Ni muhimu kushuhudia mambo machafu uliyofanya? Swali la mwezi March

Kumekuwa na shuhuda nyingi kuvutia na kusababisha wengine kuinuliwa imani yao na wengine kuwa na wasiwasi na washuhudiaji kama kweli wameacha yale mambo waliyoyafanya kabla hawajampokea Bwana Yesu.

Leo kuna ushuhuda wa dada Janeth Boynes aliyekuwa msagaji na kufikia hatua ya kuoa mwanamke mwenzake kabla Bwana Yesu hajamuita na kuacha usagaji ili amtumikie, Janeth tangu akiwa na miaka 12 mpaka alipoenda chuoni, alikuwa akiendelea kutumia madawa ya kulevya na kubeba uchungu alioumizwa na wavulana na kujikuta akivutia wanawake.

Siku moja alipoenda dukani alikutana na mwanamke akaanza kumwambia habari za Bwana Yesu na kumwalika kanisani na kukutana na akina dada wengine na Janeth akawaambia tatizo lake hivyo anahitaji kuacha usagaji aishi kwa ajili ya Bwana Yesu.

Waliweza kumsaidia na kumuombea Mungu ambadilishe baada ya muda, Mungu aliuponya moyo wake na kubadilisha aina ya maisha aliyokuwa akiishi.

Hivi sasa Janeth amekuwa msaada kwa wadada wote waliopitia hali kama yake na kuwashuhudia upendo wa Kristo kwamba unaweza kuondoa madhaifu yote na kukombolewa kabisa. “Haikuwa kazi rahisi lakini kwa uwezo wa Roho Mtakatifu niliweza kuachana na tabia nilikuwa nazo na kuwa msaada kwa wengine”

Je mtu kushuhudia mbele za watu kwamba alikuwa msagaji, shoga, jambazi, mzinzi aliye kubuhu, mchawi nakadhalika. Ni Muhimu kushuhudia kila jambo? au unaweza kufunguliwa katika hayo na ukawa ukimshukuru Mungu kisiri siri.

Advertisements

12 thoughts on “Ni muhimu kushuhudia mambo machafu uliyofanya? Swali la mwezi March

 1. shuhuda zinajenga lakini unapotoa shuhuda uwe makinni kwani shuhuda nyingine hazifai kwa sababu zinaweza kukupunguzia au kuondoa kabisa sifa na ushuhuda wako.naundana na mch.mosha.

 2. kama mtu ameokoka kuna mambo ataweza kuyashuhudia lakini siyo yote, mfano dada alikuwa ni mpenzi wa bosi wake alipokuwa anafanya kazi za ndani huyu hata akiokoka akanifahamisha alichofanya sintamruhusu aseme mbele ya hadhara kwani inagusa ndoa ya mtu

  eeee au kijana alikuwa jambamzi na sasa ameokoka huyu aseme yote au alikuwa mchawi sasa amekutana na nguvu ya msalaba hiyo haina shida japo pia shuhuda nyingine zaweza zuia mpango wa mungu kupitia ubinadamu kama mshuhudiaji atasema vitu vinavyomgusa yeye binafsi sana mfano alishatoa idadi kadha ya mimba taarifa hiyo itamuondolea point ya kuolewa

  kwa hiyo ni vema mtu na ajue kuwa amesamehewa dhambi zake zote na Yesu amebeba hatia badala yake aendelee kumuabudu Mungu katika Roho na kweli

  Pastor Thobiasi

 3. mi naona inategemea na ushuhuda wenyewe kwa mf Mungu kakubariki umepata mtoto nk unaweza kushuhudia, lkn vitendo km hv binafc naona km unaweza kuwashawishi na wengine wajaribu. kwa mf m2 unaweza kusema minilikw muhuni sn yn minaona km unakw unalicfia lile jambo

 4. Elezea makuu ya Mungu aliyofanya juu ya maisha yako..yale machafu hayatasaidia sana jinsi namna..nk bali jinsi na namna Bwana alivyokutoa katika utumwa wa dhambi ile nafikiri nilivyosoma ushuhuda wa huyu dada ameelezea vizuri sijaona tatizo

 5. kushuhudia ni vema, maana unawapa wengine matarajio ya kubadilika katika yale wa yafanyayo endapo wataendelea kumtumikia Mungu.

 6. yesu anaokoa kweli.ni vema kushuhudia vile Roho wa mungu anakusukuma,na akusukumapo anakusudi maalum la kuponya nafsi ya

 7. Si lazima.Lakini mtu akishuhudia,anawajenga wenzake ambao bado wanaangukia hapo,kubadilika.

 8. Mimi naona ni vyema kushuhudia, ili kuwapa na wengine nafasi ya kutafakari uweza wa Yesu wa kuziponya nafsi zetu. Pia kiroho watu wataweza kuamini kwa jinsi watavyoona tofauti ya maisha yako kabla na baada ya kumpokea YESU kama bwana na mwokozi wako.

 9. KWELI KUSHUDIYA NI VEMA JUU YA KUMUFEZELESHA ADUI WETU NA KUTUPA NGUVU AO WEZIO KUSIKIYA MIUCHIZA YA YESU. NA NGUVU YA MUNGU KAMA VILE MUTUME WETU PAULO ALIKUWA NA SHUHUDIYA VILE ALIKUWA NA TEMBEYA KABLA ACHA KUTANA NA BWANA YESU KWELI TU JUWE KAMA KUSHUDIYA NI KUANZA VITA KUBWA NA ADUI WETU

 10. kwa kweli ni sawa alivyosema jacqueline amani ya kristo iamue moyoni kama ushuhudie yote au sehemu tu ya maisha yako na wakati gani na sehemu gani,mtu anaweza kuwa na shuhuda moyoni mwake lakini Mungu akisubiri wakati sahihi wa kuutoa.

  Nilipata kusikia ushuhuda wa dada mmoja alishuhudia waziwazi jinsi alivyolazimishwa kuolewa na mwanaume na wazazi wake alipofika huko mwanaume alipotaka kumjua alikemea
  utendaji kazi wa kiungo cha mwanaume ulishindwa kabisa na hakumjua,ndipo huyo binti huyo alipookoka mdomoni mwa mwanaume huyo alisimulia hayo kanisani ili leta gumzo sana kanisani watu wakasema alikosea kueleza yote.

 11. kusema ukweli ni kukiri na kuonyesha hakika u have change lakini ukiona mtu hasemi eitha anaendelea na tabia mbaya au anaona aibu kitu ambacho si chema machoni pa Mungu

 12. Nadhani kwenye suala la kushuhudia kila kitu Amani ya Mungu iamue moyoni kwa mtu binafsi .Japo kwa kweli unaposhuhudia live unamuabisha shetani bali zaidi unakuwa msaada kwa wengine ambao wanapitia hali kama uliyonayo kuwa kumbe kwa Mungu inawezekana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s