Unabii wa TB Joshua na Rais wa Malawi

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika amefariki.

Mwezi wa pili mwanzoni nabii maarufu kutoka Nigeria TB Joshua alitoa unabii kuhusu kifo cha Rais wa Afrika kama ifuatavyo  “God loves us, you should pray for one African head of state, when I say President again the sickness that is likely to take life; sudden death, it could be sickness being in the body for a long time but God showed me the country and the place but I’m not here to say anything like that.”

Unabii wa TB Joshua vina mahusiano na Rais wa Malawi?

Msikilize TB Joshua kwenye video hii!

Advertisements

30 thoughts on “Unabii wa TB Joshua na Rais wa Malawi

 1. Ndg Leons,
  Nguvu kama nguvu ni jambo complex.
  Tumeona boti huko Unguja ikipinduliwa kwa upepo, au umeme ukiendesha mitambo mikubwa au kumkausha mtu kuwa kama mkaa kwa kuugusa tu. Hata nimewahi kumuona mtu mdogo kwa umbile, lakini alipopagawa na pepo, aliwasukuma watu watano wa miraba minne na kuwaangushia huko mbali! Lakini alipokuja mwinjilisti, ndani ya dakika 5 na kwa maneno yasiyozidi 10, kulikuwa shwari!!!

  Kwa hiyo suala la “Nguvu”, tukijaribu kuliangalia kiBiblia, tunaweza kusema linatafsirika kama VIPAWA. Nayo Maandiko yanatuambia Vipawa havina majuto. Yaani si lazima ufunge na kuomba ili upewe kipawa, unazaliwa nacho tu, haijalishi ni mcha Mungu au la.

  Maandiko yanaposema kutatokea Makristo wa Uongo, wengi wetu hudhania watakuwa ni watu wenye kujitambulisha kuwa wao ni Kristo, lakini si hivyo. Maana ya neno ‘kristo’ ni Mpakwa Mafuta yaani “Annointed”. Kwa hiyo hao watakuwa ni “Wapakwa Mafuta wa Uongo”, yaani watakuwa na UPAKO wa kuwadanganya watu kwa kuwahubiria watu injili isiyozaa matunda na hivyo kuwasababishia kumkosa Roho Mt ambaye kwaye mkristo hutiwa muhuri wa ukombozi. Pia pamoja na hao wako Manabii wa Uongo ktk kazi hiyo ya kuwaongopea watu kwa kwa kuwahubiria wapendwa injili hiyo inayoambatana na ishara na miujiza mikubwa; kwa hiyo Nguvu au Vipawa au Upako! 

  Kwa hiyo matumizi ya Jina la Yesu katika jinsi ya Nguvu, bado hayatufanyi kumpokea mtumishi yeyote moja kwa moja kwani linaweza kutamkwa Jina hilo na bado nguvu ikawa inatoka kwingine. Maana twafahamu Lusifa alipoasi hakunyang’anywa chochote, alibaki na vipawa vyote yaani Nguvu ambayo anaitumia hata sasa. 

  Ndio maana Maandiko yanatuambia kuwa siku hiyo watasema, Bwana tulitoa pepo kwa Jina lako…, sasa hawa si watu wa kawaida wa mitaani, hawa watakuwa ni manabii na mitume na wainjilisti na wachungaji waliovutwa kwa huo UPAKO na kukabidhiwa injili hiyo isiyozaa matunda nayo miujiza inayoambatana na injili hiyo kuwapofusha wasiweze kuikagua ktk Maandiko.

  Basi ndugu yangu kwa uchache hivyo ndivyo ninavyofahamu kuhusu Nguvu au Vipawa au Upako. 

  Ubarikiwe!

 2. Bw CV Lwembe Kwa hiyo ili Pepo Litoke Kuna Nguvu Ipi Ambayo inatumika Kulitoa Katika Jina La Yesu? Najua Jina La Yesu Lina Nguvu lakini Je Hiyo Nguvu Inakuwa Katika Mfano Gani? Au Kina mtume Paulo Walipokuwa wakikemea mapepo katika jina la Yesu Hiyo Nguvu inatokana na Kujazwa nini na mfano wake ni nini?

 3. Ndg Leons,
  Ni jambo zuri kwamba unajua kwamba Miujiza hailibadili Neno la Mungu. 

  Video uliyoileta ili tuijadili, mimi nadhani ndicho nilichokifanya, nimeijadili kwa kuleta kifungu hicho cha Maandiko cha Mt 24:24. Kwa hiyo vifungu vyote ni Neno, ila itategemea uelewa wako wa Maandiko, kwani hakuna Roho Mt nje ya Maandiko ambayo ndiye Roho Mt.!!!

  Ndio maana nikakuambia kuwa rudi ktk Maandiko uone kama Kristo au mitume waliwahi “Kushusha Moto wa Roho Mt ” ili kufukuza pepo! Au hiyo ndiyo Miujiza Mikubwa zaidi aliyosema Kristo? 

  Katika mambo ya rohoni Leons, ni lazima uwe na nanga, ambayo ni Neno la Mungu. Hiyo video uliyoileta ni kielelezo kizuri sana kwa wote wenye shauku ya kuujua ukweli, nami binafsi si kwamba nalaani, hapana nakushukuru sana na Bwana akubariki kwa jitihada uliyoifanya.

  Kuhusu nabii Mwingira, mimi si muumini ktk huduma yake, bali nilimtumia ktk kuonesha mfano tu, kwa hiyo kama naye anashusha Moto kama kwa TB Joshua, basi hizo ni gimmicks tu zinazowapumbaza watu pamoja na matumizi ya Jina la Yesu! 

  Pia si vizuri kujifunga ktk uelewa kwa kukataa jambo kwa vile tu unadhani uko sahihi. TB Joshua ni nabii lakini si wa kuliongoza kanisa kufika utukufuni maana hana Neno la Mungu linalopaswa sisi kupewa tunapomngojea Bwana. Kutoa pepo au kutabiri mambo ya mwilini ni vitu vidogo saaaana; tuambie tufanyeje ili tupate IMANI YA KUNYAKULIWA sio imani ya uponyo au kushinda mipira au watu kufa!!! 

  Mambo hayo hata wanajimu huyatabiri. Mapepo kuwagalagaza watu na kuwatambaisha kama nyoka si jambo la ajabu, hata waganga wa kienyeji huyafanya hayo au inakuwa tofauti na hiyo Marko 3 : 20-30, inakuwa kama waganga wa kienyeji wana Roho Mt ndio maana wanafukuza pepo? Nenda na Maandiko polepole ili yenyewe yakupambanulie hali unazokabiliana nazo, kwa maana hayo ndiye Roho Mt!

  Kuhusu upofu, mtu yeyote yule anaweza kuwa kipofu, pale anaposhindwa kuona Neno la Mungu lisemacho, bali kwa Neno hilo hilo hufunguliwa upofu wake, nayo furaha inayoambatana na hilo hujidhihirisha katika kumtukuza Mungu, tofauti na mtu anayelikataa Neno limponyalo na kuamua kuendelea na upofu wake, kwa hiyo furaha yangu isikukwaze sana, yatazame Maandiko na uyaamini hayo!!

  Ubarikiwe!

 4. Mpendwa CV Lwembe sijasema kwamba miujiza inabadili neno la mungu, mimi nimepost hiyo video watu waijadili sambamba na yesu alivyouliza Shetani Anaeza Kumtoa Shetani???? kwa swala la Mathayo 24:24 inayozungumzia manabii wa uongo ambao wataonyesha ishara kubwa na maajabu yamkini kuwa hadaa watu hata walio wateule hapo ndipo ninaposema criticism ya huyu T.B Joshua watu wengi wana base kwa sababu ki ukweli miujiza yake ni mikubwa lakini Je Yesu Hakusema kwamba Wanaomwamini ktk Roho Nakweli watafanya miujiza Mikubwa kuliko yake kwa maana yeye anaenda Kwa Baba? Huyu bwana Anakemea Kwa kutumia Jina La Yesu Mara Nyingi kwa kusema ” Holy Ghost Fire In the Name Of Jesus” na walokole wengi hapa TZ huwa mara nyingine wanakemea mapepo kwa namna hiyo hiyo, Kwa Mfano Hata Huyo Josephat Mwingira Unaemwamini nilishahudhuria sana mahubiri yake na Maombi Yake na tena alishawahi kuja Chuo Cha Mzumbe kutoa huduma na mara nyingine nilimsikia akisema ” Naamuru moto wa Roho Mtakatifu ushuke Juu yako Ktk Jina la Yesu Kristo” Sasa sijui point yako Yakusema sisi tu Vipofu Je Wewe pekee ndo Uliefunuliwa na Je una Uhakika Umefunuliwa?

 5. Mpendwa Leons
  Miujiza haiwezi kulibadili Neno la Mungu! Neno la Mungu ndio Major, miujiza ni Minor. Lakini inasikitisha kuona wapendwa wengi wanaMajor ktk Minor!!

  Ukitaka kuijua vizuri hiyo Marko 3 : 20-30 ni lazima kwanza uijue Mathayo 24:24, vinginevyo kila atakaye kujia na miujiza katika jina la Yesu utaondoka nae!

  Kama ungekuwa na interest na Neno la Mungu, hii video uliyoileta ilitosha sana kukuonesha kuwa hiyo ni huduma ya Mt 24:24; hivi kuna popote katika Injili ulipowahi kusoma mapepo yakikemewa kwa kushushiwa moto? “HolyGhost Fire!!” Enchantment!!!

  Amka usingizini Leons, hao jamaa wanafanya advanced au modern “EXORCISM”!! Hilo kundi unaloliona hapo SCOAN pamoja na ninyi wa kwenye tv, nyote mko under the SPELL, na mnahitaji kufanyiwa DELIVERANCE!!

  Mkono wa Bwana na uwatoe ktk kifungo mlichomo!

 6. Imani, kwanza unapaswa kujua kuwa kutoa pepo si kigezo cha kujazwa Roho Mt. Hata ninapoyarejea uliyoyaandika, yanaonesha kuwa una jazba za kidini, maana umeongea mengi sana kutetea huduma hiyo na hata kutuambia kuwa hatuna Roho Mt ndio maana tunamkataa nabii huyo. Umetupa mifano mingi pamoja na ule wa wana wa Skewa ili kutudhihirishia kuwa hatujajazwa Roho Mt na hivyo si rahisi kwetu kuzitambua kazi zake kama hiyo inayofanyika   na TB Joshua akiwa chini ya uongozi wa Roho Mt. 

  Unapojaribu kutamatisha jambo juu ya msingi dhaifu wa uelewa wa Maandiko, inaweza kuwa hasara kwako, kwani unaweza kujiingiza katika ibada za kipagani kama ninavyokuona sasa hivi, nawe ukiwa hujui! 

  Mfano ulioutoa wa wanafunzi wa Yesu, kuhusu yule waliyemkuta anatoa pepo kwa Jina la Yesu ingawa si mwanafunzi wake, mimi nilidhani mfano huo ungekuongoza kufahamu kuwa kutoa pepo au miujiza si lazima uwe umejazwa Roho Mt kama ilivyokuwa kwa huyo mtu, au alijazwa??!! Ishara sio kigezo cha kujazwa Roho Mt, angalia Fundisho iwapo linadhihirika kwa ukamilifu ktk Neno la Mungu, vinginevyo utapotea ndugu yangu kwa ushabiki wa miujiza!

  Bwana na akupe dawa ya macho!

 7. Hebu Jamani angalieni hii video hapa chini kama mnaweza na mlinganishe na maandiko kutoka Marko Mtakatifu 3:20-30

 8. Hata wakati wa Nuhu walimkashifu kama mnavyo mkashifu Pro. TB Joshua lakini afadhali unyamaze kamahujui mambo ya rohoni, Biblia ina eleza kwamba mtu hawezi kukiri wokovu isipokuwa amejaliwa na Mungu, wote waliopata wokovu wa Mungu wamejazwa Roho Mtakatifu ambae anawajulisha kwamba Mtumishi huyu katoka kwa Mungu na huyu la, kama hujajazwa kwa Roho wa Mungu lazima utasema upuuzi tu maana hujui lolote unakwenda tu yaani kipofu wa mambo ya rohoni. Hata wanafunzi wa Yesu Kristo walimwambia “Mwalimu tumemkuta mtu anatoa pepo kwa jina lako tuka mkataza” Yesu akawaambia mwacheni, waki huo walikuwa hawajajazwa Roho Mtakatifu hawa kujua lolote.

  Nisawa sawa na wewe unaye mpinga TB Joshua siku ukijazwa Roho Mtakatifu utajuta uliyo ya sema juu ya watu wa Mungu lkn najua unabisha maana hujui kazi za Roho Mtakatifu, tatizo watu wengi wana mtambua Mungu na Yesu tu, wana mwacha Roho Mtakatifu kwanza hujui Roho Mtakatifu anafanyaje kazi. Soma Matendo ya Mitume 19:14-16 Wana wa Skewa walipo sikia Mtume Paulo anasema kwa jina la Yesu mapepo yanapiga kelele yana watoka watu, wakaona mbona simpo wakataja nao “NAWAAPISHA KWA JINA LA YESU YULE ANAYE HUBIRIWA NA PAULO” yule pepo aliwajibu akawaambia “Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani”? halafu akawararuwa nguo zao wakakimbia wako uchi.

  So kutaja jina la Yesu sio tatizo hata shetani anaweza kulitaja Tofauti ni kwamba Paulo alikuwa amebatizwa kwa Roho Mtakatifu ndio maana unaweza kukuta mchungaji anakemea pepo siku nzima halijatoka toka asubuhi hadi jioni kama huna Roho wa Mungu utapigwa makofi na mapepo kama unabisha jaribu wewe kanisani kwenu au popote utakapo kuta mtu amepagawa na pepo taja tu Jina la Yesu uone nini kitakutokea maana pepo wana jua Mtu aliye na Roho Mtakatifu kwanza huwa hawamsogelei ndo maana yalisema Yesu tuna mjua na Paulo tunafahamu. Finally hata Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake alipo kuwa karibu kupaa kwenda kwa BABA, wasifanye lolote wasubiri hata watakapo jazwa kwa Roho Mtakatifu “Matendo ya Mitume 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu;……” hiyo nguvu ndo hiyo ya kutoa mapepo, Kutoa unabii, kuombea magonjwa na (What people they don’t know they call it evil and what they know they destroy it).

 9. Bahati naelewa ndugu yangu. Nami kuna wahubiri ambao roho yangu inakataa kabisa tukiachana na huyu pia hapa hapa Tanzania wapo ambao najitenga nao. Tatizo ndio wenye washirika wengi. Kweli Mungu azidi kunipa macho ya rohoni.

 10. kaka Sam mimi nimekuelewa sana sana, sijui kwa nini moyo wangu hauna connection hata kidogo na huyu nabii. Nakubaliana pia na yohana time will tell . tuendelee kuombeana Mungu atupe macho ya rohoni. wala hutahitaji ufafanuzi kutambua manabii .

 11. Wapendwa,

  Kuhusu unabii na manabii, kwanza tunapaswa kufahamu kuwa Nabii, awe wa uongo au wa kutumwa na Mungu wote hawa wawili ni manabii. Pia Nabii wa Uongo, si kwamba anajitungia mambo na kuyaleta kwa waaminio, hapana, yeye pia huja na neno la kweli wakati mwingi na kuaminika na kusanyiko lililompokea kama nabii; bali mwishoni huwaingiza kusanyiko katika ibada potofu na hivyo kuitimiza kazi aliyotumwa kuifanya!

  Kwa hiyo wakristo, wao wamepewa mwongozo thabiti ili kuwaepusha katika MTEGO huo, maana ni vigumu sana kuepuka kunasa kwa kutumia akili zako mwenyewe kama wengi wetu tunavyojiaminisha.

  Pia ni vizuri kufahamu kuwa Neno, Mungu alikwisha kulinena na lipo hapo likatanukia wakati yaani ‘stretched out in time’ na si kwamba Mungu anena kitu fulani kwa nabii fulani wakati huo, la hasha, isipokuwa nabii huweza kupanda juu na kulichukua lile Neno linalohusu kipindi hicho na kuja nalo chini kusanyikoni kwa ajili ya kuwajuza waumini. Hicho ni kipawa ambacho mtu huzaliwa nacho! Kwa hiyo vipawa hutenda kazi katika namna hiyo yaani ‘supernatural’ au ‘charismatic’ au huwa ni udhihirisho wa nguvu isiyoelezeka kwa ufahamu wa kisayansi au kiasili, nasi katika ufahamu wetu wa kawaida mambo hayo hutuvutia sana maana tunayo kiu ndani yetu ya kumuabudu Mungu. Ndio maana ametutahadharisha kuhusu jambo hilo la vipawa!

  Unabii alioutoa TB Joshua kimsingi twaweza kusema kwa uhakika umetokea na hivyo kwa kutokea kwake kumemdhihirisha zaidi kuwa huyo ni nabii! Nadhani sote twapaswa kulikubali hilo kuwa TB Joshua ni nabii.

  Katika ufahamu huu ndipo hatuishii hapo, maana twafahamu mambo yote hulenga katika kumtukuza Mungu. Nimesoma michango mingi, inayohusiana na UTABIRI HUU WA KIFO kabla na baada kifo cha Rais Bingu kutokea, sijaona chochote chenye kumtukuza Mungu! Hata katika kuuangalia utabiri huo, nilivyouona mimi binafsi si wa ki Biblia, hauendani na unabii wowote ule uliowahi kutolewa katika Biblia. Tabia ya Mungu si kuleta hofu au masononeko au kuwakatisha watu tamaa au kuwachanganya watu kwa kuwaweka katika hali ya wasiwasi kama ambavyo unabii huu ulivyopeleka shockwaves katika mataifa yote ya Afrika yaliyo na viongozi wenye umri mkubwa! A blanket prophecy, ukiwa na umri mkubwa, labda kama kawaida ya uongozi ilivyo, haikosi uadui au kuonewa wivu, ukianzishwa uvumi unaokuhusisha na unabii kama huo kutoka kwa nabii anaye aminika, hali yako itakuwaje? Utamtukuza Mungu? Kadiri siku za unabii huo zinavyosogea laweza kukukuta la kukukuta!

  Katika biblia kuna mifano mingi sana ambayo nabii hupewa unabii kwa kiongozi au taifa, kama alivyopewa Yona, Mungu alijipatia Utukufu kutoka kwa watu wa Ninawi! Malawi kuna utukufu gani Mungu aliojipatia kama si watu kujipatia kesi za unafiki mbele ya Mungu na sifa kumwendea TB Joshua!!

  Nafahamu upeo wa mtu wa kuelewa mambo huweza kugota na hivyo kutokuweza kupambanua chochote kile zaidi ya ufahamu wake ulipogotea, kama wale wanaoilaumu serikali kwa kuwakosesha kuvuna mapesa ya Deci kwa “wivu wa wakubwa”; hata katika mambo haya ya vipawa vya jinsi hii, wengi wetu hatuna uwezo wa kuitumia ile fursa ya kuzikagua ‘roho’ zilizo nyuma ya huduma hizi za kinabii, until its too late!

  Angalieni muelekeo wa hiyo ‘Roho’, sasa hivi imejikita zaidi katika URAIS!! Huyo rais mpya wa Malawi ni muumini wa Scoan! Anawatabiria watu mafanikio na vifo na kuwaombea wagonjwa na kupunga pepo, hivyo havitoshi pekee kumweka katika kiwango cha manabii tunaowajua katika Biblia, yapaswa aje na Neno la UZIMA linalohusu kizazi chetu, apande huko juu, atushushie hilo Neno litakalo tutiisha hata sote tuwe chini ya Roho Mtakatifu na Fundisho Moja. Neno litakalotufanya TUNYAKULIWE!!!! Mungu ni mmoja, tusijiridhishe na hii migawanyiko yetu tukijidanganya kuwa eti ni mapenzi ya Mungu, huo ni uongo utakaotugharimu Mbingu!

  Mungu na atupe Macho ya Rohoni!

 12. Baada ya kupitia comments zote kuhusu unabii wa TB Joshua: nataka ninene hivi:
  YAWEZA Kuwa unabii huo ulikuwa sahihi kabisa ukiangalia mazingira yenyewe! ni kweli asingeweza kumwambia rais moja kwa moja! je unakumbuka Nathani alipoenda kumwambia Daudi kuhusu dhambi ya uzinzi? je alienda moja kwa moja na kusema mzinzi wewe japo alikuwa nabii wa Mungu! hapo hekima lazima inene! LAKINI pia yaweza kuwa sio ukweli, tatizo hapa ni kwamba angetaja ni nchi gani kwa majority! hata hivyo kwa upande wangu naamini ni KWELI unabii uko sahihi.

 13. Nimewasoma wakristo wa leo wa Kitanzania jinsi mnavyoamini kila kitu bila kuchunguza. Babu wa Loliondo ni mfano mzuri sana ambaye wengi walimwita nabii.

  Hakuna unabii uliotolewa kwenye Biblia na Yesu ambao haikuwa na utukufu wa Mungu. Kuna sehemu Yesu aliongea kuhusu hekalu kubomolewa akimaanisha mwili wake ambao ulitolewa sadaka ya ulimwengu.

  Pia unaposoma Biblia connect the dots kati ya agano jipya na la kale.

  People will continue to perish because they lack knowledge.

 14. Kama huo unabii wa TB Joshua haukuwa sahihi walikuwa wapi wana wa Mimgu kuuonyesha ulio sahihi? ila kulaumu….Hata hiyo freemason wengi tunaiongelea maana imekuwa mada siku hizi lakini tunaielewa kwa ndani..Mbona hatuna Mikakati dhahiri juu ya mpinga Kristu aliyetabiriwa kwa dhati na almost ametimiza karibu kila nabii juu ya Mpinga Kristo…amepanajisi Patakatifu pa patakatifu kwa kujenga hekalu lao (Misikiti miwili) Anajifanya Yesu ni nabii kwake hali akipinga kila matendo na nguvu za Yesu kwa nguvu zote! hata wakikosea Wayahudi wanaokula kichapo Dunia nzima ni wakristu tuwe macho sana na chenga za mwili za Shetani tutajikuta tunamtumikia yeye kwa nguvu zote…! Hapa Tanzania tayari kuna Baraza la dini linaloshirikisha mpaka viongozi wa kipentekoste…! ambao tulidhania ni macho kwanza Ukristu si dini ni imani ndiyo maana inajipigania yenyewe na Mungu ndiye anayeilinda si kwa mapatano wala njaa wala adha tutavuka kwa yeye anayetutia nguvu..kama ni mateso hayakuanza leo hata mkipatana nao watatuchoma kwa nyuma kwani wao wamekuja kushinda dini zote na vitabu vyao vinasema hivyo..aliyekuja kukushinda mtapatanaje? Tuwe macho..badala ya kutafunana wenyewe kwa wenyewe nui hatari!

 15. Tatizo , ni watu kujiona wameokoka kumpita Yesu, Math 24:1- 2 Yesu alitabiri kuhusu kubomolewa kwa hekalu “……..halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambaloo halitabomoleshwa.” je ! unabii huu haukutimia? ulikuwa na utukufu wa Mungu hapo? Yesu mwenyewe akiwa ndiye Mungu na kwa Roho Mtakatifu alitabiri, angekuwa na UWEZO wa kuzuia Yerusalemu isibomolewe lakini aliacha kama ilivyo, na uharibifu ukatokea , mambo ya Mungu tusitake kujifanya kuyachambua saaaana, na kisha kujifanya kukosoa na kuweka yale tunayotaka sisi yawe,yale tunayofunuliwa ndiyo ya kwetu, na yale tuliyofichwa ni yake MUNGU na MUNGU atabaki kuwa MUNGU JINA LAKE(YESU) LIHIMIDIWE MILELE YOTE..

 16. mnataka kumfundisha roho wa Mungu kazi eeeh? Kwani angeambiwa amuite na kumuombea c angefanya hvyo? kanisa la leo linamuamini shetani na freemasons kuliko Mungu,watu hawajui kuwa wao ndo ma freemasons kwa kupinga kazi ya Mungu,,kama nabii ni wa uongo ni wauongo tu acheni kujifanya mnajua maandiko kwa kukosoa hata msichoelewa kimeshuka vipi toka kwa bwana,nabii hufanya kama alivyoagizwa kaliambia kanisa liombe na kamwe hatafanya kama mpendavyo nyie manabii wa unabii wa wenzenu,,, Mungu awabariki scholars

 17. @Walter,Ndio amefariki unabii umetumia,lakini kumbuka wakati unabii unatoka waliomba kwa ajili ya Taifa la malawi.Kwa hiyo kifo chake Bingu wa Mutharika kimetokea pasipo matatizo kwa nchi ya Malawi.Vinginevyo kulikuwa na power struggle kati ya Mutharika na makamu wake Joyce Banda,mpaka Banda alifukuzwa uanachama na kuanizisha chama kingine.Chama cha Mutharika walitaka kaka yake na Mutharika awe raisi na sio Banda. Banda ameapishwa kuwa raisi wa Malawi pasipo matatizo kutokea.Kwa hiyo Jina la Bwana libarikiwe kwa unabii uliotoka kupitia mtumishi wake nabii T.B.Joshua.

 18. Mungu kusema na mtu juu ya kufa mtu mwingine si kitu kigeni,(Isaya 38:1),(2 Wafalme 1:3-4) kwa mfano tu..
  Biblia imeweka wazi,la msingi ni sisi kuwa na mtazamo mpana wa Kibiblia katika kuchanganua mambo,
  kwenye Biblia imeandikwa..”Msimzimishe Roho,msitweze unabii;jaribuni mambo yote;lishikeni lililo jema;jitengeni na ubaya wa kila namna(1 Wathesalonike 5:19).” msisitizo ni katika”…jaribuni mambo yote.” na “lishikeni lililo Jema” ..tatizo ni pale tunapojaribu baadhi na kuacha mengine..

 19. Katika kitabu cha Isaya sura ya 38,inaelezea habari ya mfalme hezekia ambaye unabii ulikuja kwa kinywa cha nabii Isaya,alitakiwa afe lakini kwa kujinyeyekeza kwa Nabii wa Mungu,Mungu aliyarefusha maisha yake.Bingu wa Mutharika pamoja na watu wengine waliotolewa unabii na TB Joshua kama wangekubali kuombewa,ingekuwa kama vile ilivyokuwa kwa mfalme Hezekia na nabii Isaya.

 20. @Yohana,AMOS 3:7,Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri zake.Yohana acha wivu bwana.kama mchungaji wako hana maono ni kumuomba Mungu ambaye hugawa karama badala ya kuwasema vibaya watumishi wa huduma zingine.

 21. asante sana kwa mchango huo mzuri nami ndio swali langu sawa unabii umetimia amekufa then what? Ingekuwa jambo la Kimungu kama angempigia simu akamwambia Mungu amesema utakufa tengeneza mambo ya nyumbani kwako akatubu akaingia mbingini

 22. Huu unabii kwamba mtu atakufa au kitu fulani kitatokea una faida gani kiroho? Unaleta utukufu gani kwa Mungu? Chunguzeni vizuri kama huyo mnayemwita nabii sio mwanachama wa Freemason. Wakristo wa leo mmeacha mambo ya msingi mkafuatisha namna ya dunia hii,

 23. Unabii unatokana na maono katka ulimwengu wa roho. Inawezekana maono ya nabii ni ya kweli

 24. Ni kweli amefariki!.TB JOSHUA alijaribu kuwasiliana nao natumai amuombee(BINGU’S FAMILY)walikataa unabii wake na kudai kuwa Mungu ndiye anayejua kuzaliwa kwake na kufa kwake.soma net kwa ufafanuzi zaidi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s