Tunajifunza nini kutokana na kifo cha Kanumba?

Kwa vijana waliothubutu, wenye maono na kupenda kuona mafanikio yao. Steven Kanumba ni mmoja wao Tanzania, amecheza filamu kadhaa zenye mafundisho kwa jamii na hata kwa kanisa. Amefariki dunia tarehe 7 April 2012. Inasikitisha kwa kijana mdogo kama yeye kuondoka kwenye dunia hii.

Tunajifunza nini? Maisha ya mwanadamu ni kama maua. Hatujui siku wala saa, na tusipoyatunza maisha yetu kifo chetu ni hasara, lakini kufa kwa mwenye Kristo ni faida maana kuna kuurithi uzima wa milele.

Strictly Gospel inawapa pole watu wote waliohuzunishwa na msiba huu. Mungu awafariji wote!

Advertisements

30 thoughts on “Tunajifunza nini kutokana na kifo cha Kanumba?

 1. KIFO CHA KANUMBA KINAUMIZA KWA WALE WAKRISTO NA WAENDA MBINGUNI KWANI SIO KIFO AMBACHO KINALETA PICHA NZURI KWA VIJANA KWANI MUDA TULIONAO SIO MUDA WA KUFANYA STAREHE KAMA VILE NA KUBADILISHA WANAWAKE BALI NI MUDA WA KUTAFAKARI UKUU WA MUNGU,SIONI KAMA KANUMBA NI KIOOO KWA JAMII

 2. KIFO CHA KANUMBA KINATUFUNDISHA, KUKESHA TUKIOMBA MANA HATUJUI SIKU WALA SAA ATAKAYO KUJA BWANA HIVYO TUTUBU NA KUIAMINI INJILI

 3. Hata mimi ninasikitika kwa maana naona huyu ndugu alikuwa akiitwa sana na kuvutwa na Mungu . Niliwahi kuongea naye na kumsisitiza sana kwamba asimame katika Bwana na kutengeza mikanda ya kikristo ya kumuinua Mungu – Kwa kweli Kanumba alikuwa na ufahamu mkubwa juu ya kitu gani hasa anapaswa kufanya -Lakini pia dunia ilikuwa inamtaka na ilimvuta kweli kweli kaka yetu na mdogo wetu hasa ukizingatia wasichana warembo walijigonga sana kweke na yeye alijikwaa kwao na huenda ndio imepelekea situation

  Kufuatia kauli zake na movie zake zenye ulokole ndani ,na ukizingatia nyimbo za kiroho alizotunga AIC changombe alikokuwa anasali utagundua kwamba alijua yampasa kufanya nini -fuatilia sana mabo mengi ya huko byuma na maisha yake (mtu anyesafiri na bibli kila aendako kikazi ) Kweli alijua sana ilikuwa vema kuokoka -hilo alijua na nina jua manake nilishawahi pia kuongea naye , aliigiza mengi ya kilokole kama watuitavyo ,na nadhani roho yake ilikuwaga inajua -lakini dunia na umaarufu nao ulimuita sana baadae ukamzidi nguvu za kiroho na ndio kama ulivyoona – Maadui wa wokovu huwa ni MTU , MARAFIKI , na DUNIA ndipo shetani anamalizia amabye huungamanisha haya yote . Mafanikio na umaarufu huwa unatumiwa sana na shetani katika kuangamiza na ndi maana ni muhimu sana kuchunga hilo .

  Ni hatari sana kuwa Supastaa -majina haya ya usupastar sijui kwanini hata watu wa mungu watumishi waimbaji utakuta mtu anakubali kuitwa super staa -staa ni Yesu pekee -hebu tujifunze katika tukio hili na kamwe tusiruhusu msaanii kutosistizwa injili . Mimi najua inawezekana mtu akawa juu na akampendeza Mungu -hapo ni kujua kuwa mafanikio yanatoka kwa Mungu -Lakinii utukufu ukimuingia mwanadamu -Mungu hawezi kushare glory na mtu never ! hilo ndilo jambo mungu hawezi kuruhusu . Mtu akifikia kiwango alichofikia kanumba ilibidi awe amezungukwa na maombi makali na ulizi wa kimungu ungekuwa juu yake-Ulinzi wa Mungu ni muhimu sana -lakini ni lazima uwe mtakatifu wa Bwana kupata huo ulinzi . Kama angeitwa wa kwanza kabisa mchunaji kabla hata ya Dakatari huenda maombi yangebadilisha hali ile – all in all tuwahubirie wasanii wajue ukweli kuhusu superstar Kadiri unavykuwa super ndipo njia inazidi kusonga iendayo uzimani -inakuwa narrow -yaani ianbidi mtu akikane kabisa amokee yesu na sio kuishi double life – Mungu artusaidie

  Wengi wao wasanii wanamuhitaji Yesu kuliko tunavydhani . Inanisikitisha sana kwa vile nimawhi ongea naye japo sio kwa kina na urefu mkubwa kama dada grace uliyesema hapoo juu -lakini nakumbuka tulizungumzia maisha ya kiroho na kuwashuhudia wengine anaocheza nao movie -akanijibu akasema ndio hivyo tena inabidi tuwalete kundini waingie – Sasa je yeye mwenyewe aliposema hivyo alikuwa ananionyesha anamjua Mungu -Sasa ndio maana nasema maskini sijuia ameingia uzimani kweli ? ukizingatia aina ya kifo . Yaani inaniuma kumuona akishika Biblia na kuigiza baadhi ya film kama mtu aliyeokoka. Kweli mazingira ya kifo chanke ni hatari UNLESS awe alipata kutubu akiwa kwenye floo ralipoanguka -hiyo itajkuwa neema ya ajabu na sio siri nitafurahi kujua alipewa hiyo chance BUT ili kujua hilo ni mpaka tutakapofika kwa baba na tutawaona wale waliotutangulia.kama alitubu basi atakuwa amepona kama kwa moto na hiyo hakika itakuwa neema na furaha iliyoje .Labda awe alipata chamce wakati hajakata roho manake hakuna aliyeona excatly alipokata roho . Ni maumivu makali ikiwa mtu alijua kabisa nini lkilichompasa kufanya . ukichunguza sana mwanzo wake utaona alikuwa na chance kubwa sana ya kuokoka na kusimama . Inanifanya nione tuanapaswa kuwafikia wasanii ili waokoke wawe kioo cha jamii kwa maana penda usipende wana influence na jamii -ikiwa watamjua Bwana -skendo zitapungua sana
  He tufanye kazi ya uinjilisti kila iitwapo leo

 4. Tujipange sawasawa Bwana Yesu yu karibu, ukilijua hilo huta tanga tanga na madhehebu ya dunia hii ambayo hata bibilia iliyaona ndio dalili ya kurudi kwa Kristo Yesu

 5. Kifo cha kanumba kimeshtua wengi, lakini mimi napenda niwambie watu wote kwamba ,mwenzetu safari yake imeishia hapo na ameweka alama katika tasnia ya sanaa.lakini mtu anapokufa ni juu yetu sisi tuliobaki kufikria maisha yetu hasa kiroho tukoje, maisha yetu ni mafupi sana ,hebu na tuyatoe maisha yetu kwa Yesu Kristo.

 6. KWA KWELI NIMESIKITIKA JUMAMOZI ASUBUI NILIPOPATA TAARIFA KANUMBA AMEFARIKI, NILISHTUKA SANA NIKASONONEKA MOYONI SANA NA KUSKIA UCHUNGU SANA, MAANA NAKUMBUKA MWAKA 2009 NILIMSHUHUDIA AOKOKE LKN HAIKUWA IVYO

  NILICHOJIFUNZA

  1. TUSIMZOEE MUNGU NAMAANISHA TUSIWE WATU WA KWENDA KANISANI AU NYUMBA ZA IBADA KAMA DESTURI BALI TUNAPASWA KUISHI MAISHA MATAKATIFU

  2. TUSIWE WAKRISTO WA KUIMBA PAMBIO, KUKARIRI VIFUNGU BIBLIA HUKU HATUISHI SAWA SAWA NA NENO LA MUNGU.

  3. HUYU NDUGU AMENIUMA SANA YESU ALIKUWA ANAMTAKA NA DUNIA INAMVUTA, MAANA HATA MAONGEZI YAKE ANAPENDA KUMTAJA MUNGU LKN NDO IVYO ALIKUWA HAJATOA MAISHA KAMILI KWA YESU SIJUI DAKIKA YA MWISHO ALIPOKUWA CHINI AMEDONDOKA KAMA ALIPATA NEEMA KUTUBU.

  4. NDUGU JOHN RWEZAURA UMESEMA KWELI HASA, TUWE NA TAHADHARI PALE TUNAPOINULIWA NA MUNGU NA KUNG’AA KWA JAMII,TAIFA HATA KTK MATAIFA TUJUE TUNA MAADUI WENGI SANA. TUSIMAME KINYUME NAO KUWAANGUSHA LKN TUTAWEZA KAMA TUTASIMAMA VEMA KTK WOKOVU.

  ADUI ANAWEZA ONA NYOTA YA MTU INAVYONG’AA NA KUAMUA KUIUA NDICHO ADUI ALICHOFANYA KWA NDUGU YETU KANUMBA TUANGALIE WALIOKUWA NA NYOTA KALI ZING’AAZO KWENYE BIBLIA NI

  YESU KRISTO HERODE ALIPOSKIA KWA MAMA JUSI MFALME WA WAYAHUDI ALIGADHABIKA SANA AKATAFUTA NJIA YA KUMWUA YESU, MUNGU AKAMTOROSHA YESU MISRI
  MUSA ALITAKA KUUAWA NA FARAO MUNGU AKANUSURU MAISHA YAKE.
  MFALME DAUDI AKATAKA KUUAWA NA SAULI MUNGU AKAMNUSURU.

  5. KUOKOKA NI SASA SIO KESHO AU BAADAE

 7. Kwa kweli ukiwaza kuhusu kifo cha Kanumba,ambaye wakati mwingine labda,tulitamani mafanikio yake,tukanunua hata CD zake ili kuburudika na yaliyomo ktk Cd hizo,ambazo tuliona kama mafunzo,kwa maisha,lakini ukiwaza kifo chake unajifunza moja kubwa kwambahakika maisha ya duniani,yana mwisho,lakini ya maisha baada ya maisha ya duniani ni muhimu sana kuyatathmini kila wakati.Ukiwaza kifo cha Kanumba na hasa kama wewe ni mtumishi wa Mungu,ulishawahi kukutana nae,lakini matokeo yake hukumpa Injili,kinyume chake mkaongea tu habari za filamu zake nakumpongeza kwa kazi zake,na ukamuweka Yesu mfukoni pasipo hata kufunua kinywa chako,ili umpe injili Kanumba,na pengine ukamuona Kanumba kama ni mtu aliyefanikiwa sana,nafikiri kama hukumpa injili,utakuwa unajilaumu sana ndani ya nafsi yako kwamba kwanini sikumpa injili iliyo hai Kanumba,na hapo tk kifo chake mtu maarufu kama huyu ndipo tunapoona kwamba hakika maisha bila ya Yesu ni bure.Hatuna uhakika kama Kanumba alikuwa na Yesu au la !lakini kama kafa na Yesu ni vema sana,labda hata kama,mazingira ya kifo chake yana utata lakini hatujui mwisho wake kama alikumbuka kusema “Bwana Yesu,naomba uipokee roho yangu,sala ambayo ni ya muhimu sanakuliko blabla za watumishi wa mungu wasiotaka kuwaeleza watu ukweli kwama kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake ,wala mtu hahukumiwi kutokana na sala za watu kwamba muweke pema peponi,hilo nitalipinga kabisa hata kama mkuu gani wa dini aseme nitampinga sana kabisa maana linapinganana na maandiko Rumi 2;6 ‘Mungu atakayemlipa kila mtu kwa kadri ya matendo yake’ Ufunuo 20;12 ‘wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao’ Zab 62;12 Maana ndiwe umlipaye kila mtu sawasawa na haki yake,Ebr 9;27baada ya kifo ni hukumu’kumuombea mtu aliyekufa alazwe pema peponi ni sawa na kuwapa watu hope,faraja yauongo ili wasiwe na uchungu sana na waamini wamba ndugu yao kalazwa pema kumbe ni ujanja wa ibilisi, kila mtu atapata max kulingana na aivyo jibu ktk mtihani wake,duniani ni kama chumba cha mtihani ,mara baada ya mtu kukusanya karatasi ya majibu (KUFA) huwa hakunajinsi tena yakuombewa na mtu hata mzazi wake ili yale aliyokosea yabadilishwe kuwa ni pata,Mungu ahamhesabii mwenye makosa kuw si makosa,bali kwa kinywa mtu akiri Rumi 10;9 2 Pet 3;9 Mungu hapendi mtu ye yote apotee,bali wpte wafikilie toba’ ili kuingia mbinguni ni lazima mtu atubu mwenyewe ,ndipo msamaha unapotolewa na Mungu,kwahiyo kama hujawahi kutafakri juu ya kuombewa mahali pema anza kujizoeza ili uuamini ukweli ndio huo.Tunapozaliwa tunakuwa hatuna dhambi,lakini kadri tunavyoendelea kukua nakujua mema na mabaya,ndipo dhambi inapoanza kuhesabiwa,kwa hiyo kama hutachukua hatua yakutubu dhambi zile zitakufuata nkuwa ukumbusho kwa Mungu kwa jinsi gani atakuhukumu,anaangalia file lako tu,kwahiyo UKIKATA ROHO TU,HUKUMU INAANZA PALEPALE,YAANI KABLA HATA WATU HAWAJANZA KUSEMA MLAZE PEMA PEPONI TAYARI MTU ALIISHA HUKUMIWA SIKU NYINGI,KWAHIYO KITENDO CHA MTU KUHUKUMIWA NI CHA SEKUNDE.Nimejifunza kwamba,tusiwe tunabweteka na umaarufu wa mtu na vipaji vya watu wasiomcha Mungu,tutamani vipawa vya wacha Mungu,Mungu atatuona tuna akili za kiroho wala si za kimwili,maana watu maarufu nao wana kufa na ndipo hitaji la Mungu ndipo linapoonekana kwa dhahiri kwao,maana hata kama mtu aliyefariki alikuwa hahudhurii ibada ,mara baada ya kufa tu tayari mambo ya kanisa yanaanza kufikiriwa kwake kwa ajili ya ibada ya mazishi,hapa tunapaswa kumkumbuka Mungu sisi wenyewe kabla hatujafikwa na mauti.Wakati wa misiba huwa naona watu wote huwa wanyenyekevu,hata wakina dada na mama wapendao kuvaa nguo zisizo za staha,lakinI ktk msiba huwa wanavaa kwa staha na kwa hofu kubwa,uvaaji na hali ambayo Mungu hupendezewa nayo,kwa hiyo ile hali ya unyenyekevu na uvaaji wa staha msibani ndiyo hali ambayo Mungu anaitaka tuwe nayo wakati wote yaani watu wananyenyekea sabaBu maiti ipo mbele yao lakini baada tu maiti kuzikwa,basi watu wanasahau kabisa hali ya hofu,yaani tungekuwa tunamuhofu Mungu kama tunavyo ihofu mauti au maiti,Mungu angependezwa zaidi na sisi.Inawezekana kabisa kama Kanumba angefunuliwa ktk neema ya Mungu labda angekuwa bonge la muhubiri na kushangaa ni kwa nini alichelewa kuokoka,sasa ikitokea hata nasi wenye neema ya Mungu kutaka kujifunza sana ktk filamu zisizo na hata pumzi ya Mungu kidogo,hata Mungu inamsikitisha,kama wewe mpendwa,umeshindwa kubadilika kutokana na NENO la Mungu je filamu zisizo na pumzi ya Mungu (NENO)
  FILAMU HIZO ZITAKUBADILISHA,NILICHOJIFUNZA NI UMAARUFU NA ANASA ZA DUNIANI NI SAWA NA ZERO,MUNGU ATUSAAIDIE ILI TUMKUMBUKE WAKATI TUKIWA HAI NA NGUVU,KABL GIZA HALIJATUFIKIA.

 8. Kwangu mimi nimejifunza mengi, Kwa kifupi si mwangaliaji wa picha, lakini jina Kanumba halikuwa geni kwangu, kwani hata ukiwa msoma magazeti hawa wasanii ni majina maarufu katika jamiii ya watanzania leo.Lakini Kubwa katika msiba huu kwangu imekuwa ni yafuatayo…..

  1. Watanzania ni waangaliaji picha za senema….kama kweli waliojitokeza ni waangaliaji wa senema, na kama umati HUU wa watu hawakujitokeza tu kwa ajili ya udodosi (curiosity) basi michezo ya senema ni media nzuri mno ya kuwafikia watu.

  2. Kama hilo la kwanza ni kweli, Je Marehemu Kanumba ameacha nini kwa Jamii…?Picha zake zilikuwa na mafunzo gani……? Kulikuwa na senema za kurekebisha Jamii…? Au ni yale yale maisha ya kutukuza anasa……ufuska…….mali na kutafuta utajiri.,…? Kama Kanumba kwa njia ya sanaa alifundisha kinyume cha hayo ……basi ameichia jamii kitu bora….!

  3.Jambo jingine ambalo nimejifunza kwa umati uliojitokeza ni kuwa Watanzania wana kiu ya Role Models….! Jamii ina kiu ya kuongozwa……ina kiu ya kuwa na mtu ambaye watu wanapenda kujitambulisha naye….anayekoga nyoyo zao…..na Kanumba ameonyesha hilo……Kwa kifupi nilijiuliza Hivi kama (siombi katika hilo) Je Kama Zitto Kabwe angelifariki angevuta makundi yote ya jamii kumuombelezea hivyo….? Au hata kiongozi waziri yoyote…? Au Proffesor mtukuka kama Shivji angelifariki (siombi katika hilo) …….angelivuta watu hivi…? Nadhani mioyo ya Watanzania wengi inatafuta mtu wa kuwafariji na kuwafurahisha….hata kwa kitambo tu Kwa Sinema na watu kujisikia ahueni na uchovu wa maisha….kukata tamaa……au kutoa faraja ya muda…..kukosa tumaini la siku ya kesho……Marehemu Kanumba nadhani alifanya kazi ya kuziba pengo hilo vizuri… Jamii ya Watanzania imemshuhudia vizuri…!

  4. Jambo jingine ambalo Kifo cha Kanumba kimesema wazi ni kuwa maisha haya ya “kumeremeta”ambayo wengi wa vijana wa leo wanayakimbilia hayana furaha ya Kweli….maisha ya kwenda clubs……kuzuungukwa na warembo….ambao wengi hawatoi mapenzi ya kweli…..na ambao hukuganda ili kijipatia umaarufu…au kuonekana wako na wewe …ndani yamebeba “ukavu” na “utupu” (emptness) …Si kama inavyoonekana mbele ya watu…! Pesa….Umaarufu…..magari ya fahari na kupendeza mbele ya watu hakuleti furaha ya kweli….!

  4. Somo jingine ni kwamba kuumiliki umaarufu katika umri mdogo ni kazi kubwa mno……inatakiwa uwe na “mentor” au washauri wa kukuongoza…..Umaarufu unaokuwa pole pole kwa taabu na shida ni rahisi kuumiliki na kuutawala…..Kwangu mimi Kanumba na sifa zake na umri wake ulihitaji sana mtu wa kumshika mkono….! Ma celebrites wa Marekani /Ulaya huwa na timu kubwa nyuma yao kuwaongoza na kuwashauri……

  5. Kifo cha Kanumba kwangu imekuwa ni pima joto iliyoonyesha wazi Watanzania wanahitaji Injili……na Kama huduma ya Injili kwa njia ya Sinema ikitiliwa mkazo basi itafikiwa wengi……Kwangi mimi nimeona Watanzania wengi ni waangaliaji wa Sinema…..basi tufanye hima kuwafikia kwa njia hii…….

  MBARIKIWE

 9. Ndugu Noel na Wana SG wote,

  Hilo uliloliongea Noel ndilo la msingi sana. Watu wengi hatuchukua hatua ya kuwaeleza watu tulio nao karibu au watu maarufu kama marehemu Kanumba umuhimu wa wokovu au umuhimu wa kutengeneza mahusiano yao binafsi na Bwana Yesu, lakini sisi hao hao tunakuwa wa kwanza kumuomba ati Mungu ‘ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu’. Wapi kwenye Biblia palipoandikwa kwamba unaweza kumuomba Mungu akabadilisha hukumu ya mtu aliyeshakufa? Unaweza kuomba akafanya hivyo kabla ya kufa lakini si baada ya kufa. Huko ni kujifariji tu, na mtu ukiendelea kusema sana utaambiwa unahukumu!!!

  Wapendwa, roho ya marehemu yeyote itakuwa wapi baada ya kufa ipo mikononi mwa marehemu mwenyewe kabla ya kufa na wala si vinginevyo.

  Mambo ya kujifunza kutokana na kifo cha Kanumba yapo mengi sana na hilo linategemeana na anayetaka kujifunza yupo upande upi, yaani upande wa dunia isiyomjali na kumhofu Mungu au upande wa wale wenye hofu ya Mungu. Kwa leo nisingependa kuchangia lolote zaidi ya hilo ili niendelee kusoma kwanza michango ya wengine.

  Baraka kwenu nyote.

 10. Ndg zangu, tuwe wazi kama mimi nilivyokuwa wazi,ili tujifunze KWELI kupitia kifo si cha kanumba tu, Je ni kweli Mungu anamuweka mtu kulingana na sala za watu kwamba ‘Mungu mlaze pema peponi’ au kulingana na matendo yake ?

 11. Nimejifunza kuharakisha kuhubiria watu Neno wabadilike fasta, si kukaa tu na ku-admire talents zao, umaarufu wao na kalizimatic power zao, swala ni injili kwa kila kila kiumbe mwanzo mwisho kwa kwenda mbele then ndo tufurahie life na talents zetu hapo duniani, I real doubt ktk mazingira alokufa Kanumba sina uhakika alipata time ya kuclear maishuz yake na Muumba ili atinge mbinguni……. very sad indeed.

 12. Inasikitisha,pia ni wakati mzuri kwa wale tuliobabikia kuangalia upya maisha yetu na kujihoji kama tunaenenda katika njia ya Bwana. Kwa mdau aliyechangia hapo juu kuwa tumwombee marehemu naomba arejee kwenye maandiko yanasemaje.Baada ya kufa ni hukumu.Waebrania 9:27.Habari ya kumwombea mwanadamu baada ya kufa ni mafundisho ya kupotosha kweli ya Mungu na aliyeko nyuma ya mafundisho hayo ni Shetani ambaye ni baba wa uongo ambaye ndani mwake kweli haimo.

 13. Kwa kweli ya kujifunza kwenye kifo cha mdogo wetu ni mengi sana sana .
  Nilistuka mazingira ya kifo chake na swali la kwanza likawa ;Je ameurithi uzima wa milele ? Manake ni lazima awe na cheti cha kuingilia kule , so niliwaza na kuumia nikisema sijui amepona kweli au vipi ? manake vifo vya ghafla ni vya hatari sana sana kama mtu alikutwa bado hakujiandaa. Na hasa wale wanaosema nikitaka kufa nitatubu .

  Kama walivyosema wengi hapo juu .Kumpokea Yesu kuwa mwokozi wa maisha ni swala la kwanza na mhimu sana .Kuutunza wokovu na kuishi maisha matakatifu pasipo kujichanganya na DHAMBI . Ni swala la kutilia maanani sana – Hali aliyoondoka nayo mpendwa wetu ni ya ghafla mno. So usiseme nitatubu baadae .Saa ya wokovu ndio sasa a-Ukisema nitatubu na kujitakasa nikikaribia kufa unaweza kushangaa unakufa ghafla bila kupata chance ya kutubu
  makosa -tujiulize kama tukifa leo ghafla tutakwenda wapi
  Pia naona swala la mapenzi sio zuri mbele za Mungu , Halafu naona hasira sio kitu kizuri
  asanteni

 14. Kama Mwanadamu nimeguswa na kifo cha Kanumba, lakini kikubwa ni yale mazingira yaliyopelekea kifo chake kwa mjibu wa Tarifa za polisi kwamba “Alikuwa na mzozo na rafiki yake wa kike chumbani mda mfupi kabla ya kifo chake!” Nilichojifunza ni kwamba wengi wetu, mara nyingi kama si mara zote hatuko makini na andiko lilipo katika Ebr,9:27! SASA, BINAFSI NAJIULIZA, HIVI KWELI, MIMI SI MANAFIKI KWA MUNGU NA WATU? NIMEOKOKA KWELI? NINAISHIKA HAKI YOTE, KIASI KWAMBA IKITOKEA ILE “GHAFLA” YA SAFARI KAMA ILIVYOMPATA NDG. YETU KANUMBA, NITAKUTWA SINA “MZOZO” NA MUNGU? KWA MACHACHE HAYO, TUKIO HILO LA “KUSHTUKIZA” LIMENIFANYA NIRUDIE UPYA KUJIKAGUA KAMA KWELI, ILE Ebr.9:27 – KAMA KWELI NIKO NAYO VIZURI! HEBU TUACHE UNAFIKI NA KUJIFARIJI WENZANGU WOTE MPO NAYO SAWA HIYO Ebr, 9:27? – nina maana kuwa ni kweli iktokea hiyo safari kwa vyovyote na kwa namna yoyote Je, UPO FIT KATIKA HUKUMU? Mbarikiwe wote.

 15. Mimi mwenzenu niliposikia habari ya kufa kwake nilijiuliza swali moja tu…….., ROHO YAKE IMEELEKEA WAPI? na kama alijitengeneza tayari hakujua kuwa kuna siku atalala mauti.

  pole yangu kwa waombolezaji wote pamoja na mimi maana najipa pole.

  TUJIFUNZE KUWA SAFI MIOYONI MAANA SAA YA KUJILIWA KWETU HATUIJUI!!!!!!!!

 16. Wafiwa na waombolezaji wote poleni sana, maana nadhani nyumba zote zenye TV zitakuwa katika maombolezo wote poleni sana!

  @ Masanjila

  Mada ya “Kunena kwa Lugha” haijaondolewa ipo, jaribu kui search, tutakutana huko!!!!

  Mbarikiwe!

 17. Ni kweli imetokea cha msingi tulie tufute machozi Mungu alitoa na leo ametwaa jina lake lihimidiwe imeniuma sana.

 18. Kifo ni siri ya Mungu , hakuna ajuae siku wala saa, tujifunze kmupenda Mungu kwa uaminifu tukiweka maisha yetu kuwa safi katika kristo. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amen

 19. Kutokana na kifo cha Kanumba tujifunze kwamba tunapaswa kujiandaa wenyewe kabla ya kufa kwa ajili y maisha ya milele wala tusitegemee sala ya wafu kwamba Mungu mlaze pema peponi huo ni uongo na dhambi .maana unawapa watu tumaini kwamba wakifa wakiombewa Mungu atawalaza kweli pema peponi,wakati Mungu hana andiko hilo ktk neno lake bali anasemaktk waebrania 9;27 baada yakifo ni hukumu,PIA NAOMBA TURUDISHIENI,MADA YA KUNENA KWA LUGHA.

 20. kwanza nilipopata taarifa nilishtuka,baadae nikawa normal nashukuru Mungu anaendelea kutukumbusha kuwa sisi ni wapitaji hata km tutakuwa watu wa aina gani hapa duniani

 21. Ni majonzi matupu!! Mimi ni mmoja wa mashabiki wake, japo sijui athari yake Kiroho! Filamu zake zote zilibeba jumbe zenye mlengo wa kufundisha jamii ya Kitanzania na yeyote yule anaependa kujifunza masuala ya kijamii. Binafsi sikuwahi kupitwa na filamu yake yoyote, zote zipo nyumbani kwangu. Filamu zote zinaangalika na familia nzima hata ukiwa na wazazi wako au watoto wako.

  Kiroho, kifo chake kinafundisha kuwa wakati wa Wokovu ndio sasa. Hakuna Hiari japo Mungu ameacha hiari ya kumpokea YESU Kristo, lakini tukumbuke katika kitabu cha Biblia Yohana 10:10, kazi ya Shetani ni kuua na YESU ni UZIMA wa milele. Waberania 9:27 baada ya mwanadamu kufa ni hukumu. Hakuna nafasi tena ya kujipatanisha na Mungu. Yesu Kristo ndie njia ya kujipatanisha na Mungu Baba. Asiyemwamini Yesu tayari amekwishakuhukumiwa. Maana kila goti litapigwa mbele yake na kila ulimi utakiri kuwa ni Bwana, japo leo hii watu wanatumia demokrasia ya kuamua kumwamini YESU. Lakini kwa habari ya KIFO, hakuna kupinga wala kukata rufaa au kutoa rushwa. Tujiandae kwa kumpokea YESU na kuishi maisha matakatifu.

  Kifo cha Kanumba ni fundisho kuwa kifo ni siri ya MUNGU na YESU atarudi kuchukua kanisa lake takatifu ghafla!! Tujiandae maana hatuaji siku wala saa. Maisha yetu yapo mikononi mwa Boss Mungu Baba.

 22. Mtu ukiwa mashuhuri, ni vyema kujua kuwa unazungukwa na maadui wengi wanaotafuta kukuondoa ili wajulikane wao. Hilo mosi: la pili, Shetani naye yupo tayari kukatisha maisha ya kila mtu mashuhuri duniani na hasa umashuhuri unapokuwa ni msaada kwa wengi.
  Mambo ya kujichanganya changanya bila kuwa na tahadhari kunatoa nafasi kwa maadui hao kutekeleza azima yao, na matokeo yake ndiyo hayo.
  Ni kweli Mungu anatoa na kutwaa, lakini wengine wanawahishwa kabla ya wakati wao kama Kanumba. Si kwa kuwa tulimpenda tu, lakini mazingira yaliyomwondoa yanathibitisha ninachokisema. Yote katika yote, Mungu ni mwema siku zote.

 23. Tunapokuwa ktk kipindi hiki cha msiba wa mwenzetu mpendwa tutulie na maombizaidi

 24. Binafsi ninasikitika sana lakini ndo hivyo Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe

 25. Hapa ndipo wote tuliobakia, tunapotakiwa kukumbuka maneno haya kila siku za maisha yetu.

  ‘Wafilipi 1:21 ‘Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida’.

  TUJIULIZE
  – Maisha yako unamwishia nani? Yesu au ?

  – Kifo kwako kitakuwa ni faida au ndo mwanzo wa balaa la kuangamia Jehanamu

  MUNGU TUSAIDIE KAMWE TUSIJISAHAU,

  -USIJIDANGANYE KUWA U KIJANA NA NDO WAKATI WA KU-ENJOY MAISHA; inawezekana hatuna muda kama tunavyodhania

  Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s