Naomba kujua uhusiano kati ya Israel na Kurudi kwa Bwana Yesu!

BWANA YESU ASIFIWE, naomba mnielekeze uhusiano uliopo baina ya Israel na kurudi kwa YESU mara ya pili na uhusiano mbaya uliopo baina ya Israel na Iran? Pia naomba kujua Asili ya vita vya Palestina na Israel. Mungu awabariki!

Peter Juma

Advertisements

19 thoughts on “Naomba kujua uhusiano kati ya Israel na Kurudi kwa Bwana Yesu!

 1. HISTORIA YA KANISA LA MUNGU ALIYE HAI NI YA KUTISHA MNO!Kwa sasa inawasogeza wateule wa Yesu karibu sana na UNYAKUO pengine kuliko wakati mwingine wowote.Historia ya wana wa Mungu aliye hai ambao waliitwa kwa kusudi lake yaani ISRAELI ambayo inajumuhisha wayahudi,wasamaria na watu wa mataifa
  inatupa PICHA HALISI ya kile kinachoendelea duniani kwa sasa na namna ambayo
  MFUMO HUU WA MAMBO UTAKAVYOMALIZIKA.

  Tunapofuatilia historia hii KWA MACHO NA MASIKIO YA ROHONI yaani tukiwa chini
  ya uongozi wa ROHO MTAKATIFU ndani ya maandiko matakatifu yaani BIBILIA ndipo tunapoona DHAHIRI TENA BILA SHAKA YOYOTE KUWA MWISHO WA MAMBO SI TU KWAMBA UMEKARIBIA SANA LAKINI UMEKUWA HALISI NA WAKUTISHA MNO MIOYONI MWETU.KWA KUWA INJILI YA UNYENYEKEVU WA YESU INAENDELEA KUHUBIRIWA KWA KASI YA AJABU KATIKA ULIMWENGU WOTE NA KUWA USHUHUDA KWA MATAIFA YOTE NI WAZI KWAMBA MUDA WOWOTE KIPENGA CHA MWISHO KITAPULIZWA(Mathayo 24:3-14,Luka 12:2,1 Yohana 2:20,27).NAWAPA HONGERA MBWAMWITU KWA KAZI YAO NZURI YA KUTUSAIDIA KUWAELEZA WATU WENGI ZAIDI HABARI ZA YESU INGAWA WAO WATAONA TU KWA MACHO LAKINI HAWATAKULA.WAO WANASUBIRI KUNYAKULIWA NA SHETANI ILI WAENDE KATAKA UFALME WA GIZA!!!!(Wafilipi 11:17-18,Yuda 1:3-4).

  Nilipokuwa nasoma makala ya shujaa SAM,mifupa na damu yangu ilikuwa inampa
  Roho Mtakatifu ushirikiano ili aongee zaidi na mimi na kuniingiza ndani zaidi ya maelezo ambayo mtumishi SAM ametuandikia.MSUKUMO AMBAO NIMEPEWA KWA NDANI NI KWAMBA WATEULE TUPO UWANJANI TUNACHEZA MPIRA.NI MECHI KATI YA TIMU YA WANYENYEKEVU WA YESU NA WAJUMBE WA SHETANI.TUPO KIPINDI CHA PILI NA DAKIKA NI YA 88 ZIMEBAKI DAKIKA MBILI TU MECHI IMALIZIKE.NI MECHI AMBAYO NI LAZIMA TUSHINDE LAKINI YULE ATAKAYECHEZA VIBAYA,KOCHA AMBAYE NI YESU ATAMTOA NJE ILI AWE MSHABIKI NA KISHA ACHUCHUKULIWE NA SHETANI AMBAYE NI KOCHA WA TIMU YA GIZA.MPAKA SASA TUKO MBELE KWA MABAO 2 NA MBWAMWITU HAWAJAPATA KITU.SISI TULIO KATIKA TIMU YA NURU TUNA FURSA YA KIPEKEE MNO KWASABABU KOCHA WETU PIA NDIYE MFUNGAJI WETU.TUNAPOPEWA MPIRA INABIDI TUTULIZE
  VIZURI NA TUSIWE NA PAPARA ILI WAPINZANI WASIJE WAKAUMILIKI.KOCHA ANATAKA TUPEANE PASI ZA UHAKIKA HUKU TUKIMUANGALIA YEYE KAMA MFUNGAJI ASIYE ZUILIKA.KWA SASA KWA KADIRI PAZI ZINAVYOENDA,MFUNGAJI WETU NAONA AMEJIWEKA SAWA SAWA HUKU AKIWADANGANYA MABEKI TAYARI KWA KUFUNGA GOLI LA TATU ILI KUKAMILISHA UTATU MTAKATIFU……….

  Kwa upande wangu na mimi nipo uwanjani,sichezi na washabiki bali niko makini kuangalia kule mpira unapoelekea.Naona SAM ananipa pasi na mimi naupokea mpira kwa utulivu sana licha ya kwamba nimezungukwa na wachezaji wa timu pinzani.Kwa sasa na mimi nimeamua kutoa pasi makini kwako wewe unayesoma sasa hivi……KAZI KWAKO.Nakutakia utumishi mwema.

 2. Wadau mimi naomba msaada juu ya maana ya mambo haya Nini maana ya seneta neno hili hutumika sana kule marekani Pili wabunge wa mrengo wa kulia na kushoto naomba msaada
  Wanamaanisha nini?

 3. Asanten sana ndugu kwa kunijuza vingi nilivyokuwa sivifaham..MUNGU awabariki sana…

 4. Tunashukuru kwa maelezo mazuri ya kibiblia na historia nje ya biblia, HAKIKA WAKRISTO TUAMKE USINGIZINI

 5. Wapendwa, kwa kadri ya ule mtiririko wa yale maelezo niliyowaletea kuhusu Israeli na uhusiano wake na kuja kwa Kristo, leo napenda nimalizie kile kipande kilicho salia. Basi waweza kuyaunga maelezo haya kwenye kile kipande kilichotangulia, karibu!

  Takribani miaka kumi baadaye, Mataifa ya kiarabu walijikusanya tena ili wawaondoe, hiyo ni 1967: katika kile kilichoitwa Vita ya Muujiza, Israeli iliwadhalilisha maadui wake wa mataifa (gentiles) na ndani ya siku 6 iliudhihirishia ulimwengu kuwa wako nyumbani na kamwe hawaondoki! Kile kilicho shindikana katika miaka ishirini ya bendera yao kuwa juu ya mlingoti ikiwatambulisha kuwa wao ni taifa huru, walikikitimiza ndani ya siku 6, wakaikomboa ardhi yote iliyojulikana kama Palestine pamoja na jiji la YERUSALEMU na kuiteka Sinai kutoka kwa wa Misri!! YERUSALEMU YOTE IKAKOMBOLEWA!!! Luke 21:24 “… Wakati wa mataifa utakapomalizika.” Je, yawezekana kuwa andiko hilo linatutimilia machoni petu???

  Sasa injili ya wokovu iliyotujia si ya milele, bali ni kwa kipindi tu, yaani Mungu akimalizana na sisi anawarudia Israeli kama alivyowaahidi. Basi ni kwa kigezo hicho ndio Israeli kama taifa lina uhusiano mkubwa na kurudi kwa Yesu! Sasa yatupasa kuwa makini kidogo katika jambo hili la kuja kwake. Kulingana na maandiko, yeye anakuja mara tatu. Mara ya kwanza alikuja kulikomboa kanisa. Jambo ambalo limekwisha tukia, pale alipokuja na kusulubiwa. Mara ya pili anakuja kulinyakua kanisa, ile 1Wasetholonike 4:16-17, na mara ya tatu ni yule mwanakondoo aliyegeuka kuwa Simba, sasa akija kwa ajili ya Hukumu! Lakini kanisa linamsubiri kwa ajili ya huko kuja kwa pili ambako ni kwa SIRI, anapolijia kanisa lake alilolikomboa. Jambo ambalo linatamatisha ule Wakati wa Mataifa, yaani Milango ya Neema inafungwa, hakuna wokovu tena kwa yeyote yule wa Mataifa! Mungu aliye Macho na Masikio yetu anatuacha katika kipindi hicho, ule Mzabibu Mwitu, tunakatiliwa mbali kama walivyokatwa Israeli, tunaurudia upofu wetu na ukiziwi wetu, hatuwezi kuelewa chochote tena kuhusu Injili zaidi ya mapokeo yetu. Dini na mambo yote yatendelea kama kawaida. Mahubiri nayo yataendelea na watu wataendelea kudhani wanaokoka bali ile Nguvu ya Wokovu haipo, na hali itaendelea kuwa mbaya kila kunapokucha tukikuendea kule kuja kwa tatu ambako ni kuja kwa pili kwa wale waliokukosa kule kunyakuliwa kwa kanisa. Ndio maana tutashangaa pale tulipotegemea kunyakuliwa badala yake tunaingia katika kundi la kuhukumiwa!

  Basi Israeli inakuwa na uhusiano na kanisa, pale taifa hilo linapokuwa kioo chetu cha kuyatazamia mambo hayo kama yalivyoelezwa katika Maandiko.

  Hebu angalia mambo yanavyokwenda:
  Baada ya ile vita ya siku 6, Waarabu, haswa Wamisri, walijipanga upya na kuendeleza mapigano ya kuvizia katika mfereji wa Suez ili kuilegeza Israeli kinguvu na kuilazimisha kuiachia Sinai. Vita hii iliendelea hadi 1970 bila mafanikio. Misri walijipanga upya chini ya msaada wa Warusi, kwa miaka mitatu wakilijenga jeshi lao upya, ili kuishambulia Israeli katika ‘Full Scale War’

  Basi ilipofika October, 1973, Waarabu walijikusanya tena kwa vita baada ya matayarisho makubwa. Urusi ikiwa imewapa mafunzo thabiti na vifaa vya kisasa ambavyo dunia ilikuwa haivijui kuwepo kwake. Jeshi la Misri lilikuwa kinara wa mafunzo hayo. Urusi ilikuwa na uhakika wa asilimia 100 ya Waarabu kushinda vita hivyo, tena katika muda mfupi, labda katika siku ya pili kama walivyokubaliana: “kukutana Yerusalemu kwa kikombe cha chai!” kwa hiyo safari hii, jordan ilikataa mpaka wake kuwa uwanja wa mapambano bali waliwasaidia kutokea mipaka ya Syria na Misri. Hiyo ilikuwa ni vita ya kuifuta Israeli kutoka ramani ya dunia kwa uhakika kabisa!

  Wamisri waliyaanzisha mapigano wakiwavizia Israeli katika mapumziko ya sikukuu yao ya mwaka mpya. Ulinzi ulikwa duni jeshi la Misri lenye vifaa vya kisasa lilivuka mpaka na kusonga ndani huku majeshi ya Israeli yakirudishwa nyuma kwa kasi. Ndege zao chache walipozirusha hazikurudi! Syria nao wakiwa juu ya milima ya Golani walidhibiti anga lote la Israeli kwa upande wao na wakaendelea kuwarushia makombora kutokea huko juu. Mwisho wa Israeli ulikuwa dhahiri sasa. Ndipo yule mama jasiri, waziri mkuu wa Israeli wakati huo, Golda Meir, akamfuata Rais Nixon na kumueleza wazi kuwa KESHO HAKUTAKUWA NA ISRAELI kama hautanipa NDEGE za kivita.

  Akapewa ndege 12!! Mataifa ya ulaya, Spain na Italy walipoombwa ruhusa ya hizo ndege kushuka katika viwanja vyao kujazwa mafuta, WAKAKATAA, “hawataki kuharibu uhusiano wao na nchi za kiarabu”, wakristo hao! Ndege zikaongezewa mafuta angani na zikafika. Yule mama jasiri Golda Meir alikuwepo uwanjani kuzipokea na akazihesabu moja moja na akazipa jina la ‘The 12 Stephens’ wakawashukuru Wamarekani na kuwambia vita ni yao kwa hiyo watapigana wenyewe!!! Vita ilibadilika, Jeshi la Misri likakatwa jangwani na kuzuiwa kusonga mbele na wale waliokuwa huko mbele, wakabaki jangwani bila maji wala chakula msafara wa supplies ukiwa umekatwa, vikosi vikajisalimisha. Huko mbele zaidi kutokea huko jangwani, Israeli ikaendelea kuyarudisha majeshi ya Misri hadi wakabakiza km 100 kuingia mjini Cairo. Ikawalazimu kusimama hapo kwani wakiingia mjini watakuwa wameiteka nchi mwanachama wa Umoja wa mataifa! Vivyo walipowageukia Syria walibakiza km 40 kuingia Damascus, nako wakasimama!! Urusi ilikasirika na kuapa kutowasaidia tena Waarabu. Vifaa vyao vipya vilitekwa na kupelekwa Marekani kutafitiwa!

  1975: Wamarekani (super power) walishindwa vita kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ya mapigano huko Vietnam. Je, ndiyo tumemalizana na Mungu na sasa amewageukia Israeli???

  Wapendwa, tuamke yawezekana wakati umesonga sana, labda tuko katika dakika za majeruhi za ujio wake. Basi ni vizuri tukaachana na mambo ya miujiza na utajirisho, tuitafute KWELI YA INJILI ili tuwe sawa na Ratiba ya Mungu. Maana inatia shaka sana unapowaona kanisa wakijitayarisha kwa kunyakuliwa huku Maandiko yakinena wazi kuwa shurti yule mtu wa kuasi afunuliwe kwanza ndipo unyakuo uje, ukiwauliza, “huyo mtu wa kuasi ni yupi?” Wanakushangaa! Huo ndio utaratibu aliouweka Mungu kwa kusudi maalumu, turudini katika mafundisho ya Biblia huenda katika dakika hizi za majeruhi TUKAINGIA!!

  Mbarikiwe nyoooote!!!

 6. Wapendwa,kwa faida ya kuyajua mambo yanayowatukia Israeli kihistoria katika mwanga wa Biblia, huu hapa mtiririko wa matukio machache kutokea pale katika Ukumbi wa Mashauri wa PILATO.

  Israeli ni timepiece ya Mungu!
  Ukitaka kujua ni siku gani ya wiki, tazama kalenda. Ukitaka kujua ni saa gani tunayoishi watazame Wayahudi!

  Pia israeli ni mfano wa kanisa. Yaani mapito yao! Wao ni mfano wa kanisa kwa ile jinsi walivyoitwa kutoka Misri, basi nasi twapaswa kujifunza kutoka kwao katika kuitikia wito wetu wa kumjia Mungu wetu ili tuenende sawa na mapenzi yake. Ni katika njia hiyo tu, tutaikimbia Hukumu ya Mungu kwa kuyajua mambo hayo kimbele kama Rm 11 inavyotufunza na pia kutuhakikishia kuwa yaliyowakuta Israeli yalikuwa kwa ajili yetu tupate kupandikizwa pale alipokatwa Israeli!!

  Kulingana na mpango wa Mungu, israeli walipofushwa hata wakaishia kumkataa masihi wao. Walipomkataa, ndipo Injili ikatugeukia sisi wa mataifa ili Mungu ajipatie bibi arusi wake kutoka kwetu sisi (Paul anasema amemposea Kristo sisi) maana israeli ni mtumishi wake. Kwa hiyo tumegawanywa katika makundi mawili; kundi la kwanza ni Israeli inayojumuisha na wasamaria, na kundi la pili ndilo sisi wamataifa. Naye Mungu kulingana na mpango wake, hashughuliki na makundi haya mawili kwa pamoja. Bali hushughulika na kundi moja tu katika wakati alioupanga.

  Ndipo tunawaona Israeli wanaachwa na Mungu pale walipomkataa masihi wao waking’ang’ania taratibu zao za mapokeo. Tangu pale Pilato alipowasihi kuwa haoni kosa lolote kwa huyu Yesu aitwe Kristo la kumfanya asulubiwe, wao walipaza sauti na kutaka asulubiwe na Damu yake iwe juu yao na juu ya watoto wao. Hapo ndipo walipojitangazia hukumu wao wenyewe, tukageukiwa sisi.

  Kwa hiyo Israeli kama taifa, Mungu, yeye ambaye ndiye NGUVU iliyowashikilia, alipowaacha, walisambaratika. Mwanzo wa msambaratiko ilikuwa mwaka 70 AD pale Yerusalemu ilipozingirwa na jemadari wa Kirumi aitwae Titus. Wao walipomkataa masihi waliendelea na taratibu za dini zao. Pazia la patakatifu pa patakatifu lililoraruka walilishona, wakaendelea na sadaka zao wakijiaminisha kuwa wanaye Mungu!

  Alipofika Titus bila shaka walijikusanya kwa mkesha wa maombi wakitegemea Mungu kuwashindia kama ilivyo desturi. Haikutokea!! Yerusalemu ilizingirwa, hakuna kilichoingia wala kutoka. Walio ndani ya ngome hawana namna ya kutoka. Mikesha iliendelea hadi vyakula vilipokwisha. Wakawala wanyama wote hadi mbwa na paka na hata nguruwe aliyekatiza, na mimea yote ikaisha! Baada ya kumalizika vyote wakaanza KUWALA WATOTO WAO (hao ni wale watu wa Dini) ! Mwishowe wakayafungua mageti, wanahistoria wanatuambia vifereji vya damu vilitiririkia huko nje.Taifa limekwisha!! Hekalu likakombwa vito vyote vya thamani. Vifaa vyote vya dhahabu, shaba safi nk vilivyotumika katika ibada vikasombwa kupelekwa Roma ambako hata leo viko Vatikan! zile scrolls wakataka kuzichoma moto na kuzitupilia mbali, lakini walisimama Wayahudi wachache wakaziomba hizo na wale wapagani wa Kirumi wakawaachia hizo wakiwashangaa kung’ang’ania huo uchafu! kutokea hapo wakasambaratika na kutawanyika huko na kule. Nayo nchi yao ikakaliwa na mwishowe kuwa nchi ya kiarabu yaani Palestina! Ukiangalia katika ramani ya dunia ya pre-1948, hakuna nchi inayoitwa Israeli bali ipo Palestine. Huko ugenini waliendelea na maisha na kuzaana kwa miaka takribani 1900 hata kuzizoelea nchi hizo walizomo kuwa kwao na hivyo kupoteza ndoto ya kurudi kwao, ambako hata hivyo hakuko tena maana ni nchi ambayo ina wakazi wake ambao wanaitambua kuwa ni yao tena kwa asili!!

  Lakini kulingana na timetable ya Mungu yeye aliahidi kuwakusanya tena. Hilo ni wakati wa mataifa unapokwisha, yaani wakati wetu sisi wa kukombolewa. Basi Mungu mwenyewe alianzisha ndani yao kiu ya kurudi “nyumbani”. Kwa hiyo walianza volunteers huko miaka ya 1920, baada ya kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia, nayo Palestina kuwekwa chini ya uangalizi wa Mwingereza. Basi hao walioanza kujirudisha kwa hiari walipewa misaada na wenzao, nao kufunga safari ya kurudi Palestina, “The homeland”, kama kuku wanavyorudi nyumbani jua linapokuchwa, hawarudi kundi bali mmoja mmoja au wawili wawili. Ndivyo ilivyokuwa kwa Wayahudi. Jambo la kwanza wananunua shamba kwa wenyeji, nao bila ya shaka yoyote waliwauzia. Kisha wanaofuata wanakuwa na mahali pa kufikia, wakaendelea kurudi hadi wakajenga mji wao mpya wa Tel Aviv, bandari. Wewe mwenyewe piga hesabu ya maana ya bandari!!

  Kwenye miaka ya 1930s ongezeko lao likawastua Waarabu na mwishowe vita ya chini kwa chini ikaanza, Waisraeli wakijiimarisha na Waarabu wakiwataka waondoke!

  Israeli kama taifa walikuwa wanaingia katika sehemu ya mwisho ya ile adha waliyojitangazia ikiwafikia watoto wao kama walivyotamka wenyewe! Mapepo ya mateso yakaachiliwa juu ya Hitler na washirika wake, ndipo yakawabagua kweupe Wayahudi wote na kuwachukia kwa kumuua Mkombozi wao Kristo, hivyo kuwaona si watu wa maana na hivyo kuwaingiza katika mateso na mauaji ya kinyama yasiyoelezeka!!

  Ulazima wa kurudi nyumbani ukawa si wa kushauriana tena kwa makundi yaliyokuwa huko nje. Wakati vita kuu ya pili inapiganwa Israeli na Waarabu walikuwa wanapigana chini kwa chini vita vikali sana, wakiwa chini ya Mwingereza. Vita ya pili ilipokwisha, intensity ya ile vita yao ilkuwa kubwa (Mwingeza alijaribu kuwatenganisha kwa kuigawa Palestine kuwa nchi mbili), Waarabu wakiwa hawajaridhia nchi yao kugawanywa, mapigano yakaendelea, yaani kiulinganishi ilikuwa ni vicious gorilla warfare iliyoendelea mijini na mashambani! Baada ya kuona wote hawashauriki, Mwingereza akabwaga manyanga akawaacha katika vita yao! Israeli walifanikiwa kubaki ndani ya ile mipaka aliyoichora Mwingereza kuwatenganisha, nao Mei, 1947 WAKAPANDISHA BENDERA yao, ile ya Kale kuliko bendera zote duniani, ile ya ncha sita ya Daudi mfalme, wao sasa ni TAIFA!! Mwaka uliofuata wakaingia rasmi katika Umoja wa Mataifa; 1948: unabii wa ki Biblia unaohusiana na kuja kwa Bwana ulitimia. Baada ya miaka 1,900 ya mahangaiko na dhiki katika mikono ya nchi za mataifa, Wayahudi wameimiliki tena nchi yao na kurejezwa wakiwa ni nchi huru na bendera yao; Officially!!! Je, ndugu zangu wa mataifa, jambo hili mnalitazama katika macho ya kiroho?

  Waarabu waligoma kuitambua Israeli hivyo kuendelea na mikakati yao ya kuwaondoa katika “nchi yao”. Kukawa na vita tena 1956 ambayo ilihusisha Jordan pia lakini hawakufanikiwa, na matokeo yake yalikuwa kugawanyika kwa jiji la YERUSALEMU kwa kujengwa ukuta ulioutenganisha nusu ukiwa chini ya Waarabu pamoja na West bank yake na NUSU ukiwa chini ya Israeli!

  … kwa leo naona niishie hapa, Bwana akitupa tena nafasi ya kuwepo nitawamalizia kipande kilichobakia ili kuutamatisha mtiririko huo kufikia siku ya leo.

  Mbarikiwe nyooote!

 7. Line,

  Nimesoma link nyingi……

  Nadhani ni kosa la kiuandishi……. nilichotaka kusema kwa Matazamo wa Iran inaona Mauaji ya wayahudi katika vita vya pili hayakuwepo…..yametengenezwa tu ni Propaganda za mataifa ya Magharibi kuhalalisha kuanzishwa kwa taifa la Israel 1948……Mtazamo huu si Kweli kabisa……. kwani Historia iko wazi mno…..mauaji ya Wayahudi yalikuwepo wakati wa vita vya pili……..na baada ya vita vya Pili Mataifa ya ulaya……na Wayahudi wenyewe waliona kuna umuhimu wa kuanzisha taifa lao…..;.;

 8. Ndugu Orbi, naomba ukiweza ufafanue hii sentensi yako, kote nimekupata vema isipokuwa hapo umeniacha na vilevile unaweza kuweka link ulikosoma hayo? Nanukuu,

  “Kwa kifupi Iran inaona ni njama na propaganda za mataifa ya Magharibi kuhalalisha wakati huo kuwepo kwa taifa la Israel.Mtazamo huu unapingwa si na Marekani tu……bali na ukweli wa Historia.”

  Asante

 9. Israel walichukuliwa utumwani Babeli hata ufalme wa babeli ulipoangushwa na waajemi,na ndiko Israel walikochukua lugha ya kiaramu ambayo ni moja ya lugha za Uajemi,Kumbuka kuwa wakati wa maono haya ya Daniel Uajemi ilikuwa inatawaliwa na Mfalme Koresh,walikuwa na uhusiano mzuri hata akawaruhusu kurudi Jerusalem kujenga kuta,(Ezra 6:3-5,2nyakati36:23)Uhusiano wao uliendelea hata wakati wa vita vya siku sita Iran iliisaidia Israel kuwapiga waarabu,kumbuka mfalme wa Iran alikuwa anaiitwa Shah,Uhusiano mbaya ulianza baada ya mapinduzi ya kiislamu kama alivyoandika mpendwa Orbi,Ayattolah khomeini ndiye aliyetangaza kuwa Israel ni adui wa uislam,Lazima maandiko yatimie (Daniel10:1)
  ukisoma Daniel 11 na 12 utaona kumbe ni mwisho wa nyakati

  Daniel10;4Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka

 10. Ni utimilifu wa nyakati,

  Daniel10: 1 Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.

  13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

  14 Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado

  21 Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu

  Nikipata kibali nitawashirikisha kwa sehemu yale ninayoyafahamu,kwa mujibu wa maandiko

 11. Mada nzuri sana. Hata mimi nahitaji sana kujua juu ya uhusiano huo.

 12. Wana Strictly Gospel,

  Labda nitoe angalizo langu kwa tunaoipitia Blog hii, naamini wanaoleta mada/maswali wana nia ya kujifunza…..naamini pia kuna wengi hawaandiki chochote na labda pia sio wakristo lakini wanapita ndani ya Blog hii kusoma au kuona ni nini kinaendea kwenye Ulimwengu wa Imani hii kwenye Mtandao…..

  Kwa kusema hivyo (sio kwamba nashutumu) Je ni vyema kumjibu mleta mada (kama hii) kwamba akasome kitabu cha Zakaria? Hata kama kitabu hicho ni cha Kinabii…..unabii sikuzote umefichika unataka tafsri…….Kwa nini basi usijibu maswali haya kwa kutoa tafsri ya kitabu hicho? Je ni kweli kwa kusoma Kitabu cha Zecharia bila msaada mwingine unaweza kujibu maswali ya mleta mada ….?

  Hebu fikiria kwamba mtu anakuuliza swali kuwa anataka kuwa Mkristo….na wewe unamjibu nenda kasome Biblia……!! Kweli itawezekana? Ataanzia wapi hasa kuisoma? Blog ni mahali pa kujifunza….kushirikiana mitazamo……..kupeleka ujumbe unaouamini kwa jamii………Hebu tuwe makini……..tusiifanye blog hii kuwa ni kijiwe tu kisicho na maana……..huwezi kujua kwa kwa kuandika kwako unatoa msaada gani kwa wengine…….!

  Mbarikiwe.

 13. Ndugu Peter Juma,

  Labda niseme una maswali matatu ya Msingi…..

  1. Uhusiano uliopo wa Kurudi kwa Yesu mara ya Pili na Israel

  2. Uhusiano uliopo mbaya wa Iran Na Israel

  3. Asili ya vita kati ya Israeli na Palestine………

  Kwa vile kuyajibu maswali haya inaweza kuwa na maelezo marefu kama utaenda kwa kina hasa ukitumia Biblia kama kitabu cha Historia na pia kuingalia historia nje ya Biblia, Hivyo kwa upande wangu nitalijibu swali la PILI kwanza halafu la TATU………Na swali la KWANZA nitaliacha kwa sasa, Kwani linaweza kujibiwa kwa kutegemea ni msimamo gani wa kurudi kwa Yesu ambao unaouamini yaani ( Amillenianism, Postmillennialism na Premillennialism) Mitazamo hii inaweza kuangalia nafasi ya Israeli katika kurudi kwa Yesu mara ya pili kwa njia tofauti…….hii ni mada ndefu mno na imegawa baadhi ya Wakristo……!!

  1. Uhusiano Mbaya wa Iran na Israel………..

  Nchi hizi kwanza haziko jirani (umbali toka Tehran hadi Tel Aviv) ni kama Km 1589 na hata kwa masaa (time zone) zimetofautiana nadhani kwa masaa matatu. Uhusiano mbaya kati ya nchi hizi ambazo haziko jirani unaweza kulezwa kwa kifupi kwa mambo mawili makubwa 1.Dini ya Kiislamu .2 Marekani

  – DINI YA KIISLAMU: Ingawa Uislamu wa Iran ni tofauti na ule wa Mataifa ya Kiarabu…..na hasa ukizingatia kwamba Wairan si waarabu na wala hawazungumzi kiarabu bali Farsi, ile chuki ya asili kati ya Waislamu na Israel inaifanya Iran iwe na chuki dhidi ya Israel vile vile hasa baada yale mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979 yalipomuondoa Mohahmed Reza Shah Pevhlav aliyekuwa rafiki mkubwa wa Marekani na kumuingiza Ayatollah Ruhollah Khomeini na kugeuza ule uliokuwa urafiki mkubwa kuwa tena uadui.Hivyo kuingia kwa Itikadi ya Uislamu kulirudisha ile chuki ya Asili ya kila Muislamu kwamba Israel amekalia nchi ya Kiislamu …..hasa ukizingatia pia kuwa Yerusalem….kwa mtazamo wa Kiislamu nao ni sehemu yao nyingine takatifu…….hasa msikiti wa Al Aqsa ambayo ni sehemu ya tatu takatifu hasa kwa Uislamu wa Sunni…..na wala kwa kusema ukweli sio ule Uislamu wa Shia wa Iran……ambao una sehemu nyingine takatifu ambazo hazitambuliwi sana na Sunni.

  – MAREKANI: Uhusiano wa Marekani (Urafiki hadi uadui mkubwa) unaweza kuelezwa kwa Marekani kuanzia kwa utawala Mohahmed Reza Shah Pevhlav aliyechukua utawala toka kwa baba yake mwaka 1941.Kuwepo kwa mafuta Iran kwanza kuliifanya nchi hiyo iwe karibu mno na Marekani na Washirika Wake, na pia Shah kuitumia Marekani pia kuwa muhimili wa ulinzi kwa utawala wake dhidi ya maadui wengi wa ndani na nje ya Iran wakatim huo …..na vile vile kumfanya Shah naye pia aibadili Iran kuwa ya Kisasa (Modernization) kulinganisha na nchi nyingine za Kiarabu.

  Lakini licha ya yote haya utawala wa Shah uliangushwa ……na wengi wananchi wa Iran wanaamini kwamba Utawala huo Shah uliweza kusimama toka 1941-1979 kwa ajili ya Marekani. Na toka kuanzishwa kwa utawala wa huo Kiislamu chini ya Ayatollah Khomeni hadi leo Iran imekuwa ikidai kuwa Marekani inataka kuuondoa utawala huo wa Kiislamu (madai haya ni vigumu kuyapinga) na Ili kujilinda na kuweza kushindana na Marekani ambayo iko mbali mno na Iran ni kuwa na Uadui na rafiki wa Marekani aliye karibu Israel…! Vitisho kwamba itaiondoa katika ramani ya dunia……na kwamba ni uongo kuwa kulikuwepo na mauaji dhidi ya Wayahudi kipindi cha vita vikuu vya Pili, na mauaji hayo kusukuma kuanzishwa kwa Taifa la Israel mwaka 1948. Kwa kifupi Iran inaona ni njama na propaganda za mataifa ya Magharibi kuhalalisha wakati huo kuwepo kwa taifa la Israel.Mtazamo huu unapingwa si na Marekani tu……bali na ukweli wa Historia.

  Nadhani kwa leo inatosha……UBARIKIWE.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s