Bwana katoa bali shetani katwaa!

Wadau embu tutafakari huu usemi mwingine tunaopenda kuutumia ambao tumeutoa katika maandiko lakini sijui kama tumeutafsiri ipasavyo na tunautumia kiusahihi. Akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. (AYU. 1:21 SUV).

Maneno haya ya Bwana ametoa, Bwana Ametwaa, libarikiwe Jina la Bwana aliyasema Ayubu baada ya kupoteza kila kitu. Swali langu kubwa kwanza je, Ayubu aliposema hivi alikuwa sahihi maana ukiisoma hiyo sura nzima utakuta ni shetani ndo alienda kusabababisha janga lote alilokutana nalo Ayubu la kupoteza watoto na mali. Sasa Ayubu kwa kutojua nini hasa kimetokea katika ulimwengu wa roho akasema Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa libarikiwe Jina la Bwana. Napata shida kukubaliana na hili maana naona kama tafsiri ya haya maneno ya Ayubu inakinzana na maneno ya Bwana sehemu zingine katika maandiko.

Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. (RUM. 11:29 SUV).

Sasa kama karama au zawadi za Mungu na wito wake hauna majuto, kwa Ayubu alijutaje na kumnyanganya?

Ni kweli Bwana alitoa na Bwana akatwaa au ilikuwa tafsiri ya Ayubu ya hali aliyokuwa amepitia. Nikiangalia kwa makini mkasa mzima naona ni Bwana katoa bali shetani katwaa.

Andiko lingine ninaloona linakinzana na hilo ni hili lifuatalo:

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. (YAK. 1:17 SUV).

Hapa ninaona Mungu akitoa hageuki wala habadiliki. Ilikuwaje sasa kwa Ayubu akageuka kumyanganya na akambadilikia ghafla?

Je inawezekana ndo sababu kwanini baadaye Ayubu alikemewa na Mungu na kurekebishwa mtazamo? Yeye mwenyewe alikiri kuwa Mungu alikuwa anamsikiaga tu lakini baada ya jaribu akawa amemwona Mungu na baada ya kuelewa vizuri akarejeshewa mara mbili ya alivyonyanganywa na adui.

Sasa kama Ayubu alikuwa na shida ya tafsiri ya hali aliyokuwa anaipitia hata akasema Bwana Ametoa, Bwana ametwaa wakati kiukweliii ni Bwana Alitoa ila shetani alitwa sisi tunatumiaje hayo maneno mtu akifa kuwa Bwana alimtoa na Bwana amemtwaa!

Fikiria hapo mtoto mdogo anayepotelewa na baba yake au mama yake au wote wawili kwa ajali ya gari, kwa kuuawa na majambazi, kwa ugonjwa mbaya, kulogwa nk, kwenye msiba anasikia Mchungaji anasema Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, je ndani ya huyu mtoto haijengeki picha kuwa Mungu ni mkatili sana kumnyanganya wazazi wake wakati alikuwa anawahitaji sana. Mbona Mungu twamtwika hata vitu asivyohusika jamaani?

Embu tusaidiane wadau!

Pastor Carlos Kirimbai

Advertisements

10 thoughts on “Bwana katoa bali shetani katwaa!

 1. UKWELI NI HUU WAPENDWA.

  “Bwana ametoa na Bwana ametwaa” ina maana hivi:

  1. Shetani hana uwezo wa kutwaa viumbe walioumbwa na Mungu.

  2. Mungu ndiye ametoa ruhusa mtu afariki. Bila Mungu kutoa kibali mtu hawezi kufa. Kwa hiyo Mtoa kibali ndiye anayerushusu jambo litokee. Kwa mfano Rais anapotoa kibali wafungwa wachiwe huuru, tunasema, “RAIS AMEFUNGUA WAFUNGWA” Lakini kusema ukweli yeye hakwenda kufungua milango ya jela. Yeye ametoa kibali.

  3. Tangu anguko la Adam Mungu alitoa kibali kwa wanadamu kupatwa na mauti. Kwa hiyo mtu anapokua, aliyetwaa siyo Shetani bali ni Mungu Muumbaji mwenyewe.

  4. Ayubu hakukosea hata kidogo aliposema, “BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE”. Alimaanisha kwamba Mungu pekee ndiye anayetoa mema na ndiye pekee mwenye uwezo wa kuruhusu chochote kitokee kwa mtakatifu wake.

  5. Wakati wa Mazishi kusema kwamba Mungu ametwaa ni sahihi kabisa. Wala siyo kuwafundisha watoto kwamba Mungu ni katili kwa sababu ya kuruhusu kifo kiwapate wazazi wao waliokuwa wanawahitaji bado, bali ni kuwafundisha kwamba bila wamwelewe Mungu kuwa ndiye mwenye Mamlaka yote juu ya uhai wa mwanadam.

  6. Sababu yoyote inayosababisha mwanadam kufariki, iwe risasi, ajali, moto, kuumwa na simba, nyoka, kuzama baharini, yote katika yote ni KIFO. Mungu anachojua ni kwamba amekufa. Unajua KUFA mbele za Mungu ni kufa tu haijalishi mtu amekufa kwa njia gani sisi wanadam ndio tunaodhania kwamba kifo fulani ni cha ukatili lakini mbele za Mungu vyote ni vifo tu. Kwa namna yoyote ile inayotumika kuleta kifo kwa mtu lazima iwe imepewa kibali na Mungu vinginevyo Mungu akisema NDIYO hakuna awezaye kusema HAPANA, au Mungu akisema HAPANA nani atasema NDIYO? Hakunaga.

  Ni matumaini yangu kwamba wapedwa wamefunguka katika mada hii. Barikiwa sana.

 2. Naungana kwa kiasi kikubwa na Mpendwa hapo juu Ndugu Marwa.
  Nisomapo habari hii ya Ayubu; kwanza kabisa nakutana na sifa za Ayubu: mtu mkamilifi na mwenye uelekevu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu. Ayu. 1:1
  Halafu unakuja mkutano wa wana wa Mungu, na Shetani naye akaenda kati yao (hapa hakuwa amealikwa)-ujue ya kwamba kuna watu wengine huenda kwenye hafla au mikutano bila kalikwa. Pia hapa kukawa na mazungumzo kati ya Mungu na Shetani kuhusu Ayubu. (jua ya kwamba Shetani ni mshitaki wetu wamwaminio YESU) Kwenye mkutano huu Ayubu hakuwepo na tena hata baadaye hakupewa miniti za mazungumzo hayo.
  Basi hapa nataka kusema tu ya kwamba maneno ya Ayubu kuhusu “kutoa na kutwaa” yanatokana na kumwamini Mungu wake na yalitoka rohoni mwake; tena akiamini ya kwamba yote yamepita machoni kwa Muumba wake. Mwisho habari yake inajulikana ya kwamba alibarikiwa maradufu. Yatupasa hata watu wa Mungu kuona ya kwamba Shetani ni mshitaki wetu. Tena tujue ya kwamba Mungu hatutii majaribuni bali hutupa mtihani-(God doe’s not put us into temptations but He tests us). Shetani ndiye atuingizaye majaribuni ili tuanguke.

 3. Changamoto Aliyoitoa C.Kirimbai ni nzuri, hata hivyo majibu yamelenga ukweli.

  Wacha nami niongeze kikubaliana na waliosema MUNGU ndiye Ayubu alikuwa anamuona siyo ibilisi.

  Kwahiyo hakuna shetani hapo.

 4. Bwana Yesu apewe sifa. Haya yote yaliyompata Ayubu yalikuwa ni kwa kibali cha Mungu. Kama Mungu asingeruhusu yasingempata Ayubu. Ayubu 2:6-7, ”Bwana akamwambia shetani tazama , yeye yumo mkononi mwako lakini tunza tu uhai wake. Basi shetani akatoka mbele za uso wa Bwana akampiga Ayubu…”

  Kama shetani asingeruhusiwa na Bwana, Ayubu asingepatwa na mapigo yaliyompata. Kwa hiyo yoote yaliyofanyika yalikuwa ni kwa kibali cha Bwana. Hivyo naona kabisa kwa mujibu wa maandiko hayo Ayubu alikuwa sahihi kusema Bwana ametwaa kwani bila Bwana kuruhusu mabaya yasingempata ikiwa ni pamoja na kupoteza wana.
  Huu ni mchango wangu, Mungu awabariki.

 5. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,katika hili nasubiri kutoka kwa wapendwa wenzangu, ninachojua Mungu ndiye aliruhusu yote yatokee kwa mapenzi yake.Mtumishi John Paul nasubiri mchango wako katika hili.

 6. Hujapewa na nuru ya Kristo,hujahubiri/ kufundisha kitu kama hiki!!! Hata hivyo sio wengi wawezao sio tu kulipokea Neno hilo! Bali zaidi sana Kulielewa,hiyo ni kutokana na ukweli kuwa zamani hizi ni za uovu(Giza)

 7. Ayubu 42;2,Najua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, na ya kuwa kusudi lako haliwezi kuzuiwa……….. Hakuna kusudi la Mungu linalo zuilika, kama Mungu amekuahidia uzima na baraka hakuna atakaezuia na hakuna kitu kinachoweza kutokea katika maisha ya mtu kinyume na Mungu anavyo taka au kuruhusu,, kiukweli Bwana ndiye aliyempa Ayubu na aliruhusu vitwaliwe haijalishi kwa njia ipi kwani huwezi kumfundisha Mungu kuwa ni lazima avitwae kwa mikono yake, yeye ni Mungu na hutumia njia zake kutimiza makusudi yake; hata kama itaonekana kuwa Mungu ni mkatili yeye si mkatili, anapokuondolea watu au kitu unachokipenda sana haimbadili kuwa mkatili hata ukihisi hivyo kwani hata akikuondolea kila kitu bado hajajiondoa kwako hivyo kwa macho ya nyama utahuzunika ila yeye anakujali na kukupenda tu,, msemo huu wa Bwana ametoa naye ametwaa ni sahihi ila huwa unatumika vibaya pale ambapo kuna uzembe umetumika mfano, kanisa lisipo simama kwenye nafasii yake kuna mambo ambayo ni mpango wa shetani yatatokea kwani mamlaka tuliyopewa ya kumpinga mwovu hatujaifanyia kazi, kwa hiyo utakuta watu wanasema Bwana ametwaa huku ni shetani ndo amefanya ukizingatia Mungu hashuki duniani kufanyia kazi mamlaka ambayo ameshatupa sisi wanadamu, kazi yetu ni kumkemea adui asihusike kukwepesha mpango wa Mungu kwetu. Anasema ameweka mbele yetu uzima na mauti, tuchague uzima; kumbe inawezekana sisi wenyewe tukachagua mauti afu tuukifa tunasema Bwana ametwaa, ndiyo ametwaa pumzi hii si yake lakini tumeamua kuvunwa kabla ya wakati kwa maana ya kuwa tumeruhusu kusudi la Mungu kutotimia na kutoa nafasi kwa kusudi lisilo mahali pake kwa wakati huo

 8. Hakuna shetani anaweza fanya bila Mungu kuruhusu….ndio maana hayo maneno yako hivyo. Kwa kifupi ulinzi wa Mungu na kufanya mapenzi makamilifu ya Mungu kunakuja kutokana na kumjua Mungu na kufanya mapenzi yake. Mtu anayemtumaini na kuishi na Mungu vema Mungu anamlinda. Kwa Ayubu tunaona kabisa ulinzi wa Mungu ulikuwa juu yake na familia yake na shetani aliweza kumdhuru baada ya kupata ruhusa kwa Mungu…all in all God is sovereign….akiamua anaweza muepusha mtu awaye yote na kifo ata kama mtu huyo njia zake hazimpendezi. Kwa kusema hivi simaanishi hao watu wanakuwa hawauwawa na shetani.
  Huo ndio uelewa wangu,naweza kuwa nimekosea…. natumai wenye kujua zaidi watatuambia.

 9. Andiko hilo natusilinukuu vibaya ninavyoelewa mimi ayubu ktk mambo yote hakumwona shetani alimwona mungu ndio maana hakubadilisha usemi alijua ibada sio shetani ayubu 1:6,2:1 wengi wetu tunampanga mungu km rafiki yetu kwamba amlaze mahala pema peponi niupotofu

 10. Kwa makasheshe ya mapito na majaribu alopata mpendwa Ayubu yeye kama binadamu kwa kua wote tu hata kama walitembea na Mungu kiasi gani, walikua wanadamu tu ka mi na wee..( wanachoka,kwazika, kufyumu wakiudhiwa, kula, kihisi njaa, kukasirika, kukata tamaa, kufurahia maisha, kupigika kipesa,kupenda kufanikiwa, kuoga, kwenda toilet, kutandikwa na malaria kama ilikuwepo enzi zile n.k….Yak 5:17-18,so kwa Ayubu kupoteza network na kokoment alivyokoment, it was natural kabisa, tena to be honest, mi ningepoteza zaidi, ikumbukwe pia in those days, wapendwa wa zamani walikua hawakufunuliwa mambo ya Mungu kama sisi kipindi cha neema kwa kua na Holy Spirit anatupa madesa yooote, So kama mtu madisastors yamemfururizia his comments…Bwana ametoa na Bwana ametwaa was to his best of his knowledge.

  It is true, very true indeed he was wrong coz Bwana hawagi cruel kiasi hicho na hawezi kuwa kigeugeu…God is not a man that he should lie…He should chakachua issues and confuse his beloved na kua awe anaenjoy sana kuwatesa..NEVER! Today we can say kabisaa, It was BWANA ALITOA AND DEVO AKATWAA, nevertheless, naongeza ufunuo kua… BWANA ANAWEZA AKATOA NA AKATWAA BUT KUWASILIANA NA MTU WAKE-SI KIJAMBAZI JAMBAZI KAMA DEVO AMBAYE HUJA KUSLAUGHTER, KUSTEAL NA KUKILL, ALSO LAST UFUNUO NI TRUE VILEVILE HATA DEVO NAE AWEZA KUTOA NA KUTWAA PIA, TENA FAST KWA WALE WAFUASI WAKE.

  Bless u all, ndo kamchango kangu ako wapendwa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s