Tunamuabudu Mungu yupi?

Hivi sisi wanadamu tunatambua njia ya kweli ipasayo kumuabudu Mungu aliyeziumba mbingu na nchi? Mimi nashindwa kupata jibu kamili kwani wasabato wanadai wako sahihi, Katoliki pia, Lutheran nao, na makanisa ya kilokole wanadai wengine hutumia nguvu za giza kuombea watu na viongozi kujitajirisha wenyewe.

Makanisa mengine wanaruhusu ushoga, waislamu nao ndo kabisaa na majini ndani ya misikiti, nabaki njia panda ni wokovu gani uliopo kwa mwanadamu na Mungu yupi huyo tunayemuabudu? Je ni heri nifanye Ibada ndani ya nyumba yangu na kutoa misaada kwa masikini na wasiojiweza na kutembelea watoto yatima? Niko njia panda naomba atakaye nijibu anipe evidence za Bible. Ahsante!

–Elifuraha Julius

Advertisements

6 thoughts on “Tunamuabudu Mungu yupi?

 1. Hivi unajua maana ya Dini?
  Ukristo siyo dini na hakuna sehemu yoyote katika Biblia takatifu inayosema Ukristo ni dini. Ukristo ni maisha ya kuishi kama Kristo na kama ndugu zangu walivyoongea hapo juu hakuna dhehebu linaloweza kukupeleka mbinguni ila Yesu Krsito peke yake. Yohana 16:4.

  Nini tafsiri ya dini basi?
  Dini ni njia ya mwanadamu kumtafuta na kumuabudu Mungu. (Kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la kwanza)
  Lakini ukija kwenye Ukristo Mungu ndiye aliyetutafuta sisi kwa kumtoa mwanaye wa pekee Yohana 3:16
  Basi ishi kwa misingi ya kikristo (Yohana 4:23-24) na kikubwa zaidi muombe Mungu akupe sehemu ya kuabudia ambayo itakujenga kiroho na Sehemu hiyo (Kanisa hilo lazima liwe linatumia Biblia na wala si vinginevyo yaani wasimtengenezee Mungu utaratibu wa kumuabudu wafuate maelekezo ya roho Mtakaktifu.

  Amani ya Yesu Kristo iwe nanyi!

 2. ”LAKINII SAA INAKUJA, NAYO SASA IPO , AMBAPO WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI” (Yohana 4:23-24)

 3. Ndugu Bwana Yesu asifiwe….!
  Umeuliza swali zuri ambalo linasumbua watu wengi sana.
  Jibu la swali lako unaweza kulipata katika maandiko matakatifu.Njia ya kweli ni moja tu,ni Yesu Kristo mwana wa Mungu aliyehai (Yoh.14:26 ).Ukimkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako utaokoka (Rum.10:9).Kwa hiyo dini kama dini haiwezi kukupeleka Mbinguni hata kama unasali kanisa gani usipompomkea Yesu hiyo ni kazi bure.

 4. Yesu wa Nazareth ndo njia pekee,Yohana 16:4,mpe maisha yako na fata maagizo yake,Yohana14:15.Usiangalie flani anafanya nini,ila;pigania uzima wa roho yako.ukikaa kumtazama flani,utapoteza muda labda kama unawaangalia kwa kusudi la kuwaweka sawa.
  Ndugu yangu,akina yuda wengi mno.Ila,yuda alipomsaliti Yesu,wanafunzi wake 11 waliokuwa wamebaki,hawakukata tamaa.Wangekaa kusema,’mbona Yuda kafanya hivi?!’,wasingesonga mbele.

 5. BWANA YESU ASIFIWE!

  Dini ya kweli ukiitafuta kwa macho haya ya nyama itakupa wakati mgumu sana, kama dini ni njia angalia uliposimama au unaenenda kwenye njia ipi ya kukufikisha Mbinguni kwa BABA,MWANA na ROHO MTAKATIFU

  Ukiijua kweli nayo kweli itakuweka huru,YESU tu ndiyo njia ya kweli ya UZIMA NA MTU YOYOTE hataiona mbingu bila kumkiri YESU kuwa BWANA na mokozi wa maisha yake (warumi 10.9-15)

  Kwahiyo angalia popote uliposimama kama panautukuza utatu mtakatifu na unadumu katika kulisoma neno la uzima BIBLIA,maana NENO ndiyo kristo hapo ndipo utakapopewa uwezo wa mtu wako wa ndani ambaye atakuwa na uwezo wa roho mtakatifu. pia READY AND STUDY BIBLE,fuatilia historia za makanisa kwanini waislamu wapo,kwanini wasabato wapo,waroma,waporestant nk ndipo utakapofanikiwa na kujibiwa maswali magumu uliyonayo. DANIEL wakati wa Uhamisho katika ufalme wa BABELI alijua vitu vingi kwa kusoma vitabu PAMOJA na miaka 70 ya wao kukaa uhamishoni babeli, DANIEL 9.2

  kwahiyo kwenye kujisomea kuna kupanua ufahamu na maarifa, maana vitu vingi vimefichwa kwenye vitabu na maandishi. MUOMBE YESU AKUFUNGUE MACHO YA ROHONI MAANA mtesi wetu ametufunga nira ili kusiifahamu kweli ya MUNGU,lakini KWA MAMLAKA TULIYOPEWA YA KUPANDA NA KUJENGA NENO LA KRISTO MIOYONI MWETU AMESHINDWA KATIKA JINA LA YESU NAMI NAPANDA MBEGU HIYO SASA YA KUJISOMEA KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYEHAI

  AMEN

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s