ndio maana nikasema Hakuna Mkatoliki wala Mlutheri wala Mmethodist pamoja na makundi yote yaliyozaliwa katika vipindi hivyo, pamoja na Wasabato, ambayo HAYAKUPOKEA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU yanaweza kuvidhihirisha Vipawa vya RM katika UKAMILIFU wake wakiwa wangali wanaishi SEHEMU tu ya lile Neno, ni UONGO tu kama kawaida ya WAONGO ilivyo!!!! Makundi YOOOOTE yaliyo Nje ya Upentekoste, ukiacha huu mfumuko wa manabii wasioeleweka, wote wanakiri kwamba vipawa vilikwisha na mitume, lakini kutokana na pressure ya Wapentekoste na miujiza yao, makundi hayo yameingia nyufa, ndio hao Karismatiki na fellowships ktk makanisa mengine, pamoja na mipasuko kama ya Sabato Masalia nk, ndipo ukiwaangalia juu juu utadhani kwamba madhehebu yao mama yanaamini ktk vipawa, lakini si kweli, ni Unafiki tu na Uongo kama huo wa “Real New Testament Christianity” ambao watu hupenda kuuamini kwa wepesi wa kulinda masilahi yao, Hakujawahi kuwa na KUNENA kabla ya 1906 tangia Katoliki walipo takeover!!

  Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kujihakiki kama Nguvu ya Ufufuo tunayo ndani yetu, sio mafundisho ya kidhehebu, hapana Neno Kamili la Mungu mabalo ndilo Kristo, ambaye ndiye UFUFUO!!!

  Kunena kunakoendelea leo hii kunaweza kukawa na makosa, lakini hilo haliuondoi Ukweli wa Kazi aliyoifanya Mungu kwa Kanisa lake!

  Tafitini KWELI ili iwaweke HURU!!!

 3. MAJIBU KITOKA KWA MODERATORS;

  Lengo la SG ni kujifunza lkn inapoonekana kuna ubishi na maneno yenye lengo la kuubomoa mwili wa Kristo, hatutaruhusu maoni! na hata sasa tumechelewa…

  SI katika mada hii pekee, ni mada nyingi ambazo hazina hitimisho na kuacha maswali mengi zaidi ya majibu.

  Tunataka watu wamjue Mungu, wajifunze, waache njia zao mbaya na mafundisho manyonge warejee kwa Kristo. Tutasimamia lengo letu hili kuu.

  Mtu yeyote anayepingana na Roho Mtakatifu au kazi zake hatuwezi kumvumilia!!!

  Samahani kwa wote ambao hatujaruhusu/hatutaruhusu maoni yao.

 4. Sungura,
  shalom rafiki. Kutoona majibu yangu hadi sasa, siyo kwamba, sijajibu. Yakiruhusiwa utayaona tu. Na sina mawasiliano nawe zaidi ya hapa, ningekukwambia baadhi ya mambo ambayo ni vigumu sana kuyasema hapa live!!
  Anyway, Mungu atusaidie kaka. Tuendelee kusubri moderators

 5. Siyi,

  Kuna kitu lakini nilikkuliza hapo mwishoni kabisa mwa comment yangu.

  ”Siyi kama kunena kwa lugha kwenu si huku nilikosema hapa, please niambie kuwa nimekosea, na unifafanulie jinsi wewe unavyonenga kwa lugha”

  Kwa hiyo naomba ukimalize hicho kipolo kwanza maana ni cha muhimu sana kwangu katika kuendelea n ahiisafari yetu.

  Halafu katika kutafsiri biblia ni vizuri kutumia mistari ambayo iko kwenye muktadha wa kitu unachokiongelea.

  Maswali yako:

  Swali lako la kwanza liko obvious, kwamba karama za Roho na tunda la roho ni vitu viwili tofauti.

  Kunena kwa lugha ni karama ya Roho.

  Lakini kabla sijaenda mbali, nataka nikuulize swali dogo hapo, hivi; kwa nini umeandika roho ya herufi kubwa kwenye matunda ya roho? I hope umeelewa swali langu, yaani kwa nini matunda ya/tunda la Roho badala ya matunda ya/ tunda la roho?

  Swali lako la pili nalo kuna uzembe umefanya, suala la lugha kueleweka niliwahi kukwambia huko nyuma.

  Anyway acha nikujibu:

  Kwanza: Mungu lazima anaelewa hiyo lugha

  Pili: Wewe si lazima uelewe hiyo lugha, lakini inaweza kutokea ukaelewa kama Roho mt.atapenda ulewe, au kama ataamua kukupa tafsiri.

  Tatu: Unaweza kunena lugha ambayo kuna watu wanailewa, na wewe huielewi, au lugha ambayo hakuna mtu anailewa.

  Nakomea hapa.

 6. Siyi/Lenda,

  Nimesoma comments zetu nyingi kimya kimya muda sasa, ivi hasa mnatatizo gani? manaa naona kama si utani-utani tuuu basi ni kucheka-cheka tuu au kuongea mambo ya dini ya kuchosha kweli yanayonyesha ukavuuu wa Mtu ndani yake.

  Lenda, Hakuna upagani kuzidi huu wa Mtu kuchezea Utendaji wa RM kwa Kanisa la BWANA.

  Siyi, ktk mambo ya rohoni kwa mada nyingi humu, nilishakuambia ni maji marefu mno kwako na kila uyagusapo wewe hujuagi tu, ni rahisi kabia mtu wa rohoni kukuona kua hapa ni full off, full giza maskini wa Mungu, mbali mno na Wokovu wa kweli na maisha halisi yaliyobadikishwa na Yesu. Unajivua nguo hadharani Siyi kila mara kwamba wewe ni shallow mbaya kwa mambo ya kweli ya Mungu labda ya Sheria za Agano la Kale ambazo hata ivyo nazo, huna tofayuti na Mafarisayo na Masadukayo ktk kuyaelewa ya Musa in connection to Bwana wa sabato- Yesu.

  Siyi, YOU ARE TOO SHALLOW AND DRY KTK YA ROHONI, yaache mpaka hapo, Neema itakapofunuliwa kwako au utakapoamua kupokea neema iliyofunuliwa tayari, ndipo akili yako ya kichwa na rohoni, itahuishwa ii uongeapo mambo ya Mungu hapa na Neno, hali yako ya kiroho, ni rahisi mtu kuifeel/sense/smell/tambua/onja/chungulia/kui-antena nk but as it stands now, you are dead ndani and no vijito ya maji ya uhai maana mambo haya si kwa nguvu, dini, uweza,amri za M23 forest Congo bali ni kwa Roho ambaye najua hunaye , wala humjui na wala kwa mujibu wa doctrine ya mdada aliyeanzisha dini yenu Ellen akiwa na usingizi, RM hapewi nafasi wala hana supremacy yoyote, mpo mpo tu kama dini nyingine na imanI za mochwari, wakavuuuuuuuuuuuuuuuu, hamna kitu ndani ila kichwani kukariri maandiko, aaaa angalau.

  Press on.

 7. Sungura,
  Unaonekana kunikaba koo au!! Ha ha ha ha ha!!
  Mimi niliinukuu hiyo aya kwa ile dhana ya “KUFAIDIANA TU BASI”. Hi ndiyo ilikuwa maana yangu kaka. Ndiyo maana nilikwambia kuwa, ndani ya hiyo 1 Korinth 10:24 kuna suala la chakula? Na badala ya kunijibu, wewe umebaki kwenye sura nzima. Kwa maelezo mengine, hutaki aya yoyote ya 1 Korinth 10 inukuliwe vinginevyo tofauti na chakula. Nikakwambia kuwa, hebu angalia na aya zingine, kwa kuangalia mikitadha ya sura zake ili utoe maana pia. Ulikimbia tena. Umeamua kunishika shingoni tuuu ukinilazimisha nikubaliane na hiyo dhana yako.
  Anyway, sasa, naomba tuachane na hiyo tu. Maana haisadii lolote. Badala yake, tuendelee na mjadala mwanaume.
  Sungura, kunena kwa lugha wasabato tunanena sana kwa lugha. Tena kwa uzoefu wangu binafsi, nilikupa aina tatu za kunena kwa lugha. Lakini naona hukuridhika nazo. Sasa naomba nikuulize, maswali haya;
  1. Waweza kutofautisha kati ya karama za Roho na matunda ya Roho? Kunena kwa lugha ni karama au tunda la Roho?
  2. Lugha unayoinena huwa unaielewa au huwa inaeleweka kwa yeyote hata Mungu?

  Nakusubiri Sungura

 8. Siyi,
  Mbona unasema kitu ambacho hakipo ndugu yangu?
  Unataka nirudie pachiko lako mpaka mara ngapi, kwa nini na wewe usirudie ili ujue makosa uliyoandika?

  Wewe ndo ulianza kusema hivi: ”Kwa maelezo mengine, unenaji wa lugha, Paulo aliusisitiza usiwe wa mtu mwenyewe binafsi bali uwe kwa ajili ya wengine 1 Korinth 10:24, maana hiyo ndiyo ilikuwa ni uthibitishaji wa upendo (agape)”

  Nami nikakwambia kuwa huu mstari Paul alikuwa anawaambia hao watu habari za kuwatanguliza wengine wakati anaongelea suala la meza ya Bwana, si suala la kunena kwa lugha.

  Baada ya hapo makala yako iliyofuatia ukanipa msatari wa 1cor 10:20. Nakunukuu

  ”1 Wakorinth 10 :20, aya hiyo hitaji kitu kinachoitwa chakula!!”

  Ndipo nikakuuliza huo mstari umeutoa wapi tena, na nikaongeza kukuliza kuwa umeniandikia huo mstari ilinifanye nini nao? Na nikunukulia kuanzia mstari wa 1cor10:20 -26, haiongea habari za kunena kwa lugha, bali ni fafanuzi na meaelezo yatokanayo na suala la meza ya Bwana ilivyokuwa inafanyika kwa Wakorintho.

  Sasa sikuelewi unapoendelea kunisahambulia, unataka nifanye nini. Au hutaki tu kuonekana kuwa ulinukuu mistari ambayo haihusiani na suala la kunena kwa lugha?

  Huku ni kupotezean amuda, unanifanya nirudie jambo lilelile wakati wewe ndo ulikosea.
  ……………………………..

  Lakini kuna kitu ulikisema, amabcho baada ya kuwa nimekiangalia kwa umakini sana nimezidi kugundua kweli wasabato huwa hamneni kwa lugha, bali mnafalsafa yenu nyingine tu. Ona ulichosema hapa:

  ”Kuna watu wamejaliwa sana kujua lugha. Yaani wao hata akijifunza kidogo tu, au akiingia kwenye mazingira ya hiyo lugha, hachukui muda akaelewa lugha hiyo. Hii hutokana na karama yake apewayo na RM. Hivyo, watu kama hawa, wanapofika maeneo mengine for the cause of the gospel, Biblia inashuri pawe na wenye kutafsiri ili watu waimarishwe kwa ajili ya marejeo ya Kristo.”

  Siyi unaona kunena kwa lugha kwenu kulivyo!! Yaani kabisa bila aibu unakomaa kuwa mnanena sana kwa lugha, kumbe kunena kwenyewe kwa lugha unakosema ndoo huku!!

  Kwa Kiswahili kingine, wewe Siyi kama miongoni mwa watu hao waliojaliwa sana kujua lugha, ukikaa uchina siku mbili tatu utaanza kunena Kichina. Halafu mwanaume unasimama kifua mbele kuwa huko ndiko kunena kwa lugha ambako biblia inasema. Hata aibu huna!!!

  Huu ni mzaha mkubwa sana!

  Siyi kama kunena kwa lugha kwenu si huku nilikosema hapa, please niambie kuwa nimekosea, na unifafanulie jinsi wewe unavyonenga kwa lugha.

  Than u sir!

 9. Lenda,

  What are u talking about?

  Mbona unazidi tu kuibukia kusiko. Au hata huelewi maana ya kukwazika?

  Ni wapi unaponiambia kuwa nimekwazika?

  Wewe kweli naona heri uendelee tu kula bata huko uliko, maana naona hata ulishasahau kabisa mijadala inaendaje hapa SG.

  Acha sisi tuendelee!

 10. Lwembe,
  Nimekufuatilia vyema kaka.
  Habari za kunena kwa lugha sijui kama umezifuatilia kwa umakini mkubwa hadi ukaonekana kusema haya uliyoyasema. Binafsi, miongoni mwa hayo ninayoyajua kuhusu upetecoste na kunena na kwa lugha, ni upotfu tu ulioanzishwa na watu fulani kwa kuamua kujichepua kwenye misingi ya imani halisi ya Biblia tena tangu zamani sana hata kabla ya 1906 uliousema.
  Wale wanaoamini kuwa kuna urejeshwaji wa kipentecoste kaka, wamelazimishwa tu kukubaliana na cult doctrine za majesusi walioingia na dini yao “Real New Testament Christianity” wakitaka watu waamini teolojia ya Spirit-baptism with tongues,iliyokuwa ikiandamana na uchawi mkubwa wa kufanya miujiza mikubwa (Harrell, All Things Are Possible, p. 13). Miongoni mwa walioongoza kwa ufedhuli ndani ya dhehebu hilo ni MARIA BEULAH ambaye alikuwa nabii wa uwongo na kuhani mwanamke aliyetabiri vifo vya watu na bahati nzuri havikutokea. Alikuwa ni mpentekoste aliyekuwa anahubiri hata kwa Wamormons (Dictionary of Pentecostal, p. 901). Wengi wao walipoanza kugundua hilo, walianza kulihama kanisa hilo.
  Kunena kwa lugha hakukuanzishwa na Wapentekoste kaka. Sina muda ningekwambia zaidi.

 11. Sungura,
  Nimecheka saaaaaaaaaana! Unajua, hivyo ndivyo Maandiko yanavyofungwa, kila unaposoma unaona na 1 ndiyo na 2!!!!!
  “”Kama huwezi kuona tofauti ya wazi kati ya sentensi: 1.nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine.
  2. wote wakajazwa na Roh mt. wakaanza kusema kwa lugha nyingine, wewe si kipofu wa kawaida!””
  Umeona Maandiko yanavyopofua? Si kawaida, giza totoro!!!

  Halafu hata nawe unanishangaza kidogo, lakini itakuwa ni kutokana na tabia ya kutoyaamini Maandiko sawa sawa kwahiyo mapepo ya dini ni lazima yakuzingue!!

  Kunena kwa lugha kulikoma Katoliki walipofanikiwa kulizimisha Kanisa la Kwanza na wao kuwa ndio hilo Kanisa, jambo hilo liliondolewa Kanisani kwa utenzi safi ya kwamba vipawa viliisha na mitume, vikabadiliwa na Liturgia!!! Kanisa la Kweli likafa!

  Ufufuo wa Kanisa unaanza na Luther, Kuhesabiwa Haki kwa Imani. Juu yake ukaja Utakaso. Wasabato wamezaliwa katika Hatua hii ya pili, badala ya kunyoosha Njia wakachepukia porini wakijilisha Mafunuo ya Uongo!

  Katika Hatua zote hizi mbili kulikuwa HAKUNA kunena! Hakuna pepo wa dini anayeweza kumtangulia Mungu!!! Ukiona Mkatoliki au Mlutheri au Msabato au wa dhehebu lolote lile nje ya Wapentekoste, anakuambia ananenaga kwa lugha, huyo ni Mnafiki tu!!!!

  Mungu amevirejesha Vipawa vyake Kanisani kwa mara nyingine kulingana na Ahadi ya Restoration, 1906! Kwa hiyo Msabato aliyezaliwa huko 1800 hawezi kujua chochote kuhusu KUNENA; na akikuambia anajua, basi yakubali Maandiko kwamba nawe umemuona MNAFIKI wa kweli katika maisha yako, maana wanafiki wa kwenye Biblia hao wanawakilisha zile roho, hawa wengine wa mtaani ni sawa na vibaka tu!!!!

  Kwahiyo mjadala wa Kunena kwa Lugha, kimsingi unawahusu Wapentekoste, hawa wengine wakitaka kushiriki na kuyafaidi matunda yake, basi na wayatii Maandiko kwanza, vinginevyo wataishia ktk makundi ya Fellowships, ambayo ndicho kilele cha Unafiki, hawajui wanakotoka wala waendako!!!

  Hebu wazia mtu aliyeumeza uongo wa “Asante Yesu x 666” akauvamia na kuondoka nao, akawa anajitukuza ktk jambo la Uongo, yaani AMEDANGANYIKA, na hasikii la yeyote yule, kipofu akimuongoza kipofu…!!!

  Ubarikiwe!!

 12. SUNGURA.

  Samahani, sikujua kama Mkristo anaweza kukwazika hivyo. Endelea na mjadala na Siyi natoa maoni yangu juu ya Hoja ya kunena kwa lugha.

  Jitahidi uzae matunda ya Roho Mtakatifu epuka hasira uwe na Amani.

  Yakobo 3:17 “Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.”

  Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote aisudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo.”

  tumia Bibla zaidi ndio maana Halisi ya Strictly Gospel,maneno ya hekima za kibinadamu watu wengi waweza kunena na kushawishi.

  Timotheo 2:14 “Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao”

  Nafikiri wapagani wakisikia vile unajadili maneno yako hawatatamani kumfuata Kristo.
  Endelea na mjadala na siyi.

 13. Sungura,
  Naona umeniuliza swali tena. Nilikwambia kuwa, mwitiko wako wa siku ile, yaelekea kabisa hukuielewa post yangu. Nilichokwambia ni kwamba, isome tena post yangu, halafu urejee na aya nyingine zaidi nilizozinukuu kwenye pachiko langu hilo ili uone uhalisia wa kile nilichokisema. Aidha, nilikwambia kuwa, aya 1 corith 10:24 kuwa ndani ya aya hiyo, haizungumzii chakula. Wewe ukanitajia 1 corith 10;20. Mimi nakuona umechoka kaka. Ndiyo maana nilikwambia kuwa, hebu isome tena hiyo aya ya 24 na aya zingine kwa sababu nimezinukuu sehemu mbalimbali ndani ya Biblia, nazo uzikanushe kwenye post hiyo nzima!! Upo hapo?
  Karibu sana

 14. Lenda,
  Naona umeamua kuibuka tu ili useme chochote bila kujali mahali unapoibukia!!

  Kama huwezi kuona tofauti ya wazi kati ya sentensi: 1.nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine. 2. wote wakajazwa na Roh mt. wakaanza kusema kwa lugha nyingine, wewe si kipofu wa kawaida!

  Halafu ati umesema hivi ”TUNAPASWA KUNENA KWA LUGHA NYINGINE SI KWA LUGHA MPYA”
  Kati ya wewe na aliyesema hii ahadi nani mkweli ; Mark 16: 17- .. watasema kwa lugha mpya?

  Ndo maana nilisema kuwa wasabato huwa hamneni kwa lugha!

 15. 1. TUNAPASWA KUNENA KWA LUGHA NYINGINE SI KWA LUGHA MPYA.

  “IMEANDIKWA KATIKA TORATI, NITASEMA NA WATU HAWA KWA WATU WA LUGHA
  NYINGINE” 1 WAKORINTHO 14:21

  “IMEKUWAJE BASI SISI KUSIKIA KILA MTU KWA KILA MTU LUGHA YETU
  TULIYOZALIWA NAYO?”
  MATENDO 2:8

  WOTE WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU, WAKAANZA KUSEMA KWA
  LUGHA NYINGINE, KAMA ROHO ALIVOWAKALIA KUTAMKA”
  MATENDO 2:4

  2. TUNAPONENA LAZIMA KUWE NA TAFSIRI.

  “KWA SABABU HIYO YEYE ANENAYE KWA LUGHA NA AOMBE APEWE KUFASIRI” 1
  WAKORINTHO 14:13

  “LAKINI ASIPOKUWAPO MWENYE KUFASIRI NA ANYAMAZE KATIKA KANISA” 1
  WAKORINTHO 14:28

  3. KUNENA NI KWA ZAMU NA KWA IDADI MAALUMU.

  KAMA MTU AKINENA KWA LUGHA, WANENE WAWILI AU WATATU, SI ZAIDI, TENA
  ZAMU KWA ZAMU, NA MMOJA NA AFASIRI.” 1 WAKORINTHO 14:27

  “NA MANABII WANENE WAWILI, AU WATATU, NA WENGINE WAPAMBANUE.”
  1 WAKORINTHO 14:29

  “Imekuaje basi sisi Kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?. Warpathi na wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia. Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu”
  Matendo 2:8-11

 16. Siyi,
  1Cor 10:20 uliyoisema, na maneno uliyoongeza kwamba aya hiyo hitaji kitu kinachoitwa chakula!!, umeaniandikia ili nifanye nini nayo?

 17. Sungura,
  Nina waswasi kama uliuelewa ujumbe wangu huu ulioujibu. Nikuombe uusome tena ndipo ujibu. Maana nimeona uko nje nje ya kile nilichokitaka. Aidha, naomba na majibu ya maswali yangu..
  Nakusubiri sana.

 18. Siyi,

  Mbona hueleweki rafiki, mimi nimekwambia habari ya 1cor1o:24, kuwa haiongelei habari za kunena kwa lugha kama ulivyosema, wewe unaniambia niangalie 1cor 10:20. Hiyo umeitoa wapi tena!? Relax, na ukiri tu kwamba ulichemsha.

  Haya hii hapa hiyo mistari:

  1Cor 10:20 No, but the sacrifices of pagans are offered to demons, not to God, and I do not want you to be participants with demons. 21 You cannot drink the cup of the Lord and the cup of demons too; you cannot have a part in both the Lord’s table and the table of demons- Hakuna habari za kunena kwa lugha hapo, ila ni habari za kula na kunywa.

  1Cor 10: 23 “I have the right to do anything,” you say—but not everything is beneficial. “I have the right to do anything”—but not everything is constructive. 24 No one should seek their own good, but the good of others.

  25 Eat anything sold in the meat market without raising questions of conscience, 26 for, “The earth is the Lord’s, and everything in it. – Ktk habari hii, Paul alikuwa anaonya kuhusu tabia ya watu kutokusubiriana wanapokuwa wameandaa meza ya Bwana.

  Nimeweka na mistari mingine ili uone kwa uwazi kilichokuwa kinaongelewa.

  Kama unataka kujua kuwa kunena kwa lugha kulikosemwa kulimaanisha lugha usiyoijua, soma habari ya siku ya pentekoste Roho mt aliposhuka,kama waliokuwa wananena walikuwa wanazijua zile lugha walizonena.

  Acts 2:4 All of them were filled with the Holy Spirit and began to speak in other tongues[a] as the Spirit enabled them.( Zingatia neno ”Other Tongues”) ndo ujue kama zilikuwa ni lugha wanazozijua au la!

  Haya maneno si kwa mtu unayempenda ”Wakorinto walikuwa na tabia waliyo nayo leo walokole wote. Wale wenye uwezo wa kunena kwa lugha, huwa wanafikiri kuwa, wao wako karibu na Mungu zaidi ya wengine wasiyonena kwa lugha”

  Hiyo ole uliyosema inakuhusu wewe, unayezungumza vitu usivyokuwa navyo uhakika kana kwamba unavijua!

  Take care!

 19. Sungura,
  Mmh, mimi sina kinyongo na walokole. Na wala siwasakami. Hizi definitions zako tu. Na kwa vile kila mtu ana uhuru wa kufikiri, hiyo hainipi shida.
  Ninawapenda sana Walokole. Ndiyo maana natumia muda mwingi kunena nao habari za neno la Mungu. Nisingekuwa nawapenda, ningekaa kimya. Ukimya ndiyo dalili ya chuki na kutowapenda watu. Ukiona mtu hakwambii chochote, japo alipaswa kukwambia, jua kuwa mtu huyo hakupendi kabisa. Wapendanao kaka Sungura, huzungumza pamoja. Tafadhari usiendelee kuchochea uhasama na chuki dhidi ya mimi na walokole. Ila nina imani kwa wenye hekima zao, wanakielewa unachokifanya kuwa ni cha kitoto kabisa(sijui kama hilo nalo ni tusi). 1 Wakorinth 10 :20, aya hiyo hitaji kitu kinachoitwa chakula!! Angalia na aya zingine maana nilizitoa sehemu tofautitofauti useme nazo zinataja nini!!
  Nami ngoja nikuulize,
  1. Wewe unajua nini maana ya lugha mpya na lugha nyingine?
  2. Kama si mtu alikuzwa kwenye mazingira ya diglossia, leo wanaojua lugha zaidi ya moja wanapotaka kuhubiri tunasemaje? Huku nako ni kunena kwa lugha? Lugha nyingine au lugha mpya?
  3. Je, ndani ya Biblia kuna sehemu ya maandiko inayosema kunena kwa lugha nyingine au mpya, ni kunena lugha usiyoijua? Naomba rejea!
  4. Wewe kanisani kwako unaponena kwa lugha mpya/nyingine na waumini wenzako wakati wa ibada – mnanena pamoja (mnaomba), je, kuna rejea yoyote ndani ya Biblia inayounga mkono system hiyo ya makelele?
  “Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe’ – Isaya 33:1.

 20. Siyi,
  Uko na ‘grudges’ na walokole eh?

  Mbona unawasakama sana brother, huku ukisema uongo mbele ya watu, why can’t leave them alone, kama wewe ulokole ulikushinda?

  Wakorintho hawakujiinua, bali walikosa tu utaratibu wa kiibada katika suala la kunena kwa lugha kanisani, ndo Paul akaamua kuwafundisha. Ni wapi biblia inasema walijiinua? Uko na negative stereotype against walokole. Exercise love plz.

  Uongo uliosema huu hapa:” Kwa maelezo mengine, unenaji wa lugha, Paulo aliusisitiza usiwe wa mtu mwenyewe binafsi bali uwe kwa ajili ya wengine 1 Korinth 10:24..”

  1Cor 10: 24 haiongelei mambo ya kunena kwa lugha, bali inaongelea mambo ya chakula.

  Paul alichokissema ni kwamba kwenye kusanyiko mtu akinena kwa lugha lazima kuwe na wa kufasiri. Lakini kama si kwenye kusanyiko unenaji wa lugha aliokuwa anasema Paul ni kwa ajili ya mtu binafsi.

  Nakunukuu hapa: ”Kuna watu wamejaliwa sana kujua lugha. Yaani wao hata akijifunza kidogo tu, au akiingia kwenye mazingira ya hiyo lugha, hachukui muda akaelewa lugha hiyo. Hii hutokana na karama yake apewayo na RM”

  Siyi mtu akijifunza lugha fulani akilewa na akaweza kuiongea, huko nako ni kunena kwa lugha ambako biblia inakuita kunena kwa lugha? Wapi imesema hivyo?

  Aina ya tatu ya kunena kwa lugha na yenyewe sikubaliani nawe katika maelezo yako. Hakuna kunena kwa lugha kwa ki moyomoyo. Dhana nzima ya kunena kwa lugha mpya ni kusema kwa uweo wa Roho mt. lugha usiyoijua.

  Nani aliyenena kwa lugha ambayo yeye mwenyewe alikuwa anaifahamu na huko kunena kwake biblia ikakuita ni kunena kwa lugha mpya?

  Acha kushambulia wapentecoste, hiyo injili kawahubiria wasabato ambao kwanza hata kunena kwa lugha hakuamini!

  Fundisha hayo vipofu, si wanaoona!

  U are welcome!

 21. Hili ndilo somo nilijualo mimi kuhusu KUNENA KWA LUGHA kama matokeo ya kujazwa na Roho Mtakatifu. Kutimia kwa ahadi ya Kristo kwa mitume wake siku ya pentekoste, ilkuwa ni kwa lengo la kukamilisha utume hapa duniani. Huu ulikuwa ni ubatizo wa RM, mdo 2:1-4. Kila mmoja baada ya ubatizo huo, angefaa kwa kazi na jukumu maalumu la utume kwa mujibu wa karama yake aliyopewa, maana RM ndiye atoaye hizo karama-1 Korinth. 12, ambazo huwa na lengo la kulijenga kanisa-mstari 7. Akijumuisha miongoni mwa karama anazozitaja Paulo kwa ajili ya utume, ni karama nyingine za kutenda miujiza, nk. mistari ya 8-10. Na kwa sababu Paulo alisema kuwa hakuna mtu mwingine awezaye kuelewa mtu ananepo kwa lugha mpya, isipokuwa Mungu tu, 1 Korinth. 14:2 na kwamba kunena kwa lugha humjenga anenaye zaidi ya msikilizaji-msatri 4, wengi hufikiri kuwa, neno lugha mpya, hufikiri ni lugha zisizo za kibinadamu na kwamba huwa ni karama ambayo ni so personal zaidi dhidi ya jumuia/public nzima. Mtazamo huu hauko sahihi kibiblia.
  Unenaji wa Lugha huko Korintho
  Wakorinto walikuwa na tabia waliyo nayo leo walokole wote. Wale wenye uwezo wa kunena kwa lugha, huwa wanafikiri kuwa, wao wako karibu na Mungu zaidi ya wengine wasiyonena kwa lugha- 1 Korinth. 4:6-8. Wakorintho walikuwa na tabia hii, hadi ilifikia hatua ya wao kujiinua zaidi ya wale wenzao wasionena kwa lugha. Why? Lugha ya kuinjilishia ilikuwa ni kilatini au kigiriki tu. Mtu yeyote aliyenena lugha zaidi ya hizo mbili, alionekana star sana spiritually kiasi cha kuwadharau wengine. Paulo alipofika kwa wakorintho akawaangalia na kuwahurumia sana, ndipo kawaambia, “…nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote…” -1 Korinth 14:18. Walisahau kuwa, kunena kwa lugha ni sawa na karama zingine tu-1 Korinth 12:21-25. Karama zote hata ile ya kunena kwa lugha ilikuwa ni ya muhimu sana ili kanisa lipate kujengwa 1 Korinth. 14:5

  Kwa maelezo mengine, unenaji wa lugha, Paulo aliusisitiza usiwe wa mtu mwenyewe binafsi bali uwe kwa ajili ya wengine 1 Korinth 10:24, maana hiyo ndiyo ilikuwa ni uthibitishaji wa upendo (agape) 1 Korinth. 13:5. Hii inaonesha kuwa, kuomba kwa sauti kubwa ndani ya kanisa tena kwa kunena kwa lugha, kila mtu kivyake, ni hali ya machafuko, ubinafsi, chuki na kutopendana iliyooneshwa na wakorintho1 Korinth. 14:2. Hata hivyo kuitumia karama ya kunena kwa lugha kwa sauti kubwa individually ndani ya kanisa, ni kinyume na matakwa ya karama hiyo – 1 Korinth. 12:7; 1 Korinth. 10:23, 24. Kunena kwa lugha kwa mtindo huo binafsia, ni ukiukaji wa kanuni ya karama za RM katika 1 Korinth 10:31-33 za kufanya yote kwa utukufu wa Mungu na kwa malengo ya kuokoa roho za wengine kinyume na kuendeleza ubinafsi.

  Aina za kunena kwa lugha.
  Kwa mujibu wa Biblia kunena kwa lugha kumebainishwa katika makundi(aina) haya yafuatayo;
  1. Kunena lugha nyingine kwa wasioamini. Hili ndilo lililotokea siku ya Pentekoste. Na kwa sababu ya kuzingatia makusudi ya karama ya kunena kwa lugha, RM anapowashukia watu, henena matendo makuu ya Mungu. Mnenaji na/au msikilizaji, sharti waielewe lugha hiyo. Tofauti na hapo, hiyo siyo lugha nyingine. Rejea mdo 2:4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. 7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya. 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?.
  Unenaji huu wa Lugha nyingine ni sharti ueleweke kwa wengine . Ukiangalia siku ya pentekoste, walikuwepo watu wa makabila mengi sana, lakini kila mtu alielewa kwa lugha yake ya kwanza.
  Kwa maelezo mengine, unenaji huu wa lugha nyingine, hutokea kwa miujiza ya RM. Lakini jambo la msingi zaidi, ni kwamba, lugha hiyo, sharti ieleweke. Na hii ndiyo maana ya lugha, – sauti zenye kubeba maana.
  2. Kunena kwa lugha nyingine kwa waumini wakati wa kuhubiri injili. Kama mtu wa taifa jingine akija, na akapewa kuhutubu, akianza kuhutubu ni sharti awepo mfasiri ili kanisa lipate kujengwa kama mtume Paulo anavyoelekeza katika 1 korinth 14: 27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
  Kuna watu wamejaliwa sana kujua lugha. Yaani wao hata akijifunza kidogo tu, au akiingia kwenye mazingira ya hiyo lugha, hachukui muda akaelewa lugha hiyo. Hii hutokana na karama yake apewayo na RM. Hivyo, watu kama hawa, wanapofika maeneo mengine for the cause of the gospel, Biblia inashuri pawe na wenye kutafsiri ili watu waimarishwe kwa ajili ya marejeo ya Kristo.
  Wakati wa kuhutubu ama kuhubiri, kunena kwa lugha kunapaswa kufanyike kwa namna Biblia inavyoelekeza. Na kama kanisa lote litanena kwa lugha wakati wa kuhutubu/kuhubiri, Paulo anasema, kanisa litakuwa kama la wenda wa wazimu; Rejea aya 23 Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu? Walokole leo, wanaangukia kwenye kundi hili.

  3. Kunena kwa lugha kati ya mtu na Mungu wake. Huu ni unenaji wa lugha ambao, mtu hunena/huzungumza na Mungu wake yeye mwenyewe binafsi. Ni mawasiliano ya mtu ndani ya moyo wake na Mungu wake tu. Hakuna mtu mwingine anayesikia. Kwa maneno mengine, ni hali ya mtu kuwa rohoni na Mungu wake. 1 korinth 14: 2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.
  Na mara nyingi mtu anenaye kwa lugha (kwa maana ya kuwa rohoni), huijenga nafsi yake (aya ya 4), ni tofauti na anenaye kwa lugha kwa muujiza as in 1 above, au wakati wa kuhutubu. Aina hii ya kunena kwa lugha mara nyingi huwa ni kuugua kwa mtu rohoni(mtu kumwambia Mungu shida zake za moyoni bila kutamka maneno). Ishara za mtu aliye rohoni, zinaweza kuwa ni kutokwa na machozi ama kulia kabisa au kuonesha tabasamu na furaha pale sala/maombi yake yanapojibiwa.

  Kwa mujibu wa Biblia, huku ndiko kunena kwa lugha. Hata mimi Siyi hizi ndizo aina za unenaji wa lugha ninazozifanya kama matokeo ya nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yangu. Kunena kwa lugha zisizoeleweka ndani ya kanisa, tena kila mtu ya kivyake, is not Biblia.
  Mungu hajaanza kusema na watu kwa lugha nyingine ndani ya agano jipya tu. Unenaji wa lugha nyingine, ulikuwepo tangu agano la kale. Na haukuwa kama ulivyo leo kwa makanisa la kilokole na kipentekoste. Wakati umefika wa wao kukaa chini na kuichunguza vizuri Biblia, ili kuona kama kuna usahihi wa hayo wanayoyafanya kwa karama hii ya kunena kwa lugha kama kanisa lote, tena at per! Mtu akiona tofauti kati ya vile anavyofanya na isemavyo Biblia, na ageuke na kuitafuta njia iliyo njema – njia ya mapito ya zamani- njia ya Bwana- njia ya wokovu wetu –Yesu Kristo aliyekuwepo tangu agano la kale hadi leo – Mungu wetu Mkuu asiyebadilika kwa kauli au mafundisho yake.
  Ubarikiwe na Bwana.

 22. Kunena kwa Lugha ni raha sana maana shetani haelewi unayotamka, na biblia imeandikwa sisi hatujui kuomba ila Roho huomba badala yetu.

 23. Wakati wenzetu wanakuwa na umoja sisi tunabaki tukijifia ubatizo wa maji mengi,mbona walio batizwa kwa maji mengi na machache ni wale wale,wezi,wazinifu nk,maji yatabaki kuwa maji matupu kama hakutachanganyika na Neno,ingekuwa ni maji mengi basi sote tukabatizwe mto yordan,tunachoangalia ni ubatizo wa moto au Roho,ambao unambadilisha mtu kutoka katika utumwa wa dhambi,unagusa maisha ya kiroho sisi sio watu wa mwilini kama wale wanaovua viatu vya mwilini na kutawadha kwa uchafu wa ngozi,Tatizo shule hamtaki kwenda,ukishajua kupiga kelele tu tayari wewe ni mchungaji unaanzisha kanisa lako upate shekeli.vyombo hivi vyote vya neema twatumia kwa ishara tu,mikate sio halisia,divai sio halisia,maji sio halisia,ubatizo hata mchanga inapolazimu kama mazingira hayana maji we batizia,kwa imani.Kunena kwa lugha,hayo ni mojawapo ya matunda ya mtu aliyeokoka,lakini tambua kuwa hata mapepo yananena kwa lugha,unaweza usinene kwa lugha lakini ukajazwa unabii,hekima ya KIMUNGU,nk.Suala la miujiza Mungu wetu anafanya muujiza kila paitwapo leo,sio uponyaji tu,hata kuiona siku ni muujiza.kuna wagonjwa wengine Mungu kaachilia ili afanye matengezo,Huwezi kumlazimisha Mungu amponye mtu huyo,ndipo hekima ya kimungu na unabii wa kimungu unapotakiwa kupeleka ujumbe.

 24. HAIPASWI KUKAA NA KUSHKA MAPOKEO YA DN ZE2 AU KUFUATA ISHARA. HAPA TAFANUA KIDOGO ISHARA N LAZMA KWA MKRISTO ALIYE OKOKA KAMA NENO LINAVYO SEMA MARKO 16:17-18 ALIYE AMIN HUWA KUNA ISHARA AMBAZO MUNGU ANAMPATIA KUNA ISHARA NYNG AMBOZO MUNGUAMEAHD.LAKN N VYEMA KULIACHA NENO LA MUNGU LIZUNGUMZE LENYEWE KUHUSU ROHO MTAKATIFU NA S MAPOKEO YA DN ZE2 2KFANYA HVYO 2TAKWENDA SAMBAMBA NA NENO 1KOR 4:6 PAULO NA APOLO N MFANO BORA HAWAKUTA KUJFUNZA KUPTA YALIYO ANDKWA KWA SABABU ASJE M2 AKAJVUNA KUPTA YALIYO ANDKWA LENGO LANGU N KUELEZA KUWA HAPASW KUJFUZA KUPITA YALIYO ANDKWA

 25. Mpendwa
  Noel Masnjila,
  hakuna anayepinga kunena kwa lugha,tunakataa sio ishara pekee ya kuonyesha kuwa tumempokea Roho Mtakatifu(Marko 16:17-18)

  Tulipo mpokea Yesu Kristo(WOKOVU)tulibatizwa na Roho Mtakatifu, Roho mtakatifu aliweka mhuri wa Mungu SEAL usioonekana(Waefeso 1:13).Tokea hapo alitawala maisha yetu,anatuongoza/anatusaidia/pasha habari/anatushuhudia tukifanya dhambi nk.yupo ndani yetu hakuna hawezae kutupokonya isipokuwa tunaweza kumuhuzunisha kwa kutenda dhambi..

  Tunaona kina Petro wakijiliwa naRoho Mtakatifu siku ya pentekoste,lakini Matendo 4:8, tunaona tena akijaa Roho Mtakatifu,anajidhirihisha(anatuwezesha)wakati ule sisi wenyewe tunakua hatuwezi,anatupa ujasiri.

  Ni muhimu tuchunguze Maandiko tuyalinganishe na mafundisho tunayofundishwa,Bahati sisi Wakovu tuna ruksa ya kuuliza kanisa maswali,uliza.waoneshe mistari ya maandiko.tusikubali mapokea bila kuuliza.Ukisoma injili karibu yote Bwana Yesu anajibu maswali,nini wapi,lini nk
  Hapo ndipo tunaitwa wanafunzi.

  Sote tulio okoka tumejiliwa na kumpokea Roho Mtakatifu siku tulipompa Bwana Yesu maisha yetu,vinginevyo kama unajiita mwokovu hujampokea Roho Mtakatifu wewe sio mwokovu.Aliyempokea baada ya muda tunaona matunda ya Roho Mt kwa nje(kwa macho) alikua kahaba anahuishwa anaacha,mwivi,mchawi,mlevi nk.Bila Roho Mtakatifu haiwezekani.

  ila kwa hila kama shetani(anajigeuza malaika wa nuru) unaweza ukajifanya mwokovu “ukaiigiza” Ukisikia hamu ya sigara unavuta kwa kificho mbele ya washirika wewe ni Mwokovu.wewe ujue sio mwokovu unafanya mahoka tu.wana wa Mungu ni dhahiri na wa ibilisi ni dhahiri.

  Barikiwa
  ,

 26. Ndugu Msanjila ,Robert na wengineo,
  Jambo la kusikitisha ninaloliona katika haya mambo ya vipawa, ni kule kujiridhisha katika urahisi na kupenda mambo ya sifa kwa kanisa. Kama vile kunena kwa lugha na karama za uponyo, karama hizi hukutukuza mbele ya watu nawe kuonekana ni wa jinsi fulani, ndipo kanisa huzililia hizo! Utukufu huo pekee, ulipaswa kuliweka kanisa katika tahadhari. Kwani hizo ndizo sehemu adui anazoweza kuzilenga ili kulidhoofisha kanisa kama alivyofanya! Matokeo ya udhoofishaji huo, ndio hili kanisa tulilonalo likiwa limejiridhisha katika jambo ambalo si la kweli na hivyo kuufungia nje Utendaji halisi wa Roho Mtakatifu. Na kwa vile mambo hayo yana utukufu na sifa nyingi, yamelipofusha kanisa, hata unapojaribu kuwaonesha kuwa hayo mliyoyashikia bango ni mambo madogo sana, hebu mgeukieni Mwenyewe awapeni ile manna iliyofichwa, hakuna anayekusikia, wako bize wananena na kutabiri na kutabiriwa!!
  Wapendwa, ISHARA ya KWANZA kwa aliyejazwa ROHO MTAKATIFU ni UJASIRI!!! Hiyo ndiyo ishara ya kwanza inayozaliwa moyoni mwa muaminio na kujidhihirisha katika kuambatana na Neno la Mungu. Haijalishi ni mazingira gani anayokabiliana nayo. Wale waaminio waliokuwa wakikamatwa kwa kuambatana na Neno na kisha kupelekwa katika viwanja vya michezo na kufunguliwa simba wenye njaa, unadhani kilichowastahimilisha ni hizo karama? Karama hazina majuto, tumewaona wengi tu wakinena kwa lugha na wana nyumba ndogo! Tumewaona wengi tu, wakinena kwa lugha na karama ya uponyaji na unabii, lakini wamechukua pesa zao pamoja na sadaka za makusanyiko yao, wakazipeleka Deci! Mifano iko mingi sana ambayo ninyi wenyewe mnaijua na inawashangaza pia, ila mmeifanya mioyo yenu kuwa migumu tu! Hasara ya jambo hili ni kumkosa Roho Mtakatifu ambaye ndiye ile SEAL ya ukombozi wetu! Jinyenyekezeni kwa Neno la Mungu ndugu zangu, huko ndiko kumpokea Roho Mtakatifu, msing’anganie Mapokeo!
  @ Orbi
  Unajua, Uinjilisti ni kupiga makelele ya tahadhari ili kuwastua ndugu zako waione hatari! Yaani ni kama pale unapomuona nduguyo amezungukwa na wauza dhahabu feki, naye anaongozana nao kwenda benki ili akawalipe kutoka akiba yake aliyoikusanya siku ya ujana wake, usipompigia kelele aachane na hao wezi wa ghilba, ukimuacha aende nao wamfilisi akiba yake, nadhani Mungu ataidai damu yake kwako; labda yeye mwenyewe akupuuze na kuendelea na biashara hiyo! Najua ni vigumu kuamini kwamba mtu aweza kataa ushauri wa jinsi hiyo, lakini ngoja nikupe mfano wake uliotokea mtaani. Mama mmoja akitokea ofisi za Pride, huko wanakokopeshwa mitaji, akawakuta wachezesha mchezo wa karata tatu, pembeni yao kuna bidhaa nyingi mpya za kupendeza zimepangwa; pikipiki, baiskeli, simu za mikononi nk. Wale wachezeshaji na kundi lao la wanaojifanya wateja, wakamuotea yule mama, wakati wakimshawishi mwenzao mwingine akawa anachukua pikipiki aliyoshinda na mwingine simu ya Nokia. Hilo likamvutia zaidi yule mama naye akazidi kuwasogelea mpaka akawa mbele ya mchezeshaji! Nyuma yake yule mama aliongozana na mwanaume ambaye ameyaona yote yaliyokuwa yakiendelea na pia anaijua michezo hiyo. Basi akamwita yule mama pembeni na kumwambia aachane na mchezo huo kwani hao ni wahuni tu. Wale walipoona yule mama anataka kuondoka na huyo mwanaume, wakamwambia huyo ni mumiani, mnyonya damu!! Kwa vile vitisho, yule mama akamkimbia yule mwokozi wake akawarudia wale wahuni! Yule mwanaume akaenda zake akamuacha yule mama mikononi mwa wale wachezesha kamali, tamaa ya vile vitu vizuri viliyopangwa hapo ikimuwaka!!!

  Basi tuendelee kumpigia kelele huyu mwanamke (kanisa) kuhusu mapokeo na hatari zake kadiri ya Neema ya Mungu atakavyo tujaalia!

 27. Ni halali ninyi kupunga kwamba ‘kunena kwa lugha siyo ishara ya kujazwa Roho mtakatifu,sababu hamjajazwa Roho mtakatifu,sababu Yesu alisema ktk Yoh 14;17 ‘ndiye Roho wa kweli ;ambaye ulimwwengu hauwezi kumpokea,kwa kuwa haumuoni wala haumtambui,bali ninyi mnamtambua maana anakaa kwenu,naye atakuwa ndani yenu’ nisemaloni kwamba endeleeni kupinga tu maana mnatimiza maandiko,kwa kuwa Roho hayumo ndani yenu,mnajionyesha waziwazi,mpaka siku mtakapo mpokea,najua mtapata jibu.Ndugu yangu Robert na wengine wanaojua kwamba wamejazwa Roho mtakatifu,wala msigeuke kuwafuata ambao siyo wa imani hii,kaza mwendo wala msirudi nyuma,acheni waseme tu,maana hata sisi sisitulibisha hivyo,lakini baadae tumekubali kwamba Yesu ni Bwana

 28. Ndugu yangu,

  Naona umezungumza kwa “hasira’ kwa za Kiinjilisti….! Nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa sana yaani ….kutumia kunena kwa Lugha kama “Benchmark” ya pekee ya Kuwa MTU KAJAZWA NA ROHO…….! Hii ni kwenda kinyume cha Maandiko….Hata Paulo akija leo ukumuuliza swala hilo hatakubaliana nalo.Nasema hivyo kwa kuangalia Nyaraka zake zote alizoaandika….Ufahamu wake wa Agano la Kale…….Jinsi alivyooeleza Muumini aliyeko Ndani ya Kristo nini kimetendeka kwake BAADA YA KUWA NDANI YA KRISTO….!Na mafundisho yake kuhusu Utendaji wa Karama za Roho Mtakatifu ndani ya Muumini…….Ukisoma hayo yote huwezi kabisa kusema ISHARA PEKEE YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NI KUNENA KWA LUGHA TU…..!Wengi wetu ambayo tumepokea WOKOVU chini ya Kivuli cha makanisa ya Kipentekoste tumegoma kabisa kuyaangalia Maandiko zaidi ya kile tulichofundishwa…..yaani kutoka nje ya wigo huu…..! Imani tulizopokea ambazo zimejengwa juu ya Kitabu kimoja tu cha Biblia…..yaani Biblia inafundishwa kwa context ya Kitabu cha Matendo ya Mitume tu ni makosa….! tena makosa makubwa….! Ujumbe wa Biblia unaangaliwa WOTE KWA UJUMLA na ukiuangalia ujumbe wote toka kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo unatakupeleka kwa mtu mmoja tu ambaye ni KRISTO……..! Angalia katika kitabu cha Luka …..Yesu alipokutana na wale wanafunzi njia ya Emmaus……”Akaanza kutoka kwa Musa hadi Manabii wote….akawaekeza toka katika MAANDIKO yote mambo yamhusuyo MWENYEWE (KRISTO)…Luka 24:27…
  Kwa hiyo kama kuna ISHARA YA PEKEE ya kuwa MTU AKIJAZWA ROHO MTAKATIFU (sehemu nyingine anaitwa Roho wa Kristo) ni ipi…..utaona wazi Ishara kuu ya Kujazwa ROHO MTAKATIFU ni kuwa kama Kristo….! Kuwa na Nguvu za Kristo…….Kuwa na tabia za Kristo…….Kuwa na Upendo wa Kristo……Kuwa na tabia za Kristo…..kuwa na tabia za Kiungu……Hii ndio ISHARA YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU……ambayo ukiisoma Biblia kwa utaratibu…na kwa maombi utaiiona……yaani kuwa KAMA KRISTO……Lakini tukin’ga’ngania Kunena KWA LUGHA TU…!matokeo yake ndio hayo Ndugu Lwembe kayasema….. na tunayoyaona….Watu WATANENA KWA LUGHA…….Lakini wameshika mengi mikononi mwao….mara misali za waumini…….mara miujiza na “pako” ambazo ni kama sarakasi tu ambazo hazileta mabadiliko yoyote na utukufu kwa Mungu…..na mara ni hao hata sauti toka Loliondo itaiitwa ni sauti ya Mungu……Mungu na ATUBARIKI…!

 29. Mpendwa John Haule,

  Ninakushukuru sana kwa ukarimu na upendo, kwani ustahimilivu wote umefungwa humo katika Upendo, nasi tukiwa ni mwili mmoja katika Kristo, basi hilo pekee ndilo linalotufanya tuwe tofauti na ulimwengu wote!

  Bwana akutunze, akupe pia NGUVU ya kuifanya kazi yake!

 30. Wapendwa,

  Katika tafakari zaidi ya jambo hili la “Kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mt”, Je, hamulioni kwamba fundisho hili limepitwa na wakati? Nilionavyo mimi kulingana na Mapokeo, lilipotawazwa, hali ya kanisa, yaani kidhehebu, haikuwa kama ilivyo leo hii. Waliokuwa katika kunena huko walikuwa ni Wapentekoste peke yao! Madhehebu mengine hayakukubaliana nao katika hilo mpaka leo hii tunavyoyajadili haya hawalitambui jambo hilo, kwao haya mambo ya kunena na vipawa vinginevyo ni UZUSHI mtupu! Lakini ndani ya madhehebu hayo vimeinuka vikundi vya uamsho, km Wakarismatiki, New Life Crusade nk katika miaka ya 60, hawa wanavyo vipawa na huviendesha nje ya mifumo ya ibada za madhebu yao katika compromisation ya kanuni zao, kwani hayo madhehebu kikanuni hayavitambui vipawa hivyo. Hawa wote wananena kwa lugha, kwa hiyo kulingana na mapokeo ya Kipentekoste, ambayo ndio benchmark, hao pia WAMEJAZWA ROHO MTAKATIFU!

  Wapentekoste imewabidi wawapokee hawa kama wenzi wao katika Bwana kwa kujazwa kwao Roho Mt kama wao! Hayo makundi bado yamo katika madhehebu yao, na ni wafuasi wazuri wa mafundisho yote. Km wakarismatiki wangali wanaongozwa na “Baba Mtakatifu”; pia wanaamini kuwa ‘Hakosei’, wana ibada za wafu, wanasali Rosary / Bikira Maria umejaa Neema …, wanamuomba awaombee, tena wanaamini kuwa mwili wake ‘ulipalizwa mbinguni’ (nadhani mwaka 1967!); na upagani mwingi tu mwingineo. Lakini licha ya hayo wananena kwa lugha!!!

  Ninawahurumia Wapentekoste, mtatokaje katika kifungo mlichojifungia wenyewe!! Angalieni mzaha mnaofanyiwa na hivyo vikundi vinavyoukiri wokovu saa 10 jioni baada ya kutoka kwenye ibada zinazopinga mambo hayo asubuhi!

  Kwa fundisho hilo moja lililo nje Maandiko, leo hii Injili yote imekuwa vugu vugu. “Vigezo na Masharti” ya wokovu vimeboreshwa kukidhi uvunaji wa waumini, hata leo hii unawaona wahubiri maarufu wa Wokovu wakiwatangazia watu kuokoka kwa kufuatisha ‘sala ya toba’ kinyume na Maandiko, hawana hata woga:- “Unapofanya sala ya toba na kumkaribisha Yesu katika maisha yako – unaokoka.”!! Lile Agizo Kuu walilopewa mitume likifanywa si kitu!

  Hivi kama Roho Mtakatifu mwenyewe atakuwa ni wa jinsi hii, anayechukuliana na kila fundisho lililo nje ya Mafundisho yake, kwa kweli atakuwa ni Mungu wa ajabu sana tena asiye eleweka! Haya makanisa yananena kwa lugha na yanasimika mashoga, wengine makasisi walio na makesi ya kulawiti wanawahamishia miji/nchi nyingine wasikojulikana wakaendelee na ufuska wao!

  Iwapo Mungu amewapa hao nao Roho Mtakatifu wake katika hali hizo za kiroho walizomo, kufuatana na fundisho hilo la kunena kwa lugha, basi Mungu kwa jambo hili, itambidi awafufue wale wa Sodoma na Gomora awaombe msamaha kwa kuwachoma moto, ili abaki kuwa Mungu mwenye Haki!!

  Ndugu zangu tuondokeni katika mapokeo yaliyopitwa na wakati; Je, ni kweli kuwa hatuuoni huu uongo wa fundisho hill tunapolitazama katika hali iliyopo leo hii licha ya kwamba hakuna mahali Maandiko yanasema hivyo? Nafahamu mapokeo yanapofusha lakini Neno la Mungu nafahamu pia huponya, labda uwe umelikataa mwenyewe kwa makusudi!!

  Mbarikiwe

 31. Mpendwa Biniel,

  Naamini haujambo na unaendelea vizuri na kazi ya Bwana Yesu kristo.Neno la MUNGU hufafanuliwa na kufundishwa ipasavyo na Mungu mwenyewe kupitia Roho wake mtakatifu. Sisi kama sisi tunadumu katika kujifunza wakati wote, ili kulifanya Neno la Mungu likae kwa wingi ndani yetu. Umetaka kujua iwapo maelezo yaliyopo katika post yangu ya tarehe, 26/4/2012; yana Mistari yoyote katika Biblia inayasimamia, ili kwamba pengine katika kumueleza mtu mwingine aweze kujifuza kwa wepesi na kwa uhakika. Kwakweli umetaka jambo jema sana, maana Biblia ndicho kinapaswa kuwa kipimio cha yote tuyasemayo na si vinginevyo.Katika posti uliyoitaja nilikuwa nazungumza na Ndugu zangu Haule na Orbi,katika mazungumzo hayo tulifikia hatua ili kujua, Kigezo kinachopelekea Mtu abatizwe na kama iko haja ya Mtu akishaamini akae kwnza kwa mda fulani,chini ya mafundisho ya kidini, akifundishwa kanisani, ndipo abatizwe au mtu anapoamini tu,anapaswa kubatizwa hapohapo?
  Naaomba nikujibu kama ifuatavyo:- kwanza,Mtu akiamini anapata haki ya kubatizwa. Baaba ya ubatizo kuanzia hapo anakuwa Mwanafunzi kamili,ili kuyashika maelekezo yote ya Neno la Mungu. Biblia inalizungumzia hilo wazi katika; Mt.28:19-20, insema “Mitume waende wakawafanye Mataifa yote kuwa wanafunzi,wawabatize na kuwafundisha kuyashika yote yaliyoagizwa” Kwa mjibu wa maandiko hayo, Mtu akibatizwa ndipo anaendelea kufundishwa,ili afikie kiwango kizuri cha Ukristo wa kweli. La pili, Je, ni wakati gani Mtu akiamini anapaswa abatizwe? Au akishaamini afundishwe Neno la Mungu kwanza hadi viongozi wa Dini wampitishe kuwa sasa anafaa kubatizwa?, HAPANA! kama ukisoma kwa makini katika; Mdo.16:33, inasema……….akabatizwa yeye na watu wake wote wakati huohuo. Na tatu, Je, Mtu akiamini tu inatosha kubatizwa, au kuamini huko kunakompa Mtu haki ya Kubatizwa kunakamilikaje, ili kuitwe kuwa Mtu huyu ameamini tayari kwa kubatizwa? Kuamini huko ni lazima kuambatane na TOBA ndiko kunampa muumini haki ya kubatizwa, LAKINI pia ni lazima aseme mwenyewe. Ukisoma kw uangalifu, Mdo,2:37-38, inasema wazi kuwa,mahubiri walipoyasikia yaliwachoma mioyoni, na hapo wakamuuliza petro kinachotakiwa wafanyiwe – (yaani walitoa tamko kwa njia ya swali, na walipojibiwa, hawakukataa kubatizwa) – wakasema, TUTENDEJE NDUGU ZETU? Petro aliwaambia WATUBU, kisha WABATIZWE, na si vinginevyo ila kwa jina la yesu kristo ili dhambi zao ziondoshwe! Misitari hiyo, ndiyo iliyokuwa imesimamia maelezo na majibu yangu kwa Ndugu zangu hao niliokutajia mwanzo. Nitashukuru Mungu kama kunakitu utapata katika maelezo na kama yatatoa Nuru ya kukufikisha hatua kufalani itakayo sogeza mbele, nia yako katika kutaka tujifunze pamoja Nneno la Mmungu. Nnaomba usiache kabisa kuniwasilia kwa lolote, utakaloliona HALIPO sawa katika maelezo yangu, au linatatiza au kutia shaka hata shaka hiyo iwe ndogo namna gani, ukiilinganisha na Nneno la Mungu. Ubarikiwe na Bwana Yesu.

 32. Mpendwa Orbi,
  Namshukuru Mungu kwakuwa nimeeleweka. Hadi ulipofikia nipo pamoja nawe.Kinacho kufanya upate Huzuni, ni ile Huruma uliyonayo ndani yako. Huruma, namna ya kipawa cha Roho mtakatifu,ambacho Mungu humpa mtu ili asimamie HAKI ya Neno la Mungu. Ukiona yanatokea yasio upande wa maandiko matakatifu ya Mungu, usishangae wala kuhuzunika, maana IMEANDIKWA, na kama imenenwa, Basi ni LAZIMA itimie. Unatakiwa kuendelea kufundisha,kuonya na kuadabisha bila kuchoka na kwa uvumilivu. Maana aliye upande Wa Mungu lazima ataokolewa tu, endelea kutimiza wajibu wako! Endelea kubarikiwa na Bwana Yesu Kristo.

 33. Mpendwa John haule,

  Kuhusu yale maswali mengine, kama lile moja la Hawa, naona kuna thread mpya inayoendana na jambo hilo, labda huko kwatosha kulivinjari. Na kuhusu ile thread ya Mdo 2:38, nilikumbuka katika moja ya post zako katika mjadala huu, uliwahi kutushauri na ndugu Orbi, lilipojitokeza suala la ubatizo, ukatuwekea link yake, nimeiona, asante. Kwa hiyo sioni tena ulazima wa kuleta thread mpya kulihusu hilo bali nadhani itapendeza kama tutaijumuisha huko ili iambatane na hayo yaliyotangulia ili kulifikisha jambo zima katika tamati kama lilivyo ki Biblia, kwa msaada wa Bwana.

  Na kuhusu lile swali la wasomi, kuhusu mwalimu Mwakasege, najua anaitumia vizuri elimu yake ya Uchumi katika mtazamo mzima wa imani katika hayo anayoyahubiri, nikiipitia thread yake kwa utulivu, kama kuna fundisho la kimapokeo, nikiliona, nitaandika wazo langu kulihusu katika namna ya kama tunavyofanya – kufellowship Neno la Mungu.

  Ila maana halisi ya wasomi niliyomaanisha, ilikuwa katika UPOTOSHAJI wa Neno la Mungu wanaoufanya kutokana na hayo wanayoyasomea huko vyuoni. Tena wao wanapofika huko vyuoni, hufanyiwa ‘brainwashing’, hata wanapotoka hapo hukosa hata uwezo wa kupambanua mambo madogo ya msingi licha ya kutukuka kwao kwa elimu waliyonayo!

  Nimeupata mfano mzuri sana wa jambo hilo katika ile link ya UBATIZO uliyonipa. Huko nimemkuta msomi mmoja anaitwa, Mchungaji Dakta Mallisa, huyo anatufundisha kuwa MTUME PAULO ALIBATIZWA AKIWA AMESIMAMA!!!

  Ubarikiwe mpendwa!

 34. Ndugu Orbi,

  Shalom!

  Tafakari uliyoileta ni kubwa sana! Naona unajaribu kutupandisha ngazi kutufikisha katika ‘landing’ mpya, kutoka katika kimo tulichomo; Ubarikiwe!

  Katika kiwango unachotupeleka, ninaamini kuwa tutapata mwanga zaidi wa kutuwezesha kuyatupa mapokeo tuliyoyashikilia, na kisha kuyang’ang’ania Maandiko kama yule mwanamke Mkananayo, hata tuupate Uzima au kubaki na mapokeo yetu …!

  Nikikunukuu, unasema hivi: “Ndugu Haule itachukua muda watu kufunguka katika kifungo cha ‘mapokeo’ …” Jambo ambalo unalionesha hapo ni kwamba; MAPOKEO HUWAFUNGIA WATU! Sasa watu hao tulio katika vifungo hivyo vya mapokeo tukiwa ndio sisi ‘wakristo’ katika vifungo vyetu tofauti tofauti, sijui inakuwaje!?

  Lakini nakushukuru pia kwa NURU uliyoileta, maana dhamiri zetu zikiwa safi twaweza kujifunza kitu zaidi. Ninakunukuu zaidi: “Kama ni msomaji wa Historia ya Ukristo utaona kila kipindi fulani Kanisa lilijenga imani yake katika kweli Fulani ya Mungu pasipo kuuangalia wigo Mpana wa utendaji wa Mungu … na Mungu kwa Neema yake huwa anawafungua watu kwa kusimamisha tena wengine kuinena kweli ya Mungu.” Hii ni KWELI ya utendaji wa Mungu katika kulihudumia kanisa lake.

  Sasa ukweli ukiwa ndio huo, kwamba pale kanisa linapokuwa limejifunga katika mapokeo au ile ‘Kweli Fulani ya Mungu isiyoangalia wigo Mpana …’, Mungu husimamisha tena wengine kuinena ile kweli; Basi, ndio tusema katika hali kama hii, inapotokea Mungu kumsimamisha huyo mwingine ajaye na hiyo Kweli yake, kutakuwepo na watakaoipokea, hivyo kuingia katika hatua mpya, na pia watakuwepo watakaomkataa huyo aliyesimamishwa na hivyo kubaki katika mapokeo yao! Swali linalonijia ni hili: Je, hilo kundi lililomkataa huyo aliyekuja na hilo Neno, nao kubakia katika Mapokeo yao, ule ‘wokovu’ waliokuwa nao kabla ya kumkataa huyo aliyesimamishwa na Mungu, wataendelea kuwa nao machoni pa Mungu??? Yaani unaweza kulikataa Neno la Mungu na ukabaki kuwa UMEOKOKA??
  Nisaidieni wapendwa katika hatua hii!

  Mbarikiwe nyoote!

 35. Ndugu Mabinza,

  Kwa kifupi nimekuelewa…..labda kwa vile umeeandika kwa kifupi….lakini nimepata ujumbe wako.Na nimefurahi kusikia toka kwako kuwa KUNENA KWA LUGHA SI ISHARA PEKEE YA KUWA MTU AMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU…Msimamo wangu toka awali uko wazi…Sipingi kunena kwa Lugha……..kwani nitakuwa nakwenda kinyume cha Maandiko…..na vile sikubaliani na wanaofundisha kwamba Kunena kwa lugha ni Ishara Pekee ya kumpokea Roho Mtakatifu……kwani kuamini hivyo vile vile ni kinyume cha Maandiko.
  Mkristo nikiwa na maana aliyemkubali Yesu kama Mwokozi….yaani kwa kutubu dhambi….kuukubali Msamaha wake na kujitoa kwa na kumkubali kama BWANA wa maisha yake HAWEZI KUISHI PASIPO NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU….! Na Mungu alilijua hilo…..Asingelitupa Roho Mtakatifu ni sawa na Jemadari wa majeshi kumtuma askari wake vitani pasipo kumpa silaha…..!!!Hatuwezi kuishi maisha ya kushinda dhambi……kumshuhudia Kristo……Pasipo Nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha Yetu……Hatukuupata WOKOVU huu wa thamani kwa kufanya Jambo lolote lile isipokuwa toba……Je sasa tunapata Nguvu za Roho Mtakatifu kwa Juhudi zetu…..? Mara funga na kuomba……mara tamani……mara rudia rudia maneno fulani…..mara ubatizwe na maji mengi……vitu ambavyo haviko kabisa katika Biblia…!

  Naumizwa mno na mafundisho potofu ambayo waumini wanaambia kuwa mara inabidi uwe na kiu…..ndio utapata Ujazo wa Roho Mtakatifu…..ni sawa sawa kumwambia binadamu atengeneze KIU ya maji…..Kiu inatoka ndani haiwezi kutengenezwa na binadamu….! Roho Mtakatifu anabadili maisha na mwelekeo wa Muumini mara tu anapoukubali Wokovu wa Kristo

 36. Nimependa sana mafafanuzi yako Ndugu Mabinza. Nikuombe kama inawezekana kupata baadhi ya mistari ya biblia inayoambatana na maelezo haya kwani ingesaidia sana hasa pale ibidipo kumfafanulia mtu kwa kina. Hasa kwa msisitizo kwamba “Mtu huyo habatizwi mpaka aseme mwenyewe kuwa sasa yupo Tayari kubatizwa…” na swala la kumfundisha mtu kisha umbatize…kwa nini si sawa kulingana na biblia? Ahsante sana.

 37. Mpendwa Haule,
  Uwe na amani tu Ndugu yangu hujanikwaza lolote katika kuniuliza au kunijibu kwako, ubarikiwe tu mtumishi, maana kile usemacho ndicho ukijuacho, ingawa pia mtu huweza kusema kitu ambacho hakielewi.Inawezekana katika maelezo yangu, nilikuchosha kwa maelezo mengi, mimi nimezoea kufafanua jambo kwa kirefu kila niulizwapo, nashukuru umenifundisha kuwa wengine hawapendi majibu marefu! Lakini pia wapo watu wanaweza kuuliza,lakini hawana haja ya jibu la anayeulizwa, kwa sababu; ama analijua jibu tayari au anamsimamo wake mwenyewe moyoni mwake, hivyo hataki kujua anachojua anayeulizwa, au anaijua “akili” ya anayeulizwa! Nilichotaka kukieleza kwenu wote na hasa Kwako wewe na Orbi ni mambo matatu tu, kwakifupi nilimaanisha hivi; Moja, Mtu akiamini na kufanya toba moyoni mwake anapata haki ya Kubatizwa. Pili, kwamba, Biblia haiainishi mda maalumu ambao ni wa LAZIMA kwa Mtu akiamini abatizwe, nilisema ni mda wowote tu, inategemea ,mazingira na Hali. Na tatu, kwmba,Mwenye kuamini ndiye mwenyekujua kuwa sasa ameamini na kwa hiyo ana hitaji Ubatizo. Mbatizaji hanahaki yoyote ya kumbatiza Mtu ambaye hajasema mwenyewe kuwa yupo tayari kubatizwa! Ndiyo maana nilisema kwamba, mtu anaweza kukaa kwa mda mwingi, japo akishiriki mambo mbali mbali pamoja na waliokwisha batizwa kanisani hapo,laakini yeye akiwa bado hajaamini, Mtu huyo habatizwi mpaka aseme mwenyewe kuwa sasa yupo Tayari kubatizwa ndipo inapochukuliwa kuwa mtu huyo sasa tayari ameamini! Orbi, kasema kuwa, “….Kwangu mimi sikubaliani kabisa na utaratibu wa kufungua madarasa ya kuwafundisha watu WALIOAMINI miezi miwili au mitatu ndio uwabatize……..!” Mimi sikuwa na maana hiyo hata kidogo! Kwanza, mtu hafundishwi kuamini,anafundishwa kuijua na kuielewa kweli iliyomo katika Neno, na akisha kuelewa huamini mwenyewe na akisha kuamini, ndipo hupata haki ya kubatizwa palepale(ila wakati gani abatizwe, inategemea mazingira na hali ya sehemu husika), Mtu hubatizwa tu, akishasema mwenyewe kuwa, “nibatizwe” Kukili kwake huko, ndipo kunathibitisha kuwa mtu huyo kaamini! Jingine ambalo niliweke wazi ni kwamba,Kunena kwa Lugha siyo ishara pekee kwamba, mhusika ana Roho mtakatifu, Mtu huweza kunena kwa Lugha, kwa kutegemea imani ya yake na mazingira ya uwepo wa Roho mtakatifu mahali husika! Bwana Yesu kristo, aendelee kutufundisha.

 38. Ndugu Haule,

  Ubarikiwe mno….! Huwa inachukua ufunuo na muda kutambua kwamba mafundisho mengi ambayo watu wameyapokea na kuyaamni hayamo katika wigo mzima wa maandiko…..! Biblia inaonyesha wazi watu wanaweza kuuozoea utendaji fulani wa Mungu na kujengea mafundisho bila kuangalia context nzima ya utendaji huo wa Mungu….angalia Agano la Kale kwa Israel na Sanduku la Agano….! Walidhani tu kukaa na Sanduku la Agano ndio udhirisho wa kuwa Mungu yuko kati yao….wa wakalizoea kama “charm” ya kushinda vita na kuwapigia adui zao……Angalia watoto wa Eli na Israel kwa ujumla…..walilichukua Sanduku wakajua Mungu yuko nao kama ISHARA ya Mungu iko kati yao…..! Nadhani unajua matokeo ni nini…..ya kutumia ISHARA bila kuuangalia wigo mpana wa Utendaji wa Mungu…..!

  Na ndivyo ilivyo katika hii ISHARA YA KUNENA KWA LUGHA LEO….ni kweli Mungu alihuisha utendaji wa Roho Mtakatifu kule Azusa street katika mwanzoni mwa karne hii ambayo kwa kipindi kanisa la Kristo lilikuwa limesahau sehemu hiyo muhimu…..Lakini wengi wanasahau kuwa ISHARA YA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI WAKE HAIJAFUNGWA KATIKA ISHARA MOJA YA KUNENA KWA LUGHA TU….! Maandiko yako wazi kwa hilo…..! Huhitaji kuwa nabii kuona licha ya kuiweka ISHARA HII kuwa ndio pekee ya kuonyesha uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha ya muumini umelifikisha kanisa la leo wapi….? Angalia kanisa la Tanzania ambalo ungelitegemea kuwa chumvi na na nuru linaonyesha nini…..? Huoni kabisa mabadiliko ambayo yanaonyesha waumini waMEjazwa Roho wa Mungu………Soma tena kitabu cha Wakorintho uangalie karama za Mungu zinapoondolewa katika wigo mzima wa Maneno ya Mungu……!

  Ndugu Haule itachukua muda watu kufunguka katika kifungo cha “mapokeo” hasa ambayo yamezaliwa katika madhehebu ambayo wengi wameamini yameshushwa na Mungu toka mbinguni……! Bila kutulia na kuyaangalia Maandiko kwa kuomba na tafakari kubwa……..

  Kama ni msomaji wa historia ya Ukristo utaona kila kipindi fulani Kanisa lilijenga imani yake katika KWELI fulani ya Mungu pasipo kuungalia wigo Mpana wa utendaji wa Mungu…..na Mungu kwa Neema yake huwa anawafungua watu kwa kusimamisha tena wengine Kuinena kweli ya Mungu……nadhani kwa Kanisa la Tanzania umefika wakati huo……UBARIKIWE! Naomba Mungu atutie nguvu na kutuangazia UKWELI WA MAANDIKO YAKE…….

 39. Ndugu John Haule,

  Shaloom!

  Ni kweli kuna maswali na ushauri ulionipa, ninakushukuru kwa vyote! Hata hivyo kuna maswali mengine nami natatizika katika namna ya kukujibu maana majibu yake wakati mwingine yanakuwa kama yanatoka nje ya mada kwa mtazamo wako, basi inaniwia vigumu kiasi fulani maana kwa upande wangu mambo yote ninayatazama katika kumuona Kristo. Chochote ninachokizungumzia hukiona katika jinsi hiyo. Bali nikubaliane nawe katika mtazamo huo ambao ni mzuri kiutaratibu. Basi labda niyaendee machache niliyoyaona yanayoendana na “Kunena kwa lugha” kama ulivyo yaleta.

  Kwanza, katika umbali tuliofika katika mada hii, mambo mengi yameongelewa na vifungu vingi kurejewa. Kwa hiyo, ninapoyatazama mambo haya, nayo majibu ya Biblia yakiwa wazi, labda ushauri wangu ni kuwaombeni mchukue wasaa zaidi, mkijivua nira mlizofungiwa na mafundisho tofauti tofauti, ndipo mkichunguze tena Biblia inachokifundisha, ili angalau mpate kuona tofauti zilizopo na maamuzi yenu yawe juu ya ufahamu huo.

  Kwa mfano, 1Kor 14, inafundisha vizuri sana mambo ya Kunena kwa Lugha. Sasa unapolazimisha kunena kwa lugha kwa kanisa zima kwa kisingizio chochote kile, ilimradi unajua fika kuwa kunena kwenu hakuendani na fundisho la Biblia, hilo pia ni changamoto inayoishia kwenye itikadi, na kumuaminisha yule mnayejadili naye kuwa kuna tatizo sehemu fulani!

  Katika kulitatua tatizo lolote lile ni vizuri kuukagua mwanzo wa jambo ili kubaini kama msingi wake ulikuwa sawa. Basi kwa jambo naloliona katika mjadala huu, na jinsi ambavyo fundisho lisilo la Kibiblia linavyolazimishwa kuwa hivyo, imenipa shauku ya kujikagua upya ili kubaini NJIA zetu iwapo zi sawa na Biblia.

  Swali la kwanza lililonijia ni hili: “MKRISTO NI NANI?” nimefika katika kujiuliza hivyo kutokana na hali ya kanisa ilivyo katika ujumla wake. Maana leo hii kati ya kundi hilo la kanisa, yaani wakristo, wapo waliookoka na wasiookoka!! Niliporudi katika Maandiko kulitazama hilo, nimeshindwa kuiainisha hali hiyo kikanisa, yakitenganishwa makundi. Nikarejea pale mitume walipotumwa kazini kuutafuta ule mwanzo, maelezo yake yanasema hivi:Mark 16:15-16 “… Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” hicho ndicho Maandiko yanachosema! Pia tunahakikishiwa zaidi kuhusu jambo hilo katika Yoh 5:24 “Amini, amini, nawaambia, yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, …” Kwa hiyo kiBiblia suala la WOKOVU ndilo hilo hapo. Hao ndio WAKRISTO. Hili ndilo jibu nililolipata kuhusu swali langu, pia Biblia inaniambia hivi: Rum:8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu, anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” Basi haya makundi yaliyojigawa ndani ya kundi moja yamezaliwa kutoka Injili gani??? Nisaidieni wapendwa!

  Pia nilipokuja katika suala la kujazwa Roho Mt., kwa kanisa kama lilivyo katika Biblia jambo hilo liko wazi na halina mushkeli. Lakini ninapolitazama kundi hili lililopo lililojigawanya, nimeshindwa kulielewa maana ninaziona namna zaidi ya moja za kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa mfano, kati ya wanaokiri wokovu wapo wanaoamini kuwa ukinena kwa Lugha, Umejazwa Roho Mt. kundi jingine unajazwa ulipoamini, kundi jingine unajazwa Roho Mt unapopokea Kipaimara, na wengine kwa kupigwa kibao chepesi na Askofu katika kipaimara nk. Makundi yote haya YANAAMINI KUWA YAMEJAZWA ROHO MTAKATIFU!!!

  Basi ndugu yangu Haule nimefika katika hali hii ya kutatizika baada ya kuona mwelekeo jasiri wa mada ukiyavuka Maandiko na kuyafanya hadithi na kuendelea na itikadi zetu, ndipo imenibidi niyaangalie makundi yetu ili kuona kama yana uwiano wowote na lile kundi katika Biblia. Kuna similarities, nahisi hizo ndizo zinazoleta shida katika uelewa wetu!!!

  Nasubiri tafakari yako!!!

  Bwana akupe nguvu!

 40. Wapendwa wana SG
  Nikali na mengi ya kuwashirikisha katika tafakari zangu,kutokana na yaliyojiri kwenye hii thread wakati tunaitafakari,maandiko kutokana na habari ya kunena kwa lugha,Nimefungukiwa na maswali mengi kutoka yale walio yaandika wapendwa hapa,nimepata ufahamu kuwa vitu vingi hatuvifahamu ingawa twadhani twavifahamu,ebu basi tuache kuoneshana kwamba sisi ni weledi wa maandiko kwa kujihesabia haki kwa haki yetu wenyewe Tujichushe,tuchunguze maandiko kwa kina na mapana namarefu,tukiachilia fikra zetu ili Roho Mtakatifu atufunulie/atuongoze/atufundishe tupate ufahamu wa kuelewa maandiko
  na tufike pahala dhamiri zetu zibadilike kama zinatushitaki tuombe rehema,kama dhamiri zetu hazitushitaki tuwe na ujasiri zaidi wa kuendelea kushindania imani na kuvipiga vile vita vizuri,Bwana akinipa kibali nitaweka vitu kama vitatu tuvitafakari, vinavyohusiana na hii mada lakini tukiingia ndani zaidi

  Ninawaomba tuachilie ufahamu/wamazo/fikra/mitazamo/misimamo yetu ya kihema/madhehebu.il Bwana kupitia Roho wake aseme nasi.

  Amen

 41. Mpendwa ndg Mabinza,Nadhani wewe ujalielewa swali langu,hata sasa ujalielewa.Mimi nimekuelewa ulitoa maeeleza marefu,badala ya kujibu swali,ulitakiwa ujibu siku niliyompekea Bwana nilipatizwa siku hiyo au siku niliyompekea Bwana sikubatizwa siku hiyo nilibatizwa siku nyingine,ndilo nilitegemea kutoka kwako, maelezo haya uliyoandika ni tafakari yako, vema,.Samahani kwa kukutumia wewe ktk tafakari yangu ya kuchunguza maandiko ktk kanisa la leo nimekukwaza unisamehe. tunapotafari maandiko ,tusishukiane kwamba tuko hapa kupingana tu au tu weledi wa maandiko au ndio kwanza tunajifunza maandiko tuanze kufunzana ABC za maandiko,Nadhani tunajitambua ndio maana atuchangii kila thread,Mabinza nitakuwa niko chini kama kila utachoandika nibishe tu kwa kuwa kuna maandiko fulani hatukubaliani

  Asante

 42. Mabinza,

  Nadhani ulisoma kwa kurashia rashia maandiko yangu, kwani swala la muda ulilomalizia post yako ndio nililo lizingumzia….! Je Biblia imetaja muda gani mtu akae baadaya ya kuamini ndio abatizwe…? Iko Kimya….! Haijasema muda bali imeonyesha tu ni tendo linalofanyika Mara moja baada ya mtu kuamini……! Mifano mingi iko katika Matendo ya Mitume…….angalia wale elfu tatu na wale elfu tano…..angalia tena Philipo kwa yule Mkushi……angalia Paulo kwa askari wa Kirumi…..ambao ubatizo ulifanyika usiku wa manane na familia yake yote….!Maana ilibidi mlinzi arudi lindoni na Paulo usiku huo huo……..Hivyo Biblia haijasema muda gani uchukuliwe ili mtu abatizwe….au aelewe nini……..kuilewa Injili na kuikubali tu kunatosha kabisa kuwa candidate wa kubatizwa….! Sio muda…….wala mafundisho….!

  Kwa mtazamo nao uona katika Biblia huhitaji mafundisho ili ubatizwe….unahitaji kubatizwa baada ya kuamini…..na mafundisho ya kuijua na kuikulia imani yanafanyika katika maisha yote ya mwamini atakapokuwepo duniani….! Hatutaacha kujifunza mambo ya Mungu…..wala hakuna siku tutasema tumeifahamu kweli yote….sasa imetosha…..! Kila siku kuna ufunuo wa kweli ya Mungu katika maisha yetu….Kwangu mimi sikubaliani kabisa na utaratibu wa kufungua madarasa ya kuwafundisha watu WALIOAMINI miezi miwili au mitatu ndio uwabatize……..! Najua labda inafanyika hivyo kwa baadhi ya waumini walikua tayari wamebatizwa kabla hawajaamni ….Labda hapo inabidi kuchukua muda kutoa somo hilo…….hata hapo sasa inabakia kumwachia Mungu afanye mwenye conviction ndani ya mtu huyo….!Lakini lazima nitoe tu tahadhari……..kumbuka kwamba katika Agano Jipya hasa katika kitabu cha Matendo ya mitume watu walifahamu maana ya ubatizo…..wengi waliufahamu ubatizo wa Yohana….hivyo walijua toba walioifanya iliambatana na ubatizo………… Kwani ubatizo unabakia kuwa ni Ishara ya nje kwa kile kilichofanyika ndani ya Muumini…..yaani kufa katika maisha ya dhambi….na kufufuka upya katika maisha ya Kiroho…na kuenenda na Kristo katika upya wa uzima……!

 43. Mabinza,

  Sina la kuchangia kwa sasa……lakini naona umenikuu vibaya……sijatenga kubatizwa na kuamini……!!! naona umetoa maana ambayo haikuwepo katika maandishi yangu…..!

 44. Mpendwa Haule,
  Nimefurahi kwakuwa ulipitia kile nilichotoa kwako kama jibu la ulizo lako, katika swali lako kwangu, ulitaka kujua iwapo nilipompokea Yesu nilibatizwa siku iyo hiyo. Nasikitika kwamba, hukunielewa hata kidogo! Labda niseme kwamba, kwangu mimi Siku niliyobatizwa ndiyo siku iyo hiyo NILIYOMUAMINI Bwana Yesu kristo! Najua utashangaa,maana utaona kama nayaruka maelezo yangu,kumbe wewe ndiye huelewi kwamba, unaposaini makubaliano yoyote ndiyo siku inayotambulika kuwa, hiyo ndiyo siku ya makubaliano na si nyingineyo. Hata kama jambo husika lilipitishwa katika akili na mawazo ya wahusika mapema kabla! na kwa Bahati mbaya si Wewe tu ila kuna wengine wengi, hudhani kwamba siku ile watu wanapo kubali kufuata Dini, ndiyo siku hiyo WAMEMWAMINI YESU, jambo ambalo si kweli.Yesu kuna mahali alisema watu hawa hawanifuati kwa sababu ya lile Neno, ila kwa sababu walikula mikate! Kuna mambo mawili makuu katika safari ya wokovu; Moja ni KUMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO. Hapo ninamaana mtu anasikizishwa Neno kwanza – INJILI ya Bwana Yesu kristo,Neno likisha kaa moyoni mwa mhusika ndipo KUAMINI kunakuja! Kuamini huko hakujalishi kunachukua muda gani umekuwa ukihubiriwa au mda gani tangu uhubiliwe, ila siku unapoamini ndiyo siku mhimu na ndiyo tangu hapo unapata haki ya kubatitwa, na kubatizwa huko hakujalishi ni saa iyo hiyo, kesho, kesho kutwa nk! Katika Mk. 16:15, Yesu anawambia wanafunzi wakahubiri na atakayeamini wambatize. Na katika Rum.10:17 inasema,imani chanzo chake ni kusikia maneno ya Kristo. Kinachowachanganya watu wengi wanadhani kwamba, kwakuwa Biblia inasema mtu akiamini abatizwe, basi ni lazima IWE NI DAKIKA IYO HIYO AU SIKU LAZIMA IWE IYO HIYO,IWE LEOLEO, SAA IYO HIYO, Kumbe, Neno linasema,ukiamini UBATIZWE – saa ngapi, lini na au wakati gani, Biblia imenyamaza! Orbi, ametaja habari ya Filipo na ya Mkushi, lakini hakujua kwamba kubatizwa kunakubalika tu Mtu akiamini, hilo ndilo JAMBO MHIMU, wakati gani Muumni abatizwe kutategemea Mazingra, Wakati au Hali ya sehemu husika! Tatizo la watu wengi, hudhani kuwa kila anayekwenda Porini ni Mwindaji! Watu wanaweza kujaa katika mkutano Fulani wa Injili, kisha wahudumu wa Mkutano huo huwaorothesha watu wote WALIOKILI KUMPOKEA KRISTO, na ukiwauliza wahudumu hao watakwambia hao tayari WAMEAMINI! kumbe pale kinachofanyika kwa watu wengi ni kukili wokovu kwa vinywa vyao tu, na si kwasababu wameliamini Neno la Kristo kwa moyo! kulikubali neno la kristo tu, bila kuliamini Neno lenyewe, ni sawa na hakuna! Na kwa bahati mbaya sana,viongozi wa Dini wamejaza waumini ambao wengi wamebatizwa kwa kulikubali tu Neno bila kwakweli kulielewa ipasavyo hata kuliamini kwa Moyo, ukisoma kwa makini Mdo 17:10-12,ndipo utaelewa,kwanini mimi nilikuwa MBISHI JUU YA ULOKOLE! Amini usiamini inapotokea mtu akalielewa neno huanza kuonekana mzigo na chanzo cha migogoro huko makanisani; Mtu anaweza kuuliza; Inawezekanaje kukubali Neno lakini usiliamini? katika hiyo Mdo 1710-12. Niliyoinukuu, watu wale wa BEROYA, Biblia inasema walilipokea Neno kwa unyofu wa moyo, kwa maana hiyo walikubali, lakini kile kitendo cha kuwa na udadisi na kutaka waachwe kwanza wayachunguze yasemwayo na Mitume, ilikua hawaamini juu ya ukweli uliokuwa ukifundishwa kwao na mitume. Lakini Neno linaendelea mwishoni mwa mstari wa 12 kuwa baadaye waliliamini Neno. Hivyo, kujua jambo si sawa na kulielewa jambo husika, na kama ukaamini kitu usicho kijua, kuamini huko ni batili! Nikodemu pamoja na Elimu yake kubwa na akiwa mwenye uzoefu mkubwa katika Mambo na elimu ya Dini, alijua kuzaliwa ni lazima Mtu atoke tumboni mwa mama yake tu, lakini Yesu alimfahamisha kuwa kuzaliwa kwa Mtu kupo kwa aina mbili, moja ni kuzaliwa kimwili na pili ni kuzaliwa kiroho! Kukubali au kukili jambo ni tendo la mwili, maana hufanywa kwa kinywa na hivyo ni tendo la sheria. Bali, kuamini ni tendo la Rohoni kwa hiyo kuamini si tendo la Sheria! Inapotokea mtu kalikubali Neno la Kristo, na wakati huohuo akaamini, Mtu huyo huwa na haki ya kubatizwa ina weza kuwa siku iyo hiyo kama mazingira yanatoa nafasi hiyo. Watu wengi hufuata ishara na matendo ya miujiza au msisimko na ama ushawishi fulani, kama kuombewa mafanikio au kupata utatuzi wa shida fulani ya kimwili. Mtu wa aina hiyo hata akidumu kanisani kwa miaka mia, utashangaa nikikuambia kuwa anapaswa kufundishwa na kujengwa kiroho ili aamini Neno la Mungu, kuwa Yesu hakuja kwa miujiza tu, bali kuokoa kilichopotea – hivyo AMINI uokolewe, ikitokea akaamini basi, ABATIZWE! Katika Ebr.11:6, insema, Mtu akimwendea Mungu, lazima aamini kuwa Yeye yupo. Je, Biblia imetaja mda maalumu wa MTU KUBATIZWA akisha amini? Nitafurahi kuwasikia ndg. Zangu, Haule na Orbi na ama mwingine Yeyote.

 45. John Haule, asante mno kwa mchango wako…..

  Tatizo la wengi wanafundisha na “personal experience” zao na kutumia maandiko kuzithibitisha……hali hii ni hatari mno kujengea mafundisho….!…..Neno la Mungu ndio Muhimili Mkuu wa Imani na sio personal experiences zetu…..Kama unakwenda sambamba na Biblia Mtu akimpokea Yesu anaweza kubatizwa hapo hapo…..hiyo ndio iliyokuwa pattern ya kitabu cha Matendo ya Mitume……!Angalia Paulo na yule mfungwa gerezani usiku…….! Angalia Philipo na yule Mkushi…… Haya mafundisho ya kusema upate mafundisho kwanza ndio ubatizwe…….na kwa wengine unene kwa lugha ni utaratibu wa madhehebu tu…! Ukiamini tu wewe ni mufuasi wa Kristo…..na unastahili kubatizwa pale pale…..na kuanza kujifunza fundisho la mitume na kuumega mkate pamoja na waumini wenzako… Wakristo wengi leo wanashindwa kutofautisha areas of personal conviction and areas of command……!

  Na kwa upande wangu naona wengi wameshindwa kabisa kuona utendaji Wa Roho Mtakatifu na jinsi anavyojidhirisha kwa Muumini (Diversity of experiences) Na ndio maana wengi wamefungwa katika mafundisho kwamba ISHARA PEKEE YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NI KUNENA KWA LUGHA TU! Kinyume kabisa na maandiko….! Kinyume kabisa na Petro alivyothibitisha kwa kutumia Yoel 2:28-32…..Kumfunga Roho Mtakatifu kwa dalili moja tu kwa mtazamo ni kumtweza….! Roho wa Mungu mwenye uwezo Mkuu hawezi kufungwa katika dalili ya Kunena tu…..! Ni mkuu Mno anajidhirisha kwa njia mbali mbali mno…..na atafanya hivyo…..!Hebu tumwachie afanye kama atakavyo Mwenyewe…!

 46. Asante Mabinza
  nashukuru pamoja na kunijibu kwa urefu nilitaka kujua siku ile uliyoipata wokovu kama ulibatizwa siku hiyo,, nilipiopitia kwa uchache post yako ya j’mosi,kuna kitu wakati nasoma maandiko yako, nilikiona ambacho kila siku huwa nakitafakari, nachotaka kutafari nanyi ni hii kwenye biblia wate waliomini(waliompekea Kristo) walibatizwa siku hiyo,lakini naona kanisa la leo unamini(TUBU LEO) lakini haubatizwi siku hiyo inachukua muda,toka pale tulipobadilii mtazamo(kuokoka)na kubatizwa . Tafakari yangu hivi tunavyoenenda leo ni sawa,naomba elimu hapo

  Mbarikiwe

 47. Mpwendwa Haule,
  1. Asante kwa swali lako la tarehe,Monday, April 23, 2012 at 2:48pm.
  Mimi nilikuwa “mbishi” kidogo katika swala la KUOKOKA, nilikuwa M- ROMA MZURI! Kilichonifanya niokoke, ni udadisi wa kutaka kujua njia njema ya kumwabudu Mungu,nilifatilia maisha ya “walokole” nikashangazwa sana na vitu vitatu walivyokuwa navyo; Cha kwanza, walikuwa wakalimu sana, wanatembeleana na wachungaji wao walikuwa “Simple!” Cha pili, walikuwa ni watu wenye furaha mda wote na wenye kusaidiana, na kila jambo walilisema kwa ujasili, na walikuwa wanajiamini na hawakuwa na hofu ya kifo hata kidogo! Cha tatu,walikuwa wanajua kusoma Biblia na kuvielezea vifungu vyake vyote kwa ufasaha! Mimi pomoja na kutekeleza sakramenti zote,zilizokuwa zikinihusu wakati ule, nilikuwa sina ujuzi wowote wakuisoma Biblia na sikuwa na hata kimoja katika vile vitatu walivyokuwa navyo walokole wa wakati huo, kama nilivyokutajia hapo juu! Wakati nikimalizia masomo yangu pale Dodoma, Mzee Moses kulola pamoja na mahubiri yake ambayo yalinifanya nianze kutambua kuwa ninahaja ya kuokoka, mnishi alipigilia msumali wa ajabu alipoimba wimbo wa “Malebo” nikamua kununua Biblia katika mkutano ule na baada ya kama miaka miwili baadaye 1985 nikidumu nao katika maombi na mafundisho, nilitumbukizwa katika Bwawa refu la kubatizia, Mchungaji Samsoni mkuyu, wa Pale Miyuji,akanizamisha na kunibatiza. Baada ya siku mbili hivi, bila hata kuombewa nilijazwa Roho mtakatifu na kunena saaana kwa Lugha,kama nusu saa hivi, baada ya hapo nikawa mtu mwenyefuraha ya jabu mwenye kunena kwa Lugha kila niingiapo katika maombi na nisiyebabaika hadi leo!- Pale Miyuji,ambapo kuna Chuo cha Biblia cha TAG (hadi leo nadhani) na ambako pia ndipo kulikuwa na Kanisa la TAG (kabla ya kumegeka) Nilitiwa moyo mara zote na kujengwa kiimani na Mchungaji wangu mzee Mkuyu pamoja na wazee wa kanisa, nilifundishwa mambo mengi ya kuukulia wokovu, na kufunuliwa na Mungu mwenyezi mambo mengi, Mungu anaendelea kunifundisha kwa uvumilivu mkubwa akifanya miujiza na maajabu mengi tu hadi sasa, na kunielemisha kwa namna ya ajabu. Kwakweli, sishangazwi sana na matendo hayo makuu ya Mungu, maana nilikuja kujua kuwa yeye SI WAKAWAIDA, HIVYO NA MAMBO YAKE SI YAKAWAIDA VILEVILE! Naomba niishie hapo, kama sijakujibu ipasavyo mimi ni mtu wazi na sichoki kuulizwa, uliza tu kama ipo haja! Endelea kubarikiwa na BWANA YESU KRISTO.

 48. 1…“ Mimi sipingi kunena kwa lugha”.
  Amina….Sam unanena kwa lugha?
  2…” Unajua kunena kokote kule, haswa kwa mtu mzima, huwakilisha mawasiliano, yaani kupitisha ujumbe. Nayo mawasiliano hufanywa katika lugha. Kwa hiyo hata mtu anaponena kwa lugha katika kuwasiliana na Mungu, ujumbe hupeanwa kati yao, na kwa vile hilo ni kati ya Mungu na mnenaji, nao unenaji ukiwa chini ya mnenaji, tumefundishwa kutafuta faragha inapokuwa hivyo. Lakini ikiwa ni katika kusanyiko basi awepo mtafsiri, yaani hilo ni kati ya waaminio”

  kwahiyo nikiwa kwenye kusanyiko nikinena kwa lugha nitafute mfasiri!!au nitafute faragha!!Sam kunena kwa lugha ni kwa ajili ya kuijenga nafsi yangu sio kanisa, “maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.’.haiwezekani kuwapangia watu wakitaka kunena kwa lugha watafute faragha hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu yeye anakuona upo wapi,kwenye kusanyiko/nyumbani nk hatumpangii.
  3..“na kama ni kati ya wasioamini Roho Mtakatifu huwepo kwa ajili hiyo, yaani kila aliyepo hapo humsikia mnenaji kwa lugha yake. Katika yote hayo, uwe kwenye faragha yako au kusanyikoni au kati ya wasioamini; mnenaji na mtafsiri ni yeye yule yule Roho Mt.”
  Amen….

  4…’Ila kusanyiko zima, la watu 3000, linapolipuka kila mmoja akinena kwa lugha kivyake,”
  Ni uweza wa BWANA, inapotokea hivyo mara nyingi kama sio zote waamini wanakuwa wako ktk maombi binafsi/kanisa(wanasemezana)mtu binafsi na Bwana,pia wakti huu inatokea wakati mwingine kwa Manabii wanafunuliwa kama kuna kitu Roho Mt anataka kusema na Kanisa mmoja wao sauti yake itanapanda kuliko wengine na atanena unabii kwa lugha ya kueleweka,kama atanena kwa lugha itatafsiriwa.kabla au baada ya hapo mhutubu(mahubiri)yatafuatia.na kama kuna m siri za mioyo zinawekwa wazi a,haya yanafanyika kwa uzuri na utaratibu,Msisitizo wa Paul ni Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

  5….. “au muhubiri anapochomeka lugha, “Rabbabashani, akasandraaa,…!”

  Nakubaliana nawe mazingaombwe yapo,hayapunguzi uwepo wa kweli wa wanaonena kwa lugha kama moja ya ishara au karama ya kumpokea/kujazwa Roho Mtakatifu.

  6… “Pia nami nikikufuatisha wewe,
  Ndugu mpendwa wangu hatubishani/kushindana.. tunatafakari
  7.”nikaingojea Biblia itakaposema, “Kunena kwa Lugha ni Ishara ya kujazwa Roho Mt.”; naona imeendelea kukaa kimya hadi leo hii ninapoiandika posti hii, tokea mpendwa Cuthbert alipolileta jambo hili. Lakini kama yule mwanamke Mkananayo, naendelea kung’ang’ania kusubiri iseme!”
  Amen…Ipo siku Bwana Yesu atakufungua macho ya rohoni na (kukutia nuru)kukufunulia ili upate kuyaelewa yale maandiko anayokufunulia kupitia Wajoli wako hapa.ili upate ufahamu kuwa Kunena kwa Lugha ni moja kati ya zile ishara tano(5)za kujazwa Roho Mtakatifu(marko16)

  Asante kwa tafakari.

 49. Asante
  Mabinza kwa tafakari yako,nipe muda wa kupitia maandiko yako ,ila kwa sasa ningependa kukuuliza swali binafsi siku uliyomkabidhi Bwana Yesu maishayako(kuookoka)ulibatizwa siku hiyo au la,kuna kitu natafakari /nakichunguza ktk huu wokovu wetu,jibu lako litanisaidia si kujibu post yako tu na kujitazama mimi pia
  Asante

  Nitarejea kwako ….

 50. Asheri,

  Nasubiri ushuhuda wa Robert…..kabla hatujarudi kwenye Maandiko…..nataka really experience yake………!

 51. Shalomu,

  Ndugu Robert,

  Mungu akubariki kuwa unajifunza kitu katika mjadala huu, heshima, adhama na utukufu ni kwa Mungu anayestahili!

  Ndugu Orbi,
  Pamoja na kuwa bado natamani kukaa pembeni na kuona wengine wanachangia mada hii, nimeona nichangie hapa kutokana na mchango wako kwa Ndugu Robert. Nilipousoma mchango wako kuwa unamhurumia ndugu Robert na kuwa unamsikitikia nilifarijika nikiamini kuwa utachukua hatua ya kumuombea ndugu Robert ili Mungu ampe haja ya moyo wake. Hata hivyo nikashangaa baada ya kuona jinsi ulivyoendelea kuchangia, ndipo nikaona nami nitoe mchango wangu kwa lengo la kujaribu kuweka sawa baadhi ya yaliyojitokeza katika mchango wako.

  Naomba nianze kwa kujiuliza swali hili, Je wanafunzi wa Yesu waliokoka wakati gani? Waliookoka siku walipompokea Roho Mtakatifu (Matendo 2) au kabla ya hapo? Mimi naamini kuwa Wanafunzi wa Yesu waliokoka hata kabla Yesu hajapaa kwenda mbinguni, lakini walisubiri mpaka siku ya Pentekoste ndipo walipompokea Roho Mtakatifu. Nimeandika hili kutokana na maelezo yako kuwa hujawahi kumuona mtu aliyeokoka ambaye hajajazwa na Roho Mtakatifu. Kwa ufahamu wangu, wanafunzi wa Yesu walikaa kipindi fulani wakiwa wameokoka lakini hawajajazwa Roho Mtakatifu.

  Ukisoma katika Matendo 1:15-26 tunawaona Wanafunzi na wale waliokuwa nao ghorofani wakimchagua mrithi wa Yuda Iskariote. Petro anatoa sifa za mtu wa kumchagua, lakini hakuweka kipengere cha kuwa awe amejazwa na Roho Mtakatifu, sidhani ni kwa makosa, bali naamini ni kwasababu Roho alikuwa hajaja bado. Lakini katika Matendo 6:1-6 wanafunzi waliliomba kanisa lichague watu watakaolihudumia kanisa ambapo moja na sifa wa watu wa kuchaguliwa ilikuwa wawe wamejawa na Roho. Naamini ilifanyika hivi kwa kuwa katika uchaguzi huu wa pili, wanafunzi walikuwa tayari wamejazwa Roho Mtakatifu.

  Katika Matendo 19:1-7, tunamwona Paulo akiwauliza watu wa Efeso kuwa Je mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? nao wakajibu kuwa La, hata kusikia kuwa kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Mimi naamini kuwa Paulo hakukosea kuuliza swali hilo, wala Paulo asingeuliza swali hilo kama kusingekuwa na uwezekano wa mtu kuokoka akawa hajajazwa Roho Mtakatifu. Kitu kingine, hatuoni akiwafundisha kuwa haiwezekani uokoke bila kujazwa Roho Mtakatifu, bali aliwafundisha, akawaombea nao wakampokea Roho Mtakatifu. Hatujui hawa wapendwa wa Efeso walikaa kwa muda gani toka waokoke mpaka siku Paulo alipowaendea na kuwaambia habari za Roho Mtakatifu na hatimaye wakajazwa.

  Mimi naamini kuwa watu wa Efeso hawakumpokea Roho Mtakatifu walipoamini kwa kuwa hawakufundishwa habaria za Roho Mtakatifu kama wenyewe walivyomwambia Paulo. Hali hii ninaamini inatokana na mtu aliyewafundisha habari za Yesu ambaye ni Apolo (Matendo 18:24-28) inayosema wazi kuwa Apolo alikuwa hodari katika maandiko na alikuwa akifundisha kwa uhakika habari za Yesu, lakini aliujua ubatizo wa Yohana tu, kitu kilichofanya Prisila na Akila wamchukue Apolo na kumfundisha zaidi!

  Siku za leo, wapo watu wengi waliookoka lakini hajampokea Roho Mtakatifu na mojawapo wa sababu za kutokupokea ni kutokufundishwa habari za Roho Mtakatifu. Hivyo hatua ya Ndugu Robert kutambua kuwa hajampokea Roho Mtakatifu ni hatua nzuri kwa kuwa inamfanya achukue hatua kama watu wa Efeso walivyochukua hatua baada ya kufundishwa na Paulo.

  Suala lingine uliloonyesha kumshangaa ndugu Robert ni hatua yake ya kumuomba Mungu amjaze kwa Roho Mtakatifu, hivi ulitaka afanye nini? Kama mtu amejitambua kuwa hajajazwa kwanini asiombe ili ajazwe. Katika Luka 11:13, pamoja na mengine Yesu aliuliza akisema kuwa Je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? Sasa Ndugu Robert anakosa gani kumuomba Mungu katika hili hata wewe umhurumia na kumsikitikia?

  Kitu kingine ulichokisema ni kuwa watu waliojazwa Roho Mtakatifu katika Matendo ya Mitume inaonyesha hawakutamani na kuomba kwa maombi mengi ili wajazwe Roho Mtakatifu? sina uhakika kama hiki unachokisema ni kweli. Nasema hivyo kwasababu tukiangalia wale 120 waliokuwa wa kwanza kumpokea Roho Mtakatifu (Matendo 1:14) inasema kuwa walidumu kwa moyo mmoja katika kusali. Ni kweli Biblia haijasema walikuwa wakisali nini, hivyo inawezekana kuwa katika sala zao walikuwa wakiomba pia habari za Roho Mtakatifu. Mini naamini walikuwa wakiomba pia habari ya Roho Mtakatifu kutokana na sababu tutakazoziona hapa chini.

  Umesema kuwa inaonyesha hawakutamani kujazwa kwa Roho Mtakatifu, hebu thibitisha hilo. Ila mimi naamini kuwa watu hawa walikuwa na hamu ya kumpokea Roho Mtakatifu kwasababu nyingi . Kwanza Yesu aliwaambia wasiondoke Yerusalemu bali waingoje ahadi Baba (Matendo 1:4), hivyo walikuwa katika kungoja, je mtu anayengoja hawi na hami ya hicho anachokingoja? (Soma pia Luka 24:49)

  Katika Matendo 1: 6-8, wanafunzi walimuuliza Yesu maswali naye akawajibu kuwa watapokea nguvu akishakuwajilia juu yao Roho Mtakatifu, je katika hali hii, unaamini kuwa hawakuwa na hamu?, mimi naamini walikuwa na hamu ya kumpokea huyo Roho Mtakatifu ili waweze kupata nguvu. Naomba tukumbuke kuwa katika Yohana sura ya 14 – 16, Yesu aliwafundisha sana wanafunzi kuhusu Roho Mtakatifu ambapo aliwaambia kuwa yawafaa wanafunzi Yeye Yesu aondoke ili Roho Mtakatifu aje (Yohana 16:7), hivyo mimi naamini hata kama ungekuwa ni wewe Orbi ungekuwa na hamu ya kumpokea huyo Roho Mtakatifu. Aidha, kwa kuwa Wanafunzi walikuwa na Yesu aliposema kuwa MTU AKIONA KIU NA AJE KWAKWE ANYWE (Yohana 7:37) ambapo Biblia imesema wazi kuwa Yesu alikuwa akizungumza habari za Roho Mtakatifu ambaye WAMWAMINIO watampokea baadaye. Kutokana na fundisho hili la Yesu, mimi ninalazimika kuamini kuwa Wanafunzi wa Yesu na wale wengine waliokuwepo pale ghorofani walikuwa na hamu ya kumupokea Roho Mtakatifu. Aidha, kwa kuwa walikuwa na hamu, naamini pia kuwa walikuwa wakimuomba Baba kuhusu suala hili.

  Kwako ndugu Robert,
  Naomba usikate tamaa, lakini lazima ufahamu kuwa ni watu waliokoka ndiyo wenye haki ya kumpokea Roho Mtakatifu, kama tulivyoona kwenye Yohana 7:37 na Matendo 2:38. Vilevile, inahitaji mtu kuwa na kiu ya kumpokea Roho Mtakatifu, kiu itakufanya uchukue hatua ya kuomba naye Mungu ameahidi katika Luka 11: 13 kuwa hataacha kuwapa Roho Mtakatifu wale wamwombao. Aidha, unaweza kumtafuta mtu aliyejazwa na Roho Mtakatifu ili uombe naye na anaweza kukuombea kama alivyofanya Paulo katika Matendo 19:1-6.

  Mungu awabariki!

  Shalomu

 52. Mpendwa Robert,

  Ni jambo jema kwamba katika mjadala huu umebarikiwa.
  Nimejaribu kuvisoma hivyo vifungu ulivyovitaja, lakini sijaona sehemu yoyote ile iliyosema kama unavyojaribu kutuaminisha kuwa : ‘KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NI LAZIMA NA KUNENA KWA LUGHA LUGHA NI LAZIMA’; ninakushauri, jaribu kuyasikiliza Maandiko yanachosema. Unapozisikiliza hisia zako na kujiaminisha hata unaongeza maneno yako juu ya kile Mungu alichosema, ni hatari ambayo haina ulazima wa kuiingia!

  Katika shauku yako ya kujazwa Roho Mt. na Kunena kwa lugha, ni kiu nzuri ambayo yatupasa wakristo wote tuwe nayo, nakupongeza kwa hilo na kukuombea Mungu akutazame katika hilo nikiamini kuwa kwa vifungu ulivyovinukuu, wajibu wako unaujua kulingana na vigezo alivyoviweka Mungu mwenyewe na si itikadi!

  Kuhusu wachanga, nadhani mijadala nao itawasidia kama ilivyokusaidia wewe iwapo wataukimbia uvivu na kuyasoma Maandiko kuliko kujazwa itikadi maana ni vizuri kufahamu kuwa Mungu atatuhukumu kwa Neno lake na si Itikadi zetu, hata ziwe nzuri vipi!!!

  Ubarikiwe!

 53. Robert,

  Nimehuzunishwa na kuwa na huruma nyingi na post yako……..labda niombe ushuhuda wako wa kuishi maisha ya kumfuata Yesu pasipo kujazwa Roho Mtakatifu….! Maana kwangu mimi ndio itakuwa mara ya kwanza kusikia Mkristo (aliyeokolewa) anaweza kuishi maisha ya Kikristo pasipo Nguvu za Roho Mtakatifu……Na kinachoniumiza zaidi ni nipale uliposema …..”lakini natamani sana kujazwa na ni moja ya maombi yangu kwa Bwana Yesu naamini ipo siku nitajazwa ……” Kwa hiyo huyo Bwana Yesu ameweza kufanya Tendo la Kuu la kukuokoa ambalo labda hukulipata kwa kufunga na kuomba……na labda ulifanya sala ya toba kwa lugha ya kawaida tu ambayo shetani anasikia……na akakubali uwe mwanawe….ukawa kiumbe Kipya…..akakutoa katika nguvu za giza na kukuingiza katika ufalme wa Mungu…….na Biblia hiyo hiyo inasema unalindwa na nguvu za Mungu……na Uhai wako toka ulipookoka uko mikononi mwake…..! Inakuwaje Leo unatamani sana tena kwa Maombi akujaze nguvu za Roho Mtakatifu anashindwa kukufanyia Jambo hilo……? Mbona kwangu mimi nakuwa huyu Mungu anakuwa dhalimu kinyume na maneno yake…..? Mbona hata waliojazwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume inaonyesha hawakutamani na kuomba kwa maombi mengi ili wajazwe Roho Mtakatifu….?

  Kwa kifupi ndugu yangu naomba tu ushuhuda wako…..labda litakuwa somo kubwa kwangu….!

 54. Mpendwa Haule,
  1. Sasa, nimekuelewa, nazungumzia post yako ya Saturday,april14,2012 at 12:46pm
  Lo!, sawa, lakini ulichosema kwa “Sehemu” ni kweli na kwa upande mwingine umechanganya mambo mawili yanayokaribu saana kwa maana zake! KUJAZWA ROHO MTAKATIFU na KUWA NA ROHO MTAKATIFU! Labda tujiulize yafuatayo; Je, kujazwa Roho mtakatifu ndiyo Kuwa na Roho mtakatifu? Wale watu katika Mdo 10:44,kilichowatokea ni nini hasa – walipojazwa Roho mtakatifu na kunena kwa Lugha ndiyo kusema walikuwa wamekwisha mpokea Roho mtakatifu na kuanzia hapo wakampata? Labda,Mwisho kabisa, tujiulize; Kama ipo tofauti; Basi, ni nini kigezo cha mtu kujazwa Roho mtakatifu na ni kipi kigezo cha mtu kuwa na Roho mtakatifu?! Marko 16:17-18, inasema; “ Na ishara hizi zita fuatana na waaminio kwa jina langu watatoa pepo, watanena kwa Lugha mpya……….” Hapo, tumeona kuwa Mtu AKIAMINI atapata kibali kwa Yesu kristo ambaye pia ndiye Roho mtakatifu, kupata matendo ya miujiza na kunena kwa Lugha, bila hata ya KUBATIZWA kwanza! Na katika Mdo 10 kuanzia mstari wa 44 hadi 46, tunaona pia watu wakijazwa Roho mtakatifu bila ya kubatizwa kwanza! Kwa mjibu wa sura hizi mbili, ya Marko 16 na ile ya Mdo 10, tunajifunza kwamba, ukiamini utaweza kujazwa Roho mtakatifu, bila hata ya kubatizwa kwanza! Basi, kumbe kigezo cha kujazwa Roho mtakatifu ni KUAMINI. Lakini, hapa ni lazima kujua kwamba Pamoja na Mtu kuamini ni lazima awe katika mazingira ambayo yana ruhusu Roho mtakatifu kuja.Katika Mdo 10 :47-48, utaona vitu vinabadilika, Petro anasema watu wale wanaweza pia kubatizwa kwakuwa wamejazwa Roho mtakatifu KAMA akina Petro, kwanini? Kwasababu WALIAMINI kumbe ukiamini, unaweza kubatizwa,kwa nini? kwasababu kuamini kunaambatana na toba! Kwa makini utaona hapo kwamba, JAMBO MHIMU LILIKUWA KUBATIZWA! Ndiyo maana Petro alisisitiza Ufanywe ubatizo,kwakuwa katika kubatizwa Mtu hufanya toba, na watu wale tayari, WALIKWISHAAMINI, Na huko kuamini ndiko pia kuliwafanya wajazwe Roho mtakatifu – tendo ambalo lilimhakikishia Petro kuwa, watu hao walikuwa wamemwamini Yesu kristo na hivyo wanayotoba ya kweli kwa Yesu kama wao (akina Petro) Hivyo, iliwapasa kutekeleza agizo la Bwana wao Yesu kristo,maana aliagiza kuwa; Atakaye amini abatizwe! Hapa tunazidi kujifunza kwamba – KUBATIZWA ndiyo wokovu, na si kujazwa Roho mtakatifu! Ukisoma; Marko 16:16, inasema “……….,akiamini na kubatizwa ataokolewa” na siyo “…….,akiamini na kujazwa Roho mtakatifu, ataokolewa” Hapana! Ingawa kujazwa Roho mtakatifu kunategemea pia imani yako kama kulivyo kubatizwa, lakini, wokovu wako unaanza kukuingia ukibatizwa si pale unapojazwa Roho mtakatifu! Kwani, kubatizwa ni mhimu sana, kuliko kujazwa roho mtakatifu? Naweza kusema NDIYO! Kwanza, kubatizwa kunaambatana na TOBA! Ukisoma,Marko 1:4-5,Neno linasema “4Yohana alitokea,akibatiza nyikani,na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la thambi.5Wakamwendea nchi yote………., wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao.” Waweza kuliona hilo waziwazi pia katika Matayo3:5-6. Mtu akisha batizwa ubatizo unaoambatana na Toba na ondoleo la Dhambi, ndipo Mungu kama lilivyo Neno lake hulitekeleza. ukisoma,1kor.12:28 na Efeso. 4:11, inasema, “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wakwanza Mitume, wapili, Manabii, watatu waalimu………….na aina za lugha.” Ukitazama hapo kwa makini, utaona kwamba, cha kwanza na cha pili na cha tatu ni vipawa na si matendo ya miujiza.Hata kwa kanuni ya kawaida tu ndani ya madhehebu yetu, si rahisi Mtu kuwa Mtume au kuwa Nabii au kuwa mchungaji au kuwa mwalimu, KABLA HAJABATIZWA! Na Kubatizwa lazima ifanyike toba kwanza kwa anayebatizwa, na hapo Mtu hupata kibali kwa Mungu ya kutumika. Lakini mtu anaweza kunena kwa Lugha hata kama hajabatizwa, wala haishangazi na haina kigezo, na hiyo haimpi mtu haki ya Kutumika katika kuhubiri Injili. Mtu anapobatizwa ndipo anapofungua mlango kwa ROHO MTAKATIFU AJE AKAE NDANI YA MUUMINI NA KUWA NAYE MDA NA WAKATI WOTE! Pale ndipo mtu, hupata kibari cha kupata na kudumu na VIPAWA, si matendo ya miujiza na ishara tu kama wanazopata waaminio wanapojazwa Roho mtakatifu! Aliyebatizwa hujifungulia mlango wa kuvipata vyote yaani ishara na vipawa – karama za Rohoni, maana mwenye Vitu hivyo unakuwa naye ndani yako mda na wakati wote,ili akutumie katika kazi yake kama apendavyo- hiyo ndiyo hasa maana ya Mdo 2:38, maana ni wazi tu inaeleza kuwa; Mtu akitubu atabatizwa kwa Jina la Yesu Kristo na akisha kubatizwa ndipo atapata Vipawa. Vipawa mtu anapewa na Mungu ili apate kutumika hasa katika ujilishaji, injili ndicho chanzo cha kuja, kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu kristo! Kama nilivyokwisha eleza hapo juu, kuwa kujazwa Roho mtakatifu hakutegemei sana ubatizo, bali Imani ya mtu na uwepo wa Roho mtakatifu mwenyewe mahali husika.Lakini Mtu kumpata Roho mtakatifu kunategema vitu vifuatavyo, Imani,Toba, na Ubatizo.Maana ni mwenye Roho Mtakatifu ndiye pekee anakuwa katika Usambazaji wa huduma ya Neno la Mungu- Injili! Ukisoma,Mdo.1:8,inasema,”Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu; Nanyi makuwa mashahidi……………hata mwisho wa nchi” Roho mtakatifu kuja juu ya Mtu, nikama alivyofanya kwa Yesu,pale mtoni katika kubatizwa na Yohana-Roho alijitokeza hivyo kwa yesu, ili Yesu aanze Utekelezaji wa kile kilicho mleta- Kufanya kazi ya ukombozi! Bila hivyo nathubutu kusema kuwa, tusingepaswa “kumsikiliza” kama tufanyavyo leo! MAANA SHETANI ANGEFANIKIWA Kutuvuluga! Mungu, alisikika akisema waziwazi, wakati tukio la Roho mtakatifu la kumjilia yesu likifanyika, Mungu aliona aliweke hilo sawa, ili kuweka bayana kuwa mtu aliye na Roho mtakatifu tu ndiye apaswaye kutusikizisha Neno la Mungu Mwenyezi, ndipo alisema “…….msikieni yeye” vivyo hivyo, Yesu aliwataka wanafunzi, wasitoke Yerusalem, hadi Roho mtakatifu aje kwao kwanza! Na kwakweli, kile kilichofanyika siku ya Pentekosite,Kilikuwa kuja kwa Roho mtakatifu ili akae na Mitume ndani yao tayari kwa kutumika, na si kuwajaza ili wanene ka Lugha; Hiyo ndiyo nguvu, mafunzo na ujuzi katika kulinena Neno la Mungu,ambako kulifanywa na Roho mtakatifu alipowajilia Mitume na kukaa kwao! Mwisho, Mtu anapotekeleza ile Mdo 2:38 ndipo hukamilika, na hivyo kupata vipawa ambavyo ndivyo vitendea kazi,bila kwakweli kuitekeleza hiyo Mdo 2:38; Nasubutu kusema,kwamba, huna HAKI ya kujiita mtumishi KAMILI wa Mungu, MAANA huna vitendea kazi! Ubarikiwe Ndugu yangu.

 55. Wapendwa Bwana Yesu asifiwe, ninachokiona hapa kuna wale waliofunuliwa kuhusu hili tunalolijadili hapa la ujazo wa Roho Mtakatifu na ishara tuionayo kwa anayejazwa. Pia wapo wanaosimamia itikadi zao na wala si neno la Mungu. Je neno la Mungu linajipinga lenyewe? La hasha! Mimi binafsi sijajazwa Roho Mtakatifu lakini natamani sana kujazwa na ni moja ya maombi yangu kwa Bwana Yesu naamini ipo siku nitajazwa na kunena kwa lugha.ANGALIZO:Kama huna ufunuo wa jambo linalojadiliwa hapa bora ukae kimya usichanganye wale wachanga kwa kutoa mawazo yako binafsi au mawazo ya kutokana na itikadi ya dini yako. Neno la Mungu liko wazi,ujazo wa Roho Mtakatifu ni lazima na kunena kwa lugha ni lazima.Hii ni ahadi yetu tuliyopewa na Bwana Yesu.(Matendo 2:37-39,1Wakorintho14:1-5)
  Ndugu zangu;Noel Msanjila,Asheri,Rosemary just to list a few kwa kweli nimebarikiwa sana na michango yenu.Mungu awabariki wote mliochangia na kuwafumbua macho ya rohoni ili neno la Mungu likae ndani yenu.

 56. Ndugu Haule,
  Je, nawe unaungana na wanaosema Hawa “ALIONGEZA” katika Neno la Mungu??

  Ubarikiwe ndugu!

 57. Unajua ndugu yangu Haule, mstari unaotenganisha mambo ya kunena kwa lugha ni mwembamba sana. Mimi sipingi kunena kwa lugha. Unajua kunena kokote kule, haswa kwa mtu mzima, huwakilisha mawasiliano, yaani kupitisha ujumbe. Nayo mawasiliano hufanywa katika lugha. Kwa hiyo hata mtu anaponena kwa lugha katika kuwasiliana na Mungu, ujumbe hupeanwa kati yao, na kwa vile hilo ni kati ya Mungu na mnenaji, nao unenaji ukiwa chini ya mnenaji, tumefundishwa kutafuta faragha inapokuwa hivyo. Lakini ikiwa ni katika kusanyiko basi awepo mtafsiri, yaani hilo ni kati ya waaminio; na kama ni kati ya wasioamini Roho Mtakatifu huwepo kwa ajili hiyo, yaani kila aliyepo hapo humsikia mnenaji kwa lugha yake. Katika yote hayo, uwe kwenye faragha yako au kusanyikoni au kati ya wasioamini; mnenaji na mtafsiri ni yeye yule yule Roho Mt. Hayo ndiyo mapana na marefu kuhusu kunena kama nimeielewa vizuri Biblia! Ila kusanyiko zima, la watu 3000, linapolipuka kila mmoja akinena kwa lugha kivyake, au muhubiri anapochomeka lugha, “Rabbabashani, akasandraaa,…!” jambo hilo ndio bado nalitafakari nikijaribu kusubiri labda Biblia Toleo Jipya yaweza kutupa mwanga zaidi! “Mbombo ngafu fijo”!!!!

  Umezungumzia Biblia kukaa kimya. Kukaa kimya tafsiri yake ni moja tu:- kutokusema chochote pale unapotarajiwa kutoa kauli au kusema neno, kama ilivyotokea katika majibizano siku ile baina ya Kristo na Pilato, Mathayo 27:12-14 “Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno” pia “Asimjibu hata neno moja, hata liwali akastaajabu sana.” Labda nikilinganisha na maelezo yako ya awali, kuhusu towashi kujazwa Roho Mt, pale ulipolishuku hilo, ukiliangalia tendo la kujazwa Roho Mt katika udhihirisho wa kunena kwa lugha, nawe ukitegemea kuambiwa hivyo na Maandiko, hapo ndipo huo ukimya wa Maandiko unapotokea!! Ni kweli yamekaa kimya, hayajakujibu!!! Pia nami nikikufuatisha wewe, nikaingojea Biblia itakaposema, “Kunena kwa Lugha ni Ishara ya kujazwa Roho Mt.”; naona imeendelea kukaa kimya hadi leo hii ninapoiandika posti hii, tokea mpendwa Cuthbert alipolileta jambo hili. Lakini kama yule mwanamke Mkananayo, naendelea kung’ang’ania kusubiri iseme!

  Kuhusu wale wale 120, kwao andiko la Mt 3:11 “… yeye atawabatiza kwa Roho Mt na kwa moto” liliwatimilia. Hao walikuwa na Injili kamili kama tunavyowaona wakiweko hapo juu kuingojea ahadi hiyo ili watoke wakaifanye kazi ya Bwana wao. Kuhusu wale waliobatizwa na Paulo baada ya kuwa wamebatizwa na Yohana, Maandiko yanayowahusu ndiyo hayo kama ulivyoyasoma hayabadiliki, ila wewe jaribu kubadilika na kuyaamini yanachosema, yaani ile Injili; yanasema hivi, “ Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu” Walipoisikia Injili hiyo WAKABATIZWA kwa JINA LA BWANA YESU. Kama leo ungekutana na Paulo, halafu akakusikiliza pamoja na kunena kwako, kisha akakuuliza ulibatizwaje hata unanena kwa lugha? Ukimjibu bila kumzungusha, atakuhubiri Injili ipasayo ambayo hujawahi kuisikia, na kukutimizia kama hao, na Mungu kukupa stahili yako katika urahisi!!

  Ubarikiwe ndugu yangu!

 58. Mpendwa wangu Haule,
  Nashukuru kwamba uliipitia ile post yangu ya tare 14/4/2012, naomba unisamehe kwa kutonipata kwa mda katika hii Site, kuna kizuizi kidogo nilipata, hata hivyo naomba. Kama Mungu akitupa nafasi, kesho tukutane tena juu ya sisitizo langu lihusulo Mdo 2:38.Natiwa moyo sana nawe, kwa jinsi unavyo wezeshwa katika kuchukuliana na Nami katika kujifunza. Mungu akubariki

 59. Mpendwa Sam
  Nilikuandikia hivyo sababu uliposema Kornelio na jamii yake ndio walikuwa mataifa wa kwanza kuupokea ufalme wa Mungu, nikakuletea andiko la Towashi na Filipo kwamba alipobatizwa alipokea. ,ulilikataa ndio maana nilikuandikia hivyo.mimi kwa ufahamu wangu mtu akimpokea Bwana kwa kumaanisha Roho wa Bwana anamjilia juu yake,kwa hiyo Towashi kama mmataifa kwa maandiko ninavyofahamu alipokea ufalme wa Mungu kabla ya Kornelio.
  Sam…biblia ikikaa kimya usiweke maneno yako,hatujui kama towashi alinena au hakunena maandiko yako kimya,hata Paul alipompokea bwana Mdo9:18 maandiko yalikaa kimya mpaka pale aliposema “1kor14:18 Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;”

  Sam huo mstari 22, wa 1Kor14:unautumia vibaya,kama dhamiri yako ni kupinga tu kunena kwa lugha kanisani basi kazi ipo(wanyakyusa wanasema “mbombo ngafu”)

  Imeandikwa…
  ”1kor14:2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.”
  Ninavyofahamu Kuna kusemezana(kuomba) na BWANA kwa aina mbili;
  (i).kwa roho, hii inaweza kuwa kwa kunena kwa siri lugha (isiyoeleweka) pia lugha inayoeleweka(unabii) kama Roho apendavyo,na kwa maono unayoyaona waziwazi kama alivyoomba na kuona Stefano.
  (ii)kuna kuomba kwa akili.

  Sam ni kweli kunena ni ishara kwa wasioamini. Ndio maana siku ile ya pentekoste wasiio amini waliiona ishara wakashangaa jamaa wakinena kwa lugha za huko waliko toka wao japo(wanafunzi) ni wagalilaya,Mwisho Petro akahutubu(unabii)na wasio amini wakamini wakampokea Bwana.
  Kama unautumia huo mstari kwa madhumuni ya kupinga unenaji wa lugha kanisani, Basi mistari yote inayozungumzia kunena kwa lugha haina maana yoyote kwako na biblia ni kitabu kinachojipinga chenyewe!.
  Yale maneno yako yanatimia tunatengua maandiko

  Imeandikwa..
  “1Kor14:4-5Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.
  Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa. ‘

  Mpendwa Sam maandiko yote ya 1kor14;Paul anatuasa kulijenga kanisa la Bwana(kuhutubu/unabii) ndicho anachosisitiza kama wewe unavyotaka lakini anatutaka wote tunene kwa lugha(hautubuye”unabii’ ni mkuu,anenaye ujenga nafsi yake)
  Sam..tafari huu mstari 1kor14;20

  Bwana akusaidie.

 60. Shalom..
  Natafakari….
  1…..Ubarikiwe kwa tafakari na bidii!
  (i)Ni kweli maandiko yanasema mtakapo sikia sauti yangu kwa bidii…..wanitafutao kwa bidii….ufalme utekwa na wenye nguvu…mtafuteni ..maadamu anapatikana,Asante
  2…Kuhusu yule mwanamke Mkananayo, waweza kuona yeye ali interrupt programu. Huduma ya Kristo katika wakati ule ilikuwa kwa nyumba ya Israeli,
  (ii)Sam tulikuwa tunajadili habari ya kuchangamana Israel na Mataifa,roho hiyohiyo iliyomtuma huyo mama ndio hiyohiyo ilimtuma Kornelio ingawa yeye tunaaona anashauriwa na Mjumbe wa Bwana alituma ujumbe ukamchukue Petro huku akijua awachangamani,pamoja hayo asnte kwa mafundisho.lazima kung’ang’ana kumbuka habari ya mwanamke na kadhi.
  (3)Kuhusu Kornelio, kunena kwake kwa lugha mbele ya kundi la Petro, ili kuelewa kilichofanyika hapo, inakulazima ulifuatilie jambo lote kama Mungu anavyolifunua. “Sala na sadaka zake Kornelio, zimepokelewa mbinguni na kuwa UKUMBUSHO!!” Hebu lizamishe hilo kwanza moyoni ndipo uendelee. Hili tunaliona likiwa ndani ya wakati, basi kunena kwao hakuwezi kubeba maana nyingine zaidi ya ile tuliyofundishwa -“USHUHUDA KWA WASIOAMINI”! Ndio maana tunapokiamini kifungu hicho,kukiwapo kunena kwa lugha, macho yetu huwatafuta ni akina nani wasioamini kati ya hao waliopo? Tukawaona wakina Petro!!!! Hiyo ndiyo sababu tunashangazwa na unenaji uliopo leo hii ndani ya makusanyiko yetu, Je ni kwamba kundi lote ni la wasioamini?
  (iii)Maana aonavyo nafsini mwake……

  4..Kama nilivyoandika katika posti za nyuma, ninayarudia tena ili kama hukuyaona, basi hebu litafakari hili pia kuwa Kazi kubwa ya Roho Mtakatifu ni kukuongoza uliamini Neno lake! Basi unapoona unayatilia shaka Maandiko au kuyakagua kwa kuyalinganisha na mafundisho tunayopata kutoka kwa walimu wetu wa vyuo, jua kwamba bado una hatua ya kupiga.
  (iv)Ni kweli Sam,sijafika bali napiga mbio mpaka niifikie ile mede/tunzo yz haki.
  5…Roho Mtakatifu hawezi kukuongoza katika mambo nusu nusu. Yeye ni Mkamilifu naye hutuongoza sisi kuufikia Ukamilifu. Ndio maana akatuwekea kanisani zile huduma tano, yaani wachungaji, mitume, manabii, wainjilisti na walimu ili watukamilishe katika Utakatifu. Lakini badala yake kanisa limebuni mpango wake na kufungua vyuo kama vile Israeli ilivyokataa kuongozwa na Mungu kupitia Samweli nabii, na kuishia kuongozwa na Sauli katika mapenzi yao, ILE NGUVU YA MUNGU ILIWAONDOKA!!! Hiyo ndiyo hali ya kanisa leo hii, wakishikilia zaidi mafundisho ya walimu wao ambayo yametuleta katika umbali wa MOYO MPYA wa NYAMA na ROHO MPYA tu ambavyo huambatana na misisimuko kama tuliyo nayo. Nao walimu wetu wametudanganya kuwa TUNAYE Roho Mt!!!!
  (v) Ingependeza haya maandiko Kama ungeyapeleka kule kwenye thread ya KUJIFUNZA KUMTUMIKIA MUNGU

  6…Najua ni vigumu kuamini kuwa hawa walimu wasomi, kuwa wanachapia kwenye mambo ya Mungu. Lakini hebu jaribu kutafakari hili kuwa Hawa alikula matunda kutoka katika ule Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya wakati Biblia haisemi hivyo!!

  (vi)Sam unaposema walimu wasomi unamaaninisha nini sijakupata mpendwa,Ni wasomi wa maandiko( Bachela ya theologia) au wasomi mfano wa Mwakasege ana (digree uchumi)lakini ni mwalimu wa maandiko? Nifafanulie.
  (vii)Biblia inasemaje kwani Sam?.. ..hii ya kwangu(inaweza kuwa tofauti na yako)imeandikwa” Mwanzao3:6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.”
  tofauti hili andiko nifundishe nipate ufahamu kuwa Hawa hakula tunda .
  (viii)Ninavyo fahamu hilo halikuwa tunda(ujuzi) kama embe, Mungu alitaka Adam ajue pamoja na mema anayoyaona kuwa kuna mabaya(shetani)hapo bustanini.
  7….Kuhusu ile thread Mdo 2:38, unajua hiyo ndiyo inayomzuia Roho Mtakatifu kutoka ndani ya Boksi! Maana ikitufungukia hiyo, tutakuwa na UJASIRI wa kuyapokea MAANDIKO YOOOTE!! Bwana akitupa wasaa na ikiwapendeza wenye blogu waweza kutuletea tukaijadili kwa faida yetu sote maana katika hali tuliyomo kulingana na Maandiko, hatuna cha Kupoteza bali Kupata!
  (ix)Ni kweli…E.mail ni hii strictlygospel@googlegroups.com
  Mawazo yangu kama yatapata nafasi moyoni mwako Sam ni vema wewe ukaandika ndio muamini(mdo2;38) leta mafundisho tuyatafakari tupate kupona ,mpendwa Cuthbert ndio aliyeanzisha hii thread si unaona tunajifunza.Shaka ondoa SG admiin/Mods ndio utumishi wao huo dhamiri zetu ni sawa nao kuujenga mwili wa Kristo(Kanisa)
  Basi nichukue nafasi hii kumshukuru Bwana kwa ajili yenu/yako wa/mpendwa kwa kuwaweka hapa kwa mahali sahihi na wakati sahihi.
  Bwana Awatunze.
  Amen

 61. Ndugu Haule,

  Univumilie kidogo, maana nilipokujibu kumbe niliiruka ile habari ya towashi, ambayo umesema hivi, “(i)… Towashi Mkushi inawezekana hakujazwa Roho Mtakatifu.” Labda nikusisitizie tu kuwa Biblia haijapungukiwa kitu hata tuanze kuingiza fikra zetu kwa kukisia kisia. Maandiko yametufunza kuwa kunena kwa lugha ni ISHARA kwa WASIOAMINI. Kwa hiyo jambo la towashi kumnenea Filipo kwa lugha lingeyatangua Maandiko kama mafundisho yetu yanavyofanya!

  Ubarikiwe!!

 62. Ndugu yangu Haule,

  Ubarikiwe kwa tafakari na bidii!

  Kuhusu yule mwanamke Mkananayo, waweza kuona yeye ali interrupt programu. Huduma ya Kristo katika wakati ule ilikuwa kwa nyumba ya Israeli, kwa hiyo huyu mwanamke mmataifa aliingilia katika huduma asiyohusika nayo. Hakuwa na Ahadi yoyote ambayo kwayo angelidai kuhudumiwa. Tazama anavyojaribu kumuita Kristo; “Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi”. Kristo hakumjibu neno, asingeliweza kuliruka Neno lake kwa kumuitikia huyu mwanamke anayemwita yeye BWANA nje ya wakati! Yeye ni BWANA kwa kanisa nao mataifa wakati wao ulikuwa bado. Pia anamwita ‘Mwana wa Daudi’ Kristo ni Mwana wa Daudi pale anapokuja kutawala (Israeli), na si katika ujio ule wa kukomboa wala kwa mataifa! Lakini tunajifunza jambo kubwa sana kutoka kwa huyo mwanamke, kwamba kwa kung’ang’ania kwake licha ya kufananishwa na mbwa, hakukata tamaa, na AKAPEWA nje ya programu!!!!

  Ila sijui kama nasi tuking’ang’ania nje ya programu kwa kuongozwa na hisia zetu Mungu atatujaza Roho wake!

  Kuhusu Kornelio, kunena kwake kwa lugha mbele ya kundi la Petro, ili kuelewa kilichofanyika hapo, inakulazima ulifuatilie jambo lote kama Mungu anavyolifunua. “Sala na sadaka zake Kornelio, zimepokelewa mbinguni na kuwa UKUMBUSHO!!” Hebu lizamishe hilo kwanza moyoni ndipo uendelee. Hili tunaliona likiwa ndani ya wakati, basi kunena kwao hakuwezi kubeba maana nyingine zaidi ya ile tuliyofundishwa -“USHUHUDA KWA WASIOAMINI”! Ndio maana tunapokiamini kifungu hicho,kukiwapo kunena kwa lugha, macho yetu huwatafuta ni akina nani wasioamini kati ya hao waliopo? Tukawaona wakina Petro!!!! Hiyo ndiyo sababu tunashangazwa na unenaji uliopo leo hii ndani ya makusanyiko yetu, Je ni kwamba kundi lote ni la wasioamini?

  Kama nilivyoandika katika posti za nyuma, ninayarudia tena ili kama hukuyaona, basi hebu litafakari hili pia kuwa Kazi kubwa ya Roho Mtakatifu ni kukuongoza uliamini Neno lake! Basi unapoona unayatilia shaka Maandiko au kuyakagua kwa kuyalinganisha na mafundisho tunayopata kutoka kwa walimu wetu wa vyuo, jua kwamba bado una hatua ya kupiga.

  Roho Mtakatifu hawezi kukuongoza katika mambo nusu nusu. Yeye ni Mkamilifu naye hutuongoza sisi kuufikia Ukamilifu. Ndio maana akatuwekea kanisani zile huduma tano, yaani wachungaji, mitume, manabii, wainjilisti na walimu ili watukamilishe katika Utakatifu. Lakini badala yake kanisa limebuni mpango wake na kufungua vyuo kama vile Israeli ilivyokataa kuongozwa na Mungu kupitia Samweli nabii, na kuishia kuongozwa na Sauli katika mapenzi yao, ILE NGUVU YA MUNGU ILIWAONDOKA!!! Hiyo ndiyo hali ya kanisa leo hii, wakishikilia zaidi mafundisho ya walimu wao ambayo yametuleta katika umbali wa MOYO MPYA wa NYAMA na ROHO MPYA tu ambavyo huambatana na misisimuko kama tuliyo nayo. Nao walimu wetu wametudanganya kuwa TUNAYE Roho Mt!!!!
  Najua ni vigumu kuamini kuwa hawa walimu wasomi, kuwa wanachapia kwenye mambo ya Mungu. Lakini hebu jaribu kutafakari hili kuwa Hawa alikula matunda kutoka katika ule Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya wakati Biblia haisemi hivyo!!

  Kuhusu ile thread Mdo 2:38, unajua hiyo ndiyo inayomzuia Roho Mtakatifu kutoka ndani ya Boksi! Maana ikitufungukia hiyo, tutakuwa na UJASIRI wa kuyapokea MAANDIKO YOOOTE!! Bwana akitupa wasaa na ikiwapendeza wenye blogu waweza kutuletea tukaijadili kwa faida yetu sote maana katika hali tuliyomo kulingana na Maandiko, hatuna cha Kupoteza bali Kupata!

  Bwana akubariki.

 63. Asante Mpendwa Sam
  Natafakari machache kati ya yale uliyoandika
  1…“Kuhusu Kornelio kuwa mmataifa wa kwanza kuingia katika Ufalme wa Mungu”
  (i)nikubaliane na wewe kuwa Kornelio alikuwa mmataifa wa kwanza kuingia ktk ufalme wa Mungu na tuachane na Towashi Mkushi inawezekana hakujazwa Roho Mtakatifu.
  2….“ Huenda katika kujihami na Mdo 2:38 ukawa unajaribu kulizunguka jambo hilo”.
  (ii)Sam anzisha thread ya Mdo2;38 tutafakari kwa kina acha kushuku mpendwa.
  3….. “Au tuamini kwa kauli yako kuwa Maandiko hayajui yanachokisema? Maana katika Mdo 10:28 Maandiko yanatuambia dhahiri, “Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea…”
  (iii)Sam nakubaliana na wewe…pata ufahamu hiyo ni torati(watu wa tohara)myahudi awachangamani na mataifa (wasiotairiwa)walikuwa wanaiitwa mbwa,lakini tumeona ktk maandiko Yesu akijiwa na mataifa mfano yule mama wa Tiro”mathayo15:21-28” Lakini tunaona Paul pamoja na wayahudi kuamini akishitakiwa kwalo(kuchangamana) alipofika Jerusalem Mdo21:27-30,Sam..Mungu alitaka kupitia Petro, wayahudi wajue hana upendeleo yeye ni Bwana wa wote.mimi sipingani na maandiko ila mayahudi .
  4….”Kuhusu ‘Kujazwa Roho Mt. kwa njia ya mkato bila kutimiza Mdo 2:38…” unapolileta jambo hili kwa akina Kornelio ili kuweka fundisho la Kujazwa Roho Mt. bila kupitia Ubatizo wa Ondoleo la dhambi kama ulivyowekwa na Roho Mtakatifu katika Mdo 2:38, hilo ni KOSA!!!”
  (iv)Mpendwa Sam, Toba ni kubadilisha mtazamo(change mindset)ni kufungua moyo wako mdo22;16 ni wewe mwenyewe unaliitia(kiri)jina lake Yesu na kumpokea Kristo, Bwana anakupa uzima wa milele ndio ondoleo la dhambi Yesu mwenyewe ndio anabatiza(Mdo11;18)kubatiza kwa maji ni kutimiza haki yote,Mpendwa Sam siku utakayofika mbinguni utashangaa kuwakuta pia watu walibadilisha mtazamo(toba) sekunde chache kabla ya kufa na kumpokea kristo,nao wameingia ktk ufalme wa Mungu.wala awakubatizwa kwa maji(haki yote) ila kwa Roho Mtakatifu na moto tu.
  Ooops Nadhani turudi kwenye mada maana tunazidi kutoka kwenye mada.
  SSam ulimwandikia Noel
  ”; vivyo kujazwa Roho Mt. kwa njia ya mkato bila kutimiza Mdo 2:38 ni kujidanganya, unapaswa upite hapo ili uondolewa dhambi zako kwanza ndipo Mungu aendelee kushughulika nawe katika hatua zinazofuata hata AKUJAZE huyo Roho Mtakatifu ili utakapoihubiri Injili kwa UJASIRI iwe sawa na ile waliyoihubiri ndugu zako mitume!
  Sam hitimisho langu ni hapo chini,Sikupata tafakari ya kutosha toka kwako.
  “Mdo10:44 Wakati Petro akiwa anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe”.
  Hapa awajapatizwa bado na maji lakini wamebatizwa na Roho Mtakatifu(Yesu) kwa kusikia neno na kutubu ndani yao(kubadilisha mtazamo wao na kuondolewa dhambi).
  “Mdo10: “Je, kuna mtu ye yote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.”
  Hapa wakitimiza haki yote.

  Mpendwa Sam sijawahi ona maandiko kuwa wanafunzi wa Yesu wale 120(siku ya pentekoste) wakibatizwa kwa Jina la Yesu kabla halafu ndio Roho mtakatifu akawajilia juu yao, Kama kuna maandiko unaweza kuyaleta na sio mafundisho nichafahamu walibatizwa ubatizo wa Yohana tu,
  Nimeona tena paul akiwabatiza wanafunzi ambao walisha batizwa ubatizo Yohana lakini hawakumpokea Roho Mtakatifu(Mdo19),Mungu ana makusudi yake afungwi na mafundisho mawazo yetu sio mawazo yake.Mpendwa usiuweeke ubatizo wa Roho Mtakatifu mpaka kwa mstari wa Mdo2:38.
  Kwa maandiko haya napingana na hoja uliyomundikia Noel.
  Mtume Petro anawaambia Mayahudi,Mdo11;17
  “mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mungu?”
  “Mungu hana upendeleo’
  Mangine ni mafundisho yetu tu.tunajaribu kuwafungia watu waliompokea Roho Mtakatifu kwa kutumia maandiko na mafundisho.
  Poleni kwa maandiko marefu.
  Ubarikiwe na Bwana

 64. Ndugu John Haule

  Asante kwa yote uliyoniandikia!

  Umezungumzia Mdo 2:38, ni kweli kifungu hicho huibuka sana katika mijadala. Nadhani ni kutokana na umuhimu wake katika suala zima la wokovu. Wako wapendwa wanaoamini kuwa si muhimu, wengi wao husema “wameamua kumfuata Yesu Mwalimu badala mitume wanafunzi” na wengine huushangaa mtazamo huo wakiamini kuwa mitume hawajakosea. Kwa hiyo Injili imegawanyika sana katika suala hili na ubatizo kwa jumla. Tuombe REHEMA maana ni jambo zito!!

  Nataka niliendee jambo hili la sahihisho ambalo limenitia moyo sana, kwani Neno la Mungu pekee ndio Ngome iliyo salama. Sote tunaweza kukosea lakini Neno ni Imara. Kuhusu kile kifungu nilichoandika; “…bali ilipaswa iwe damu ya kondoo na si kuku au mnyama mwingine yeyote.” Tunapokiweka sambamba na ile Kut 12:5 kama ulivyoinukuu, msisitizo wangu niliouweka kuhusu ulazima wa damu ya kondoo, UNAPWAYA saaana! “Damu ya mwanakondoo” imekaa sana kichwani hata wakati mwingine katika kusisitiza jambo nimekwenda nje ya Maandiko katika kuliwazia hilo, wakati Mungu mwenyewe aliwaambia damu ya mbuzi pia ilifaa. Basi Napenda niwaombeni radhi wote mliosoma na mtakaosoma post hiyo MNISAMEHE SANA kwa usumbufu wa mawazo katika kulitafakari Neno la Mungu!!! Pia ninamuomba Mungu ANISAMEHE kwa kuongeza katika NENO lake!!! Pia ninakushukuru ndugu yangu Haule kwa hilo, vinginevyo mshitaki angenifikisha nalo kwa Hakimu kosa la ‘Kuongeza juu ya Neno la Mungu’, asante saana!!!

  Ni kweli kwamba sadaka zote za wanyama zilizotolewa zilikuwa pia ni ishara, hilo ni kweli, lakini umuhimu wa mnyama gani atolewe katika sadaka hiyo pia ilikuwa na ulazima ili sadaka hiyo ikubaliwe kulingana na Agizo la Mungu! Kwa hiyo ningesema, Maandiko yakisema mwanakondoo au mbuzi, unapaswa uwatoe hao na si mnyama yoyote yule. Pia umeandika kuhusu Ibrahimu, nimekuelewa katika umbali uliomzungumzia, lakini unaponiuliza swali, “Je, Mungu anazaa?” Nimeshindwa kukuelewa, na wala jibu lake sina!

  Kuhusu Kornelio kuwa mmataifa wa kwanza kuingia katika Ufalme wa Mungu, huenda inahitajika utulivu kidogo na si kuunga mawazo yetu kama nilivyofanya mimi katika “yule mwanakondoo”! Huenda katika kujihami na Mdo 2:38, ukawa unajaribu kulizunguka jambo hilo na katika kufanya hivyo ni rahisi kutokuyaona Maandiko yanachotufunza na kuishia kuwa na Neno la Mungu nusu! Kwa mfano, unaponukuu kifungu cha Mdo 10:47 na kisha kusisitiza ule mshangao uliowapata Petro na Wayahudi wenzie, kule kunena kwa lugha kwa wamataifa kama wao; halafu hapo hapo unaniambia hao walikuwa sio wamataifa wa kwanza kuingia katika Ufalme wa Mungu, ukimrejea yule towashi; labda nikuulize huyo Petro na wenzake walikuwa hawana habari ya towashi? Au tuamini kwa kauli yako kuwa Maandiko hayajui yanachokisema? Maana katika Mdo 10:28 Maandiko yanatuambia dhahiri, “Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea…” Ukisoma Mdo 2: 5- 12 ukawafikia na wale 3000 waliobatizwa siku hiyo, ukienda katika uvuvio wa jinsi hiyo ya kuwapa kabila kila mtu kwa sehemu atokako, Injili itaanza kuwa ya uongo!!! Tena Filipo alipopelekwa kwa towashi, hatuoni akitayarishwa kama Petro ili akamhudumie towashi huyo mmataifa ambaye alikuwa akitoka Yerusalemu kuabudu, huko ambako Wayahudi hawashikamani na mataifa; Injili inavurugika! Twende pole pole tukiyatafakari Maandiko.

  Kuhusu ‘Kujazwa Roho Mt. kwa njia ya mkato bila kutimiza Mdo 2:38…” unapolileta jambo hili kwa akina Kornelio ili kuweka fundisho la Kujazwa Roho Mt. bila kupitia Ubatizo wa Ondoleo la dhambi kama ulivyowekwa na Roho Mtakatifu katika Mdo 2:38, hilo ni KOSA!!! Roho Mtakatifu alipomhudumia Kornelio alifanya huduma mbili kwa pamoja; aliwadhihirishia Wayahudi KUWAPOKEA mataifa, na pili kumpa ruksa Petro ya kuwafungulia Lango la Ufalme mataifa!!!

  Unaposema “hawakutimiza Haki yote” nadhani itakuwa ni tatizo lile lile la kuikimbia Mdo 2:38, lakini ukiendelea mbele katika kifungu ulichonukuu, utamuona Petro akiwabatiza ubatizo huo wa ONDOLEO LA DHAMBI, huko ndiko kuitimiza Haki yote!

  Hivyo ndivyo anavyo funguliwa Roho Mtakatifu kutoka kwenye boksi; kwa Maandiko!!!

  Ubarikiwe, ndugu yangu John Haule!

 65. Sam
  Nakushukuru kwa tafakari nzuri
  Kiu yangu ni kufahamu yale uliyomwandikia Noel, kujazwa mpaka upitie ubatizo
  Huo mstari wa Mdo 2:38 niliutumia kwa sababu uliuweka.usikutoe nje ya yale ninayowiwa kufahamu.
  Nimepata uzoefu kwa muda sasa, unapoingizwa mstari Mdo 2:38 ktk mjadala, wapendwa waliobatizwa nao wanapoteza hoja/swali walio ulizwa kwa kukusudia au bila kukusudia wananza kugonga injili ya Mdo2:38.
  Napendekeza Moderator atuanzishie mjadala mwingine wa huo mstari Mdo2:38. Pia mpendwa Sam unaweza kuleta maandiko/mafundisho toka huko uliko na kuandika hapa kulingana na ufahamu wako wa Mdo2;38 ikawa thread mpya kusudi huu mstari utuweke huru tuujadili na kutafakari kwa kina/kimo/mapana/marefu tukitumia maandiko kwa upendo wa kindugu tukichunguza kama waberoya.na yale yatakayojiri.

  Umeandika
  “Kuhusu Malaika wa Kifo aliyepita Misri, twafahamu yeye aliangalia ‘damu’ ile ya kondoo waliyoamriwa kumchinja na kupakwa katika vizingiti vya mlango. Ikiwepo hiyo damu, hilo lilionesha UTII, bali ilipaswa iwe damu ya kondoo na si kuku au mnyama mwingine yeyote”.

  Kut12:5 imeandikwa

  “Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi”.

  Sam maandiko hayamaanishi mwana kondoo kama kondoo bali yanamaanisha sadaka na pia ishara,yaliofanyika kut12: ni mambo ya ulimwengu wa Kiroho zaidi,hata kama yalifanyika kimwili kwa wana israel.ilikuwa ni ishara/mfano kwa ukombozi wa ulimwengu, Ni sawa na mwana kondoo aliyejitwalia Bwana wakati Ibrahimu anataka kumtoa Mwanae wa pekee(first born)Isaka Mw 22:8,ukiangalia kwa macho ya kimwili Isaka sio mzaliwa wa kwanza,ukitafakari utaona mw22;1-13 ni mpango kamili wa Mungu kumtoa mwanae mzaliwa wa kwanza ili kuukomboa ulimwengu,swali je Mungu anazaa!!.

  Umeandika..
  “Kornelio, alikuwa ni mmataifa wa kwanza kuingia katika Ufalme wa Mungu. Petro akiwa ni Myahudi, hao kulingana na Torati yao walikuwa hawachanganyiki na mataifa, Mdo 10:28”

  Sam kumbuka habari ya Filipo naTowashi Mkushi Mdo8;26-39, Naomba ufahamu wako Sam kushi si mmataifa!la sawa,vinginevyo Kwa neno hilo Kornelio sio mmataifa wa kwanza kupokea Ufalme wa Mungu.wala Petro sio myahudi wa kwanza kujishikamanisha na mmataifa.

  Kwa kweli Sam ukujibu swali na kumaliza kiu yangu kupata ufahamu toka kwako,ulichofanya umenihubiria habari ya Petro na Kornelio pamoja na injili ya Mdo2:38 ni vema na inapendeza.

  Uliamwandikia Noel…”
  “ vivyo kujazwa Roho Mt. kwa njia ya mkato bila kutimiza Mdo 2:38 ni kujidanganya, unapaswa upite hapo ili uondolewa dhambi zako kwanza ndipo Mungu aendelee kushughulika nawe katika hatua zinazofuata hata AKUJAZE huyo Roho Mtakatifu”

  Ndipo nilipotaka unipe ufahamu..
  Hawa mataifa walijazwa Roho Mtakatifu( Mdo10:44) mbona hawakutimiza haki yote? ..Kulikoni .
  Wasiwasi wangu ulipo tumechukua kazi ya Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu Tunamfungia kwenye boksi kwa maandiko(neno) na mafundisho ya walimu wetu wa kiroho.
  Petro na Wayahudi wenzie walishangaa mataifa wanaena vile vile kama wao ndipo pale Petro alipowauliza wayahudi Mdo10:47.

  Barikiwa

 66. Ndugu John Haule,

  Ubarikiwe!

  Ni kweli, kama ulivyosema, uwezekano wa kuufungia ‘Uweza wa Roho wa Bwana’ ndani ya boksi ni mkubwa sana, haswa pale tunapoyatazama maandiko kwa ‘rear sight mirror’! Yaani unajiongoza kwenda mbele usikokutazama kwa kukuangalia huko nyuma ulikokwisha kupita, ni lazima utapata ajali!!

  Kama safari yoyote ilivyo, hata ikiwa ni ya wokovu, kadiri ya hatua tunazozipiga kuelekea hiyo pointi ya safari yetu, mambo tunayokutana nayo katika njia hiyo, kadiri ya hatua tunazokwenda, hutupa tumaini na uhakika wa safari yetu. Kila tunaposonga mbele tunakutana na ishara za barabarani zikituonya na kututaarifu umbali na sehemu tuliyopo. Basi katika kuuendea huo mji wa wokovu, tunapoianza safari huko Mwanzo 1:1, katika kila hatua tunayopita, twaukulia wokovu! Nako kukua, ishara kubwa ni pale yale mambo tuliyo kuwa tumeyashikilia ambayo yalikuwa ni kwa sehemu yanapojiachilia pale yale yaliyokamili tunapoyafikia!

  Kwa hiyo, kama nasi tunavyopiga hatua katika safari yetu, tunapoukaribia ule mji wa ‘Kujazwa Roho Mtakatifu’, ni muhimu sana kuziangalia ishara kwa makini ili tusifike mahali tukawa tumekata kona isiyotakiwa! Kwa mfano, ili kufika katika kiwango cha kuichukua Mdo 2:38 katika uzito uliokusudiwa, yakupasa kwanza kufika katika kujitambua kwamba wewe ni mwenye dhambi kama walivyojitambua wale 3,000 siku ile ya Pentekoste na hivyo kuhitaji HURUMA ya Mungu! Yawezekana nasi, katika mafundisho tuliyoanza nayo katika safari yetu yakawa na mapungufu kidogo, yaani yakiwa ni ‘ya kwa sehemu’; basi katika umbali tuliofika, sasa ni wakati ‘wa kuona uso kwa uso’ maana ile ya kamili ituwezeshayo hayo ndio hii imetufikia katika blogu hii mbali wanyapara wetu wa kidhehebu! (1Kor 13:10)

  Kornelio, alikuwa ni mmataifa wa kwanza kuingia katika Ufalme wa Mungu. Petro akiwa ni Myahudi, hao kulingana na Torati yao walikuwa hawachanganyiki na mataifa, Mdo 10:28; ndipo tunaona alichofanyiwa Petro pale alipotakiwa kwenda kwa Kornelio, Mdo 10:11-23. Kama maandiko yanavyomshuhudia Kornelio katika uchaji Mungu, licha ya sadaka yake kukubaliwa na Mungu, bado tunaona Mungu asingeweza kumpokea Kornelio katika Ufalme wake nje ya Neno lake ambalo kwalo Funguo za Ufalme alimpa Petro. Na katika kumdhihirishia Petro kukubalika na Mungu kwa wamataifa, ndipo tunaona Mungu akimshushia Kornelio na nyumba yake Roho Wake mbele ya Petro na kundi lake lote (ambao walikuwa ni WASIOAMINI kuhusu wokovu kwa mataifa, ambao walishuhudiwa kwa kule kunena kwa lugha!) na ushuhuda wa tukio hilo tunauona kama ulivyo katika Maandiko. Yaani ule ubaguzi uliokuwepo kwa Wayahudi ulikuwa ni ile ‘kwa sehemu’, ilipokuja ya kamili, kama tunavyoiona hapo, Petro akiiona ‘uso kwa uso’ na ule ubaguzi ukaachilia kwa Wayahudi walio Wakristo! Kazi kuu ya Roho Mtakatifu kwa muaminio ni kukuweka katika kweli yote. Kwa hiyo tunapoendelea nao, tunamuona Petro akitamatisha tukio zima kwa KUMFUNGULIA Kornelio lango la UFALME, akawabatiza! Hiyo ndiyo tabia ya Mungu: KULIHESHIMU NENO LAKE!!!

  Kuhusu Malaika wa Kifo aliyepita Misri, twafahamu yeye aliangalia ‘damu’ ile ya kondoo waliyoamriwa kumchinja na kupakwa katika vizingiti vya mlango. Ikiwepo hiyo damu, hilo lilionesha UTII, bali ilipaswa iwe damu ya kondoo na si kuku au mnyama mwingine yeyote! Basi huku mbele katika safari yetu, ahadi ya Malaika huyo katika namna ya Misri, uharibifu utakuwa mkubwa zaidi kama tunavyouona katika Ufu 7:1-3 “… nikaona malaika wanne… … Nikaona malaika mwingine akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliyehai; akawapigia kelele wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu…” Sasa hao ni Israeli, ambao ni wa kimwili, nao wakiwa ni mfano wa kanisa; basi muhuri wa Mungu kwa kanisa ndio huo tunao uona katika Efeso 4:30 “Wala msimuhuzunishe yule Roho Mt. wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.” Glory!!!!

  Basi huo ndio umuhimu wa Roho Mt. tunapoiendea siku hiyo ya uharibifu kama inavyoonekana katika Malaki 4:1 ambapo tunaambiwa, “… angalieni siku ile inakuja, inawaka moto…” basi unapaswa uwe umetiwa muhuri ili kuiepuka siku hiyo; nao ‘muhuri ya Mungu’ inapatikana kwa kuwa na UTII na kupitia ule Mlango alioufungua Petro katika siku ya Pentekoste ambao umefunguliwa hata kwetu sisi kadiri ya Mapenzi yake Mungu alipotuita tumjie, Mdo 2:38! Kunena kwa lugha hakutakuepusha na moto huo ujao!

  Ubarikiwe na Bwana wa Vipawa!

 67. Asante Mabinza kwa masahihisho,hujafanya kosa kuingilia kati ndio tunajifunza.
  Nilikuwa nimekopi kwenye bibilia ya mtandao http://churchages.com/sw/bible/acts/10/,naona ni makosa wamefanya ktk namba au makusudi mnisamehe kwani mistari yote imekosewa. Hata sasa natumia tena BIBLICA kama kuna makosa mchukuliane nami tafadhari, nipo kwa ofisi nagonga mzigo kidogo,Hayo tuachane nayo twende kwenye hoja..
  Nilikuwa nazungumzia mstari wa Mdo10:44 unaosema
  “Wakati Petro akiwa anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe”
  Na pia Mdo10:47. Ndipo Petro akasema,
  “Je, kuna mtu ye yote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.”
  Tunaona hawa mataifa wakipokea Roho Mtakatifu kabla hawajabatizwa hilo ndilo swali langu kwamba hawakupita Mdo2:38 kwanza baadaye wabatizwa,kama anavyoutumia huo mstari ndugu Sam.bila kupita hapo ni kujidanganya!!kuwa hakuna njia ya mkato,udadisi wangu je kina kornelio walijazwa kabla kuna udanganyifu?au ni sisi ndio wadanganyifu tunaotaka Roho Mtakatifu afanye sawa na mafunzo tuliyofundisha,ndipo niliposea wasiwasi wangu tunamwekea mipaka kwamba pasipo hivi haiwezekani tena tukitumia maandiko

  Umeandika…
  “Sasa, Kama ungesoma kuanzia huo mstari ulioutaja ule Mdo 10:46 hadi ule wa 48, ndipo ungejua kwamba Kinachosisitizwa pale ni kile kile kilicho semwa kwenye Mdo 2:38 yaani UBATIZO KWA JINA LA YESU KRISTO.- Ni wazi kuwa watu hao WALITENDEWA SAWASAWA NA Mdo 2:38!”

  Sio sawa kutokana na hoja ya Sam ya kubatizwa kwanza(Mdo10;38) ndipo umpokee ,tunaona Mdo10:44-48 wanampokea kwanza wanabatizwa baadaye. Hata kama watu hawajabatizwa Lazima tukubali kuwa wamejazwa. Ukiangalia nimepata kuandika hapa kwenye hii thread siku za nyuma, kuna watu wanabatizwa ndio wanajazwa,lakini kuna wengine kabla ya kubatizwa wanajazwa( kunena kwa lugha tu kama ishara)kama moja kipawa cha Roho Mtakatifu.

  Maana kule kwenye Marko16 ishara ziko nyingi za waaminio sio lazima kila mtu anene kwa lugha tu ndio anaonekana kuwa amejazwa,kuna wengine watatoa pepo,wengine watakula vitu vya kufisha havitawadhuru,wengine watawawekea wagonjwa mikono juu yao watapata afya,kushika nyoka nk ni vipawa tofauti tofauti kadri Roho apendavyo wengine hawaneni kwa lugha lakini wamejazwa vipawa vingine,ila kama unataka karama/vipawa zaidi paul kwenye 1kor14 anasema na tuombe.kwa mfano yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

  Hapo ndipo ninapotaka tupate ufahamu kuwa watu wanampokea Roho Mtakatifu si kwa kupatizwa tu ni pamoja na kuamini tu neno lake Mungu.unapakwa mafuta ya Roho Mtakatifu sawa sawa Isaya10 pale aliposema tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta
  kulingana na maandiko ya Sam kwa Noel.sio lazima ubatizwe ndipo ujazwe,kubatizwa(maji mengi) ni kutimiza haki yote,pia ni kitu cha kuangalia sio kwa sababu Yesu alibatizwa ndipo Roho akamjilia juu yake,basi itakuwa hivyo kwa kila mtu la hasha tumefunuliwa kuwa Roho Mtakatifu anawez kukujilia juu yako kwa kusikia neon nawe ukaamini Mdo 10;44-48kumbuka Roho Mtakatifu sasa tupo naye,na YESU NDIO ABATIZAYE
  Mpendwa Mabinza tunajaribu kumfungia (kumzimisha) utendaji wa Roho Mtakatifu kwa kutumia maandiko matakatifu kwa kudhani kuwa wote wanao nena kwa lugha kama hawajapitia Mdo10:38 kuwa wana mapepo ni mafundisho potofu.
  Mpendwa Sam bado nasubiri shule yako nipate ufahamu,pole kwa usumbufu uliotokea wa kuchanganya mistari,nilikuwa, Nakubaliana na masahihisho ya Mabinza,lakini nilikuwa najibu pia hoja zake zilizokuwa zinasisitiza Mdo10:38
  Mubarikiwe wote wana SG na samahani kwa maandiko marefu.

 68. 1. Mpendwa Haule,
  2. utanisamehe kwa kuingili kati, Roho yangu imesukumwa kukuandikia,tokana na maulizo yako kwa Sam, nineona nikuandikie kwa sababu mbili, kwanza Sam mwenyewe hajajibu, pili kwakuwa tunjifunza wote. Ili unielewe naanza kwa nukuu uliyoyandika kama ifuaatavyo:-
  “…………….Lakini tukiangalia Mdo10:43,tunaona Kornelio na wote walio sikia lile neno wakipokea vipawa vya Roho Mtakatifu na nguvu zake pasipo kupita Mdo2:38,tunaona pia Mdo10:46 Petro akiuliza nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
  Naomba kufundishwa nawe ili nipate ufahamu,wasiwasi wangu tusije fungia uweza wa Roho wa Bwana kwenye boksi kwa kushikilia mstari mmoja.Mdo10:37
  Ubarikiwe” mwisho wa kunukuu.
  3. Mpendwa usome tena vizuri mstari ulioutaja wa ile Mdo 10:43, mstari hou unazungumzia ONDOLEO LA DHAMBI na si VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU. Kumbuka Mjadala uliopo mbele yetu ni JE, KUNENA KWA LUGHA NI LAZIMA ILI KUTHIBITISHA KUWA NI ISHARA PEKEE KUWA UMEJAZWA ROHO MTAKATIFU? – Hivyo, mstari uliounukuu hauendani na Maada, hapo sina la kujibu. Na Petro alianza kuulizia habari ya Maji ni katika Mdo 10:47 na si katika Mdo 10:46. Lakini Kinachoelezwa katika Mdo 2:38 ni ……WATU WABATIZWE KWA JINA LA YESU KRISTO na hivyo waweze kupata vipawa vya Roho mtakatifu –Sasa, Kama ungesoma kuanzia huo mstari ulioutaja ule Mdo 10:46 hadi ule wa 48, ndipo ungejua kwamba Kinachosisitizwa pale ni kile kile kilicho semwa kwenye Mdo 2:38 yaani UBATIZO KWA JINA LA YESU KRISTO.- Ni wazi kuwa watu hao WALITENDEWA SAWASAWA NA Mdo 2:38! Kwa hiyo, Neno la Mungu limehakikishwa. Mungu hawezi kusema Neno halafu ajipinge eti aseme hapo sikuwa na maana hiyo, au hapo tumieni neno hili na huku msitumie neno hili! kwakweli hakuna “shoti kati” neno la mungu linasema, TUNAPASWA KUITIMIZA HAKI YOTE. Naamini Sam, atakujibu na kukufafanulia kwa uzuri na kwa kirefu zaidi. Hapa Mimi ni kama nilikuwa “Nakata tu kipande cha kuchoma” Naamini “Kilo nzima” ya kutosha kupika na kukushibisha atakuja nayo, na hapo ndipo utapata chakula kamili kwa kadri Roho atakavyo mjalia; maana Neno la Bwana ni chakula! Asante.

 69. Mpendwa Sam,
  Nisamehe tu maandiko yako yamepelekea kwangu udadisi wa kutaka kupata ufahamu zaidi unaposema
  “Siku atakapopita Malaika wa Kifo kama kule Misri, ataangalia waliojazwa Roho Mt., ambaye ndiye Damu ya leo, na sio wanaonena kwa lugha, maana hata mapepo yananena kwa lugha!”
  Naomba nijue ni wakati gani huo Malaika atapita?na ni maandiko au ufunuo
  Barikiwa na Bwana

 70. Mpendwa Sam,
  Shalom,
  Umeandika …nakunuu
  “ vivyo kujazwa Roho Mt. kwa njia ya mkato bila kutimiza Mdo 2:38 ni kujidanganya”,
  Lakini tukiangalia Mdo10:43,tunaona Kornelio na wote walio sikia lile neno wakipokea vipawa vya Roho Mtakatifu na nguvu zake pasipo kupita Mdo2:38,tunaona pia Mdo10:46 Petro akiuliza nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
  Naomba kufundishwa nawe ili nipate ufahamu,wasiwasi wangu tusije fungia uweza wa Roho wa Bwana kwenye boksi kwa kushikilia mstari mmoja.Mdo10:37
  Ubarikiwe

 71. Mpendwa Noel Masanjila,

  Kuhusu mwaminio ‘KUJAZWA ROHO MTAKATIFU’ :- fundisho la “Kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mt.” ni sawa kabisa na sala ya “Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi!”

  Kama vile sala ya marehemu kuingizwa peponi isivyoweza kukubalika na Mungu kulingana na Heb 9:27 inayotuthibitishia kuwa “Baada ya kifo ni Hukumu”; vivyo kujazwa Roho Mt. kwa njia ya mkato bila kutimiza Mdo 2:38 ni kujidanganya, unapaswa upite hapo ili uondolewa dhambi zako kwanza ndipo Mungu aendelee kushughulika nawe katika hatua zinazofuata hata AKUJAZE huyo Roho Mtakatifu ili utakapoihubiri Injili kwa UJASIRI iwe sawa na ile waliyoihubiri ndugu zako mitume!

  Siku atakapopita Malaika wa Kifo kama kule Misri, ataangalia waliojazwa Roho Mt., ambaye ndiye Damu ya leo, na sio wanaonena kwa lugha, maana hata mapepo yananena kwa lugha!!

  Ubarikwe!

 72. Mpendwa NOEL,
  Nimepitia post zako zote mbili ile ya 4/4/2012 na ile ya 5/4/2012, nimekuelewa vizuri sana. Mjadala uliopo mezani ni JE, NI LAZIMA KUNENA KWA LUGHA KAMA ISHARA PEKEE YA LAZIMA KUONYESHA KUWA MTU AMEJAZWA ROHO MTAKATIFU. Kimsingi nakubaliana na wewe kwamba, kila aaminiye atapata kwendana na ishara zinazowahusu waaminio! Lakini nikuweke wazi kwamba waaminio wanaotajwa ni wale tu, WANAOLIAMINI NENO LA MUNGU LOTE – Mstari kwa Mstari, Ukurasa kwa ukurasa na Sura kwa Sura! Kuamini huko LAZIMA kwendane na MATENDO Na si vinginevyo! Umesisitiza, nanukuu “………… ‘MUNGU ULISEMA KTK MARKO 16;17 BILA KUBAGUA KWAMBA ISHARA HIZI ZIMPATE NANI ILA KWA KUKUAMINI TU’ Mimi naendelea kusema KUTOKUNENA KWA LUGHA KUNATOKANA NA KUTOKUAMINI TU,BASI,MAANA NENO LIMESEMA ‘NA ISHARA HIZI ZITAFUATANA NA HAO WAAMINIO. kwahiyo hata ukimwona nani haneni kwa lugha,ujue tu hajaamini……….” Mwisho wa nukuu. Maandiko hayo ni ya kweli na yana maana hiyo, wasi wasi wangu ni sijui IWAPO umeelewa kama nilivyoelewa. Hebu anzia juu kidogo ya sura hiyo iyo ya Marko 16, anzia mstari ule wa 15, unasomeka hivi “15 akawaambia. Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka: asiyeamini, atahukumiwa”. Hayo ni maneno ya YESU na ndiyo yameachwa kama MASHARTI kwa mtu autakaye wokovu pamoja na vipawa vyake, kama inavyoeleza kwa pamoja katika sura hiyo ya Marko 16 ukiunganisha hadi ule mstari wa 17, uliounukuu. Ukisha kukubaliana na hayo, na kwa kuwa tunajifunza kwa misingi ya kama walivyo fanya MITUME PASIPO KUACHA AU KUPUUZA NENO LOLOTE, Ndipo tunapounganisha hiyo sura ya 16 ya Marko kuanzia mstari 15 (ambao wewe uliuacha katika kujifunza) hadi ule wa 17; ili kutufikisha katika haki ya kupokea vipawa vya Roho mtakatifu, inabidi kuwatazama mitume wao walifanyaje katika kutekeleza hayo yaliyosemwa na Yesu katika hiyo Marko 16:15, 6,7. Ndipo bila kupunguza au kupuuza sentesi yoyote tunayakuta maelekezo yatupasayo kufanya, ili kupokea hivyo vipawa na ahadi alizosema Yesu kuwa Mtu akiamini na kubatizwa atambatana na ishara zilizotajwa katika Marko 16:15 – 17, tunapokubali na kuutia katika vitendo ule mstari 38 katika sura ya 2 ya Matendo ya Mitume. Ambao unasema wazi kuwa; 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.SASA Ukinijulisha NI KAJUA kuwa; Je, hiyo Mdo 2:38 unaiamini kuwa ni NENO LA MUNGU? Kama ni ndiyo, jiulize kama umeuweka mstari huo katika matendo ili kudhibitisha kuwa nawe ni pamoja na WAAMINIO –Kwakuwa kutotii hata mstari nusu tu wa Biblia kunatosha kabisa kutufanya WASIOAMINI, maana IMANI BILA MATENDO IMEKUFA!
  Namalizia kwa kusema kwamba, huwezi kudai vipawa bila kukubaliana kwanza na mwenye kutoa vipawa! Kwa kifupi Marko 16:15 – 17, ni maagizo ya YESU mwenyewe, ambaye ndiye Vipawa vyote ni mali yake, na ndiye mwenye kuvigawa kwa waminio kadri apendavyo. Na Mdo 2:38 niutekelezaji wa yale maelekezo ya yesu ya hiyo Marko 16:17 uliyoitaja.Ubarikiwe.

 73. Masanjila,

  Hauko mbali sana na ukweli wa ki Biblia, bali jitahidi usiufanye moyo wako kurudia ule ugumu wa jiwe, jaribu kwenda pole pole na maandiko utakiona tunachokisema!

  Unapozungumzia kuamini, uliamini nini? Unaweza kuwa umeamini injili dhaifu na kisha kujihesabia haki, pia waweza kuwa umeviamini vipawa ukadhani vinatosha kukudhihirishia kuwa UMEJAA ROHO MT!

  Vifungu vyote vya maandiko ulivyovinukuu, hakuna hata kimoja kinachosema “KUNENA KWA LUGHA NI ISHARA YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU” bali ukiwa chini ya mafundisho fulani, waweza kuyaona maandiko yakisema hivyo!!! Kwenye hii blogu tunayajadili mafundisho au mapokeo tuliyonayo, pamoja na hayo mafundisho ya mwalimu Mwakasege, ili kuona kama ni Neno la Mungu au la; haijalishi kutukuka kwao! Tunayafanya hayo ili kujiweka sawa na Neno, maana leo tunajua kwa uhakika Mungu atatuhukumu kwa Neno lake ambalo ni Biblia yote na si “Yesu mwenyewe alisema…”!! Unapoanza kulibagua Neno la Mungu, hicho ni kipimo tosha kuwa hujafika katika KULIAMINI na hivyo huwezi kujazwa Roho Mtakatifu, na ndio maana kuna kulazimisha kwingi leo hii kwa kisingizio cha kunena kwa lugha isiyoeleweka mbele za watu bila mtafsiri kinyume na fundisho la ki Biblia!

  Kunena kwa lugha ni kipawa kidogo sana kihuduma, ndio maana mtume Paul, nikirejea nukuu yako, anatufundisha hivi: 1 Kor 14;2 – ‘ANENAYE KWA LUGHA, HASEMI NA WATU BALI HUSEMA NA MUNGU, MAANA HAKUNA ASIKIAYE; LAKINI ANENA MAMBO YA SIRI KTK ROHO YAKE.’ Sasa ni jambo lipi lisiloeleweka katika fundisho hili? Iweje mnapokusanyika kwa ibada muanze kunena kila mtu kivyake mambo yenu ya siri hata wapita njia wawaone wendawazimu? Kwa ushuhuda wa maandiko, tunafahamu kuwa kipawa kiko chini ya mnenanaji, sasa inakuwaje ninyi mnakiuka utaratibu uliowekwa na Mtoa kipawa? Ni Roho gani aliyewapa hicho kipawa na kukiongoza katika jinsi hiyo?
  Hayo ndio maswali yanayotufanya turejee hapo vipawa vilipoanzia, katika maandiko, ili tuone kama vinafanana na hivi vilivyopo!

  Katika kuzikagua Roho, tukizilinganisha na ile Roho iliyoandika Biblia, tumeona kuwa SI Roho yule yule bali ni Roho mbili zilizo tofauti but SIMILAR!
  1. Roho wa Biblia anawapa waumini kunena (a) kunena kwa ushuhuda mbele ya wasioamini; Yeye Roho Mt huwepo kutafsiri. (b) kunena kwa kuongea na Mungu; kwa vile kipawa cha Roho Mt si kama kupagawa na mapepo ambapo mnenaji huwa hana uwezo wakumiliki kunena kwake, basi huyu wa kipawa halisi anapotaka kunena na Mungu hujitenga na kuingia katika faragha yake ambako huendelea kunena na Mungu kadiri ya shauku yake
  2. Huyu Roho mwingine yeye pia huwapa waumini kunena: (a) na (b) wote hunena, lakini bila utaratibu wala wanenaji hawana uwezo wa kumiliki kunena kwao, na huyo Roho huwa anakimbia kutafsiri!

  Wanenaji wote wa staili hizo mbili, WAPO! Kulikoni na Injili ni moja? Kwanza vipawa havina majuto. Unaweza kuwa nacho na ukapotea nacho vile vile. Kwa hiyo tutavitofautishaje? Biblia ndiyo kigezo kikuu kwa yeyote yule aliyeamua kuambatana na Neno la Mungu. Unajua, uamuzi wa kuambatana na Neno ni mkuu saana. Pale unapoamua hivyo, mbingu hutikisika kwa furaha, naye Mungu hushuka na kukuvisha taji la ujasiri wake na kukufanya mwanawe, yaani kule kuzaliwa mara ya pili! Jambo la UAMUZI, Mungu ameliacha katika hiari yetu kama ilivyokuwa kwa Adamu. Adamu hakudanganywa, (ingawa wahubiri wengi hutueleza hivyo!), yeye ALIAMUA KUAMBATANA NA MKEWE (kanisa) BADALA YA NENO!! Hivyo ndivyo muumini wa kawaida afanyavyo, huamua kuambatana na mafundisho ya dhehebu lake badala ya Neno kama linavyojidhihirisha katika maandiko!

  Basi utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na hivyo vipawa vya kunena mtaongezewa. Ifuateni injili, nendeni mkabatizwe maji mengi kwa jina la Bwana Yesu Kristo ili mpate ONDOLEO la dhambi zenu kwanza ndipo Roho Mtakatifu atakuja kwenu kufanya makazi!

  Kwa yeyote yule aliye amua kulifuata Neno la Mungu, jambo la kwanza analolipata ni UHURU. Taratibu zote na mafundisho yake ya kimapokeo vilivyo nje ya Neno la Mungu, hata kwa nukta, vyote hujiachia na kudondoka huko chini, ile mizigo! Maana unapomfuata Kristo yeye hukuondolea hiyo mizigo uliyobebeshwa kama hilo zigo la kunena kwa Lugha katika jinsi ya kimapokeo na kukuongoza katika njia yake hata kukupa vipawa halisi utakavyo vimiliki na kuvifurahia! Tena kwa ule uamuzi wako Mungu huwajibika kukuonesha mambo yote kama alivyo ahidi, hukupa Roho wake AKUONGOZE NA KUZISHIKA SHERIA ZAKE ZOTE. Ukiwa na Mtoa Karama, utapungukiwa na nini?

  Hebu fikiri jambo hili, kwamba umefika mahali, katika Biblia, kuna vifungu unavikubali na kuna vifungu huvikubali kwa kisingizio kuwa viko tofauti na Yesu alivyosema, halafu mbele kidogo unavitumia vifungu vingine alivyofundisha huyo aliyeleta fundisho tofauti na la Yesu; kama si unafiki nini? Wengine asubuhi wako kwenye ibada inayokataza ishara, halafu jioni wanajikusanya peke yao na kuanza na ishara zao; kama si unafiki ni nini jamani? Roho Mt; huo ndio ushuhuda wake??? Acheni kujidanganya wapendwa, ujasiri uko wapi? Mtu hataishi kwa mkate pekee, bali kwa KILA NENO litokalo katika kinywa cha Mungu, na kama kinywa hicho ni mitume, ndio hivyo kulikataa Neno lolote kunakuondoa utukufuni mwa Mungu!

  Roho Mtakatifu haingii katika hekalu lisilo safishwa ile dhambi ya asili. Hakuingia kwa watakatifu wa Agano la Kale sembuse sisi! Dhambi ni kutokuamini Neno la Mungu. Basi inashangaza sana mtu anapodai kuwa anachokipawa cha Mungu ambacho amekipata nje ya utaratibu aliouweka Mungu mwenyewe, licha ya shuhuda lukuki zinazotolewa na watu wengi, shuhuda nyingi hazimbadilishi Mungu mawazo labda zinasaidia kuwashawishi watu wajitoe mioyo na Roho zao katika kuvitafuta hivyo vipawa ili wasionekane tofauti katika kusanyiko!

  Ni Roho Mt yupi huyo mliye naye anayeyakimbia maandiko aliyoyaandika mwenyewe? Kazi ya Roho Mt ni kukufanya uliamini Neno lake, yeye hukuongoza katika hilo na Ujasiri huja unapoliamini Neno. Neno nusu hukupa kiburi ambacho wengi hudhani ni ujasiri haswa vipawa vya kujitafutia vinapoinuka! Lakini njia aliyowaambia mpite ili awape hivyo vipawa mnaiona, hao wenzenu waliopewa hivyo vipawa halisi mnawaona walivyopita katika njia hiyo kwa ushuhuda wa Biblia na vifungu vyote mnavyovinukuu; walibatizwa maji mengi kwa jina la Bwana Yesu Kristo. Sasa tujifunze nini katika hili, kwamba hatuna tena uwezo wa kuiona au kuisikia Injili iokoayo? Kwamba milango ya Neema inafungwa na ushahidi ndio huu tunaouona kwa sehemu katika blog hii? Kwamba mtu atainukuu Mdo 2:38 na wala haelewi anachokinukuu, kwamba tunaendelea bila DAMU!!

  Ndugu zangu mnaopita kwenye blogu hii, tafakarini mnayoyaona humu, yakagueni kwenye Biblia zenu bila kuongeza chochote, msiache kuyaamini na kuyatimiza mnayoyaona yako sawa na maandiko. Msifanye mioyo migumu eti kwa sababu mada zilipochangiwa mlitofautiana basi kuyafuata hayo utajidhalilisha, hicho ni kiburi cha Kaini kinachokunyemelea! Hebu wazia hili kuwa hii ndiyo ilikuwa fursa pekee uliyopewa ya kuwa sawa na Mungu, nawe umeidharau, sasa umepewa roho ya kuamini fundisho lako la kutunga, ni nguvu gani iwezayo kukutoa hapo alipokutelekeza Mungu baada ya kumfanyia ujeuri!!!

  Bwana utuvumilie japo kidogo tena!

 74. Labda kwa kuongezea,ninukuu pasipo kuongeza wala kupunguza,mafundisho ya Mwalimu anayeaminika karibu na madhehebu mengi sana Tanzania na nje ya nchi,si mwingine bali Christopher Mwakasege;NANUKUU-WALIOJAZWA ROHO MTAKATIFU NI WENGI SANA;Katika eneo hili Bwana Yesu alifanya mambo ya ajabu sana.Si tu kwamba aliwajaza Roho Mtakatifu wale waliokuwa na kiu naye;bali hata wale ambao walikuwa wanapinga habari za kunena kwa lugha mpya;na hata wale ambao hawakujua kilichokuwa kinaendelea. Kuna watu waliotueleza jinsi walivyo subiri kwa hamu wapate ‘Double dose’ ya upako lakini hawakufanikiwa.Lakini walipokuwa wakirudi nyumbani kwao wakiwa ndani ya ‘taxi’ walianza kusimuliana habari za yule kijana aliyepona mguu na wakauona ukikua.Wakiwa ktk kuongea juu ya habari hiyo wakatja jina la Yesu-na mara hiyo hiyo wakashukiwa na nguvu za Mungu na kuanza kuomba hadi walipofika nyumbani kwao,na hata hivyo mmoja wao alishindwa kutembea maana alipotelemka tukutoka kwenye ‘Taxi’ alianguka chini na kuendelea kuomba.Watu wengi wakawazunguka na kushangaa kulikoni !Pamoja na kwamba Yesu hakuwapa double dose ya upako pale uwanjani,aliamua kuwapa ndani ya taxi’.Mma mwingine alishuhudia mbele ya maelfu ya watu kwamba,alikuwa anapinga habri ya kunenakwa lugha,na kwamb wale waliokuwa wanadai wananena kwa lugha mpya walikuwa wakijifanya tu.Lakini Mungu aliamua kumthibitishia jinsi alivyokosea ktk kuwaza kwake!Alisimulia ya kuwa alikuwa amekaa kwenye kiti wakati wa somo likiendelea,alishtukia ameanza kunena kwa lugha mpya !Na wakati wa maombi mwishoni mwa somo alisogea na yeye mbele ya jukwaa na nguvu zikamshukia na kunena kwa lugha mpya lakini pia na kucheka sana .Aliondoka uwanjani na kwenda nyumbani na kupanda basi huku akiendelea kucheka ktk Roho Mtakatifu.Tangu siku hiyoubishi ukaisha na ana uhakika kwamba wanaonena kwa lugha huwa hawajifanyi-bali ni halisi na ni kweli tupu.Mama mwingine alitusimulia jinsi alivyojikuta anazungumza lugha asiyoijua akiwa amekaa kwenye kiti wakati wa maombi ya ujazo wa Roho Mtakatifu,hakujua ni kitu gankimemtokea hadi tulipokutana naye baada ya semina.Tukamwambia ya kuwa kilichotokea ni alijzwa Roho Mtakatifu na ‘NA ISHARA ILIYOTOKEA KUTHIBITISHA HILI,NI YEYE KUNENA KWA LUGHA MPYA.Alipopata ufafanuzi huo alifurahi sana .Na sisi tunamtukuza Mungu pamojanaye!Sifa ni kwa Bwana Yesu Kristo.Maelfu ya watu walijazwa Roho Mtakatifu hata wengine kushindwa kutembea na kubebwa kwenda nyumbani na wengine hata kushindwa kuongea kwa muda!Laiti ungekuwepo na uone jinsi Mungu alivyotembelea na kuwajaza upako wa Roho Mtakatifu vijana.Mwisho wakunukuu,BILA SHAKA NDUGU ZANGU MNAYESOMA MAELEZO HAYA,MSHAWAHI KUHUDHURIA MIKUTANO AU KUSIKILIZA NYUMBANI MAFUNDISHO YA Mwl Mwakasege,Na lile swali lililotusumbua sana limejibiwa kupitia maelezo haya kwamba ishara ya kwanza ya mtu kujazwa Roho mtakatifu,ni kunena kwa lugha,na mwalimu huyu anaaminiwa sana na siyo sisi washirika bali hata na Wachungaji wetu,huwa tunafunga makanisa ili kupata mafundisho mazuri,je kwa usemi au msimamo wenu kwamba kunena kwa lugha,siyo ishara ya kwanza ya kuthibitisha mtu kujazwa Roho Mtakatifu,Je mnaweza kuwa na ujasiri wa kuwashauri wachungaji zenu kwamba Mwakasege anafundisha kitu ambacho si kweli ?au yapo mambo ambayo huwa hamkubaliani na Mwakasege,ila tu mnashindwa kusema ?Jamani,kunena kwa lugha ndiyo ishara ya kwanza ya kuthibitisha kwa mtu kujazwa Roho Mtakatifu,Mdo 2;4 Mdo 10;44-46,kama mnampinga mtumishi wa Mungu Mwl Mwaksege,kwa ushuhuda wake huo ambao mimi kama Noel sijaongeza kitu wala kupunguza je,mnakubali tumwite Mwakasege ni mwalimu wa uongo ?Ushuhuda huu hata mimi umenifundisha kitu sana.MUNGU ATUSAIDIE KUAMINI.

 75. Bwana asifiwe sana,Mimi naomba Mungu atufungue macho zaidi,nikiliongea hili Mngu akiwa shahidi moyoni mwangu kwamba,hakika tunahitaji nuru ya Mungu,maana ktk Marko 16;17-imeorodhesha maneno ya Yesu mwenyewe,akiahidi ishara zitakazo wapata watakao muamini,wala hakubagua ila kanuni ni ‘KUAMINI TU’ haiingii akilini,kuniambia ktk kanisa ishara hii yakunena kwa lugha,ni kwa baadhi ya watu ? Wapendwa tuwe wazi mbele za Mungu ili tupate msaada kwake,ila tusikwepe,maana hata wanafunzi waliposhindwa kuamini jambo fulani,waliomba kwamba Bwana tusaidie kuamini,nawashauri kwamba,OMBENI MUNGU AWASAIDIE KUAMINI, kunena kwa lugha,maana haiwezekani,ktk ishara zile ambazo hazikubagua mtu yeyote ila sharti la kuamini tu,wewe useme ‘kunena kwa lugha ni kwa watu fulani tu’ basi mngesema hata kutokudhurika na sumu ni kwa watu fulani tu,au kutoa pepo ni kwa watu fulani tu,kuweka mikono ili kuponya watu ni kwa watu fulani tu nk.Kwani shida iko wapi kumwambia Mungu kwa kumdai kwamba, ‘MUNGU ULISEMA KTK MARKO 16;17 BILA KUBAGUA KWAMBA ISHARA HIZI ZIMPATE NANI ILA KWA KUKUAMINI TU’ Mimi naendelea kusema KUTOKUNENA KWA LUGHA KUNATOKANA NA KUTOKUAMINI TU,BASI,MAANA NENO LIMESEMA ‘NA ISHARA HIZI ZITAFUATANA NA HAO WAAMINIO. kwahiyo hata ukimwona nani haneni kwa lugha,ujue tu hajaamini,basi.Ukisoma ktk 1Kor 2;11, inasema,NI NANI KTK BINADAMU AYAJUAYE MAMBO YA BINADAMU ILA ROHO YA MWANADAMU ILIYOMO NDANI YAKE-? ktk 1 Kor 14;2 inasema ‘ANENAYE KWA LUGHA,HASEMI NA WATU BALI HUSEMA NA MUNGU,MAANA HAKUNA ASIKIAYE;LAKINI ANENA MAMBO YA SIRI KTK ROHO YAKE. ktk 1 Kor 14;14 inasema,NIKIOMBA KWA LUGHA,ROHO YANGU HUOMBA,kwa mistari hii michache,inaonyesha ni jinsi gani ambavyo,asienena kwa lugha, kwa asilimia zote akili yake ndiyo inayoomba siku zote,na roho yake haijaomba hata siku moja na haitaomba hata siku moja,ikiwa hatanena kwa lugha,maana kunena kwa lugha kuna faida kwamba,roho yako ndiyo inayoomba,kinyume cha kunena kwa lugha,roho yako haitaomba,maana roho zetu ndizo zinazofahamu mambo yetu yote,roho haisahau,ila akili inasahau,sasa kuomba huko ambako unakwepa,kunena kwa lugha,kulingana na biblia hakika,unapoteza kitu kikubwa sana ktk maisha yako ya kiroho. Ktk Yohana 7;37-38 Yesu anasema,Mtu akiona kiu,na aje kwangu anywe,aniaminie mimi,kama vile maandiko yalivyosema,mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake,na neno hilo alilisema ktk habari ya Roho ,ambaye wale wamuaminio watampokea baadae,’KIU’ NDIO TATIZO,MAANA ILI UPATE KIU,LAZIMA ULE CHAKULA CHENYE VIRUBISHO VIZURI NA MUNYU KUKOLEA VEMA,SASA UKIPATA CHAKULA DHAIFU,HATA KIU,UNAWEZA USIIPATE, ndio maana vijana huwa wanataniana akimkuta mwenziwe anakunywa maji kwamba ”wewe unakunywa maji,UMEKULA ? maana yake baada ya chakula, hua KIU inaanza na hasa kama mwili wako uko vizuri,kwahiyo tatizo ni watu kukosa mafundisho sahihi,ndio maana wanapinga kwamba ujazo wa Roho mtaktifu unaendana na kunena kwa lugha,HAVITENGANI NG’O,WALIOJAZWA ROHO WANALIELEWA HILI,LABDA NIISHIE KUSEMA KWAMBA,MIMI NILIFIKIRI, KWA SWALI HILI LA KUNENA KWA LUGHA KWAMBA NI LAZIMA,TUNGEJIFUNZA KITU,NAKUFUNGULIWA,LABDA NIISHIE HAPA,KWA KUCHANGIA,ILI KAMA MPAKA HAPA,BADO WATU HAWAJAELEWA,BASI WABAKI HIVYO HIVYO MAANA SI SWALA LA KULAZIMISHA HATA YESU ALIFIKA MAHALI HAKUFANYA MIUJIZA MINGI KWA KUTOAMINI KWAO,MUNGU TU ATUPE MACHO,LABDA TUENDELEE NA KUCHANGIA HOJA NYINGINE TOFAUTI NA HII,NAFIKIRI INGEKUWA VEMA TUISHIE HAPA TUSIENDELEE NAYO TENA,AMINI.WALIOPATA WAWE WAMEPATA WALIOBISHA BASI.AMINI

 76. Mpendwa wangu JOEL,
  Tumshukuru Mungu wetu pamoja, kwakuwa anatufundisha anataka tuijue ile kweli, maana hiyo kweli ndiyo itakayotuweka huru. Nilidhani katika majibu yaliyopita, nitafikia katika maulizo yako yote Samahani kwa hilo. Hata hivyo, nivema niendelee mbele kwa kukujibu kama ulivyo uliza, nanukuu:- “………kwamba, ktk 1Kor 12;7-11 Karama zimetolewa kwa kufaidiana, wapo waliokirimiwa hekima,maarifa,imani,kuponya,matendo ya miujiza,unabii,kupambanua roho,aina za lugha,tafsiri za lugha, Swali ;Je sisi wengine tunaojidhani kwamba,hatuna karama nyinginezo kati ya hizo, Je hatuna hata chembe ya karama moja wapo,…… ? Mfano:kwa kuwa,Mungu hakunipa karama fulani,labda yakuponya,kwahiyo sitamuwekea mikono mtu yeyote……. ? ” Mwisho wa kunukuu. Kwakuwa maulizo yako ni yanamna moja, naomba nikujibu kwa jumla kama ifuatavyo; Kwanza nikubaliane nawe kwamba yaliyosemwa katika 1kor.12:7-11 Nikweli kuwa, Roho mtakatifu, hutoa karama kama apendavyo kwa ajiri ya mahitaji ya Kanisa, na si vinginevyo! Swali lako kwamba, Unajizania huna karama; je, huna hata chembe ya karama zinginezo? Umeuliza kama unajizania huna karama ya jambo fulani, lakini ikatokea shida inayohitaji jawabu la mwenye karama husika, je huwezi kumhudumia? Kwanza kwa mjibu wa hiyo 1kor 12:7 -11, imeainisha wazi, kuwa Roho hutoa karama kwa kufaidiana, sasa basi lengo la matumizi au manufaa ya karama hizo ni KWA MATUMIZI YA KANISA LAKE! Sisi sote tuliookoka ndiyo hilo kanisa lake. Naye Roho mtakatifu ambaye kwakweli ndiyo Yesu mwenyewe, ndiye mwenye karama hizo, na ndiye mwenye kuzitoa kama aonavyo. Kama ndivyo hivyo, basi swala la kujidhania HALIPO – kwa hiyo kuwa au kutokuwa na karama si swala la DHANA, ni maandiko! Biblia imejaa ahadi kwa kanisa, na mojawapo ni hilo swala la vipawa vya Roho mtakatifu. Lengo kuu la ahadi hizo ni kujenga kanisa imara la Yesu Kristo, lisiloweza kutikiswa na nguvu yoyote ya kuzimu! Iko pia haki ya kuomba kwake majibu ya matatizo yetu, maana sisi tumefanywa kuwa ni watoto wake, hivyo tunazo haki za kitoto kwake! Kutojua au kuwa na dhana mioyoni, badala ya kuwa na hakika, ya unachostahili katika yaliyoahidiwa,inatokana na Mtu mwenyewe kutokuijua ipi ni haki yake kwa Mungu apate kuidai – na kama Mtu hajui hilo, basi, niwazi pia hana hakika kama ni Mtoto wa Mungu! Kama ni hivyo, ni vema Mtu aanze na hilo, ili kujihakikishia pasipo na mashaka yoyote kuwa ni Mtoto wa Mungu. Kwa maana baba ana wajibu wa kumpa mtoto wake haki yake, vivyo hivyo, mtoto ana haki ya kuidai haki yake kwa baba yake. Sasa, sisi tukiwa watoto wa Mungu lazima tuzijue haki zetu zote, ili tupate kuzidai. Hata inapotokea kupewa tu bila kuziomba (Kukirimiwa) yatupasa kujua kuwa ni kweli ni stahili yetu ili tuilinde, tuitunze na kuitumia kwa uaminifu ipasavyo. LAKINI, yapasa uelewe kuwa hakuna HAKI pasipo na WAJIBU. Hili ndilo la msingi sana kujua, wajibu wako ni upi ulikufanya uwe na haki ya kudai Ahadi unayoamini kuwa ni Ahadi ya Mungu kwako kama Mtoto wake? Nimalizie kwa kusema hivi; KWAKUWA AHADI NI DENI,YAKUPASA UJUE NI KIGEZO GANI UTATUMIA KUDAI AHADI HIYO. NENO LA MUNGU LIMEAHIDI KUMPA MTU KIPAWA IWAPO ATATEKELEZA YALIYOANDIKWA KATIKA Mdo 2:38 ambayo kwa uwazi yanasema; “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, NANYI MTAPOKEA KIPAWA cha roho mtakatifu” Kwakuwa hilo ni NENO la Mungu,nasikitika kuwa hatuna uwezo wa kulipinda, ila nakushauri ufuate kama linavyoagiza ili uwe na haki ya kudai Ahadi zako zote ikiwemo na ile ya kupokea VIPAWA kama Mtoto halisi wa Mungu! Usiache kunilejea kila unapoona kuwa inafaa. Ubarikiwe Sana!

 77. Mabinza, ahsante, nimekuelewa,umejibu vizuri, kwamba,ahadi hizi zinawapata waaminio,yaani waliondani ya neno. Lakini swali langu lingine,hujalijibu, kwamba, ktk 1Kor 12;7-11 Karama zimetolewa kwa kufaidiana, wapo waliokirimiwa hekima,maarifa,imani,kuponya,matendo ya miujiza,unabii,kupambanua roho,aina za lugha,tafsiri za lugha, Swali ;Je sisi wengine tunaojidhani kwamba,hatuna karama nyinginezo kati ya hizo, Je hatuna hata chembe ya karama moja wapo,kwa kuwa tu tumejidhania kwamba hatukukirimiwa ? Mfano:kwa kuwa,Mungu hakunipa karama fulani,labda yakuponya,kwahiyo sitamuwekea mikono mtu yeyote,kwa kuwa mimi najidhani sina karama ya kuponya ? Kwa kuwa ipo karama ya hekima,kwahiyo mimi sina hekima kabisa yaani ni zero wa hekima ? yaani,hata kupambanua roho,sina hata chembe,kwa kuwa Mungu hajanikirimia hata kama mtu aseme,Yesu si mwana wa Mungu,sitaweza kupambanua,mpaka aje mwenye karama hiyo ya kupambanua ? Mfano halisi;Kaseja ana kipawa cha kudaka,je akiingizwa ndani,hataweza kucheza kabisa,kwa kuwa yeye kipawa chake ni kudaka tu ? au kushindwa kwake kucheza namba za ndani ni uzembe wake na woga,je si kwamba kama Kaseja atapewa namba za ndani,atacheza,lakini akikaa golini atafit zaidi ?

 78. Wapendwa nimefurahi sana, kwakuwa naendelea mbele katika kujifunza kutoka kwenu.Nakubaliana na ndg. Orbi na Ndg. Sam kwa mafundisho kwamba Neno la Mungu halina mapungufu na kwamba hilo pekee liachwe kuwa ndicho kipimo pekee cha ukweli wa Neno la Mungu. Nimeelewa pia kwamba, tafsiri na msimamo wa mtu kutotoka katika aliyoyakopi katika mafundisho ya kidini ni kikwazo katika kumjua Mungu na mapenzi yake!
  NDUGU YANGU NOEL,
  Nimepitia katika post yako ya tarehe Friday, March 30, 2012 at 2:06 Nimeona umeuliza maswali kadhaa – ambayo yote naweza kuyaweka ktika kundi moja, na kuyajumuisha katika jibu la jumla maana kama sikosei, unataka kujua inakuwa je, iwapo Mtu anapatwa na tukio “Lisilo zuri” kinyume na ahadi “Nzuri” za YESU ambaye ndiye pia ni Roho mtakatifu. Umeandika nanukuu baadhi, “……… Bwana YESU aliposema,ktk Mark 16;17 kwamba ‘Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio,kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka;hata wakinywa kitu cha kufisha,hakitawadhuru kabisa,wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,nao watapata afya, SWALI;Je ikitokea amekufa muumini aliyeahidiwa na Yesu kwamba hata akinywa sumu,(kwa bahati mbaya) haitamdhuru kabisa, je itakuwa ROHO MTAKATIFU AMEPENDA ?, kwa kuwa yeye Roho mtakatifu hakupenda kumpa ile karama ya kutodhurika yule muumini marehemu ingawa Yesu alituahidi ? nk…” Ndg. Yangu, elewa hivi; AHADI HIYO NI YA KWELI KABISA,LAKINI KWA YEYE TU AAMINIYE – MAANA HUWEZI KUJIITA KUWA UNAAMINI, IWAPO UTAKUWA UMEURUKA , HATA MSITARI MMOJA TU WA NENO LA MUNGU KWA UBISHI AU KWA MAKUSUDI AU KWA SABABU ZAKO ZOZOTE ZILE, UTAKUWA UMEKOSA HAKI YA AHADI HIZO; Biblia haina tukio la “BAHATI MBAYA” Na hilo pekee ndiyo kanuni ya kupimia, madai ya wote wanao dai kwamba, wamepokea Roho mtakatifu, na kwamba wanaishi naye, ILI KUAMINISHA kwamba, yale yote wayasemayo na kuyafanya yanatokana na Neno la Mungu. Biblia inasema ; Mt 24:35 Mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe! – hapo jua kwamba, kilichonenwa kimenenwa na kwamba hakuna tukio la BAHATI MBAYA kwa mtu wa kristo! kwa kifupi sana ni kwamba, aliye katika kristo Yesu HAPATWI na jambo lililo nje ya ahadi yake kwa watu wake! Lk 11:28 inasema; “Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na KULISHIKA” Yote yanatupata si kwa bahati mbaya, bali yanatupata sawa sawa na Neno la Mungu. Ijulikane tu wazi kuwa, ukiwa Nje utapatwa ya walio nje, na ukiwa ndani ya Neno utapatwa na yaliyomo ndani. Soma Yn 5:38 “Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwakuwa ninyi hamwamini yule aliye tumwa na yeye” .
  Umesema, nanukuu, “…………… kwa kuwa yeye Roho mtakatifu hakupenda kumpa ile karama ya kutodhurika yule muumini marehemu ingawa Yesu alituahidi……..” mwisho wa kunukuu. Soma kwa utulivu Mdo 2:38, inasema “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, NANYI MTAPOKEA KIPAWA cha roho mtakatifu” Kupokea kipawa au karama za Roho mtakatifu ni AHADI si jambo la bahati na sibu,eti kwamba kapenda na eti hakupenda! NI AHADI YA MUNGU KUWA TUMUOMBE, NAYE ATUPE TUMWOMBACHO. Mt 7:7,8. Tatizo ni kwamba watu hujiaminisha kuwa, wana haki ya kupata kipawa bila haja ya kuzingatia matakwa ya mstari huu wa Mdo 2:38, kwa kuyatimiza matakwa ya mstari huu ndipo mtu atapata kipawa cha Roho mtakatifu. Ukisoma ; Isa 55:11 Mungu anasema “………kwa maana Mungu atalifanikisha Neno lake katika kila jambo alikolituma……” Hivyo hakuna kufa au kupatwa madhara kwa bahati mbaya, eti kwa sababu ya kubahatisha kwamba, Roho mtakatifu alipenda au hakupenda,. NENO litafanya kama lilivyo tumwa (kunenwa) Hakuna kubahatisha wakati unalo Neno la Mungu wa kweli. Maana hata kipawa kipo kutokana na Neno la Mungu! Tazama. Kwakukosa kuyaamini maneno ya Mungu, watu wengi hawana kipawa cha Roho mtakatifu hatakimoja! Pengine utashangaa na kujiuliza, mbona kuna watu wanafanya matukio na ishara mbali mbali, bila kwakweli kutimiza yaliyomo kwenye Mdo 2:38?! Jibu ni lahisi na fupi sana, NI kwamba; NENO LA MUNGU LINASEMA WATU KAMA HAO WATAKUWEPO KWA WINGI, Soma 1Yn 4:1, hivyo hawaishi wapo PICHA TU ZA MAIGIZO, UKIWAONA UTADHANI WANA VIPAWA VYA KWELI , KUMBE VIPAWA MFU, MAANA JAPO KWA MACHO YA NYAMA UNAWAONA,KUMBE, KWAKWELI WENYEWE TAYARI WALISHA KUFA ZAMANI! – Maana bila kuamini HATA MSTARI MMOJA WA NENO LA MUNGU UMEKUFA! Mtu utamkuta amekalia tu kwakujivuna kwa ujuzi wa Roho yake, na kusikizishwa mafundisho ya Dini yake huko makanisani; kumbe masikini mtu huyo alisha jifia zamani, na kwavyovyote hana haki ya kuishi! Neno linasema hivyo katika; Habakuki 2:4 BILA KUAMINI HUWEZI KUISHI – MFU HAWEZI KUWA NA VIPAWA, KUMBE AKAVITUMIE WAPI, KUZIMU? – Kaka, mtu wa jinsi hiyo hatakama atunywa sumu hiyo kwa bahati nzuri namna gani, kufa lazima afe!. Ubarikiwe kaka yangu.

 79. Ndugu Orbi,

  Shalom!

  Ndugu yangu, pole sana. Naona ulipoisoma post yangu, hukuiangalia tu kwa utulivu, maana nilichokisema chenye upungufu ni “fundisho la ‘KUNENA KWA LUGHA NI ISHARA YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU’ lina mapungufu au si la ki-maandiko licha ya kuzoeleka hivyo”. Maandiko hayana mapungufu yoyote na hata uelewa wetu wa maandiko hautakuwa na upungufu iwapo tutaongozwa na Roho Mtakatifu.

  @Ndugu Masanjila
  Jitahidi kuyapa maandiko nafasi yake. Mungu sio mtoto mdogo hata sisi tumsemee! Ishara zinatokana na Mungu, kwa hiyo ni vizuri kumtazama yeye kwa ajili ya kuongozwa katika njia yake. Hauwezi ku major in a minor! Kunena kwa lugha, sio major bali ni mojawapo ya vipawa. Matumizi yake ndiyo yanachokifanya kipawa hicho kitumike kama kilivyo katika Biblia; kutoa ushuhuda wa mambo makuu ya Mungu! Na pia kipawa hicho hukuwezesha kuongea na Mungu kibinafsi katika faragha na si katika makusanyiko. Tena Roho Mtakatifu akiwepo huratibu vipawa vyote kanisani.

  Ishara zinabaki kuwa Ishara, naye Roho Mtakatifu hageuki kuwa Ishara! Hebu watazame wale 70, waliambatana na ishara, na Yuda Iscarioti alikuwemo kati yao. Waliponya wagonjwa, kukemea pepo nk. Je, walijazwa Roho Mtakatifu? Hawakujazwa ! Sasa, leo wakiwepo wa jinsi hiyo, kwa ishara wanazotufanyia, tunakuwa wepesi wa kuyapokea yote wanayotuletea bila ya kuchukua wasaa wa kuyakagua mambo hayo kulingana na maandiko, kama tulivyokupokea kunena kwa lugha!

  Ni vizuri kurudi katika Biblia na kujitazama katika kioo hicho ili tujione iwapo tunastahili mambo hayo kulingana na Neno. Roho Mtakatifu ni Kristo ndani ya muumini, kama alivyokuwa ndani ya Paulo au Stefano na wengineo, huo ndio ushuhuda wa umilikaji wake. Petro na mitume wote walikuwa na wale 70, hata wakajisifia kwa mambo makuu waliyoyafanya, lakini pale bustanini walitimua mbio! Ila BAADA YA KUJAZWA ROHO MT., cowardice iliwaondoka na badala yake wakawa JASIRI!!!! Basi kama kunena kwa Lugha ndio kujazwa Roho Mtakatifu, tungeuona ujasiri wa KUSHIKAMANA NA NENO kwa hao wenye kunena. Lakini hatulioni hilo, hata kwenye mambo ya msingi kama ubatizo wa ondoleo la dhambi kama Injili ilivyouweka katika Mdo 2:38, tunashindwa kulisahihisha hilo kwa kukosa ujasiri!

  Mbarikiwe nyote!!

 80. Bwana YESU aliposema,ktk Mark 16;17 kwamba ‘Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio,kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka;hata wakinywa kitu cha kufisha,hakitawadhuru kabisa,wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,nao watapata afya, SWALI;Je ikitokea amekufa muumini aliyeahidiwa na Yesu kwamba hata akinywa sumu,(kwa bahati mbaya) haitamdhuru kabisa, je itakuwa ROHO MTAKATIFU AMEPENDA ?, kwa kuwa yeye Roho mtakatifu hakupenda kumpa ile karama ya kutodhurika yule muumini marehemu ingawa Yesu alituahidi ? nk. na ktk 1 Kor 12;7-11, kuna karama tofauti, waliopewa hekima-je sisi wengine hatuna hekima hata kidogo ila tu kwa waliokirimiwa hekima ? na sisi wengine hatuna maarifa kabisa ila kwa waliokirimiwa maarifa tu ? je sisi wengie hatuna imani hata kidogo,isipokuwa kwa waliokirimiwa imani ? je ikitokea muislamu aseme Yesu si Mwana wa Mungu,je wewe hutaweza kupambanua,kwamba hiyo ni roho ya namna gani mpaka ukamwite mwenye karama ya kupambanua roho ? ASANTENI,BARIKIWENI NA BWANA

 81. Sam,

  Ubarikiwe,

  Nashukuru sana kwa mchango wako na hasa kama umejifunza kitu……Jambo ambalo Nataka kuweka sawa ni kuwa hakuna ANDIKO LENYE MAPUNGUFU kama ulivyosema….! Bali tafsri zetu kama wanadamu……na wigo wa ufahamu wetu ndio una mapungufu….Andiko au Maandiko ya Kunena kwa Lugha/Kubatizwa/Kujazwa Roho Mtakatifu….. yana uvuvio MKUBWA kabisa sawa sawa na Maandiko mengine yoyote yale katika Biblia…..huu ndio mtazamo wangu…..!

  Swali ni kuwa …….Je tunayatafsri kama yalivyo.? Je maana yetu “TUNAYOIVALISHA” katika Maandiko hayo ndiyo ile ile ambayo Mwandishi aliyeandika akivuviwa na Roho Mtakatifu alikuwa akiimaniisha….? Kitu kikubwa cha kujizuia ni kutoweka maana zetu katika maneno ya Mungu……Au kulazimisha Maandiko yatoe jibu tunalolitaka sisi…….! Tusiilazimishe Biblia iseme kama dhehebu letu…….au waalimu tunaowaamini na kuwathamini wanavyosema…..au kuupindisha ujumbe wa Biblia useme kile ambacho tumezoea kukisikia……!Acha Maandiko yajitetee yenyewe……maana yana nguvu hiyo…..ni Upanga ukatao kuwili…..!

  Hivyo tunapo Soma Maandiko ni LAZIMA PIA KUOMBA Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu atufunulie maana ile ile aliyoitaka……Na pia kutumia kanuni ya kuyatafsri Maandiko kwa kutumia Maandiko….hii ndio njia salama….!

  Ombi langu ni kwamba mada hii itusaidia kuliweka fundisho la Kunena kwa Lugha/Kujazwa Roho Mtakatifu/Kupokea Roho Mtakatifu mahali pake halisi katika Maandiko…..!

  Amen.

 82. BWANA YESU ASIFIWE
  POLE KWA KAZI WAPENDWA.
  Ndugu yangu, NOEL;
  Nimefurahi kwa kuainisha kile ambacho sikueleweka, na huko ndiko kujifunza. Kwakuwa kwingine kote nimeeleweka, nitanzia katika kukujibu kama ulivyouliza. Umeuliza….nanukuu “……Lakini pia NIKUJIBU NDUGU YANGU MABINZA,AMBAYE HUJAAMINI PAMOJA NA WENGINE, KUWA ISHARA YA MTU KUWA AMEJAZWA ROHO MTAKATIFU NI KUNENA KWA LUGHA,NAOMBA UTAFSIRI MAANDIKO HAYA KWA UNAVYOELEWA WEWE (Mdo 19;6) ”…….. na (Mdo 2;4)……….NAOMBA TAFSIRI KWA MAANDIKO HAYA MACHACHE TU,TAFADHARI MABINZA NA WENGINEO,TAFSIRI YA HAPO TU. MUNGU ATUBARIKI SOOOTE” mwisho wa kunukuu.
  Mpendwa, mimi SIKATAI kwamba Mtu akijazwa Roho mtakatifu HANENI kwa lugha, NINACHOSEMA; kunena kwa Lugha si LAZIMA kuwa ni ISHARA au kigezo pekee kwamba Mhusika amejazwa Roho Mtakatifu, na kwamba wote wasionena kwa Lugha Roho mtakatifu HAYUMO ndani yao!. Nasema kwamba, kunena kwa lugha ni mojawapo ya vipawa vinavyotolewa na roho mtakatifu kwa kadri ya yeye Roho Mtakatifu anavyomjalia mtu kunena ( Mdo 2;4 – Wote wakajazwa Roho mtakatifu,wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka,)- Mstari huo ni wazi hausemi kuwa, ukijazwa Roho mtakatifu ni LAZIMA unene kwa Lugha…..bali, kinasema ni MAJALIWA! Naendelea mbele, katika mstari uliounukuu wa –Mdo 19:6…mstari huo unasema,…” Na Poulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa Lugha, na KUTABIRI….Sasa hukuumaliza mstari wote, ungeumliza wote, ungejua kuwa hawakunena kwa Lugha tu bali pia WALITABIRI,…..wewe uliishia ”……..Roho mtakatifu akaja juu yao;wakaanza kunena kwa lugha” Naendelea mbele kusisitiza kwamba, kujazwa Roho mtakatifu, si LAZIMA ujulikane kutokana na kunena kwa Lugha! Kuthibitisha hilo soma; Mdo 4:31 – inasema “31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU, WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI. Unaelewaje hapo, walinena kwa Lugha baada ya kujazwa Roho mtakatifu walipokwisha kuomba? Labda utasema kwamba,huko nyuma wlikwishajazwa na wakanena kwa Lugha, sasa hapo si lazima kurudia kunena! Aliyekuwa akiongoza maombi hayo alikuwa petro na yohana( hao sawa walishanena labda sawa na Mdo 2:4), lakini pale walikuwepo watu wengine wengi ambao ndiyo ilikuwa mara yao ya kwanza.
  SAMBAMBA NA HILO HEBU SOMA; Mdo 4:4 – panasema,”4 Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano”. kisha lukia mstari wa23 hadi wa 24 – pasema; “23 Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao,wakawapasha habari ya mambo yote……. 24 Nao waliposikia, wakampazia Mungu zao,……..” Ndipo sasa uje ule 31 niliokutajia mwanzo. Ambapo pana hitimisha kwa kusema; 31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa roho mtakatifu, wakanena neno la mungu kwa ujasiri. Hapo utaona kuwa wao walipojazwa Roho mtakatifu, hawaku nena kwa LUGHA bali walinena NENO LA MUNGU – naweza kusema kuwa hapo Roho mtakatifu ALIWAJALIA kushuhudia Injili ya Bwana Yesu kwa ujasiri!
  Kama kunajambo ambalo sijaliweka sawa, naomba uniambie kwa kusimamia vifungu kama ulivyofanya,ili tulijadili wote,nitapenda kusikia maoni na mtazamo wako katika mada hii. Ubarikiwe sana.

 83. Wapendwa, katika Kristo,

  Kwa kweli, michango mliyoitoa ni changamoto kubwa saaana! Mjadala ni mkali na wenye manufaa sana kuliko wengi wetu tulivyoudhania ulipoanza.

  Umbali huu tuliofika yaonekana wazi, kwa rejea ya maandiko, kuwa lile fundisho la “KUNENA KWA LUGHA NI ISHARA YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU” lina mapungufu au si la ki-maandiko licha ya kuzoeleka hivyo. Basi fundisho hilo yaonekana pia kuwa ndilo sababishi ya kuzagaa kwa kunena kwa lugha zisizoeleweka lakini zikikubalika!

  Jambo hili laonesha kuwa hatukumpokea Roho Mtakatifu, huenda ni msisimko tu unaoambatana na Roho Mpya tunayopewa kulingana na utaratibu wa Wokovu wetu. Yaani zile hatua tatu: Kuhesabiwa Haki kwa Imani; Kutakaswa na mwisho Ubatizo wa Roho Mtakatifu.

  Mkristo hupita katika mabadiliko haya katika hatua hizo, na hayo yote huambatana na misisimko haswa zile hatua mbili za mwanzo, hizo hutubadilisha sana kutoka yule mtu wa kale. Uzima wa Mungu huanza kumuingia mkristo katika hatua hizo na kufikia kipeo chake katika hatua ile ya tatu ambayo Roho Mtakatifu hutushukia kukaa ndani yetu, ambaye ndiye ile nguvu ya ufufuo. Yoh 11:25 “… Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi …”

  Basi Roho Mtakatifu ndiye Ufalme wa Mungu. Nayo maandiko yanatuambia siku Roho Mtakatifu akitushukia, tutajua; siyo tutanena kwa Lugha! Yeye ni “Nguvu” akitushukia tutaipigania IMANI (Neno lake) na si mafundisho yetu!!!

  Katika “miwani ya maandiko” basi yaonekana sote, tuliokataa kunena kwa lugha na tulioneneshwa nje ya utaratibu wa Mungu, tuna makosa ya ‘Kupunguza’ na ‘Kuongeza’ katika maagizo ya Mungu. Makosa ambayo Biblia inaainisha adhabu yake katika Ufu 22:18! Ndugu zangu hivyo ndivyo ilivyo rahisi kutumbukia katika dhambi!!!

  Sasa, “Tutendeje ndugu zetu???”; Swali hili lina umri wa zaidi ya miaka 2,000 na bado li hai kwa yeyote anayeujia Ufalme wa Mungu. Pia Jibu lake liko vilevile, maana Mungu habadiliki, “Ni yeye yule, jana na leo na hata milele”. Wala hajabadilisha njia yake, ichukue Njia yake aliyotutayarishia na kuwapa watumishi wake tuifuate: Mdo 2:37-38 “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Kwanini mjihangaishe na vipawa feki wakati halisi vimejaa! Angalieni wenzetu wa Mdo 19:1-5, hawa walikuwa wamepitia zile hatua mbili kama sisi tulivyozipitia kwa kuipokea Injili na kubatizwa kwa ubatizo tofauti tofauti uliotuingiza katika madhehebu yetu, sasa twapaswa tupige ile hatua KUU, nasi tubatizwe katika jina la Bwana Yesu Kristo kama wenzetu hao, naye Mungu anawajibika kutufanyia kama wenzetu kulingana na Ahadi yake; “Ahadi hii ni kwa ajili yenu, … na kwa WATU WOTE WATAKAOITWA NA BWANA MUNGU WETU WAMJIE!!

  Ndugu zangu wapendwa, tusirudi tena kwenye mioyo migumu ya mawe tuliyokwisha kutolewa na kupewa hii ya nyama inayoweza kulihifadhi Neno la Mungu, bali twendeni tutiwe muhuri (“…Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri …” Efe 4:30) na tuingie Yerusalemu Mpya!!

  Bwana Tujalie ile “NGUVU” ya Ufufuo!

 84. Glory…Glory…

  Orbi……Nina furaha kuwa umesikia na kutii sauti ya Roho Mtakatifu kwa unyenyekevu kwa.yote aliyokushuhudia, Na pia kuendelea kuchangia,Nilipokuwa natafakari uamuzi wako na wa Mpendwa Asheri kusimama kwa muda kuchangia nilikutana na mistari hii ktk pitapita ya kusoma maandiko

  Mathayo24:45-47

  “Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu, mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya. Amini, nawaambieni atamweka juu ya vitu vyake vyote”

  Wana SG,Nawaombea dua pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote.sisi SOTE tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake Bwana….ndiyo……. ni siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

  Nina kila sababu kuwakumbusha kuwa hii ndio HUDUMA tuliyoiitiwa, kuna mitume,manabii,wainjilisti,wachungaji na walimu mahala hapa,tunawafikia maelfu kwa elfu hata miisho ya nchi kwa hii teknolojia ya habari,Watu wanapokea/ponywa/funguliwa,Utukufu ni kwake Kristo Bwana.

  kwa dhati kabisa naomba wale walioacha kuchangia kwa sababu moja au nyingine Shetani ashindwe,Na tuendelee kujishikamanisha pamoja ktk upendo wa kindugu tukitafakarI mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,

  Ndugu siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu.(wana SG)

  Wapendwa, ninaowaonea shauku.

  Amen

 85. Asante kwa maelezo na ushauri wenu,Lakini naomba sasa nielewe kuwa,je mjadala huu unaishaje,je kila mtu amebaki kama alivyokuwa anaamini kabla ya mjadala ? Maana swali ni Je NI LAZIMA KILA MKRISTO KUZUNGUMZA KWA LUGHA MPYA AU KUNENA KWA LUGHA ? Swali hili linajibiwa na YESU mwenyewe ktk Marko 16;17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya. Mbona kitu kiko waaazi kabisa,hivi tunapishania wapi ? hivi Yesu ameshasema kwamba,tutashika nyoka;hata tukinywa kitu cha kufisha;hakitatudhuru kabisa;wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,nao watapata afya,swali, Je ikitokea umekunywa kitu cha kufisha,halafu ukahangaika na hiyo sumu bila hata kumdai Mungu kwamba,MUNGU ULISEMA HATA TUKINYWA KITU CHA KUFISHA,HAKITATUDHURU KABISA, je siutakuwa mjinga au mpumbavu ? maana hiyo ni ahadi ya Mungu kwa waaminio,sasa UNATAKA MUNGU ASEMAJE AU AFANYEJE KAMA HUMDAI…. ? AU NDUGU YAKO UNAMUONA ANAUMWA HOI,NA PEPO LA MAUTI LIMEMZINGIRA KABISA,NA WEWE HATA HUWEKI MIKONO YAKO JUU YA MGONJWA NA KUOMBA AU KUKEMEA,JE UNATAKA MUNGU AFANYEJE,YAANI HUJAWAHI HATA SIKU MOJA KUDAI ALICHOAHIDI MUNGU,LAKINI UNABISHA TU,JE MUNGU AFANYEJE,KAZI NI KWAKO KUJISEVIA CHAKULA KIPO MEZANI,MUNGU AFANYEJE ? KWANI UNAWASIWASI GANI NA KUNENA KWA LUGHA SI MDAINI MUNGU, JE AKITOKEA MTU AKAUMWA NA NYOKA HALAFU AKAKEMEA TU NA ILE SUMU IKATOKA,JE HUTAAMINI KWAMBA HUYU NI MGANGA WA KIENYEJI,MAANA MAWAZO YETU WENGI TUMEYAZOEZA KTK KUONA MAMBO YA WAGANGA TU,MUNGU AKITENDA TAYARI TUNAKUWA NA MASHAKA , MAANA HATA SIKU YA PENTEKOSTE WAPO WALIODHIHAKI WAKISEMA WAMELEWA KWA MVINYO MPYA WAKATI WATU WAMEJAZWA ROHO MTAKATIFU NA KUNENA KWA LUGHA,WATU HAWAJAONA UMUHIMU WA KUNENA KWA LUGHA NDIO MAANA,WAKO RADHI KUFUATILIA KUPONYWA MAGONJWA YA MWILI MPAKA LOLIONDO,LAKINI HABARI YA KUNENA KWA LUGHA AMBAYO NDIO YA MSINGI WA YOTE,HATA HAWANA HABARI NAYO,INGAWA YESU ALIVIORODHESHA VYOTE PALE KAMA ISHARA YA MKRISTO ALIYEMUAMINI YESU,( Mdo 2;13 ) kwa kuwa waliwasikia watu wakinena kwa lugha mpya kwao; PIA KUNA SHIDA NIMEIONA,KWAMBA NI LUGHA IPI NI YA ROHO MTAKATIFU; JIBU (1) LUGHA ISIYOELEWEKA KWA MTU YEYOTE DUNIANI ILA MUNGU TU (1 Kor 14;2) ‘maana hakuna asikiaye ;lakini anena mambo ya siri ya roho yake’ (2) Mdo 2;7 b-8,tazama,hawa wote wasemao si wagalilaya ?Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo ? MAANA YAKE UNANENA LUGHA AMBAYO SI YAKO,LAKINI MWENYE LUGHA,ANAKUELEWA VILIVYO. TATIZO LINGINE NIMELIONA NI WATU WANATAKA INGEKUWA HIVI KWAMBA,WANENAJI WANENE KWA MAKABILA YANAYOELEWEKA KTK SEHEMU ILE HALAFU,IWE RAHISI MWENYE KABILA MMOJA WAPO KUTAFSIRI, NASEMA INGEKUWA HIVI BASI KARAMA YA KUTAFSIRI ISINGEKUWA NA KAZI,MAANA HATA MTU AKINENA KISUKUMA AU KIGOGO NK, ANATAFUTWA TU MSUKUMA AU MGOGO NA ANATAFSIRI,KWAHIYO ILE KARAMA YA TAFSIRI ZA LUGHA TUTAIWEKA WAPI KAMA WATU WATANENA TU KWA KABILA ZAO KAMA WATAKAVYO WAO 1 Kor 12;10 -‘karama ya tafsiri za lugha’ kwahiyo tukinena tu kwa lugha za kueleweka za makabila yetu ya kisukuma na wagogo nk na kupata ile tafsiri kwa mtu wa kabila ile,karama ya kutafsiri,tutaisemaje ?.Lakini pia NIKUJIBU NDUGU YANGU MABINZA,AMBAYE HUJAAMINI PAMOJA NA WENGINE, KUWA ISHARA YA MTU KUWA AMEJAZWA ROHO MTAKATIFU NI KUNENA KWA LUGHA,NAOMBA UTAFSIRI MAANDIKO HAYA KWA UNAVYOELEWA WEWE (Mdo 19;6) ”Roho mtakatifu akaja juu yao;wakaanza kunena kwa lugha” na (Mdo 2;4) Wote wakajazwa Roho mtakatifu,wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka,NAOMBA TAFSIRI KWA MAANDIKO HAYA MACHACHE TU,TAFADHARI MABINZA NA WENGINEO,TAFSIRI YA HAPO TU. MUNGU ATUBARIKI SOOOTE.

 86. HALELUYA!
  Nimefurahi sana jinsi uchangiaji wa hoja hii ulivyo mzuri, mimi nimejifunza mengi na naamini na wengi watajifiunza pia kwani hii mada imeleta sana utata na hata kuwagawa wakristo katika makundi makundi kitu ambacho hata mtume Paulo alikikemea akisema,’kwani Kristo amegawanyika?’
  Kubwa nililoliona hapa ni kwamba tunapaswa kutambua kuwa kwanza inatupasa kutafuta UFALME WA MBINGUNI NA HAKI YAKE,na haya mengine tutazidishiwa tu,MATHAYO 6:33.
  Kumbukeni kuwa Yesu mwenyewe alipinga sana suala la watu KUTAFUTA ISHARA TU,na kuacha kushughulikia mambo ya ufalme wa mbinguni,akisema,’KIZAZI HIKI CHA ZINAA KINATAKA ISHARA,HAKITAPATA ISHARA ISIPOKUWA YA YONA’

  MTAZAMO WANGU NI KWAMBA WATU WAJISHUGHULISHE KUTAFUTA UFALME WA MBINGUNI NA AUTOMATICALLY MUNGU ATAWAPA VIPAWA VYA KUFANYA ISHARA MBALIMBALI KATIKA UTUMISHI WAO KWANI ISHARA HAZITAKUPELEKA MBINGUNI ILA NI UTAKATIFU TU.
  WENGINE WATASEMA TULITOA PEPO KWA JINA LAKO LAKINI ATAWAAMBIA SIWAJUI NINYI!
  NIMEBARIKIWA!

 87. Wapendwa

  Imebidi nirudi tena, Kwanza baada ya kurudia post mbali mbali nimeona nahitajika kumuomba msamaha ndugu Asheri…..kwani nilipotamka mambo ya dhehebu dhidi yake inaoneka nimemkwaza….kwa hivyo naomba sana msamaha kwa hilo….Labda kwa kumjibu ndugu Asheri nilimchanganya na Ndugu yangu Noeli Masanjila.

  Hata hivyo Naomba tena wachangiaji kwa kuendeleza kujifunza naomba mnieleze upya tena ……..Je Ni Kweli kwa Kutumia Maandiko ya Agano Jipya Kunena kwa Lugha ni Ishara Pekee tu…?Utasemaje juu Maandiko juu haya……?

  1. “KWA SABABU ATAKUWA MKUU MBELE ZA BWANA HATAKUNYWA DIVAI WALA KILEO NAYE ATAJAZWA ROHO MTAKATIFU TOKA TUMBONI MWA MAMA YAKE (Luka 1:15) Huyu ni Yohana Mbatizaji……

  – Hili ni Agano jipya…….maana Kitabu cha Malaki (Miaka mia nne nyuma kimefunga Agano la Kale) Je ALINENA KWA LUGHA tumboni mwa mama yake……?Je Kujazwa huku kwa Roho Mtakatifu si kulimfanya Yohana Mbatizaji azaliwe akiwa na Nguvu za Mungu…….Je Nguvu hii si ishara tosha ya Kujazwa Roho Mtakatifu?

  – ELIZABETI AKAJAZWA ROHO MTAKATIFU AKAPAZA SAUTI KWA NGUVU AKASEMA UMEBARIKIWA WEWE KATIKA WANAWAKE NAYE MZAO WA TUMBO LAKO UMEBARIKIWA (LUKA 1:42) (Hapa inasema akapiga sauti kwa Nguvu….! Utasemaje juu ya Msimamo wangu kuwa Nguvu ya Kutangaza Ujumbe wa Mungu nayo ni Ishara ya Kujazwa Roho Mtakatifu….! Si kunena Lugha ngeni tu….?

  Kwa hiyo mtu akisema UNAWEZA KUJAZWA MTAKATIFU ROHO BILA KUNENA KWA LUGHA kwa kutumia Maandiko haya unamakosa….?Maneno haya haya ( MTAPOKEA NGUVU/MTABATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU/WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU) katumia Luka mwandishi wa Kitabu cha Luka na Matendo ya Mitume….!

  Wapendwa hatujengi doctrines kwa andiko moja tu……..hata andiko moja tu likipiga Kelele ndani ya Biblia unalisikiliza……na unalipa nafasi….!

  Petro alipotetea kunena kwa Lugha siku ya Matendo ya Mitume alitumia Andiko la Yoeli 2:28-32) Andiko hili halina kabisa KUNENA KWA LUGHA……Je Roho Mtakatifu ambaye aliyemvuvia Petro atamke nukuu hii ya Yoeli alifanya Makosa….? Au andiko hili liko kwa bahati mbaya….? Hebu hesabu Ishara katika kitabu cha Yoeli……hebu nenda Agano la Kale usome kifungu hicho kizima…!

  Kama unayaheshimu MAANDIKO na kuyaacha yapige kelele yenyewe utasema kuwa Roho Mtakatifu anaposhuka anakuja na udhihirisho wa aina mbali mbali (Diversity of Experiences) ndio maana Roho Mtakatifu Mwenyewe alimuongoza Petro kunukuu kifungu hiki…..!Na maadamu kifungu hiki cha Yoeli kipo ndani ya Biblia tutegemee Udhihirisho wa Roho Mtakatifu na mafunuo yake ya Nguvu ya Kumtangaza Yesu ….pasipo kuufunga katika Ishara moja tu…..

  Kwangu mimi maadamu Maandiko haya yako Katika Maandiko Msimamo wangu utabakia KUNENA KWA LUGHA SI ISHARA PEKEE YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU…….

 88. Mpendwa Noel, Bwana Yesu Asifiwe.
  Naendelea kuufatilia mjadala huu kwa ukaribu sana, kwakweli mjadala upo vizuri tu. Shida ninayoiona kwako ni KULAZIMISHA kwamba watu walio na mtazamo kinyume na wako, kama Ndg. Orbi – wakubaliane nawe tu kwamba “kunena kwa lugha ni lazima” ukijazwa Roho mtakatifu –Unataka WAJUE hivyo na si kwamba WAELEWE hivyo! Mtu mwenye ufahamu hueleweshwa kwa vigezo na hivyo HUELEWA! Unapotumia Lugha ya kwamba; Orbi amezaliwa kwenye Dini inayoamini imani unayoikataa wewe – hiyo ni kutaka kumlazimisha bila kigezo ambacho yaani pasipo na Neno la Mungu, ama kumkalilisha tu ili AJUE kidesturi kuwa hivyo ndivyo. Mtu hujifunza kwa kuelewa na si kwa kukalilishwa (kujulishwa) – katika mjadala huu kama nimeuelewa vizuri, ninaweza kuuita kama hivi; kesi ni kwamba – HIVI NI LAZIMA KUNENA KWA LUGA ILI UJULIKANE KUWA UMEJAZWA ROHO MTAKATIFU? – Sasa kama ni hivyo, usitoke nje ya mada kwa kutaka kumburuza Orbi, akubaliane nawe tu kwa kukalili. Toa maelezo yenye kusimamiwa na Neno la Mungu; Labda niseme tu kwamba mimi nami kama Orbi, sijakubaliana nawe moja kwa moja, kwani kila nikisoma hiyo mistari uliyoitaja, sioni inaposema kuwa ukijazwa Roho mtakatifu ni LAZIMA unene kwa Lugha! Nilichoona na kujifunza katika hilo, ni kwamba,KUJAZWA ROHO mtakatifu ni jambo lingine na KUNENA KWA LUGHA ni jambo lingine. Naemdelea kuelewa kwamba; Roho mtakatifu ndiye anazo au ndiye kisababishi cha KARAMA au VPAWA TISA (9) ikiwemo kunena kwa Lugha, na kunena kwa Lugha ni moja ya ishara za wazi (Nje) Na kunena kwa Lugha ni tukio ambalo mtu hujaliwa kama ambavyo angejaliwa na karama nyingine pia. Kwakuwa kunena kwa Lugha ni karama ya wazi (Nje) huenda ndiyo maana watu huikazania sana hiyo na kuona kuwa ndicho kipimo pekee cha kujazwa Roho mtakatifu, napengine hujiona ndiyo wamemaliza na kwaba tayari – ni lazima hapo wanye Roho Mtakatifu! Na katika hilo wengine hujitamkia maneno ya hovyohovyo tu bila kujua kama wayanenayo ndiyo hasa Lugha yenyewe, ili tu wasije wakapuuzwa kwamba hawajajazwa Roho mtakatifu! Wapendwa swala si kunena kwa Lugha tu ndiyo ujulikane kuwa umejazwa Roho mtakatifu,bali mhimu ni kuwa na huyo Roho mtakatifu kwanza – naye atakujalia kipi akupe kwanza,kunena kwa Lugha kwanza au kipawa kingine kwanza kwa ajili ya kanisa! Sambamba na hili, Paulo pia aliwahi kusema kama hivi,“……….kama kunena kwa Lugha mimi nanena kuliko ninyi……” Sasa, hapo unaweza kusemaje, Paulo alikuwa akiwajulisha wenzake kuwa hawajajazwa Roho mtakatifu? Labda tujiulize kwanza hivi, Yesu alipo batizwa na Yohana, Roho mtakatifu kwa mfano wa Huwa alikuja juu yae. Baada ya hapo,……. akiwa amejazwa Roho mtakatifu Yesu alinena kwa Lugha ili kuthibitisha kuwa tayari anaye Roho mtakatifu? Au tuseme nini, kwa kuwa hakunena kwa LUGHA pale hakuwa na Roho Mtakatifu? Neno linasema……..Roho alimuongoza nyikani, sasa ilikuwaje iwapo hakunena kwa Lugha Roho amuongoze wakati hakuwa naye? Maana umesema aliye na Roho mtakatifu Lazima yake anene kwa Lugha!; Akiwa kule nyikani, Yesu hakuwa na kipawa chochote kwanza kabla ya kupambana na Shetani nyikani,kwa kuwa hakunena kwa Lugha? (Maana hapa tunaona tayari Roho mtakatifu alikuwa akimuongoza) au alipambana tu na Shetani bila Roho mtakatifu kumjalia kipawa chochote?- Maana hapa Neno halisemi kama alianza kunena kwanza kwa Lugha mara tu baada ya ubatizo, kuthibitisha kama amejazwa Roho mtakatifu,………kumbuka Yesu alimruhusu Yohana ambatize ili kuitimiza haki yote ipasavyo!….Tafadhali mpendwa wangu Noel, endelea kutuelewesha tu kwa uvumilivu – napenda sana unavyo nukuu maandiko! UBARIKIWE.

 89. Asheri na wengineyo,

  Naamini tuko hapa kufundishana, naamini wote hapa kwa njia moja au nyingine tunamjua Bwana….naaamini pia wengine kati yenu ni dhaifu wa imani (Rom 14:1) na wengine kati yetu ni wenye nguvu na wanauweza kuuchukua udhaifu wa wasio na nguvu (Rom 15:1) ……na nikisema tena kama Paulo….”Wewe u nani unayemuhukumu Mtumishi wa Mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama na Huanguka….(Rom 14:4)

  Hivyo kwa nia njema ya kuutunza umoja wetu Katika Kristo nami pia nafuata nyayo za Ndugu yangu Asheri nasimamisha kuchangia…..

  Mbarikiwe.

 90. Mimi naamini kunena kwa lugha si lazima, ila muhimu. Kwanza kwa nini iwe lazima wakati anayetoa hicho kipawa si wewe ni roho mtakatifu.

 91. Precious,nimejaribu kufuatilia maandiko unayoyatoa lakini hayahusiani kabisa na ulichokisema. Kwa mfano unaposema Babeli maana yake ni Mungu mke Diana katika Mwanzo11:1 mimi sikuelewi.
  Tusemeni vitu ambavyo tunavijua barabara siyo vya kukaririshwa kwa njia ya mafunua ya watu fulani.

 92. Wapendwa,

  Naufuatilia mjadala huu kwa umakini mkubwa.
  Muuliza swali alitaka kujua mambo makubwa mawili;

  1. Mtu anapompokea Roho Mtakatifu au kwa maneno mengine hujulikana kama kujazwa Nguvu ya Roho Mtakatifu, je ni lazima mtu huyo azungumze kwa lugha mpya?

  2. La pili alilotaka kujua ni kwamba mtu huyo akifanya ishara zingine za Roho Mtakatifu mbali na hii ya ‘kuzungumza kwa lugha mpya’, mtu huyo anakuwa hana Roho Mtakatifu ndani yake?

  Labda mimi niongeze tu maswali zaidi kufuatana na mijadala iliyoendelea hapo juu kwamba; je, kila anayejazwa au anayejaa Nguvu ya Roho Mtakatifu ni lazima ishara zote zilizosemwa na Yesu kwenye Marko 16:17-18 na zile zote zilizofanywa na Mitume wa kanisa la mwanzo zionekane kwa mtu huyo ndipo ijulikane kwamba Roho Mtakatifu yupo ndani yake?

  Hebu twende mbali kidogo au twende mbele zaidi kwa kujiuliza, Hivi nini hasa kusudi la Mungu la kutupa Roho Mtakatifu pamoja nasi, juu yetu na ndani mwetu? Je, ni ili tuzungumze kwa lugha mpya tu au ili Roho huyo atuwezeshe kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi na matunda na vipawa vyake vipate kuujenga mwili wa Kristo? Je mwili wa Kristo unajengwa zaidi kwa kunena kwa lugha mpya?

  Mtume Paulo kwenye Waraka wake wa Kwanza kwa Wakorintho sura ya kumi na nne ameeleza kwa kirefu sana juu ya kunena kwa lugha mpya na ameweka maangalizo mengi sana juu ya karama hii ya kunena kwa lugha mpya.

  Hapa ndipo ninapofika mahali pa kuungana na Orbi kwamba hili neno ‘LAZIMA KUNENA KWA LUGHA MPYA BAADA YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU’ linataka kutumiwa vibaya ili kujenga wigo fulani kwamba usiponena kwa lugha mpya, basi wewe hujampokea Roho Mtakatifu. Ni ukweli wa kimaandiko kwamba kunena kwa lugha mpya ni moja tu ya ishara nyingi zinazoandamana na kila mtu ampokeaye Roho Mtakatifu, lakini si lazima ishara zote zionekane kwa kila mtu aliyempokea Roho Mtakatifu. Kunena kwa Lugha ni moja ya karama nyingi ambazo Roho Mtakatifu huwagawia watakatifu wake kama apendavyo Yeye kwa kusudi la kuliimarisha kanisa ambalo ni mimi na wewe.

  Naomba niendelee kuufuatilia mjadala huu lakini tahadhari kwa wanaotufunza kutokuyangalia maandiko tokea kwenye kona moja tu, tuyaangalie maandiko katika mapana yake kuhusiana na jambo hili. Kwa mfano Yesu alipokuwa karibu kabisa kupaa aliwaambia wanafunzi wake kwamba si juu yao kujua nyakati na majira ambayo Baba yake ameyaweka katika mamlaka yake, ‘LAKINI MTAPOKEA NGUVU AKIISHA KUWAJILIA JUU YENU ROHO MTAKATIFU, NANYI MTAKUWA MASHAHIDI WANGU KATIKA YERUSALEMU, UYAHUDI KOTE NA SAMARIA, HADI MIISHO YA DUNIA’ (Matendo 1:7-8). Je, unaweza kuwa shahidi mwaminifu wa Yesu kwa kuzungumza lugha mpya tu ambayo wanaokusikiliza hawakuelewi?

  Nadhani hakuna hata mmoja aliyejadili hapo juu anayekataa kuwa kunena kwa lugha mpya si moja ya ishara za ujazo wa Roho Mtakatifu, lakini si LAZIMA kila aliyempokea Roho Mtakatifu azungumze kwa lugha mpya! Ila ninachojua ni kwamba kila aliyempokea Roho Mtakatifu atasema au atanena kwa ujasiri mkubwa siri za Ufalme wa Mungu zinazopatikana ndani ya Habari Njema ya Wokovu kwa kumkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Kiongozi wa maisha yake. Ndio sababu Mtume Paulo akasema anenaye kwa lugha mpya anazungumza na Mungu na anaijenga nafsi yake, lakini mwenye kipawa cha kuhubiri (ambacho pia ni moja ya ishara za kuwa mtu amejaa nguvu za Roho Mtakatifu) ni bora zaidi kwa kuwa analijenga kanisa.

  Baraka za Bwana ziwe pamoja nasi sote.

 93. Shalomu,

  Mpendwa Orbi,

  Katika mchango wanyu uliopita nilianza kwa kueleza nisivyopenda kujadili hoja hii kwa misingi ya kidini/kidhehebu kama baadhi ya watu wanavyohusianisha mchango wa mtu na dhebu fulani. Nasikitika katika majibu yako umesema kuwa inawezekana maoni niliyoyatoa ni utaratibu wa dhehebu langu, hivi unalijua dhehebu langu? sikumbuki kama katika mchango wangu nilifanya reference kitabu cha dini yoyote. Hivi kama siko sahihi kwanini usiseme Asheri hapa huko sahihi kwasababu hii au ile?

  Binafsi, nisingependa kuchangia hoja kwa kutafuta ushindi, siko hapa kushindani jambo fulani, nilichokuwa nakifanya ni kutoa mchango wangu tu!

  UFAFANUZI
  NILIPOSEMA MTU ATAFUTE KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA SIYO KUTAFUTA KUNENA KWA LUGHA si kuwa na maana uliyosema kama ninavyonukuu “unaanza UVUMI WA UPEPO TOKA MBINGUNI ……UNAOENDA KASI………..HALAFU NDIMI ZA MOTO……HALAFU LUGHA INAYOELEWEKA……”

  Nilichokuwa namaanisha ni kuwa kwa kuwa ANAYEFANYA MTU ANENE NI ROHO MTAKATIFU, BASI MTU ATAFUTE KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU ILI AWEZE KUNENA. KAMA UNATAKA KUONA MOSHI NI LAZIMA UWEPO MOTO.

  Aidha umenukuu kutoka mchango wangu maneno yafuatayo
  “Kama yalivyo mambo mengine ya MUNGU, KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU KUNATAKA IMANI PIA. MTU ANAAMINI KISHA ANAPOKEA, LAKINI LAZIMA PIA IWEPO KIU YA KUPOKEA (Yohana 7:37-39 na Isaya 44:3) KUOMBA (Luka 11:13) KUMTII MUNGU (Matendo 5:32), LAKINI LA KWANZA KABISA NI KUOKOKA (Matendo 2:38)”.

  KISHA UKAULIZA IFUATAVYO
  – Tumeona watu Wakinena kwa Lugha siku ya Kuokoka hawajui hata nini……na wala hata KIU hawakuwa nayo…..utasemaje…….?

  Kabla sijakujibu, hivi maandiko niliyoyasema katika nukuu yangu hayana uhusiano na hicho nilichokisema? Kama nimekosea kuyaweka hapo basi nionyeshe nilichokichanganya.

  Naomba nijibu kuwa naamini mtu anaweza kunena bila kufundishwa na nimeona hayo yakitokea ndiyo maana katika mchango wangu uliounukuu maneno hayo kuna mahali nililielezea jambo niliposema “Hata hivyo, kwa kuwa Mungu hana mipaka, anaweza akamjaza mtu Roho Mtakatifu bila kuwa na mafundisho rasmi au kuombewa kama ilivyotokea kwenye Mdo 10:44-46. Kwa hiyo ikitokea mtu amejazwa namna hii, tutampa Mungu utukufu.”

  Wapendwa, kutokana na hoja hii inavyoenda, nimeamua kunyamaza kwanza, hivyo ikionekana sisemi chochote basi ijulikane kuwa nimenyamaza kwasasa. Hata hivyo, ikiwepo haja au msukumo wa kuchangia, basi nitachangia.

  Mungu awabariki,

 94. Wapendwa,

  Tukiziendea hoja vizuri zitatufaidia wengi, si wachangiaji peke yenu bali zaidi sisi wasomaji.

  Jambo ninaloliona ni ufunikaji wa hoja kwa makusudi ya kuuleta mjadala mzima kutokuwa na maana yoyote! Kuna maswali yameulizwa ambayo majibu yake yangeliweka jambo hili la kunena kwa lugha katika stahili yake na kutufunua macho yetu ya kiroho zaidi kulihusu. Kwa mfano swali limeulizwa: NI WAPI MAANDIKO YANASEMA KWAMBA MTU AKIJAZWA ROHO MTAKATIFU NI LAZIMA ANENE KWA LUGHA? Hilo ndilo swali lililoulizwa. Kabla hujalijibu ni vizuri utafute kulielewa swali kwanza! Unapokuja na maelezo mengi yanayolizunguka swali haisaidii kitu. Kama jibu ni HAKUNA MAANDIKO HAYO, sema hivyo tu!! Maandiko yanayo zungumzia jambo hilo kimsingi ni Matendo 2:38, yanasema mtapokea KIPAWA!!! Mungu hawezi kuliruka Neno lake, kwa kuyakimbia maandiko ndio maana hakuna kinachoeleweka!!

  Wewe kama umenena kwa Lugha, basi jua kwamba umepokea kipawa hicho, endelea katika njia hiyo siku moja Roho Mwenyewe atakushukia aje kukaa kwako, hilo ndilo kusudi kuu la Mungu!! Yawezekana kunena kwako ni kiwango cha Roho Mpya tu (na si Roho Mtakatifu) Mungu aliyokupatia, usikurupuke, tulia katika unyofu Roho Mt. atakujia katika majira yake, furaha yako itakuwa kuu kuliko hiyo uliyonayo.

  Ukikurupuka, kama wengi wetu tulivyo, kutokana na mafundisho yasiyo sahihi, tunakwamia hapo maana Mungu halazimishwi. Matokeo yake ndiyo haya, unaulizwa swali hili, yule Mwalimu wa kukuongoza katika Neno lake uliyedhani unaye hayuko, unabaki unajibu yasiyoeleweka! Hivi uchungu wa kuzaa unahusiana nini na Ujazo wa Roho Mt.? Maandiko yanashuhudia tofauti na maelezo wanayotoa; Biblia inasema kunena ni ishara kwa wasio amini, sasa yanakuwaje hayo ukilinganisha na huo uchungu? Msimlazimishe Mungu akubaliane na mawazo yenu ya dini, amesema “usiongeze wala usipunguze” kama amekwambia hicho ni Kipawa nawe sema hivyo. Kama amekwambia hiyo ni ishara kwa wasioamini, basi nawe iwe hivyo kwako ndipo italeta maana vinginevyo its a WASTE!

  Kuhusu watu walionena kwa lugha vifungu viko vingi sana, tena Biblia inasisitiza kuwa walijazwa Roho Mtakatifu. Hilo wote tunalifahamu hata Katoliki wanalijua hilo pia! Na hao wote waliotajwa katika Biblia lugha walizonena zilishuhudiwa, hivyo kukileta katika maana halisi kipawa hicho, siyo alimradi tu…! Mmekivuruga kipawa cha Mungu mpaka mnenaji wa kweli leo hana nafasi tena, anaonekana ndio wale wale! Labda muwe mmejikusanya wenyewe!!!!

  Mungu tuongezee muda kidogo tujirekebishe!

 95. Mpendwa Asheri,

  Nitaanza ulipomalizia……na nitaitumia nukuu yako ambayo umetumia kuwakilisha mawazo yako…..hebu isome tena…..!

  ”Bado naomba nimalizie kwa kusema kuwa MTU HAANZI KUNENA KWA LUGHA, BALI ANAANZA KUJAA/KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU, NDIPO ISHARA TUTAKAYOIONA KWA NJE NI KUNENA KWA LUGHA. KWA HIYO USHAURI WANGU NI KUWA MTU ASITAFUTE KUNENA KWA LUGHA, ATAFUTE KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU, NDIPO ATAKAPOMPOKEA ATAONA JINSI ATAKAVYONENA KWA LUGHA.”

  – Kama utayaangalia maandiko ni vitu vinavyoenda kwa pamoja “simultaneously”

  – Na kama unataka kuyaangalia MAANDIKO kama unavyodai basi mpangilio utakuwa kama ifuatavyo unaanza UVUMI WA UPEPO TOKA MBINGUNI ……UNAOENDA KASI………..HALAFU NDIMI ZA MOTO……HALAFU LUGHA INAYOELEWEKA……..

  – Umeshauri Mtu asitafute Kunena kwa Lugha atafute KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU…..inawezekana huu ni utaratibu wa dhehebu lako….Lakini si utaratibu ulioko ndani ya Biblia…….Siku ya Pentekoste HAWAKUTAFUTA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU…..walikaa kusubiri ahadi ya Mungu kwa maombi……Kutafuta KUBATIZWA kwa Roho Mtakatifu ni mafundisho ya baadhi ya madhehebu leo na ndio yameleta mada kama hizi…..Kinyume kabisa na Petro alivyowaambia wale waliouliza maana ya Kunena siku ya Pentekoste……

  Halafu umeendelea kusema…….angalia tena nukuu yako….

  Kama yalivyo mambo mengine ya MUNGU, KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU KUNATAKA IMANI PIA. MTU ANAAMINI KISHA ANAPOKEA, LAKINI LAZIMA PIA IWEPO KIU YA KUPOKEA (Yohana 7:37-39 na Isaya 44:3) KUOMBA (Luka 11:13) KUMTII MUNGU (Matendo 5:32), LAKINI LA KWANZA KABISA NI KUOKOKA (Matendo 2:38).

  – Tumeona watu Wakinena kwa Lugha siku ya Kuokoka hawajui hata nini……na wala hata KIU hawakuwa nayo…..utasemaje…….?

  – Tumeona watu wenye Kiu ya Kunena kwa Lugha………wakifunga……wakiombewa……..wakibatizwa unatizo wa maji mengi……na formula mbali za kanisa …….zikilazimishwa kwa kutumia vifungu vingi vya Maandiko…….Utasemaje…?Hawana Roho Mtakatifu…….nini Kimewaongoza (convict of sin) mpaka kikawafanya watubu…..Ni Roho Mtakatifu…..? Kwa Hiyo baada ya Kuwaokoa anaondoka…..anataka waanze safari ya kumtafuta……ali awarudie tena kwa ujazo……?

  Hebu tusaidie kwa haya machache…..nitaendelea…..

 96. Mpendwa Noel Msanjila,

  Nashangaa sana kwa nini unapenda kutumia mtazamo huu unapojibu hoja

  “…………na kwa asilimia kubwa kila dini au dhehebu wanaamini kulingana na walivyowakuta wazazi wao wanavyoamini,hata wewe ORBI inaonyesha uko ktk dhehebu ulilowakuta wazazi wako wanaliabudu,lakini nenda polepole ukidadisi naamini Mungu atakufunulia tu ukweli siku moja,maana ukifuata mambo ya Mungu kwa sababu ya wazazi,itakuwa ngumu……”

  …….Kwa hoja hiyo ndugu yangu Masanjila unataka kusema na hata wewe Umeamini Kunena Kwa Lugha kwa sababu uliwakuta wazazi wako wako katika dhehebu la Kunena Kwa Lugha….? Nami narudisha hoja huyo kwako ndugu Masanjila….ukiamini Kunena Kwa Lugha kama Wazazi wako walivyosema itakuwa ngumu kulielewa Neno la Mungu……au kama dhehebu lako ulilosema itakuwa ngumu……hebu acha Maandiko yaseme yenyewe…….

  Kwa kukusaidia tu Imani hii niliyo ni Hai na wala sikuirithi kwa wazazi wangu ……niliipata kwa Kutubu Dhambi….na Kukubali sadaka iliyotolewa pale Msabalani…..kama malipo yangu ya dhambi nilizotenda dhidi ya Mungu aliye hai …….Kwa kumwamini Yesu alinifanya mtoto wake………Nikawa kiumbe kipya…..na kwa njia ya Roho Wake Mtakatifu amenipa uwezo na Nguvu ya kuishi maisha matakatifu ambayo nisingeliweza kwa nguvu zangu mwenyewe……..Kwa kumwamini Yeye amenipa mlango wa kuzungumza naye katika Maombi……..nimemwona Yu hai Kwangu kwa kujibu Maombi yangu…na Kuniitikia kila Nimwitapo……….Kwa Kuongozwa na Roho wake Mtakatifu nimemwona akinifungulia milango mbali mbali katika maisha yangu ambayo kwa akili zangu za Kawaida zisingeweza kufungua milango hiyo………..amenipa uwezo wa Kumkiri na Kumuhubiri kwa wengine……amenipa Neema ya kuwafanya wengine wamjue yeye….! Na zaidi amenipa Neno lake….ambalo ni hai……..na ambalo nimeyatoa maisha yangu kusimama katika hilo tu…….na kulitetea Neno lake tu wala si mafundisho ya dhehebu…….huu ndio wasifu wangu ndugu yangu Masanjila…..sina Imani ya kurithi kama unavyodai…….

  Labda kwa kukusaidia tena….kama Mkristo nawakubali Wakristo wote ambao wamemkiri Kristo kama Bwana na Mwokozi wao….Wakristo hawa wako katika madhehebu mbali mbali…….na wana vipawa, Karama mbali mbali kadri Bwana alivyowapatia…….. wanaweza kuwa na mitazamo tofauti kwa vitu visivyo vya msingi katika kuuishia Imani hii…..na ule Upendo wa Kristo aliomimina mioyoni mwao unafanya kumuona Kila Mkristo aliyempokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wake ni Ndugu halisi…kuliko hata ndugu wa damu……..

  Labda kwa kukusaidia pia……dhehebu langu halina uhusiano wowote katika Kuimiliki Imani yangu…..Nakubaliana na wanachofundisha kama kina kwenda sambamba na Maneno ya Mungu…….Sitahukumiwa Mbele za Mungu kwa vigezo vya mafundisho ya Dhehebu langu….bali kwa Maneno ya Mungu yalio wazi ambayo ameatuachia na Roho Mtakatifu ni mwalimu Mkuu………

  Labda kwa kukusaidia tena….rudia post zangu……Sipingi Kunena kwa Lugha………napinga Kunena kwa Lugha kama Ishara Pekee ya kuwa Mtu kampokea Roho mtakatifu…..Maandiko yako wazi mno kwa hilo…….

  Ubarikiwe ndugu….tutaendelea na hoja…..Na nikipata muda pia…nitajibu hoja za Mpendwa Aheri……Siku Njema.

 97. Orbi,umeuliza swali kwamba,ni wapi panapoonyesha kwamba ukijazwa Roho mtakatifu UTANENA KWA LUGHA ? Soma Mdo 19;6- ‘Na Paulo,alipokwisha kuweka mikono yake juu yao,Roho mtakatifu akaja juu yao; WAKAANZA KUNENA KWA LUGHA;na kutabiri, Mdo 10;44-46,Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho matakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno na wale waliotahiriwa,walioamini,wakashangaa,watu wote waliokuja pamoja na Petro,kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu, kwa maana waliwasikia WAKISEMA KWA LUGHA na kumwadhimisha Mungu Mdo 2;4 Wote wakajazwa Roho mtakatifu,wakaanza kusema kwa lugha nyingine,kama Roho alivyowajalia kutamka .Orbi,napna ungeweza kufuta maandiko yanayohusu kunena kwa lugha,ungeyafuta,maana hutaki kujifunza,bali kubisha.Achana na mapokeo ya dini ya tangu uzaliwe ukayakuta,kwa hiyo inakuwa ngumu kwako kuamini unachokiona nakukisikia,Soma hayo maandiko,kwa utulivu,uyatafakari,siyo uufunge moyo wako bali uufungue moyo,umruhusu Mungu aseme nawe,,hebu toa jibu kwa maandiko hayo,maana umesema,hakuna maandiko yanayoonyesha kwamba,mtu anapojazwa Roho mtakatifu lazima anene kwa lugha,unajua ni ngumu,kujua uchungu wa kuzaa kama hujazaa,utawabishia kina mama kwamba hakuna uchungu,lakini watakushangaa tu,au kama hujaungua moto huwezi kuujua uchungu wake zaidi ya alieungua moto,Nakwambia kweli,watu waliojazwa Roho Mtakatifu NA KUNENA KWA LUGHA,huwezi hata kuwaambia kitu tena,maana wameona uzuri wake,na wanajua ni nini wanachokiona ndani yao,labda useme tu kwamba ktk dini yenu hicho kitu hakiaminiwi. Mbona dini inaamini kivyakevyake japo tunasema Mungu nimmoja ? kila mtu anaamini aonavyo,na kwa asilimia kubwa kila dini au dhehebu wanaamini kulingana na walivyowakuta wazazi wao wanavyoamini,hata wewe ORBI inaonyesha uko ktk dhehebu ulilowakuta wazazi wako wanaliabudu,lakini nenda polepole ukidadisi naamini Mungu atakufunulia tu ukweli siku moja,maana ukifuata mambo ya Mungu kwa sababu ya wazazi,itakuwa ngumu maana hata Yesu ilifika mahali akasema ‘Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya Luka 8;21,NAKUSIHI ENDELEA KUDADISI HABARI HII YA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU ULIVYO NA MAHUSIANO NA KUNENA KWA LUGHA, hata YESU ALISEMA KTK YOHANA 3;5- Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuungia ufalme wa Mungu, UBARIKIWE SANA NDUGU ORBI MPENDWA KTK BWANA

 98. Shalomu,

  Nilipoanza kuchangia mada hii nilijua kuwa tunajifunza, lakini kadri mjadala unavyoendelea, nimegundua kuwa tumeingiza misimamo ya dini na hivyo kuwa vigumu kuendelea kujifunza. Binafsi nisingependa kuchangia hoja zenye mlengo wa kidini au kusimamia misimamo ya kidini katika suala hili kwa kuwa kunena kwa lugha ni suala la kiroho na si la kidini. Sijapenda baadhi yetu tulivyoanza kuzungumza habari za dini na kuwa baadhi ya dini zimeanza kubadili mafundisho yao. Nashukuru Mungu kuwa dini zitabadili mafundisho yao, lakini hazitabadili neno la Mungu kama lilivyo kwenye maandiko.

  Ndugu ORBI
  kuhusu mchango wako wa FRIDAY MARCH 23, 2012 at 7:05 napenda kukiri kuwa Biblia yangu inavyo vifungu ulivyovitaja katika mchango huo isipokuwa Matendo 17:39. Biblia yangu inaishia msitari wa 34. Nakushukuru sana kwa kuleta maandiko hayo, nami nimeyapitia na ufafanuzi wangu ni kama ifuatavyo:

  Matendo 4:8- 13 Ndipo Petro AKIJAA Roho Mtakatifu Akawaambia……..walipoona UJASIRI WA PETRO……

  Kwanza naomba tukubaliane kuwa Petro alikuwa mmoja wa watu waliojazwa Roho Mtakatifu katika Matendo 2 na alikuwa mmoja wa walionena kwa lugha kama ishara kwa amempokea Roho Mtakatifu. Hivyo Petro alikuwa ananena kwa lugha.

  Katika Matendo 4:8 Petro alikuwa mbele ya Baraza akihojiwa kuhusu uponyaji uliofanyika katika Matendo 3. Kwa sababu hiyo, Petro asingekuwa ananena kwa lugha maana alikuwa anazungumza mbele ya Baraza. Hiki kilichotokea ni utendaji wa Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani yake ambaye alikuwa akizungumza. Kilichotokea hapa ni kile alichokisema Yesu katika Mathayo 10:18-20.

  Matendo 4:31 Hata walipokwisha Kumwomba Mungu mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI

  Hapa Biblia inaelezea kilichotokea baada ya Petro na Yohana kutoka mbele ya Baraza na kurudi kwa watu wao na kuamua kumuomba Mungu kutokana na vitisho vya kuzuiwa kunena habari za Yesu (Matendo 4:23-31). Naomba tukubaliane pia kuwa Petro na Yohana walienda kwa Mitume wenzao na watu wengine waliokuwa nao katika ushirika. Kama hivyo ndivyo, basi ni wale waliompokea Yesu katika Matendo 2 na walinena kwa lugha kama ishara kuwa walimpokea Roho Mtakatifu. Kwa hiyo hapa walikuwa wakimuomba Mungu kwa pamoja. Ukisoma msitari wa 29 utaona kuwa maombi yao yalilenga kuomba ujasiri wa kunena neno la Mungu na ndicho kilichotokea katika msitari wa 31.

  Matendo 7:55 ” Lakini yeye (Stephano) AKIJAA ROHO MTAKATIFU AKAKAZA MACHO…….AKASEMA…….

  Habari za Stefano zinaanzia Matendo 6 alipochaguliwa kuwa wahudumu wa kundi lililokuwa likiongozwa na akina Petro. Katika Matendo 6:1-6 tunaona jinsi walivyochaguliwa. Moja ya mtu kuchaguliwa ilikuwa kujaa Roho (msitari wa 3) na msitari wa 5 unasema kuwa Stefano alikuwa mtu aliyejaa Roho na Imani. Swali ninalojiuliza ni kuwa Petro alisema mtu anayechaguliwa awe amejaa Roho, je wachaguaji wangemjuaje kuwa amejaa Roho kama hakuna Ishara? Inawezekana Stefano alikuwa mmoja wa wale 120 waliokuwepo pale ghorofani au miongoni mwa watu walioendelea kuongezeka kwenye kanisa la wakati huo. Kilichotokea katika Matendo 7: 55 ni pale Stefano alipokuwa akihojiana na watu waliokuwa wakimpinga (soma Mdo 6:9-7:60) Katika Mdo 6:10, Biblia inasema “hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye”. Hapa tunaona inafanana na ile ya Petro katika Mdo 4:8 kama alivyosema Yesu kwenye Mathayo 10:18-20. Hivyo Mdo 7:55 haimaanishi ndiyo wakati Stefano alikuwa akijazwa Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza.

  Paulo alipojazwa Roho Mtakatifu Magamba yalimtoka ( Matendo 17:39)

  Kama nilivyosema hapo juu, Biblia yangu inaishia Msitari wa 34, na maudhui ya sura nzima ya 17 haijazungumzia suala hili, hivyo kwasasa zitazungumzia msitari huo.

  KUHUSU KUNENA KWA LUGHA INAYOELEWEKA, sitalizungumzia hili kwa kuwa katika mchango wangu wa March 13, 2012 (4:55) nilifafanua suala hili.

  Matendo 2:41- 42 Lile kundi la watu elfu lililopokea Neno la Mungu kwa Mahubiri ya Petro…….lilibatizwa na kuendelea na mafundisho ya Mitume pasipo kunena kwa Lugha…..Je Petro alisahau kuwafanyia ubatizo huo….!

  Katika hili Biblia iko kimya kuhusu namna watu hao walivyobatizwa kwa Roho Mtakatifu, hivyo si ushahidi kuwa walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu hawakunena kwa lugha. Ninachoamini ni kuwa Petro hakuwaacha bila kubatizwa kwa Roho Mtakatifu.

  KUHUSU YALE MENGINE ULIYOYAZUNGUMZA KATIKA MCHANGO WAKO IKIWEMO LUGHA ISIYOELEWEKA, PAULO KULAZIMISHA AU KUTOKULAZIMISHA sitayapitia kwa kuwa hayathibitishi kuwa kuna watu wanabatizwa kwa Roho Mtakatifu bila ishara ya kunena kwa lugha.

  Ndugu Orbi,
  Nilichotegemea nilipokuomba utoe uthibitisho wa mtu kupokea/kubatizwa kwa Roho Mtakatifu bila kunena kwa lugha, nilitegemea ungekuja na maandiko yanayoonyesha tukio la wazi linalotuonyesha kuwa kundi fulani walijazwa na Roho Mtakatifu lakini bila kunena kwa lugha, jambo ambalo hujalifanya. Ulichokifanya ni kuleta maandiko yanayoonyesha utendaji (madhihirisho) ya Roho Mtakatifu ndani ya mwamini. Hili linanifanya niamini kuwa kuna mambo yanayochanganywa hapa.

  Suala la miujiza mbalimbali, wanafunzi walianza kufanya miujiza hata kabla Yesu hajapaa kwenda mbinguni. Katika Luka 10:17 tunaona wanafunzi wakimshuhudia Yesu matendo Makuu yaliyotendeka kwenye huduma yao. Aidha, Luka 9:49, Yohana anamwambia Yesu juu ya mtu waliyemuona anatoa pepo kwa Jina la Yesu wakamkataza kwa kuwa hakuwa miongoni mwao na majibu ya Yesu yapo wazi, hivyo mimi naamini kuwa mtu akiokoka anaweza kuomba na miujiza ikatokea hata kabla hajabatizwa kwa Roho Mtakatifu. Nasema hilo kwasababu Yesu aliwapa wanafunzi mamlaka siku nyingi.

  Kuhusu mtu kufundishwa kuhusu Roho Mtakatifu, ninavyojua mimi ni kuwa Wanafunzi wa Yesu walifundishwa sana kuhusu Roho Mtakatifu. Wapo waliozisikia habari za Roho Mtakatifu kutoka kwa Yohana Mbatizaji, wengine kutoka kwa Yesu MWENYEWE. Katika Yohana 3,14, 16, Luka 24:49, Matendo 1: 4 Yesu anawaambia wanafunzi waingoje ahadi ya Baba ambayo walisikia habari zake kwake Yesu. Hivyo si sahihi kusema kuwa wanafunzi walimpokea Roho Mtakatifu bila kufundishwa. Katika Matendo 19 tunamwona Paulo akiwafundisha watu wa Efeso habari za Roho Mtakatifu, Hivyo mtu akiokoka anapaswa kufundishwa habari za Roho Mtakatifu na wengi hawajabatizwa kwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha mpya kwasababu ya kukosa mafundisho kama ilivyokuwa Mdo 19:1-7.

  Hata hivyo, kwa kuwa Mungu hana mipaka, anaweza akamjaza mtu Roho Mtakatifu bila kuwa na mafundisho rasmi au kuombewa kama ilivyotokea kwenye Mdo 10:44-46. Kwa hiyo ikitokea mtu amejazwa namna hii, tutampa Mungu utukufu.

  Napenda nimalizie mchango wangu kwa kurudia baadhi ya maandiko kuhusu kunena kwa lugha kama ishara. Katika Matendo 2:4, biblis inasema kuwa wote wakajazwa Roho Mtakatifu, WAKAANZA KUSEMA KWA LUGHA NYINGINE… Hapa tunaona kuwa wote waliojazwa siku ile walisema kwa lugha nyingine, vinginevyo Biblia ingesema kuwa BAADHI YAO wakaanza kusema kwa lugha nyingine. Mimi naamini kuwa kama kungekuwa na njia nyingine ya kujazwa bila ishara hii ya lugha kuwepo, basi biblia ingeonyesha kuwa baadhi.

  Katika Matendo 10:44-46, Biblia inasema Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliolisikia lile neno. Msitari wa 46 unasema kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha…hapa napo ingekuwa ni baadhi tu walionena kwa lugha basi Biblia ingesema baadhi yao waliwasikia baadhi yao wakisema kwa lugha.

  Katika Matendo 19:6 inaonyesha pia kuwa wote 12 walipompokea Roho Mtakatifu walianza kunena kwa lugha.

  Katika Matendo 8:14-19, tunaona Biblia inasema kuwa Samaria watu walimpokea Roho Mtakatifu baada ya kuombewa na Petro pamoja na Yohana nadhani Filipo pia. Hapa biblia hajatamka kuwa walinena kwa lugha, hata hivyo, biblia haijasema pia kuwa walimpokea bila kunena kwa lugha. Lakini jambo la msingi ni kuwa baada ya kumpokea Roho Mtakatifu, Mitume na wote waliokuwepo walijua kuwa hawa ndugu wamempokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono na ndiyo maana hata yule mchawi aliomba auziwe uwezo wa kuwajaza watu Roho Mtakatifu kwa kuwawekea mikono. SWALI LA MSINGI NI JE mitume na huyo mchawi na wengineo walijuaje kuwa hawa wapendwa wamebatizwa kwa Roho Mtakatifu? Hatuwezi kusema kuwa waliona wakiwaponya wagonjwa au kuwa walianza kuhubiri kwa ujasiri, wamhubiri nani? Petro?, nadhani hapana, lakini ilikuwepo ishara iliyodhihirisha kuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Lakini swali la msingi, ni je, hivi tunataka Biblia iendelee kusema kuwa fulani alimpoke Roho Mtakatifu, akanena kwa lugha mpya? Mimi naamini kuwa hakuna haja maana imeshatuonyesha mara tatu katika Matendo kuwa watu walijua kuwa mtu amempokea Roho Mtakatifu kwa kumuona ananena kwa lugha, hivyo si lazima iendelee kusema. Vilevile, kama ipo njia nyingine inayoonyesha kuwa mtu amempokea Roho Mtakatifu, basi ingetuweka wazi pia.

  Bado naomba nimalizie kwa kusema kuwa MTU HAANZI KUNENA KWA LUGHA, BALI ANAANZA KUJAA/KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU, NDIPO ISHARA TUTAKAYOIONA KWA NJE NI KUNENA KWA LUGHA. KWA HIYO USHAURI WANGU NI KUWA MTU ASITAFUTE KUNENA KWA LUGHA, ATAFUTE KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU, NDIPO ATAKAPOMPOKEA ATAONA JINSI ATAKAVYONENA KWA LUGHA.

  Kama yalivyo mambo mengine ya MUNGU, KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU KUNATAKA IMANI PIA. MTU ANAAMINI KISHA ANAPOKEA, LAKINI LAZIMA PIA IWEPO KIU YA KUPOKEA (Yohana 7:37-39 na Isaya 44:3) KUOMBA (Luka 11:13) KUMTII MUNGU (Matendo 5:32), LAKINI LA KWANZA KABISA NI KUOKOKA (Matendo 2:38).

  Mungu awabariki,

 99. Wapendwa,

  Huu ni ushuhuda wa Mchungaji wa Assemblies of God anayefahamika Marekani- Robert Glenn Brown, kama baadhi ya wengine katika kanisa hilo sasa hivi , amekuwa na msimamo kwamba Kushikilia kunena kwa Lugha kama alama pekee (Ishara) ya kuwa muumini Kapokea ubatizo wa Roho Mtakatifu si sahihi kimaandiko….na ameandika Kitabu……”Pentecostal Revisited” Nimeleta sehemu ya ushuhuda wake ndogo tu…hasa alipoulizwa swala kama hili tunapojadiliana katika mada hii…….unaweza kusoma habari zake mtandaoni…..

  Robert Glenn Brown has been an ordained Assemblies of God minister for more than fifty years. He is a graduate of Denver University, Denver Seminary, Princeton Seminary and the Navy’s Senior Chaplain’s School.

  He began his ministry as founding pastor of an Assemblies of God church in Colorado in 1955 while in seminary.

  In 1960, Brown began his career as a U.S. Navy chaplain assigned to a Marine battalion in Camp Le Jeune, NC.

  Eight years later, he was the assigned chaplain aboard a helicopter carrier off the coast of South Vietnam, loaded with a reinforced battalion of battle weary Marines.

  It was during this assignment in the combat zone that Brown came to grips with doubts about the validity of a doctrinal statement his church asked him to affirm annually before renewing his credentials.

  Knowing it might cost him his career, he dared to question the validity of this Assemblies of God doctrine:

  “The baptism of the Holy Spirit is witnessed by the initial physical sign of speaking with other tongues as the Spirit of God gives them utterance.”
  This resulted in ongoing disputation with his denomination that continues to this day. This book gives the opportunity to do so.

  Though Brown was convinced that the Assemblies of God doctrine tying tongues to the initial baptism of the Holy Spirit was not based in Scripture and disclosed his dissent to his supervisors in church leadership, he resolved never to preach his views from the pulpit as long as he was shepherding an Assemblies of God church.

  QUESTION: If speaking in tongues are not, according to Scripture, the evidence that one has been baptized in the Holy Spirit, what is?

  PASTOR BROWN: Listen carefully to the words of Jesus, the Baptizer, the Chief Shepherd: “You will receive power when the Holy Spirit comes on you; and you will be my witnesses…” (Acts 1:8)

  The sign or evidence that the Holy Spirit has come upon a believer is an outpouring of spiritual power that produces people who exhibit Christ-like character. They therefore can be legitimate witnesses to Jesus. (In this text “witness” is a noun, not a verb.)

  All that Jesus did when He was on earth was accomplished in the power of the Holy Spirit. The same Holy Spirit that anointed and empowered Jesus has been dispatched to anoint and empower His followers. And what are the character qualities of Jesus that we are to emulate so as to bear witness to Him? Paul describes them:

  “The fruit of the Spirit is love, joy, peace, patience, kindness, goodness, faithfulness, gentleness, and self-control…” (Galatians 5:22) These character traits will follow Spirit baptism, some rapidly, some slowly.

  A further proof of being Spirit-filled is the manifestation of spiritual gifts. Paul affirms this positively:

  “Now to each one the manifestation of the Spirit is given for the common good. To one there is given through the Spirit the ability to speak with wisdom, to another the ability to speak with knowledge by means of the Spirit, to another faith by the same Spirit, to another gifts of healing by that one Spirit, to another miraculous powers, to another prophecy, to another the ability to distinguish between spirits, to another the ability to speak in different kinds of tongues. All these are the work of one and the same Spirit, and he gives them to each man, just as he determines.” (I Corinthians 12:7-11)

  When the Holy Spirit fills believers, he determines how and to whom the gifts of the Spirit are distributed.

  Continue reading on Examiner.com Interview with Glenn Brown, author ‘Pentecost Revisited’ – National Christian books | Examiner.com http://www.examiner.com/christian-books-in-national/interview-with-glenn-brown-author-pentecost-revisited#ixzz1qEZJy63G

 100. Mpendwa Orbi, Bwana Yesu asifiwe, nikweli tusitetee wachungaji wetu au yasemavyo mathehebu yetu, bali tusimamie Neno la Mungu, umesema vizuri pale ulipokumbuka kusema katika mchango wako wa 20/3/2012; nanukuu……”Hivyo ndugu yangu Masanjila baadhi yetu hapa kwenye Blog hatupingi wala hatutetei chochote kwa vile Wachungaji wetu wamesema….bali tunajaribu kuangalia JE MAANDIKO YANASEMAJE…….? Hapo ndio mahali Imara……” mwisho wa kunukuu. Michango ya Lwembe ilisimamia sana hilo, ila kwa bahati mbaya siioni michango yake tena!

 101. Sam,

  Kila unapoandika unakuja na new insight ….UBARIKIWE……Mafundisho mengi juu ya Kunena kwa lugha Kama ISHARA PEKEE ni vigumu mno kusimama nayo kama umeamua kuvua miwani ya dhehebu na kuyaachia Maandiko yapige Kelele yenyewe…! Kilichofanyika katika kambi ya Pentecoste tokea pale Azusa Street ni kujaribu Kumjengea Roho Mtakatifu zege kubwa la nondo katika wigo wa mafundisho mbali mbali yasiyo na msingi …hata kama mafundisho hayo yalifanyika kwa nia njema kabisa……Lakini hayakusimama katika Kweli ya Biblia.

  Baadhi ya Madhehebu yanayofundisha Kunena Kwa lugha kama Ishara pekee na ni lazima kupita hatua hiyo baada yakuoka, yameanza kufikiri upya kuhusu mafundisho hayo….! Assemblies of God (Makao makuu – Springfield Missouri) mara nyingi imepata vita toka ndani ya dhehebu hilo kwamba…..msimamo wa KUNENA KAMA ISHARA PEKEE si sahihi….! Hii ni kutokana kwamba wameona UKWELI si kutokana na Maandiko tu, bali hata hali halisi ndani ya Makanisa yao wenyewe na nje pia. Utasemaje juu watu waliokoka, ambao unaona kweli wamebadilishwa na Injili, na wamejitoa kumuishia Mungu lakini hawaneni kwa Lugha….? Na ikumbukwe pia wengine wanataka kunena kwa Lugha……wameombewa…..wamebatizwa kwa maji mengi……..wametumia formula zote walizopewa za mafundisho ya Kanisa lakini hawakupata huo ubatizo…!

  Utasemaje juu watu wanaonena kila kukicha lakini unaona bado kabisa ni watoto wachanga katika Kristo……miaka na miaka katika kunena kwao tabia za Kiungu hazijaumbika ndani mwao….! Utasemaje juu ya mfumuko wa mafundisho potofu…”cults” ambazo zimechipuka kama uyoga leo lakini zinadai zina Roho wa Mungu kwa ajili ya Kunena kwa Lugha tu! ….lakini wanachofundisha ni Injili nyingine na Yesu Mwingine kabisa amabye hatumuoni kwenye Maandiko….!

  Kitendo cha Kulazimisha Kunena kwa Lugha kama Ishara Pekee hakuna tofauti na mafundisho yaliyosumbua Kanisa la Kwanza kwamba LAZIMA watu wamataifa walioamua kumfuta Yesu ni LAZIMA WATAHIRIWE…..! Madhebu ya kwanza kuzaliwa katika Ukristo yalizaliwa kipindi hiki……Rudia Matendo ya Mitume.

  Kwa kifupi hatuwezi Kumjengea Roho Mtakatifu ukuta wa zege…! Nguvu na Utendaji wa Mungu na ISHARA YA INJILI IOKOAYO haijafungwa katika KUNENA KWA LUGHA…..

  Hebu tumiachie Roho Mtakatifu atende anavyotenda……..Mbarikiwe.

 102. Asheri, Haule na ndugu yangu mpendwa Masanjila

  Maandiko yanasema Yesu alisema yafuatayo……

  1. Bali waingoje AHADI ya Baba……. AMBAYE MLISIKIA HABARI ZAKE KWANGU.. (Matendo 1:4A)

  2. Yohana alibatiza kwa Maji bali ninyi MTABATIZWA katika Roho Mtakatifu (Matendo 1:5b
  )
  3. Lakini MTAPOKEA NGUVU AKIISHA KUWAJILIA ROHO MTAKATIFU AKIISHA KUWAJILIA JUU YENU ROHO MTAKATIFU nanyi Mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu,…..Uyahudi na Samaria…

  Ndugu zangu kwa mistari hii tunajifunza yafutayo;

  Ujio wa Roho Mtakatifu ni AHADI ambayo Yesu aliizungumza mapema mno hata kabla ya kusulibishwa, na huko nyuma (Katika Injili) Yesu anasema Roho Mtakatifu atakuja kwa mambo mengi….

  1. Kama MSAIDIZI….
  2. Kama Mwalimu…..
  3. Roho wa Kweli…..

  Kwa hiyo ukiunganisha maneno ya Yesu ya huko awali katika Injili na yale aliyosema siku chache kabla ya kupaa katika Kitabu cha Matendo ya Mitume tunaona kuwa, Roho Mtakatifu aliposhuka siku ya Pentekoste alikuja kama AHADI…..wanafunzi waliambiwa wasubiri tu …..ni ahadi ya muda mrefu….Petro aliianza kuithibitisha AHADI HII toka katika kitabu cha Nabii Yoeli…….Hawakuambiwa wafanye lolote, ujio huu ni sehemu ya Mpango wa Mungu wa mrefu….

  Na siku ya Pentekoste AHADI HII ilikamilika Roho alishuka na KUWABATIZA (kuwazamisha ndani ya Kristo) (ubatizo wa Yohana uliwazamisha ndani ya maji) na ujio huu uliambata na ISHARA nyingi kama UVUMI KAMA UVUMI WA UPEPO, NDIMI ZILIZOGAWANYIKA KAMA NDIMI ZA MOTO na Wote WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU (Kwa hiyo KUJAZWA ROHO MTAKATIFU na KUBATIZWA KATIKA ROHO MTAKATIFU, KUPOKEA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU ni kitu Kimoja……Kwa kufuata Maneno ya Yesu Mwenyewe alivyonukuliwa na Luka! Rudia tena Matendo 1:5 (MTABATIZWA) Matendo 1:8 (MTAPOKEA NGUVU) Matendo 2:4 (WOTE WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU)

  Je sisi tumevuviwa zaidi ya Luka tunapojaribu kutenganisha Jambo hili……..katika context hii…..

  Tukirudi upande wa ISHARA…..Je Kulikuwa na ishara ya KUNENA KWA LUGHA TU watu WALIPOBATIZWA na WALIPOPOKEA NGUVU na WALIOJAZWA ROHO MTAKATIFU siku ya Pentekoste? Jibu ni Hapana….? Je unaweza kuorodhesha Ishara mbali mbali zilizoambata na kuja kwa Roho Mtakatifu…..(nadhani sina haja ya kuziorodhesha)

  Hata kama utaamua Kutetea Ishara ya Kunena kama ndio ISHARA PEKEE…..Petro kwa kuthibitisha ujio wa Roho Mtakatifu kwa kutumia andiko la Yoeli 2:28-32 anavunja hoja hiyo, Kwani andiko alilotumia HALINA KABISA KUNENA KWA LUGHA…….bali linatimiza Maandiko ya Waebrania 2: 3-4 JE SISI TUTAPAJE KUPONA TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII AMBAO KWANZA ULINENWA NA BWANA UKATHIBITISHWA KWETU NA WALE WALIOSIKIA, MUNGU AKISHUHUDU PAMOJA NAO KWA ISHARA NA AJABU NA NGUVU ZA NAMNA NYINGI NA MAGAWANYO YA ROHO MTAKATIFU KAMA ALIVYOPENDA MWENYEWE.

  Kwa nini leo mafundisho yatokee ya KULAZIMISHA ISHARA MOJA…tu kama sehemu kuupokea WOKOVU? UTASEMAJE JUU YA ISHARA YA NGUVU JUU YA MITUME ILIYOSHUKA SIKU HIYO ya kutangaza Injili…? Nguvu ya Roho Mtakatifu ilivyokuwa ikishuka pasipo Ishara ya miujiza…?

  Na hata kama tunang’ang’ania Kunena kwa Lugha kama Ishara ya KUBATIZWA/KUJAZWA/KUPOKEA ROHO MTAKATIFU……Mbona asilimia 100% ya Wanapompokea Roho Mtakatifu leo hata kwa mara ya Kwanza mbona wanazungumza kwa Lugha isiyoeleweka?Kinyume kabisa na siku ya Pentekoste! Ambayo Lugha ilieleweka watu waliposikia matendo makuu ya Mungu kwa Lugha zao? Je leo wanapokea Karama…? Na kama ni Karama mbona hakuna tafsri….? Maswali haya yanavunja dhana ya kutetea baadhi ya experiences za zinazofanyika Leo kwa kutumia Matendo 2:4 kama mfano wa kuufata na kuhalalisha yanayofanyika leo…..!

  Hebu tujiulize Kuna ISHARA ngapi ndani ya Biblia zinazoambata kwa watu walipoamua Kumfuata Yesu….? Je ni vyema kuchukua Ishara moja na kuifanya ya PEKEE NA kuamua kuijengea mafundisho?

  Hebu kila mmoja wetu hapa atoe ushuhuda wake jinsi alivyompokea Yesu……! Je kwa nini kupokea Nguvu za Roho Mtakatifu tunataka Ishara Moja ya Pekee….!

  MBARIKIWE- Nawatakia Mapumziko ya mwisho ya wiki mema.

 103. Ndugu John Haule, Masanjila na wengine

  Ni kweli yaonekana tunatoka nje ya mada. Ingawa kumbe kulishawahi kuwepo mada ya ubatizo huko siku za nyuma, lakini mimi nadhani kujitokeza tena kwa jambo hili katika mada hii ni udhihirisho tosha kuwa sasa jambo hilo linaingia katika ukamilifu wake, kwani karibu wakati wote lilipojitokeza liliambatana na lugha, haswa mwanzoni, pale msingi wa kanisa ulipokuwa ukijengwa.

  Maelezo aliyoyatoa ndugu Orbi, kimsingi ni toshelevu sana kiufafanuzi katika kuvitenganisha; kipawa na Mtoa kipawa. Lakini napenda kwenda mbele kidogo kuyaleta mambo hayo katika jinsi tunavyoyatumia kutuongoza kiibada.

  Kwanza yaonekana katika mjadala tuliokuwa nao, wengi wetu tumechanganya mambo mawili ambayo ni tofauti na kulifanya MOJA! Kunena kwa lugha na kujazwa Roho Mt. ni vitu viwili tofauti licha ya sisi kuvilazimisha kuwa kimoja. Biblia inatueleza waziwazi kuwa kunena ni kipawa cha Roho Mt anachokirimiwa muumini. Roho Mt anazo karama 9 tofauti ambazo huwakirimia kusanyiko lake ili kuliongoza katika njia yake. Karama za Roho Mt si Roho Mt!!! Jambo hili ndilo linalolisumbua kanisa hasa siku hizi ambapo wanafellowship, wakarismatiki nk nao wananena jambo ambalo huko nyuma, tokea upentekoste ulipoanza halikuwepo, kunena kwa lugha kulikuwa ni kwa wapentekoste tu mpaka miaka ya 60 vilipoingia vikundi vya karismatiki. Kuanzia hapo imekuwa ni tafrani katika ulimwengu wa kipentekoste. Kosa walilofanya la kuitafsiri kazi ya Mungu kwa akili zao ndilo linalowagharimu leo hii. Wao walipotafsiri Kunena kwa lugha na kukufanya ni Ishara ya Kujazwa Roho Mt , katika umbali waliofika, hawana uwezo wa kulisahihisha jambo hilo kama kundi, nako kuibuka kwa hao wanakarismatiki na kunena kwa lugha bila ya ubatizo wa maji mengi, ambao ulionekana ndicho kigezo cha kujazwa huyo Roho Mt, kumewachanganya hata sasa hivi hakuna kinachoeleweka! Hao wasiobatizwa maji mengi wanaishara kama za wapentekoste na pengine kuwazidi! Basi linapojitokeza suala la kujazwa Roho Mt, tegemea mjadala mkali usio na mwisho maana rejea yao wote ni kanuni yao walioitunga na kuigeuza kuwa Neno la Mungu.

  Maelezo ya kwanza tunayopewa kuhusu kunena kwa lugha kunapoanza ni katika Mdo 2:38 tunapoambiwa nasi “Tutapokea kipawa cha Roho Mtakatifu…” hajasema “tutajazwa Roho Mt” !! Ukipokea kipawa cha Roho Mt leo, hakitafanya kazi tofauti na siku ile ya pentekoste na katika instances zilizofuata, akikunenesha kwenye kadamnasi ya watu atafanya kama alivyofanya siku zile, atatafsiri! Biblia ndiyo kigezo tulichopewa, ukidhania imekosewa katika chochote kile utakuwa umechukua njia ya mauti kwa hiyari yako mwenyewe! Leo unapozungumzia ubatizo, inakuwa kama mtu unayeongelea jambo lisilo na umuhimu, kila mtu anakwambia mtafute Roho Mt, kwa maana iliyojificha, anakwambia tafuta kunena kwa Lugha!!!

  Siku tulipowaona karismatiki wakinena kwa lugha na ishara nyinginezo wakizidhihirisha licha ya kuendelea na ” Salaam Maria” zao, hilo lilipaswa kuwa ishara kwa wapentekoste ya kulitafakari upya neno la Mungu ili kubaini mahali walipokosea! Lakini hawakufanya hivyo. Wao wakalifurahia hilo wakiamini kuwa sasa wamemgeukia Mungu! Bali hiyo ilikuwa ni ishara ya mwanamwali mpumbavu akiyaendea ‘mafuta’!

  Hebu kirejeeni alichokisema Orbi, kuhusu Ahadi ya Yesu kwa mitume inayohusu kumpokea Roho Mt.; INAZUNGUMZIA NGUVU! Nguvu ya kuihubiri injili katika jinsi yote. Roho Mtakatifu ndiye NGUVU ya Kanisa!!! Yule mwanamke aliyekuwa akivuja damu alipotafuta kuligusa pindo la vazi la Kristo AKIAMINI kuwa atapona, alifundishwa hilo? Hata hao waliokanyaga kivuli cha Petro wakapona, walifundishwa? Ukimuamini Mungu, unamvuta Roho Mtakatifu akuhudumie katika dhiki yako. Roho Mtakatifu katika utimilifu wake akiwa ndani ya Kristo, alipoguswa vazi lake, alimpungukia yule mwanamke kumponya, naye Kristo akahisi NGUVU kumpungukia, akageuka kumtafuta na kuongea naye. Kunena ni jambo zuri na lenye kumtukuza Mungu, iwapo litatokana na Mungu. Maana huwezi kumtukuza Mungu nje ya mpangilio wake, hataikubali ibada hiyo!

  Wapendwa hizi lugha zinazonenwa si za kiBiblia!!! Maana kunena kwa lugha kunakuwa ni ishara pale anapokuwapo mtafsiri ambaye ni Roho Mt., nayo ishara maana yake ni ‘a pointing finger’ kwa Roho Mt. ambaye huwa ndio huo ujumbe au injili wanayoletewa hao waliopo; “Maneno haya nisemayo ni Roho na Uzima”. Hata tunawaona akina Petro na Wayahudi alioongozana nao kwa Kornelio wakihubiriwa na nyumba ya Kornelio hata wenyewe kukiri na kuamua wawatimizie Haki yote kwa kuwabatiza! Umeona? Lugha ni LAZIMA ieleweke! Paul alipofundisha wengi hatukumuelewa vizuri; anasema hivi, Roho Mtakatifu asipokuwepo, MSINENE! Mkinena bila Roho Mtakatifu MTAKUWA WENDAWAZIMU!!! Nalo neno la Mungu halitanguki, hebu wazia ni wangapi wanaopata wendawazimu makanisani leo hii wakati wa ibada nao hawajui kuwa ni wendawazimu hata wanawashawishi na kuwafundisha watu wengine kuwa wendawazimu??!!!

  Wapendwa, turudini katika maandiko tusahihishe ubatizo wenu kwanza. Twendeni pale Mdo 2:38 tuleni dozi hiyo nasi tutapokea KIPAWA cha Roho Mt kama ilivyokuwa kwa wenzetu! Tusidanganyike na vipawa, vipawa vyote vinaweza kuigizwa, kama mnavyoviona leo hii vilivyotapakaa kila kona na kila mmoja anadai kujazwa Roho Mt halafu anakwambia kubatiza watoto au kunyunyiza maji au maji mengi yote sawa tu mradi ujazwe Roho Mt!! Jamani Roho Mtakatifu akija na kuchukua utawala wa kanisa, sote tutawekwa katika kweli moja. Migongano itaondoka. Hebu kagua hizi posti zetu, angalia tunavyosigana, lakini sote tukidai kumuwakilisha Roho Mt. kila mmoja kwa staili yake. Wengine ukiwarudisha kwenye maandiko wanajifanya hawajaona, unawauliza maswali kuhusu walichokiandika wakidai kuongozwa na Roho Mt. wanajifanya wako bize na mada mpya, ni aibu kubwa kwa kanisa kunga’ng’ania kuendelea kuongozwa na ROHO anayeyakimbia maandiko!

  Mwalimu wa mambo haya ni nani? Wapentekoste, walipouacha ubatizo wa kiBiblia na kujitungia kanuni yao ya kujazwa Roho Mt kuwa ni kunena, wakamfungulia mlango Roho wa Uongo, ndiye anayeendelea kulichanganya kanisa na huenda Kristo akarudi na kulikuta kanisa limegubikwa na uongo licha ya kila muumini kubeba Biblia yake kwapani, sijui itakuwaje siku hiyo, sipati picha!!!!

  Mungu atupe ile ‘NGUVU’ itusahihishe katika UPENDO!

 104. John Haule,

  Kwa sehemu kubwa kinachofanyika leo katika kunena kwa lugha ni abuses…….kwa mtazamo wangu mimi abuses hizi zinaweza hata kupelekea kumfukuru Roho Mtakatifu ambaye baadhi yetu wanadhani wanamtetea…………..kwani kinachofanyika leo kwa sehemu kubwa ni kinyume na maandiko yenyewe yalioandikwa kwa kuvuviwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ……..Kwa kifupi ndio maana kuna kelele nyingi makanisani…lakini HAKUNA NGUVU ZA MUNGU……Wengi hawaishi maisha matakatifu……..Hakuna ushindi dhidi ya Dhambi………hakuna uaminifu….hakuna upendo wa kweli wa sisi kwa sisi kama ndugu na dada Katika Kristo…..Roho Mtakatifu sio nguvu ya kupiga Kelele na kusema kwa lugha nyingine tu….ni zaidi ya hapo……Roho Mtakatifu ni Nguvu ya Mungu katika Maisha ya mwamini inayomuezesha kuishi Maisha ya tabia za kiungu duniani….!

  Hebu angalia hata kwenye Blog hii….maelekezo ya Kujazwa Roho Mtakatifu yanavyotofautiana….! Mara inabidi kufundishwa………Mara inabidi uwe umebatizwa na maji mengi…….Mara inabidi uwe kwenye maombi……..Mara mchungaji wako akipinga hata wewe huwezi kuulewa…..!Naona wanaogopa kusema tu anayepinga yuko dhebu la “dini”sio la Kiroho…ndugu zangu baadhi ya tunaondika hapa baadhi yetu inawezekana tupo tuko madhehebu ya Kiroho na tumebatizwa kwa maji mengi…..Kwa kifupi hatuandiki kutetea experiences zetu bali maandiko…….wala sio Maandiko……!

  Na kama ulivyosema hatujaona mambo mengi yakifanyika Kinyume na Maandiko katika baadhi ya Makanisa yetu kinyume kabisa na Biblia ili watu wajazwe au Wampokee Roho /Wabatizwe kwa Roho Mtakatifu….?

  Je hujaona Kunena kwa Lugha kwa baadhi ya watu ni kule kule yaani kunafana au kuigana?….! Kunawakati kunakumuiga yule aliyekuombea kuupata Ujazo huo……..Au kunakumuiga Mchungaji wako………au yoyote yule ambaye wewe umemuweka kuwa yuko juu Kiroho kuliko wewe…! Jirani yangu alikuwa ni mtu muombaji wa usiku wa manane mtaa mzima ulisikia akiwa katika maombi…..kwangu halikuwa jambo baya sana…..lakini ile lugha yake ilikuwa ni ile ile…maneno yale yale…….miezi nenda miezi rudi….hata majirani wengine waliweza kuikariri…..Lakini Kilichonistua zaidi nilipofungulia TV na kukuta Nabii wake, kule anakoabudu jirani yangu naye anaomba kwa Lugha ile ile….Maneno yale yale….! Inaleta maswali mengi..mno ..!

  Wale wanaoishikilia kunena Kwa Lugha kuwa ni Lazima kwa kila muumini….wanaruka maandiko mengi mno yalio wazi kuhusu Roho Mtakatifu….lakini wanatuhumu Wakristo wenzao kuwa wanamopinga Roho Mtakatifu kuwa hawaoni Ukweli wa Ujazo huu….Je ndugu zangu nami nauliza hamuoni abuses nyingi zinazofanyika kwaJina La Roho Mtakatifu….?

  Mbarikiwe…..

 105. Asheri,

  Hii ni post iliyokuwa sehemu nyingine kuhusu watu kujaa Roho Mtakatifu pasipo kunena kwa Lugha…..

  Ni Biblia ipi hiyo inayofundisha kuwa mtu anayejazwa Roho Mtakatifu matokeo yake ni Kunena kwa Lugha….tu?”…? Hata Yesu alisema mtapokea Nguvu………matokeo ya Mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu ni Nguvu anayopata ya kumtetea KRISTO….KUMUHUBIRI KRISTO….KUWA TAYARI KUMFIA KRISTO……Hivyo ndivyo navyoona ndani ya Maandiko……….Je Maandiko haya hayako ndani ya Biblia yako…….

  1. Matendo 4:8- 13 Ndipo Petro AKIJAA Roho Mtakatifu Akawaambia……..walipoona UJASIRI WA PETRO……

  (Hakuna kunena lugha yoyote hapa……bali Ujasiri wa kutangaza Kristo)

  2. Matendo 4:31 Hata walipokwisha Kumwomba Mungu mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”

  (Hii inazidi kuthibitisha maneno ya Yesu ya Kupokea Nguvu……sio lugha wala kunena….)

  3. Matendo 7:55 ” Lakini yeye (Stephano) AKIJAA ROHO MTAKATIFU AKAKAZA MACHO…….AKASEMA…….

  (Stephano alipojazwa Roho Mtakatifu…..alipata Nguvu….Ujasiri….hakuna Lugha au kunena lugha mpya……)

  4. Paulo alipojazwa Roho Mtakatifu Magamba yalimtoka ( Matendo 17:39)

  Matokea ya Kujazwa Roho Mtakatifu sio Kunena kwa Lugha…..bali ni ujasiri/Nguvu ya kushuhudia Kristo……

  5. Kunena Kwa Lugha katika Matendo ya Mitume kuliambata na NGUVU /UJASIRI wa kunena Habari za Mungu na ili kuwafikia kundi la watu waliojazana Yerusalem Roho Mtakatifu aliwawezesha MITUME Kunena kwa Lugha INAYOELEWEKA……..Kila mtu alisikia Matendo ya Mungu kwa Lugha yake Mwenyewe……..!

  6. Matendo 2:41- 42 Lile kundi la watu elfu lililopokea Neno la Mungu kwa Mahubiri ya Petro…….lilibatizwa na kuendelea na mafundisho ya Mitume pasipo kunena kwa Lugha…..Je Petro alisahau kuwafanyia ubatizo huo….!

  6. Lugha “ISIYOELEWEKA” INAYOONGIZWA na Roho Mtakatifu kama itazungumzwa mahali ambapo pana Kundi la Watu (waumini) Ni LAZIMA IWE NA TAFSRI……..Hivyo ndivyo anavyosema Paulo katika Kitabu cha Corintho…..

  7. Paulo anataka TUNENE KWA LUGHA KAKINI HALAZAMISHI Kunena kwa Lugha…….anasema tutake sana Karama za Rohoni…..ambazo ziko nyingi…….

  8.Paulo anasema anayehutubu ni MKUU kuliko anenaye Kwa Lugha…..

  Asheri……..Maandiko haya yako katika Biblia yako…..?

 106. Wapendwa..

  Katka maisha yangu ya Wokovu pia nimewahi kuona Mhubiri akihutubu kisha kunena kwa lugha,Naye mtafsiri ,akitafsiri kwa kunena kwa lugha pia ,Je hayo sio mazingaombw!!?Kama yule mhubiri ananena kwa ajili ya nafsi yake au ni Unabii
  sasa kwanini mtafsiri ananena lugha tena,Kinachofanyika sio maandiko ni mapokeo ya kibinadamu,ilipaswa mtafsiri awe amejazwa Karama ya Tafsiri za Lugha ili atafsiri ule ujumbe ulionenwa na Mhubiri kwa karama ya lugha ile isiyofahamika Na yeye mtafsiri atafsiri ktk lugha ya kawaida inayoeleweka na hao wanaohubiriwa ili kanisa/kusanyiko lile wapate ule ujumbe.

  Je Tumetweza Unabii na Kumzimisha Roho!!!?

  Naomba kujifunza toka kwenu wapendwa

  Tunajifunza

 107. Mpendwa,
  Msanjila,Hoja yangu ilikuwa tuzungumzie kuhusu Roho mtakatifu kama mada na mada ya ubatizo ilikuwa tueendeleze na ile Thread ya ubatizo wa maji mengi ni lazima?
  Ktk hii mada najifunza toka kwenu wote wanaochangia,kwa sehemu nimepokea toka kwako unachangia vizuri tu,Pia Orbi,kwa hiyo najifunza.

  Kwa ufahamu wangu,Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na maandiko ya Orbi kuwa tumekuwa tunapewa maundisho mengi ya ufunuo wa kibinadamu na wala sio maandiko.

  Ktk wokovu huu nilionao nimeona watu wakinena kwa lugha wala hawajawahi kubatizwa kwa maji mengi wala maji machache,hata habari ya darasa la Roho Mtakatifu hawana.Ni pale tu walipompa Yesu maisha yao awe kwa Bwana/Mwokozi/Mfalme kwao

  Hebu tafakari nami pale Petro alipokuwa anagonga Injili ya habari njema ya amani ya Yesu,pale Kaisaria kwa mcha Mungu Kornelio na jamaa zake,Wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe Roho Mtakatifu aliwashukia. Imeandikwa ..Matendo10: 44-47

  Pia nimeona wapendwa ambao wamempa maisha yao Bwana Yesu lakini hawakunena kwa lugha mpaka siku walipobatizwa ndipo wakanena.Ukisoma metendo ya mitume 19:1-6,hawa mpaka walipobatizwa kwa jina la Yesu,

  Kuna wale mia na ishirini walimpokea Roho Mtakatifu wakiwa wambatizwa kwa ondoleo la dhambi(Ubatizo wa Yohona)

  Pia nimeona ambao wamepokea Bwana na wamebatizwa maji mengi lakini hawaneni kwa lugha, lakini ninaamini kuwa wamejazwa Roho Mtakatifu.kama SIVYO wasingeweza kukua kiroho wangebaki kuwa watoto wachanga

  kwenye kundi hili ndio hao wanaofanya mafundisho ,wanatamani karama za Roho,kwa hiyo wanahitaji kuomba karama.sawasawa na Paul anavyotufunza kwenye 1kor14:11

  “Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.

  Kwangu mimi Karama za kunena kwa lugha ni kitu kipana sana,Ni kuwezeshwa na Roho Mtakatfui mtu anapewa karama
  Kuna karama ya kunena kwa lugha inayoeleweka tunaita karama ya UNABII,mfano wa kina Agabo.
  Kuna karama za aina za lugha tunazoziona ktk matendo2:4 na marko16:17 huyu ananena na Mungu hakuna asikiae ni uvuvio 1kor14;2

  Kuna karama za tafsiri za lugha hii mara nyingi unaambatanana karama ya aina za lugha,Kwa hii tuona wapakwa mafuta wa Bwana wengi wakati wakihutubu ghafla ananena kwa lugha halafu anaendelea kuhutubu,Tunaona kuwa hakuwa anazungumza sisi bali na Mungu kwa ajili ya nafsi yake,inaweza kuwa anapewa ufunuo wa kile anachohutubu au vinginevyo. Hawa tunawapata 1kor14:5

  Masanjila umeandika
  ……..,lazima yawepo mafundisho sahihi ya Roho mtakatifu na nguvu zake ndipo ujazo uwepo,japo ni ahadi lakini lazima maandalizi na mafundisho.Lakini pia upo uhusiano wa ubatizo wa maji mengi wenye mafundisho sahihi na ujazo wa Roho mtakatifu,kama”

  Sio lazima kuwe na mafundisho ya ujazo na nguvu zake Roho Mtakatifu kama maandalizi,
  Ni apendavyo Roho,lakini kama unatamani karama unaweza kuomba sawa na 1kor14:11

  Kuhusisha kunena kwa lugha na ubatizo,Kwa sehemu nafahamu kuwa Ubatizo una maana tofauti tofauti ukisoama mandiko mojawapo tunaona Bwana Yesu akizungumzia ubatizo wake wa kusurubishwa msalabani”Luka 12: 50 “
  ‘Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe! ‘

  Ndipo nilitoa hoja ni vema suala la ubatizo tuendelee na ile mada ya ubatizo wa maji mengi ni lazima?, kina John Paul walitafakari kwa kina na kimo.

  Kwa hiyo Mpendwa Masanjila Bwana akutie nguvu kazi yako unayofanya hapa si bure.

  Huu ndio ufahamu wangu Masanjila ,nahitaji kujifunza toka kwenu wa SG,

  Barikiwa

 108. Naomba nijue kwanza muuliza swali,umefaidika na nini katka yoote haya yaliyoelezwa humu,maana wewe ndiye mlengwa mkuu. CUTHBERT,Lazima kila aliyeokoka anene kwa lugha,sababu,ndiko tunakoipata nguvu ya kiroho,maana nafsi yetu inajengwa haiwi dhaifu (1 Kor 14;4) Pia elimu hii yakunena kwa lugha itakuwa ngumu kwako kama humo kwenye makanisa yanayoamini nakupokea kipawa hiki,maana hata anaekuwekea mikono Mchungaji wako lazima awe amejazwa Roho mtakatifu,Lakini pia kama Mchungaji wako amejazwa Roho mtakatifu lakini kila anapokuombea bado hujazwi,basi nakushauri endelea kusubiri kwa hamu kubwa (KUAMINI) na kudai kwa Mungu maana hii ni ahadi kwao wote waliookoka au kumwamini Yesu,sio wewe pekee yako ambaye umekuwa unasubiri kipawa hiki lakini hujapokea,hata wengine walisubiri ,lakini hatimae siku ya siku wakapokea,ili mradi tu,maisha matakatifu na bila kukata tamaa,maana ukikata tamaa,shetani ataingiza kutokuamini na hatiama hata kumbeza Mungu,yaani kuona kama kitu hiki ni cha watu fulani tu. KUHUSU KWANI NI LAZIMA UFUNDISHWE ILI UPOKEE KIPAWA HIKI;( Mdo 19;2) Paul aliuliza,Je mlipokea Roho mtakatifu mlipoamini (yaani mlipookoka) wakajibu ,la hata kusikia kwamba kuna Roho mtakatifu,hataukusikia (Warumi 10;17..)Imani huja kwa kusikia neno laKristo,ili umpokee Roho mtakatifu,imani inahitajika,na huwezi kuwa na imani kama hujasikia,na wakati unasikia ndipo kwenye mafunzo kwenyewe,haiwezekani Roho mtakatifu aje juu ya mtu asiyeelewa nini kinaendelea,maana ikiwa hivyo huyo mtu atashangazwa kwamba nini kimempata,lakini akipata mafunzo trena yaliyo sahihi,haitakuwa shida kwake,inawezekana kabisa kwamba watu wengine hawampokei Roho mtakatifu sababu hawajapata mafundisho sahihi,ndio maana makanisa mengine tangu yaanzishwe,hawajanena kwa lugha sababu hawajapata elimu hii,lakini wakiipata,nakuhahakiishia,watajazwa Roho mtakatifu vizuri kabisa,ndio maana nimetangulia kukupa mfano wa (Mdo 19;2) kwa kuwawalikuwa hawajawahi kusikia habari za ujazo wa Roho mtakatifu,kwa hiyo hawakuweza kupokea kipawa hicho, (sawa ndugu yangu Orbi na wengineo ? La msingi ni kwamba,kila mkrist oaliyeokoka,anapaswa kujazwa NGUVU YA rOHO MTAKATIFU ILI ANENE KWA LUGHA,NA APATE NGUVU YA KIROHO,KINYUME XHA HAPO HUTAKUWA MKRISTO KAMILI ( Mdo 1;8) Lakini Mtapokea nguvu, akiisha wajilia juu yenu Roho mtakatifu (mdo 1;4) ….aliwaagiza wasitoke Yerusalem,bali waingoje ahadi ya Baba (Luka 24;49 Lakini kaeni humu mjini hata mvikwe uwezo utokao juu….Ujazo wa Roho mtakatifu ni muhimu na lazima,hata Yesu aliwaambia wanafunzi wake,wakati anataraji kuondoka,wasitoke mjini mpaka WAVIKWE UWEZO UTOKAO JUU,Yesu aliona umuhimu wa Roho mtakatifu akaona ili wanafunzi wake waanze kazi ya Mungu,lazima wajazwe nguvu kwanza,karama zooote alizozitaja Paul,zote zinategemea kipawa cha Roho mtakatifu ,ndio maana Yesu alisema ,Luka 24;49,WASITOKE MPAKA KWANZA WAVIKWE UWEZO UTOKAO JUU,(WAJAZWE ROHO MTAKATIFU.

 109. Shalomu,

  Ndugu Orbi,

  Nakushukuru kwa maonyo uliyotupa kuwa tunapojadili hapa tunasomwa na wengi, hivyo tuwe makini na kile tunachokiandika. Napenda nikiri pia kuwa uko makini katika michango yako mingi unayochangia hapa.

  HATA HIVYO ndugu yangu Orbi, katika kumjibu mtoa hoja hapo juu, hujatumia maandiko kuonyesha kuwa si lazima mtu kunena kwa lugha. Ulichoongea ni maoni yako tu. Nasema hivyo kwasababu nilitegemea ungetuonyesha mahali ambapo Biblia inaonyesha kuwa mtu anaweza kujazwa na Roho Mtakatifu lakini asinene kwa lugha kama ishara. Ama ungetuonyesha mahali ambapo Biblia inasema si muhimu mote wanene kwa lugha kama ISHARA YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU.

  Nakuomba tena, utuletee ushahidi kimaandiko kuwa mtu anaweza akajazwa na Roho Mtakatifu bila kuonyesha ISHARA YA KUNENA KWA LUGHA.

  Naomba pia utenganishe kati ya KARAMA ZA LUGHA na KUNENA KWA LUGHA KAMA ISHARA.

  Mungu awabariki.

  Shalomu

 110. Ndugu Merere Cuthbert,

  Nashukuru mno kwamba wewe uliyetuletea mada hii uko pamoja na nasi….angalau unafuatilizia hata kwa kusoma tu…..hivyo naamini tunapoandika hatupigi ngumi hewani…….nashukuru mno kusikia umejifunza mengi…….!

  Umeuliza tena kwa nini Mtu alyeokoka na ISHARA ZOTE NYINGINE ZIMEONEKANA KWAKE ameombewa SANA na ameomba mwenyewe Lakini ameshindwa kunena kwa Lugha….!

  Swala la kuijuliza kama Ishara zote za Roho Mtakatifu zimeonekana kwako au kwa huyo mtu aliyeokoka uliyemtaja, sasa kwa nini utafute ishara nyingine….? Kama kweli umeokoka, umeona Mungu amebadili maisha yako…umeona Mungu amekupa nguvu ya Kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu…anakupa nguvu ya kumshuhudia na kumtangaza kwa maisha na matendo yako…..unaona Mungu anajibu maombi yako……katika maisha yako….anazungumza na wewe katika Neno lake…unatafuta nini cha zaidi…….!

  Biblia inasema….MUNGU NAYE AKISHUHUDIA PAMOJA NAO KWA ISHARA NA MAAJABU NA NGUVU ZA NAMNA NYINGI……NA KWA MAGAWANYO YA ROHO KAMA ALIVYOPENDA MWENYEWE (Heb 2:4)

  Mungu analeta ISHARA na MAAJABU…..Kwa waliompokea Kama ANAVYOPENDA MWENYEWE……..Paulo anauliza…….Je wote ni mitume…….? wote wanatenda Miujiza…? Wote wana Karama za kuponya Magonjwa….? Wote wanena kwa Lugha…? Angalia Ishara na Maajabu aliyosema Nabii Yoeli……..Uvumi wa upepo wa nguvu……..ndimi za moto……na mambo mengine mengi…….! Usilazimishe wa kulazimishwa kuwa na Ishara moja pekee…..mwachie Bwana nafasi afanye kama anavyopenda Mwenyewe…!

  Kama ishara nyingi za kupokea Wokovu zimedhihirika kwako kwa nini kulazimisha Karama….?

  Naona swali lako linajibu maswali mengi yanajitokeza Leo…….wengi wanafundisha na kudhani Karama fulani ni bora zaidi……! Wengi wanataka KULAZIMISHA kwamba katika mwili wa Kristo wote tuwe….sikio……wote tuwe kichwa…….wote tuwe macho……nk…! Na ndio maana tunapata mafundisho kama haya ya wote LAZIMA Tunene kwa Lugha…….!

  Paulo amefundisha kutaka Karama zilizo kuu…..! Lakini hajaorodhesha Karama kuu ni zipi……na hata kama Kunena kwa Lugha ni Karama…….basi sio Karama kuu kwa Mtazamo wa Paulo….! Kuhutubu…(Kuhubiri) Habari za Mungu na siri ya Injili…….ndio yalikuwa maombi ya Paulo…….”MKIDUMU KUWAOMBEA WATAKATIFU…..PIA KWA AJILI YANGU MIMI NIPEWE USEMI WA KUFUNGUA KINYWA CHANGU ILI NIHUBIRI KWA UJASIRI ILE SIRI YA INJILI……HATA NIPATE UJASIRI WA KUNENA JINSI IPASAVYO KUNENA (Efeso 19-20)

  Hebu tutake Karama za Rohoni……Hebu Tuchochee Karama tulizo nazo……!

  Mungu AKUBARIKI….umetupa changamoto kubwa kwa kuleta mada hii……

 111. Ndugu Masanjila,

  Ni wapi katika Biblia walipompokea Roho Mtakatifu kwa kufundishwa kwanza?Je Siku ya Pentekoste walikaa na Kujifunza ?…..ndio Biblia yako inasema? Paulo anauliza Je mlipokea Roho kwa …..au kwa kusikia kunakotokana na Imani…..? Tumeona wengi “Wakifundisha” Kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia mbali mbali mno….lakini ni hivi ndivyo Maandiko yasemavyo……? Nimeona watu wakisema….Asante Yesu……Asante Yesu….mara mia……matokeo yake ni kulazimisha ulimi useme chochote….na nimeona kwa mtindo huo baadhi ya makanisa wananena kwa lugha ile lugha anayonena mchungaji wao…..!Je Huku ndio kufundishwa kumpokea Roho Mtakatifu…….! Au Je kuna mahali katika Biblia inasema tufunge na kuomba ili tupokee kitu ambacho ni Ahadi tuliyoahidiwa toka Kwa Baba……? Tulipokea Ahadi ya Wokovu wa Yesu kwa kufunga?……Sasa kwa nini tupokea Roho wake wa Ahadi kwa kufundishwa……! Nimeona katika mahubiri mengi Wachungaji wakisema….fungua mdomo….pokea sasa……anza kuzungumza………Je haya ni mafundisho ya Biblia…….? Na kama ukitetea hili….ni lipi sasa utazuia ambalo likija kwako haliko kwenye maandiko…..? Mtazamo wangu ni kuwa kila siku chukua tahadhari kwa kitu chochote kile ambacho hakijasimama kwa miguu minne katika maandiko.

  Ndugu yangu Masanjila inawezekana kabisa unafundisha kumpokea Roho Mtakatifu kama dini yako au labda mafundisho ya kanisa lako yasemavyo…..nahisi tu lakini sidhani unaleta msimamo wako kama Biblia inavyofundisha…….bali nataka kuamini unazungumza Kanisa lako linavyofundisha……! Kumbuka kwamba sipingi Kunena kwa Lugha……..kwa sababu nimeona ndani ya Biblia ni mojawapo ya Ishara iliyokuwepo siku ya Kushuka kwa Roho Mtakatifu……na Biblia imesema ni mojawapo ya Ishara………Biblia nayosoma inaonyesha kushuka kwa Roho Mtakatifu kunadhirishwa kwa NGUVU ya kumtangaza Kristo……na ndio dalili ya kwanza…….na hata siku ya Pentekoste ilikuwa hivyo……..WATU WALISIKIA MATENDO MAKUU YA MUNGU

  Kushuka kwa Roho Mtakatifu kunaweza kuambatana na Ishara mbali mbali…….angali tena kitabu cha Yoeli……..ambako hata Kunena kwa Lugha hakupo katika orodha ya Yoeli…….

  Na kunena kwa Lugha kunapokuwa ni sehemu ya Karama…..basi kunatumia na mtu binafsi kati yake na Mungu kuwasiliana kumjenga…..ama sivyo lazima tafsri iwepo….na pia kwa utaratibu…! Haya ni mafundisho ya Paulo aliyeandika sehemu kubwa ya Maandiko………

  Paulo HAKUZUIA kunena kwa Lugha kama wengi wanavojaribu kufanya leo…… na Paulo HAKULAZIMISHA kunena kwa lugha kama wengine wanavojaribu kufanya leo……..Na wala Paulo hakufundisha kujenga NAFSI kwa njia ya Kunena ni bora zaidi ya Kujenga nafsi kunakotoka na KULISIKIA NENO LA MUNGU NA KULIWEKA MOYONI…….!Paulo alitaka sana tunene kwa Lugha kama kitu cha binafsi ….tukiwa peke yetu…..na wala sio kitu cha kujivunia na kuonyesha sisi ni bora kiroho…… hayo ndio matatizo yaliyosumbua kanisa La Korintho ambalo naona yanasumbua baadhi ya makanisa leo……..

  UBARIKIWE.

 112. Kama nimekuelewa vizuri ndugu John Haule,je unawashauri ambao hawaneni kwa lugha ya Roho Mtakatifu waendelee kusubiri tu kwa kuwa ni mpango ulio ktk kalenda ya Mungu ?Ninachoelewa huwezi kumpokea Roho mtakatifu mpaka kwanza ufundishwe,na baada yakufundishwa unapata kiu Yh 7;37-39 Mtu akiona kiu na aje kwangu,huwezi kuwa unapinga halafu Roho mtakatifu aje kwako ndio maana Mdo 2;37 inasema’walipoyasikia haya wakchomwa mioyo yao ,wakamwambia Petro na mitume wengine tutendeje ndugu zetu ndipo Petro akawaambia,tubuni ,mkabatizwe nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu.(Mdo 19;2-Paul nae alikuwa akiuliza wanafunzi kama baada yakuamini je walimpokea Roho mtakatifu,kwa hiyo unaweza kusema unamwamini Yesu ,lakini udhihirisho hasa ni kumpokea Roho mtakatifu……..,lazima yawepo mafundisho sahihi ya Roho mtakatifu na nguvu zake ndipo ujazo uwepo,japo ni ahadi lakini lazima maandalizi na mafundisho.Lakini pia upo uhusiano wa ubatizo wa maji mengi wenye mafundisho sahihi na ujazo wa Roho mtakatifu,kama ungeweza kuhudhuria ktk ubatizo wa wapendekoste,ungeshuhudia hili saa ya ubatizo,watu wengine hapohapo hujazwa Roho mtakatifu,hata Yesu mwenyewe Roho mtakatifu alikuja juu yake mara baada tu yakubatizwa na Yohana.(Math 3;16).Lakini pia habari ya kubatizwa kwa maji mengi ni muhimu sana wala si yakudharau hata kidogo,lakini hakumfungi mtu ambaye amemkiri Yesu wakati hakupata nafasi yakubatizwa,ila inamfunga yule ambaye muda na nafsi alikuwa nayo yakubatizwa lakini akadharau,huyo kwa kweli,atakuwa ameonyesha dharau kwa Mungu,maana hata Yesu alisema ,lazima tuitimize haki yote,mbona watu wengine,wamelichukua jambo hili kwa uzito ingawa si kibiblia,wamefikia hata kuwabatiza watoto wadogo,na kama mtu ikatokea mwanawe akafariki kabla kubatizwa atasikitika,kana kwamba mtoto yule ataenda motoni,ingawa Yesu alisema waacheni watoto wadogo waje kwangu Yesu aliwabariki tu watoto (Marko 10;14 ) nimefika mwisho lakini bado nasisitiza kwamba,ifike mahali kwamba tufikie mwisho mwema,wala isiwe tumepoteza wakati wetu bure,mruhusu Roho mtakatifu aseme nawe wala usiweke mipaka yakuwaza kwamba,mbona wazazi wangu na ndugu na dini yangu wanaamini hivi,ukaona kwamba hivi ndugu zangu au dhehebu langu lote limepotea ? kama kweli unayo nia ya kweli ya MUNGU,hakika nasema Mungu ataonekana kwako,lakini ikiwa lengo lako ni kupinga tu pasipo kutulia nakutafakari,utapoteza mudawako bure,Mungu awabariki wote.

 113. Haleluya!
  tangu niulize swali hilo nimekuwa nikifuatilia suala hili kwa umakini mkubwa hasa michanganuo mbalimbali kutoka kwa watumishi wa Mungu,nashukuru sana kwa kuwa nimeelewa kadri mlivyoeleza,ila changamoto iliyopo kichwani mwangu ni hii:
  Kwa nini mtu mwingine ALIYEOKOKA (NA ISHARA NYINGINE ZA ROHO HUONEKANA KWAKE) anaombewa sana,au anaomba mwenyewe sana lakini bado hapokei uwezo wa kunena kwa lugha mpya?
  ni kwamba Roho hugawa karama apendavyo?
  Kama ni hivyo kwa nini tuseme ni LAZIMA KILA ALIYEOKOKA ANENE KWA LUGHA?
  au kuna shida gani kwa mtu huyo?
  Anatakiwa afanye nini?

 114. John Haule,

  Nashukuru kwa mchango wako…..hata mimi nilikumbuka mada hiyo……lakini naona kwenye mjadala huu naona ndugu yangu Masanjila anakuja na mambo mapya kila leo……! Kuwa na mtazamo tofauti kuhusu Kunena kwa Lugha kunamfanya Ndugu Masanjila aamini labda umebatizwa na maji machache…..! Kunena kwa lugha hakuna uhusiano wowote na ubatizo wa maji Mengi au machache…….Je wale watu mia Ishirini siku ya Pentekoste walibatizwa ubatizo wa maji mengi….? Roho Mtakatifu alishuka kutimiza ahadi ya Baba (Mungu) wala si kwa ajili ya juhudi Maombi yao….au kusubiri kwao….!Ujio wa Roho Mtakatifu ulikuwa kwenye Kalenda ya Mungu kama vile Ujio Wa Yesu kuokoa wanadamu…….! Binadamu hakufanya kitu chochote kuanzisha mpango wa Mungu……….Na hakufanya chochote siku ya Pentekoste….bali alisuburi tu akiwa kwenye maombi kusuburi ahadi ya Baba itimie……..kama vile Zakaria alivyokuwa akifanya ibada Hekaluni ni kusubiri ujio wa Masiha……

  Nadhani vile vile ndugu Haule tunapojadili kitu mtandaoni tusijaribu kukimbilia kushuku…….Kwa vile huyu hakubaliani na mimi…basi ni kwa ajili ya Mafundisho ya mchungaji wake……..au lazima kabatizwa kwa maji machache……….au mtu wa “dini”……au hajaingia kwenye maombi…….Je maombi yanaweza kufanya tuwe na mitazamo sawa……..!..Au kwa vile sijaelewa kama wewe basi mimi si mtu wa Maombi……?Naamini Maombi yanaweza kufanya tuwe na mitazamo sawa ndio!….lakini pia Maombi hayo hayo yanaweza kutufanya tuwe na mitazamo tofauti…bali yakatupa UWEZO WA KUCHUKULIANA………! Wale watu wa Beroya walipolipokea Neno toka kwa Paulo hawakuingia kwenye maombi…….. bali walilichunguza lile Neno ili kuona kile kilicholetwa na Paulo kilikuwa ni sahihi……..Hata Petro alipotetea Kunena kwa Lugha alisema hiki ni kile kilichotabiriwa na Nabii Yoeli……. Hakusema mkingia kwenye Maombi mtafunuliwa….mtaelewa…….!

  Naamini mada hii inataka TUYACHUNGUZE MAANDIKO…..tukianzia hapo hapo Matendo 2:1-3 na kwenda mpaka mstari wa mwisho katika Biblia unaouzungumzia Kunena kwa Lugha na Kubatizwa kwa Roho Mtakatifu kwa Muumini……..Hatujengi mafundisho ya Biblia kwa kutumia mstari mmoja tu….au personal experiences zetu tu………….tunapongalia na kujenga fundisho lolote katika Imani ya Kikristo tunaingalia Biblia kwa Mtazamo mpana…..bila kubakiza mstari hata mmoja kuhusu fundisho hilo……na kujaribu kujibu kila swali linalojitokeza……Huku ndiko kuyachunguza Maandiko……..! Naamini kama tunataka kuitumia Blog hii kwa kuwafundisha wengine hii ni njia tusiyoweza kuimbia……UBARIKIWE!

  Nakushukuru ndugu yangu Haule kwa mchango wako………UBARIKIWE.

 115. Mdo 11;16 UNAELEWAJE UNAPOSOMA NENO UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU MAANA WA MAJI UPO NA UNAELEWEKA JAPO NAO TUNAHITAJI MAELEZO NA NAAMINI MUNGU HATATUACHA JUU YA MJADALA HUU UENDE BILA YA FAIDA KWA WATU WAKE NA NDIO OMBI LANGU. JE WA ROHO MTAKATIFU ? AU WEWE UMEJIJUAJE KAMA UMEJAZWA ROHO MTAKATIFU ? JE NI LUGHA IPI YA ROHO MTAKATIFU UNAYOINENA ? MAANA SIKU YA PENTEKOSTE WALISIKIKA WATU WAKINENA ,WALISIKIKA WATU WAKISEMA LUGHA YA WATU WENGINE (MFANO UMSIKIE BIBI YAKO AMBAE HAKUSOMA AKISEMA KIINGREZA MDO 2;8 NINGEPENDA TUFIKIE MUAFAKA WA JAMBO HILI ILI IWEPO FAIDA YA MJADALA HUU NDIO MAANA KILA NINAVYOJIZUIA NISIUSEME NAJISIKIA KUUSEMA TU,LABDA MUNGU ANA MAKUSUDI KAMILI

 116. Amani ya Bwana Yesu iwe juu yenu nyie watakatifu mliopendwa,

  Wapendwa Sam na Orbi itakuwa jambo jema kujishikamanisha zaidii na mada kwa habari ya kunena kwa lugha ,hii ya ubatizo huko siku za nyuma ilipatwa kutakafariwa sana na wapendwa,Tafadhali angalia hii Link(URL)chini hapa

  https://strictlygospel.wordpress.com/2008/07/16/swali-8/#comments

  Mada:Ubatizo wa maji mengi! kwani ni lazima kuzamishwa?

  Unaweza ona wapendwa John Poul,Mch Dr Malisa,mwenda,na wengineo wengi wakichangia,Nadhani jambo jema kama tunatafakari habari ya ubatizo kwa sehemu hapa ni jambo la kupendeza kama tutaiendeleza Thread hii ya ubatizo wa maji mengi kwani ni lazima? hili tujifunze zaidi kuhusu Ubatizo na kupata ili tuzidi kupata neema na ufahamu tukijifunza/kuyaunganisha na yale,vinginevyo hapa twende mkabala na mada iliyopo mezani.

  Naomba kutoa hoja

 117. Nakuunga mkono Noela Msanyila maelezo yako ni sawa kabisa,pamoja na hayo kujazwa Roho mt.inahitaji juhudi sana ktk kumuomba Mungu na utakatifu wengi mtihani huu unakuwa mgumu,wanageuka kupinga jinsi ya kupokea Roho mt.na kuzusha maswali ya udadisi na kutaka kula kitu lazima kiwe kimeandikwa biblia imeweka wazi haikuwezekana kuandikwa kila kitu wino na karatasi zisinge tosha.

  kwani wapi imeandikwa wagonjwa wakipita juu ya kivuli cha mtumishi watapona? mbona yalitokea kwa akina petro.utendaji kazi na udhihirisho ni ngumu kuufahamu kwa udadisi wa kujenga hoja hauna mwanzo wala mwinsho maana Roho mtakatifu ni Mungu.

 118. Ingekuwa ni kweli kwamba Mkristo wa kweli hatetei jambo lolote kama Madhehebu yake yanavyosema,basi nafikiri hata wewe uungeshaanza kujiuliza kwamba hivi kwanini madhehebu yetu yanabatiza watoto wadogo au wachanga,wakati ktk biblia watoto wadogo au wachanga walibarikiwa tu(Marko 10;13-16) Akawakumbatia ,akaweka mikono yake juu yao,AKAWABARIKI.(Luka 18;15-16 Wakamletea na watoto wachanga ili awaguse……na mstari wa 16 waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie, maana watu kama hao ufalme wa Mungu niwao,watoto wana tiketi ya mbinguni hawahitajiki kubatizwa,SAWA Orbi,

 119. Kwani tangu tuanze,kuelezea habari za Kunena kwa lugha katika mada hii ilivyo,ni lipi ambalo mlikuwa hamlifahamu na sasa mmelikubali ?maana lazima nijue kwanza hapo ili,nijue au tujue pakuanzia au kuendelea (1)Je mnaamini kwamba udhihirisho wa mtu kujazwa Roho mtakatifu ni kunena kwa lugha na ndiyoishara kuu ya kwanza ? au mnaamini kwamba,nguvu ya Mungu inamjia mtu baada ya Roho mtakatifu kuja juu yake Mdo 1;8 ? Je mnaamini kwamba,ishara ya aliyemuamini Yesu moja wapo ni KUNENA KWA LUGHA,na kinyume cha hapo,hutakuwemo kati yao waaminio ipasavyo (Marko 16;17) (Mdo 10;44-46)’Mataifa nao walimwagiwa kipawa cha Roho mtakatifu maana waliwasikia wakisema kwa lugha,nakumwadhimisha Mungu,(1 Kor 14;22 Lugha hizi ni ishara si kwao waaminio,bali kwao wasioamini,…… ,Paul anasema wazi kuwa ishara hii ya lugha ni kwao wasioamini yaani Kunena kwa lugha, 1Kor 14;4 Kunena kwa lugha kunajenga nafsi, 1 Kor 14;2’5 anenaye kwa lugha hasemi na watu bali Mungu,nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha 1 Kor 14;39 sizuie kunena kwa lugha…..baada ya maandiko yooote haya na mengine mengi nimeyaacha kipi ambacho mmekipata na kipi ambacho mnakikataa,Roho mtakatifu ni nafsi nyeti sana,Maana Yesu alisema heri mtu amkufuru Mungu ATASAMEHEWA kuliko kumkufuru Roho mtakatifu hatasamehewa ktk ulimwengu huu na hata ule ujao (pia kama hujui ulimwengu ujao uliza)(Math 12;31-32)kwahiyo tuwe makini pia ktk kujifunza,mruhusu Mungu afanye kitu ndani yako,na kama unayo nia hasa yakutaka kujua hasa,MWAMBIE MUNGU KWA DHATI YA MOYO WAKO KABISA KWAMBA’NAOMBA UNIFUNULIE JAMBO HILI’MUNGU NI MWAMINIFU ATALIFUNUA KWAKO.

 120. Ndugu Orbi,
  Kwanza, tuwekane sawa katika hili la watu waliokufa bila ubatizo wa maji mengi kupata nafasi tena ili wabatizwe, hili halipo na wala hakuna maandiko kuhusu hilo! Nadhani hukunielewa tu.

  Kuhusu yule mwivi msalabani, huyo alikuwa ni mwenye dhambi aliyemtambua Kristo na kumpokea pale msalabani kwa ukiri thabiti alioutoa hapo, kama alivyomuomba, Kristo alimtimizia, ‘Yesu akamwambia, Amin nakuambia, leo hivi tutakuwa pamoja peponi’. Sasa huyu yalimfika hayo kabla ya Injili ya Wokovu haija achiliwa, lakini dhabihu ya dhambi ikitolewa. Hivyo huyu twaweza kuventure kuwa aliungana na Watakatifu wa Agano la Kale ambao Kristo alishuka kuzimu kwenda kuwafungulia akiwa amekwisha kuwalipia deni ya dhambi zao!

  Niliongelea kuhusu ‘wokovu’ unaoonekana leo hii ambao sisi huingizwa humo kwa kukaririshwa hicho kifungu cha Rum 10:9. Baada ya hapo hujifunza kunena na mwishowe huwa wajuzi! Lakini Biblia inasema wazi kuhusu hiyo Injili iokoayo, ‘Aaminiye na KUBATIZWA ATAOKOKA, asiyeamini ATAHUKUMIWA’. Neno ndilo linalo ‘zigawanya roho na nafsi…’ Sasa sote katika umbali huu twafahamu kuwa Yesu ni Neno, nayo sehemu ya Neno hilo ndiyo hiyo hapo inayotutaka tuliamini na kisha tubatizwe ikiwa ni ishara ya kulipokea hilo neno, au kwa maneno tuliyoyazoea “Tumempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wetu!” Sasa kwa anayeukataa ubatizo wa maji mengi, anakuwa amempokea nani, askofu wake au nabii wake au Papa wake? Maana Yesu ndiye huo ubatizo!!

  Je, waliokufa wakiwa wamempokea Kristo katika vipindi bila ubatizo wa maji mengi vipi….? Mungu wetu ni mwingi wa Rehema. Hakuna fundisho asilolijua, anajua ni kiasi gani litawaathiri wanae, na pia anajua umbali gani hilo litafika. Kwa hiyo huwatayarishia njia ya kutorokea. Moja wapo ndio hicho kifungu cha Rum 10:9. Leo kinatutatanisha kutokana na tafsiri. Kimewekwa katika urahisi fulani ambao si halisi (ukichanganya na mambo ya miujiza, ndiyo hakuna kinachoeleweka). Dhambi au Wokovu, vyote hivi huamuliwa mahakamani! Basi maana halisi ya ‘kukiri’ waweza kuipata mahakamani. Mtu anakiri mambo yaliyomtokea na sio atakayoyafanya au kukariri vifungu au kumimic baada ya kiongozi wako! Kwanza unahubiriwa Injili, inakukamata, unajiona ulivyo mwenye dhambi wewe mwenyewe, UNATAMANI kupatana na Mungu, maana umejitambua kuwa umetokana na Yeye, unajitupa chini mavumbini na suti suti zako unalia ukijutia na kumsihi Mungu akusamehe, asikuunganishe katika kesi na wale waliomsulubisha mwanae, hawa wanao likana Neno lake hata leo hii (zamani haya makanisa yanayonena, walikuwa wanaliaaa!), kisha unatumbukizwa majini pamoja na mambo yako ya miaka yooote ya uasi; unapoibuka toka huko chini ya maji ulikozikwa, ni KIUMBE KIPYA! Yule jeuri na muasi umemuacha kule chini ya maji, umemzika! Maisha yako yamekuwa waraka wa Kristo kwa jamii inayokuzunguka; wewe sasa, ukiulizwa na wahuni wenzio, wale wa zamani, kulikoni? Ndipo UNAPOKIRI kwa kinywa chako yaliyokutokea. Vivyo kwa aliyekwenda umbali wote huo lakini hakupata fursa ya kubatizwa.

  Kwa hiyo, tukilitazama jambo hili katika maana yake halisi, twaweza kufaidika nalo zaidi kwa kuyatimiza yale yanayotupasa, kuliko kung’ang’ania mapokeo huku tukiyaona wazi yalivyo kinyume na maandiko yanavyotutaka tuitimize hiyo haki ili tupate kuokoka, au wokovu wa kweli!

  Nimejaribu tu kuyajibu hayo maswali, lakini suala lenyewe bado twaweza kulifuatilia zaidi kwa pamoja katika maandiko ili kujihakikishia usalama wetu kwanza tunaopenda kuandika andika kwenye blogu, halafu ndio usalama wa wasomaji; usishangae, ndio kibinadamu!!!!!!
  Ubarikiwe!

 121. Sam,

  Hebu nieleze maana ya nukuu yako hii…..

  ‘Kuhusu yule mwivi msalabani, naamini hesabu yake itakuwa pamoja na wale mamiloni waliouawa kwa kumpokea Kristo wakati wa Dark Ages, yaani wale ambao hawakupata fursa ya kuitimiza haki yote, waende wakabatizwe kama ilivyo amriwa kuhusu kuokoka, hivyo wao Mungu aliwatayarishia mlango wa kuingilia ambao ndio hicho kifungu cha Rum 10:9 ambacho sisi tunakitumia bila sababu ya msingi,…..”

  Sijaelewe….ina maana wale Wakristo huko nyuma ambao hakubatizwa ubatizo wa maji mengi watapata nafasi ya kubatizwa tena…….?

  Kwa nini wawe waumini wa Dark Ages tu…….?Je waliouawa vipindi vingine vya historia utasemaje……..? Je ubatizo huo utarudiwa kwa Waliouawa tu……..Je waliokufa wakiwa wamempokea Kristo katika vipindi bila ubatizo wa maji mengi vipi….?

  Kwa hiyo pasipo maji Mengi hakuna Mbingu…….?

  Hebu tupe Maandiko…..! Ya kurudia ubatizo tena baada ya kufa…….!

  Hebu tupe tafsiri yako sahihi ya Rom 10:9……..maana unasema kifungi hicho sisi tunakitumia pasipo msingi………

 122. Sam……

  Sijapinga ubatizo……nakataa tu maana ambayo Ndugu Masanjila anaijenga……anauondoa ubatizo (kwa mtazamo wangu) kwenye context ya Biblia…….

 123. Ndugu yangu Masanjila,

  Labda tuwekana sawa tena, hivyo uelewe wa neno la Mungu umefungwa katika mipaka ya uwelewa mchungaji….? Maana umesema nanukuu…. “habari hii ya Kunena kwa lugha,ni ngumu kuielewa kwa wewe mfuasi ikiwa kama hata Mchungaji wako bado haielewi na anaipinga”

  Mkristo wa kweli ufahamu wake haujengwi juu ya mchungaji hata awe na “upako” wa aina gani….! Awe anatoka Dhehebu linalobatiza kwa maji mengi au Machache…….awe anatoka dhehebu linalojiita la “Kiroho” au La…! Msimamo wa Mkristo umejengwa Juu ya Neno la Mungu tu….!

  Halafu uelewa wa Neno la Mungu hauhitaji kwamba Mchungaji wangu anaelewa au la….! Mchungaji wangu anaweza kutoilewa Kweli fulani ya Biblia…….na hata Kuipinga….hii hainifanyi mimi au haimfanya Muumini kutoilewa Kweli hiyo……..Ni Mungu mwenyewe kwa njia ya Roho Mtakatifu anafunua UKWELI wa Maneno ya Mungu kwa Muumini yoyote aliyeamua kuitafuta Kweli….au aliyeamua kuyapokea mafundisho yoyote na kuamua kuwa Mberoya kwa kuyachunguza Maandiko kuona kweli ndivyo yalivyo ….na kukataa kuyakariri na kuyameza kama Kasuku……..eti kwa vile yametoka kwa Mchungaji/Mtume/Nabii/…….

  Ufahamu wa Mkristo hautakiwi kuwa wa kukariri………yawe ni mafundisho ya Dhehebu au mapokeo ya Kanisa….liwe kanisa la “dini” au la “kiroho” …….Hata kanisa likifundisha kuwa NI LAZIMA KUNENA KWA LUGHA…Lazima niangalie Je Maandiko yanasema hivyo….? Na hata likifundisha HAKUNA KUNENA KWA LUGHA……naingalia Biblia ili ionyeshe je Kweli…..?

  Narudia TENA…….Mkristo wa Kweli hatetei jambo lolote “kama dhehebu lake” linavyosema ……wala “mchungaji wake” anavyosema…..Bali kila siku anajiuliza….”JE YANENAJE MAANDIKO….?

  Jambo la kusikitisha sana naloliona kwa wengi ni kwamba, Wachungaji wengi sana na pia hata waumini huwa wanatetea zaidi Mafundisho ya Kanisa…..na wala sio mafundisho ya Biblia……..Ndio maana utasikia…..sisi Wapentekoste tunasema hivi………Sisi Wabaptist………Sisi Walutheri……….Sisi Efetha nabii anasema hivi……..Sisi wa Imani ya Msukule tunaamini kwamba……..Unajua Nabii……fulani anasema hivi….nk nk…..! Hii ni njia dhaifu mno ya Kuitetea Kweli ya Biblia……..KWELI YA BIBLIA HAIJAFUNGWA KATIKA KUTA NNE ZA MADHEHEBU YETU…!

  Hivyo ndugu yangu Masanjila usitetee Kunena kwa Lugha kama labda Wapentekoste wanavyofundisha…..na Wala usipinge Kunena kwa Lugha kama Walutheri wanavyofundisha……Sema nini Biblia inasema…..! Nini Biblia inafundisha…..!

  Hivyo ndugu yangu Masanjila baadhi yetu hapa kwenye Blog hatupingi wala hatutetei chochote kwa vile Wachungaji wetu wamesema….bali tunajaribu kuangalia JE MAANDIKO YANASEMAJE…….? Hapo ndio mahali Imara……

  UBARIKIWE……

 124. Ndugu Masanjila,
  Umenena vizuri katika kufika kwenye uhakika wa jambo!
  Kwanza ni muhimu tukafahamu ukweli juu ya makanisa yetu. Yapo ambayo hayaamini katika kunena wala uponyo (kundi lote la CCT na TEC)! Wao wanasema kuwa mambo hayo yalikwisha na mitume, leo hii hayapo, kwa hiyo wanaoyafanya ni waigizajitu! Lakini ndani ya makanisa hayo wamo waliompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao, kwa ukiri huo kama ulivyo katika Warumi 10:9; hao ni wanaFellowship na Karismatiki ambao kimsingi wananena kwa lugha na hawajabatizwa maji mengi, tena wengi wao walibatizwa utotoni kwa hiyo hawakuwa na fursa ya kuungama. Je stahili zao ni sawa na waliobatizwa maji mengi baada ya kutubu? Na hao wanaoyakana mambo hayo, je, wanaye ROHO MT.????

  Ndugu Orbi,
  Naamini tafsiri ya jambo, ni lile jambo lenyewe. Kwa mfano TV, chombo hicho hakina jina katika lugha zetu zote za hapa Tz kwa vile hatujawahi kuwa nacho! Nadhani hata Ubatizo, tafsiri halisi yapaswa kuwa kama ilivyo katika Biblia kulingana na Mungu alivyoileta huduma hiyo kwa maana maalumu. Ndio maana tunaiona ikiambatana na wokovu katika Injili. Kwa umuhimu wa Huduma hiyo tunaona Mungu akimleta nabii wake hata kubeba jina la Huduma hiyo – Yohana ‘Mbatizaji’. Na huduma ilifanywa mtoni au kwenye maji ‘mengi’, basi sehemu zote katika Biblia tunaposoma UBATIZO tunapaswa kuelewa hivyo ; sina uhakika kama Mungu alilibadili hilo.

  Kuhusu yule mwivi msalabani, naamini hesabu yake itakuwa pamoja na wale mamiloni waliouawa kwa kumpokea Kristo wakati wa Dark Ages, yaani wale ambao hawakupata fursa ya kuitimiza haki yote, waende wakabatizwe kama ilivyo amriwa kuhusu kuokoka, hivyo wao Mungu aliwatayarishia mlango wa kuingilia ambao ndio hicho kifungu cha Rum 10:9 ambacho sisi tunakitumia bila sababu ya msingi, sana sana tunajaribu kuukimbia ubatizo kwa kisingizio hicho tu, LAKINI TUNANENA KWA LUGHA!!!!

  Je, yawezekana Mungu ana DOUBLE STANDARDS?

  Mbarikiwe nyote!

 125. Ndugu yangu Masanjila.

  Kwa hiyo una maana wanaouliza maswali juu ya Kunena kwa Lugha ……wamebatizwa kwa maji madogo….? au hawamjampokea Bwana Yesu kama Mwokozi wao…..kwa kutubu dhambi na kuikubali kazi ya Msalabani….?

  Je ukibatizwa kwa maji mengi ufahamu na uelewa wa maneno ya Mungu unakushukia….? Kumbuka kuna mwizi msalabani bila ya ubatizo aliambiwa atakuwa na Yesu milele…….! Kumbuka Paulo amewahi kusema kuwa Mungu hakumwita kubatiza…..! Ina maana kuwa watu walikuwa wanajivunia Ubatizo……..! Ubatizo bila kuwakilisha kazi iliyotendeka ndani hauna maana yoyote……!

  Je unaweza kusema nini na juu ya Paulo na Sila kubatiza watu saa nane za usiku…….nje ya gereza…..? Kulikuwa na mto na mto hapo……inaonyesha aliwabatiza hapo hapo….Biblia inasema (wakati huo huo) (Soma Matendo 16:30-34) Nataka kukufungua macho tu kuwa Ubatizo ni sehemu ya Muumini lakini angalia sana usiupe maana ubatizo ambao haujapewa na Biblia………

  ubarikiwe

 126. Wapendwa (1)habari hii ya Kunena kwa lugha,ni ngumu kuielewa kwa wewe mfuasi ikiwa kama hata Mchungaji wako bado haielewi na anaipinga.(2)Habari hii ni ngumu kuielewa ikiwa kama hata Mchungaji wako bado anaamini ubatizo wa watoto wadogo,lazima utakuwa na maswali mengi maana unataka kumwabudu Mungu kulingana na mapokeo(3)Habari hii itakuwa ngumu ikiwa hata Mchungaji wako anaamini sala ya ‘mlaze pema peponi,mtu ambaye amekwisha kufa ambaye alipaswa atubu mwenyewe wakati akiwa hai Andiko lasema ktk Rumi 10;9 kwa sababu ‘UKIMKIRI’ Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana,na ‘KUAMINI’ moyoni mwako na ANDIKO LINASEMA KTK WAEBRANIA 9;27 na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja,na BAADA YA KIFO NI HUKUMU,maana kinachotakiwa ni ‘KUKIRI’ NA KUAMINI SASA MTU ALIYEKWISHA KUFA ANAWEZA KUAMINI AU KUKIRI, sasa kwa maelezo haya naomba tuelezane ukweli je Wachungaji wetu wanaamini nini juu ya haya niyasemayo,maana tusijetukawa tunampaka mafuta mtu ambaye hata kuoga hajaoga na hataki tutakuwa tunabandika uchafu juu ya uchafu, maana UBATIZO WA MAJI UNAENDANA NA KUUNGAMA DHAMBI (Mathayo 3;6) Kwa mfano rahisi tu,ubatizo baada ya kutubu ndiyo ubatizo sahihi,sasa kama ulibatizwa tena kwa maji kidogo utakuwa umeenda kinyume na neno eti ubatizwe bila kukiri kwa kuwa ulikuwa bado hujui ufanyacho,utawezaje kuelewa swala la ‘KUNENA KWA LUGHA’ Kwa ushauri wangu OKOKENI KWANZA NDIPO TUFUNDISHANE HABARI ZA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU,Mungu awabariki sana wapendwa.

 127. Mpendwa Orbi,
  Kwa upande wangu, maelezo yako sijapata kuelewa hata kidogo, naomba ufafanue kwa vifungu vya Biblia kwa kujibu maulizo ya Ndg. Sam,ili nami nijifunze na kuelewa! Ubarikiwe.

 128. Sam,

  Nisingependa kuwa nakwenda mbali na mada hii, lakini kwa ajili ya kujifunza tu na kusaidiana itabidi niandike….

  – Lugha iliyokuwa ikitumika kipindi cha Agano jipya inajulikana……Ni kipindi kipi cha historia kinajulikana….Tunajua Yesu alizaliwa Kipindi cha Herod the Great (Ambaye alitawala toka 37- 4BC)…..Injili ya Luka imeandika taratibu kwa mpangilio mno kwamba tunajua ni kipindi kipi na mambo mengine yaliyoambata na kuwepo kwa Yesu Ulimwenguni….Hivyo kusema hatujui Lugha gani ilikuwa inazungumzwa ni kukataa ufahamu wa kawaida tu…..Kumbuka kwamba tukio la Yesu halikuandikwa na Mitume tu…..kuna vitabu sambamba vya wakati huo viliandika habari za Yesu…….

  – Kama unasoma Maandiko (Vitabu vyote vya Agano Jipya) kwa umakini utaona wazi Wanafunzi wa Yesu na Wayahudi kwa ujumla hawamkujua kabisa Yesu ni Nani na Huduma yake……toka mwanzo walidhani ni Nabii Yule…….ni Elia……au Ni Mesiah anayekuja kuwakomboa katika dola ya Warumi…..hebu rudi tena kwenye maandiko hata Petro hakujua maana ya Yesu kwenda kufa msalabani…..hata waliojua Yesu ndiye Messiah hawakujua kama atakufa msalabani…….bado ilikuwa imefichika……Hivyo hata aliposema Eloi Eloi Lama Sabachtani …..Biblia inasema “Na baadhi yao waliosikia walidhani anamwita Eliya” ………walisikia anasema nini ……! Lakini haijazungumzwa ilikuwa lugha ngeni…… Kwa hiyo unaposema tungepewa sababu kwa nini hawakumuelewa….Injili nzima zinasema ” Alikuja kwao (Wayahudi) lakini Hawamkupokea”…….

  – Ufunuo wa Yesu ni nani na amekuja kwa ajili ya Nini ULIANZA kujulikana baada ya Yesu kufufuka…na aliporudi kwa Baba kwa kupaa na kunziwa Mbinguni na Kumtuma Roho Mtakatifu…….

  Kwa hiyo mpendwa Sam….hebu tusome Maandiko kwa upana wake…..!

  Ubarikiwe….

 129. Precious,

  Ubarikiwe!

  Kuna mambo machache yaliyojitokeza katika post zako ambayo ningependa kujifunza zaidi kutoka kwako. Ninanukuu hapa sehemu ya hayo nikiyaweka katika mtiririko ili niambatanishe maswali machache kuhusu hayo.

  1. “Tatizo watu wengi wanadhani Yesu alizaliwa ndo maana, bado hawafunguliwi. kilichozaliwa, ni kristo (mwana wa adamu) ila, Yesu(Roho) alishuka siku ile Kristo alipomwendea Yohana mbatizaji kwa ajili ya kubatizwa.”
  Je, maelezo haya uliyoyatoa, yana uhusiano wowote na maandiko (Biblia)? Ukitupatia vifungu hivyo itatuweka vizuri zaidi kuyafahamu mambo hayo katika kina hicho.

  2. “Watu wanadhani Yesu alikuwa mtoto tu wa Mariam na katika kuomba, utasikia wanatumia vyeo (Baba, Mwana, Roho), Mwishowe hawafunguliwi!
  Je, unaposema wanatumia vyeo, utakuwa unaukana UTATU MTAKATIFU? (kwani vyeo si nafsi)

  3. “Hawakujua kama wanatembea na Mungu (Baba).”
  Je, kwa maelezo hayo tuelewe kuwa YESU ndiye MUNGU BABA?

  4. “Ni muhimu sana tupate kujua Yesu ni nani?”
  Wengi wetu tungependa kulijua hilo kutoka kwako.

  Naamini ukiyaweka sawa hayo twaweza kuendelea vizuri pamoja

  Ubarikiwe!

 130. Wapendwa

  Italeta maana na faida kubwa kwetu sote wachangiaji na wasomaji, iwapo tutakubaliana kuwa, Mhimili au Nanga ya majadiliano yetu, iwe Biblia (ya vitabu 66), kuliko kuwa na mihimili mingi inayotokana na mafundisho yetu tofauti. Hilo litatusaidia sana katika kupanuana uelewa wa Neno la Mungu.

  Basi tunapoongelea kunena kwa Lugha, tunaliona jambo hilo likianza katika siku ya Pentekoste, maelezo yake tumeyaona na yametufunza yaliyojiri hapo. Mitume waliponena kwa lugha, waliokuwepo kila mmoja alimsikia kwa lugha yake! Hilo laashiria kuwa Roho Mt. alifanya kazi ya kumtafsiria kila aliyekuwepo pale. Pia twapaswa kuamini kuwa ilikuwa hivyo kila muujiza huo ulipotendeka, kwani katika kunena huko kulikuwa na ujumbe uliofikishwa kwa washuhudiaji wa jambo hilo, yaani hao waliokuwepo hapo (Mdo 10:44-47). Pia huko kunena (akiwepo mtafsiri, yaani Roho Mt) huwa ni ishara kwa wasioamini, maana hufikishiwa ujumbe! (1Kor 14:22)

  Lakini kwenu ninyi mlio itwa hata mmekusanyika pamoja, yaani kanisa, ninyi mkinena basi awepo wa kutafsiri. Maana mnenaji atakuwa na ujumbe kwenu ninyi nyote. Naye Roho alipoliweka angalizo hilo, nacho kipawa cha kunena kikiwa ni chake, yeye humlazimu kumuinua mtafsiri kati yenu, ili yooote yaende sawa!

  Lakini asipokuwepo mtafsiri, basi mnenaji asinene. Au mnenaji akiwa kwenye faragha yake, na anene, maana hayo ni kati yake na Mungu.

  Pia wachangiaji wengi wanasema kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu, lingekuwa ni jambo jema na la msaada mkubwa iwapo wangetupa na maandiko yanayosema hivyo au kufundisha hivyo ili tupate uhakika wa jambo hilo.

  Kuhusu yale maneno aliyoyatamka Kristo pale msalabani, “Eloi Eloi Lama Sabachthani”, michango mliyoitoa inaleta changamoto. Kama mlivyoitoa; tukisema kuwa alinena kwa lugha, hata wale waliokuwa jirani pale msalabani wakasema anamwita Elia, nadhani hatutakuwa mbali na ukweli, maana twaweza kusema hao waliodhani anamwita Elia walikuwa ni watu wa dini, ndio maana wanamjua Elia! Pili twapaswa kukumbuka kuwa huwezi kukijua mtu akinenacho katika lugha yoyote ile mpaka uwe unaijua lugha hiyo au awepo mtafsiri. Kwa hiyo twapaswa kujiridhisha kwanza kuwa siku ile hakuwepo mtafsiri kwa ajili ya lile kundi lililokuwepo pale Golgota. Na hivyo wale waliondoka wakijua kwamba Kristo alimwita Elia! Lugha gani aliongea hatujui, maana hayo hayakuandikwa siku hiyo!

  Lakini ilipofika saa ya hayo kuandikwa, ndio hayo tunayoyasoma kama Mtafsiri anavyotufunulia sisi tulio katika Pendo lake, yaani kanisa. Basi kama ilikuwa ni Kiaramu jambo hilo lilipofunuliwa kwao kwanza ndio hivyo walivyoliweka katika Biblia. Ila angekuwa amezungumza Kiaramu, basi tungepewa na sababu ya wale kadamnasi kutokukielewa alichokisema, tukichukulia kwamba Kiaramu ilikuwa ni mojawapo ya lugha zilizotumika katika jamii hiyo. Au labda angetuambia kuwa ufahamu wao ulifungwa ili wasielewe, lakini si hivyo. Kwa hiyo ni vizuri tukakubaliana na Maandiko kuwa, lugha aliyoitamka Kristo pale msalabani haikueleweka mpaka siku Roho Mt alipoiweka wazi kwao mitume nasi pia tuliompokea Kristo. Basi sisi ndio tunaojua alicho kisema katika maana kamili, lakini wafarisayo na wengineo katika rekodi zao watakuwa na ile hadithi waliyotokanayo viongozi wao kuwa “anamwita Elia”!

  Mbarikiwe!

 131. Ndugu Line,

  Maswali hayo si yangu mimi, nimedhani tu labda aliyeleta mada hii ndiyo anayo hata akaileta mada hii kwetu ……..yaani hizo zilikuwa ni assumptions zangu tu…………… na labda nilidhani kwa kujiuliza maswali haya tunaweza labda kufikia kiini cha mada yenyewe kama wewe ulivyosema………sikuona kabisa baadhi ya wanablog wakiangalia pande zote nne za Maandiko kumsaidia muuliza swali………Njia rahisi ingawa ni ndefu na Ngumu kujibu swali la Muuliza Mada….ni kuchukua MISTARI YOTE AU MAANDIKO YOTE KUHUSIANA NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU……..MISTARI YOTE INAYOZUNGUMZIA KUNENA KWA LUGHA…….HATUA KWA HATUA KUPITIA MAFUNDISHO YA PAULO KUHUSU KARAMA AU KUNENA KWA LUGHA………ndiyo naweza kujenga views mbali mbali nilitaka yaipeleke mada kwenye kiini chake……yaani iwafanye wanaochangia kuangalia mada pande zote za maandiko…….hiyo ndio njia ya kujifunza…….

  Kuhusu swali lako……sipendi kulijibu moja kwa moja…napenda zaidi kwa nia ya kujifunza kuona wachangiaji watasemaje…….Maana kama nilivyosema tafsri yoyote ya Andiko inakulazimisha kuangalia Maandiko mengine kama hayo na ikiwezekana yote yanayohusiana na pia context ya Andiko……na hilo Andiko ulilolite haliko pekee…..angalia…….1 Cor 14:15…na pia…..Yuda 1:20…..na unaangalia pia Maombi mengine ndani ya Biblia kwa mfano maombi ya Stephano…….aliomba akiwa Rohoni kwa maneno ya kawaida…… na akiwa amejaa Roho Mtakatifu mpaka akaona Mbingu…..Maombi mengi ya Paulo kwenye Nyaraka zake na pia Matendo ya Mitume….nk…..

  Kwa kifupi huwa naepuka kabisa kujibu swali kwa kutumia text moja ya Biblia…..ni njia isiyo yakini…na njia hii ya kutumia Text moja ndani ya Biblia moja kujenga fundisho hiyo inaleta utata hata na kutatiza wengi….mfano mzuri ni mada hii iliyopo mezani leo……..

 132. Ndugu Orbi, mimi binafsi ningependa kama ungeweza kuyajibu hayo maswali uliyojiuliza kama unayajua majibu yake maana yataipeleka hii mada kwenye kiini chake!. Hii itatufanya sote tunaofuatilia kuangalia pande zote za mada hii.

  Na kwa kuongezea labda nami niulize kwamba Je kuomba kwa Roho kuna maana ya kunena kwa lugha au kuna maana gani haswa? ( Efeso 6:18)

  Shalom

 133. Ndugu Noeli Masanjila,

  Mtu mweledi mara nyingi anakua tayari kujifunza na kukubali anapokosea, na huwezi kutetea hoja ya Biblia kwa kuilazimisha Biblia iseme isichosema, Kweli ya Biblia ina Nguvu ya Kujitetea, na mafundisho mengi potofu na yasio potofu mara nyingi hujengwa kwa kutoelewa historia ya Maandiko, Lugha iliyotumika,Kuyaacha Maandiko yatafsiri Maandiko, kuwa kimya Maandiko yanapokuwa Kimya,Kukataa kabisa kuweka maana unayoijua wewe katika Maandiko… Na Kama hivyo sio vitu muhimu Luka asingemwandikia Theofilo mtukufu kuwa anataka kuandika kitabu cha Luka kwa USAHIHI zaidi…! Alikataa kuandika anachodhani yeye…….na barua aliyodhani anamwandikia Theofilo mtukufu ikawa ni Maandiko matakatifu…..!Hatuikunji Kweli ya Biblia kujenga hoja zetu kwa fundisho lolote lile…!Na wala hatuogopi kusoma andiko ambalo linakwenda kinyume na uelewa na ufahamu wetu dhidi ya hoja tunayoitetea…!

  Hivyo nashindwa kuelewa unaposema tunapotosha mada…..mimi nadhani kwa wanaoelewa nilitoa mchango wangu kuboresha mada tu……na kutaka isizae uelewa potofu….! Je kuchangia mada unakozungumza wewe unataka kuweje…? Nimesoma michango mingi kwa upande wangu katika Mada hii lazima nikiri sikuona kipya ….kwangu mimi nadhani hawajamwelewa hata aliyeleta swali….

  Kabla hujajibu hoja/Swali lolote lile ni lazima ujaribu kuuliza mleta hoja alikuwa na maana gani…ni kipi kilichomsukuma…? Ni muumini au sio muumini….nini anataka kujua……..Kwangu mimi kwa kusoma tu swala la mada…”HIVI KUNA UKWELI MTU ALIYEMPOKEA ROHO MTAKATIFU NI LAZIMA AZUNGUMZE KWA LUGHA MPYA?
  Kama aliyeuliza ni Muumini (Mkristo) aliyeokoka basi unaweza na kujiuliza maswali mengi yaliyomsukuma kuuliza swali …….na maswali yaliyomtatiza yanaweza kuwa yafuatayo…

  1. Je ni kweli Maandiko yanafundisha kwamba Mtu aliyempokea Roho Mtakatifu ni Lazima azungumze kwa Lugha Mpya …? Hakuna Maandiko mengine mengi yanaoonyesha pia watu wakijazwa Roho Mtakatifu pasipo kusema kwa Lugha mpya…..!Tunatafsirije Maandiko hayo…..?

  2. Je Muumini anapookoka ni nini Kinatokea……..nafasi ya Roho Mtakatifu katika kuokoka ni ipi…Maandiko yanasemaje…?

  3. Je Kunena kwa Lugha mpya ni ISHARA pekee tu..au ni mojawapo ya Ishara kama Marko alivyosema katika Marko 16:17-18.Maana ziko ISHARA NYINGI ndani ya Biblia kwa Muumini aliyejazwa Roho Mtakatifu…..na Luka kataja Ishara nne…tu….labda muuliza mada anataka ufafanuzi…Kwa nini Ishara moja ndio iwe Kuu..?Maandiko yanasema hivyo….?

  4. Je inawezekana Kunena kwa Lugha ni mojawapo ya ISHARA…maana hata Petro aliposema katika Matendo 2:16 “kuwa Jambo hili ni lile lilonenwa na Nabii Yoeli”Kunena kwa Lugha hakupo kabisa ndani ya Maandiko ya Yoeli…..Je Petro alinukuu Maandiko visivyo…..?

  5. Labda Muuliza mada….ameambia autafute Ubatizo wa Roho Mtakatifu na Kunena kwa Lugha….kitu ambacho hakiona kikifundidwa na Mitume katika Agano Jipya….

  6. Au ni labda pia mleta Maada aliambiwa akizungumza /Akinena kwa Lugha anazungumza na Mungu moja moja na Shetani hasikii….Kitu ambacho labda alipotafuta katika Maandiko alishindwa kuona wapi imeandikwa……..

  7. Labda muuliza pia aliambiwa akinena kwa Lugha anajenga nafsi yake….Lakini aposoma Maandiko akakuta hata Neno kwa njia ya mahubiri linajenga nafsi yake…..sasa ni nini kinafanya kunena kwa Lugha kukawa kinajenga zaidi ya Neno…? Kipi kipo juu ya Mwenzake…..?

  8. Labda Muuliza mada ametatizika na Matumizi ya Kunena kwa Lugha tofauti kabisa na Mafundisho ya Paulo katika kitabu cha Matendo ya Mitume…….na kujiuliza Je ni Kweli ni Roho yule Mwenye Utaratibu anayefundisha Paulo…?

  9. Labda Muuliza mada baada ya kusoma Biblia akaona hakuna ususiano wowote wa Kunena kwa Lugha na kukua Kiroho na kuwa Karibu na Mungu……Kitabu cha Wakorintho kimefundisha hivyo…..?Labda ni hilo lilomtatiza.

  10. Labda pia ndugu yetu aliposoma 1 Cor 12: 28-31 akaona si Lazima Kunena Kwa Lugha…..na hata Paulo aliposema “Takeni Karama zilizo kuu” Je Ni lazima Karama hiyo iwe Kunena Kwa Lugha…?….na hata Kama kwa Ukuu…Paulo kasema Ahutubuye ni Mkuu kuliko anaenaye kwa Lugha…..

  Hivyo ndugu zangu niliposoma Mada hii sikujua nianzie wapi kuchangia….sikujua muuliza mada ana maswali yapi yaliyofichika………kwangu mimi haya ni machache sana niliyojiuliza….nilidhani wachangiaji wengi wangeligusa haya……..na nilipoona kuwa hata Yesu alinena kwa Lugha…nikatambua sasa mada inalazimishwa……..

  Huo ndio mchango wangu……..tumsaidie ndugu yetu……kwa kuiendeleza mada…..

  Mbarikiwe..

 134. Shalomu,

  Ndugu Noel na John Haule, namshukuru Mungu kuwa tunaendelea kujifunza katika hili, sifa na utukufu ni kwa Mungu anayestahili heshima, utukufu wote na adhama. Mungu awabariki.

  Ndugu Orbi

  Nakushukuru sana kwa ufafanuzi ulioutoa kusuhu maneno Eloi, Eloi lama sabakthan. Mungu akubariki kwa kutuongezea maarifa. Naendelea kujifunza katika hili.

  Katika mchango wako umesema kuwa “..na kuna baadhi ya maneno wakati wanaandika habari za Yesu walishindwa kuyapatia maana halisi kwa Kigiriki na kuyaacha katika lugha ya Aramaic……kama hilo tamko la Eloi Eloi Lama Sabachthani…..na kila watafsri wa Biblia katika lugha nyingine wameyaacha hivyo hivyo.” Kwa kuwa hivi sasa maana ya maneno hayo inafahamika na imewekwa wazi kwenye biblia kwanini bado waandishi na hawa watafsiri wanaendelea kuyaacha maneno hayo katika lugha hiyo?

  Hata hivyo, nadhani ni vema sasa turudi kwenye hoja ya msingi katika mada hii. Hapa sina maana kuwa masahihisho yasifanyike.

  Dada Rosemary,
  Nakushukuru kwa kuongezea, Mungu akubariki sana kwa ufafanuzi mzuri.

  Mungu awabariki,

  Shalomu

 135. Shalom wapendwa,
  asante kwa michango mizuri inayojenga, nami naomba kuongezea kwenye mchango wa ndg Asheri
  Kitu muhimu kujua kwa wanaouliza kuhusu kunena, ulazima na kwanini baadhi ya makanisa hawana ni kujifunza mwanzilishi na mtoaji wa karama alikuja kwa kusudi gani.

  1. Kwa kifupi ni Yesu ndiye alituahidi ujio wa msaidizi wake yaani Roho mt
  Yohana 14:15-17 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

  2. Ni ahadi ya wote waliompokea Yesu na kumpenda kama alivyoeleza ktk Yohana itakayoambatana na nguvu, kusema kwa lugha nyingine kadri Roho alivyowajalia, ikumbukwe kuna lugha za malaika pia ambazo binadamu hatutaelewa na hii mara nyingi imetajwa Yesu akiwa anaomba kwa faragha (kuugua rohoni kusikoeleweka)
  Matendo 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
  Matendo 2:4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

  3. Ni msaada wa jinsi ya kuomba, kuomba au kusema kwa lugha ni kumwachia Roho akuombee kadri Mungu apendavyo
  Rumi 8:26-7 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
  4. Ni moja ya silaha za Mungu kama ilivyoelezwa hapo juu, tunaambiwa kuomba kwa Roho kila wakati ni moja ya silaha tuliyopewa na Mungu
  Efeso 6: 1-18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

  Hivyo kusema au kunena kwa lugha ukiongozwa na Roho mt na si utashi wako ni muhimu kwa kila Mkrosto aliye hai. Mbarikiwe

 136. Naona Mada Mama inazidi kurukwa,ya kunena kwa lugha,habari ya historia ya lugha iliyotumika mahali wakati Yesu anahubiri,siwapingi lakini hiyo ni historia ambayo hata muislamu anaweza akaifuatilia na akatoa jibu sahihi,lakini habari ya Kunena kwa lugha inafanywa na mtu binafsi,si jambo dogo,hata Wakristo wengi linawachamganya,Mimi nafikiri tujadili hilo,na kama mmeweza kufuatilia ktk mitandao habari ya lugha aliyotumia Yesu na mkaamini kilichosemwa,nafikiri ni vema mkafuatilia na habari ya kunena kwa lugha mkatupa majibu ili tusihame saana mada kuu,Lakini nimependa sana changamoto zenu nami nimejifunza kitu kwa habari ya lugha alizotumia Yesu wakati anahubiri,MBARIKIWE.

 137. Samahani Orbi na wengine,nakubaliana na wewe na kila kitu ulichosema,Yesu aliposema Eloi Eloi Lama Sabachthani aliongea kiaramu.Swali langu nililowauliza wapendwa mnisaidie Wayahudi walikuwa wanafahamu kiaramu(sina uhakika)nilitaka kujifunzaa kwanini Yesu alipoongea Eloi Eloi Lama Sabachthani hawakumwelewa, ndilo swali langu,Samahani kwa wote niliwakwaza, hata mmwenyewe niliposoma bandiko langu la kwanza niligundua swali alikueleweka,nikalipanga tena mara ya pili.Kuhusu wikipedia nilikuwa namwelekeza Noel njia rahisi ya kuchanganya ulichonacho na wengine

  Barikiwa wote

 138. Ndugu yangu Haule,

  Mimi nilitoa ufafanuzi tu na Ukweli wa Historia usiopingika, Lugha iliyokuwa ikizungumza kipindi hicho ni Aramaic……umesema unatumia Wikipedia…basi nikurudishe kwenye Wikipedia…..

  Aramaic is a group of languages belonging to the Afroasiatic language phylum. The name of the language is based on the name of Aram,[3] an ancient region in central Syria. Within this family, Aramaic belongs to the Semitic family, and more specifically, is a part of the Northwest Semitic subfamily, which also includes Canaanite languages such as Hebrew and Phoenician. Aramaic script was widely adopted for other languages and is ancestral to both the Arabic and modern Hebrew alphabets.

  During its 3,000-year written history,[4] Aramaic has served variously as a language of administration of empires and as a language of divine worship. It was the day-to-day language of Israel in the Second Temple period (539 BCE – 70 CE), some speculate was the language spoken by Jesus,[5][6] is the language of large sections of the biblical books of Daniel and Ezra and is the main language of the Talmud.[7] However, Jewish Aramaic was different from the other forms both in lettering and grammar. Parts of the Dead Sea Scrolls are in Jewish Aramaic showing the unique Jewish lettering, related to the unique Hebrew language.

  Je Agano jipya iliandikwa kwa Lugha ya Aramaic ?…….Jibu ni hapana…….iliandikwa kwa Lugha ya Kigiriki…….Kwa maana katika kipindi cha cha Yesu Palestine ilikuwa inatawaliwa na Warumi (Romans) baada ya kuungusha himaya ya Kigiriki iliyokuwepo muda mrefu mno……Hivyo Maandishi Yote ya Agano Jipya tuliyonayo ya zamani (Old Manuscript) yako kwa Lugha ya Kigiriki…..Wala sio hata kwa Lugha ya Kiebrania…..!

  Na ndani ya hizo Old Manuscript unakuta Mitume waliaacha baadhi ya Maneno mengi tu kwa Lugha za Aramaic….nadhani nilikueleza……Je Yesu aliposema Ephata…..Talitha Kum……na mengineyo alinena kwa Lugha…?

  La msingi ndugu yangu Haule mbona una Maandiko mengi ya kutetea hoja yako ya Kunena kwa Lugha..? Tumia Maandiko mengi hayo yahusuyo kunena kwa Lugha ndani ya AJ….bali usipindishe ukweli huu wa Historia……Kanuni ya Msingi ya kutafsri Maandiko ni kutolazimisha yaseme yasichosema…..Na kufanya yaseme unachotaka wewe kusema……Wewe kwa kujaribu kutetea Kunena kwa Lugha kwa Kutumia mfano wa Yesu kunena kwa Lugha unalazimisha Maandiko yaseme yasichosema……!

 139. Hii Karama ya KUNENA KWA LUGHA ni ya Makanisa fulani tu,au ya mtu mmoja mmoja tu,maana naona makanisa mengine hayana kabisa karama hii,hata wachungaji wao hawaneni kwa lugha, nami naomba jibu.

 140. Napata swali na mimi lakini kulingana na mada kuu,kwamba Kama siyo lazima kwa kila mtu kunena kwa lugha,Mbona makanisa mengine hata huyo mtu mmoja anayenena kwa lugha,na mimi tangu ninakuwa ktk kanisa nililowakuta wazazi wangu wanasali sijamsikia hata mchungaji wangu akinena kwa lugha,Je hii ni karama ya makanisa fulani tu,au ni karama ya mtu mmoja mmoja ? Jamani tuache ubishi kama hatuna hakika na kunena kwa lugha,bora tutulie tuwasikilize ambao tayari wameshahakiki jinsi ulivyo ujazo wa Roho mtaktifu,KAMA HUNA UHAKIKA MUNGU SI DHALIMU,OMBA SALA HII KWAMBA ‘EE MUNGU NAOMBA UNIFUNULIE SWALA HILI KAMA NI KWELI AU LA,MUNGU ATAJIFUNUA KWAKO,NA KUJUA UNDANI WA HILI.’

 141. Noel

  Eloi Eloi Lama Sabachthani ni matamshi ya Kiaramu,
  Mara nyingi uwa natumia wikipedia kupata ufahamu wa wengine nachaganya na yale ninayojifunza kwa kusoma/kufunzwa biblia na walimu wangu,Nakushauri jaribu ku google utapata majibu.

 142. Ngoja niweke vizuri swali langu lieleweke,kwa nini Wayahudi kama walikuwa wanasikia kiaramu Kama lugha ya wakati huo,kwanini Bwana Yesu alipoita Mungu wangu kwa kiaramu Eloi Eloi Lama Sabachthani wao walidhani/walimwelewa kuwa anamwita Eliya?

  Soma Zab 22 yote, Kwa ufahamu zaidi

 143. Asante ndugu Orbi kwa maelezo yako mazuri,ambayo ni kama yamezua hoja nyingine nzuri na nimejifunza kwa hilo japo nitafanya uchunguzi zaidi kuhusu ‘Eloi Eloi’maana Mathayo 27;46-47inasema baadhi yao walisema anamwita Elia,lakini Orbi sijaona uzungumzie hoja iliyoko mezani ya kuhusu’kunena kwa lugha,tunaweza kupata kitu cha ziada na changamoto toka kwako,lakini mimi bado namshukuru Mungu kwa ajili ya Asheri,kwa maelezo yake anaonyesha amejazwa Roho Mtakatifu na ananena kwa lugha sina maswali naye

 144. Wapendwa kwa nini Bwana Yesu alikuwa anapenda kuongea lugha hii ya Aramaic!!!?,je wayaud/waebrania walikuwa wanaelewa aramaic na kama walikuwa hawamuelewi kwa nini!!Bwana Yesu aliongea wakati anajua kuwa hawamuelewi!!

 145. Ndugu Orbi,ubarikiwe kwa kuwaelewesha.Nafurahi sana tukiwa tunapata changamoto kama hizi.maana,zitatusukuma kutaka kujua zaidi yaliyo ya Mungu na kutufungua ufahamu kuhusu Neno.
  Ushauri:Tufurahie changamoto ikijitokeza maana,mtu hawezi kusonga mbele kiroho pasipo changamoto.Mbarikiwe!.

 146. Asheri na Noel Masanjila na wapendwa wengine pia,

  Kama mnatetea hoja au kupinga hoja basi tumieni Maandiko kwa usahihi.Hoja ya kusema Yesu kuzungumza Eloi Eloi Lama Sabachthani ni kunena kwa lugha inaonyesha wapendwa wengi hawajachukua hatua za ziada tu kujifunza angalau historia kidogo ya Maandiko, na mara nyingi ningeomba kwa vile kwa kuandika kwetu katika Blog hii tunafundisha wengi basi tutetee hoja kwa Maandiko yaliyo wazi na ambayo unajua kwa hakika yana maana gani…….maana kesho usije sikia Mchungaji anafundisha kwa bidii kwa kunukuu yale aliyopata toka kwako.

  Kwa kutusaidia tu kuwa kuna uwezekano mkubwa Yesu alizungumza lugha ya Aramaic, lugha amabayo ilikuwa inazungumzwa Palestine kipindi hicho cha Greco Roman karne hiyo…na kuna maneno mengi ya lugha ya Aramaic ndani ya Agano Jipya ambayo Yesu alitumia…..kama Talitha Kum…..Ephata……Abba……Raca…..Korban…nk

  Na lugha hii ya Aramaic ndio iliyotumika katika sehemu baadhi ya maandiko kama Ezra….Daniel…na Jeremiah…..Licha ya kwamba Maandiko mengi ya Agano la Kale yalikuwa katika lugha ya Kiebrania. Hivyo kusema Yesu alinena kwa Lugha aliposema Eloi Eloi Lama Sabachthani na kuwa alikua haeleweki ni hoja dhaifu mno……Yesu alieleweka kwa maana lugha iliyokuwa ikitumika ya wakati huo ilikuwa ni Aramaic.

  Halafu ileweke kwamba Maandiko ya Agano jipya tunayosoma leo awali yaliandikwa kwa lugha ya Greek….. na Rumi ilikuwa ni na mtawala tu… LAKINI lugha iliyotumika na wasomi ilibakia Greek…..Hiyo ndio lugha walitotumia Mitume kuandika Agano jipya…..na kuna baadhi ya maneno wakati wanaandika habari za Yesu walishindwa kuyapatia maana halisi kwa Kigiriki na kuyaacha katika lugha ya Aramaic……kama hilo tamko la Eloi Eloi Lama Sabachthani…..na kila watafsri wa Biblia katika lugha nyingine wameyaacha hivyo hivyo.

  Kama nilivyosihi hapo awali ni vyema kama Mungu amekupa muda na wasaa kujifunza haya maneno ya Mungu tunayoyahubiri yamefikaje kwetu, kwa njia gani yalitafsriwa…upungufu katika tafsri nk….. itatusaidia mno kwa sisi kuyaelewa na kufikisha ujumbe kwa usahihi zaidi

  Mbarikiwe.

 147. Ndugu yangu Asheri,nakupongeza sana hata Mimi umenipa kitu cha ziada na nimekikubali kwamba hata Yesu aliposema ‘Eloi,eloi lama sabakthan’ilikuwa ni kunena kwa lugha maana waliokuwa wanamsikiliza hawakumuelewa anasema nini. Ushauri wangu tu ni kwa wale ambao hawana uhakika na swala la kunena kwa lugha,wasisemeseme ovyo bora watulie maana wasije mkufuru Roho mtakatifu. Maana Yesu wakati anaponya watu,mafarisayo wakasema Yesu anatumia nguvu ya shetani,kwa neno hilo tu ni kufuru kwa Roho mtakatifu. Watu waelewe kwamba nguvu ya Mungu ndani ya mtu inapatikana kwa kunena kwa lugha lakini mtu mwingine anabisha wakati hata ukimwambia nipe tafsiri ya nguvu ya Mungu,hajui. Tulikaa sana makanisani pasipo kujua mambo haya,bali tuliyasoma kama hadithi,tulikaa na watu wenye mapepo makanisani,lakini wakuu wetu wa dini hawakuthubutu hata kuyakemea wala hawakuelewa cha kufanya,bali tuliabudu tu kwa taratibu tulizozikuta walizokariri wazazi wetu toka kwa wazazi wao,kwahiyo imefika wakati sasa wakuambiana ukweli,maana haifai kufichana,tusijekuhumiwa sote

 148. Shalomu,

  Suala hili liliwahi kujadiliwa kidogo katika ukumbi huu, ijapokuwa sikumbuki hasa mada yake ilisema nini. Katika mjadala huo nilitoa mchango wangu ambao nimeona vema niiurudie pia hapa ingawa nimeuboresha kulingana na michango mbalimbali iliyojitokeza.

  Tunapoliangalia suala la lugha kwenye Biblia hasa Agano Jipya, ni vema tutofautishe kati ya KUNENA KWA LUGHA kama ISHARA na LUGHA kama KARAMA ya Roho Mtakatifu.

  Naomba tukubaliane kuwa tunaposema kusema kwa lugha mpya au kunena kwa lugha inamaanisha kuwa mtu anasema kwa lugha ambayo hajawahi kujifunza au lugha ngeni. Anasema lugha hiyo kutokana na jinsi Roho anavyomjalia kutamka.

  Katika Marko 16:17 Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa moja ya ishara zitakazofuatana na waaminio ni Kusema kwa Lugha Mpya. Ishara zingine alizozitaja Yesu ni pamoja na kutoa pepo, kuweka mikono juu ya wagonjwa, kutokudhuriwa na vitu vya hatari kama sumu n.k. (And these signs will accompany those who believe; in my name they will drive out demons; they will speak in new tongues … (NIV)) Hivyo kulingana na maneno ya Yesu, waamwaminio watafuatana na ishara mbalimbali ikiwemo kusema kwa lugha mpya.

  Katika Biblia, ishara iliyotumika kuonyesha kuwa mtu amempokea Roho Mtakatifu ilikuwa ni kunena kwa lugha mpya kwa kadri Roho Mwenyewe anavyomjalia mtu huyo kutamka. Katika Matendo 10:45 -47 inasema …. “Wakashangaa watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu”…. Vilevile katika Matendo 19:6 huko Efeso watu walianza kunena kwa lugha na kutabiri baada ya Roho Mtakatifu kuja juu yao walipoombewa na Paulo.

  Katika Matendo 2:4 tunaona pia kuwa siku Roho Mtakatifu aliposhuka kwa mara ya kwanza, wanafunzi walianza kunena kwa lugha mpya na ndiyo ishara iliyoonekana hata kwa mataifa wakaamini. Paulo anaandika pia katika 1Korintho 14:22 kuwa lugha ni ishara.

  Pamoja na kunena kwa lugha kutumika kama ishara ya mtu kujazwa na Roho Mtakatifu, biblia inatufundisha faida nyingine za mtu kunena kwa lugha mpya ambazo ni kusema na Mungu (1Wakorinto 14:2) na pia anenaye hujijenga nafsi yake ndiyo maana biblia inasisitiza waamini kunena kwa lugha 1Kor. 14.4-5, 39.

  Kwa hiyo, kunena kwa lugha ni ishara ya kuwa mtu amempokea Roho Mtakatifu na ni njia ya mawasiliano kati ya mtu na Mungu. Aidha, kunena kwa lugha kunamjenga mtu na ni muhimu sana wakati wa maombi, ingawa wapo wengine huwa wanaimba nyimbo za kumwadhimisha Mungu kwa kunena kwa lugha.

  Katika Agano Jipya, hasa baada ya Yesu kuondoka, sijaona mahali ambapo mtu alijazwa na Roho Mtakatifu bila kuwepo kwa ishara inayoonyesha kuwa mtu huyo amejazwa na Roho, na ishara iliyotajwa na biblia ni kunena kwa lugha mpya.

  Katika Matendo 2 tunasoma kuwa siku ya Pentekoste watu wa mataifa mbalimbali waliwasikia Mitume kwa lugha zao na ndiyo maana mchangiaji mmoja amesema kuwa kila mtu anaponena kwa lugha, basi ni lazima watu wengine wasikie. Hata hivyo, katika 1Wakorintho 14:2 Biblia inasema kuwa “Yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; bali anena mambo ya siri katika roho yake”. Hapa tunaona kuwa si lazima kuwa kila mtu anaponena ni lazima wengine waelewe anachosema, inategemea na mapenzi ya Mungu kwa wakati huo. Katika 1 Wakorintho 13:1 Paulo anasema nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, hii inatuonyesha kuwa upo uwezekano wa mtu kusema kwa lugha za malaika pia. Vilevile, wakati Yesu alipokuwa msalabani alisema Eloi, Eloi lama sabakthani? na watu waliokuwepo pale wakadhani anamwita Eliya kwa kuwa hawakuelewa alichokuwa akikisema.

  Kama nilivyosema hapo juu, kunena kwa lugha kuna maanisha kusema lugha ambayo mtu hajawahi kujifunza. Inaweza ikawa lugha ya wanadamu, kwa maana kuwa inazungumzwa na kabila fulani hapa duniani au lugha ambayo haizungumzwi hapa duniani. Kwa mfano, kama tumekusanyika watu wa kabila moja mfano wote ni wasukuma, ili mtu akinena sote tusikie, basi ni lazima anene kisukuma. Sasa kama na anenaye ni msukuma, basi hatakuwa akinena kwa lugha, maana anazungumza lugha aliyojifunza na anayoifahamu vema. Binafsi nimepata shuhuda nyingi za watu walionena lugha za wanadamu, mfano mtu anazungumza kifaransa lakini hajawahi kujifunza na wala hajui kama alikuwa akinena kifaransa.

  Biblia inazungumza pia lugha kama karama. Katika 1Wakorintho 12: 9-11 na 1Korintho 12:27-29 biblia imesema lugha kama karama, lakini naomba tuzingatie kuwa biblia inasema aina za lugha na si kunena kwa lugha tu. Biblia ya kiingereza inatumia maneno “speaking in different kinds of tongues” na siyo speaking in tongues” tu kama ilivyoyumika kwenye Matendo 10:46. Naomba izingatiwe pia kuwa katika sehemu hii biblia imetaja karama zingine ikiwemo imani, kuponya, matendo ya miujiza, kupambanua roho na tafsiri za lugha. Katika Marko 16:17 tuliona Yesu akitaja ishara zitakazofuatana na waaminio ikiwemo kusema kwa lugh mpya na kuponya wagonjwa, hivyo ni muhimu tufahamu kuwa kila mwamini amepewa mamlaka ya kuweka mikono juu ya wagonjwa nao wakapona, lakini wapo waliopewa kitu cha ziada ambacho ni karama ya uponyaji. Vilevile, kila mwamini amepewa ishara ya kunena kwa lugha, akijazwa Roho Mtakatifu, lakini wapo waliopewa karama ya aina za lugha, hiki ni kitu cha ziada.

  Ninachokiona mimi hapa ni kuwa kuna kunena kwa lugha kama ishara ya mtu kumpokea Roho Mtakatifu na pia kama sehemu ya Mawasiliano ya Mtu na Mungu na ndiyo inayomjenga mtu aliyeokoka na kuna suala la lugha kama karama ambayo ni aina za lugha.

  Kwa hiyo, suala la lugha kama karama si lazima kila mtu aliyeokoka awe nayo kwani karama hutolewa na Roho Mtakatifu kama apendavyo Roho Mwenyewe na wala si kwa matakwa ya mtu. Kwa kuwa Mungu ndiye anayeamua nani apewe karama gani wanadamu hawawezi kusema lolote juu ya mtu asiyekuwa na karama fulani na wala mtu asijihukumu kwa kukosa karama fulani bali aiangalie ile aliyo nayo na kuifanyia kazi. Vilevile, hatuwezi kumlazimisha mtu kuitafuta karama fulani, bali Biblia inatutaka tutafute sana kuwa na karama za Rohoni, ila si karama fulani tunayoipenda sisi.
  Kwa upande mwingine, suala la kunena kwa lugha kama ishara ya kujaa Roho Mtakatifu na kama njia ya mawasiliano ya mtu na Mungu na kama njia ya kumjenga mtu aliyeokoka ni muhimu/lazima ili mkristo awe na nguvu ya Mungu.
  Yesu alisema kuwa mtapokea nguvu atakapowajia juu yenu Roho Mtakatifu (Matendo 1:8, tazama pia Luka 24:49), maneno haya yanatuonyesha kuwa mtu anapokea nguvu baada ya kumpokea Roho Mtakatifu, kwa maana nyingine, mtu akishaokoka anahitaji sana kumpokea Roho Mtakatifu ili aweze kuwa na nguvu za Mungu na hivyo kuishi maisha ya ushindi na kumpendeza Mungu na maisha ya utumishi pia.

  Tumeona kuwa Ishara ya Kumpokea Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha mpya, swali la msingi ni kuwa je mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu bila kunena kwa lugha? Kama jibu ni ndiyo, tumeona pia kuwa faida nyingine ni kuwa mtu anaponena kwa lugha anasema na Mungua na pia anaijenga nafsi yake, je yule asiyenena kwa lugha anasemaje na Mungu na anajijengaje nafsi yake? Kama kunena kwa lugha siyo muhimu kwa wote, kwa nini Mungu awape fursa ya kujijenga watu wachache na wengine asiwape fursa hiyo?

  Hivyo, ninalazimika kuhitimisha kuwa ili mtu aliyeokoka awe na nguvu ya kiroho (Mungu) ni lazima ampokee Roho Mtakatifu (ajazwe) na ishara ya kuwa mtu amejazwa ni kunena kwa lugha. Vilevile, kunena kwa lugha ni sehemu ya mtu kuwasiliana na Mungu wake na ni njia ya mtu kujijenga nafsi yake (mtu anapojijenga ndipo anapata nguvu za Mungu na kuwa imara katika Imani na wokovu), basi suala la kunena kwa lugha ni muhimu na la lazima kwa mtu aliyeokoka ili awe na nguvu za Mungu na aishi maisha ya wokovu kwa furaha na ushindi. Hili linathibitishwa na jinsi watangulizi wetu (Mitume) walivyosisitiza watu kujazwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha siku zote.

  Mungu awabariki.

 149. Ndugu,Matonya.
  Yesu akupe neema ya kumuelewa na kuelewa neno.’Roho wa Mungu’,sawa.Lakini huyo Mungu analo jina.naye anaitwa Yesu wa Nazareth.Ubarikiwe!.

 150. Mtu ukiokoka unapewa vyote kwa sehemu,ila kimoja wapo kile ambacho ni karama yako kitakuwa na nguvu zaidi.Hta wachezaji wa mpira si kwambaKaseja atashindwa kabisa kucheza namba za ndani,atacheza ,lakini akikaa golini anafiti zaidi. Hata kunena kwa lugha tunapaswa wote tuliookoka tunene,isipokuwa wapo ambao watakuwa zaidi ya wengine,kwa kuwa imempendeza Roho Mtakatifu hivyo.Paul alisema,anenae kwa lugha hujenga nafsi yake (1 Kr 14;4),Je kama Karama hii ni kwa baadhi,hawa wengine nafsi zao zitajengwaje ? Anenae kwa lugha hasemi na watu bali husema na Mungu,bali anena mambo ya siri ktk roho yake (1 Kor 14;2)Mtu asiponena kwa lugha ingawa ameokoka,mambo yake ya siri yatafikishwa kwa Mungu vipi ?(1Kor 14;15-Kunena kwa lugha,ni kuomba kwa roho,Je mtu asiponena kwa lugha,ingawa ameokoka,roho yake itaomba lini ?maana akili yake ina mipaka yakujua mambo lakini roho ndiyo inayoweza kuona mambo wa mbali zaidi.Mdo 2;4-Wote wakajazwa Roho takatifu,wakaanza kusema kwa lugha nyingine,(WOTE)ZINGATIA NENO WOTE (Mdo 10;44-Roho Mtakatifu akawashukia ‘WOTE’ waliolisikia lile neno!Mdo 2;39- Ahadi hii ni kwa wote waliookoka,na kwa watakaookoka (Mdo 2;33)Kipawa(AHADI) hiki kimemwagwa,kwa kuwa kimemwagwa hakina mwenyewe ila,mwenye utayari wakukipokea,(Tatizo la watu hawana utayari,ndio maana hawajazwi,(Mdo 1;8-usiponena kwa lugha,sahau kuwa shahidi wa Yesu,hutakuwa jasiri(Mdo 4;31),tofauti moja wapo kubwa ya waliookoka na wasiookoka,ni ujazo wa Roho Mtakatifu pia(Mdo 10;45-47Hata wamataifa walimwagiwa kipawa cha Roho mtakatifu ! sembuse waliookoka ? ndio maana Petro akaamuru wabatizwe kwa kuwa neno limeshapenya ,limewatakasa,kwa hiyo wakabatizwa,kwa sababu wamejazwa Roho Mtakatifu.(Mdo 18;24)Hata Apolo,alikuwa anajua maandiko,(habari za Yesu kwa usahihi na kujua ubatizo wa maji tu)lakini kwa kuwa alikuwa hajajazwa Roho Mtakatifu,ikabidi afundishwe na Prisila na Akila habari za ujazo wa Roho takatifu(maana hakuwa anafundisha habari za Roho Mtakatifu mahali alikokuwa anapita kuhubiri kwa kuwa Paul aliuliza watu waliokuwa wanahubiriwa na Apolo kama wameshasikia habari za Roho Mtakatifu.( Marko 16;17-)Na Ishara hizi zitafuatana na hao waaminio ‘kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya,watashika nyoka;hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa nk,kama nilivyosema mwanzo kwamba woga wa watu na kutokuamini ndivyo vinavyosababisha ishara hizi zisiwatokee, kama jinsi ambavyo watu wanakuwa wavivu/waoga kuweka mikono yao juu ya wagonjwa vivyo hivyo wanakuwa wavivu hata katika kutamani au kuwa na kiu yakujazwa Roho Mtakatifu,lakini si kweli kwamba kipawa hiki ni kwa baadhi ya makanisa au watu fulani tu la hasha,watu hawajazwi kwa sababu hawajaamini ipasavyo au kanisa kukosa utaratibu huu wakujazwa Roho Mtakatifu kwa wanakuwa hawana mafundisho sahihi ya UJAZO WA Roho Mtakatifu,,kujazwa Roho Mtakatifu ni kwa wote kwa sharti tu lakumpokea Yesu kikamilifu,USHAURI WANGU KWAKO KAMA KANISANI KWAKO HAKUNA UTARATIBU HUU WA WATU KUJAZWA ROHO KISHA KUNENA KWA LUGHA,NAKUSIHI KIMBIA MAANA UTAKOSA AHADI NYINGI TULIZOAHIDIWA NA MUNGU. kuweka wenye karama hupewa zaidi ya wengine,ndio maana wote tumepewa amri ya kuhubiri Injili(kuhutubu)ingawa Wainjilisti wenye karama yao wapo,hata kuimba ni karama,lakini wapo waliokirimiwa karama ya kuimba ingawa sote tunaweza kuimba kwa sehemu nk.1 Kor 14;5 Paul anasema ‘Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha’ 1Kor 14;

 151. Precious,biblia imeweka kila kitu kwa utaratibu wake,usije ukachanganya watu,ndiyo maana AGANO LA KALE Roho mtakatifu imeandikwa ‘Roho wa Mungu’ndio maana hata Agano jipya kuna neno ‘Mitume,Wachungaji ‘lakini Agano la kale hakuna neno ‘mitume wala Wachungaji nk’ na mifano mingi tunapaswa tufuate biblia ina maana yake ndio maana Mungu akaruhusu migawanyiko hiyo iwepo.

 152. Swali la mwanzoni kama nilivyolielwa mimi ni hili: Ni lazima kuzungumza kwa lugha?
  Pengine nisema (Speaking in tongues).
  Kwanza najishusha na kusema wale wote waliochangia swala hili wamechangia vema.
  Hapa nina maswali mafupi: Kuzungumza, kusema, koongea, kunena nk je maneno haya ya kiswahili yana maana gani? Pengine itakuwa vizuri sana kuchanganua maana ya maneno haya.
  “Speaking in tongues” ina maana ya kunena kwa lugha na wala si kuzungumza kwa lugha; maana kuzungumza ni kati ya watu kadhaa wazungumzapo pamoja; na kusema; mtu anaweza hata kusema mwenyewe au kujisemasha mwenyewe. Nimewahi kuwaona watu njiani wakijisemesha wenyewe, hata mimi wakati mwingine hijisemesha mwenyewe.!
  Kunena kwa lugha kibiblia (speaking in tongues) ni karama; tena kibilia ni karama kwa Wakristo itokayo kwa Mungu mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu wake. Na Karama hii si wote wapewao maana mwingine amepewa hii au ile(uponyaji, maombezi, ushauri nk) hili tunalisoma katika maandiko. Kama Kanisa au kundi la watu limepewa karama hii, basi linene kwa lugha na sisi wengine tupate mwingine aliyepewa karama ya kutafsiri ndimi hizo ili tupate kuelewa anenacho.
  Kwa ajili hiyo basi kweli si lazima watu woooooooooooooooooote wiliokolewa kunena kwa lugha ila kukubali na kumpokea YESU MASIHI kuwa BWANA katika maisha yao. Mimi nikiwa mmoja wao.
  Wapendwa nawaomba sana someni na pitieni yale aliyoaandika Mtume Paulo katika Waraka wake wa Kwanza kwa Wakorintho kuhusu asili na matumiza ya kunena kwa lugha (Speaking in tongues).
  Bwana atubariki

 153. Ndugu Matonya,labda hujapata kuelewa kuwa Yesu kwetu ni nani?
  Yesu alikuwepo tangu mwanzo.Yohana8:58-Alikuwepo hata kabla ya Ibrahimu.
  Yesu ndiye Mungu,muumba vitu vyote,Baba wa milele,Isaya9:6.
  Ila,alikuja duniani kwa njia ya Kristo(Mwana wa Adamu)ili,apate kutuokoa.
  Tatizo watu wengi wanadhani Yesu alizaliwa ndo maana,bado hawafunguliwi.kilichozaliwa,ni kristo(mwana wa adamu) ila,Yesu(Roho) alishuka siku ile Kristo alipomwendea Yohana mbatizaji kwa ajili ya kubatizwa.Na ndoo maana, Roho aliposhuka,yaani Yesu;kazi ikaanza kutendeka kisawasawa.Kwakuwa,bila Yesu(Nguvu),mwanadamu hawezi chochote.Watu wanadhani Yesu alikuwa mtoto tu wa Mariam na katika kuomba,utasikia wanatumia vyeo(Baba,Mwana,Roho).Mwishowe hawafunguliwi!.Hawafunguliwi sababu hawatumii mamlaka (Yesu)-jina lipitalo majina yote,vyeo vyote n.k.
  Si shangai sana.Maana,hata wanafunzi wake walipata kufunuliwa kuwa Yeye ndiye Mungu(Baba wa milele)baada ya kukaa naye muda murefu sana.Hawakujua kama wanatembea na Mungu(Baba).Inachanganya kweli kuona wanafunzi wanatembea na Yesu muda wote bila kumjua.Soma kilichotokea katika Yohana14:8-11,Yohana8:19,10:37.
  Tatizo lililopo leo ni kwamba,kushindwa kutambua Yesu ni nani,tunakosa nguvu(Mamlaka).
  Yesu hakutaka kujiweka wazi maana walikuwepo wanamwandama sana na ilibidi akamilishe mission yake.
  Ni muhimu sana tupate kujua Yesu ni nani? Ili,tujue tunachoamini na kuabudu,ni nini?!.
  Mbarikiwe wapendwa!.

 154. Ndugu Presious
  Nakupongeza sana na nimebarikiwa na mchango wako mzuri.
  Labda kwa kuongezea ni kwamba wale wote tunaojiita tumeokoka kwa maana tunaamini juu ya uPentecost ,
  Je ni kweli tunavyonena ndivyo ilivyoamriwa na kama sio basi tujihoji ni wap tumekosea maana Biblia inasema kwamba kunena ni karama na wanenapo watu lazima wawepo wa kutafsiri na si hivyo tu bali hata lugha wanenazo lazima ziwe za kueleweka kwa watu wa karibu au eneo husika mfano kama hapa Tanzania lazima tunaponena kwa lugha fulani lazima iwe ina tafsiri na makabila yetu hapa.-Hii nanukuu kutoka ktk kitabu cha Wakorntho 1Wakorintho9:11 na 1Wakorintho13:1

  Kama nionavyo mm bado sisi kama tuliozaliwa mara ya pili tunayo haja ya kujihoji na kutafakari kama kweli tunenapo twafwata kama neno lisemavyo au ni mapokeo ya kanisa la Mwanzo hasa kutokea lile la Marekani.

  Thanx!!!
  Be Blessed!!!

 155. Mpendwa katika Kristo,ahsante kwa swali zuri sana.Swali lako ndiyo changamoto tunayokabiliana nayo katika kipindi hiki.
  Kwanza ni vyema kutafakari mwanzo wa kunena kwa lugha.Ukisoma Mdo.2:5-13,siku Roho mtakatifu alipowashukia Wanafunzi wa Yesu,kulikuwa na watu kutoka mataifa mbalimbali waliokuwa wamekuja Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya ”Vibanda”, yaani Mavuno.
  Wakati Roho Mtakatifu amewashukia wanafunzi wa Yesu,aliwawezesha kusema lugha za watu wote waliokuwa wamekusanyika Yerusalemu.Ndo maana ukisoma fungu nililonukulu utaona wengi wanajiuliza na kuwashangaa wanafunzi maana walisikia wakisema kwa lugha zao,wakati si wenyeji wa mataifa yao.
  Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kunena kwa lugha.kadiri siku zilivyokwenda,ndivyo watu walivyoanza kunena kwa lugha zisizo na tafsiri. 1Kor.14:1-19 utaona Paulo anasemaje juu ya wale wanaotamani kunena kwa lugha.
  Kwa hiyo ndugu yangu katika Kristo, kunena kwa lugha,isiyo na tafsiri si Kipawa cha Roho Mtakatifu,bali wengine wanafanya mbwembwe tu,na kufikiri wanaongozwa na Roho Mtakatifu.
  Nakutakia BARAKA ZA MUNGU katika ufuasi wako.

 156. Precious naona kama hueleweki,mara useme Yesu alitawanya babeli wakati biblia haisemi kama Yesu alikuwepo kipindi hicho.

 157. Shalomu,

  Nasubiri kwa hamu mwanga kutoka kwa Precious kuhusu swala la lugha mpya.

  Mungu awabariki.

 158. Ndugu zangu,zipo karama tofauti,waefeso 4:1-15.Kunena kwa lugha ni ishara ya kubadilika kuwa kiumbe kipya,1Wakorintho9:11.Kunena kwa lugha,kulikuwepo siku ya Pentecost.Maana yake,siku 50 toka Yesu alipoenda mbinguni.Pentecost ilikuwepo tangu awali ila,ilikuja kutimia pale mitume walipopokea roho wa Yesu.
  Kuna Pentecost 2,
  (a); Ya kale=ilikuwa ni ya kuvuna mazao kwa Wayahudi
  (b); Ya sasa=ni ya kuvuna roho za watu waliopotea
  Aina 2 za Pentecost,
  1. Ya babeli,Mwanzo11:1.Na mnara wa babeli maana yake ni mungu mke(diana):kanisa la babeli,Mwanzo11:8-9,11:4 na Kumbukumbu la torati 72:5.
  Yesu alipotawanya babeli,watu walitawanyika wakinena kwa lugha.lugha ipi? Ufunuo16:19,Matendo ya mitume19:21.
  ***kanisa la sasa lenye mungu mke ndo freemansions,Ufunuo16:19.
  babeli maana yake,machafuko na kunena kwa lugha ya babeli,kulimaanisha kutawanya mataifa.Hivyo,kulisababisha uwepo wa machafuko,Mwanzo11:9.
  2. Ya Yerusalemu,na huku ni kunena kwa lugha ya kweli na ni kunena udhihirisho wa roho ya Yesu ambaye ndiye Mungu Mwenyezi,Yohana8:58.
  ***Watu wanatakiwa wanene lugha mpya,roho wa Yesu(Mungu) anapowashukia kama alivyowashukia mitume na kila mtu akanena kwa lugha yake tofauti.sio kuneneshwa!.
  1Wakorintho13:1.Hivyo,tujitahidi kufuata neno la Mungu kumtumikia Yesu ipasavyo.
  Aina mbili za lugha:
  -Ya wanadamu
  -Ya malaika
  ***waumini wengi wamejikuta wananena lugha ya kibabeli na sio lugha ya Mungu,Matendo ya Mitume2:6,Isaya28:11.
  ***Ukinena kwa lugha,lazima mtu wa pembeni yako asikie na kuelewa.Lugha ya Mungu hueleweka!.
  Pentecost ya Yerusalemu inamaanisha,kuvuna roho zilizopotea(ambazo hazijampokea Yesu),1Wakorintho12:4.Pia,kuna kunena ishara na kunena karama.Ni kweli kuwa kunena kwa lugha ni muhimu kwa mtu anayetaka kukomaa kiroho lakini,sio kwamba ni lazima au si kwamba mtu asiponena basi hana roho mtakatifu,hapana.zipo karama tofauti na kila mmoja wetu anayo ya kwake ya kipekee.
  Tukinena wote,nani atatafsiri?sote tukiwa manabii,nani atakuwepo kufundisha.zote ni karama na zote zina umuhimu wake.
  Kuna changamoto niliipokea toka kwa Nabii Mkombo.Alipomaliza kutufundisha kuhusu hili somo,alisisitiza,”muombeni Yesu apate kuwafungua macho na masikio ya rohoni.Ndo jambo la msingi kwa mtu anayetaka kumuona Bwana.Maana,mnavyosikia kuwa parapanda italia siku ya kurudi kwake Yesu,ni kwamba wale tu, wenye macho na masikio ya rohoni ndio watakaosikio hio sauti na kumuona Bwana Yesu akiwa amekuja kuwachukua.Na hao ndo watakaonyakuliwa!”
  Je,tuseme parapanda imelia muda huu.Ni wangapi watasikia na kumuona Yesu?
  Wapendwa,kuiona mbingu sio mchezo.tuweke sana bidii ya kumtafuta Yesu na
  kuishi kama apendavyo.

 159. kunena kwa lugha mpya ni lazima.hii ni kwa sababu ni ahadi ambayo tumepewa.mfano, wanafunzi wale walioambiwa na Yesu wasiondoke Yerusalemu mpaka waipokee ahadi ya Roho Mtakatifu ni hakika kuwa,kila aliyeipokea ile ahadi alinena kwa lugha mpya.

 160. kunena kwa lugha mpya ni miongoni mwa ishara ya wazi kwa mtu aliyejazwa na roho mtakatifu, hata hivyo tafsiri hiyo imezua maswali mengi sana kwa wachambuzi wa Biblia katika vyuo vingi duniani vinavyojulikana kama schools of thoughts! Mfano mmoja wapo ni pale ambapo Petro alinena kwa lugha tofauti na ile aliyozaliwa nayo na kuwafanya wale waliokuwa wakimsikiliza kila mtu kuelewa kwa lugha yake halisi mfano warumi walielewa kwa kirumi, wagiriki katika kigiriki nk, wakati muongeaji aliongea kwa lugha ya kwao huko kunaitwa kunena kwa lugha mpya.Paulo alinena waziwazi kwamba wakutanikapo mahali watu wakimwabudu mungu watu wasinene kwa lugha mpya kwa sababu wataonekana kama wendawazimu kwani wasikiaji watashindwa kuelewa vinginevyo awepo mfasiri yaani mtu anayeyaelewa maneno hayo akayatafsiri.Kwa hiyo kwa upande wangu sio lazima mtu aliyejazwa na Roho mtakatifu apewe uwezo huu, kuna karama nyingine nyingi mtu anaweza kuwa nazo.

 161. Hi Merere,Yesu atukuzwe.si lazima kila mtu kunena kwa lugha mpya.vumilia,kesho ntakupa mwanga zaidi kuhusu hili swala la lugha mpya!.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s