Nani Mshamba – Stara Thomas

Muimbaji wa Injili nchini Tanzania, Stara Thomas. Ameachia wimbo wake wa Nani mshamba unaopigwa kwenye vituo vya redio za injili nchini. Wimbo huo una maneno yafuatayo

“Aliye kwa Yesu ni mjanja,

Aliye kwa Yesu si mshamba,

Yuko kwenye mwanga, mwanga wa milele”

Stara akiongea na moja ya redio ya Injili amesema baada ya yeye kumpa Yesu maisha yake “wengi walinitenga na wengine kunidharau lakini mimi sijali maana mtu anayekuwa kwa shetani ni mshamba”

Album ya dada Stara NANI NI MSHAMBA iko tayari na itasambazwa mwezi wa nne.

Habari nyingine zinazosikika ni kuhusu Beatrice William aliyepata umaarufu kupitia Bongo Star Search naye ameokoka tarehe 7/3/2012 kwenye kanisa la Mikocheni B Assemblies of God (Mlima wa moto)

Alipoongea akiwa madhabahuni tarehe 9 Machi kwenye mkesha kuhusu uamuzi wake wa kumpokea Bwana Yesu alisema “Ni uamuzi wangu wa dhati kuokoka na akili zangu timamu. Mara nyingi nilipenda sana kuokoka lakini niliogopa kumbipu Mungu kama wengine wanavyofanya”

Kufahamu mengine kuhusu Stara Thomas fuatilia link hii

https://strictlygospel.wordpress.com/2011/02/21/stara-thomas-ameokoka/

6 thoughts on “Nani Mshamba – Stara Thomas

  1. Kama ni kweli Mungu akubariki, manake wengine wameshaona mziki wa gospel una lipa bac kila m2 anasema ameokoka. kuna baadhi ya wasanii maarufu wanasema wameokoka lakini pombe bado wanakunywa kwenye akudo wapo. Mungu a2saidie wapendwa.

  2. Asante Yesu kwa kuwaokoa hawa ndugu,naomba sisi wengine tuwaombee sana hawa ndugu kwa kuwa bado ni wachanga!

  3. Sikuwa nafahamu ya kwamba dada Stara Thomas ameokoka. Hongera sana dada Stara. Ni uamuzi wa maisha ya uzima wa milele. Wewe kweli ni mjanja. Nataka sana kuusikia wimbo huu wa NANI MSHAMBA. Yaonesha ni wimbo wa kumwaibisha shetani na kuliinua jina la Yesu.

    BARIKIWA!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s