Karama Za Mungu Zisizo Za Majuto

Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. (daima hazirudishi pale azitoapo, na habadili mawazo yake juu ya wale awapao Neema yake au juu ya wale awapao mwito wake) (Warumi 11:29 AMP).

Mstari wetu wa ufunguzi katika tafsiri ya King James unasema: “Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.” Maana yake hakunyanganyi kitu alichokupa. Kama amekubariki na karama ya unabii kwa mfano, kamwe hatakaa aichukue. “Lakini vipi kama wakati mwingine ninajisikia kama sina karama hiyo tena?” unaweza ukauliza. Haihusiani na hisia; bado iko katika roho yako; ni juu yako wewe kuichochea karama ya Mungu ndani yako, na nitakuambia namna.

Kwanza, hakikisha umejitoa kwa Bwana; kumbuka yeye ndiyo chanzo cha karama, na ni mkuu kuliko atoacho. Endelea kujiunga naye na mtumikie kwa moyo wote. Tambua kwamba yeye ni Bwana wa maisha yako, sio wakati fulani tu, lakini kila wakati; acha kujitoa kwako kwake kuwe wazi wazi kabisa kwako.

Pili, lazima upalilie tabia ya maombi. Kila kitu kutoka kwa Bwana hutunzwa kupitia ushirika na Roho Mtakatifu. Kadiri unavyotumia muda katika kushiriki mara kwa mara na Bwana katika maombi, roho yako itajengeka. Vile vile, omba kwa lugha zaidi. Hili litatia nguvu, imarisha na kuchochea roho yako, na kukuleta katika uwanja wa mafunuo makubwa. Kunena kwa lugha huimarisha ufahamu wako wa kiroho, na kukusaidia kupata mwanga zaidi na kutembea katika njia ya Bwana.

Mwisho, jifunze kusoma na kulitafakari Neno. Unavyojifunza, ataleta ufahamu wa Neno katika roho yako! Na kwa sababu roho yako imekuwa sikivu zaidi, utakuwa na uwezo wa kupokea ujumbe wa Mungu kutoka kwa Roho Mtakatifu na kuishi vizuri, maisha yenye kuongezeka ushindi.

Sala

Baba Mpendwa, msimamo wangu kwako hautikisiki, na ninavyonena kwa lugha, na kutafakari Neno kwa kusali, roho yangu inatiwa nuru na kupangwa vizuri ili kupokea mawazo ya juu kutoka kwa Roho Mtakatifu kwa ajili ya uimara wangu, na kulijenga kanisa, katika Jina la Yesu. Amina.

somo zaidi:Warumi 11:29; Yakobo 1:17

—Christ Embassy 

Advertisements

One thought on “Karama Za Mungu Zisizo Za Majuto

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s