Tumeanza na Mungu, tutamaliza na Mungu – Joshua Nasari

“Cha kwanza kabisa namshukuru sana Mungu ambaye alinipa maono ya kuwa mbunge wa Arumeru mashariki, nimekuwa nikiyasema kwa muda mrefu watu walifikiri natania, lakini vilevile nikishukuru chama changu cha CHADEMA ambacho kilinipa ridhaa ya kusimama kuwakilisha kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki, kwakweli niwashukuru sana watu wa Arumeru mashariki ambao hawakujali umri wangu, hawakujali uwezo wangu kifedha, hawakujali historia ya familia yangu katika siasa, hawakujali kila mapungufu ambayo nilikuwa nayo, lakini wakaamua kunichagua…..napenda niseme  na kama nilivyosema tangu mwanzo kwamba tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu na siyo kwenye kupata kura peke yake, tutaendelea kumtumikia Mungu na kumuweka Mungu mbele, tutamtanguliza yeye na tutaongozwa na yeye siku zote”

Haya ni maneno ya mbunge wa CHADEMA mtumishi wa Mungu, Joshua Nasari (26) aliyeshinda Jimbo la Arumeru mashariki kwa kura 32972 ambazo ni sawa na asilimia 54 na kufuatiwa na mgombea wa chama cha mapinduzi, Sioi Sumari aliyepata kura 26,757 sawa na asilimia 42.

Advertisements

28 thoughts on “Tumeanza na Mungu, tutamaliza na Mungu – Joshua Nasari

 1. HALELUYA…..,
  MH.JOSHUA NASARI MUNGU AKUBARIKI SANA TENA SANA, KWAKUA UMEKUA NJASIRI KUMKIRI MUNGU,KUKIRI UWEZA WA BWANA YESU HADHARANI JAPOKUWA NI MBUNGE,WENGINE BWANA YESU AKIWAINUA WANAMSAHAU MPAKA WAPATE MATATIZO NDIO WANAMRUDIA,

  MI NASEMA HIVI, BWANA ALIYEKUPIGANIA MPAKA UKAWA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI,NDIYE HUYOHUYO ATAKAE KUINUA ZAID,
  1SAMWEL 17:37-39
  WATU WATASHANGAA KIPINDI KIJACHO UTAKAPOKUWA WAZIRI.

  JAPOKUWA WATU WENGI WAMECHANGIA,WENYE HEKIMA WAMEPONGEZA,WASIO NA HEKIMA NAO TUMEWASOMA, MH.JOSHUA,KUMBUKA WASWAHILI WANASEMA, “MILUZI MINGI HUMPOTEZA MBWA KTK MAWINDO” HIVYO MSIKILIZE MUNGU ALIYEKUITA.

  USIOGOPE CHANGAMOTO “ALUTA CONTINUA”

  NIMIMI DP. LEONARD N. MAPUNDA
  MOROGORO

 2. mi nadhani hakuna tatizo juu ya maneno ya mh.wameanza na Mungu watamaliza na Mungu wao dats all sasa complication zinatokea wapi ndugu zangu ktk Bwana?

 3. Hongera Mh.Nassari.Kumbuka Mungu amekupa nafasi hiyo kwa kusudi maalum na ameona akutumie wewe kama sababu na mfano tu wa kile anachotaka kufanya juu ya taifa hili.KUMBUKA UPO HAPO KWA KUSUDI MAALUM!!

 4. Ndg Kellysia naona unatoka nje ya mada, wana SG walichopongeza ni maneno yake Nassari, tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu… hata angekuwa ni CCM amemtukuza Mungu nami ningemtukuza naye. endapo Nassari angeshindwa na kusema Mungu amemfundisha hivi ningesimama naye, mradi hapa kinachohusika ni Mungu na si hayo mengine. Jaribu kurudi kule juu this is STRICTLY GOSPEL kwa hiyo chochote kilicho chema. chochote chenye kumpa Mungu utukufu, chochote chenye upendo wa kweli wa Mungu tutakitafakari na kukijadili hapa iwe ni uongozi, umiliki, kazi, ndoa, uzazi hata kifo. Ubarikiwe

 5. Mheshimiwa juma tafadhali,Wachadema wanahusishwa na udini(Wakristo).Sikufahamu hapa SG wako upande gani?Its something i come to agree with as i go,mind you mi pia mkristo.All along tumekuwa tukisema cuf cha waislamu then Chadema mkiambiwa cha wakristo mnakataa.Mi sio mwanachama wa chama chochote.Lakini mh,bye the way I am christian.Over

 6. Ni muhimu sana kuliko chochote, Kwenda na maandiko. Neno linasema KILA MAMLAKA IMEWEKWA NA MUNGU! Na hata Yesu, alipata kusema, alipokuwa katika baraza la wale waliomhukumu, ni kama alisema maneno yanayo fanana na haya “…….pasipo Mungu usingekuwa na nafasi uliyonayo” Sasa, iwapo kila Mamlaka iliyopo madarakani ipo hapo kwakuwekwa na mungu; na kwamba, kwa mjibu wa maandiko yapaswa kuheshimiwa. Msemo “TUMEANZA NA MUNGU TUTAMALIZA NA MUNGU” Unamaanisha nini? Unataka kusema CCM haikuanza na Mungu na hivyo haitamaliza na Mungu? Je, Mungu yupo upande wowote katika siasa? Nijuavyo mimi Mungu, hulichunguza zaidi Neno lake ili apate kulitimiza, kwa nini kumpongeza mh. Mbuge mpya kuambatane na kumhusisha kuwa Mungu yupo upande wa Chadema? – Mnajuaje, kama Nasari hazungumzi tu ili kuona au kutaka aungwe mkono na “wakristo”? Nionavyo mimi hisia na ushabiki wa kikristo kwa mkristo mwenzenu hakutoshi kumsemea Mungu, kwamba anakubaliana na Chadema kwa ujumla. Maana neno “Tumeanza” lina maanisha wingi yaani nasari na labda Chama chake. Pengine kama angesema “Nimeanza” nisingesema sana kwani, mtu ana mahusiano ya moja kwa moja na Mungu wake – maana siwezi kujua walivyokubaliana na Mungu wake, kwamba anawekwa katika nafasi hiyo ya kitaifa kwa kazi gani, labda “Kukomboa” au “Kuadabisha”! Ningependa watu wasimwingize Mungu katika mambo yao ya siasa kuwa eti ni maono yatokanayo na MUNGU mwenyewe ili watu “WAPONE” Hii ni kwasababu kwamba utawala uliopo madarakani umewekwa na Mungu, kwa sababu za Mungu, kama uwaponyeshe watu na shida zao au uliadabishe taifa tokana na dhambi za Taifa husika. Cha msingi Wakristo wanatakiwa wajifunze kwanini Utawala uliopo madarakani unafanya hicho unachofanya! Ili kama kutubu watubu au kama kuneemeka wampe Mungu utukufu! Ukisoma Blia kwa makini, utaona mara kadhaa Mungu ametumia tawla mbali mbali ili klilejeza Taifa lake katika uchaji Mungu; na pia alitumia Tawala mbali mbali kulifurahisha, au kulipatia ahueni Taifa lake. Hivyo si sahihi Baadhi ya wakristo kujikita moja kwa moja kumsemea Mungu, eti chama Fulani kikija Madarakani kitakuja kuwaponyesha. CHA MUNGU MPENI MUNGU CHA KAISARI MPENI KAISARI – Msiingize udini katika mapenzi yenu ya kisiasa, MAANA ROHO YA UDINI KATIKA MAMBO YA SIASA NDIYO INAYOLITESA KANISA TANGU KALE!

 7. Mungu anasema Niite nami nitakuitika. Joshua alimuita Mungu naye akamuitikia akampa ujasiri wa hali ya juu na akamwangusha Goliati kwa kombeo tu.

  Joshua endelea kumpa Mungu utukufu kwa kila jambo naye atakufanikisha siku zote na utakuwa kichwa wala hutakuwa mkia daima

 8. Willy uisso on thursday 2012
  hongera mtoto wa mchungaji kwani umeonyesha kwamba uongozi sio lazima uwe na umri mkubwa ila ni hekima zaidi. pole kwa uvumilivu wa matusi yote uliotukanwa.mungu akupe nguna ya kuwatumikia wanaarumeru na kutekeleza ahadi ulizoahidi.nakuomba mweshimiwa nasariwaambie viongozi wote pamoja na wewe ni wakati wa kuzunguka nchi nzima,mtaa hadi mtaa kunadi sera na lengo la chama na kuwahimiza vijana wote kuanzia secondary hadi vyuo vikuu umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura mwaka 2015. kwani vijana wengi hawapigi kura.naomba mtambue taifa lolote wanaolete mageuzi ni vijana, kwa mfano zambia.

 9. “Cha kwanza kabisa namshukuru sana Mungu ambaye alinipa maono ya kuwa mbunge wa Arumeru mashariki, nimekuwa nikiyasema kwa muda mrefu watu walifikiri natania”

  Nimeamua kunukuu maneno haya sasa ndio nimeona jinsi kijana mwenzetu alivyofanya kazi katika maono aliyopewa. Nimeguswa sana na maneno haya kwa kweli yanatia moyo sana kwa watu waliokoka ambao Mungu amewapa maono mbalimbali, hata mimi binafsi nina ya kwangu ambayo nimepewa.

  Kitabu cha (Habakuki 2:1-3) anasema “Bwana akanijibu, akasema iandike njozi ukaifanye iwe wazi katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake; wala haitasema uongo; ijapokawia, ingonjee. Kwa kuwa haina budi kuja haitakawia.”

  Neno iandike njozi katika Biblia ya kiingereza linasema ” Write down the vision” andika maono.

  Kama alivyosema Joshua kwa muda mrefu alikuwa anawaambia watu na watu walikuwa akifikiri anatania. Hivi ndivyo mambo yalivyo, watu wanaweza kuona kama unacheza lakini alipewa maono ambayo yapo connected na kusudi la Mungu ndio maana sifa zote anarudisha kwa MUNGU, wapendwa haya ni mambo ambayo kwa kweli inabidi tujifunze kuna mahali hata mimi pia ninaelekea na huwa ninawambia watu na wengine wanacheka na kudharau lakini nimekwishaiona picha ya maono mbele yangu, na ninaelekea huko huko.

  Wakati au muda unapofika wa kusimama katika kusudi la Mungu au mahali Mungu anapotaka usimamame haijalishi umri wako, wala uzoefu wako, wakati unapofika milango inafunguka upate kupita haijalisha kuna upinzani kiasi gani.

 10. We encourage those who fear the Lord God to participate in politics, because there is no way of reducing corruption out of increasing this kind of people who go on the throne with the mind of being allowed by God himself to be there!

  Keep on CHADEMA find them.

  I am also encouraging other parties especially CCM to change and allow people who fear the Lord God of Jesus Christ to be candidates. They will help them to settle some problems facing Tanzania.

 11. Napenda kumwambia Bw. Kellysia kwamba hajaelewa anachokisema. Hajajua kutofautisha mada inayozungumzwa na mawazo yake.

  Hivi, pale Bw. Nape Nnauye alipompongeza Bw. Joshua Nassari na akakipongeza CHADEMA naye alikuwa ni mwanachadema?

  Kwa nini uanze kuwaza kinyume na facts kwamba eti Gospel forum ni CHADEMA kwa sababu tu wamenukuu maneno ya Mbunge wa Arumeru Mashariki na kuyaleta hapa ili tuyasome na kisha tuwe na lolote la kusema.

  Hivi kumpongeza mshindi lazima uwe katika Chama chake? Hivi kuwa mfuasi wa CHADEMA au CCM ni dhambi?

  Hivi wewe huwa hutazami nchi zilizoendelea kidemokrasia kuwa walioshindwa humpongeza aliyeshinda na aliyeshinda pia huwapongeza washindani wake na kuwataka wote kwa pamoja wajenge nchi kwa pamoja?

  Kumbe naanza kuona kwamba ndiyo maana watanzania hatupigi hatua ya maendeleo. Kuna watu wanadhani kwamba ukishabikia chama ambacho hakiko madarakani wewe unakuwa siyo mzalendo. Ujinga mtupu.

  Kumbuka Siasa ni kama upepo unaovuma. Waweza kuvuma kuelekea upendako na wala wewe huwezi kuuzuia.

  Subiri uone mwaka 2015 upepo wa siasa utavuma kuelekea wapi. Usishangae upepo wa siasa ukavuma kuelekea chaama cha CUF au AFP au TLP, nk. Hii haitajalisha wakristo au waislam wanapenda Chama gani. Ni upepo wa Siasa. Usije kushangaa kama utaona CHADEMA upepo umewageuka.

  Ni lazima CHADEMA kama ilivyo kwa vyama vingine vijipange kisera, kisiasa, kifedha, kimaadili ili kuvutia watanzania wengi ifikapo 2015 Oktoba.

  Napenda kumkumbusha Kellysia na wote wenye mawazo kama yeye wabadilike. Kushabikia CHADEMA au CCM au CUF au TLP, nk isionekane kama dhambi.

  Chama chochote iwe CHADEMA, CUF, TLP, nk endapo kitatwaa madaraka ieleweke kwamba ni wananchi wa Tanzania ndio wametwaa madaraka na wala siyo maharamia au wavamizi toka nje ya nchi watakaokuwa wametwaa nchi yetu. Hivi nchi hii ikitawaliwa na CHADEMA au CUF kuna dhambi gani?

  Kwani ni lazima CCM ndio washinde kila uchaguzi milele na milele? Imeandikwa wapi kwamba CCM watatawala Tanzania milele na milele?

 12. KAMA SIYO MUNGU JOSHUA NASSARI NA ASEME SASA
  kumbuka wewe ndiye utakaye watoa watanzania wengi kwenye giza hadi kwenye nuru ambayo BWANA ameingazia Tanzania,TORATI ya BWANA isiondoke kinywani mwako kuwa hodari na bidii kama kuyatimiza yake MUNGU.

  2Nyakati 26.5

  Akajitia nia amtafute MUNGU katika siku za Zekaria,aliyekuwa na fahamu katika maono ya MUNGU,na muda alipomtafuta BWANA,MUNGU alimfanikisha.

  Mtumikie MUNGU wala usigeuke kushoto wala kulia wala nyuma,BWANA ANAJIBU MAOMBI YA WANAOMLILIA JUU YA TZ

 13. Congl Mp Nassari, We are together, May our good God be with you as you step forward

  CHADEMA Oooooooooooooyeeeeeeeeeeee

 14. ukimwamini mungu ktk roho na kweli kl ki2 ni simple. mungu aendelee kukupigania na kukuongoza.

 15. safi sana, Mungu ameonyesha kweli pesa si kitu chochote kwa mambo ya Mungu, ukimtegemea utashinda tu, mwanadamu hawawezi kuzuia timilifu la Mungu alilopanga, Mungu aendelee kuonekana kwa wengine ncdy.

 16. kamanda joshua kwanza hongera sna kwa ushindi huo wa kishindo!mm naamini ss kma vjana nchi hii inatuulza”utaifanyia nn Tz”mh.kaza buti nasi tunafuata hko kuongeza nguvu 2015.Mungu akubariki sna na akujalie uongozi ulio “BORA”

 17. Kama Mungu alivyokuwa na Joshua kuwavusha wana wa Israel ndivyo atakavyokuwa na wewe kuwavusha watu wa jimbo lako kny changamoto zinazowakabili….songa mbele na uzidi kuwa na moyo wa ushujaa na kusimama katika haki Mungu hatakuacha.

 18. Hotuba ya Mbunge Joshua ilinibariki sana hata nilitokwa machozi.

  Kumuweka Mungu mbele namna hii ndiyo inayombariki Mungu. Hongera sana Mheshimiwa Mbunge Joshua na Chadema kwa ujumla.

 19. Nakupongeza sana mh Joshua na Mungu akizidishie maisha malefu yenya mafanikio,ili wewe ukishilikiana na wabunge wenzako muendelele kuwaonyesha watanzania tofauti iliopo kati ya Mbunge wa kweli na mbunge gamba. Ili watanzania tusiendelee kufanya makosa kwenye chaguzi zijazo

 20. Wapendwa,

  Nampongeza Joshua Nasari kwa hotuba yake nzuri. Kwa kweli niliisikiliza alipomaliza kutangazwa kuwa mshindi kupitia TBC1. Nampongeza kwa hotuba yake ya papo kwa papo aliyoitoa bila kuandika kwenye kalatasi na ikawa imepangiliwa vizuri. Inaonesha ana uwezo wa kuongoza. Wengi hawawezi kutoa hotuba zenye busara etu mpaka waandikiwe.

  Nampongeza sana kwa ushindi alioupata kupitia CHADEMA. Nakipongeza chama hicho pia kwa jinsi walivyojipanga kulinda kura hadi kieleweke. Hata kama kulikuwa na uchakachuaji nadhani ulidhibitiwa. Haki bin Haki ndicho kinatakiwa wakati wa Uchaguzi.

  Hata hivyo, Bwa Joshua Jitahidi kuwa mkweli na uwe “Fair” kwa wananchi wote kata zote bila kujali ushabiki wa vyama. Jitahidi kuwa karibu na uongozi wa chama chako. Jitahidi kutafuta uzoefu wa wabunge wenzako toka vyama vyote. Epuka kuwa na kiburi mbele za wananchi. Epuka kejeli zozote ziwe kisiasa au vijembe nk. kwa waliokuwa washindani wako.

  Ukishindwa kutimiza ahadi zako kwa wananchi, uwe mkweli kuwaeleza ni wapi umefanikiwa na kwa nini umeshindwa kutimiza ahadi fulani. Jitahidi kuwa karibu na wapiga kura wako siyo lazima kuhudhurua misibani lakini kuwa unawatembelea kwenye kata angalau kila baada ya miezi 3 inawatia moyo zaidi. Usijichimbie Dar na ukawasahau wananchi. Tembea hata kwa Muguu wakati wa ziara zako kukagua miradi ya maendeleo. Tembelea mashule ya Sekondari, msingi na vyuo vyako katika Jimbo lako. Sikliza maoni ya wanachi na malalamiko yao.
  Yafanyie kazi yale yanayowezekana. Fuatilia yale yaliyoko nje ya uwezo wako.

  Fanya utafiti wa takwimu na taarifa kabla ya kusema jambo bungeni. Jitahidi kusoma majalida ya ndani na nje. Be an informed MP on all issues global and local issues. Pendekeza mabadiliko pale unapoona panahitajika.

  Nakutakia kila la Kheri.

 21. jina la bwana lihimidiwe hasa kwa wamtumainio bwana ni kama mlima wa sayuni hawatatikisika milele ndivvjo bwana amefanya njia

 22. Kwa kweli ni jambo la kumshukuru sana mwenyezi mungu kwani uwepo wake umeonekana na kijana huyu amekiri na kumshuhudia kwamba yeye ndiye muweza wa yote, sifa na utukufu tumrudishie yeye aliye juu. Naamini kabisa kwamba kama kijana huyu atafanya kazi yake kwa kumtanguliza na kumtegemea mungu badala ya miungu kama ilivyo kwa wengine bac miujiza itakwenda kuonekana Arumeru Mashariki “ATATENDA”. Hongera sana Joshua, sisi wote tunaomtegemea Mungu tuko pamoja na wewe mpaka tuhakikishe shetani ameaibishwa, yaliyoshindikana kwa miaka 50 yatawezekana kwa miaka 2 HALELUYA.

 23. Sifa na utukufu kwako Mungu, songa mbele mtumishi Bwana atakuwa nawe kama alivyokuwa na Joshua iwapo utalishika neno lake. Joshua 1:8

 24. Amen! These are the kind of Leaders that our Almighty God is looking to lead his people since they know whom they are trusting!
  Keep up the good work Nassari….our prayers are with you always and may the good Lord strengthen you as you embark into this challenging role in politics!

 25. Mungu akupe hekima na ujasiri zaidi ukadai ardhi iliyoporwa irudi kwa wananchi wako

 26. Mimi ni mchungaji kijiji cha King’ori. Nilitishiwa kufungiwa kanisa na mwenyekiti wa kijiji changu kwa sababu ya kumuunga mkono Joshua Nassari! Mungu amewapiga piga la aibu…. Bwana asifiwe!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s