Vigezo vya kushiriki Gospel Star Search Vyatajwa!

Mwenyekiti na Mratibu wa Gospel Star Search Harris Kapiga

Gospel Star Search imerudi na tayari Vigezo vya kushiriki vimeshawekwa wazi. Akiongea na waandishi wa habari za Kikristo nchini, Harris Kapiga ambaye ni Mratibu wa shindano hilo alisema vigezi ni pamoja na 1. Awe Ameokoka 2.  Awe Hajatoa Albam Yake Sokoni 3. Umri Wowote Wa Mshiriki Utaruhusiwa. Na Vigezo Vingine vya ki-uweledi vitazingatiwa kwa ajili ya Kutunza nidhamu ya Washiriki Katika Mchakato huo.

Kapiga, aliendelea kusema “Tarehe 14 April, 2012 Kinyang’anyiro Cha Kuwasaka Washindi katika Kanda Ya Wilaya Ya Temeke Kitafanyika katika Ukumbi wa Saba Saba Opposite na Banda la Maonesho ya Biashara la Ofisi Ya Waziri Mkuu. Mchakato Utaanza Saa 3 Kamili.Tarehe 21 April, 2012 Jopo la Majaji Litaamia Katika Wilaya Ya Ilala Katika Ukumbi wa Msimbazi Centre Kuanzia Saa 3 Kamili asubuhi Washindi 30 Watakuwa wakitafutwa.

Washiriki Wengi Wilaya Ya Kinondoni Kinyang’anyiro Kitafanyika katika Hotel ya Etina Eneo la Survey Karibu na Mlimani City Kuanzia Saa 3 Kamili Asubuhi.

Harris Kapiga ameendelea kutabanisha kwenye Blog ya Papaa kwa kusema kuwa Tarehe 2 Mwezi wa May, 2012 Kuanzia Saa 3 Kamili Asubuhi Katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Songea, Musoma, Mwanza, Kigoma, Tanga, Arusha na Kilimanjaro. Zoezi la Kuwasaka Nyota Wapya wa Muziki wa Injili litafanyika Kwa mpigo. Mara baada ya Washindi Kupatikana katika mikoa hiyo wataungana na Washindi wa Dar-es-Salaam na Kukaa Kambini kabla ya Kumsaka Mkali Mpya wa Muziki wa Injili Tanzania.

Kinyang’anyiro cha Gospel Star Search litafungwa rasmi 5 August, 2012 katika Jiji la Dar-es-Salaam, ambapo Mzizi Wa Fitina utakatwa siku hiyo.Kwa Watu Wanaotaka Kushiriki GSS 2012 na Mikoa yao hajatajwa basi wataombwa kushiriki katika Mikoa Jirani.

—Sam Sasali Blog

5 thoughts on “Vigezo vya kushiriki Gospel Star Search Vyatajwa!

 1. mi naona co mbaya lengo lao nikuwasaidia waimbaji ambao hawajui waanzie wp. may be wabadilishe jina. coz mi naona km jina ndiyo ambalo wa2 linawapa utata.

 2. Jamani Kanisa linahitaji maombi…! hv mnatumia maandiko gn katika kuhalalisha hili,naomba mtu mmoja anisaidie katika hili labda ufahamu wangu ni mdogo..!! u-star hautafutwi,utakuja wenyewe kutokana na jinsi kile kipawa kinavyofanya kazi,wala hupimwi na mwanadamu..!!
  Jamani eeh acheni mchezo na maandiko,mbna kuna mambo mengi tu ya kufanya huko duniani pasipo kumhusisha na Mungu..!!!
  Haya mambo ya kdunia kuwemo kanisani yametosha sasa,tunahitaji watu wenye wivu kweli na Bwana ili wamtumikie Mungu kwa usahihi naye Mungu atajidhihirisha pasi na mashaka.

 3. HUU NI MTAZAMO WANGU TU…..!!
  Kwa kweli wakristo tunahitaji kumuomba Mungu,unatafuta U-Star kwa Mungu,kazi ya Mungu haina u-star,wala huo u-star hauji kwa kuchaguliwa na watu……!!! Hvi tunatumia Biblia gani katika kuendesha mambo hayo…!!
  Naomba kama kuna mtu mmoja ajaribu kunishawishi kwa kutumia maandiko ili nami niunge mkono hili maana mpaka sasa naona hili jambo nikiliweka katika mzani wa misingi ya ki-biblia halikubali ku-balance kabisa…!!! please anyone there to help me.

 4. Romans 12:2
  Do not conform yourselves to the standards of this world, but let God transform you inwardly by a complete change of your mind. Then you will be able to know the will of God — what is good and is pleasing to him and is perfect.

  Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s