Ijumaa Kuu, Pasaka!

Baada ya alhamis kupita, Ijumaa Bwana Yesu alipigwa mijeredi, alichubuliwa, alidharauliwa na kuteswa sana. Wakamcoma mkuki ubavuni, akafa na Jumapili siku ya tatu. Akafufuka. Yu hai hata leo, tunaishi naye!! Kwa kupigwa kwa Yesu sisi tumewekwa huru, tumehesabiwa haki bure pasipo sheria, magonjwa yetu, huzuni zetu alizibeba msalabani. Tumepona

Je kuna haja ya wakristo kukumbuka kuteswa na kifo cha Bwana Yesu Ijumaa Kuu? Kuna wakristo wengine hawali nyama, wengine wanahuzunika sana. Nk

Warumi 14:5 imeandika ” Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa ni sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe” 

Tunaweza kuweka akilini mwetu kwamba siku hii ni siku ya kukumbuka kifo cha Bwana Yesu, Mateso aliyoyapata ni kwa ajili yetu, Damu yake ilimwagika msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.

1 Wakorinto 11:24-26 “Naye akisha kushukuru akaumega, akasema, huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.  Na vivi hivi baada ya kula akakitwa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo”

1 Petro 3:18 “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa”

Wakristo wengi tunaikumbuka siku hii na pengine kuimba nyimbo za kuhuzunisha za kusulubiwa kwa Bwana Yesu, kufanya maombezi na kumshukuru Mungu.

Tunakumbuka siku ya kusulubiwa na kufufuka kwa Bwana Yesu maana Imani yetu iko hapo.

Ijumaa kuu zijazo:
2012 = April 6
2013 = March 29
2014 = April 18
2015 = April 3

Advertisements

8 thoughts on “Ijumaa Kuu, Pasaka!

 1. Wapendwa,

  Mapokeo katika kanisa ni mengi sana kama alivyosema ndugu John Haule. Pia si kwamba mapokeo yamesimama, la hasha, yanazidi kulimiminikia kanisa!

  Tumezoea kuyapokea Mapokeo tukiyachukulia kama ni jambo fulani tu, labda na yale maelezo mafupi ya kisomi kuyahusu ambayo hutuchosha na hivyo kuishia kuyapokea na kuendelea nayo katika ibada zetu tukijiridhisha kuwa ni Neno la Mungu. Lakini ukweli ni kwamba Mapokeo ni Roho, hata ikiwa ni ya Kristo au yaweza kuwa ni ya Ibilisi! Tunapaswa kuyakagua kwanza kabla ya kuyameza. Maana ni hatari kumeza kitu kwanza halafu uulize baadaye eti kina madhara gani? Kama ni mbegu, kama yalivyo Mapokeo, yametuotea na sasa hayang’oki!!

  Kanisa, yang’oeni hayo mapokeo au yawekeni wazi kwenye makusanyiko yenu ili uongo ujitenge. Sikukuu zetu zote zimetekwa. Kiroho hao walioziteka, hawazi sherehekei kama wanavyojionesha, bali huwakilisha ibada zao za giza wakituunganisha sote katika hizo bila kujua!!!

  Angalieni Mapokeo mapya yanayolijia kanisa, USHOGA na USAGAJI!!! Kwa sehemu yamekwisha kupokelewa na kanisa, ni suala la wakati tu tutayapokea nasi na kuyazoea! Kwa nini? Tumeshindwa kuyakataa yaliyotangulia, nasi kwa ushahidi wa Maandiko tukiyaona kuwa ni Mapokeo yasiyodhihirika ki Maandiko, lakini tukayapokea hivyo hivyo! Tunaitisha mikutano mikubwa ya Injili kwenye viwanja vya wazi na kuombea magonjwa na mafanikio, kwanini tusiombee kanisa litapishwe hili gonjwa la Mapokeo lililolimeza???

  Nawasifu kanisa moja linaitwa Siloamu, kama niko sahihi, wao angalau wameikataa hii sikukuu ya Krismasi ya uongo ya siku ya tarehe 25 ya Desemba, walipoamua kuukataa uongo wa Kirumi waliolidanganya kanisa na kulisherehesha kwenye sikukuu yao ya kipagani ya mungu wao anayeitwa Jupiter! Siloamu wamesherehekea Krismas mwezi wa pili, yaani Februari, ingawa nao hesabu yao waliyopiga itakuwa na makosa kwani wamechukulia kuwa Malaika Gabrieli alimwendea Mariamu katika mwezi wa sita, lakini mwezi huo wa sita unaotajwa katika maandiko ni mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeth mama yake Yohana Mbatizaji! Lakini bora ya hao kuliko sisi tulioamua KUCHUKULIANA NA UONGO!!!

  Mbarakiwe nyote!

 2. Sam Mpendwa mwaminifu wa Bwana,Ni kweli Bwana Aturehemu, Mapokeo ktk kanisa ni mengi mno toka kwa shetani/wapagani,Adui hatuzuii tusifanye ibada kumwabudu Mungu, anatuzuia tusiabudu Mungu ktk Roho na kweli, Napata moyo/ujasiri na haya maandiko Yoh17 hasa ule mstari wa 15-17.
  Wapendwa Tuyafikiri /kutafakari yalio juu, yaulimwengu huu yasitukwaze vinginevyo Bwana angesha tutoa ktk huu ulimwengu,kuna maandiko alisema(Bwana) mkuu wa ulimwengu haja lakini hana kitu kwangu,shetani hana kitu kwetu,Utukufu tunampa Bwana na uhai wetu umehifadhiwa na Bwana Yesu.Tumefufuliwa pamoja naye(Kristo).tumetengwa mbali na asili ya dhambi.Inatupasa kuushinda ulimwengu.
  ‘Tusimuonee AIBU Kristo’….Amina… neno la faraja kwetu ni kuwa Roho Mtakatifu anatusaidia.Peke yetu tusingeweza.Bwana Yesu anasema pasipo Mimi ninyi hamwezi jambo lolote.kumbuka ibilisi ndiye mkuu wa ulimwengu huu Lk4:6-8,Yatupasa kumwambia shetani na wajumbe wake kuwa Lk4:8
  Neema ya Bwana izidi kwenu wapendwa,Bwana awaketishe mahala pa siri pake,Mketi ktk uvuli wake,Awafunike na uzuri wa utukufu wake.
  Amen

 3. Ndugu Haule na wote,

  Katika kulifuatilia jambo hili la Pasaka, juu ya yale maelezo uliyoyatoa, nimekutana na haya katika Gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 April 2012:-

  “Tarehe ya Pasaka inafuata mwandamo wa mwezi, hivyo sikukuu hiyo haina tarehe maalumu katika kalenda ya kawaida. Hivi sasa sherehe za Pasaka hufanyika kati ya Machi na Aprili baada ya viongozi wa kwanza wa Kikristo kuamua kusherehekea Pasaka jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza, baada ya tarehe 21, tarehe ambayo saa za mchana na usiku ni sawa.

  Kwa sababu mwezi mpevu baada ya tarehe 21 Machi, inaweza kutokea kati ya Machi 22 na Aprili 19, tarehe ya Pasaka ambayo ni jumapili inayofuata, hutokea kati ya Machi 22 na Aprili 25 na tarehe hizi zilianza kutumika mwaka 325 Baada ya Kristo (AD).”
  *NB. Mwandishi wa makala hii, source ya habari hii ni katekesimu ya Kikatoliki na rejea zake.

  VERSION nyingine ambayo ameniambia mkatoliki ni kwamba: wanahesabu siku arobaini kuanzia Jumatano ya majivu hadi kufika Jumapili ya Pasaka. Kwa hiyo katika kuitafuta Jumatano hiyo ya majivu (ambayo sijui andiko lake ni lipi), ili kufika katika uwiano huo na Jumapili itakayokuwa ndio Pasaka, ndiko kunakosababisha huko kuhama hama!

  Kwa hiyo Pasaka hii tunayoisherehekea, sisi pia tunaokiri Wokovu, yaani tuliojazwa Roho Mtakatifu, ambaye hutuweka katika kweli yote; tunapaswa kujiuliza kuhusu sikukuu hii kubwa, imekuwaje hata tunaisherehekea katika jinsi isiyoeleweka ki Maandiko?

  Wasomi wetu wenye kuyajua mambo makuu ya kanisa katika trail yake; ukusanyaji wa nyaraka, upambanuzi wa makanisa, Othordoksi, nk, wameshindwa kuliondoa kanisa katika makucha ya ibada za mizimu? Sijui “Mwezi Mpevu” au ‘Mwezi Mchanga’? au “Jumatano ya Majivu”, vina uhusiano gani na Kristo?

  Kimsingi ushiriki wowote wa Ibada iliyotayarishwa nje ya misingi ya Kikristo, hata katika hatua yoyote ndogo, hilo linatuingiza katika shtaka la Ibada hiyo!

  Tusimuonee AIBU Kristo, kwa kuongozana na umaarufu wa kilimwengu, tumuombeni msamaha atupe Roho Mtakatifu wa Kweli atuongoze katika njia yake!

  Basi itafakarini hali ya kanisa, linalo ongozwa katika ibada za mizimu bila ufahamu!!!

  Bwana aturehemu!

 4. Mpendwa Sam…Pasaka kuhama hama
  Ni kazi yake Papa Gregory alipokuwa anamrekebisha Julius Caesar na Julian Calendar yake kwenda kalenda hii tunayotumia sasa ya Gregorian
  calendar,Fahamu kuwa miezi ya kalenda ya rumi ya zamani ilikuwa 10..wenye ufahamu zaidi tafadhari mwaweza kutujuza.

 5. Sikukuu ya Pasaka, ambayo inajumuisha siku ya Ijumaa Kuu, kimsingi, ninavyoifahamu, inatokana na agizo walilopewa Israeli ili kuwa kumbukumbu kwao ya jinsi Mungu alivyowatoa Misri kwa mkono wenye nguvu kama tunavyosoma katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati, 16:1 “Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako.”

  Nasi wakristo Pasaka tunayoiadhimisha, pia ni agizo lililo katika maana hiyo hiyo isipokuwa kwetu sisi ni adhimisho la kusulubiwa kwa Mwanakondoo Halisi, tukio ambalo lilitokea majira ya maadhimisho hayo katika mwezi wa Abibu ambao ni mwezi wa Aprili. Je, ni kwa kigezo gani hata sikukuu ya Pasaka tunayoisherehekea ina hama hama, mara mwezi wa March mara wa Aprili! Na pia ningependa kufahamu ni nani anayepanga sikukuu hii, maana kama inavyojionesha katika maelezo yaliyotolewa katika posti hii, inahama hama!!

  @ Shadrack & Clara
  Mambo ya kula nyama ni sheria au kanuni waliliyojitungia makanisa, haina uhusiano wowote na Maandiko labda mizimu! maadhimisho ya sikukuu hii tunayafanya kila mwaka kulingana na agizo la kumbukumbu hiyo kama lilivyo katika Maandiko ambalo chimbuko lake ndio hilo andiko hapo juu.

  Mbarikiwe nyote!

 6. napenda nijue kuna uhusiano gani kati ya kutokula nyama siku ya ijumaa kuu na mateso ya Yesu? na pia katika 1 Petro 3:18 “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa” sasa mbona sisi tunafanya kila mwaka?

 7. Bwana asifiwe!.hebu tusaidieni kutuondolea giza lililotanda usoni mwetu,je ni hairuhusiwi kula nyama siku ya ijumaa kuu. Kama hairuhusiwi nisaidieni kupata maandiko kutoka kwenye biblia.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s