Kusomea kumtumikia Mungu!

Watu wanaoenda kusomea huduma mbali mbali za kanisa ni wengi. Kuna maoni ya wengine wanaona hakuna umuhimu wa kusomea uinjilisti, uchungaji au huduma za kanisa. Wengine wanaona kusoma ni muhimu sana hasa kutokana na jamii inayotuzunguka.

Na tumeona Mungu akiwatumia wengi ambao hawajaenda shule, katika historia amefanya hivyo na hata sasa bado anafanya. Pia kuna wengine wamesoma na bado Mungu amewatumia katika kazi yake.

Je, kipi ni muhimu kutokana na mtazamo wako!

Advertisements

41 thoughts on “Kusomea kumtumikia Mungu!

 1. Bwana Yesu Apewe Sifa,
  Habari Zenu Watumishi Wa Mungu.
  Napenda Kuchangia Mada Kama Ifuatavyo:
  1.Efe.4:11 Anasema Alitoa Wengine Kuwa WALIMU Kama Hakuna Shule Au Chuo Je Walimu Wanafundisha Wapi? Kwa Hiyo Uwepo Wa Shule Au Vyuo Ni Kitu Ambacho Kwa Mtu Anayejua Kupambanua Vizuri Karama Hawezi Akapingana Na Hilo
  1.(b)Ndiyo Maana Yesu Alisema Mkiwafundisha Kuyashika Yote Niliyowaamuru Ninyi. Je Kuna Mwanafunzi Bila Mwalimu? Je Kuna Mwanafunzi Bila Shule Au Chuo?
  2.Ukiokoka Unahitaji Kufundishwa Na Anayefundisha Ni Mwalimu Anayejua Neno La Mungu Siyo Anayepapasa Na Kumzingizia Roho Mt.Wakati Hajui Chochote Kuhusu Biblia.
  Na Kama Ulikuwa Hujaenda Shule Nenda Kwanza Ukirudi Tuambie Kwamba Wamekupotosha Kitu Gani Kuliko Kusema Vitu Ambavyo Huelewi.
  Wasiliana Nami Kwa Namba 0714528418

 2. Bwana Yesu Apewe Sifa,
  Habari Zenu Watumishi Wa Mungu.
  Napenda Kuchangia Mada Kama Ifuatavyo:
  1.Efe.4:11 Anasema Alitoa Wengine Kuwa WALIMU Kama Hakuna Shule Au Chuo Je Walimu Wanafundisha Wapi? Kwa Hiyo Uwepo Wa Shule Au Vyuo Ni Kitu Ambacho Kwa Mtu Anayejua Kupambanua Vizuri Karama Hawezi Akapingana Na Hilo
  1.(b)Ndiyo Maana Yesu Alisema Mkiwafundisha Kuyashika Yote Niliyowaamuru Ninyi. Je Kuna Mwanafunzi Bila Mwalimu? Je Kuna Mwanafunzi Bila Shule Au Chuo?
  2.Ukiokoka Unahitaji Kufundishwa Na Anayefundisha Ni Mwalimu Anayejua Neno La Mungu Siyo Anayepapasa Na Kumzingizia Roho Mt.Wakati Hajui Chochote Kuhusu Biblia.
  Na Kama Ulikuwa Hujaenda Shule Nenda Kwanza Ukirudi Tuambie Kwamba Wamekupotosha Kitu Gani Kuliko Kusema Vitu Ambavyo Huelewi.

 3. Ndugu wapendwa Amani iwe nanyi, nashukuru kwa mada hii nzuri sana. Naomba kuchangia yafuatayo. Mungu ana mpango n makusudi kwa kila mmoja na mpango na makusudi aliyonayo Mungu kwa kila mmoja wetu hutofautiana kabisa kati ya huyu na yule, au mtumishi huyu na yule, wako waliotokewa na Bwana Yesu wakaokoka wito huu ni tofauti na waliotokewa na wainjilisti kama Filipo. Wako waliookoka kwa maonyo na makalipio makali sana na Mungu na wengine Mungu aliwaokoa kwa namna fulani na wengine namna fulani. Kubwa zaidi ni kuhusu jinsi ya kutumika hili nalo Mungu wengine atawaambia waende vyuo vya Biblia na Wengine Wasiende na Huduma zao zikasimamiwa na Roho Mtakatifu na zikawa Nzuri. Nirudi kwenye HOJA -KUSOMEA KUMTUMIKIA MUNGU- Hili ni Lazima KABISAA KWA MTU YEYOTE YULE ANAYEITWA NA MUNGU LAZIMA ASOMEE TOFAUTI NI UELEWA WA WATU= Petro alisomea kumtumikia Mungu ndio maana aliitwa Mwanafunzi wa Yesu- Mwalimu wao alikuwa Yesu. Hivyo kusema kuwa hakuna Elimu kwa watumishi ni kujidanganya na ni rahisi Kupotea kwenye Ulimwengu huu uliojaa Mchanganyiko wa Mafundisho potofu. KUNA ELIMU RASMI -YA VYUONI AU MASHULENI. NA KUNA ELIMU ISIYO RASMI HII IKIJUMUISHA POPOTE UNAPOPATIA MAARIFA HATA KAMA NI ROHO MTAKATIFU ANAKUFUNDISHA HIYO TAYARI NI ELIMU. Mtumishi anayekataa kwenda chuo cha Biblia na akasema ROHO ANATOSHA AWE MAKINI NA MAFUNUO HAYO- KWANI NAYO NI ELIMU ROHO MWENYEWE HUITWA MWALIMU. Musa na wengine wote walifundishwa Kusema na kutoa Unabii kwa njia mbalimbali kama hakufundishwa na MANABII WAKUBWA BASI ALIFUNDISHWA NA ROHO MTAKATIFU- HIVYO NASHAURI HIVI KILA MMOJA AUANGALIE WITO WAKE NA MUNGU ANAVYOKUONGOZA-ELIMU NI LAZIMA NA YA MUHIMU ILA WAPI UNAIPATA HUTOFAUTIANA. Asante

 4. MAASKARI WA YESU WANASONGA MBELE MPAKA KIELEWEKE!!!
  Sikujua kwamba Mtume Paulo alikuwa BONDIA tena mbabe wa vita
  vya ulingoni kwa jinsi ya rohoni!Alikuwa bondia na mwanariadha shujaa!

  Hebu tumsikilize kwa makini kile anachosema hapa;
  “Nami nafanya mambo yote KWA AJILI YA INJILI ili kushiriki pamoja
  na wengine.Je! Hamjui ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio
  hupiga mbio wote lakini apokeae tuzo ni mmoja?PIGENI MBIO NAMNA
  HIYO ILI MPATE.
  Na kila ASHINDANAE katika michezo HUJIZUIA KATIKA YOTE, basi
  hao hufanya hivyo kusudi WAPOKEE TAJI IHARIBIKAYO,bali sisi
  TUPOKEE TAJI ISIYOHARIBIKA.Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo,
  SI KAMA ASITAYE,NAPIGANA NGUMI VIVYO HIVYO, SI KAMA APIGAYE
  HEWA, BALI NAUTESA MWILI WANGU NA KUUTUMIKISHA ISIWE,
  NIKIISHA KUWAHUBIRIA WENGINE, MWENYEWE NIWE MTU WA
  KUKATALIWA”

  Tunapozungumzia maangamizi ambayo yako ndani ya masuala ya
  Theolojia HATUPINGANI na wanatheolojia bali tunapambana na
  upotoshaji na mafundisho yaliyo kufa ambayo yameingizwa
  ndani ya kanisa kwa kutumia KIVULI CHA THEOLOJIA.

  Tunataka wateule wajitambue kiroho kwa kuzijua hila na kazi
  za mbwamwitu ambao wanajiita wanatheolojia ambao wameupaka
  MAVI mfumo mzima wa THEOLOJIA na makusudi ya Mungu.Watu
  kama kina PANDAELI wameathiriwa na hii harufu ya mavi ndani
  ya theolojia na kazi zake nyingi zilizokufa.Inahitaji hekima na uvumilivu
  wa rohoni.Tunataka hao wanatheolojia wa kweli kama kina CATHERINE
  ambaye ni mama wa kiroho wa BENNY HIN ndiyo watamalaki ndani
  ya mikusanyiko ya wateule.Hata hivyo hali ilivyo sasa ni tofauti sana.
  Watumishi ambao hawajasoma Theolojia kama mwalimu mwakasege
  wako mstari wa mbele kuhakikisha Wateule wanajitambua kiroho.
  Mwakasege hajasoma theolojia lakini theolojia na wanatheolojia duniani
  kote wanamvulia kofia na kumpa heshima yake aliyopewa na Yesu!
  Wengi wanatamani Mwakasege afundishe theolojia katika vyuo vyao
  lakini tunao kina Mwakasege wengi tu ambao tumeshindwa kuwatumia!Mteule anayetembea na macho saba ya maarifa ya Mungu
  ana zaidi ya theolojia ndani ya ufahamu wake!(UFUNUO 5:6).Elimu
  ya neno la Mungu siyo taaluma kama zilivyo taaluma nyingine.Ni
  MAFUNUO na HEKIMA ya Yesu.Kuielewa elimu kuhusu Mungu tunahitaji roho ya hekima na ufunuo pamoja na nuru ndani ya macho
  yetu ya rohoni(WAEFESO 1:17-19).Wanaopinga hili labda hawajitambui
  au ni mbwamwitu.HUU MOTO WA YESU HAUZUILIKI.NI NGUMI
  ZA CHEMBE.PAULO ALIKUWA ANAJUA APIGE WAPI ILI ADUI
  ATEME DAMU NA KUPOTEZA UHAI.KAMA WEWE NI MBWAMWITU
  LEO NATAKA NIKUFUNDISHE NAMNA NGUMI ZINAVYORUSHWA
  KWA MAARIFA NA UJUZI WA YESU WA KUPIGANA ULINGONI.
  UNAWEZA UKAWEKA BIDII ULINGONI ALAFU USHINDI WAKAPEWA
  WENGINE!!

  Katika nyakati hizi za hatari kuangalia tu uzuri wa theolojia na
  wanatheolojia wanaotembea na Mungu HAITUSAIDII SANA.Tunataka
  wateule wajue tena kwa undani sana ni kwa kiwango gani wajumbe
  wa shetani hasa mitume,manabii na waalimu wa uongo WAMEJIFICHA
  NDANI YA THEOLOJIA ILI KUWALISHA WATEULE SUMU KALI KULIKO
  SUMU YA FIRA.Vyuo vya theolojia vinavyomilikiwa na mbwamwitu
  ni vingi sana na wateule wasiojitambua wamemezwa humo.Wakishahitimu wanarudi makanisani mwao kuwalisha wenzao
  sumu.Ni dhahiri kwamba hatumjui vizuri Mungu tunaemtumikia.
  Sikiliza, Mungu anaweza kukuonyesha matukio yote ya jinsi ilivyokuwa
  wakati Ibrahimu anakwenda kumtoa sadaka Isaka.Anaweza kukuonyesha picha halisi kwenye ulimwengu wa roho.Kwahiyo ukajua
  zaidi ya kile unachosoma katika Biblia au kufundishwa katika Theolojia!
  Kuna watu walipelekwa kufanya ziara ya mafunzo ISRAELI kwenye
  ulimwengu wa roho kabla ya kupelekwa katika ulimwengu huu wa kawaida!!!Walipofika ISRAELI hakukuwa na jambo geni kwao zaidi ya
  wao kuwapa wenzao mafunuo!!Maaskari wa Yesu huwa wanaonyeshwa kwenye ulimwengu wa roho kuhusu sumu zinazofundishwa katika vyuo vya theolojia.Unaweza ukawa Tanzania
  ukaonyeshwa yote yanayoendelea katika vyuo vya theolojia Marekani!!
  Ndiyo maana mashujaa kama kina Mwalimu Mwakasege hawabwatuki,
  hawatishiki bali WANAPIGA KWENYE TARGET MPAKA KINAELEWEKA.
  Huyu ni mmoja kati ya manabii wa kweli katika nchi ya TANZANIA.
  Hata shetani huwa anawapiga mawe wafuasi wake ambao wanajaribu
  kushindana na Mwakasege kwa kukurupuka!!Na wengi wanajikwaa
  sana kwa nabii Mwakasege.Yesu amewakamata kooni, hawatemi wala
  hawamezi!THEOLOJIA inayokomboa nafsi za wateule ni ile inayofundishwa na wateule wenye huduma ya ualimu.Unapokimbia
  usikimbize upepo, inabidi ujue ni kwanini unakimbia na ni wapi unaelekea.Usituambie umetimiza ndoto yako kwa kuwa umefika
  Marekani, tuambie huko Marekani ni nani kakupeleka na umeenda
  kwa kusudi lipi.Ni lazima tulenga kuacha alama za unyenyekevu
  kila tunapopita na siyo alama za KIBURI CHA KUMTUKANA YESU.
  Ukipinga au kulipotosha neno la Mungu ni sawa na kumtukana
  Yesu kwa sababu Yesu ni NENO LA MUNGU.Kwa vyovyote vile
  ROHO MTAKATIFU ndiye mwalimu anayetufundisha KWELI YOTE.
  Elimu ya neno la Mungu siyo taaluma BALI NI MUONGOZO ULIO
  HAI KWA TAALUMA ZOTE DUNIANI(Tafakari 1 WAKORINTHO 1:19-25).

  NGUMI ZA MIALE YA MOTO ZINAENDELEA MPAKA KIELEWEKE……

  CK LWEMBE , PANDAEL na wengineo tuendelee KUYAANIKA WAZI.
  Asante sana MABINZA LS kwa point yako iliyoipindua dunia pale
  uliposema kuwa INJILI NI UNYENYEKEVU.Mungu wangu akukumbuke
  kwa hili.

 5. Sungura, MITHALI 17:11 ” Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu; Kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake.” Hayo ni maswali ya upumbavu yasiyo na maana.( 2Timotheo 2:23).UNA UHURU WA KUONESHA KILE ULICHO.

 6. Huwa sipendi sana kurudia mambo ambayo tulishayadili tena kwa kina.

  Suala la kubatiza kwa jina la Yesu na kwa jina la Baba, Mwana, Roho mt.tulishaliongea sana kwenye mada ya utatu ile ya kwanza kabisa kwa wanaofuatilia.

  Lakini najiuliza tu swali rahisi kuwa; ivi inahitaji mpaka mtu awe mwanatheolojia ku-argue kuwa mitume walifanya kinyume na agizo la Yesu kwenye kubatiza?

  Hapo si mtu yeyote tu anayesoma biblia anaweza akaibuka na hiyo hoja, maana alichoagiza Yesu kiko kwenye biblia, na walichofanya mitume kiko kwenye biblia na viko wazi!

  Lakini mimi nimemtaka Pendael atutajie tu watumishi watatu ambao wamefanikiwa kihuduma kwa viwango vya juu lakini hawajaenda shule!!!

  Au atuambie kama mchungaji wake nae hajaenda shule anaenda tu kwa ufunuo!!

  Mimi nimempa mifano ya watu ambao shule walienda na wametembea na Mungu isivyo kawaida.

  Je unahitaji kufunuliwa ili kujua Yesu alikuwa anaongea lugha gani alipokuwa duniani au unatakiwa tu kusoma historia?(kwenda shule)

  Mtu anashindwa kuelewa kuwa biblia imeandika mambo machache sana kati ya mengi ambayo Yesu alifanya.

  Ivi leo wanatheolojia ambao ni watafiti wa maandishi wakiibuka na nyaraka zilizoandikwa na Barnabas akiwaandikia kanisa fulani, si akina Pendael watasema hiyo ni kazi ya kuzimu!!

  Lakini watu wenye fikra pana watasema hiyo bila shaka ni kweli maana Barnabas alikuwa si mtu wa kawaida pia, japo record ya kazi yake kwenye biblia haijaandikwa kama ya Paul.

  Ujinga ni mzigo tu kama ilivyo dhambi!

 7. Watumishi ORBI na PETRUS

  Tunahitaji kuwa na uvumilivu wa rohoni ili Kuyajua MAPENZI
  YA MUNGU ALIYE HAI.Mada hii kuhusu Theolojia na wanatheolojia
  ni NYETI SANA na inaweza kujadiliwa kwa mapana mno na kama
  ni mitazamo ipo mingi mno.Kila mada inapowekwa mezani bila
  kujalisha ni ya namna gani, KUNAKUWA NA KUSUDI LA MUNGU
  ambalo wateule wanapaswa walijue ili wawe Huru.Tusipoyajua mapenzi
  ya Mungu pale anaporuhusu mada fulani iwekwe mezani TUNAJITIA
  KATIKA VIFUNGO VYA MATESO YA KUTOMUELEWA MUNGU YAANI
  NENO LA KRISTO!

  Maelezo ya Mtumishi Petrus kuhusu Theolojia ni mema na yanajenga
  uelewa fulani.Ni sawa na jinsi Mtumishi Sungura anavyojaribu kutufundisha ili tuelewe maana na umuhimu wa Theolojia na wanatheolojia wa kweli.Haya yote ni mema sana.Mimi naangalia na
  kujifunza kile ambacho Roho Mtakatifu ananifundisha na siyo kile
  ambacho kinasemwa kwa utashi wa kibinadamu.Ndiyo maana naepuka
  sana kurushiana MAWE na watu wengine wanaochangia najitahidi
  kuenenda kwa hekima ya Rohoni na Mungu anisaidie na kuwasaidia
  na wengine KATIKA HILI.Mtumishi ORBI nimevutiwa sana na michango
  yako katika mada hii hata hivyo kwenye maelezo yako ya tarehe 12/12/2014 at 10:07 pm nimevutiwa tu na maneno “Ndugu yetu Pandaeli
  anahitaji msaada, tena msaada mkubwa….”.Swali la kujiuliza ni hili,kama
  kweli ndugu yetu Pandaeli anatakiwa kusaidiwa tunafanyaje ili kumsaidia
  katika hekima ya Kristo? Kwa sababu tukumbuke kila mmoja wetu
  hapa anatakiwa kusaidiwa kwa namna moja au nyingine na bila kutanguliza upendo wa kristo hatutaweza kusaidiana.Bila shaka kuna
  mengi mema ambayo Mungu ametukusudia katika mada hii.Mimi
  ninachofuatilia zaidi ni MAPUNGUFU ya mfumo wa theolojia na namna
  wanatheolojia na wale wanaofundishwa nao wanavyoweza kupambana
  na mapungufu haya ili kuujenga mwili wa Kristo kama Mungu alivyokusudia.

  Katika mada hii inayosema KUSOMEA KUMTUMIKIA MUNGU! Tunaweza
  kupata UELEWA MPANA MNO kama tukitafakari na kuunganisha
  maelezo ya watumishi ORBI, MARGARETH MKIWA, GEORGE MATHIAS,
  TAKWA D. ASAPH, SAM, MABINZA LS,AMANISAREPTA,PASTOL DICKSON,
  PANDAEL SIMON.Ndani ya maelezo yao tunapata changamoto za
  kutisha.Nimependa mchuano mkali unaojenga sana kati ya ORBI,SAM
  na MABINZA LS.Lakini pia navutiwa kujifunza kwa UVUMILIVU MKUBWA
  katika majadiliano kati ya watumishi SUNGURA na PANDAEL.Wote kwa
  ujumla wao WANAKUBALIANA JAMBO MOJA LA MSINGI KWAMBA
  MWALIMU WA WANATHEOLOJIA NA WALE WASIO WANATHEOLOJIA
  ANAPASWA KUWA ROHO MTAKATIFU.1 YOHANA 2 :20 inasema
  “………..wala hamna haja ya mtu kuwafundisha, lakini kama mafuta
  yake(upako wa Roho Mtakatifu) yanavyowafundisha HABARI ZA MAMBO YOTE,tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha
  KAENI NDANI YAKE”

  Kwako Mtumishi Pandael Simon

  Namshukuru sana Roho Mtakatifu kwa kututia katika KWELI YOTE
  katika maswali ambayo tulimuuliza.Ndani ya maelezo yako nimepewa
  MAFUNUO zaidi ya kile ulichokiandika.Ni kweli kabisa kwamba Yesu
  Kristo ndiye Mungu Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.Na hivi ni vyeo
  vya hekima ya utendaji wa Mungu.JINA HALISI LA MUNGU ALIYE HAI
  NI YESU KRISTO(soma YOHANA 17:6).Pia ni kweli kabisa pasipo
  roho ya UFUNUO na HEKIMA hatuwezi kujua Yesu ni nani wala kujua
  hekima ya utendaji kazi wake.Mafunuo na hekima ndiyo yanayofanya
  tuyajue maono na wito wetu katika kumtumikia Mungu(soma WAEFESO
  1:17-19)

  Najisikia kukueleza hili katika ujasiri na hekima ya Roho Mtakatifu.
  Aliyeweka mada kuhusu THEOLOJIA katika meza ya wachangiaji
  katika BLOG hii ni Mungu na siyo wewe wala mtu mwingine yeyote!
  Bila shaka Mungu ana kusudi la kufanya hivyo ili TUJIFUNZE MAMBO
  MAKUBWA NA MAGUMU ambayo hatukuyajua(YEREMIA 33:3).
  Kinachotakiwa TUACHE KUJIHESABIA HAKI katika jambo lolote
  na tukubali kunyenyekea sana ili Yesu atupe NEEMA ya kuyajua
  mapenzi yake katika mada hii.Lengo kuu hapa ni UKOMBOZI WA NAFSI
  ZETU.Ni kweli wakati mwingine imekuwa ni vigumu kuvumilia kutazama
  MAANGAMIZI yanayoendele ndani ya THEOLOJIA lakini kumbuka ili
  ni JARIBU la wateule na mlango wa kutokea ni MAARIFA YA YESU.
  Zaidi ya yote tunayaweza MAMBO YOTE KATIKA YESU ATUTIAYE
  NGUVU(WAFILIPI 4:13).Tusikatae kuwa wanafunzi wa Yesu kuna mengi
  bado hatujayajua jinsi inavyotupasa KUYAJUA.Unachoongozwa KUKIFICHUA usisite kukiweka wazi kwa hekima na Maarifa yaliyo hai.

  Mungu wangu awakumbuke wateule wote wanaomtafuta Yesu
  kwa bidii na Maarifa yaliyo hai.Mbele za Mungu mimi ni mtupu
  na mwenye kiu kali ya maji ya upendo wa Kristo.Nahitaji Mungu
  anivalishe vazi la unyenyekevu wa Yesu(WAFILIPI 2:3-4).

 8. Orbi,Nakujua kuwa wewe ni mtetezi wa Teolojia na Si mtetezi wa NENO.HIVYO HAYO NI MAONI YAKO NA UKO HURU KUZUNGUMZA.KILA DHEHEBU LINA CHUO CHAKE CHA BIBLIA,HEBU TUAMBIE DHEHEBU MOJA LINALOFUNDISHA THEOLOJIA YA KWELI.INJILI YA THEOLOJIA NI INJILI YA USHUNGI WA JOGOO. INJILI YA THEOLOJIA HAIJARUTUBISHWA HIVYO HAINA UHAI,NDIO MAANA WANAOSIKILIZA HUFA KIROHO WAKINGOJEA KUFA KIMWILI.MIMI SITISHIWI NA WANATHEOLOJIA NA MAFUNDISHO YA DHEHEBU LOLOTE.MADHEHEBU NDIO WALIOANZISHA VYUO VYA THEOLOJIA LEO HII WAMEONGEZA VITIVO MBALIMBALI KWA AJILI YA MATUMBO YAO. UDHEHEBU KWA MUNGU NI UKAHABA (UFUNUO 17:3-5). Majina ya MADHEHEBU ni Majina ya MAKUFURU.Madhebu ndio chimbuko la Mafundisho potofu.

 9. Ndugu zangu,

  Ndugu yetu Pendael anahitaji msaada, tena msaada mkubwa, nadhani hata hiyo Biblia anayoinukuu anadhani” ilishushwa” kama Quraan…! Hajui kuna watu walihangaika kusoma maandiko mengi yaliyokuwepo wakati huo, au yaliyokuwa yakizagaa wakati huo hadi kufikia hitimisho kwamba vitabu hivi 66 ndio Neno halisi la Mungu….! Kulikuwa na vitabu vingi mno….! Nadhani vile vile anadhani Biblia ilishushwa toka Mbinguni katika Lugha ya Kiswahili….! Bila kujua kuna watu walihangaika kuitoa katika lugha za awali, wakijaribu mno kuitafsri na kutopeza maana yake ya awali mpaka ndugu yetu Pendaeli ameweza kuisoma….Lakini sasa hivi nasema….hakuna maana yoyote ya mtu kukaa na kujifunza Maandiko ya Mungu….Je kama tunategemea “Ufunuo” Kwa Nini toka awali Neno liliwekwa kwenye Gombo……! Kwa Nini Amri za Mungu ziliandikwa…..! Mungu angaliweza kutufunulia moja kwa moja……!

  Nachelea kusema ndugu yetu hajui anolizungumza, Elimu ya theolojia (Kujifunza habari za Mungu) Inaweza ikaingiliwa na Shetani….na Inaweza kutumika kwa ajili ya kumjua Mungu wa Kweli…..! Kwa kifupi Pendaeli bila kusita ana elimu ya theolojia yenye mwelekeo wa ufunuo mwingine……..!

 10. Mrs CHRISTINA K.
  SHALOM.Namshukuru Mungu aliyekusaidia kuona LA KUJIFUNZA.
  KWANZA NI VEMA TUKAMUJUA MPINGA KRISTO NI NANI.
  Wapo wenye MAANA tofauti tofauti za MPINGA KRISTO.
  Mpinga Kristo si mtu mwenye pembe wala si mtu asiyejua KUSOMA bali ni mtu mwerevu sana anayejua KULIPINDA AU KULIGEUZA NENO LA MUNGU KWA HILA KAMA NYOKA ALIVYOKUWA, aliweza KUMBADILISHIA HAWA NENO MOJA TU KWA KUONGEZA “HA”.
  KUWA MPINGA KRISTO NI KWA KUONGEZA AMA KUPUNGUZA NENO LA MUNGU (UFUNUO 22:18-19)
  NAWAJIBIKA KUKUJIBU MASWALI ULIYOYAULIZA;
  WAKRISTO WA KWELI WAMEJENGWA JUU YA MISINGI YA MITUME NA MANABII.
  (WAEFESO 2:20 ” Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.”)
  MKRISTO YOYOTE HAPINGI BIBLIA.
  Waosema MITUME wana Mafundisho yao tofauti na ya BWANA YESU ni WANATHEOLOJIA WANAOTUMIWA NA IBILISI KULIUA NENO LA MUNGU,bali HAWATAWEZA Kwani NENO NI MUNGU (YOHANA MT.1:1-5)
  Mitume HAWAKUKIUKA AGIZO LA BWANA YESU bali kinachoonekana hapo ni UFUNUO WA ROHO MTAKATIFU. Kinachomtofautisha MKRISTO NA ASIYE MKRISTO NI UFUNUO juu ya NENO LA MUNGU.Hilo liko wazi katika MATHAYO 16:13-17 ” Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?
  Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
  Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
  Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
  Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”
  PETRO ALIPATA UFUNUO wala si THEOLOJIA (LLD,DD,….)
  Pia BWANA YESU ASINGEWACHAGUA watu ambao WATAFUNDISHA KINYUME CHA ALICHOFUNDISHA ndio maana ALIWAAMBIA WAKAFUNDISHE HAYO ALIYOWAFUNDISHA. MATHAYO 28 :18-20 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
  Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
  HAKIKA unakumbuka kuwa BWANA YESU Katika INJILI YA YOHANA ALIAHIDI UJIO wa ROHO MTAKATIFU na KAZI ZAKE ZIKATAJWA mojawapo atakuwa NI MWALIMU. WANAFUNZI waliambiwa wasiende kufundisha MPAKA ROHO MTAKATIFU ATAKAPOKUJA, NA MUNGU MWAMINIFU KWA NENO LAKE,ROHO MTAKATIFU AKAJA KWAO.
  HAPA YUDA HAKUWEPO KWA SABABU YEYE ALIKUWA NI ULE UZAO WA NYOKA AMBAO MWISHO WAO NI MAANGAMIZI.
  BWANA YESU ALIMWITA YUDA ni IBILISI.KWA KUMTUMIA YUDA KAMA MFANO;
  Hapa unaweza kupata picha ya MPINGA KRISTO kuwa ni MTU ANAYETUMIA BIBLIA,ANAFANYA ISHARA NA MAAJABU TENA KWA JINA LA YESU,ANA HURUMA KWA MASKINI KAMA YUDA NA ANAPENDA KUONEKANA MBELE ZA WATU NA KUTAFUATA UMAARUFU MBELE ZA WATU KAMA YUDA ALIVYOTAFUTA UMAARUFU KWA KUMSALITI MWANA WA ADAMU (BWANA YESU)
  Ndio maana BWANA YESU alisema “Nimekwisha kuwaonya mbele” na hata akaongeza kusema baada ya YUDA kufurahi kwa sababu pepo amemtii “msifurahi kwa sababu pepo wanawatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa Mbinguni”
  > >Kuwa Mpinga Kristo ni kuwa Mpinga Neno,na kuwa mpinga Neno ni kuwa mpinga YESU (Luka Mtakatifu 10:16)
  MUNGU NI WA KUABUDIWA,HIVYO MUNGU AMEDHIHIRIKA KAMA BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU.YESU NI BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU KULINGANA NA BIBLIA.
  YESU NI MUNGU (SOMA ISAYA 9:6, YOHANA MTAKATITIFU 1:1-3,…14 , TITO 2:13, MATHAYO 1:23)
  YESU NI MUNGU ALIYEDHIHIRISHWA KATIKA MWILI (1TIMOTEO 3;16 ” Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.” )
  YESU NI BABA ( ISAYA 9:6, YOHANA MTAKATIFU 14:7-8, 17:1-26)
  YESU NI ROHO MTAKATIFU ( 2 WAKORINTHO 3:17, WAFILIPI 2:10-11 YOHANA MTAKATIFU 14:16-20, 17:1-26).
  BABA ,MWANA NA ROHO MTAKATIFU NI VYEO VYA MUNGU wala si JINA.BALI JINA ni BWANA YESU KRISTO.
  HIVYO;
  BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU =BWANA YESU KRISTO
  MAANIKO YANAONESHA MATUMIZI YA JINA( WAKOLOSAI 3 :17)
  NI KILA MFANYALO KWA NENO AU KWA TENDO, FANYENI YOTE KATIKA JINA LA BWANA YESU. KWA MFANO:
  -MAOMBI (NENO) NI KWA JINA LA BWANA YESU
  -UBATIZO (TENDO) NI JINA LA BWANA YESU KRISTO ( MATENDO 2 :37-39)
  Hakuna mtu aitwaye Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu Duniani.Hilo lilikuwa fumbo (MATHAYO 13:34-35)Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni Bwana Yesu Kristo.Soma-MATENDO 2;36, 4;10-12,YOHANA MT,17;6,11-12WAFILIPI 2;10-11.
  Mitume ndio walioachiwa Maagizo na wengine wote wanaotaka kwenda Mbinguni hujenga kwenye Msingi huo,soma-1KOR 3;10-15, LUKA 10;16,WAEFESO 2;20.Mitume Waliokuw na Ufunuo Walibatiza KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO.Soma BIblia Yako vizuri-MATENDO 2;38, 8;12,16, 10;47-48, 19;4-5,
  Sasa kama HUJABTIZWA Kwa Jina La BWANA YESU KRISTO, UMELAANIWA( SOMA KWA MAKINI-WAGALATIA 1:8-9).
  ****BIBLIA HAIJIPINGI POPOTE, BALI WATU NDIO WANAOPINGA BIBLIA***
  SHALOM.

 11. Mtumishi Pandaeli Simon

  Na naomba turudi katika maelezo yako ya tarehe 11/12/2014 at 5:58pm

  Katika point namba 2e umesema moja ya mafundisho ya mpinga Kristo
  yaliyoletwa na wanatheolojia ni kuwabatiza watu kwa JINA LA BABA
  NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kinyume na mitume ambao walibatiza
  kwa jina la YESU KRISTO na ukanuu MATENDO 2:38,8:14-17,10:48,19:1-5.
  Ni kweli katika vifungu hivi mitume walibatiza kwa jina la YESU KRISTO.
  LAKINI tukiangalia katika point namba 5 ambapo umeongelea AGIZO
  LA YESU kwa kunukuu MATHAYO 28:18-20, Yesu mwenyewe anasema
  “……….mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi MKIWABATIZA kwa
  JINA LA BABA, NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU…….”

  MASWALI YA KUJIULIZA
  1.Je mitume walikiuka AGIZO LA YESU la kubatiza kwa JINA LA BABA,
  NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU na badala yake tunaona katika
  kitabu cha Matendo ya mitume wakibatiza kwa jina la YESU KRISTO
  peke yake?

  2.Je suala la kuwabatiza watu kwa JINA LA BABA,MWANA, NA ROHO
  MTAKATIFU ni mafundisho ya wapinga KRISTO au wafuasi wa KRISTO
  ambao wanafuata AGIZO LA KRISTO sawa na MATHAYO 28:18-20?

  3.Je kuna tofauti gani kati ya kubatiza kwa jina la YESU KRISTO
  na kubatiza kwa jina la BABA,MWANA, NA ROHO MTAKATIFU? Je kuhusu
  suala hili Biblia IMEJIPINGA YENYEWE?

  ROHO MTAKATIFU tunaomba utupe majibu.

 12. Teolojia, pia theolojia[1] (Kigiriki θέος theos “Mungu” + λογία logia “usemi”) ni elimu juu ya Mungu hasa katika Ukristo. Hiyo haitenganiki na utendaji wake wa nje, yaani uhusiano wake na viumbe vyote.

  [2]

  Kumbe ikitajwa kwa jina la mkopo kutoka Kigiriki, fani hiyo inachunguza hasa imani ya Kikristo kadiri ya Ufunuo wa Mungu uliokamilika katika Yesu Kristo na Mitume wake.

  Kwa sababu hiyo inategemea hasa Maandiko Matakatifu ya Biblia, lakini pia, kadiri ya madhehebu husika, Mapokeo ya Mitume yasiyoandikwa na mamlaka hai ya Kanisa (Ualimu).

  Teolojia hufundishwa katika vyuo na katika nchi mbalimbali iko pia kama idara ya Chuo Kikuu. Idara hizi mara nyingi zinatenganishwa kidhehebu. Mtu aliyepita mafundisho ya chuo huitwa mwanateolojia.

 13. pendael simon na sungura,
  Sungura na kuunga mkono mia kwa mia leo hii theolojia (Elimu juu ya Mungu si tu kanisani imekuwa zao ya taaluma nyingi sana duniani….Nna ndugu yangu anasomea degree ya sheria lakini anakili kwamba sheria chanzo chake kimetokana na biblia (Kumbukumbu la torati)..Mimi ni mwenyewe nimepewa neema yakusomea saikolojia lakini licha ya baadhi ya wataalamu wengi kusema tofauti lakini mengi yaliyozungumzwa kuhusu maisha ya mwanadamu kisaikolojia asili yake ni neno la Mungu na ukiangalia nadharia zao utaona misingi yake iliingia ktk theolojia…..sitaki kuzungumzia taaluma ya uchumi nadhani watu wa uchumi watanisaidia hapo……..LEO HII NASHANGAA SANA WAKRISTO WANAOINYOOSHEA KIDOLE THEOLOJIA….pasipo kufahamu hata historia kwamba vyuo bora vingi duniani pote vina misingi ya kanisa yaani wale wamishenari waliosomea theolojia wakavuka mipaka kwenda mataifa mbalimbali ndio wakawa wahasisi wa elimu ya juu. kwa mfano Havard university.

 14. Pendael,

  Wewe sema watatu tu ambao unawajua hawajaenda shule lakini wamepindua ulimwengu, mbona ni kazi ndogo hiyo nimekupa!

  Unaelewa hata maana ya kielelezo lakini, neno la Mungu ndio kielelezo cha wakristo, so what?

  Kwamba mimi ni mpinga Kristo, hiyo kauli nimeipenda.
  Ukiona mtu anaanza kuropoka hivyo ujue amefika mwisho wa kile alichokariri, kwa hiyo ameishiwa cha kusema!

  Ulikuja ukiwa unadhani unakuja kutufundisha, lakini umejikuta wewe ndo unapaswa kukaa chini ujifunze. Maana u mchanga wala hujaweza chakula kigumu.

  Tuendelee, lakini naona si muda mrefu utaanza na kutukana kabisa maana umeishiwa.

  Nguvu yako ilikuwa ndogo ndio maana unazimia hovyohovyo!

  Umelichokoza mwenyewe, kwa hiyo jibu hoja, manenomaneno hayasaidii.

  Ulidhani unaongea na watoto wa shule eh, ili uwapige tu blablah?!!!

  Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa!

  Kaa chini ujifunze!

 15. SUNGURA,
  Si lazima useme KWA SABABU INAONESHA WAZI, WEWE NI MPINGA KRISTO.
  HATA MAADILI YAKO YA THEOLOJIA HAYAJAKUSAIDIA!
  HAWA WASOMI ULIOWATAJA SI KIELELEZO CHA MKRISTO KWENDA MBINGUNI,
  NENO LA MUNGU NDIO KIELEZO CHA WAKRISTO.

 16. Pendael,

  Mimi sijasema hiyo amina!

  Umesema kwamba jogoo hajifunzi kuwika, bila shaka ulimaanisha kuwa nasi hatuhitaji kusoma!

  Oops,what a poor idea!!!

  Kwa hiyo mtu kuwa na ufahamu fulani hahitaji kujifunza maana huwa inakuja tu yenyewe kama ambavyo jogoo hujikuta tu anaweza kuwika.

  Huyo anayesema hayo na kuyaandika hakujua kuandika kiotomatiki, bali alifunzwa na walimu na hiyo ndio inyomsaidia kuweza kusoma biblia na kuandika haya. Lakini kwa kutokujua tu anasema elimu si ya muhimu.

  Kwamba Yesu hakuwahi kuagiza watu waende shule ili wamtumikie, hiyo inaweza kuwa ni kweli. Lakini mwenye fikra yakinifu angekumbuka pia kinyume chake kwamba hakuwahi kukataza watu kwenda kujifunza.

  Lakini hakuwahi pia kutuagiza kuwa ikifika usiku tulale, sasa sijui kwa nini huwa tunalala.

  Lakininhakuwa kutuagiza pia kwenda shule kujifunza kusoma na kuandika ili itusadie kulisoma neno lake, sasa sijui kwa nini huwa tunaenda!

  Sijui kwa nini anawaagiza akina Petro wakawafundishe watu kuyashika yote aliyowaagiza. Kwa nini awaagize, si angeacha tu wafundishwe na Roho mtakatifu.

  Mahali mafundisho yanatolewa huitwa shuleni au chuoni, kwa hiyo mitume waliagizwa wawaweke watu vyuoni!

  Pendael, mbona unarudia kusema vitu vilevile vya kubatiza watoto wadogo, huna kipya, au hayo ndo umekariri!

  Ngoja tuirahishe hii kazi;

  Kwenye mada ya Theolojia nilisema mfano wa wanatheolojia wa ukweli ninaowafaham na wametembea na Mungu isivyo kawaida:

  Nilimtaja Oral Roberts, nikamtaja Benson Idahosa, nikamtaja T.L. Osborn, nikamtaja Catherine Kuhman!

  Pendael tutajie watumishi watatu ambao wamepindua/walishawahi kupindua ulimwengu kwa kutembea na Mungu lakini hawajawahi kukaa shuleni kujifunza. Taja hata wa hapa Tanzania tu!

  Vipi, je mchungaji wako nae ni mbumbumbu kwa habari ya shule ila anatumiwa tu na Roho mtakatifu?

  Ni hayo tu!
  (Sijaedit)

 17. AGIZO LINGINE LA BWANA YESU KWA KANISA ;
  MARKO 16:17-20 ” Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.
  Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.”
  ****WATU WOTE NA WASEME AMINA.***

 18. SHALOM.
  WAPENDWA,
  IKIWA ASILI YAKO NI YA MBINGUNI HUTAKWENDA KUSOMEA CHUONI.
  KWA MFANO;
  HIVI, JOGOO ANASOMEA KUWIKA?
  Hebu tutafakari,
  1.Kama teolojia inaongozwa na ROHO MTAKATIFU mbona kila dhehebu linafundisha kivyake?
  2.Mbona wanatheolojia wakimaliza VYUO na wengine humaliza mpaka miaka saba huja na Mafundisho Ya Mpinga kristo? Mfano;
  a. Ubatizo wa watoto wadogo.
  b.Kipaimara
  c.Ibada za Kuombea wafu.
  d.Kuwafanya wanawake kuwa WAHUBIRI,MASHEMASI au WAZEE WA KANISA.
  e.Huwabatiza watu KWA JINA LA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kinyume na MITUME ambao walibatiza Kwa JINA YESU KRISTO ( MATENDO 2:38, 8:14-17, 10:48, 19:1-5,)
  f.Madai kuwa MITUME walifundisha kinyume Cha Bwana Yesu.
  g.Petro alikuwa papa wa kwanza wa dhehebu la Katoliki.
  nk.
  3.Wengi hutuambia kuwa YESU alisoma,mbona hawatuambii alisoma wapi mpaka darasa la ngapi?
  4.Mbona katika Maagizo Ya Bwana Yesu hakuna hata AGIZO MOJA kwa KANISA kuhusu kujenga Vyuo,hospitali au Shule? Bwana Yesu hakujua umuhimu wa elimu?
  5.Hawa MITUME wa YESU walisoma Chuo gani Cha BIBLIA?
  (AGIZO LA BWANA YESU KWA KANISA – MATHAYO 28:18-20, ” Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
  Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
  na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” )
  6.Dhehebu gani linafundisha teolojia kwa usahih?
  Haya ni baadhi tu ya mambo Ya kutafakari.
  Ahsante.

 19. haleluja!!!!!watu wa mungu mnamaoni mazuri sana na mungu awabariki sana,,…maoni yangu ni kwamba kuna watu ambao tayari wapo kwa ajili ya kuangusha kazi ya mungu kwanza tutambue ilo na adui mkubwa wa bnadamu ni ndugu yako mnayeishi pamoja nafikiri mnafahamu kikubwa ni kwamba Yesu alisema dunian mnayo dhiki lakini jitien moyo kwa kuwa yy ameshnda iyo dhiki kingne tukikaa kimya hakuna wa kumwinua mungu asanteni sana

 20. ktk ulimwengu tuliomo wakati huu; theology school ni ya muhimu. hata nami ningelipata chance ningeli join

 21. nina ushuhuda wa watu wengi ambao hawajasomea huduma lakini wanafanya kazi ya Mungu vizuri kuliko waliosomea.

 22. Mpendwa, Orbi.
  Naomba nieleweke kuwa Mtu kutafuta Elimu na ujuzi na kujifunza Maarifa ni jambo zuri sana, ali mladi ajue kuutawala moyo wake na ajue anajifunza cha nini hicho anachojifunza, ajue kuwa anachojifunza ndicho hasa suruhu ya tatizo la mazingira anamoishi. kwakuwa jambo hilo linapigania Maendeleo na Ustawi wa Kimwili lakini jambo lingine mhimu linaloletwa na Elimu ya kisayansi ni kuiongoza akili ya mwanadamu kujua kuwa YEYE HAWEZI LOLOTE! Ndiyo maana sayansi inapokwama kusuruhisha jambo lolote hudai kushindwa huko kunatokana na nguvu zilizo nje ya uwezo wa sayansi yao- NATURE! Lakini ukiwauliza “WHAT IS NATURE? – hugwaya!” Na inapotokea sayansi kushindwa ndipo Mwanadamu mwenye akili hujiuliza na kujua kuwa yupo Mkuu kulikoni hiyo sayansi, kwani watu wana pona, Saratani zao, vilema vyao, TB zao na hata ukimwi wao kwa urahisi tu kwa kutaja JINA LA YESU! Lakini kutokana na ujanja wa shetani, mtu hudhani kuwa na Elimu basi anajiweza! Watu wa kale walioitwa wsio na ustaarabu (hawakuwa na Elimu) ndiyo waliokuwa wakiadubu, japo miti au mungu Fulani – Utaona kuwa watu hao ndiyo walau walikuwa “na hofu kuwa wameumbwa” yaani mioyoni mwao, japo kwa UJINGA, wanajua yupo Mungu fulani! Lakini Wasomi na wataalamu wa Elimu ya sayansi wao kupitia Usomi wao, husema MUNGU hayupo! Biblia husema wanao abudu Mungu mwingine ni Wajinga, Bali anayesema Mungu hayupo ni MPUMBAVU! Natofauti ya Mjinga na mpumbavu ni kuwa; Mjinga hufundishika bali Mpumbavu hafundishiki – hadi hapo utaona kuwa Upumbavu NI GIZA la moyoni, kwa hiyo haliondoleki kwa maarifa yoyote ! lakini Ujinga ni GIZA la akilini, Mtu mjinga akieleweshwa huelewa, bali mpumbavu hujidhania anajua kumbe hajui kile anachofikili anakijua, mtu kama huyo utamgeuza ufahamu wake na nini? Ndiyo maana nashawishika kusema kuwa Mungu alijua hayo ndiyo maana hakuna pahala popote katika Biblia inaposema watu waende chuo kwa ajili ya utumishi wa Injili. Kwakifupi Wasomi ndiyo husema Mungu HAYUPO na hao ndiyo WAPUMBAVU! Utasema labda kuwa hao ni wanasayansi na siyo wana siolojia, ni kweli lakini, huoni Siolojia ilivyoshindwa kumthibitisha Mungu na hivyo kuzalisha mifarakano na ongezeko la madhehebu yanayotokana na kuitafsili Biblia KISOMI? Sifa za shetani kuu ni mbili, UONGO na KIBURI! Wasomi ndiyo wenyesifa hizo. Mjinga atamuongopea nani? AU mjinga atajivuna kwa lipi? Maana hajui lolote – kwake yote sawa tu!

 23. INJILI NI SHULE YA ROHONI!
  Wapendwa, kuweka matumaini katika kujitegemea kiuwezo na kiakili alikonako mwanadamu hakukuanza leo. Mara zote Watu wa “Mwilini” hudhani wanajiweza, kumbe ni masikini, vipofu na wamejaa mashaka! Neno lina sema “Bila mimi ninyi hawezi Neno lolote!” Kujaribu kulitafsili Neno la Mungu kwa kupitia Elimu ya vyuoni, ambako kwa kweli hutolewa elimu kulingana na ujuzi wa akili za kibinadamu, ni mpango wa shetani tangu zamani na kwamba aliuingiza katika moyo wa kanisa kwa akili nyingi tangu kale, na ni hatari kubwa sana ya kiroho. Isaya katika kitabu chake sura ya 43 na mstari wa 27 anasema “Baba yako wa kwanza alifanya dhambi, na WAKALIMANI wako wameniasi”Utaona na kugundua kuwa, Maarifa yameongeeka sana hasa ilipokaribia karine ya 21 hivi. Mfano,Gari la moshi limeundwa mwaka 1825, motokaa 1885, Ndege ulaya 1903 lakni pia TV na kompyuta zimeundwa 1930. Lakini ukirudi nyuma mfano mwaka 1300 katika maktaba ya chuo kikuu cha Sorbonne, Paris, Ufaransa kulikuwa na aina ya vitabu 1338tu, lakini sasa katika makitaba iitwayo Library of congress, ya Washington, DC,; inavitabu na magazeti zaidi ya 98milioni! Unaona, watu hufikiri kwamba,Elimu na Sayansi zitaleta Ufumbuzi wa matatizo ya Ulimwengu na kujidanganya kuwa wanaweza kuishi kwa ushindi! Elimu na Sayansi ya kimwili kamwe haiwezi kumfanya mtu amjue Mungu ili eti apate ujuzi, hekima au busara ya kutosha kutoa elimu ya Neno la Mungu kwa watu wasiomjua Mungu ili wamwamini! Mungu hathibitiki kisayansi – maana yeye ni ROHO – Si wakawaida na hivyo hafundishiki kwa ukawaida wa kisomi! Ndugu zangu, swala kuwa, eti tunajisomesha vyuoni ili kupata uwezo wa kuwasiliana na kufundisha na au kufanya watu walielewe Neno la MUNGU Kwa usahihi na kwa urahisi, kwa sababu kwamba si wa kabila zetu, si wa Taifa letu, si wa mira zetu nk, ni kujifariji kiungo! Neno katika Yn. 8:47 linasema “Yeye ailiye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu…………..” Mwanafunzi wa kweli ni Yule akaaye katika Neno la Mungu, soma Yh8:31. Roho mtakatifu ndiye mwalimu wa kweli, Yeye Alisha onya juu ya elimu zitakazotolewa na watu wa Dini kwa MAKUNDI YAO! ambayo tayali yapo; Waweza kuliona ONYO hilo wazi ukisoma,2Tim. 4:2-5. Vyuo vyetu hivi haviwezi kufundisha Injili ya Bwana Yesu, kwakuwa vimegawanyika na kusimama juu ya misingi ya imani ya Kimadhehebu – na Dhehebu halimpeleki Mtu mbinguni, maana hizo ni akili za wanadamu! Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu watu wake huwafundisha yeye kwa kadili ya kila Mtu na karama aliyopewa ili kuujenga mwili wa Kristo. 2Tim 2:7 ninasema, ” ……….maana Bwana atakupa akili katika mambo yote” Kufa na kufufuka kwake Bwana Yesu Kristo, ndiko pekee kulikowawezesha watu wawe,Wahubiri, Mitume naWaalimu; Soma, 2Tim 1:10-11.Vile vile, mwenye kuelewesha , useme nini ni Yesu, yeye alisema nitakuwa nanyi siku zote! Mt.28:20, Cha msingi mtu mwenyewe aichochee karama aliyopewa ili awe mwalimu mzuri wa Injili.2Tim.1:6. Mwisho namalizia kwa kusema kwamba Mafunzo ya Vyuo vya Dini, yamebuniwa Kwa mjibu wa Madhehebu husika, amboyo yapo kibinadamu zaidi,yanazingatia akili na Busara na Hekima za watu zaidi, hivyo hayawezi kuubeba Utukufu wa Mungu. Naweza kusema kuwa Injili ni UNYENYEKEVU! YESU ana sema katika Mt 20:26-27,”……………Bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwe wenu” Je, Kuna kiongozi wa taaluma au mtu mwenye cheo,asiyesoma?kuna msomi na Digrii zake hupokea maelekezo kwa mtu asiye msomi?- kwa wasomi wahubiri nao ni hivyo hivyo; Je, ulishapata kusikia Papa ana zamu ya kusafisha kanisa – Inagawa jengo hilo hudaiwa ni la Mungu anaye mtumikia? Au hata ulisha muona Mtume na Nabii Mwingira,akipiga deki kanisani na kupanga viti humo? Au hata kalidinali Pengo ulisha muona akinywa chai na watu wa kawaida mtaani? – Wasomi ndivyo walivyo!

 24. Ndugu Orbi,

  Nimepaona tulipoachania! Mimi nilipoiona mada, nikaichukulia katika ujumla wa kanisa, kumbe ilikuwa ni katika fungu la kidhehebu, haswa wanaokiri wokovu.

  Katika mtazamo huo wa kanisa, kama kundi dogo au dhehebu fulani, nayo tafsiri ya dhehebu ikiwa ni: “Jamii iliyokubaliana yenyewe juu ya utaratibu wa kumuabudu Mungu ambao ni bora kuliko wa wengine”; basi kulingana na viwango hivyo vya ubora wa ibada, vigezo vilivyokubalika huwa na umuhimu wa kuwekwa katika rejea ambazo ni lazima kwa viongozi kuzisoma, hivyo kuhitaji vyuo! Ni kwa mantiki hiyo ulazima wa “Kusomea kumtumikia Mungu” huwepo ili kubaki na ibada BORA. Basi katika hali kama hii ambayo kuna IBADA ZILIZO BORA zaidi ya 3000 ambazo kila moja ni BORA kuliko nyingine, navyo VYUO vikiwa vimegawanyika kuyahudumia makundi hayo, hapo nakubaliana na wewe kuwa ni vigumu kumchukua mchungaji wa Kipentekoste na kumpeleka kwenye chuo cha Kikatoliki!

  Bali dhana ya mada, katika mtazamo wa kanisa kama Mwili wa Kristo, suala hili kidogo litakuwa tofauti na mtazamo wa kidhehebu.

  Tunapozungumzia utumishi wa kazi ya Mungu, kuna umuhimu mkubwa wa kuyaangalia matakwa ya mwenye kazi kwanza, kabla ya sisi kuongeza ufundi wetu. Mifano iliyomo katika Maandiko ni kiongozi mzuri sana iwapo nasi tutafika katika kiwango cha hao walio mifano kwetu.

  Labda kwa vile sisi ni wa Agano Jipya, basi tuanzie hapo tu kwa uchache, tuyakague Maandiko ili tupate uhakika wa suala hili na jinsi lilivyotendeka. Tuanze na Yohana Mbatizaji. Tunaona Mungu akimpeleka majangwani badala ya chuoni kwa Gamalieli, ukizingatia baba yake alikuwa mtu mkubwa katika Dini ya Kiyahudi. Aliporudi kutoka huko majangwani na kuwajia Israeli na kuwahubiri, Maandiko yanatushuhudia kuwa, “Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote na nchi zote za kando kando ya Yordani; naye akawabatiza …” ukiendelea utawaona hadi wale magwiji waliosomea Torati walimwendea! Ni NGUVU gani iliyowavuta makundi yote haya? Je tuseme ni ELIMU yao ya Torati au ujenzi? Tukienda mbele kidogo tunamuona Kristo akiwa na umri yapata miaka 12 akitimua mjadala na wasomi wa torati hekaluni hata kuwastaajabisha kwa uelewa wake ilhali katika umri wake alipaswa kujua zaidi michezo! Tatizo kubwa alilokumbana nalo Yesu ni kukosa reference ya chuo. Wale magwiji wa torati walikuwa wanashangazwa naye kwa jambo hilo, kila mmoja akijaribu kukumbuka chuo alichosomea lakini waliishia kumuona akichonga meza za mbao na babaye Yusufu!

  Basi waweza kuona kuwa sisi mkononi mwa Mungu ni kama a bunch of change, mmoja ni senti hamsini mwingine shilingi mia nk, kwa hiyo Mungu hututumia katika jinsi hiyo. Paulo kwa elimu ya jamii aliyokuwa nayo, Mungu alimtumia katika namna iliyofaa kulingana na wigo aliomuwekea katika huduma, hata tunaona wale wanao mfahamu kwa usomi wake wakimtegemea kuchukua pengine nafasi ya Ukuhani Mkuu, lakini sasa kwa maneno anayoyahubiri wanamuona ana kichaa! Hata yeye mwenyewe anapoilinganisha elimu aliyokuwanayo na hii Mpya aliyoipata kwa Kristo, ameiona ni takataka!!! Hata hao wasiosoma elimu jamii, sote tu mashahidi wa udhihirisho wa NGUVU ya Roho Mtakatifu katika kutimiza yale aliyo yaagiza kwa watumishi wake.

  Uanafunzi wa mitume uko wazi kama unavyoonekana. Sijaona katika maandiko popote pale Mungu alipojenga chuo, si Agano la Kale wala Jipya. Lakini kama tukiyaangalia vizuri Maandiko na kuyaamini katika ukamilifu wake, tutaona wazi kuwa chuo ni kusanyiko, maana humo Mungu ameweka vile vipawa na zile huduma tano kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu, yaani mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na walimu! Huo ndio ukweli na kusudi la Mungu katika kuikamilisha yeye mwenyewe kazi aliyowatuma mitume kama tunavyoiona katika zile Injili nne; “Enendeni mkaihubiri Injili kwa mataifa yote mkiwafanya kuwa wanafunzi wangu….” bali hilo halitimii, ila kwa kuyaamini Maandiko

  Kwa hiyo tulipotoka nje ya mpango wa Mungu na kujenga vyuo, hiyo ilikuwa PERMISSIVE WILL yake kwetu, ambayo tumeshindwa kuinyoosha na tumeishia kuwa na migawanyiko mingi juu ya wazo la Mungu, kila mmoja akilitafsiri kwa hekima yake na hivyo kuwa na ‘school of thought’ nyingi na tofauti kwa wazo moja la Mungu. Kuhusu hizo ELIMU mtume Paulo anasema, “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake…” Kol 2:8.

  Matokeo ya kutoka nje ya Programu ya Mungu, wewe mwenyewe Orbi na ndugu wengineo walio na open mind mnaweza kuona tofauti iliyopo kati ya kanisa la kwanza, yaani mitume, kusanyiko lao liliwahi kufikia watu 70, hiyo ikiwa ni ndani ya ile miaka 3 na nusu, tunawaona wakitoka kwenda kuhudumu, na pia tunawaona mitume wakikamilika kihuduma katika muda huo. Lakini makanisa yetu ya leo, yakiwa chini ya viongozi waliotokea vyuoni, sisi wanafunzi wao tuliomo ndani ya makanisa wengine tuna zaidi ya miaka ishirini humo tunachojua na kuridhika nacho ni kuwatukuza mitume na manabii wetu, na kunena kwa lugha na mambo ya jinsi hiyo ya mwilini! NGUVU haipo kusanyikoni!

  Sasa kuwa na hiyo NGUVU, hulichukua kanisa lililo chini ya Programu ya Mungu kuyadhirisha hayo kama ilivyokuwa kwa mitume, katika kada zake zote wakidhihirisha kuukulia wokovu. Hebu niambie, dhehebu kama Katoliki, lina waumini labda tuseme 200,000 hapa Dar, je, wakifikia kiwango cha mitume katika miaka yao minne ya kwanza, ni uamsho kiasi gani ungekuwepo hapa Dar? Sasa chukua idadi yote ya wakristo waliopo Dar, halafu walete katika kiwango cha hata wale 70 tu, yaani akiwemo na Yuda Iskariote, unadhani ule umati uliokusanyika kumuaga Kanumba ungebehave kama ulivyofanya, kubadili mwelekeo ghafla kutoka hali ya msiba kuingia katika Hip Hop na kumshangilia Idol wao msibani? Hao ni watoto wa kikristo! Ile NGUVU haipo tena, wametia maziwa mengi kwenye kikombe cha kahawa imepoteza nguvu! Wahubiri wetu ni watoto wa Kish; tunamuhitaji Daudi ili tupate Ushindi, wako wapi wapakwa Mafuta wa Bwana waitetee Injili halisi itutie NGUVU badala ya hii cosmetic gospel iliyopo leo hii yenye ahadi za mafanikio kuliko hata mafanikio yenyewe?

  Basi injili za kutokea vyuoni, kwa kusanyiko lolote lile, likiitegemea hiyo, ni sawa na kuku anayeatamia mayai yasiyo rutubishwa na jogoo, atafia hapo kwa njaa usipomuondoa!!

  Bwana akubariki

 25. HEKIMA YA MUNGU
  Kuna hekima aina mbili

  i.Hekima katika Nuru (Hekima ya Mungu)
  ii. Hekima katika giza (yatoka kwa marehemu shetani na utawala wake)

  Utendaji unaoendana sawasawa na Neno ni hekima katika Nuru. Utendaji unaopingana na hekima ya Mungu ni utendaji wa giza (taratibu za dunia).

  I Kor 2: 1
  Kuna hekima zenye kushawishi akili za watu. -Hekima ya wanadamu, hekima ya mwilini, hekima za dunia.

  Wewe mwana wa Mungu unanena hekima ya Mungu katika siri – I Kor 2: 7. Vile vile, mimi na wewe tunayo nia na uhai wa Kristo ndani yetu. ‘Mimi siwezi nikaitwa marehemu hata siku moja’.
  Mt 6: 33.

  Lazima uwe na moyo gume-gume na uso gume-gume. Ndani ya hekima ya watu hakuna jawabu la kila ulitakalo. Lakini katika hekima ya Mungu kuna majibu yote. Unaweza ukatafakari kwa kina, “Mungu hufungua njia pasipokuwa na njia, liwe jangwani au baha-rini.” Pitia kwa undani msingi ulio nao ndani ya maisha yako, jikague bara-bara. Na uishi kwa jinsi na taratibu za Neno.

  Saa watu wote wamekukataa, Mungu ana uwezo wa kukupa chakula na kukuvisha hata kwa kuwatiisha kunguru. Soma Eliya alivyoishi bila taabu karibu na kijito cha Kerithi katika I Fal 17: 3-6.

  Yak 3: 13; Dan 2: 27, 5: 14

  Watu wa dunia walimtafuta Danieli kwa sababu alikuwa na hekima ya Mungu na hekima ya dunia (akili bora, nuru, ufahamu). Ukiwaza sawa sawa na Neno, unakuwa katika viwango vya Kiungu, na mambo makubwa ni la-zima yatokee.

  Dan 1: 1-5 – Shadraki, Meshaki na Abednego walifundishwa lugha na elimu ya Wakaldayo ili waende na desturi ya wakaldayo wapate kuwaelewavizuri. Mimi na wewe tunapata hekima ya kusomea kwenye vyuo vya wayunani ili tupate kuwaelewa vizuri.

  Kuwa mwangalifu katika mataifa na lugha unazotembelea na ulinde sana vitu vyako vya thamani usije ukaibiwa begi na adui.
  Hekima iliyomuinua Danieli ni hekima ya Mungu na ndiyo inayoniinua mimi na wewe pamoja na ufahamu na akili bora katika roho.

  Karne ya kwanza kwenye Kizazi cha Kwanza au cha Pili au hata cha Tatu cha Uumbaji hawakuwa na vyuo via thiologia via kuchambia Neno la Mungu kwa misingi na vigezo vya watu yet they thrived. Walidumu katika Neno na hao ndio wakatusimamishia misingi.

 26. Mabinza,

  La msingi kila leo ni kuweka uwiano wa Maandiko……Utasemaje kuhusu Paulo…..? Ni kweli kuwa hawakuwa na Elimu…..na wala hapa hatupingi kuwa na Elimu…..toka awali nimesema kuwa kadri Bwana alivyomwita ndivyo atakavyomtumia……na ni kweli Petro na Yohana hawakua na Elimu…..labda ndio maana hata katika Biblia wana Maandiko Machache mno kulinganisha na Paulo alielimika……! Roho Mtakatifu alijua hilo….na kutowatumia sana katika huduma ya Maandiko ambayo inahitaji elimu…..! Hata Petro kwa vile hakuwa na Elimu kubwa anakiri kabisa Nyaraka za Paulo ni ngumu….” KAMA VILE NA NDUGU YETU MPENZI PAULO ALVIVYOOWANDIKIA KWA HEKIMA ALIYOPEWA VILE VILE KAMA KATIKA NYARAKA ZAKE ZOTE PIA AKITOA HUMO HABARI ZA MAMBO HAYO KATIKA NYARAKA HIZO MAMBO AMBAYO NI VIGUMU KUULEWA NAYO NA MAMBO AMBAYO WATU WASIO NA ELIMU, WASIO IMARA HUYAPOTOA KAMA VILE WAYAPOTOAVYO MAANDIKO MENGINE…(2PET 3:15)
  Petro anakiri wazi watu wasio wasio na Elimu (ambayo hawajaelimika katika Maandiko) wanapotoa Maandiko Maandiko ya Paulo…….!

  La msingi ambalo Nalirudia kuwa Elimu ya Maneno ya Mungu ambayo Imevuviwa na Roho Mtakatifu kwa mtumishi ni kitu chema…..! Hata Roho Mtakatifu akitenda jambo lolote lazima awe katika wigo wa Maandiko yake mwenyewe…..!
  Utasemeje kuhusu Paulo aliposimama mbele ya Mfalme Agripa…? Kumbuka Agripa alivyosema….”PAULO KUSOMA KWAKO KWINGI KUMEKUGEUZA AKILI…….na Paulo alijibu…..SINA WAZIMU EE MTUKUFU FESTO….BALI NANENA MANENO YA KWELI NA AKILI KAMILI (Matendo 26:24)

  Nahitimisha kwa kusema sisi ni vyombo tu…..Bwana anaweza kututumia Apendavyo…..kama alivyofanya kwa Petro na Yohana wasio na Elimu na Ndivyo alivyofanya kwa Paulo alivyokuwa na Elimu…..na labda ndio maana (kwa matazamo wangu) Roho Mtakatifu kwa kutumia Elimu ya Paulo, aliisambaza Injili kwa umbali zaidi katika Greco Roman World na Maandiko yake kubakia mhimili mkubwa wa Agano Jipya…..

 27. INJILI HAISOMESHWI KIMWLI!
  Wapendwa, Neno la Mungu linasema, katika Mithali 16:25 kwamba “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti” 16:1 inasema “Maandalio ya Moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ULIMI hutoka kwa Bwana“ lakini mstari wa 3 unasema “Mkabithi BWANA njia zako, na mawazo yako yatathibitika” ukiundea mstari wa 21 unasema “aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye Busara; utamu wa maneno huongeza Elimu, mwisho angalia mstari wa23, unasema, “Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake” Aletaye Maarifa na Ujuzi na Hekima na Busara ni Roho Mtakatifu – HUYO NDIYE MWALIMU. Wapendwa yatupasa kuwa makini, Watu huangamia kwa kukosa MAARIFA, Na maarifa hupatikana kwa M walimu mkuu – Roho mtakatifu. Kabla hatujaenda mbele sana na mjadala wetu huu mzuri, tutofautshe kwanza maana ya hasa tunacho maanisha katika mjadala huu. Kwanza ieleweke kuwa Hakuna Chuo Duniani KINACHOFUNDISHA MTU KUFUNDISHA NENO LA MUNGU; Bali kipo chuo Duniani, kinachofundisha MTU KUHUBILI “MAHUBILI” KWA IMANI YA DHEHEBU FULANI! Ndiyo maana utakuta, kuna vyuo au chuo cha Romani katoliki, cha Anglikana, cha Wasabato, cha Waluteri, Chuo cha AIC, chuo cha Wapentekoste (Ambao nao tayari hawako katika imani moja!) utakuta chuo cha pentekoste swidish, holliness, pentecoste of canada n.k! na kama mnakubaliana nami kuwa hayo ni kweli, basi tusiende mbali sana, tujiulize tu kwa kifupi kwamba; Kama vyuo na shule hizi zinazoitwa za Biblia, zinawatayalisha “Watumishi” kwa imani ya madhehebu husika, Je, hili halitoshi kufikia mkataa kuwa; YANAYOFUNDISHWA HUMO NI MAFUNDISHO YA WANADAMU NA SI MAFUNDISHO YA MUNGU? Je, liko andiko linalo sema kuwa MWANADAMU YAMPASA KWENDA HUKU NA HUKO DUNIANI KUJIFUNZA INJILI KWA BIDII KABLA HAJAANZA KUIHUBIRI?! Hapa sizungumzii Elimu inayotokana na Hekima za Wanadamu, kama vile; Uhasibu, Udakitari, uchumi, sayansi ya udongo, madini au ya viumbe hai nk, bali hapa nazungumzia Elimu ya Neno la Mungu – Biblia ambayo kwa uwazi inasema kuwa UJUZI KATIKA NENO LA MUNGU hupatikana tu kwa KUFUNDISHWA roho mtakatifu. Hivyo Chou cha Mambo ya Rohoni ni Biblia na Mwalimu wake ni Roho Mtakatifu tu basi!, Nikodemo aliambiwa na Yesu “………..kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Huwezi kamwe kujifunza mambo ya Kimwili yakatumika kiroho, na kutoa matokeo ya Kiroho! Elimu kama ya uhasibu, utunzaji hesabu za fedha nk.ni Elimu vitu vya kimwili – Elimu hii ya Sayansi, Elimu ya mambo ya Jamii, nk. kwakweli ndiyo inayosimamia kanuni za kawaida za Ulimwengu na mwenendo wa dunia na mazingira yake. Na hii si mbaya, maana imewekwa hapo na Mungu, ili ithihilishe ukuu wa Mungu na utimilifu wa Neno lake! Pengine watu hawajui kuwa, zinapofeli kanuni na sheria za kimaumbile, muujiza wa Mungu ndipo unapo hitajika! Mfono mmoja, Tunajua kupitia elimu ya sayansi kwamba, Density inapokuwa ndogo, Volume huongezeka na hivo hupelekea kitu kuelea katika maji. Wote tutakubali kuwa kwa kanuni ya uhusiano wa Density na Volume,mtu haiwezekani kutembea juu ya maji! Lakini Yesu kwa” kuopozi” hiyo kanuni ya ’flotesheni’ akatumia kanuni tuyoiita leo “muujiza!” Na kwakuwa hapo mwanzo aliwahi kukaa juu ya maji haikuwa vigumu kwake kutembea juu ya maji, watu wanaona huo ni muujiza kwa kuwa kanuni za Elimu ya maumbile ya Dunia haikubaliani na tukio kama hilo. Lakini sioni popote kama Yesu mwenyewe alikiita kitendo hicho Muujiza! Biblia inasema alitembea tu juu ya maji! Na watu wa kiroho hawashangazwi na hilo, maana wanajua kuwa, Mungu wao huyo hapo mwanzo alikuwa akiishi juu ya Maji –kwao huo si muujiza! Kwakifupi kujifunza na kujua kuwa Biblia ilikuja lini, Lugha yake ya asili, au kuitafasili au kujua Dini gani ilitangulia au kujifunza namna ya kuhutubu, au kuwatambua watu kisaikolojia nk yote hayo si Dhami na si mabaya, ila siyo KUIJUA INJILI, ni kama kujifunza kuandika, kusoma kupika, kuongea Lugha nyingine, kufanya biashar nk. Yote hayo si dhambi lakini si INJILI – kuongeza au kutafuta maarifa yahusuyo elimu ya kimaumbile au historia ya mambo fulani ni jambo jema lakini yote hayo hayakupi uwezo wa kweli wa kuishuhudia injili! Ujuzi au elimu ya kuelewa na kasha kuihubiri Injili upo hapa:- kwa uchache Soma, Mdo 1:8,2:38, 4:1-3 na malizia na 4:13.ambayo inasema “Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na ELIMU, wasio na MAARIFA,wakastaajabu,WAKAWATAMBUA YA KWAMBA WALIKUWA PAMOJA NA YESU”
  Taafadhali tuendelee kujifunza kwa uvumilivu, Mbalikiwe wote.

 28. Asante Orbi na Sam kwa tafakari nzuri,
  Bado kusoma ni muhimu “mshikikeni sana elimu “,

  Asante Mpendwa Orbi kwa maandiko yako.

 29. Sam,

  Nimekuelewa na Bwana Akubariki kwa kutuelimisha, Lakini ulipomalizia kwa kusema kumpeleka mchungaji wa Pentekoste akasome chuo cha kikatoliki naona unatoka nje ya Mada……..na sidhani hapa tunazungumzia hilo…….Je Wapetenkoste wanaweza kumpeleka mtumishi wao akapate mafunzo kuhusu msimamo wao wa Imani katika chuo cha Katoliki….? Au Wakatoliki kumpeleka mtumishi wao katika chuo chenye utofauti wa tafsri

  ya imani na wao wanavyoamini…? Na hata mada hii inapozungumzia “Kusomea kumtumikia Mungu” nadhani imejikita katika imani fulani…..na kwa sababu tuko katika Blog hii tunajua wazi ni Imani ya Wokovu…….!

  Hivi kama Hakuna kukaa chini na Kujifunza Kwa nini Yesu aliitwa Mwalimu au wakati mwingine aliitwa Rabbi….unajua maana ya Rabbi katika dini ya Kiyahudi…? Kwa Kifupi Rabbi (Mwalimu) alikuwa ni mwelewe wa maandiko ya Kiyahudi (Talmud) au Torah….na kwa nini wafuasi wa Yesu kuanzia mwanzo waliitwa Wanafunzi….? Na kwa nini Yesu hakuamua kuleta “Mafunuo” ya kumjua Mungu yawashukie wanafunzi wake….? Kwa Nini aliamua kukaa nao miaka mitatu…akiwafundisha…? Kwa kifupi mafundisho ya Neno la Mungu na Ufunuo kutoka kwa Mungu vinaenda pamoja…! Wakristo katika kanisa la Kwanza “wakawa wakidumu katika FUNDISHO LA MITUME” .

  Hebu angalia katika ibada karibu zote za Kikristo….Kulifundisha Neno la Mungu ni sehemu kubwa ya Ibada….na utaratibu huu tumeupokea toka dini ya Kiyahudi……Yesu mwenyewe alipoingia Hekaluni mara ya kwanza alipewa gombo na kufundisha…..! Tunapokwenda Jumapili makanisani la awali kabisa ni kujifunza….na tunatimiza maneno ya Yesu ya kuwa Wanafunzi wake….!

  Hivyo basi napokwenda Chuo cha Biblia badala ya kujifunza kwa utaratibu wa Kila Jumapili kama muumini mwingine…..mimi hujifunza kila siku kwa utaratibu maalumu kwa kipindi cha utaratibu wa chuo ulichoniwekea….! Inaweza kuwa miezi sita…mwaka….miaka miwili….minne nk! Hebu niambie ni kinyume cha Roho Mtakatifu kufanya hivyo….? Kwangu mimi naona ni baraka kwa mtu kumpa Mungu muda wake iwe miezi sita…..mwaka….miaka ili tu kukaa na kujifunza Maneno ya Mungu pasipo bugudha yoyote….! Kwa lengo la kwenda kuwafundisha wengine…!

  Labda utauliza miaka hiyo yote najifunza nini…? Itategemea….! Kwa mfano mafunzo kuhusu Agano jipya (New Testament survey) Nitafundishwa Historia ya Maandiko hayo….ni lini yaliandikwa….yaliandikwa na Nani….kwa nini aliandika……mwandishi alimwandikia nani (kumbuka kwamba Maandiko haya kwa sehemu kubwa hatukuandikiwa sisi…! ) Utapata muda wa kukaa na kujifunza kwa nini Wagalatia……kwa nini Wakorintho…….kwa nini Waefeso waliandikiwa nyaraka hizi……Hivyo kwa utaratibu kabisa unakwenda mstari hadi mstari……aya hadi haya kupata dhana nzima ya mafundisho….historia…..mazingara ya wakati ule….lugha iliyotumika….na kwa nini sisi (dhehebu lako linatafsiri hivi maandiko haya…..kwa nini dhehebu lile linatafsri vile) nk…! Utajifunza Kanuni za kutafsri Maandiko) Kila Dhehebu lina kanuni zake…..ambazo linaamini zitatupa maana halisi ya Maandiko……..! Hata madhehebu yanayodai Roho Mtakatifu ndio atakayetufunulia….lakini mara nyingi wamekataa mafunuo fulani ya Maandiko kwa kutumia tu Kanuni ambazo dhehebu hilo limeamini zinaweza kutoa maana halisi ya Maandiko kutokana na msimamo wa dhehebu hilo…..!

  Kwangu mimi narudi pale pale Wito wowote ambao Bwana amemwitia Mtumishi wake unahitaji mafundisho fulani……hata kuwa chini ya mtumishi fulani aliyekutangulia katika huduma bado ni mafundisho….! Sina ujasiri katika mtu anayesema ameitwa na Bwana……bila ya huyo kukaa katika aina fulani ya kufundishwa kwa usahihi…..na mtu mwingine…….sio kudai “MAFUNUO” naona ni utaratibu ambao umejikita sana katika Kitabu cha Agano Jipya……

 30. Orbi, asante kwa challenge!

  Nimekuelewa unachokisema au wazo ulilonalo kuhusu jambo hili. Lakini bado nadhani kuna umuhimu wa kuitazama tena mada yenyewe ili maelezo yetu yafikie kui address mada kama ilivyoletwa.

  Jambo ninaloliona katika maelezo yako ni glorification ya elimu. Hilo ni sawa, lakini ni lazima ieleweke pia kuwa elimu ina mapana ‘marefu sana’ na yanazidi kuongezeka kila kukicha. Kwa mfano, kuna elimu ya viumbe, elimu ya nyota, elimu ya dini, hesabu, nchi, historia, mambo ya kale, nk msururu ni mrefu sana maana uvumbuzi katika kila nyanja unaendelea kujitokeza! Elimu zote hutusaidia kukabiliana na mazingira na changamoto za maisha katika dunia yetu iliyojaa matatizo. Kwa hiyo utaalamu wowote ule hukupa ajira katika kuyasawazisha hayo yanayotutatiza, yaani kimsingi elimu ni ‘nuru’ kwa jamii yoyote ile. Huo ndio Mwanzo na Mwisho wa elimu! Pia ni vizuri kufahamu kwamba elimu si jambo geni kwa Mungu, bali linamhusu yeye kikamilifu. Ndio maana tunaona akiwaagiza watumishi wake ‘kuandika’, akijua wazi msomaji wa hayo atakuwa ni nani!

  Labda kabla hatujaenda mbali, katika kuweka msingi, niseme kwamba Elimu katika ujumla wake kulingana na mapana yake, chimbuko lake ni ule Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya! Kwa hiyo mema ya elimu ni mema tu kama lilivyo jambo lolote jema. Hilo hutumika hata makanisani katika kiwango chake hicho, bali haligeuki kwa wema wake huo kuwa Neno la Mungu! Yaani unajifunza kutunza mahesabu huko elimu ya kutunza mahesabu inakotolewa, ukifuzu, ujuzi wako huo, kanisa laweza kuutumia katika kutunza mahesabu yake, lakini kutunza mahesabu ya kanisa hakukupi UZIMA wa Milele! Je, pale Mungu anapoufunga unabii licha ya kwamba umeandikwa, ni chuo gani kinaweza kuufungua? Kama kipo chuo hicho, hebu tuwapelekee Dan 12:4 watufungulie!

  “Hekima” ni jambo complex kidogo, wakati mwingine sisi hutumia akili zetu na watu hututambua kuwa sisi ni wenye Hekima! Ndio maana ili kuepuka jambo hilo, Mungu ametenganisha kwa makusudi NJIA yake na njia zetu ili kusiweko na kujichanganya, 1Wokor 1:18-19.

  Unajua ndugu Orbi katika kumtumikia Mungu, kuna Mapenzi ya Mungu Makamilifu na Mapenzi yetu Anayoyaruhusu, ambayo pia Mungu huyaruhusu kulingana na tulivyoomba. Kuyatenganisha Mapenzi haya mawili unahitaji kuwa na Hekima ya Mungu. ‘Kusomea Kumtumikia Mungu’ ni mojawapo ya hayo Mapenzi yetu ambayo Mungu ameyaruhusu ili iweko tofauti na wale anaowatuma Yeye katika Mapenzi yake Makamilifu. Waweza kuona mfano wa Mapenzi hayo mawili jinsi yanavyotimia ukimuangalia Balaamu nabii katika huduma yake. Katika Hesabu 22:5-35, humo utamuona Balaamu alipojiwa na wale wajumbe, aliipeleka ile shida yao Mbele ya Mungu na kupewa jibu lake kuwa asiongozane nao hao wageni. Jibu alilopewa lilikuwa ndio PERFECT WILL ya Mungu. Lakini mbele kidogo wageni walirudi tena kuja kumsisitizia ile shida yao na ahadi ya zawadi nono zaidi akiwatimizia! Balaamu AKARUDI TENA KWA MUNGU KWA SUALA LILE LILE ALILOKWISHA PEWA JIBU LAKE, yeye, kwa makusudi ya kupata sifa/cheo na pesa, akajidhanisha kuwa huenda Mungu alijichanganya katika jibu lake la kwanza! Naye Mungu akiyajua mawazo yake, akamruhusu aongozane nao, hiyo ndiyo PERMISSIVE WILL ya Mungu!! Israeli pia, ambao ni mfano wa kanisa, walipotoka Misri hawakuwa na Sheria, bali Neema. Walikuwa na nabii wa Mungu, Nguzo ya Moto na Wingu vikiwaongoza na kuwahudumia. Lakini mbele kidogo yakaanza manung’uniko, hata waliposhushiwa mana na kuambiwa siku ya saba wasitoke kuitafuta, wao wakatoka kuitafuta wakimtaka Mungu awawekee Sheria!! Mungu akawaletea SHERIA baada ya Neema kuwashinda!!! Soma Kutoka milango ya 17- 20.

  Basi kanisa, kama Israeli, ambao ni wa kimwili, tusipoyapokea mambo ya ROHONI, hujikuta katika mapito ya Israeli maana ndio kivuli chetu. Kama sheria ya maumbile ilivyo, ukikiona kivuli, utakapokifuatilia kivuli hicho utalikuta umbile lake halisi, ambalo kwa Israeli kuwa kivuli umbile ni kanisa! Maana kama Israeli walivyo ikataa Neema na kuililia Sheria, vivyo kanisa limeukataa Uongozi wa Roho Mtakatifu na kuchagua Elimu kuliongoza!!

  Nimeziona “SIAMINI….!” nyingi ulizozitoa, lakini confession za namna hiyo zina hatari kwa afya ya Kiroho, maana hizo humfungia Mungu nje pale anapotaka kukuvusha katika hatari nyingi zinazotukabili. Yuko mtu mmoja, mkristo, ambaye alikuwa haamini katika Uponyaji. Alipokutana na muinjilisti anayeamini katika ahadi hiyo, ambaye pia huombea wagonjwa, katika mazungumzo yao yule mkristo akamwambia, “siamini mambo hayo hata ukimfufua mfu mbele yangu!” Alipoona muinjilisti anamshangaa, akaongeza akasema, “ili niamini labda unipige upofu sasa hivi”, muinjilisti akacheka na kumwambia ‘hapo ulipo kipofu tayari, labda nikuombee upofu ukutoke, lakini hata hivyo haya ni mambo kwa wale wanoamini tu!

  “Abc” ya kwanza ni kuliamini Neno la Mungu. Kama amesema Roho Mtakatifu atutosha, AMINI hilo kwanza, ndipo utaweza kuzipambanua ALGEBRA za Mungu maana yeye ni MIUJIZA MITUPU, hasomeki shule bali kwa IMANI ambayo ni UFUNUO!!!

  Kuhusu mitafaruku, nadhani tukiviangalia vyuo vyetu na doctrines zinazo vitawala, twaweza kuliona hilo kwa uhakika, vinginevyo hebu tujaribu kuwapeleka wachungaji wetu wa Kipentekoste wakasomee katika vyuo vya Kikatoliki!

  Tunaendele kujifunza kwa ajili ya Utukufu Wake!

 31. Sam,

  Kwangu mimi siamini kuwa kukaa na kusoma ili kumtumikia Mungu ndio kiini cha mtafaruku katika imani leo….! Maana hata mwingine anaweza kusema kinyume na wewe yaani kutokaa na kusoma/kujifunza maneno ya Mungu ndio kiini cha mtafaruku uliopo katika Imani leo…….Labda nikuulize ni mtafaruku gani huo unaozungumzia

  Kumbukuka tu roho ya ukengeufu na upotevu inaweza kumwingia “mtumishi” yoyote yule…! Aliyekwenda chuo au kuketi kujifunza maneno ya Mungu au hata yule ambaye ameamua kuongozwa na mafunuo yake tu…..! Hapo sio mafunzo…bali ni roho ya upotevu ambayo inaweza kumuingia mtumishi yoyote ambaye hajajitoa katika Maneno ya Mungu.

  Na tunapozungumzia kwenda kukaa masomoni kujifunza neno la Mungu si kwamba tunakataa na kupinga kuwa chini ya Uongozi wa Roho
  Mtakatifu la hasha…..maana hata asiyekwenda shule au kuingia masomoni anaweza kabisa kuongozwa na hekima zake za mwilini na kukataa kuwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.

  Kumbuka kwamba Roho Mtakatifu anatakasa ufahamu na uelewe wetu…..na kama nilivyosema awali kila mtu anapoupokea Wito wa kumtumikia Mungu lazima aongozwe na Roho Mtakatifu katika kuutenda Wito alioitiwa….! Siamini kwamba Bwana ataniita niwe mtunza mahesabu ya Kanisa/ au Huduma yoyote ya fedha wakati hata sijui kabisa angalau misingi ya kutengeneza ripoti ya mapato na matumizi ya mwisho wa mwezi……Siamini kabisa Bwana ataniita katika kuwafundisha wachungaji jinsi Maandiko yalivyotufikia kutoka kwenye Gombo mpaka leo tunapolishika mkononi bila kunikalisha katika mafunzo ya aina fulani……! Siamini kabisa Bwana anaweza kunipa wito wa kufundisha historia ya taifa la Israeli katika mpango wake wa Wokovu na hata taifa hilo lilivyofika hapo lilipo leo bila kunikalisha katika mafunzo ya aina fulani……Siamini kabisa Bwana anaweza kunipa wito wa huduma ya counseling (ushauri) wakati sijui lolote lile kuhusu hata “abc” ya
  psychology ya mwanadamu…..Naamini kila wito wa Mtumishi unaandamana na aina ya mafunzo fulani kwa mtumishi huyo….! Maandalizi haya huyafanya Mungu mwenyewe hata kabla ya wito kuwa wazi…..pengine hata kabla ya Kukoka…! Musa aliandaliwa kupata Hekima ya Misri katika nyumba ya Pharaoh hata kabla ya hajaupokea wito wa Mungu….na Kwa Paulo vile vile…unaona maandalizi ya mafunzo ya huduma zao hata kabla ya wito……! Na nimeona Mungu akifanya hivyo leo…..!

  Kwangu mimi siamini kwamba Ukiokoka Mungu anaondoa hekima ya kibinadamu…..la ! bali Mungu anaitakasa kwa ajili ya utumishi wake

 32. Wapendwa,

  Mada iliyopo ni ‘Kusomea kumtumikia Mungu’. Sasa ni vizuri tukaelewa kwamba ili uende ukasomee huko kumtumikia Mungu, unalazimika kwanza kuwa na elimu hii ya kawaida inayofunzwa mashuleni halafu ndio ukiusikia “wito” au kazi za kuajiriwa zikiwa duni, unaweza kuamua kujiunga na chuo cha Teologia.

  Elimu ni jambo zuri sana katika namna yoyote ile kwa maisha yetu. Lakini suala la “Kusomea kumtumikia Mungu”, nadhani ndilo kiini cha mitafaruku yote ya kidini tuliyo nayo. Vyuo vya Teologia katika ujumla wake hufundisha Biblia, lakini pia hupandikiza mawazo ya kibinadamu juu ya Neno la Mungu kama alivyolielewa mtu maarufu fulani katika fani hiyo, mapandikizo ambayo huwa rejea ya kukuwezesha kufaulu mitihani ya chuo husika na kukubalika na jamii inayohudumiwa na chuo hicho! Kwa hiyo muhitimu hukabidhiwa cheti pamoja na “theme” atokapo chuoni hapo na hivyo mahubiri yake huelekezwa katika mtazamo huo na si ule wa Neno la Mungu kama inavyopaswa! Basi mafundisho huanzia katika vyuo, ambako misingi ikiwa imekwisha kuwekwa, vyuo vya manabii!

  Lakini Mungu katika kuikamilisha kazi yake, yeye hututumia sisi kulingana na Hekima yake. Jambo la kwanza tunaloliona Mungu anapotaka kumtumia yeyote yule, huiondoa hekima itokanayo na elimu! Maana hivyo viwili havikai pamoja. Paulo alikuwa msomi mzuri wa Torati lakini haikumsaidia kumjua Mungu! Musa alikulia katika nyumba ya Farao, alipata elimu iliyo bora katika Misri, lakini haikumsaidia kuitimiza kazi ya Mungu! Wote hawa wawili tunaona Mungu aliwatoa katika mifumo waliyokuwemo na kuwaingiza katika Mfumo Mpya ambao yeye mwenyewe ndiye Mkufunzi. Elimu ya kawaida ni muhimu kwani ndiyo inayotuwezesha kuyasoma Maandiko.

  ‘Kusomea kumtumikia Mungu’ ndiko kulikoleta UBARIDI katika kanisa!! Mungu akikuteua kwa Huduma yake, hushughulika na wewe kikamilifu. Nimewaona watu wakitaka uhakika kutoka kwa Mungu kabla ya kuyaendea Mungu anayowatuma wakayafanye, kama akina Gideoni, Musa nk. tofauti na hawa waliojifunza vyuoni hadi namna ya kuwaomba watu pesa!!!

  Ukifuzu Chuo, unapewa Shahada na cheo kikubwa, hili pia huleta msisimko! Lakini shahada hiyo huwa ni badala ya Roho Mtakatifu!!! Kwa hiyo yule Roho anayepaswa kukuweka katika kweli yote anapokosekana, rejea za wale maprofesa uliowakariri huwa mbadala unakubalika na kuaminika!

  Mbarikiwe nyote!!

 33. KUNA TOFAUTI KUBWA SANA KATI YA MTUMISHI WA MUNGU AMBAYE AMESOMA NA AMBAYE HAJASOMA.HUWEZA KUFUNDISHA NENO LA KWELI LA MUNGU KAMA HUJASOMA NA KULIELEWA NENO. VINGINEVYO UTAANZA KUWA NA MISIMAMO NA MAFUNUO YANAYOTOKANA NA HISIA ZAKO TU. MBARIKIWE!

 34. wito na kusoma vyote ni lazima viende pamoja! bila wito hata kama ukiwa na degree za theology hamna kitu, lakini pia unaweza kuwa na wito LAKINI elimu yako ikakuzuia kutumika katika kile kiwango ambacho Mungu anataka utumike! amen.

 35. Hakuna ubaya wowote katika kusomea huduma, lakini inapunguza uonekano ya nguvu za Mungu. Kilichokuwa kinawastaajabisha Mafarisayo na Waalimu wa sheria pamoja na wayahudi wote ni jinsi gani watu hao ambao malikuwa hawajasoma walikuwa wananena kwa ujasiri na kuongea kana kwamba wamesoma. Na hiyo elimu ya injili hasahasa ni ile ya Roho Mtakatifu.

  It was really spectacular and amazing. They all knew only God could do something like this and His full power and glory was seen and revealed. I even think that’s why there was so much power to perform signs and wonders which I think we do lack today.

  God’s power is fully revealed when you are nothing and have nothing to boast of….
  It also puts routine to naught and gives room for the Holy Spirit to take total control in all that’s been done and said by the used person.

  I’ve met people who are not yet ministering just because they didn’t get a sponsor to a Theological college. That’s really bad dependence. It’s really tragic when it gets to this stage.

  I’ll better not robt he cross of it’s power.

  God bless you all.

 36. Mpendwa Haule,

  Naogopa mno watu wanaobeza watu wa Mungu kwenda kusoma……nadhani hawajasoma Kumbukumbu la Torati, na kuuuona umuhimu ambao Musa alitoa katika KUJIFUNZA torati, maadamu Mungu alitupa Maneno yake katika maandishi hiyo ni sababu tosha kwa wale wanaotaka kuwafundisha wengine kukaa chini na kujifunza ili kufundisha wengine.

  Na kama nilivyosema katika post ya awali ni kujua Mungu amekuitia huduma ipi na wapi, Hebu angalia uhitaji wa Masomo kwa yule aliyeitwa kuwahubiria wanafunzi wa Chuo Kikuu au wakazi wa mijini na waliosoma na ambao wanajua dunia inaendaje na mtumishi ambaye ana wito wa kukaa vijiji ambavyo havijafikiwa na Injili,

  Kwa kifupi Changamoto za ufahamu wa maneno ya Mungu zitatofautiana…! Atakayehudumu kwa wanafaunzi wa chuo kikuu ufahamu wa dunia ya leo (current issues) ni muhimu mno, critics (wapingaji) wa imani ya Kikiristo katika mazingara ya wasomi ni tofauti na kijijini…..Uelewa wa mafundisho ya Darwin (evolution theory) madhaifu na mapungufu yake ni muhimu mno kuufahamu ………kujua angalau abc ya economics, sociology, pyschology, world history nk vinafanya Mtenda Kazi wa Bwana kuufikisha ujumbe wa Yesu kwa kuuonyesha kuwa uko juu zaidi ya hekima yoyote ya mwanadamu…….! Kujua imani nyingine kama Uislamu/Hinduism nk zinafundisha nini…….na nini mapungufu yake katika kumkomboa Mwanadamu…..! Je kuna tumaini katika siasa ziwe za mlengo wowote ule kutengeneza dunia bora….? Je technolojia ya mwanadamu itamfikisha wapi………Paulo katika Ulimwengu wake aliyajua haya yote ……na hata aliposema Hekima ya Mwanadamu ni upumbavu mbele za Mungu alikuwa anajua anasema nini ….! Aliisha ona Greek Logic……Judaism na Romans Law huviwezi kabisa kuvipambanisha na INJILI YA KRISTO….!

  Hivyo wapendwa angalia huduma yako umeitiwa nini……..na kuichochea huduma kwa wengine ina maana kwenda shule za Biblia…..ili kwaq wale wanaoubeza watambue kwamba INJILI YETU sio ya kuionea aibu……ni juu ya hekima zote za mwanadamu…!

  MBARIKIWE

 37. “Our Churches Need Pastors Who Can
  Teach the Truth and Refute Error”

  For the overseer must be…holding fast the faithful word
  which is in accordance with the teaching, so that he will be able both
  to exhort in sound doctrine and to refute those who contradict. (Titus 1:7, 9)

  The shift of our culture toward a post-modern worldview is affecting the way that
  some folks view the church and the role of the pastor. On the church side of the equation,
  they are urging the church to be less certain of its answers—when relativism is in style,
  dogmatism is outdated. Regarding the pastor, the post-modern church doesn’t need “a
  seminary-trained theologian dispensing truth”—when relativism and experientialism are
  considered chic, truth-filled theology is passé. This view of the pastor needs to be
  examined carefully under the light of Scripture.
  When Paul charged Titus to see to it that elders were ordained in the churches of
  Crete, he also laid out standards by which to measure the qualifications of those men for
  this office. The character qualities listed in passages like 1 Timothy 3 and Titus 1
  properly receive great attention, but I am afraid that the ministry qualifications listed in
  the verses above are too often neglected. It seems that the contemporary church, both
  evangelical and fundamental, is content, if men have good character, to ignore the fact
  that God said He wanted men who hold faithfully to the doctrines of Scripture and have
  the ability not only to teach them, but to refute those who are contradicting them.
  Please don’t misunderstand me, I don’t think we should pit one against the
  other—God wants both! Anything less is short of what God requires. I have been
  absolutely shocked at times to hear of churches that will call a man to be their pastor
  while openly admitting that although he is not a very good preacher, he really loves
  people, is a good organizer, etc. Those things are certainly necessary, but if a man can’t
  preach and teach the Word, what good is that kind of pastorate? It would be like buying a
  car that has a great stereo system or a nice paint job, but has a blown engine. You buy a
  car to drive, not to look at or sit in to listen to the stereo! The primary task of the pastor is
  to preach and teach God’s Word, cf. 1 Tim. 3:2; 4:6; 5:17; 2 Tim. 2:15; 4:2; 1 Ths. 5:12;
  Acts 6:4. God cares about the character of the pastor because it has either a positive or
  negative effect on the ministry of the Word. In other words, a pastor’s character matters
  because he is supposed to be a man of the Word he preaches.
  And our text above says that the ministry of the Word has both positive and
  negative sides to it. The pastor must teach the truth and refute error. Paul understood that
  the devil was actively seeking to sprinkle error into the beliefs of God’s people. He
  warned the Ephesian elders to watch out for false teachers who would come from outside
  the flock and some who would arise from within it (Acts 28:29-30). The danger is no less
  real today, and one could argue that the advent of the printing press, radio, and TV make
  the threat even greater.
  Any view of pastoral ministry that minimizes the preaching and teaching of sound
  doctrine is out of step with the Bible. The full-blown error represented by those who want
  to reinvent the church is more recognizable than the subtle error of those who try to
  minimize doctrinal issues in order to promote unity, win souls, or whatever happens to be

  the issue of the moment. Contemporary evangelicalism seems too happy to minimize
  doctrine in order to save the culture; how else can anyone justify forging alliances
  between evangelicals and Catholics? Sadly, some sections of contemporary
  fundamentalism seem more interested in creating an appearance of unity than in
  preaching and protecting the doctrines of God’s Word; isn’t there a real difference
  between showing “deference” and tolerating false doctrine?
  Both movements are suffering from their common heritage of pietistic
  pragmatism. Pietism tends to put religious feeling (heart) ahead of doctrinal truth (head).
  Pragmatism tends to evaluate everything by the standard of success—if it works it must
  be right. Pietism and pragmatism cannot effectively guide God’s people. The short-term
  benefits of religious sentimentality and carnal success are always followed by long-term
  damage to the health of God’s people.
  To their shame and detriment, both pietism and pragmatism are uninterested in
  the kind of ministry Paul told Titus to establish on the island of Crete. If biblical
  Christianity is to flourish again in America, it will only happen if God’s people return to
  faith in God’s solutions for our problems—godly and gifted men with deep convictions
  about God’s truth who will proclaim it accurately and authoritatively! Our desire at
  DBTS is to train men for that kind of ministry. May God help us to hold fast to the
  standard set forth in these verses, and may He cause those who are likeminded to
  flourish!

 38. Kwa kifupi vyote ni muhimu…….ni mtu kuisikia sauti ya Bwana amemwitia lipi la kufanya katika Ufalme wake…..! …..Lakini jiulize kama kuna watu wasingelikuwa wamekwenda shule hata hili Neno la Mungu tunalolisoma lingetufikia Leo? Kuna watu waliliondoa Lugha ya Kigiriki (Mfano New Tastement) wakalipeleka kwa Lugha mbali mbali mpaka likatufikia sisi……Je hakuna
  umuhimu wa shule hapo….? Utafanya tafsiri ya Biblia kutoka Lugha moja kwenda nyingine bila utaalamu wa Lugha…?

  Mungu ana watu wa kila aina katika Kuineza kazi yake…….Yesu aliita wanafunzi wake kutoka katika kila kundi la watu…..Tunaona watu wasiosoma….kama Petro….na tunaona watu wenye elimu kama Mathew (Mtoza Ushuru katika katika Dola ya Rumi hakuwa mtu asiye na elimu)

  ……Paulo aliyekuja baadaye katika utumishi alikuwa anajua elimu ya dini ya Kiyahudi na alikuwa chini ya Rabbi Gamalieli mwalimu mwenye sifa katika Maandiko ya Agano la Kale……alikuwa mwelewe wa Greek Logic….aliweza kusoma kuelewa Maandiko yao na kuwa na mjadala na wanazuoni wa Kiyunani katika Aurepago (Epicurean and Stoic philosophers ) na Pia alikuwa mwelewa wa Sheria za Warumi……Hebu angalia Mahubiri ya Paulo katika Matendo ya Mitume……kwa Wayahudi alitumia Maandiko ya Agano la Kale……lakini kwa Wagiriki (wayunani) alianzia kwenye elimu yao ( Acts 17:28). Na Labda kwa Elimu aliyokuwa nayo Paulo ndio maana Roho Mtakatifu aliruhusu Maandiko yake kuwa sehemu kubwa ya Agano jipya

  Je Maneno ya Mungu tunayosimama juu yake leo yameandikwa na akina nani…….? Mungu ametumia (alivuvia) watu wa hali zote…..wenye elimu na wasio na elimu…..Na ndio inabakia kwenye wito wa utumishi wake hadi leo…..

  Hivyo kusoma ili kumtumikia Mungu ni jambo jema kabisa…….kama Bwana amekupa kibali hicho yaani cha kwenda kusoma, Je si vyema kujua Maandiko haya tunayosimama juu yake yametufikiaje….? Maandiko haya yaliandikwa (yametofautiana kwa kama miaka 1,600) Je si vyema kujua ni akina nani waliokusanya vitabu hivi 66 na kuviweka pamoja…? Ni Vigezo gani vilitumika kuyakubali baadhi ya Maandiko na kukataa Maandiko Mengine kuwa hayana Uvuvio….? Je kama Lugha ya Agano Jipya ilikuwa ni Kigiriki si vyema angalau kujifunza “abc” ya Lugha hiyo ili uweze kusoma Agano jipya kwa Lugha ya awali kusaidia kuepuka mapungufu yanayojitokeza katika kulitafsri hilo Neno kwa Lugha (tafsiri) mbali mbali tunazozisoma leo…?

  Baada ya Kitabu cha Matendo ya Mitume ni nini kimefanyika kwa Kanisa kanisa la Mungu katika karne nyingi hadi kufika hapa lilipo leo…? Wapi Kanisa lilikwama…..wapi liliinuka….? Je haya tunayoyaona leo katika Kanisa la Yesu hayajawahi kutokea huko nyuma…..? Nini tunaweza kujifunza kwa Kanisa la Mungu huko nyuma….?

  Hivyo wapendwa kuna kila la Maana la kujifunza kama Bwana amekupa kibali cha kuwa Chini ya akina “Gamalieli” kama Mungu alivyofanya kwa Paulo, Lakini pia Bwana anaita pia watu kama akina Petro….wasio na elimu…..kwa makusudi yale yale….Kuujenga Mwili wa Kristo….kwa msaada wa kila kiungo kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo……

  Kila anayeuitikia wito wa Mungu ni Lazima kujia Bwana amemwitia nini…..Huduma yake Bwana aliyomwita imelengwa kwa nani….? Je inahitaji kukaa na kujifunza zaidi….?

  Mbarikiwe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s