Sera ya mavazi kwa wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Yaanza kutumika!

Eneo la mbele la Jengo la Utawala la Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam. Chuo hicho kimeanzisha sera ya mavazi kwa wanafunzi wawapo chuoni hapo ambayo imeanza kutumika rasmi kwa kuwataka kuvaa mavazi ya heshima na wale wanaokaidi kuchuliwa hatua za kinidhamu.

Baadhi ya wanafunzi wa la Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam wakiwa darasani. 

Uongozi wa Chuo cha elimu ya biashara (CBE) kampasi ya Dar es salaam umesema kuwa hautasita kumchukulia hatua mwanafunzi au mfanyakazi yeyote atakayefika chuoni hapo akiwa amevaa mavazi yasiyo ya heshima huku ukitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kampeni hiyo yenye manufaa katika kujenga taifa lenye maadili mazuri.

Akizugumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kaimu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Bw. Athman Ally Ahmed amesema chuo hicho kimefikia uamuzi huo kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uvaaji wa mavazi yasiyokuwa na staha vinavyofanywa na wanafunzi wa kike na wale wa kiume wawapo chuoni hapo hali inayosababisha udhalilishaji wa utu wa wanafunzi ndani na nje ya chuo.

Amesema wanafunzi ambao wengi wao ni vijana chuoni hapo wamekuwa mstari wa mbele katika kuiga kila aina ya vazi kutoka tamaduni za watu wa magharibi hali ambayo ameielezea kuwa ni ukiukaji wa mila , desturi na tamaduni za mtanzania .

“Mtindo huu wa kuiga tamaduni za magharibi pasipokuangalia wapi tunakwenda haukubaliki hata kidogo,ukiangalia katika vyuo vingi vya elimu hapa nchini wanafunzi wamekuwa wakivaa mavazi ya ajabu na yasiyofaa kabisa katika maeneo ya chuo” amesema.

Amesema kuwa Chuo hicho kimekaa na kubuni sera ili kuyaondoa mavazi ambayo hayaruhusiwi kuvaliwa katika maeneo ya chuo na kubuni sera ya mavazi kwa ajili ya wanafunzi hali itakayowajengea nidhamu wasomi hao wa fani mbalimbali pindi watakapomaliza masomo yao chuoni hapo.

Amefafanua kuwa adhabu mbalimbali zitatolewa kwa wanafunzi watakaokiuka agizo la uvaaji wa mavazi yenye heshima amabazo ni pamoja na kuzuiliwa kupita getini kwa mwanafunzi husika kuingia katika eneo la chuo kwa wale wanaotoka nje ya hosteli na wale wanaoishi ndani ya eneo la chuo hawatapewa huduma yoyote kama vile kuingia darasani,kantini , maktaba au ofisi yoyote ya chuo.

Aidha amefafanua kuwa wanafunzi ambao hawatakua tayari kufuata utaratibu huo watafikishwa mbele ya kamati ya nidhamu huku akibainisha kuwa adhabu itakayotolewa ni mwanafunzi kusimamishwa chuo kwa muda wa miezi mitatu.

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo Bi. Bertha Kipillimba amesisitiza kuwa zoezi hilo litawahusu wafanyakazi wote wa kampasi ya Dar es salaam na wanafunzi zaidi ya 6000 wa chuo hicho.

Amesema hivi sasa taratibu hizo za uvaaji wa mavazi yenye staha zimeingizwa kwenye kanuni za chuo na kuongezwa kwenye masharti ya fomu za kujiunga na chuo hicho huku akifafanua kuwa tayari wametoa kipindi cha wiki mbili kwa utekelezwaji wa kanuni hizo na watakaokiuka kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni hizo.

Naye mlezi wa wanafunzi wa hicho (Dean of Students) Bw. Faustin China amefafanua kuwa umefika wakati wa wanafunzi hao kujitambua huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakinyoshewa vidole na jamii kuhusu suala la uvaaji na mienendo ya wanafunzi chuoni hapo.

“Tumesemwa vibaya kwa muda mrefu hatuwezi kuachia suala hili likaendelea, tunataka wanafunzi wetu wavae vizuri kwa mujibu wa kanuni tulizojiwekea ili kujenga heshima ya chuo” amesema.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na uanzishawaji wa sera ya mavazi chuoni hapo wakieleza kuwa inaingilia uhuru wao wa kuamua huku wengine wakiupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuliona suala hilo na kulichukulia hatua ili kuleta na kulinda heshima ya chuo hicho.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

28/3/2012, Dar es salaam.
Advertisements

6 thoughts on “Sera ya mavazi kwa wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Yaanza kutumika!

 1. Safi sana CBE huu uwe mfano ktk vyuo vyote nchini maana vijana hawajitambui kabisa kuvaa mavaz ya nusu uchi ni kawaida kwao, ni aibu tosha kwa wazazi.

 2. na vyuo vyote viangaliwe kwa upya kwa kweli navyo. pia mpite na maofisini kuna baadhi za ofisi zinatisha kwa mavazi pia hata huko mtaani kuwepo na askari ambao watakamata watu ambao wanatembea uchi wanavaa kaptula zimewabana na vichupi wakituonyesha na mambo mengine ya aibu ambayo hayafai kuonekana suruali zimebana, skin tati wanazo zimeshika mwili na mwli unauona kama ulivyo utadhani yupo uchi, vitopu, maziwa kuonekana hovyo, vijana suluari nusu makalio vichupi vichafu vinaonekana kwa kweli kuna haja ya kuingilia kati hiki kitu. nawatakia mafanikio mema kwa kazi hii ambayo mmeianza na Mungu awatangulie sana tu.

  Betty.

 3. Very good CBE , keep it up.
  Wakati nasoma DIT wanafunzi baadhi wa CBE walikuwa wanawacheka DIT students eti washamba ! But unajua engineers hawana mda wa kupoteza, nawashauri viongozi wa chuo waongeze strickness katika mitihani na tests ili wanafunzi wakose mda wa kujiremba.

 4. SAFI SANA CBE NAMI NAUNGA MKONO KWA UAMUZI WENU WA KUREKEBISHA MAADILI NDANI YA JAMII,HAIPASI HATA KIDOGO KUFUMBIA MACHO SUALA HILO.
  NAPENDA KUWAPONGEZA KWA MKONO WANGU JAPO UPO MBALI NANYI.

 5. Kwa kweli hapa sasa nchi imeanza kupata watu wanaostahili. Swala la mavazi limekuwa tatizo sana hapa Tanzania hasa maeneo ya vyuo vya elimu ya juu.

  Kwa kweli CBE imeonesha mfano ambao kila taasisi ya elimu ya juu iige mfano huo. Inashangaza kuona watoto wa kike hasa wakiwa wamevaa mavazi ambayo yanaonesha hadi maumbile yao ya uke. Hii ilikuwa kero kubwa.

  Nimewahi kuandika sana kuhusu mavazi ya Mkristo kwa kuzingati Biblia. Ukienda pale CBE au vyuo vyote wale wanaovaa mavazi yasiyo na staha karibu 70% ni wakristo. Kwa nini?

  Naunga mkono hoja ya kurekebisha swala la mavazi katika maeneo yote yaliyo rasmi.

  Kama mtu anataka kuvaa mavazi yanaonesha hadi ndani azivae akiwa ufukweni au ukumbi wa disko siyo darasani, kanisani, mtaani, ofisini au kwenye maeneo ya hadhara.

  Imefika wakati Bunge letu lipitishe sheria ya mavazi (National Dressing Code Act) ili kuwa na sheria moja ya mavazi nchi nzima.

  Hongera sana CBE

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s