Hekima Hujenga

Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote (Luka 7:35).

Hekima ni udhihirisho au ufunuo wa usahihi wa Mungu katika maisha ya mtu; ni msukumo unaokusababisha kutenda, kuitikia au kuongea katika namna ipitayo ufahamu wa kawaida wa kibinadamu. Vile vile ni mwonekano wa nguvu ya Mungu katika mawazo, mipango, makusudi na katika kufanya maamuzi. Hekima ya Mungu inapokuwa inatenda kazi ndani yako, hufanyika kuwa ni nguvu inayoshawishi maamuzi yako ya maisha; hufanyika kuwa msukumo katika kuyaongoza maisha yako. Hekima hukupeleka katika mwelekeo sahihi katika maisha, na kukuweka katika nafasi ya faida.

Mwanzo 39 inaelezea habari ya namna Yusufu alivyouzwa Misri katika utumwa na ndugu zake. Lakini Biblia inasema aliona neema pachoni pake Potifa, bwana wake na kumtumikia: “…Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake” (Mwanzo 39:4). Hata hivyo baada ya muda, Yusufu alitiwa gerezani kwa sababu mke wa bwana wake alimshitaki kwa uongo. Lakini hekima ilimwinua, na kumfaidisha, kiasi kwamba hata akiwa bado gerezani, alifanywa kuwa kiongozi wa wafungwa wengine.

Baada ya muda fulani, ilionekana kama vile hapo ndio ingekuwa mwisho wa habari. Siku moja usiku, Farao akaota ndoto ambayo hakuna hata mmoja kati ya waganga wake aliyeweza kuifasiri. Mtu mmoja akamkumbuka mfungwa mmoja wa Kiebrania mwenye busara na akamwakilisha kwa Farao. Yusufu akaletwa mbele za Farao, na akafasiri ndoto ya Farao. Yusufu alipomaliza kuongea aliwaambia watumwa wake, “Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe…Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri” (Mwanzo 41:38-41).

Eneo lote la Misri lilihifadhiwa na hekima ya kijana mdogo, Yusufu. Kama hekima ilimwinua mfungwa wa Kiebrania mwenye umri wa miaka thelathini tu na kuwa Waziri Mkuu ufalme mkuu kuliko yote kama ule kwa usiku mmoja tu, inaweza kufanya zaidi kwako. Iinue hekima; mpe umakini unaostahili, kipaumbele na umuhimu, na atakuinua na kukuletea heshima na utukufu.

Ukiri

Nanena hekima ya Mungu katika kila hali kwa sababu Kristo amefanywa kuwa hekima kwangu. Nina usahihi, akili na nina uelewa wa haraka! Hekima ya Mungu inadhihirishwa katika mawazo yangu, maneno na matendo kwani akili yangu imekaa katika Neno; kwa hiyo ninatenda kwa busara katika mambo ya maisha leo, katika Jina la Yesu. Amina.

–Evangelist Marcus Kilindo

Advertisements

One thought on “Hekima Hujenga

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s