Kwenye wakati mgumu utatoa kikumi?

Kuna wakati wa matatizo wapendwa, wakati una mgonjwa, huna kodi ya nyumba na madeni ya shule. Na wakati huo huo kanisani unasubiriwa utoe fungu la kumi kama ilivyo kawaida. Je utatoa? kama tulivyowahi kujadili hapo nyuma kuhusu fungu la kumi na wengi kusema ni Agizo tutoe. Je wakati wa mapito magumu kiuchumi, unatoa pia?

Advertisements

18 thoughts on “Kwenye wakati mgumu utatoa kikumi?

 1. Kuna swali linawasumbua sana watu wengi ikiwa ni pamoja na wakristo wenyewe pia, nala ni hili:

  “kwa nini wakristo wengi leo ni masikini sana yawezekana ikiwa ni pamoja na wewe, pamoja na ahadi kedekedi za Mungu za kuwabariki?”

  Jibu langu mimi ni hili: wakristo wengi ni masikini kwa sababu ya laana ya kutoa fungu la kumi.

  Nimesema laana ya kutoa fungu la kumi wala si ya kutotoa fungu la kumi, soma vizuri.

  Wakristo wengi wanatoa zake kwa manung’uniko makubwa sana maana ni kongwa zito. Na wengi wamelaaniwa kwa sababu wanatoa hiyo zaka kwa kumnung’unikia Mungu. Mungu anapenda anayetoa kwa moyo wa kupenda. Na wengi wako radhi kukuacha ufe na njaa kuliko kukununulia chakula pesa ambayo wanaenda kutoa kwa wachungaji wao kama zaka.

  Zaka ni miradi ya wachungaji tu, ndio maana lazima ujisajili kwenye daftari ili wakufuatilie vizuri.Ati zaka mpaka niandike jina,lol, kwani Mungu halijui jina langu!!

  -Zaka haijawahi kuwa fedha hata siku moja,fuatilia sheria ya zaka.

  -Zaka ilitolewa kwa walawi maana ndio walikuwa makuhani. Na ni kwa sababu hawakuwa na urithi wa ardhi. Lakini leo ukuhani umehamia kwa wayuda ambao wana urithi wa ardhi,sasa sijui zaka anakula nani.

  -uliyesema zaka ilianza kabla ya sheria umepatia. Kwa maana hiyo zaka hiari maana Ibrahim alitoa kwa hiari wala si Mungu aliyemwambia, Yakobo pia alitoa kwa hiari tena kama nadhili wala si Mungu aliyemwambia

  – wewe unayesema kuwa Mungua alikushughulikia ulipoacha kutoa zaka uko sawa, kwa sababu uliacha kutoa nadhili ambayo kwa hiari yako umejifunga nayo.

  Watu wengi hawajui nini maana ya Agano Jipya. Wanadhani tu ni biblia ilikuwa inaendelea kuandikwa. Nashukuru Mr. Milinga umejaribu kufafanua. Hawajui kuwa torati ni laana na ilikuwa ni kivuli tu cha mambo halisi ambayo ndio Neema.

  Siku moja mch. wangu alisema kuwa kuna kanisa moja Wingereza hawatoi zaka, lakini ndio kanisa tajiri kuliko yote Wingereza, lakini akasema hata yeye hajui ni kwa nini ndio kanisa tajiri. Mimi ninajua ni kwa nini.

  Yesu alisema “wapeni watu vitu nanyi mtapewa….. Luk 6:38. Wala hakusema mpeni Mungu vitu nanyi mtapewa. Mungu hahitaji pesa yako, wala kitu chochote cha kwako,maana vyote ni vyake.

  Kutoa zaka sio kitu kibaya lakini sio lazima. Na wengi inawatesa kwa sababu tu ya neno “ni lazima” siku watu wakiambiwa ukweli kwamba zaka ni hiari watatoa sana. Palipo sheria ndipo palipo dhambi.

  Mnaotoa zaka hebu niambieni kisheria zaka anatakiwa kuliwa nani, na je wachungaji wanaigawanya kama biblia inavyoagiza?

  Halaf naomba mnaotoa zaka msome vizuri zaka ilivyokuwa inatolewa muone kama na ninyi mnaitoa kwa usahihi wake. Sio tu kwenda kwa mapokeo.

  Vipi, ukipewa zawadi ya gari moja zaka yake ni nini?

 2. Wapendwa Mabinza na Shinja,

  Nashukuru kwa maoni na maswali yenu. Nashukuru kwa kusoma maoni yangu na kutaka ufafanuzi zaidi.

  Watu wengi husoma Mathayo 5:17-18 lakini huwa wanashindwa kuelewa maana ya maandiko hayo.

  Naomba niyanukuu tena, ” 17“Msidhani kwamba nimekuja kuondoa Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza. 18Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia” Biblia ya Kiswahili cha kisasa.

  Katika maandiko haya, watu wengi huwa hawasomi kwa kina maneno ya mwisho yasemayo,”………..Hadi hayo yote yatakapotimia……”

  Yesu anaposema hakuja kutangua Torati wala Manabii bali kutimiliza alimaanisha kwamba YALE YOTE YALIYONENWA NA MANABII NA TORATI hangeyabadilisha hata nukuta moja mpaka nyakati zitimie. Nyakati zilipotimia YESU ALIBATILISHA TORATI NA SHERIA ZA AGANO LA KALE ZIKAWA HAZITENDI KAZI TENA.

  Kwa wakaati ule akiwa hapa duniani hangeweza kuitangua Torati wala maagizo ya Manabii na Makuhani.

  Ukitaka kuelewa kwamba huo ndio ukweli wa Mathayo 5:17-18 JIULIZE ni mambo mangapi yaliyotanguliwa na Yesu ambayo leo hii hayafanywi ili mwanadam ahesabiwe haki mbele za Mungu. Yapo mengi sana. Nimeyataja katika post yangu ya awali. Hebu yasome tena.

  Siyo kweli hata kidogo kwamba Yesu alimaanisha kwamba Torati iendelee kuwa ndiyo mwongozo wa maisha ya kiroho kwa wafuasi wake wa Agaano Jipya. Miongozo yote ya maisha ya kiroho ya Agano la Kale yaliandikwa ili kutufundisha mifano. Ni kivuli tu. Hatutawaliwi na Torati ya Musa tena.

  Nikupe Mfano mmoja tu, Je, leo hii wakristo ni lazima watahiriwe govi zao ili kuhesabiwa haki mbele za Mungu? Torati ilikuwa inaagiza hilo kama sharti la kuhesabiwa haaki kwa Mungu. Je, hapaa Yesu alitangua Torati au bado?

  Nikupe Mfano wa mwisho, Je wakristo ili wasamehewe wanalazimika kutoa kafaraa ya mbuzi au ng’ombe kwa kuhani mkuu? Zamani za Torati ilikuwa lazima. Leo hii, kafara ya Yesu Kristo ilimaliza yote hayo. Huku ndiko kutimilizwa kwa torati na Manabii anakokusema Yesu. Kutimiliza maana yake ni kukamilsha (Fulfillment) yaliyokuwa yametabiriwa au kunenwa na Manabii na torati.

  Sadaka aina zote za Agano la Kale ikiwemo zaka, vilikoma pale Yesu alipopaa Mbinguni na kumleta Roho Mtakatifu. Ndipo Agano la Kale linapoishia mipaka yake. Katika Agano Jipya tuna mwongozo Mpya wa jinsi ya kumtolea Mungu yaani , MOYO WA HIARI, SADAKA ZA UPENDO, SADAKA KWA YATIMA, SADAKA ZA WAJANE, HIARI, HIARI, HIARI………… MOYO MKUNJUFU.

  Kumbuka utoaji wa ZZAKA huwa siyo hiari wala kupenda kama ilivyokuwa enzi za Torati na manabii. Ndiyo maana nasema Utoaji wa zaka ni utaratibu uliotimilizwa (amended laws) wakati wa enzi za Yesu.

  Karibuni kwa maswali zaidi.

 3. Fungu la kumi ni agizo la Mungu na Yesu anasema hakuja kutangua torati (shera) ila kutimiliza. Asomaye na afahamu!!!!!

 4. Bwana Yesu asifiwe.
  Naomba samahani kama nitawarudisha nyuma. Maelezo ya Ndg. Yangu Obed Milinga, yamenivuta kuuliza ili nami nijue yafuatayo:
   Nijuavyo, Biblia imegawanyika katika sehemu kuu mbili, Agano la kale na Agano jipya (Injili) Nyote hiyo ndilo Neno la Mungu na kwamba haikinzani (hijipingi), vilevile kila Neno lilomo humo imeagizwa lisipunguzwe wala kuongezwa, na kwamba limeandikwa kwa uweza wa Roho mtakatifu ili lifae kwa mafundisho! Kama naelewa sawasawa, Ndg. Yetu Obedi katika swala la Zaka, unasimamia kifungu gani kinachosema waziwazi kuwa Zaka ili wahusu watu wa Agano la kale tu na si wewe unayejifunza kwa kupitia Injili ya Paulo?

   Najua Paulo alikuwa mtume na mjumbe wa Yesu kristo, alichokifanya ni wazi alitenda kwa uongozi wa Yesu mwenyewe, iwapo yesu alikuta watu wakitoa Zaka kwa mjibu wa torati, na Yesu alipata kusema ”…….mimi sikuja kutangua torati ila kuitimiliza….na sehemu nyingine anasema ….hata nukta moja ya Torati haitaondoshwa” Je, kwa Mstari upi wa Biblia unaniweka sawa niamini kuwa, Paulo kwa mafundisho yake anathibitisha kuwa, kutotoa Zaka ni sawa na kwamba, HUJAONDOSHA SEHEMU YA TORATI NA HIVYO UNASAIDIANA NA BWANA YESU KUITIMILIZA? Kwasasa ni hayo tu nisaidie Ndugu yangu. Mbalikiwe wote!

 5. Ndugu milinga.
  si kweli kwamba wahubiri wengi wanawatisha watu wasipotoa watapata mikosi.neno lenyewe limeweka bayana kuwa watu wakitoa zaka na sadaka Mungu atamkemea alaya,kama hutatoa yule alaye ataharibu.

  kwamba mambo ya zaka kwenye agano jipya hayajasisitizwa si sawa Yesu aliwaambia wayahudi kwamba mnatoa zaka za mnanaa na mchicha na kuyaacha mambo ya adili,akamalizia kuwa mlipaswa kuanza na hayo bila kuyaacha ya kwanza(yaani zile zaka).pia zaka ilianza kutolewa kabla ya torati ya musa pale yakobo alipomwambia Bwana wakati anamkimbia nduye Esau kuwa ukinifanikisha ktkt safari yangu nami nitakutolea fungu la kumi.

  kwamba Mungu ni mwema kwa watu wote ni kweli lakini Mungu toka zamani aliweka utaratibu kwa watu wanaomcha ndiyo maana hata sasa anaagiza tusienende kama mataifa tukijaribu kuiga tunatenda dhambi.hao unaoona hawamchi Mungu nao hutoa sadaka zao kwa miungu au waganga japo wapo wengine wasiotoa kokote.

 6. sikiliza, nyakati ngumu haziishi, mungu amesema mnijaribu kwa kuleta sadaka zenu ili muone kama sitawabariki na kufungua madirisha ya mbinguni.Hivyo kwa wakati wowote unaoona wewe ni mgumu wewe kuwa mwaminifu kwa upande wako na umkumbushe na haja zako katika roho na kweli uone kama hutabarikiwa.,

 7. TUSICHANGANYE AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA.

  Wahubiri wengi wamekuwa wakikimbilia kufundisha kanisa kwamba watoe zaka ndipo watabarikiwa na kuepuka mikosi, laana na magonjwa. Hapa hakuna ukweli kabisa. Huu ni upotoshaji kwani Mungu huwapa mema wamchao na wasiomcha. Huwapa mvua waovu na wema. Huwawashia Jua wampendao na wasiompenda. Hutajirisha wote bila kujali nani anamcha au nani hamchi.

  Mungu hana upendeleo. Hili wahubiri huwa wanalisahau. Wengi huhubiri ujumbe wa vitisho badala ya ujumbe wa upendo. Wahubiri wengi wanadhania wasipoweka vitisho katika mahubiri yao watu hawataitikia wito wa kwenda mbele kutubu au kutoa sadaka na zaka.

  Imegundulika kwamba, wahubiri wengi na wafuasi wao hushindwa kuelewa maana ya Agano Jipya na Agano la Kale. Wanashindwa kuelewa mipaka ya Agano Jipya ni ipi na Agano la Kale ni ipi?

  Yapo maswala makanisa yote tunakubaliana. Maswala yafuatayo tunakubaliana kwamba yamepitwa na wakati; yaani yaliishia enzi za Agano la Kale, nayo ni:

  1. Kutoa mbuzi, ng’ombe, njiwa au kondoo achinjwe ndipo usamehewe dhambi.

  2. Tohara kwa wanaume ili wahesabiwe haki na Mungu. Swala hili wakristo wote hakuna wanaolisisitiza kama swala la muhimu ili wapate Uzima wa milele na Baraka ya Ibraahimu aliyekuwa wa kwanza kukubali kutahiriwa kwa Imaani.

  3. Ulazima wa kupumzika siku ya Sabato (Jumamosi) imepitwa na wakati. Wote tunakubaliana.

  4. Kizuizi cha kutokula baadhi ya vyakula vitokanavyo na wanyama, mimea, au viumbe wa bahaharini. Mfano: Wakristo wote (ukiacha wasabato) wanakubali kwamba kula nyama ya nguruwe ni HALALI KIBIBLIA pamoja na kwamba Maandiko mengi ya Agano la Kale yamekataa kabisa. Agano la Kale liliwakataza watu kula nyama ya Nguruwe, sungura, kumbikumbi, samaki-kambale, nk. Maandiko yamesisitiza sana lakini wakristo wanakula tena kwa kujifariji kuwa “Kila kitu Yesu Kristo alikitakasa” ingawa hawakubali kwamba basi hata BIA au POMBE ilitakaswa na Yesu.

  5. Agano la Kale lilikataza wanaume kunyoa ndevu ili kuwatofautisha wao na wanawake. Kwamba kama mwanaume atanyoa ndevu hapangekuwa na njia ya kumtofautisha na mwanamke katika jamii. Lakini leo hii, wakristo hawasisitizi kwamba ni kosa kunyoa ndevu.

  6. Mwanamke akijifungua mtoto wa kike alipaswa kufichwa chumbani kwa zaidi ya siku 60 bila kugusana na mtu yeyote wala kwenda katika Ibada au makusanyiko ya watu wengi. Aidha, Mwanamke pia akiwa kwenye HEDHI hakutakiwa kusalimiana na mtu yeyote hadi atoke katika Hedhi yake.

  7. Kuoa wanawake wengi iliruhusiwa kabisa katika Agano la Kale. Ibrahimu alioa zaidi ya mke Mmoja, lakini hadi leo anaitwa Rafiki wa Mungu. Je, Mkristo leo akioa wanawake 2 ataitwa rafiki wa Mungu? Suleimani, Daudi, nk walioa zaidi ya mke mmoja.

  8. Kutoa talaka ilihalalishwa enzi za AK (Agano la Kale). Watu waliweza kutoa talaka bila wasiwasi.

  9. Makuhani hawakuruhusiwa kumiliki ardhi wala mali yoyote ya urithi.

  10. Waisraeli wote waliamriwa kutokuoana na watu wa makabila tofauti na wao. Ukioa Kabila tofauti na la kwako ulipewa adhabu au ungetengwa na jamii yote.

  Hayo na mengine mengi yalikuwa HALALI ENZI ZA AGANO LA KALE. Yaliandikwa ili kutufundisha sisi wa Agano Jipya wenzetu walivyoishi na kumwabudu Mungu. Yaliandikwa siyo yawe AMRI au MAAGIZO kwa vizazi vyote.

  Linapokuja swala la kutoa zaka, wahubiri wengi husahau kwamba hatupo tena chini ya Maagizo yaliyokuwepo enzi za TORATI YA MUSA.

  Wahubiri wengi wamesahau kwamba tuko chini ya TORATI YA YESU KRISTO.

  TORATI HIZI MBILI kila moja ina miongozo na mashaarti yake.

  Watu wengi hudhania kwamba kwa kuwa maandiko ya Agano la Kale (AK) na Agano Jipya(AJ) yamewekwa pamoja na kuwa kama kitabu kimoja chenye maandiko matakatifu basi kila kitu kinapaswa kutekelezwa na watu wote wa tangu AK na wale wa AJ.

  Napenda kutumia mfano huu wa Noti ya fedha za Tanzania. Kuna noti zile za zamani wakati wa Nyerere au Mzee Mwinyi. Noti zile za miaka ya 1980 au zile za miaka ya 1990 ukizitazama bado utakutana na maandishi yasemayo: “FEDHA HALALI KWA MALIPO YA SHILINGI ELFU MBILI”. Swali. Ukitembea na noti hiyo ya mwaka 1980 pamoja na kwamba imeandikwa maneno hayo utaitumia kununua bidhaa sokoni?

  Ukweli utabaki kwamba, Maandiko ya Agano la Kale yapo ili kutupa picha ya jinsi wenztu walivyoishi na kumwabudu Mungu.

  Katika Agano Jipya, maswala yote yahusuyo: NDOA, MAVAZI, IBADA, FEDHA, SADAKA, INJILI, PEPONI, KUZIMU, MALAIKA, ROHO MT. MAZINGIRA, SIASA, UCHUMI, KILIMO, UFUGAJI, UVUVI, NYOTA, ANGA, UNAJIMU, nk. tunapaswa kuwafuata Mitume wa Yesu kama nao walivyomfuata.

  Unaposoma Biblia unapaswa kuelewa kwamba umeshika kitabu chenye kueleza matukio na maagizo kwa nyakati mbili tofauti yaani Enzi za Musa na Enzi za YESU.

  Unapaswa kuchagua kufuata maagizo ya Musa na Manabii waliomfuatia au Ufuate maagizo ya YESU na Mitume wake walioagizwa kusambaa ulimwenguni kote kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu na siyo wanafunzi wa Musa.

  Wapendwa na wahubiri wanaosisitiza kwamba kutoa zaka ni lazima yaani ni amri, au ni kodi ya Mungu, nk hawana tofauti na wasabato wanaosisitiza kwamba ni lazima katika Agano Jipya kuitii siku ya sabato na kuiadhimisha kwa kusali siku hiyo (jumamosi).

  Kama unadhani kutoa ZAKA ni agizo la lazima kwa nyakati za AJ, basi hata KUTOKULA NYAMA YA NGURUWE, KAMBALE na KUMBIKUMBI ni agizo halali hadi sasa 2012.
  Wakristo hawapaswi kujitetea. Wanapaswa waache kula kabisa nyama ya nguruwe kwani nalo ni andiko lililomo kwenye Biblia hiyo hiyo tunayoitumia kulazimisha watu watoe zaka wapende wasipende.

  Wapendwa wanasahau hata msemo wa kiswahili usemao, “KUTOA NI MOYO SIYO UTAJIRI”. Mtume Paulo alilisitiza kanuni hii ya kuwataka wapendwa watoe kwa moyo mkunjufu, kwa hiari, kwa kupenda, kwa dhamiri safi, kwa kiwango chochote, nk.

  Hata Yesu alilisisitiza hilo, aliposema, “….wapeni watu vitu nanyi mtapewa. Kipimo kile kile mtakachopima ndicho watakachowapimia na kujaza hadi kusukwasukwa……”

  Mungu hapendi sadaka zilizotolewa kwa vipimo vya asilmia ya mapato. Mungu anataka utoe kulingana na moyo wako ulivyopenda, ulivyodhamiria, ulivyokusudia moyoni, unavyotaka wewe (mchungaji apendavyo, au hata Mungu apendavyo) yaani wewe mwenywewe unatakaje kumtolea Mungu?

  Napenda kumalizia kwamba, hata kama wewe hutoi chochote kanisani bado Mungu anakupenda na atakulinda na mabaya yote. Kutoa sadaka hakupaswi kugeuzwa kuwa kama hirizi au ushirikina fulani ambao ukiufanya unapata ulinzi au utajiri. Kuna watu wanadhani usipotoa zaka hutabarikiwa na Mungu kwa hiyo wanajitahidi kujaribu kumhonga Mungu ili eti afungulie madirisha ya baraka kutoka pande zote nne za dunia.

  Kumbuka “UPENDO WA MUNGU HAUNA MASHARTI” Mungu anakupenda jinsi ulivyo. Mungu anawapenda watu wooooote ila hapendi DHAMBI. Kumbuka kuwa DHAMBI ni kitu kingine na BINADAMU ni Kiumbe kingine tofauti. Mungu hampendi Mtu kwa sababu eti anatoa zaka au sadaka.

  Nitaendelea kuwafuata na kuwaiga mitume wa Yesu kama wao wenyewe walivyomfuata na kumwiga. Mtume Paulo atakuwa ndiye atakuwa mtu wa juu kabisa kumwiga katika maswala yote yahusuyo kumtolea Mungu sadaka (Apostle Paul will remain my sole role model in all issues of offerings). Kwa kuwa Mt. Paulo hakutoa zaka hata mimi sitatoa zaka.

 8. BWANA asifiwe!Kama ilivyo agizwa haikusemwa wakati wa neema au wakati wa ugumu kutoa nilazima rejea MALAKI yote inasisitiza,na utaona jinsi unavyojaribu kukwepa kutoa fungu la kumi ndivyo unavyozidi kuwana matatizo mmoja baada ya lingine maana ile ahadi ya kukemewa yule alaye haiko upandewako!kwahiyo kama ilivyo amriwa wetoa usiji fariji kwakujiweka ktk halingumu zaidi!mwovu sikuzote atakufariji kwa mbinu mbali mbali iliusitoe aku pige kila kona kiuchumi!
  Barikiwa kwajinsi utakavyo endelea kumtolea BWANA maana vyote nimali yake!.
  Frederick Marandu

 9. Emen, nakubaliana na ndugu Milinga na Orbi. Tunaona ktk kanisa la kwanza walikuwa ni watoaji wa kiwango cha juu sana kilichozidi hata fungu la kumi! Maana wengine waliuza vitu vyao vyote na pia walishirikiana kwa kadiri ya kila mtu alivyohitaji. Angalia Matendo sura ya 2:42-47 , na Matendo 4:32,

 10. Ndugu John Bethania…..

  Nadhani mafundisho yako ni njia mbaya mno ya kufundisha utoaji wa fungu la Kumi……Hivyo ni vitisho ambavyo havisimami katika Maandiko……Je kama kuna mapigo hayo kwa kutotoa fungu la Kumi utasemaje sasa juu ya mapigo kwa wale ambao hawamjui Mungu…?Mbona mara nyingi tunaona wema wa Mungu unawavuta watubu….? Mbona watu wengi leo wangelikuwa kwenye vilio na mateso…? Mungu wetu ni Mungu anayeleta mvua kwa wanaomjua na wasiomjua…….!

  Tunamtolea Mungu kwa kuwa tunampenda….tunamtolea Mungu kwa vile ametundea Makuu katika maisha haya….la msingi kwa Njia ya Yesu Kristo ameurudisha uhusiano wetu uliovunjika kwa ajili ya dhambi…..msukumo huu hufanya tumtolee Mungu….si kwa ajili ya baraka…..mafanikio…..kuponya magonjwa nk……!

  Msimamo wangu ni kuwa kama Jamii ya Israel ilimtolea Mungu fungu la kumi…….sisi ni zaidi ya Israel……..hatuna sheria….kila kitu kwetu ni mali ya Mungu……..zaidi ya fungu la kumi….hatuna mipaka ya utoaji……….wala hatusukumwi na mapigo….na vitisho…….

 11. Kama Fungu la Kumi lingekuwa agizo la Kristo kwa wanafunzi wake au katika Agano Jipya, ni matumaini yangu kuwa Mtume Paulo, Petro, Yohana, Yakobo na wengineo walioandika nyaraka wangesisitiza sana.

  Kama utanisomea andiko la Agano Jipya (Acha Agano la Kale) linalowaagiza wanafunzi au kanisa la kwanza kutoa fungu la kumi, basi mimi kuanzia kesho nitatoa.

  Wapendwa wengi wanashindwa kuelewa kwamba kuna tofauti ya fungu la kumi na Sadaka za hiari. Agano Jipya halina kipengere hata kimoja cha kutoa sadaka za lazima.

  Mtume Paulo pamoja na kufundisha Mada nyingi sana kwa kurejea maandiko ya Agano la Kale hakuna hata siku moja aliwahi kufundisha waumini au wafuasi wake watoe zaka. HAKUNA. Petro Mtume naye hivyo hivyo. Hakuna siku alifundisha au aliandika katika nyaraka zake NENO ZAKA.

  Kama kweli zaka ingekuwa inapaswa kuendelezwa katika Agano hili Jipya, nina uhakika Paulo Mtume asingeacha kuzungumzia swala la aina hiyo ya sadaka yaani Zaka.

  Tafuta nyaraka zote za Paulo, hakuna neno zaka wala fungu la kumi.

  Mimi namwiga na kumfuata Paulo Mtume kama alivyomfuata Kristo. Wewe Je?

 12. FUNGU LA KUMI KTK AGANO JIPYA HAKUNA BALI KUNA KUMTOLEA MUNGU SADAKA KWA MOYO MKUNJUFU 2WAKORTO 9:6-8 BARIKIWA SANA

 13. Fungu la kumi ni kodi ambayo ni lazima tumlipe Mungu kila tunapopata mapato yoyote yale iwe zawadi, lunch, nguo, nk. Kama vile usipolipa kodi ya serikali unashitakiwa ndivyo na wewe utakavyoshitawa na mshitaki wetu (shetani) kwa Mungu. Na kama vile unavyoadhibiwa na serikali kwa sababu ya kosa la kutolipa kodi ndivyo na Mungu atakavyokuadhibu. Watu wengi sana wana magonjwa, shida mbalimbali za kifamilia na kiuchumi sababu ya kula mafungu ya kumi. Kusema kweli Yeye Mungu haelewi juu ya hali yako mbaya anachotaka toa kodi yake hata kama ni sh 50/= tena kwa wakati usijaribu kumkopa Mungu utaadhibiwa.

 14. Mpendwa Bwana Yesu asifiwe!
  Kutoa fungu la kumi ni agizo kutoka kwa Mungu mwenyewe hivyo tunatakiwa tuwe waaminifu katika hilo. Mpendwa Mungu wetu sio dhalimu akaagiza utoe kitu ambacho hauwetuzi. Mungu anatuwazia mema na hufungua milango kwa kila amtegemeaye. Ukiwa mwaminifu katika kutoa fungu la kumi, Mungu hatakupungukia na kumbuka kuwa neno la Mungu halitarudi bure. Kwa Mtu aliyeokoka kukata tamaa ni dhambi.Hivyo ndugu yangu mtegemee Mungu kwa kila jambo na uwe mwaminifu katika kutoa fungu la kumi.

 15. Bwana yesu asifiwe, mimi huwa nashindwa kufanya mahesabu vizuri ya kiasi cha kumtolea mungu fungu la kumi, ninatoa lakini sina huwakika km kwel namtolea ipasavyo, lengo langu ni kumtolea sawasawa na nisimpunje kwa sababu naamin hata hiki nikipatacho kinatoka kwake, Naomba sana mnisaidie kwa hilo,
  Mfano mimi napata mshahara wangu Tsh laki mbili kwa mwezi sadaka ninayopaswa kumtolea ni sh ngapi?

  Mungu awaongoze vyema, Amen

 16. Abrahamu alipoinua kisu ili amtoe Isaka sadaka, alikuwa mzee na mkewe pia, hapa ilikuwa ni mtihani mkubwa. Hakuwa na tumaini la kuishi na kupata tena mwingine na hivyo ni kama kufutika ukoo wake, lakini kwa Imani kubwa aliyokuwa nayo alitoa. Tutoe tu wapendwa kama walivyosema hapo juu hata mie nimeishakutana na mitihani hiyo na kujaribu kumkopa Mungu na kuona matokeo yake. Hakikisha kama umeshindwa kabisa mara upatapo toa na sio kuanza visingizio. Tukumbuke Yeye Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri (Kumbukumbu la Torati 8: 1-18). Mbarikiwe sana

 17. Kwa kweli mtihani huo umeshanipata, najikuta namkopa Mungu, lakini wapendwa hailipi, mimi sitaki kabisa tabia hii ya kumkopa Mungu, vyema kutoa na mengine yatajitatua. Mungu kwanza mengine yanafuata.

 18. Mimi ukweli ni kwamba ntatoa hata kama uchumi ni mbaya.Nimeshapata madhara ya kutotoa fungu la kumi.Unajua fungu la kumi,linakufungulia madirisha ya mbinguni.Yaani,linasababisha upate mlango wa kutokea incase,umekumbwa na matatizo.
  Ina maana,ukiwa na matatizo na kushindwa kutoa fungu la kumi,utashangaa na hizo pesa unazobana ili zikusaidie badala ya fungu la kumi,hazitoshi au hazikusaidii chochote.
  Mi ntawashauri wapendwa kutoa fungu la kumi kila wapatapo ela.Wataona maisha yao hayawi na ugumu wowote.Maana,kila uombacho utapewa haraka kwakuwa,Mungu huwajali sana wanaomtii.Mbarikiwe!.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s