Tatoo, ni sawa kwa Mkristo?

Wapo wakristo (waliookoka) wanaochora tatoo, kwenye nchi nyingine hata wachungaji nao wanachora tatoo. Biblia imeandikwa katika Mambo ya Walawi 19:28 “Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu, mimi ndimi BWANA”  Je mtu akichora Neno la Mungu kwa mwili wake, inakubalika?

 

Advertisements

15 thoughts on “Tatoo, ni sawa kwa Mkristo?

 1. WALIOMPOKEA YESU MIILI HAIWATUMIKISHI KWA YASIYO NA MAANA KATIKA MAHUSIANO NA MUNGU, BALI HUIHIFADHI MIILI KATIKA AFYA NA USAFI KAMA HEKALU LA ROHO MTAKATIFU

  WARUMI 12:1

  “BASI, NDUGU ZANGU, NAWASIHI, KWA HURUMA ZAKE MUNGU, ITOENI MIILI YENU IWE DHABIHU ILIYO HAI, TAKATIFU, YA KUMPENDEZA MUNGU, NDIYO IBADA YENU YENYE MAANA.”

 2. WALIOMPOKEA YESU WAMENUNULIWA, MIILI SI MALI YAO BALI YA BWANA.

  WARUMI 6:13
  “WALA MSIENDELEE KUVITOA VIUNGO VYENU KUWA SILAHA ZA DHULUMA KWA DHAMBI; BALI JITOENI WENYEWE KWA MUNGU KAMA WALIO HAI BAADA YA KUFA, NA VIUNGO VYENU KWA MUNGU KUWA SILAHA ZA HAKI.”

 3. Ningependa kutoa ufafanuzi juu ya kile alichouliza lucyson kuna madhara gani kiroho katika kujichoro kule,kama sijamuelewa vibaya.madhara ni kuwa kitu muhimu kiroho kuliko vyote ni kutii na kuamini hata kama madhara hayajulikani au hakuna.mfano Musa aliambiwa atamke neno tuu maji yatoke kwenye mwamba yeye akaupiga mwamba hicho kilimfanya asiingie kanaani.sehenu zingine waIsrael walitakiwa kuangamiza kila kitu sehemu zingine waliambiwa wachukue baadhi ya vyitu kama nyara,kutotii kulileta madhara makubwa.

  Hata kama kinachochorwa ni mwili na utaoza hautakwenda mbinguni,Mungu anachotaka kusikiliza kwa bidii na kutii hata kama madhara hayaonekani.

 4. Mpendwa Eucalyptos,

  Kitu muhimu cha kuangalia,unafanya kwa maagizo au utukufu wa nani?.
  Kut20:4
  “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.”
  Kut25:17-18
  “Tengeneza kiti cha rehema cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu na upana wa dhiraa moja na nusu.
  Tengeneza makerubi wawili kwa dhahabu iliyofuliwa kwenye miisho miwili ya hicho kifuniko.”
  Hata Mfalme Solomoni alitengeneza Makerubi kwa mfano
  1Wafalme6: 23
  “Katika mahali Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza makerubi wawili kwa mzeituni”,
  Ukisoma Kut25 yote utaona vitu alivyotengeza Musa ilikuwa ni mfano(copy)vya mbinguni,Na kuwa wakati uleule alipopewa zile amri 10, Musa pia alipewa kielelezo kule Mlimani wakati uleule akipokea amri kumi.cha kuafanya sanamu ya kuchonga kwa mfano wa vitu vya mbinguni.hata alipo tengeneza nyoka ya shaba yalikuwa maagizo ya Mungu,Ibrahimu alipatiwa mtoto pia alitii agizo alipo ambiwa amtoe sadaka tunaona mwisho Bwana alijitwalia sadaka mwanakondoo wake(Yesumwanzo22:7-8).Usifanye kitu Bwana hajasema nawe kama alikataza.
  ,BWANA ametukataza tusichore alama miili Lawi19:28.
  Yatupasa kusikie tena agizo/ufunuo/maono yatakayobatilisha agizo la kwanza na kutupa kibalii,Aseme nasi/nawe Vinginevyo tukitii sauti nyingine isiyo ya Bwana au kwa mapenzi yetu tutakuwa tumekaidi kwa kutosikia sauti yake na kuacha maagizo yake.
  Tumefungia ktk boksi Uweza na Ukuu wa Mungu uwa tunajaribu kuuwekea mipaka kwa kukosa ufunuo au maono.
  Bwana atupe neema yake tuweze kutembea ktk ile njia kuu Isaya 35:8(Kristo,)ili tuweze kuingia barazani pake Bwana kama Mitume Petro,Yohana na Yakobo Huko tutasikia na kuonyeshwa yale yasipaswa /yanayopasa kunenwa au kutenda ktk utumishi/huduma zetu

  Samani wapendwa kama nitakuwa nimetoka nje ya mada, Nilikuwa natoa yale yalio ktk ufahamu wangu kuhusu kuchonga sanamu kwa mpendwa Eucalyptos,

  Neema na izidishwe kwenu,
  Amen

 5. Nawasalimu kwa Jina lipitalo majina yoote, Jina la Yesu Kristo!

  Naomba tuangalie tena mstari wenyewe unaotupa msingi wa kujadili.
  Leviticus 19:28 “Ye shall not make any cuttings in your flesh for the dead, nor print any marks upon you: I am the LORD.”

  Japo tunazungumzia jambo la TATOO ambalo kwenye mstari inasomeka “PRINT” au kwa kiswahili “ANDIKA au CHORA”, nataka niseme kuwa kuna mambo mawili hapo kwenye mstari. Mambo haya mawili ni “MAKE ANY CUTTINGS FOR THE DEAD” & “PRINT ANY MARK”.
  Kwa kifupi tunaonywa kuto kujikata/kutoboa popote katika miili yetu “kwaajili ya wafu” na “kutojichora alama yoyote popote”. Je kwanini Mungu anaonya hivi? Jibu rahisi ni kwakuwa MIILI HII INAHUSIKA NA IBADA. Mungu anasema “MIILI YENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU”, kama ni hekalu basi ni mahali pa ibada.

  Ukifuatilia kwa makini, wengi wanaojichora wanahusika moja kwa moja na ibada ama kwa kujua au pasipo kujua. Watu hawajajua kama kujichora kunaanzia HINA, WANJA, LIPSTICK, RANGI ZA KUCHA NA TATOO KWA MAPANA YAKE. Pia kwenye kujikata ama kujitoboa ni pamoja na MASIKIO,MACHO, PUA, MIDOMO, NDIMI, VITOVU N.K.

  Jambo lingine ni; Tatoo na michoro au alama nyingine ambazo mtu huweka/huwekewa ni “CONTACT POINTS”, kwa hizi nguvu za shetani huweza kujua na kutembelea “walio wao”.
  Kuna mtumishi mmoja wa Mungu nchini Tanzania alinishtua sana siku moja aliposema kuwa “TATOO ZINAISHI”, alishuhudia kitu alichokutana nacho kwa mzungu mmoja. Alikuja ibadani na mchungaji huyu alipomuwekea mkono nguvu za giza zikaanza kujidhihirisha na kumtoka. Shida ilikuwa ni michoro iliyokua mwilini mwake (tatoo).

  Miaka ya karibuni nimewaona idadi ya watu wengi sana ikiongezeka hasa mabinti wakijichora alama/picha mbalimbali zikiwemo; VIPEPEO, MIGUU YA MBWA/nyayo, MAUA, MAJOKA/DRAGON, MTU/WATU/binti/mwanamke, MOYO, MSALABA, MANENO n.k.
  Kila moja ya alama hizi zina maana ambayo inahusika na ibada yake juu ya mwili wa aliyejichora/aliyechorwa.

  Kwanini Mungu alionya hivi?
  Kwa mtazamo wangu ni “ILI MIILI YETU IWE HURU” na hata wakati wote unapomtukuza Mungu juu ya uumbaji alioufanya kwenye mwili wako “UMUAMBIE KWA KILE AMEFANYA NA SI KILE MTU/WATU/RANGI VIMEFANYA. Pia ibada yetu na Mungu aliyetuumba isikinzaniwe (opposed) na nguvu za adui kwa kudai uhalali wa kumiliki nyumba ya ibada(makao).

  Nitarudi tena.
  Mbarikiwe!

 6. mi nataka tufikiri nje ya box, miili yetu imeumbwa kwa ajili ya Mungu, na mwisho itaharibika, jee ukijichora maandiko, kuna lipi baya ulifanyalo? sisemi hakuna ila naomba mwongozo, zaidi tuu ya kusema maandiko yanasema…maandiko yanasema pia usichonge sanamu, lakini Mungu alimuamuru Musa kuweka nyoka wa shaba, hebu tujadili madhara yake spiritually!!

 7. Suala la mtu kujichora, mwilini kwanza si la kibusara, na ndio maana wanaofanya hayo ni wale watu wa mataifa na biblia imesema msienende kama wa mataifa waenendavyo.

  Bwana awabariki sana.

 8. Bwana Yesu apewe sifa.

  Ni kweli biblia iko wazi ila msingi wa swali upo ili kujadiliana kwaajili ya kufundishana “kweli” na si vinginevyo.
  Tunaposema “maandiko yako wazi” ni swala tata kidogo kwani “kwa mambo yote hata yale tunayodhani yanawakanganya wanadamu, maandiko yako wazi juu yake” CHANGAMOTO NI “JE TUNAYAELEWA KAMA YALIVYOKUSUDIWA?”. Je tunamshirikisha Roho Mtakatifu kwenye kujifunza kwetu? Yesu alisisitiza “…atakapokuja HUYO ROHO…ATAWAFUNDISHA…KWELI…”. Nimekuwa nikishuhudiwa kulirudia hili mara kwa mara na hapa ninarudia kuwa PASIPO ROHO MTAKATIFU HATUWEZI KUELEWA YALIYOMO KWENYE MAANDIKO NA MAISHA YETU KWA UJUMLA WAKE.

  Nitarudi punde kujadili TATOO.

  Mbarikiwe.

 9. POLENI KWELI KAMA NENO LA MUNGU INASEMA MAMBO FULANI SIO SAWA NA KWELI NI MUBAYA AINA AJA TENA KUWAULIZA INABAKI KUWAFUNDISHA UKWELI KUPITIA NENO. TATOO HAISAIDII NENO LOLOTE KWA MAISHA YA MWANADAMU

 10. hapo Biblia ipo wazi kabisa maana Mungu amesha waonya watu wake kwamba usichore wala usichonge alama yoyote juu ya mwili wako.Iyo ni dhambi kabisa kwa binadam yeyote haswa kwa wakristo.

 11. Tatoo sio sawa kwa Mkristo.Nilishawahi kusikia kuwa kwenye uchoraji wa tatoo,wengi wanachapwa alama za 666 bila kujua.cha msingi mkristo inabidi aishi maisha matakatifu.Na kama yabidi tuwe watakatifu,tatoo ya nini?

 12. Bwana Yesu Asifiwe wapendwa
  Unaweza kuona bibilia ilikuwa wazi sana kuwa mtu asiandike alama yoyete mwilini hata kama ni hayo maneno ya Mungu but si unayaweka mwili basi hapo utakuwa unaenda kinyume na neno la Bwana

  Mbarikiwe sana

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s