Kama Chembe ya Haradali – I

Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali  mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu” Mathayo 17:20

Kama mbegu ya haradali unavyoipanda, unaweka mbolea na kumwagilizia,  inakuwa mmea mkubwa wenye afya. Ndivyo hivyo nasi tunavyompokea Bwana Yesu, Unapanda Neno la Mungu ndani yako, unazidi kukuwa zaidi na zaidi, unapata mafunuo na mwenye kukuwa kiroho. Neno litazungumza ndani yako, Neno litakuwa chakula chako, na nguvu ya Neno itatembea ndani yako na kuhusika katika kila sehemu ya maisha yako.

Unaanza kidogo tu, kama chembe ya haradali.

Mara nyingi tunaangalia mambo mengi ya kiroho kwa nje, Ashukuriwe Mungu wetu huangalia ndani kabisa ya mioyo yetu. Sio mpaka uwe mkuubwa kwa nje, una huduma kuubwa au unahamasa kwa watu wengi ndio umekuwa mkubwa kwenye ulimwengu wa roho, Mungu anaangalia tofauti na wanadamu. Kama mtoto anavyotungwa, anazaliwa, anatambaa na baadae kukimbia!! Haanzi kukimbia mara tu anapotoka tumboni mwa mama yake! Kama chembe ya Haradali!

Nadhani wengi tunajua kuhusu Mbegu kwenye maisha yetu, tunaipanda kwanza, mti haukuwi pasipo mbegu yake kupandwa (kwenye udongo) Nasi tumeitwa kukuwa (kwenye roho) kama mfano wa mti. Msongamano unaweza kusababisha mti usikuwe, jua kali, upepo na mvua kali, lakini uwezo wa Mungu uko ndani yetu!

Imani, Kama chembe ya Haradali!

Advertisements

2 thoughts on “Kama Chembe ya Haradali – I

 1. Umesema, “Imani, Kama chembe ya Haradali!”
  Ndiyo, ni kweli, hicho ndicho kipimo cha Imani yetu ktk Neno tulilopewa. Hilo Neno ndio Imani yetu!

  Mtafiti Milinga, je, unajua kuwa ktk mbegu zote duniani, ni mbegu ya Haradali pekee usiyoweza ku HYBRID? Sayansi imeshindwa ku hybrid mbegu hiyo, ile IMANI yetu!!

  Tena wameonywa ktk Agano la kale na pia ktk Agano Jipya kuwa WASIONGEZE /WASIPUNGUZE  katika hiyo Imani yetu, Biblia, kwa ushuhuda wa Hukumu maana Mungu ni mwenye Haki hivyo wote huwapa nafasi ya kujirudi kama alivyopewa Kaini!

  Basi, na tutulie hapo ktk Imani yetu hiyo isiyoweza kuchanganywa na mapokeo yoyote yale, itatufikisha ktk kipeo cha Neno lake hata dunia nzima isimame ktk hatua zake na kusema, “Huyu kweli ni mwana wa Mungu!”

  Mbarikiwe nyooote!!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s