Askofu asimamisha mvua kwa muda Jijini Mbeya!

Moja ya miujiza mikuu iliyoshangaza maelfu ya watu waliohudhuria katika mkutano wa injili wa huduma ya Overcomers Power Center (OPC) na Kanisa la End Time Harvest inayoongozwa na Askofu Boaz Sollo, ni neno la Mungu la Mamlaka alilotoa kwa kuiamuru mvua isinyeshe hadi mkutano huo ulipomalizika.

Mkutano huo ulifanyika hivi karibuni katika viwanja vya Uhasibu Jijini Mbeya na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jiji hilo na mikoa ya pembezoni. Jioni ya siku ya pili ya mkutano huo wakati washiriki wake wakijiandaa kutoa sadaka, mvua kubwa ilianza kunyesha, ambapo Askofu Boaz alilazimika kusimama na kuiamuru isimame hadi mkutano huo umalizike; jambo ambalo lilitekelezeka na watu waliokuwa wameanza kukimbia wakarudi na kuendelea na mkutano.

–WAPO RADIO

Advertisements

5 thoughts on “Askofu asimamisha mvua kwa muda Jijini Mbeya!

  1. Kama wachawi wanaweza kufunga mvua kwanini watumishi wa Mungu washindwe kusimamisha mvua wakati aliye ndani ya watumishi wa Mungu ni Mkuu kuliko aliye ndani ya wachawi

  2. KAMA YESU ALIVYO SEMA TUKIMWAMINI
    KAZI ALIZOFANYA SISI TUTAFANYA NAM NAKUBWA KULIKO HIZI KWA NEEMA YAKE
    TUTAFANYA.

  3. Suala ni kuamini au kutotilia mashaka kuwa Mungu yupo na Mungu huwasikia watumishi wake kwa ajili ya Utukufu wake. Kila jambo linatendeka kwa ajili ya Utukufu wa Mungu, binadamu yeyote asije akajisifu. Hata wewe kama umepatanishwa na Mungu kwa njia ya kumpokea Yesu Kristo miujiza yaweza kuambatana nawe kwa mapenzi ya Mungu. Kazi kwenu kutafuta maandiko.

  4. Lipo jina leye nguvu na mamlaka liwezeshalo yote ikiwa alitumiaye anaamini katika roho na kweli.YESU.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s