Askofu Gamanywa amshukuru Mungu, miaka 23 ya ndoa!

Askofu Gamanywa na mkewe Alhappiness wakitoa shukrani

HABARI KUTOKA GOSPEL KITAA

Rais wa shirika la kidini la Wapo Mission International Bishop Sylvester Gamanywa,wiki iliyopita alimshukuru Mungu pamoja na familia yake kwa kutimiza miaka 23 ya ndoa pamoja na mkewe katika kanisa la Pentekoste Tanzania Lindi street(city centre), kanisa ambalo ndilo lilimpatia vibali vya utumishi shambani mwa BWANA mpaka leo hii.

Akiwa na watoto wake wanne Excellent,Excel,Samael, David pamoja na mkewe mpenzi Alhappiness, Bishop Gamanywa alipata nafasi ya kuzungumza pamoja na familia yake na kubariki waumini waliofika kanisani hapo,wakimshukuru Mungu kwa uzima na afya pamoja na yote anayowatendea toka walipofunga ndoa mnamo tarehe nne mwezi wa tatu mwaka 1989.

Shirika la Wapo analoliongoza ndani yake kuna vituo vikubwa viwili vya ushauri wa kibiblia na maombezi(Biblical Counselling and intercession centres) BCIC Mbezi beach pamoja na Mbagala maji matitu ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakibarikiwa na kufunguliwa kutoka matatizo mbalimbali yanayowaandama vituo hivyo ni maarufu kwa jina la Hakuna lisilowezekana kutokana na yale Mungu amekuwa akiyatenda katika maisha ya watu wake.

Kutoka kushoto, Askofu Gamanywa,mkewe Alhappiness watoto wao David,Samael,Excellent pamoja na Excel.

Pamoja na vituo hivyo pia shirika hilo linamiliki kituo cha redio cha kikristo cha Wapo radio FM 98.0 kilichopo maeneo ya kurasini jijini Dar es salaam,kituo ambacho kimekuwa baraka kwa wengi kutokana na vipindi vya kijamii na kiroho vinavyoendeshwa chini ya uangalizi wake Bishop Gamanywa.

Baadhi ya waumini waliokuwepo ibadani.
Askofu Gamanywa na familia yake wakiwa katika pozi na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
Askofu Gamanywa akiwa na familia yake.
Advertisements

5 thoughts on “Askofu Gamanywa amshukuru Mungu, miaka 23 ya ndoa!

 1. My brother in Christ, Gamanywa

  Waitu hongereni, rest assured that you have shocked me why? your good 23 years in marriage is equal to 3 and 1/4 of my existence time in this Dunia, kha! Me am living such 3 and 1/4, you already ni marriage!!!! Aisee, kwakweli Some of the people have really eaten the good of the land. You are blessed indeed.

  Live longer ila sikubaliani na Milinga on ”summarization of numbers of humans from our waist/loins to strictly 4!! let them come out and land hapa mujini in as many as the stars in Kigoma sky, I am in that preference…causing creatures to land to see and enjoy the Wonderful World

  Press on

 2. Familia yenu inapendeza sana Hongereni, Sifa na Utukufu apewe Mungu

 3. Hongeeeeera sana. Nakupongeza sana kwa kuzaa watoto 4 tu. Natamani kujua ulitumia njia gani kuzaa watoto 4 tu.

  Natamani kuona wachungaji wote wakiiga mfano wako. Watoto 4 tu. Hata mimi nadhani Mungu akinijalia naomba anipe watoto 4 tu siyo lazima wawe wa jinsi tofauti. wawe wa kike au wa kiume sawa tu kwangu.

  Askofu tunatamani huduma ya Redio WAPO ifike Kigoma. Hivi una habari kwamba huku Kigoma hatuna Redio kabisa ya Injili. Mkoa mzima hatuna redio ya Kipentekoste.

  Mungu akubariki sana wewe na watoto wako na mkeo na huduma yenu ikue zaidi.

 4. Hongera sana Bishop Gamanywa.Yesu awape maisha marefu zaidi na yenye furaha!.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s