Solomon Mukubwa azindua UTUKUFU KWA MUNGU

Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Christina Shusho wakiingia uwanjani

Katikati muimbaji kutoka Kenya, Emmy Kosgei na Rose Muhando wakiwa uwanjani

Solomon Mukubwa akiwapungia mashabiki

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akiangalia album ya UTUKUFU KWA MUNGU, Kushoto ni John Merere, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, Solomon Mukubwa, Askofu Gamanywa

Pamoja na umaridadi wa kucheza. Rebeka Malope amehaidi kununua nyumba Tanzania na kuhamia kabisa.

Ephrahim Sekeleti kutoka Zambia

Rose Muhando na Utamu wa Yesu

Tumaini John

Mh. Bernald Membe alipata muda wa kutosha kutoa salamu kwa maaskofu, Raisi na waziri Mkuu, na kuongelea msiba wa Kanumba, akawaomba watu wasimame dakika moja kuomba Mungu amlaze pahali pema peponi na Raisi wa Malawi.

TAMASHA LA PASAKA siku ya Jumapili limehudhuriwa na idadi kubwa ya watu, kuliko matamasha yaliyowahi kutokea hapo nyuma, waandaaji wa tamasha hilo MSAMA PROMOTION wamefanikiwa kuwaleta waimbaji wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo kufanya watu wapate mahali pa kwenda kufurahia sikukuu ya kufufuka Bwana Yesu Mwokozi!

Ilikuwa ni Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, ukumbi uliwaka furaha kumuona Rebecca Malope aliyeimba nyimbo zake huku akizunguka uwanjani, pia Rose Muhando na wimbo wake wa Utamu wa Yesu, John Lisu naye alikuwepo akiimba nyimbo zake Live, Ephrahim Sekeleti, Solomon Mukubwa na uzinduzi wa album yake KWA UTUKUFU WA MUNGU, Tumaini John, Mwalyambi kutoka Sumbawanga, Christina Shusho, Upendo Kilahiro na wengine ambapo walichelewa kuanza hivyo kupelekea waimbaji wengine kutopanda jukwaani.

Baada ya Tamasha hili nimewaza, pamoja na watu kuhudhuria kwa wingi, na waimbaji kuimba na kucheza kwa furaha lakini kuna haja ya kufikiria roho zinazotaka kuokoka, waandaaji wa matamasha ya Injili nchini, kuna haja ya kufikiria kuwaleta watu kwa Bwana Yesu!

 —Picha na John Bukuku

Advertisements

8 thoughts on “Solomon Mukubwa azindua UTUKUFU KWA MUNGU

 1. Shalom, it was quite fine, managing time was a shortcoming, political people spoke unnessary speech,upambaji wa jukwaa zero, jukwaa not covered,suppose mvua ingechanganya,tungeumbuka, please Msama improve da problem

 2. Praise be to God, the bliss was great, I like to join other Gospel music fans in congratulating Msama from such a good work for the kingdom of God in N.stadium..! However then can do even better in next one, need to more punctual,music speakers need be improved and Mc’s need to be more hoot, otherwise you did so goooood

  God bless you..!

  WINLAND
  FORM: TANZANIA-AFRICA

 3. Nilifurahia tamasha. Lakini kuna mambo ya msingi inabidi waandaaji wayaangalie kwa umakini wa hali ya juu na kuyarekebisha ili kuboresha matamasha yajayo. Suala la sauti ambalo kwa maoni yangu limechangiwa na kukosa vyombo maridadi vya muziki, kutokuwepo na wataalam vya kutumia na kucontrol vyombo hivyo lilikuwa ni tatizo sugu na lilituboa sana wapenzi tuliokuwepo uwanjani. Siamini kama mtu aliyekuwa kwenye mixer ni mtaalam wa mambo hayo, maana mara nyingi nilimwona akiwa ameinamia mixer anaangalia chini wakati jukwaani wasanii wakilalamikia mic hazifanyi kazi!!! Sound engineer wa Rebeka alijitahidi kwa kweli ingawa ubovu wa vyombo nao ulimuangusha na alionekana wazi kuwa dissappointed. Hili pia kwa kiasi kikubwa limewaaibisha waandaaji, Msama chukua hatua!

  Lingine ni lile tatizo sugu la watu wa dunia ya tatu – muda. Tamasha lilitangazwa kuanza saa nane mchana lakini hadi saa kumi bado mafundi walikuwa wanahaha kuweka vyombo sawa. Swali ni je, hawakujiandaa vema, hawakujua kwamba saa nane mambo yalitakiwa kuwa yanaanza? Udhaifu huu usijirudie. Ndio maana waimbaji wengine hawakupata kabisa nafasi ya kuimba, huku wengine wakipewa muda kiduchu, mfano Rose sio msanii wa kumwambia aimbe kwa dakika kama kumi tu! Kama muda ungeruhusu kwa ninavyomfahamu Rebeka angeweza kuimba hata kwa masaa mawili. Waandaaji walituangusha katika utunzaji wa muda.

  Watu (wengine ni waimbaji) kujazana uwanjani bila sababu za msingi na hivyo kuzuia watazamaji wengine kuona vizuri uwanjani hasa wakati Rebeka alipokuwa akiperform maana yeye hakupanda kabisa jukwaani! Na waandishi na wapiga picha wetu nao walifanya mambo niliyoyaona kuwa ni ya ajabu maana walikuwa wanamzonga na kumzunguka Rebeka hadi akalazimika kulalamika na kuwafukuza, walikuwa wanamblock kuwaona na kuwasiliana na watazamaji waliokuwa jukwaani!

  Nashauri haya yazingatiwe na kufanyiwa marekebisho katka matamasha yatakayofuata.

 4. Nimefurahia Tamasha japokuwa kulikuwa na hitilafu ya sauti. Mungu ambariki Rose Muhando

 5. Hivi kweli kuna utukufu wa ki-Mungu pale muimbaji wa Injili anapomualika mpagani mashuhuri awe ni mgeni rasmi wa kuzindua (kuiweka wakfu) album yake badala ya kuhani?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s