Je, unafahamu uzuri wa Mbinguni?

Mpendwa msomaji, kwanza pole sana na shughuli nyingi za kila siku. Ninajua kwamba muda wako ni mchache sana, kutokana na shughuli zako nyingi. Hata hivyo ninakuomba muda wako mfupi tu, ili tuzungumze juu ya jambo muhimu ambalo nimeona kwanba ni vema nikushirikishe. Je umekubali ombi langu? Natumaini umelikubali. Asante sana. Basi ninakusihi tufuatane pamoja katika mazungumzo haya.

Huenda utakuwa umewasikia watu wengi waliofiwa na ndugu, jamaa au marafiki zao wapendwa, wakisema, ”Mungu waweke mahali pema peponi“. Jambo hili linadhihirisha jinsi kila mmoja wetu anavyoamini kwamba kuna mahali pema peponi yaani mbinguni. Na tena inaonyesha jinsi sisi sote na jamaa zetu tunavyopenda kwenda huko. Je,wewe una shauku ya kwenda mahali pema peponi au mbinguni, baada ya kuiaga dunia hii? Najua wewe pia una shauku ya kwenda mbinguni siku moja. Hata hivyo, shauku yako itaongezeka zaidi utakapokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu uzuri wa mbinguni. Peponi au mbinguni, ni wapi na kukoje? Peponi au mbinguni, kuna uzuri usioweza kufananishwa. Tukifahamu jinsi mbinguni kulivyo kuzuri, kila mmoja wetu atazidi kuwa na shauku ya kufika huko siku moja. Tufuatane basi ili upate ufahamu wa kutosha kuhusu mbinguni au peponi.

Peponi au mbinguni ni wapi na kukoje? Mbinguni au peponi, ni juu sana, mbingu ya tatu. Biblia inasema katika 2 WAKORINTHO 12:2-4, ”Namjua mtu mmoja katika Kristo,…Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo,…ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi…“ Mbingu ya tatu ni wapi? Mbingu ya kwanza, ni hii iliyo na mawingu yanayoleta mvua, na mawingu mengine. Ni anga hili lililo juu ambalo sehemu yake huonekana kwa macho ya kawaida. Ndege au eropleni zote zinazobeba abiria, huruka katika mbingu hii ya kwanza. Mbingu ya pili, ni mbingu iliyo mbali zaidi yenye sayari na nyota zote, Sayari zilizoko katika mbingu ya pili, ni pamoja na Zebaki, Zuhura, Mars, Mshtarii, Zaharii, Uranus, Neptune, na Pluto. Sayari nyingine ziko mbali sana. Kwa mfano, umbali wa dunia yetu kutoka kwenye jua ni maili 93 milioni (kilometa 148,800,000). Lakini umbali wa sayari ya pluto kutoka kwenye jua ni maili 3,666 milioni (karibu kilometa 5,900 milioni). Nyota ziko nyingi sana, zinakisiwa kufikia bilioni 400. Nyota ziko mbali sana na dunia yetu. Nyota iliyo karibu zaidi na dunia, iko karibu maili 26,000 bilioni (karibu kilometa 42,000 bilioni). Sasa basi, baada ya sayari zote hizi na nyota hizi, ndiyo tunafikambingu ya tatu. Mbingu ya tatu, au Peponi, kwa msingi huu ni kilometa mabilioni kutoka hapa duniani. Yesu Kristo alipopokelewa na wingu, na kupaa kwenda juu mbinguni ( MATENDO 1:9-11) alikwenda mbali sana kiasi hiki. Huko ndiko waliko watakatifu waliotutangulia.

Tupige hatua tena na kuangalia mambo mengine. Sasa je, mtu anapokufa, anasafirije kwenda mbinguni, mbali kiasi hiki? Hatupaswi kuogopa kifo, ikiwa tunaishi maisha yaliyo mbali na dhambi. Biblia inasema katika ZABURI 116:15, ”Ina thamani machoni pa Bwana, mauti ya wacha Mungu wako“. Kufa kwa watakatifu ni faida (WAFILIPI 1:21). Ni heri wafu wafao katika Bwana (UFUNUO WA YOHANA 14:13). Kufa kwa mtu anayeishi maisha yaliyo mbali na dhambi, ni mwanzo tu wa utukufu. Mtu anayeishi maisha yaliyo mbali na dhambi, anapokufa, roho yake humiminwa katika mwili mwingine wa roho unaoitwa mwili wa mbinguni, kama mafuta yaliyo katika chombo kibovu kinachovuja, yanavyoweza kumiminwa katika chombo kingine kilicho kizuri. Kufa, ni kumiminwa! Mtume Paulo aliyepata neema ya kuchukuliwa na kupelekwa mpaka mbingu ya tatu wakati wa uhai wake ( 2 WAKORITHO 12:2-4) ulipofika wakati wa kufariki kwake, alijua ni wakati mzuri wa kumiminwa. Kwa maneno yake, katika 2 TIMOTHEO 4:6, alisema, ”Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika“.

Kuhusu miili ya mbinguni, Biblia inasema katika 1WAKORINTHO 15:40-41,44, ”Tenakuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani, lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota…Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko“. Miili hii tuliyonayo ni mibaya sana. Ni kama vyombo vibovu. Fahari yake, yaani uzuri wa ile miili ya mbinguni ni zaidi sana kuliko miili tuliyo nayo. Miili ya mbinguni inang’aa mno na kupendeza sana. Mtakatifu anapokata roho, roho yake mara moja humiminwa katika mwili mzuri wa jinsi hii. Mtu akiwa katika mwili wa mbinguni, atapenda kujitazama wakati wote. Mwili huu hauna makovu wala ulema wala makunyanzi ya uzee! Baada ya mtu kuwa na mwili mzuri wa jinsi hii, huvikwa mavazi mazuri meupe sana yanayometameta sana. Weupe wa mavazi haya, ni weupe usio na mfano duniani (UFUNUO WA YOHANA 3:4-5;7:9; MARKO 9:2-3). Baada ya kuvikwa mavazi haya, mtu hufunguliwa mlango wa gari na malaika, na kuingizwa katika gari zuri sana lisilokuwa na mfano duniani. Yako mabilioni ya magari ya Mungu, yanayowasubiri watakatifu. Biblia inasema katika ZABURI 68:17, ”Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu“. Mtu huchukuliwa na malaika katika magari haya yanayoitwa magari ya moto, yanayoambatana na farasi wa moto na kuchukuliwa kwenda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli (LUKA 16:22; 2 WAFALME 2:11).

Magari yanayoitwa magari ya kifahari yanayowabeba Marais na Wafalme duniani kama Mercedes Benz, BMW n.k.si kitu yanapolinganishwa na magari haya. Magari ya Mungu  hayatumii dizeli au petroli, bali huendeshwa na upepo wa kisulisuli, na huenda kasi sana. Kwa muda mfupi sana, mtu hufika mbinguni na kulakiwa na malaika wanaoimba nyimbo za shangwe. Hakuna mapokezi yoyote ya Rais au mfalme yeyote duniani, yanayolingana na mapokezi ya mtu anayeingia mbinguni, yanayofanywa na malaika.

Sasa tupige hatua nyingine. Mbinguni kwenyewe kukoje? Mbinguni ni nchi iliyo bora kuliko nchi yoyote duniani (WAEBRANIA 11:16). Waza juu ya nchi yoyote duniani inayowavutia watalii wengi kutokana na uzuri wake. Nchi hii siyo kitu ikilinganishwa na Peponi. Mbinguni ni kuzuri mno! Hakuna usiku wala mchana. Hakuna joto wala baridi. Jua au mwezi havitumiki kutoa mwangaza. Utukufu wa Mungu ndiyo nuru ya mbinguni (UFUNUO WA YOHANA 21:23-25). Neno ”Peponi“, linatokana na neno la Kiyunani, ”Paradeisos“, linalotafsiriwa pia, ”Paradiso“, na kwa tafsiri fasaha, lina maana ya ”bustani nzuri kubwa iliyojaa matunda mazuri“ na tena linamaanisha mahali palipojaa furaha na raha kuu isiyo na kifani (UFUNUO WA YOHANA 2:7; WAEBRANIA 4:1-11). Matunda ya miti iliyomo katika bustani hii isiyokuwa na mfano, ni pamoja na mti  wa uzima uzaao matunda aina kumi na mbili. Maisha mbinguni, ni pamoja na kula matunda haya katika bustani ya Mungu, na kupunga upepo wa raha kuu isiyo kifani, Paradiso (UFUNUO WA YOHANA 2:7; ).

Kipi cha ziada tena kuhusiana na mbinguni? Mbinguni, ni mji uliobuniwa na kujengwa na Mungu (WAEBRANIA 11:10-16). Miji yote ya dunia hii imebuniwa na kujengwa na wanadamu wenye upungufu wa ubunifu wa michoro, fedha, vifaa n.k. Mbinguni, ni mji uliobuniwa na Mbunifu Mkuu, Mungu mwenyewe mwenye uwezo wote. Hakuna mji kama huu duniani. Barabara zake siyo za lami, bali ni za dhahabu iliyo kama kioo kiangavu ambayo hakuna mfano wake duniani. Mtu anapotembea barabarani, hujiona kama katika kioo (UFUNUO WA YOHANA 21:21). Katika YOHANA 14:2, Yesu anasema, katika mji huu kuna ”makao“ mengi. Neno la kiyunani linalotafsiriwa hapa ni ”mone“, linalotafsiriwa katika kiingereza ”Mansion“, katika Biblia ya tafsiri ya King James Version. ”Mansion“, ni jumba kubwa la kifahari. Jumba la Meya wa Jiji la London, Uingereza (”Lord Mayor of London), linaitwa ”Mansion House“. Vivyo hivyo mbinguni, kuna makao mengi, au majumba mengi  ya kifahari. Kila mtu atakayeingia mbinguni, atapewa ”kao“, au ”jumba mojawapo la kifahari“, la kuishi. Kao lako linakusubiri! Majumba haya, hayakujengwa kwa tofali za sementi au udongo, bali kuta zake zimejengwa kwa madini ya aina nyingi. Biblia inasema katika UFUNUO WA YOHANA 21:18-20,  ”Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwayaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi mfano wa kioo safi. Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolith; wa nane zabarajadi; wa kenda (tisa) yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso, wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto“.

Vito hivi au madini haya, yanafanya majumba ya mbinguni, yapendeze mno. Yaspi,ni madini yanayong’ara sana yenye rangi ya kijani iliyochanganyika na bluu. Yakuti samawi, ni mawe ya bluu, mazuri sana yenye ugumu unaofuatia madini ya almasi.Kalkedoni, ni aina ya madini mazuri sana yenye rangi aina nne  balimbali-nyekundu iliyochanganyika na njano, hudhurungi (brown) iliyochanganyika na nyeusi, bluu iliyochanganyika na nyeupe, na rangi ya maziwa. Zumaridi, ni madini yenye rangi ya damu. Krisolitho, ni madini yaliyo kama dhahabu, ila yana rangi aina ya kijani iliyochanganyika na njano, Zabarajadi, ni madini maangavu (yanayoona ndani), yenye  rangi ya bluu iliyochanganyika na kijani. Yakuti manjano, ni madini  mazuri yenye rangi ya njano na mchanganyiko wa kijani.Krisopraso, ni madini yenye rangi  tatu pamoja; njano, kijani, na bluu. Hiakintho, ni madini yenye rangi iliyochanganyika na njano. Amethisto, ni madini yenye rangi ya zambarau, yenye bluu na wekundu ndani yake.

Nini zaidi? Mwangaza wa mbinguni siyo kama wa duniani usio na rangi. Mwangaza wa mbinguni ni wa rangi ya yaspi yaani kijani iliyochanganyika na bluu (UFUNUO 21:11). Mavazi meupe ya wale walioko mbinguni, hubadilika  rangi mara kwa mara kutokana na rangi ya mwangaza na ya majengo hivyo kufanya watu wapendeze mno. Ndani ya makao ya mbinguni kuna fenicha za kifahari. Fenicha alizoagizwa Musa kuzitengeneza na kuziweka katika maskani, zilikuwa mfano tu wa fenicha za mbinguni(WAEBRANIA 8:5; KUTOKA 25:9-40). Chemchemi za maji na mito ya maji ya uzima inazunguka mji. Mbinguni kuna  kula na kunywa, hakuna mauti wala maumivu au taabu (LUKA 22:14-16, 29-30; UFUNUO 2:17; 21:4-5; 14:13). Kuna kuimba nyimbo za sifa, na vinanda (UFUNUO 14:2-3; 15:2-4). Ufahamu wetu utaongezeka (1WAKORINTHO 13:12). Kuna mengi zaidi yasiyotamkika katika lugha hii ya duniani (WAKORINTHO 12:4). Ni heri twende wenyewe kujionea. Tusikubali mume au mke kutuzuia kuingia mbinguni maana mbinguni hakuna kuoa au kuolewa (LUKA 20:34-36; MATHAYO 22:30).    

Ni sifa ipi ya kukuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia chochote kilicho kinyonge (UFUNUO 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, Ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini, hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14;6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni,

”Mungu Baba, asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.Bwana yesu, niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen.“

Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI!!! 

Advertisements

11 thoughts on “Je, unafahamu uzuri wa Mbinguni?

 1. Elia,

  Najaribu tu kuleta mawazo mbali mbali ili ndugu Milinga aweze kuona mawazo mbali mbali…….

 2. Milinga

  Question: “What happens after death?”

  Answer: Within the Christian faith, THRE IS A SIGNIFICANT AMOUNT OF CONFUSION regarding what happens after death. Some hold that after death, everyone “sleeps” until the final judgment, after which everyone will be sent to heaven or hell. Others believe that at the moment of death, people are instantly judged and sent to their eternal destinations. Still others claim that when people die, their souls/spirits are sent to a “temporary” heaven or hell, to await the final resurrection, the final judgment, and then the finality of their eternal destination. So, what exactly does the Bible say happens after death?

  First, for the believer in Jesus Christ, the Bible tells us that after death believers’ souls/spirits are taken to heaven, because their sins are forgiven by having received Christ as Savior (John 3:16; 18, 36). For believers, death is to be “away from the body and at home with the Lord” (2 Corinthians 5:6-8; Philippians 1:23). However, passages such as 1 Corinthians 15:50-54 and 1 Thessalonians 4:13-17 describe believers being resurrected and given glorified bodies. If believers go to be with Christ immediately after death, what is the purpose of this resurrection? It seems that while the souls/spirits of believers go to be with Christ immediately after death, the physical body remains in the grave “sleeping.” At the resurrection of believers, the physical body is resurrected, glorified, and then reunited with the soul/spirit. This reunited and glorified body-soul-spirit will be the possession of believers for eternity in the new heavens and new earth (Revelation 21-22).

  Second, for those who do not receive Jesus Christ as Savior, death means everlasting punishment. However, similar to the destiny of believers, unbelievers also seem to be sent immediately to a temporary holding place, to await their final resurrection, judgment, and eternal destiny. Luke 16:22-23 describes a rich man being tormented immediately after death. Revelation 20:11-15 describes all the unbelieving dead being resurrected, judged at the great white throne, and then being cast into the lake of fire. Unbelievers, then, are not sent to hell (the lake of fire) immediately after death, but rather are in a temporary realm of judgment and condemnation. However, even though unbelievers are not instantly sent to the lake of fire, their immediate fate after death is not a pleasant one. The rich man cried out, “I am in agony in this fire” (Luke 16:24).

  Therefore, after death, a person resides in a “temporary” heaven or hell. After this temporary realm, at the final resurrection, a person’s eternal destiny will not change. The precise “location” of that eternal destiny is what changes. Believers will ultimately be granted entrance into the new heavens and new earth (Revelation 21:1). Unbelievers will ultimately be sent to the lake of fire (Revelation 20:11-15). These are the final, eternal destinations of all people—based entirely on whether or not they had trusted Jesus Christ alone for salvation (Matthew 25:46; John 3:36).

  Nadhani baada ya kusoma hii article tunaweza kuanza mjadala……umegusa baadhi ya maswali yako…..

 3. Milinga……..article hii inaweza kukupa mwanga wa maswali yako….

  Question: “What is paradise? Is it different than Heaven?”

  Answer: The word paradise is used as a synonym for “heaven” (2 Corinthians 12:4; Revelation 2:7). When Jesus was dying on the cross and one of the thieves being crucified with Him asked Him for mercy, Jesus replied, “I tell you the truth, today you will be with me in paradise” (Luke 23:43). Jesus knew that His death was imminent and that He would soon be in heaven with His Father. Therefore, Jesus used “paradise” as a synonym for “heaven.”

  What we do know for sure is that there has always been a separation of believers and unbelievers (Luke 16:19-31). The righteous have always gone to paradise; the wicked have always gone to hell (hades). For right now, both heaven (paradise) and hell (Sheol) are “temporary holding places” until the day when Jesus Christ comes back to judge the world based on whether or not they have believed in Him. The first resurrection is of believers who will stand before the Judgment Seat of Christ to receive rewards based on meritorious service to Him. The second resurrection will be that of unbelievers who will stand before the Great White Throne Judgment of God. At this point, all will be sent to their eternal destination—the wicked to the lake of fire (Revelation 20:11-15), and the righteous to a new heaven and a new earth (Revelation 21-22).

 4. Milinga,

  Haya si mawazo yangu…….. jamaa huyu anasema mbingu iko kaskazini…….!

  Does the Bible give us specific clues as to where heaven is located? Yes, it does! Read on and you’ll know. It appears from a study of the Scriptures that heaven is located in the North of our universe. When they would offer the sacrifice in the OT they would offer them northward toward the Lord. Notice what Moses said in [Lev. 1:11]. Now, north is always the same direction from this planet no matter what time of day. Salvation comes from the north [Psalm 75:6], east, west, south us mentioned, but not north-therefore salvation comes from the north [from God, of course]. What else on North is there? Check out [Job 26:7]. This reference also says, “He stretched out the north over the empty place. There is an empty place or void in the North of our universe. This place is so large it could contain 200 of our Milky Way galaxies. The Milky Way is 100,000 light years across. Light traveling @ 186,000 miles per second would take 100,000 years to travel from one end of our Milky Way to the other. We believe that heaven is located in that void in the north of out universe! Other references to the north are: [Isa. 14:13; Psalm 448:1-2; and Hebrews 12:22]

  nikipata muda tutaendelea na mada….nimekupa kitu cha kukufikirisha…….

 5. Mpendwa Orbi Ubarikiwe.

  Natamani kupata mjadala wa maswali yote na ninaona maswali yote kama yana maantiki kabisa Kibiblia.

  Swali la 1: Wako Kaburini na wamerudi mavumbini? Nimeliuliza kwa sababu kila siku tunapokuwa kwenye mazishi ya mpendwa Mchungaji anapoendesha Ibada ya mazishi huwaaminisha waliohudhuria mambo mawili: Kwanza, Anachukua udongo na huku anatamka maneno haya, “Umetoka mavumbini na mavumbini utarudi…..” huku akitupia udongo kwenye kaburi la mzikwa. Hapa utaona kwamba tunaaminishwa kuwa siyo tu mwili unarudishwa mavumbini bali pia Uhai wa mtu na roho yake maana ndiyo inayoambiwa. Pili, anapokuwa anawafariji waliobaki au wafiwa anawaambia kwamba huyu mwenzetu ametutangulia kwenda mbinguni na siku moja tutakutana naye wala tusiwe na huzuni sana kama wasiokuwa na tumaini. Mchungaji anapotamka hayo maneno anakazia kwamba marehemu hayuko nasi pale makaburini bali yuko mbinguni tayari anakula raha na starehe za mbinguni. Kwa hiyo utaona kwamba hapa kunahitaji mjadalaa wa kuweka Imani yetu sawa.

  Swali la 2: Hili nimeliuliza kwa sababu bado Wakristo tuna maandiko mengi ambayo yanahitaji ufafanuzi kuhusu wafu na Mbinguni. Wapo wafundishao kwamba mtu akifa haendi Mbinguni papo hapo. Pili kuna wanaosema mtu akifa anakaa mahali fulani (siyo mbinguni) akisubiri sauti ya parapanda ndipo wafufuke. Hapa napo pana mjadala.

  Swali la 3: Mjadala ni kwamba majina yaatumikayo kueleza watu wa waliofariki waliko ni mengi. Wengine hutaja; peponi, mbinguni, mbingu ya 3, paraadiso, Yerusalem, nk. Hapa ndipo penye mjadala.

  Swali la 4: linajadilika kama ulivyosema. Naomba sasa swali la 5 niliondoe kwenye majadiliano haya.

  Nakushukuru sana bwana Orbi. Mchango wako ni muhimu sana.

 6. Ndugu Milinga,

  Mimi naona maswali mawili yanahitaji kuondolewa kabisa…….hayako katika misingi ya Imani ya Kiristo kabisa

  1. Wako Kaburini na wamerudi mavumbini?……

  Binadamu ni zaidi ya mwili………mwili ndio unarudi mavumbini……..binadamu ni nafsi hai……..hata kama Biblia itatumia binadamu kurudi mavumbini kumbuka Biblia ina figurative speech……Si dhani swala hili linahitaji mjadala……..Nafsi hai ya Mungu haikutoka mavumbini….!

  5. Wafu Hawapo popote pale bali kumbukumbu yao imetoweka?…….

  Biblia inafundisha Binadamu ni nafsi hai…..kumbukumbu yake haipotei……nafahamu kuna twisted teachings mbalimbali….kuhusu “annihilation” Kutowesha au kuteketezwa kwa wasiomjua Mungu (kama imani ya Sabato na baadhi ya madhebu ya Kikristo)…..Lakini mafundisho haya yanahoja dhaifu……..na mara nyingi yanaishia malumbano ya maana ya “moto wa milele” nk……inabidi turudi tena kwenye Lugha ya awali ya Biblia……”Greek” kupata maana ya maneno hayo…….Ukikubali mafundisho haya ina maana inabidi uondoe mistari mingi mno katika Biblia……na kukiondoa Kitabu chote cha Ufunuo……….

  Hivyo nadhani (Kwa mtazamo wangu ni maswali 2,3,na 4 ) ndio tunaweza kujadiliana hapa………Labda ueleze kwa nini unaona maswala haya mawili yana utata……

  UBARIKIWE…..

 7. Mpendwa Orbi,

  Asante kwa jinsi ulivyoeleza kutokana na maoni yangu. Inapendeza kwani naona una mawazo na uelewa unaorandana na wa kwangu.

  Hebu pia naomba unisaidie kwa faida ya wasomaji wengine pia,

  Je, watu wanapofariki wanaenda wapi?

  1. Wako Kaburini na wamerudi mavumbini?

  2. Wafu Wamelala tu usingizi wa kifo na siku moja wataamushwa na parapanda?

  3. Wafu Wako Mbinguni, Paradiso, Peponi, au Yerusalem Mpya aliko Yesu?

  4. Wafu Wamefichwa sehemu fulani tu wakisubiri ufufuko?

  5. Wafu Hawapo popote pale bali kumbukumbu yao imetoweka?

  Maswali haya matano yanahitaji majibu.

  Majibu yaweza kuwa “Biblical analyzed” au “logical analyzed” ili kumfanya msomaji aelewe.

  Mtu yeyote mwenye majibu anisaidie siyo lazima Mr. Orbi peke yake anisaidie.

  Nasubiri majibu kwa hamu sana.

 8. Ndugu Milinga,

  Mimi naona la msingi ni kuwa Mbinguni ni mahali hakika Bwana alipo…….kule aliko kwenda kutuandalia Makao……kule alikoketi mkono wa kuume wa Mungu Baba…….kule ambako wazee Ishiri nne wanamzunguka wakisema MTAKATIFU MATAKATIFU MTAKATIFU……..

  Sidhani kabisa unaweza kui- position Mbingu iko wapi …….maana hii sayari yetu (Dunia na solar system) ni nukta ndogo mno katika hili anga tunaloliona…….nashindwa kuweka kwa kiswahili maneno kama “Milky way” na Galaxy……lakini ukiniambia nitoe mfano ili watu wajue basi ….Dunia yetu na jua na mwezi na sayari zake ni kama nukta moja ndani ya Biblia million mia moja…..!Inatisha kwa ufahamu wa kawaida…….sisi na dunia yetu ni wadogo mno mno mno mno……kinachotia moyo tu sisi viumbe vya Kiroho……..na tutaishi milele….!

  Hivyo wapendwa siwezi kujua kwa hakika Mbinguni ni wapi….kwa ufahamu wa kawaida wa kibinadamu huwa tunaonyesha ni juu…… …..lakini hata ukiwa mwezini……duniani kunaonekana ni juu pia……..! Hayo ndio maajabu ya uumbaji wa huyu Mungu……

  Hivyo tukazane Kwenda Mbinguni Mungu aliko……….na Yesu ndio Njia……

  Mbarikiwe…..

 9. Asante kwa ujumbe,

  Nimebarikiwa na kutiwa moyo mno, ujumbe kwamba kuna Mbingu au kuna makao aliyotuandalia Mungu baada ya maisha haya ya kitambo umekua ni adimu katika mimbari nyingi, na taratibu waumini wanajikuta wanasahau kwamba wao ni wapitaji na wasafari hapa duniani.Mafundisho mengi kwa sasa hivi yamekua si kuwaandaa watu jinsi ya kutembea kuelekea Mbinguni bali nini jinsi ya kukaa duniani kufurahi na kufanikiwa…..!

  Wengi tunasahau kabisa hakuna furaha ya kweli katika maisha haya, furaha zozote zile ambazo ulimwengu unaweza kutupa ni za kitambo….! Nakumbuka wengi wanavyosema nikimaliza shule nitafurahi…inakuwa kweli ni furaha, lakini furaha ya muda tu……kwani baada ya hapo wanasema nitafurahi nikipata kazi…….wanapata kazi……furaha inakuwa kubwa mno…..lakini baada ya muda wanaona kazi haina maana mpaka waongeze elimu ili wapate nafasi ya juu zaidi…..wanafanya hivyo……..wanamaliza masomo ya juu, wanapanda cheo…….wanaona pia havileti furaha kamili………mara wanaona watakamilika kabisa na kuwa na furaha wakioa na kuolewa ………wakiwa na watoto……….wakijenga nyumba……..wakinunua gari………mume na mke kuwa kila mmoja na gari………kufungua miradi….. mara watapumzika na kuwa na furaha ya kweli watoto wakienda vyuo…! Orodha inaweza kuendelea na kuendelea………Kila furaha inakuwa ni ya kitambo tu………! HAKUNA FURAHA YA KWELI KATIKA MAISHA HAYA……….!

  Wakristo wengi tunasahau tunaishi ulimwengu uliomwasi Mungu….ulimwengu unaongoja Hukumu…….tunaishi mahali ambapo panasuburi kuteketezwa………! Ni kweli sisi hatuko katika Hukumu itakao upata Ulimwengu…lakini tunaishi mahali ambapo huwezi ukaipata furaha ya kweli…….Majengo mazuri……..furaha iletwayo na mahusiano ya kijamii (ndoa) …..furaha ya kuwa na mali……..sifa………haigeuzi ule ukweli wa hofu na giza la hukumu ya ambalo limetanda na liko juu ya Ulimwengu…….na kufanya Ulimwengu kuwa mahali pa kutisha…..!

  Ujumbe huu nilipousoma umenifanya nirudi kwenye Kitabu cha Ufunuo…..KISHA NIKAONA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA;KWA MAANA MBINGU ZA KWANZA NA NCHI ZA KWANZA ZIMEKWISHA KUPITA………TAZAMA MASKANI YA MUNGU NI PAMOJA NA WANADAMU…….WATAKUWA WATU WAKE NA MUNGU MWENYEWE ATAKUWA PAMOJA NAO……NAYE ATAFUTA KILA CHOZI KATIKA MACHO YAO, WALA MAUTI HAITAKUWEPO TENA, WALA MAOMBELEZO,WALA KILIO, WALA MAUMIVU,HAYATAKUWEPO TENA KWA KUWA MAMBO YA KWANZA YAMEKWISHA KUPITA (Ufunuo 21:1-8)

  Kuna siku ya kukutana na huyu Mungu….Ipo siku hakika…! Lakini kwa Wakristo sio siku ya kutisha…..Ni siku ambayo Mungu atafuta machozi tuliyolia kwa yale yaliyotupa katika maisha haya ya kitambo….! Machozi ya kila aina…….kwa wengine waliishi maisha haya kwa kuhangaika……bila kuwa na kazi zenye kipato cha kutosha……..bila kuwa na makazi mazuri……… mshahara kufika wiki ya pili ni muujiza…!wengine bila kuwa na wenzi….wamelia mchana na usiku…..lakini hawamkupata wa mwenzi wa kumpa furaha na kuishi naye katika maisha haya ya kitambo……wengine kukosa watoto…….wengine ni machozi ya ndoa ambazo zimegeuka kuwa mwiba mchungu na wa maumivu mazito…lakini wakaishikila Imani…….wengine ni machozi kwa ajili watoto walioasi wazazi…..au wamekataa kuipokea Imani…….au kwa wengine ni vilio vya kuonewa makazini….kwa ajili tu ya kumuisha Kristo……Kwa kifupi Mungu atafuta kila CHOZI…..!

  Sina haja ya kuandika maombelezo…….maumivu……Mungu anasema kuna siku yatakwisha….!

  Kwa kifupi wapendwa uko mji tuliondaliwa, huo ndio wa kuungalia na kuutafakari………nakumbuka maneno machache katika ule wimbo katika nyimbo za Injili…….

  “Hapa chini sio kwetu……tushikwe na dunia na dhambi kutulemea……tutupe ya chini pia….”

  Mungu na Awabariki…

 10. WAFU WAFAO KATIKA BWANA WAKO WAPI KWA SASA.

  Baada ya kusoma somo hili inaonekana kwamba mwalimu wa somo amefundisha kwamba watu wote waliofariki katika Bwana wako Mbinguni.

  Hii ameisema katika moja ya aya za somo hili nanukuu, “Mtu anayeishi maisha yaliyo mbali na dhambi, anapokufa, roho yake humiminwa katika mwili mwingine wa roho unaoitwa mwili wa mbinguni, kama mafuta yaliyo katika chombo kibovu kinachovuja, yanavyoweza kumiminwa katika chombo kingine kilicho kizuri”

  Swali: Je, Watu wote waliokufa katika Bwana wako Mbinguni? Kama jibu ni ndiyo huo mji wa mbinguni unaoandaliwa, unaandaliwa vipi wakati watu tayari wanaingia kila siku kwa njia ya kifo? Yesu anapoandaa mji huo mtakatifu wale walikwishakufa wanamsaidia kuandaa au wako tu mahali wakimtazama anavyochakalika na ujenzi?

  Kama wafu wako mjni Yerusalem au tuseme mbinguni, unyakuo wa kanisa utafanyikaje kwani tunaambiwa kwamba wafu watanyanyuka toka makaburini na kuungana na watakaokuwa hai wakati huo? Au watashuka toka mbinguni na kuingia makaburini ili waanze kufufuka tena?

  Kama waliokufa wako mbinguni aliko Mungu yaani mbingu ya Tatu, kazi zao za kila siku ni zipi ukiacha kuimba na kusifu?

  Maandiko mengine yanasema, kuna kipindi kimesemwa katika UFUNUO: Bahari na Kuzimu vikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wengine wakahukumiwa kwa kadri ya matendo yao.

  SWALI LINGINE: Hivi tunaposema Mbinguni ni Juu huwa tunachukua kigezo kipi? Tunasema Mbinguni ni Juu kwa sababu Yesu alipaa juu au kwa sababu imethibitika kwamba Mbinguni ni Juu. Hivi mtu akiwa kule mwezini au kwenye sayari yoyote anapotaka kuonesha Juu atasonta kidole kwenda wapi? Nadhani watu wakiwa mwezini dunia huwa inaonekana kuwa juu yao. Hapo watasema mbingu ya kwanza kwao ni wapi?

  Mimi nadhani tuondokane na mawazo mgando kama ya kanisa la kwanza lililoamini kwamba dunia ilikuwa kama meza na siyo mduara kama tufe au yai hadi wanasayansi walipothibitisha kanisa likaonekana lilifuata nadharia za ujinga.

  Mbinguni kwa mtazamo wangu siyo katika anga hili linaloonekana wala lile lisiloonekana kwa macho yaani kwa sababu ya umbali wa mamilioni ya maili.

  Mbinguni kunakosemwa na maandiko mimi naamini kuwa ni ulimwengu mwingine kabisa (It is another spiritual world that can not be seen by physical ayes). Ni ulimwengu ambao hauna uhusiano na huu ulioundwa na nyota na sayari. Hapo juu tunapopaona ni anga tu (It is just a space or vacuum with stars and planets rotating on their axises).

  Nategemea kupata majibu ya maswali yangu kutoka kwa mtoa mada au wachangiaji wengine.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s