Ukubwa wa Makanisa

Je! Ni kipi kilicho bora: Kuwepo kwa Makanisa MENGI madogo madogo, mtaa kwa mtaa AU Makanisa makubwa makubwa lakini MACHACHE?

NB: Kanisa kwa maana ya Makusanyiko ya Wakristo!

Advertisements

17 thoughts on “Ukubwa wa Makanisa

 1. Ukwel ni kwamba ukubwa wa kanisa au wingi wa waumin ktk kanisa moja hauleti migogoro. Migogoro inaletwa na uongozi uliopo. Tujifunze kwa wenzetu wakorea ibada moja inabeba watu laki saba.

 2. Ni kweli nami nimebarikiwa na michango ya ndg Millinga na Orbi, nimekuwa najiuliza sana gharama kubwa ktk kujenga makanisa makubwa ili kubeba wauimini wengi wengine wanatoka mbali sana kwenda kuabudu kwa gharama kubwa. Hii hela yote si ingepeleka injili kwingine kusikofikika? Ile dhana kwa yule mwanamke msamaria kwamba saa inakuja ambapo hatutakuwa na haja ya kuenda mlima huu au ule kuabudu naona imeachwa badala yake tuna mahekalu yetu… tufanyeje? maana kwakweli injili hainezwi ipasavyo tunaabudu, tunaomba, tunanena kwa lugha, tunatoa matolea basi, miaka nenda miaka rudi hakuna kuhubiria wengine? Hata ndugu waliojitoa kwenda kuhubiri sehemu ambazo Ukristo unapingwa hawapewi msaada wowote…nimekaa na ninaenda Unguja na Pemba mara kwa mara kule watu wanahudumu ktk mazingira magumu sana ni kweli wametoa maisha yao kwa Injili Mungu awabariki…. kwakweli inaogopesha sana tutatoa hesabu siku ya mwisho. Tuombee hawa viongozi wetu watoke ktk upofu huu na ikibidi tusimame wenyewe ingawa kama alivyosema John Paul ni gharama na haitakuwa na matunda. Hebu tumwombe Mungu kanisa liamke! mbarikiwe sana

 3. Ndugu Milinga,

  Kweli umenigusa……….nguvu ya kanisa haiko katika maelfu na maelfu kukutanika na kujazana mahali pamoja….haipo hiyo
  ndani ya Biblia……nguvu ya Kanisa iko katika kutawanyika na kusambaa……kutawanyika na kusambaa ilikuwakifikia wengine…….nadhani somo la Kitabu cha Matendo ya Mitume limeshindwa kueleweka kwa wengi……Imani iliyoanza Yerusalemu kwa muda wa miaka michache ilitapakaa na kufika Rumi na kuiteka Dola ya Rumi……Wapenda naomba tuangalie zile ramani nyuma ya Biblia zetu…….zina maana zile..,…..na Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume anaonyesha Paulo alikuwa anataka Kwenda Spain (Hispania) na Kwenda huko atapita Rumi………!

  Kwa kifupi Mchungaji/Mtume/Nabii anapojitengenezea himaya anajitengenezea kuanguka kwake………..Kama mchungaji /Nabii/Mtume akitaka kuwafikia wengi ni yeye kuanzisha makundi madogo madogo ambayo nayo yatazaa makundi mengine na kuendeleza kazi ya Mungu…..

  Somo gumu kwa wengi kulitambua wingi wa watu si lazima ya hapo ni mahali pa Rohoni……..Si lazima kwamba Mungu yuko hapo…….wingi wa watu unaurahisi sana kujenga tumaini kwa anayelivuta kundi kuja Kwake……..

  Yesu angeliweza kuchagua kundi kubwa….bali alichagua watu kumi na mbili tu…….Roho Mtakatifu alishuka kwa watu mia na Ishirini tu……! Hebu angalia hao watu mia na Ishirini wakijaa Roho Mtakatifu walivyobadili dunia…….hebu angalieni Ramani tena……Toka Yerusalemu…..hadi Rumi………!

  Hebu jiulize leo maelfu na maelfu wanaojazana kila jumapili kwenye ministry mbali mbali Dar es salaam tu …..Je wanajazwa Roho gani….? Ni kweli wanajazwa Roho Mtakatifu yule yule aliyewajaza wale watu mia na Ishirini…..? Roho Mtakatifu wa Kitabu cha Matendo ya Mitume alitawanya waumini…alifanya waende na kuneza Injili………Je huyo Roho sasa amebadilika na kuanza kuwakusanya tena pamoja…..na kulundamana pamoja chini ya miguu ya Mitume na Manabii…. Kuna unabii gani ho unatolewa kila Jumapili…….kila katika ibada za katikati ya wiki? Ni kweli Mitume na Manabii wa Leo wamempokea Roho Mtakatifu wa Kitabu cha Matendo ya Mitume…..? Kwa msomaji wa Biblia anajua jibu ni nini……..

  Mungu na atubariki…….

 4. KANISA LA YESU KRISTO LILIKUWA LA WATU KUMI NA MBILI TU

  Hakuna atakayebisha kwamba Yesu alikuwa na waumini wachache sana enzi za uhai wake.

  Alipoanzisha kanisa lake hapa duniani alianza na wafuasi 12 ambao baadaye aliwatuma kuanzisha huduma za kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wake.

  Inashangaza leo watu wanajona waona ni Manabii na Mitume kumzidi Yesu. Wanadhani kuwa kama huna waumini maelfu na maelfu wewe siyo Mhubiri wala Mchungaji wa ukweli.

  Hata wakristo wengi wamedanganyika kwa kudhani kanisa lenye mamia na maelfu ya watu ndilo liko safi na Mungu yuko nao. Huku ni kupotea njia.

  Kanisa la kwanza lilipotaka kujikusanya pamoja Mungu aliruhusu mapigo toka kwa Sauli na Wayahudi likatawanyika lote. Yakabikia makundi madogo yaliyokuwa yanakutanikia majumbani mwa watu. Hiki ndicho kitayakumba makanisa makubwa sana mijini. Itafika siku yatatawanyika tu. Mungu atatumia njia mbalimbali hadi makanisa hayo yatawanyike kwa nguvu kama siyo wao kuanza kujitawanya kwa kuanzisha matawi madogo madogo.

  Huwa nayashangaa makanisa makubwa kama yaliyoko Dar mfano; FGBF, EFATHA, LIVING WATER CENTRE, BCIC, AGAPE CHURCH, MZEE WA UPAKO, nk. Mimi nawashauri tu waavunje makanisa yao katika matawi na wahakikishe mji mzima wa Dar umejaa makanisa hayo katika makundi ya watu 30 kila tawi. Kundi la watu 30 wapewe kiongozi wao na mahali pa kukutania hata kama ni sebuleni kwa mpendwa sawa tu.

  Hayo majengo makubwa baadaye yatauzwa tu au yatumike kuendeshea mikutano ya Injili kila baada ya miezi 3 siyo lazima iwe kila Jumapili.

  Mimi nawahakikishia kabisa kwamba Askofu au Mchungaji mwenye waumini zaidi 30 (Ingawa hata hii idadi ni kubwa ukilinganisha na ile ya Yesu ya watu 12 tu) utaona kwamba mafanikio yoyote wanayojaribu kuanzisha hufa mapema.

  Hebu watu wajaribu kujifunza kwa askofu wa FGBF yanayotokea kwake hadi wachungaji wenzake wanadiriki kumfungulia mashitaka mahakamani. Au chukua mfano wa huduma ya Efatha ya Mzee Mtume na Nabii Josephat Mwingira. Kashifa kibao kuelekezwa kwake za nini jamani. Nyingi hutokea ndani ya waumini aliowahi kuwa mchungaji wao. Wengi wanaojitoa humo ndiyo wanaosambaza taarifa mbovu ziwe na ukweli au zisiwe na ukweli.

  Kanisa dogo ndilo Yesu alitaka. Yesu alimaanisha kwamba ukiwa na kundi dogo utaweza kulifundisha na kulifanya likuige wewe imani, falsafa na itikadi badala ya kuwa na watazamaji tu wanaofika kila siku za Ibada kutazama mechi ya kutenda miujiza ya uponyaji nk.

 5. Ndugu yangu Sam,

  Labda tuangalia Mada upya….. nadhani ukisoma imesema pale chini “Makusanyiko ya Wakristo” na hiyo ndio maana iliyoko ndani ya Biblia….. yaani makusanyiko ya Waumini……..na kwa mada hii maana yake Makusanyiko makubwa ya waumini……..au makusanyiko madogo madogo………! Labda mada iwe na maana nyingine…..

 6. Ndugu wachangia mada!!

  Mimi naomba niwaulize kabla ya kuchangia mada hii. Je kanisa ni nini?

  Mbarikiwe.

 7. Wapendwa,

  Kama tukiangalia tamko la kwanza la Yesu kuhusu kusanyiko lake ni kutawanyika na kuenea…”Lakini mtapokea Nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalem na katika Uyahudi wote na Samaria hadi mwisho wa nchi” (Matendo 1:18) Kwa mtazamo huu basi kama Roho Mtakatifu tutamwachia afanye kazi juu yetu hatujazana mahali pamoja…bali tutawanyika….nguvu ya Kanisa iko katika kutawanyika na kuenea ili kuwafikia wengi na ujumbe wa Yesu…!

  Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonyesha wazi Kanisa lilikuwa na kuongezeka…toka 3000 hadi 5000 Lakini Mungu aliruhusu mateso kutoka nje kulitawanya lile kundi kutoka hapo Yerusalemu…..na kuenea hadi kwa mataifa….na hata baadaye kitovu kikubwa kikawa Antiokia…! Angalia Matendo 8:1-2 …”Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa Yerusalemu wote WAKATAWANYIKA katika nchi ya Uyahudi na Samaria isipokua hao mitume….” Hivyo ni Mungu mwenyewe aliruhusu adha na mateso kutoka nje kuligawanya Kanisa….! na maandiko yanasema “Philipo akatelemka akaingia mji wa Samaria akawahubiri Kristo (8:1) Kwa lugha nyingine kama adha na dhiki zisingalitokea hata Karama ya kuhubiri ya Philipo isingelichuliwa na Injili isingelifika Samaria…!

  Tukumbuke kwamba wingi wa watu mahali pamoja hauna uhusiano na UWEPO WA MUNGU…..Yesu anasema wawili watatu wakutanapo kwa Jina langu…..na sehemu nyingine anasema…”Msiogope enyi kundi dogo….” Wingi na uchache hauonyeshi Ukiroho wa Kanisa……Kwa msingi wa Biblia na ukiangalia Kitabu cha Matendo ya Mitume… waumini wanavyokuwa wengi basi ndio wanakuwa na uwezo wa kutawanyika kuwafikia wengi….! Hebu niambie kuna mantiki gani muumini kutoka Mbagala Rangi tatu kwenda Mwenge kuabudu…? Kama kuna uwezekano wa na Nabii au Mtume kuanzisha kazi nyingine Mbagala ili kuitawanya kwa kuitoa Mwenge kuekekea Mbagala au mbele zaidi…! A.unaweza kusema hivyo hivyo kwa Huduma nyingi pia…..Kutoka Boko na kwenda kuabudu Temeke….! Huduma ile ile inaweza kabisa kadri inavyokua na kupanuka kuanzisha huduma nyingine….huo ndio mfumo wa Agano jipya……Kazi ya Mungu haijengwi kumzunguka au katika muhimili wa Nabii/Mtume/Mchungaji/ au Mtu yoyote yule…bali Roho Mtakatifu tu…!

  Hatuwezi kuwa mashahidi wa Mungu kwa kujazana mahali pamoja….! Na mtume na nabii hata awe na uwezo namna gani hawezi kabisa kugusa mahitaji ya kila muumini kundi linapokuwa kubwa…..Angalia kanisa la Kwanza…kundi lilipopanuka na kuongezeka tu malalamiko yalitokea kuwa kuna upendeleo wa kuhudumia wajane…! (6:1) Ukubwa na wingi wa watu unafanya hata matatizo madogo kuwa makubwa…..Watu wa Mungu wanaanza kushugulikia zaidi utawala kuliko kuhudumu injili…….! Hata Musa Agano la kale ilimshinda…! Hivyo kwa mtazamo wangu sioni kabisa uthabiti “effectiveness” iko katika kundi kubwa la waumini kujazana mahali pamoja…..bali katika kutawanyika…kunafanya Chumvi na Nuru izidi kuenea…….na kanisa linazidi kuwa linaoneka “visible” kila mahali……na pia kufanya vipawa na karama nyingi za waumini kuzidi kufichuka na kuonekana……

  Leo nitakomea hapa……nitaendelea nikipata nafasi kuonyesha ukaribu “Fellowship” wa

  makundi madogo madogo ulivyokuwa na nguvu katika Kanisa la Matendo ya Mitume

 8. Labda na mimi niandike machache kuchangia mada hii.Toka kuokoka kwangu nimekua mshiriki wa makanisa madogo na makubwa ndani ya nchi yetu na nje ya Tanzania, nimeziona faida na hasara zake, lakini ukiniambia nichague ni wapi ningelipendea kuwa mshiriki, basi mtazamo wangu utakuwa ni makanisa madogo. Nimeokoka katika fellowship ndogo za chuoni na baada ya hapo kuwa muumini kwenye makanisa madogo madogo ambayo kila muumini wa kanisa tulikuwa tunafahamiana…Ule ukaribu “fellowship” wa kusaidiana…kuombeana….kutiana moyo…..kuonyana ulikuwa ni sehemu ya kundi, kitu ambacho tunakiona wazi katika AGANO JIPYA……na ni kweli Mchungaji alikuwa anafahamu Kondoo zake…..na hata kama kulikuwa na mbwa mwitu na magugu ilikuwa ni rahisi kuyatambua na hata kuchukuliana nayo…na kusaidia ili waijue kweli. Na ilikuwa ni rahisi mno kumsaidia muumini mmoja katika kuukulia wokovu

  Makanisa makubwa licha tu kwamba yanapoteza ukaribu wa waumini “fellowship” pia yanakuwa na waumini wengi ambao ni watazamaji…au yanazaa ugonjwa tunaouita “Spectator Syndrome” Wengi ndani ya kanisa kwa kuwa mbali na Mchungaji na wazee wa kanisa huishia kuwa watazamaji…na mbaya zaidi wengine kuwa washabiki wa kundi…..Mchungaji/Mtume/Nabii.Ni kweli kuna baadhi hujaribu kuziba pengo hili kwa kuwa na “Cell group” lakini mara nyingi nyingi zinashindwa kufikia waumini wote, hivyo ile nafasi ya ukaribu wa Muumini kwa mchungaji….muumini kwa muumini inapotea….na kanisa linashikamanishwa na mtu mmoja tu…Kiongozi….Utaratibu huu haupo katika Agano Jipya.Kwa kifupi kanisa kubwa linapoteza ile picha ya Kanisa katika Agano Jipya.

  Tatizo jingine kubwa unaloliona katika makanisa makubwa ni ile gharama inayotumika katika vitu ambayo kwa hakika si vya msingi- Majengo, sisemi kwamba tusiwe na mahali pazuri pa kuabudia, la hasha, lakini majengo mazuri hayana uhusiano wowote na kumjua Mungu au kutembea na Mungu…! Paulo alisema…”Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa Mbingu na Nchi hakai katika Hekalu zilizojengwa kwa mikono” Matendo 17:24-25.Nia aibu kwa kanisa kutumia Gharama kubwa katika kutunza jengo…yaani kulipa bili za umeme….maji…ulinzi… magari mengi kwa mtumishi mmoja nk kuliko kuwaleta watu kwa Kristo…au kuonyesha upendo wa Kristo kwa kutunza yatima na maskini…! Kama unafualizia habari hivi majuzi Marekani kanisa kubwa na mashuhuri linajulikana kama “Crystal Cathedral” la Muhubiri Robert Schuller limeuzwa kwa kanisa Katoliki kwa gharama ya USD 57.7 ili kulipia madeni ya kanisa…na kanisa kutafuta jengo dogo…! Kwa wale ambao Mungu amewapa kibali cha kufika Marekani na kuona uzuri wa majengo ya kanisa…lakini ndani ni matupu ataona wazi uzuri na ukubwa wa jengo hauna uhusiano wowote na hali ya Kiroho ya Kanisa.

  Na baadhi ya wachungaji ambao wamenivutia hapa Marekani ni makanisa yao yanapofikia tu watu kati ya 3000-5000 huyavunja ukubwa huo kwa kufungua makanisa mengine madogo madogo na kuhamishia waumini wao katika kanisa jipya sehemu wanazoishi ili kuanza tena upya kuwafikia wengine…..wanaamini ukubwa wa kanisa si kujazana mahali pamoja….bali kutawanyika…Mungu alifanya hivyo kwa kanisa la Kwanza walipokuwa wamejazana mahali pamoja Jerusalem! Wachungaji wanaofuata mfumo huu huamini kwamba watu wakiwa wengi kwanza kuwalisha kiroho ni kazi, na pia kama kweli wamekuwa kiroho ni lazima waondoke na kuanzisha kazi….lazima katika wingu huo kutakuwa na wachungaji wapya……wazee wa kanisa wapya….na lazima maono mapya yatakuwa yanazaliwa na Roho mtakatifu……!

  Labda nikipata nafasi nitatea zaidi msimamo wa makanisa madogo kwa kutumia Agano Jipya…..na kuweka wazi hasara au upungufu wa makanisa makubwa.Mbarikiwe.

 9. WALIPO WAWILI AU WATU MIMI NIPO KATI YAO, ASEMA BWANA.

  Ukweli unaotaka kutetewa na Bwa. John Paul umejikita katika mafanikio ya kimwili au kifedha zaidi kuliko Bwana Yesu alivyokusudia.

  Kanisa kubwa lina matatizo mengi zaidi kuliko kanisa dogo la mahali pamoja. Mr. John Paul na wengine wenye mtazamo huo wameacha msingi alioutaka Yesu wa kuwa na kanisa kila mahali yaani mtaa kwa mtaa.

  Ukitazama hata wayahudi walikuwa na masinagogi karibu kila mtaa. Hili wameliiga Waislam kwani liliasisiwa na dini ya Kiyahudi na hata wakati Yesu Yupo hapa duniani alikuwa akienda katika masinagogi yao kila juma. Utaona kwamba pamoja na kwamba kulikuwepo Hekalu kuu pale Jijini Yerusalem, bado kulikuwepo na masinagogi ambayo yalikusanya watu wachache kila iitwapo sabato.

  Wakati wa Mitume hasa wakati wa Mtume Paulo utaona kwamba kulikuwa na mikusanyiko ya makanisa ya nyumbani. Kila mtaa ungekuta kuna kanisa la nyumbani kwa mpendwa fulani mfano Onesforo (2tim 4. 19),kwa akina Prisila na Akila, tazama Rum 16:5 inasema hivi, “…. lisalimuni kanisa linalokutana nyumbani mwao…”

  Nyakati zile michango mingi iliyokuwa ikitolewa na wapendwa wa nyakati za akina Paulo Mtume ilikuwa kwa ajili ya watu masikini, wajane, yatima na wakimbizi zaidi si kama ilivyo leo michango na sadaka nyingi huelekezwa katika ujenzi wa mahekalu makuuuubwa. Sielewi watu wa siku hizi wanatoa wapi miongozo ya kuendesha na kujenga mahekali makubwa jinsi hii.

  Hebu mtazame Bwana YESU anasema watakapokuwepo watu wawili au watatu atakuwa kati yao. Kwa nini bado watu wanakuwa na fikra potofu kwamba hekalu kuubwa lenye kukusanya watu wengi ndiko kuwa na faida. Mr. Paulo John anasema kwamba , Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu”. Lakini umoja wa Roho na kanisa anaoutaka Yesu auone kwa Kanisa lake siyo kukutanika pamoja katika umati mkuuubwa sana mahekaluni. Ni umoja wa Imani, mafundisho, na maadili yanayotokana na kuwa na Biblia moja ingawa siku hizi kutokana na kazi ya kusimamia(kuchunga) makanisa imegeuzwa kuwa kama miradi na biashara zenye manufaa au faida.

  Wachungaji wenye makanisa yenye mikusanyiko midogo siku hizi wanaonekana kama hawana Mungu wala upako wa kinabii na kimitume. Ujinga gani huu!!!!

  Mimi nabakia kuamini kwamba Mungu hapendi tujazane pamoja kila juma au kila mara. Kwa mfano kuna makanisa mengi sana Dar es salaam ambayo yameamua kufuata utaratibu wa kuwa na kanisa moja kuuubwa mahali pamoja. Na kweli wanapotoa sadaka siku za Jumapili utakuta kiasi cha mamilioni ya sadaka hupatikana kwa makanisa hayo.

  Kwa mtazamo wangu kanisa ili liwe na ufanisi wa kulea waumini ni bora liwe na waumini wasiozidi 30 na wasipungue 3. Kanisa lenye mkusanyiko wa watu zaidi ya 30 kusema ukweli lina matatizo mengi ya kiuchungaji kuliko faida.

  Kanisa lenye watu wengi (kwa mfano 150) ni sawa na darasa la shule ya msingi lenye wanafunzi 150 lakini lote linashindwa kufaulu mitihani ya majaribio kutokana na mwalimu wao kushindwa kusahihisha majaribio ya kila wiki au kuamua kutokuwapa majaribio ya kila wiki kwani akianza kuwaza ugumu wa kusahihisha kazi zao anaona ni vyema asitoe mazoezi. Jaribu kuwafuatilia wachungaji wenye waumini zaidi ya 30 utaona kwamba wanaweza kumaliza miezi kama siyo miaka bila kwenda kuwatembelea waumini wao majumbani kwao. Hivi ukiwa na waumini wapatao 5000 katika Jiji la Dar unaweza kuwatembelea kweli kuwatia moyo wakati wa furaha au huzuni? Haiwezekani kabisaa. Utaona kwamba makanisa mengi yenye waumini zaidi ya 500 mfano kanisa la FGBF la DAR, au kanisa la SCOAN la Abuja Nigeria lenye watu zaidi ya 10,000 katika mji mmoja utaona kwamba wanalazimika kuwa na makanisa madogo (wanayaita Home Cells Churches) ambayo hukutania katika sebule za wapendwa kila wiki (ingawa siyo siku za Jumapili) ili waweze kujuana zaidi na kusaidiana katika nyakati za Harusi, misiba, sherehe,nk.

  Yesu alipopaa aliwaambia wanafunzi wake waende ulimwenguni kote kuwafanya watu kuwa wanafunzi wake. Hakusema waende kuwafanya watu kukusanyika pamoja katika majengo makubwa sana kama tuyaonayo leo. Aidha, huwezi kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Kristo kwa kuwakusanya kwenye mikusanyiko mikuuubwa kama ule ambao Yesu aliuutumia kufanya muujiza wa kubadilisha samaki mmoja kuwa masamaki maelfu na mkate mmoja kuwa maelf ya mikate ili kulisha maelfu ya watu waliokuwa na njaa jangwani.

  Makanisa makuuubwa kwa idadi ya watu (kama hawana utaratibu wa makanisa madogo madogo mtaa kwa mtaa yanayokutana kila wiki) yafuatayo utegemee kuyakuta kanisa hilo:

  1. Wapendwa kutokujuana na mchungaji wao uso kwa uso (Kumbuka mchungaji wa kweli huwajua kondoo wake kwa majina yao).

  2. Mchungaji wa kanisa hilo (lenye watu zaidi ya 30) hataweza kuwepo kuwafariji waumini wake wawapo kwenye wakati wa furaha mfano Harusi, sherehe za kawaida au wawapo katika majonzi kama ya misiba, nk. Kumbuka Yesu alihudhuria harusi za wapendwa wakati akiwapo duniani. Wewe ni nani usiyefanya hivyo.

  3. Kanisa linakuwa kichaka cha watu watendao maovu. Kutokana na wingi wa watu kanisani, siyo rahisi mchungaji au waumini wenyewe kujua maovu yatendwayo na waumini wake mtaani au majumbani. Hawezi kujua hata kazi wafanyazo ili kupata vipato vyao. Makanisa mengi leo hii ni vichaka vya watu watendao maovu kwa sababu ya wingi wa watu kiasi kwamba waumini wenyewe hawajuani, hawatembeleani, wala mchungaji hawajui kwa sura na majina yao. HII NI HATARI SANA KWA KANISA.

  4. Waumini wengi wanakosa kukua kiroho, kiimani na kimaandiko kutokana na kwamba waumini hao hawapati muda wa kujifunza maandiko kama walivyofanya wakristo wa Beroya. Matokeo yake watu wanakuwa wafuasi wa kiongozi fulani tu na wala siyo wanafunzi wa Kristo YESU.

  5. Makanisa makuubwa yenye waumini weeeengi, huwa hayawezi kujirudi hata kama yanatenda ndivyo sivyo. Kwa mfano, kanisa kama Katholic lenye watu wengi sana Tanzania haliwezi kukubali kukosolewa na watu wanaojiita walokole kwa sababu tu kwanza walokole hao ni wachache sana Tanzania. Au mchungaji huyo anayewakosoa ana elimu ya Form IV au Diploma ya Theologia tu wakati wao viongozi wamesoma hadi shahada za Uzamivu (PhD) na wana watu wengi na makanisa yao ni makubwa na yanajaa tele watu. Kanisa Katholiki hapa ndipo lilipofanya makosa. Makanisa yao yana watu weeengi lakini wasiolielewa Neno au Biblia kiasi kwamba hata Mwislam anaweza kuwalaghai kirahisi kabisa katika maswala madogo tu.

  6. Makanisa makubwa yana tabia ya kushindana kwa hali za kifedha na kimavazi, nk. Nyakati za Mtume Paulo ilitokea kanisa la Korintho lilifikia mahali linashindana kwa mapishi ya chakula cha meza ya Bwana hadi Paulo akawaonya akitaka wakati wa meza ya Bwana kusiwepo mashindano ya nani kapika vizuri au ni nani ana chakula kingi, nk na kwamba wangojane wakati wa kula meza ya Bwana. Enzi zile watu walikula kabisa na kushiba wakati wa chakula cha Meza ya Bwana siyo kama leo watu wanakula slice ya biskuti na pafu moja la zabibu (dodoma wine).

  7. Kanisa lenye watu wengi mchungaji wake hataweza kutoa hesabu ya kila muumini anayesali kwake. Utatoaje hesabu ya kondoo usiowajua kwa sura na kwa jina. Kusema ukweli makanisa makubwa hayafai.

  8. Mchungaji mwenye kuchunga kondoo zaidi ya 30 hawezi kujua kondoo wenye kifafa cha kiroho, wenye utapiamulo wa maandiko, wenye UKIRO, nk.

  9. Mchungaji mwenye wanafunzi zaidi ya 30 hawezi kuwafanya kondoo wake kuwa walimu wa wengine kwani hawezi kuwafundisha kwa upana maandiko kutokana na uhaba wa muda.

  10. Kondoo mmoja akipotea inakuwa vigumu kuwa na uchungu naye kwani unazidi kuona makondoo mengi yamekuzunguka tofauti na mwenye kondoo wachache anakuwa na uchungu na kondoo mmoja kutoonekana katika zizi. Lakini makanisa makubwa sana, hata kondoo asipoonekana zaidi ya miezi 3 mchungaji hata hajui.

  Mwisho, natamani kila mtaa ungekuwa na kanisa. Hata kama lina watu 3 tu. Yesu alisema hilo ni kanisa. Kanisa siyo lazima liwe jengo hata sebule ya nyumbani yaweza kuwa kanisa.

  Kama kila mtaa ungekuwa na kanisa (hasa mijini) nadhani uvivu wa kuabudu na kukusanyika pamoja haungekuwepo miongoni mwa wanafunzi. Jaribu kujifunza kwa madarasa ya Shule ya Msingi au Sekondari yenye wanafunzi wengi darasani, utakuta mtoto yuko anajiandikia madudu tu ndani ya daftari lake na wala mwalimu wake hana habari. Hata mwanafunzi asipohudhuria vipindi darasani, mwalimu hana muda wa kumfuatilia kwani hata alionao darasani hajafanikiwa kuwatosheleza mahitaji yao. Na mwanafunzi anayetoka katika darasa lenye wanafunzi wengi haoni kosa kutohudhuria vipindi kwani hata mwalimu wake hamfuatilii. Ndivyo na makanisa yenye watu wengi yalivyo.

  Mbona misikiti iko kila kona mijini? Mbona baa za pombe na Guest Houses ziko kila kona za miji yetu? Mbona maduka ya biashara yapo kila kona za mitaa yetu? Mbona shule za Sekondari ziko kila kata? Mbona Zahanati tunataka ziwe kila kijiji?

  Inakuwaje makanisa tuone taabu kuomba Mungu awafunulie watu ili makanisa yawepo kila kona ya mitaa yetu? Kosa liko wapi kwa mtaa kama ule wa Sinza Dar, au Mtaa wa Mabatini Mwanza au Mianzini Arusha kuwa na makanisa kila kona ya mtaa huo?.

  Hivi kwa nini tunaona kinyaa kuabudu katika makanisa yenye watu wachache (watu chini ya 10 kwa mfano). Mbona misikiti unaweza kukuta kuna watu wachache tu hata kama wako 5 utakuta wanaswali. Kwa nini kwa makanisa inakuwa NOMA? Mbona mabenki ya biashara yamejaa kila mji. Mbona NGOs ziko kila mahali. Mbona SACCOS zimejaa kila mahali? Kwa nini isiwe makanisa.

  Nadhani John Paulo na wengine wamenielewa vizuri.John Paulo anzisha kanisa hapo nyumbani kwako hata kama utasali na watoto wako na familia mbili au moja za jirani yako, hata kama kanisa hilo litakuwa na watu 3 wewe wape Neno na abuduni na kusifu kwa bidii kwani Yesu yuko nanyi.

  Nategemea kusikia makanisa mengi yakisajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ili kuendesha ibada zao kwa kuziunganisha familia 2 au 3 na Yesu atakuwa kati yao. Ameeeeeeeni.

 10. Kutokana na ile dhana ya UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU kuna mambo ambayo Ni rahisi kufanyika katika kanisa Kubwa kuliko kanisa dogo. Biblia pia inataja jambo hili kwa mfano wa Kamba Yenye Nyuzi 3, (three corded rope) kwamba haikatiki upesi kuliko kamba yenye uzi mmoja tu.

  Kutokana na uzoefu wa kuhudhuria katika ibada za makanisa makubwa na madogo, kuna jambo la uwingi wa watu, jambo ambalo huleta “joto”, mtu hujisikia kuwa kumbe hayupo peke yake, huwa hajisikii mnyonge. Pale mlimani, Gehazi alipofunguliwa macho ya rohoni aliona JESHI KUBWA lenye Farasi wa Moto, “Jeshi Kubwa”. Hii inaonyesha kuna nguvu fulani katika UWINGI.

  Katika kanisa kubwa siyo rahisi kupatikana kwa nafasi ya watu kuchunguzana maisha binafsi, ambayo siyo ya DHAMBI. Miaka fulani huko nyuma Nikiwa mwanachama katika kanisa fulani, lenye watu wachache, yaani kanisa dogo, tulianzisha utaratibu wa kila Mwisho wa mwezi watu watembeleane majumbani, ili kuongeza urafiki na kufahamiana. Lakini cha kushangaza ikawa mtu akifika kwa mwingine na kukuta mambo hayako kama anavyomuona mtu huko nje, mfano akikuta mtu anakalia “stuli” badala ya kochi, akitoka hapo anaanza kutagaza kuwa “kumbe fulani hana kitu, yaani hata kochi kwake hakuna!”. Kutokana na hali hiyo ilibidi Utaratibu huo ufutiliwe mbali, kwa kuwa kuna watu waliamua kuwa upande wa shetani, lakini kwa sababu ya kitendo kilichosukumwa na “udogo wa kanisa”.

  Kwenye uchache wa watu ni vigumu kufanya mambo yanayohitaji kukusanya pesa kwanza ndipo yafanyike. Hata pakifanyika mchango utakuta ni pesa kidogo sana inayopatikana kuliko katika kanisa kubwa. Maana kwenye WENGI PANA MENGI. Hiyo inaweza kumaanisha pia kuwa penye WENGI PANA PESA NYINGI!

  Udogo wa makanisa, maana yake ni kuwa na wachungaji wengi, wenye tabia tofauti tofauti. Hilo hupelekea wakristo wenye tabia tofauti tofauti kutokana na wachungaji wao. Hali hiyo hupelekea utengano katika ya wakristo kwa kuonana kuwa wale walio katika kanisa fulani ni bora kuliko wenzao. Hali hii inaweza ikamezwa na kuwepo kwa makanisa makubwa, kanisa linaloweza kukutanisha watu wa sehemu kubwa kwenye kituo kimoja.

  Nimeandika kwa haraka haraka lakini hayo ni mawazo kuhusu FAIDA ya kuwa na Kanisa Kubwa. Yaani bora kuwepo na makanisa machache Makubwa kuliko Makanisa madogo madogo yaliyosambaa!

  Nimeandika hayo ili tuendelee kujadiliana!

 11. shalom,
  ukubwa au udogo wa kanisa sioni tatizo yote ni sawa, cha muhimu kanisa kama kusanyiko la wakristo ni vyema likawa ni kanisa ambalo watu wanadumu katika fundisho na kumjua vizuri kristo na kukutana na majibu ya mahitaji yao. Neno la Mungu ni Roho na akiwa mtu anakutana na neno halisi linauwezo wa kubadilisha maisha yake kutoka kwenye uovu na kuwa mtu mwema. Mbarikiwe.

 12. Ninavyojua mimi biblia matendo 1:8,8:4 kuna kitu kimeandikwa pale (1)walikusanyika pa1 wakadumu ktk kuomba (2)wakatawanyika baada ya mitume kukamatwa na watu wengi wakaanza kuhubiri injili mbali zaidi kwasababu yesu alisema enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili hapo hafungwi mtu kuhubiri namakanisa kuendelea kujengwa bd hatujafanya vyakutosha ktk kuihubiri injili nainjili yakweli inategemea wewe unaelewa nini naunashauku gani ktk kumpenda mungu hofu yawengi hatuijui kweli utaijuaje feki hofu inawatawala uf 21:8 mungu anataka watu waliojikana nadunia wasimame imara ktk kweli,maombi na utakatifu na utii kwa mungu wengi wanataka ibada ziishie pale walipo mapokeo ya wengi hawataki kusimama upya nawengine hawamjui mungu bd hawajapata nuru ni vizuri kujifunza zaidi hata maduka hayauzi vitu vya kufanana

 13. Kuwepo na makanisa madogo madogo kila mtaa,au makubwa au kanisa moja;haijalishi.
  Lengo ni kwa injili ienee pote duniani.Na kila mtu atimize wito wake hapa duniani.Lakini,tatizo ni kwamba,tunajichimbia mjini tu.Wakati watu wa vijijini wanahitaji injili kwasababu,hawana wa kuwahubiria.Na hata kama wapo wachache,wanahitaji wapate muamko kwa wale wanaowazidi kiimani!.
  Hili bado tatizo Africa nzima.

 14. BWANA YESU asifiwe!Naona yote ni sawa tu yawe mengi madogo madogo au makubwa machache nikitukile kile mradi yawepo na yafundishe mafundisho sahihi,
  mbarikiwe

 15. mimi nadhani yote sawa mradi yanaongozwa na Roho mt na kufuata misingi ya Biblia. Lakini kwa kanisa au huduma yenye waumini wengi ni bora isogezwe na kugawanywa hata mtaa hadi mtaa kufikika kirahisi na kuweza kuwafuatilia kwa ukaribu waumini wake.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s