Waimbaji wa nyimbo za Injili, kuimba kumbi za starehe!

Bwana Yesu asifiwe, hivi karibuni kumeibuka mjadala wa kanisa, jijini Kampala. Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Judith Babirye ambaye hapo awali hakuwa akienda kwenye kumbi za starehe kuimba hivi sasa anakubali mialiko hata kuimba kwenye kumbi zinazopiga nyimbo ambazo sio za kikristo.

Wachungaji wameonekana kukerwa na tabia hii mpaka kuibua mjadala huo kwenye vyombo vya habari za Kikristo. Kazi ya uimbaji ni kuhubiri pia, je Kwanini wanaona si sawa kwa yeye kuhubiri kwenye kumbi hizo? hii haina tofauti na waimbaji wanaoalikwa kuimba kwenye harusi zisizo za kikristo na pia Ma MC waliookoka.

Advertisements

22 thoughts on “Waimbaji wa nyimbo za Injili, kuimba kumbi za starehe!

 1. Kuna mchungaji mmoja akaamua kwenda kuhubiri, AKAFIKA PALE aKAVUTA KITI AKAKAA,MUHUDUMU AKAJA, AKAAGIZA SODA ,AKAMWAMBIA NAYE ACHUKUE SODA,

  AKAANZA KUMHUBIRIA YULE DADA KUMBE MWANAMKE ALIKUWA ANAMTAMANI ,AKAANZA KUMSHIKA SHIKA MCH AKESEMA ” WEWE MIMI MCHUNGAJI ACHA BWANA”

  Mchungaji akazidiwa na yule dada akaishia kuondoka naye,

  sasa hapa huyu mtumishi alikuwa hajalewa lakini kazidiwa nguvu na shetani, itakuwaje huko kwenye ma night club ambako moto unawaka wa jehenum??

  Mchangiaji mwingine amesema hapo juu,ni sawawa kuhubiri masokoni au barabarani, kwenye club inajulikana kabisa kule ni anasa na watu wasio na hofu ya mungu,lakini sokoni au barabarani ni mchanganyiko wa watu tofauti tofaut,hapo kusudi la mungu litafanyika,

  Kama dada Judith ana uwezo wa kumshinda shetani huko club, ni vizru sana,

  tunahitaji roho mtakatifu atuongoze ili tuweze kuzishinda tamaa za mwili, Gal 5:16. basi enendeni kwa roho hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili,

  mwili huu unapenda raha, pesa, na mambo meeengi mabaya ya kukurudisha nyuma, but msaidizi wetu huyu roho anatuhuisha na kutuongoza,

  Barikiwa .

 2. yote ni kumuhubiri mungu popote si dhambi.Gilbert mbulinyingi wa mbeya Tanzania

 3. mimi binafsi naona hakuna tatizo kama kweli anaenda kumwimbia Mungu na kutangaza neno la Mungu hakuna shida maana neno lake MUNGU hutangazwa popote pale na atazidi kubalikiwa kila kukicha.namuombea baraka kwa MUNGU.Nipo mpwapwa Dodoma

 4. Amen mtumishi,mimi pia ningependa kujua ulipo ila nafikiri haitakuwa vyema kurusha my persona email adress humu,ila ninamu-authorize huyu bloger akupe then tutawasiliana.
  Ubarikiwe

 5. Mpendwa Lulu. Ninamshukuru Mungu kwa ajili yako na pia kwa yale mazuri uliyoyataja hapo juu. Ninakubali kabisa ya kwamba kumhukumu mtu mwingine si kazi ya mtu aliyeokoka ila kama nilivyosema hapo juu “tufundishane, tuonyane, tusaidiane na pia kubebana kwa upendo- Upendo ukiwepo kati yetu basi haitakuwa rahisi kumhukumu mwingine. Ila pia ni lazima tujue ya kwamba hukumu iliyo kamilifu ni yake Mungu tu. Maana Maandiko yanasema “usihukumu ukaja ukahukumiwa”
  Tena kama nilivyosema hapo awali kwamba; iwapo Mwimbaji atakwenda kutoa huduma yake katika sehemu ya starehe au harusi ya watu wasiomjua Yesu kwa maadili yake na shabaha ya kupeleke ujumbe wa wokovu, mimi siwezi kusema na kumhukumu ya kwamba ametenda dhambi. Kama nitakuwa nimealikwa na mimi kwenye sherahe hiyo na Roho wa Mungu akinionyesha mapungufu ya mtu huyo basi nitamwomba Mungu anipe neno kwa ajili yake. Tena nitapenda nikutane naye ili tuombe na kuzungumza pamoja. Nina hakika ya kwamba Roho wa Mungu atazungumza nasi bila ya kuonyesheana kidole.
  Kutoa huduma kwenye sehemu hizo si dhambi.
  Dada Lulu, mimi pia ni Mtanzania kabisa na ninaishi huku Ughaibuni. Usemi wa watu kusema ya kwamba watu huku hawamjui Mungu sijui unaanzia wapi. Swali linakuja tu waliokuambia hivyo walikuwa na maana gani? Je walikuwa na maana ya kwamba huku hakuna makanisa? Au hakuna Walokole? Umemtaja Bhonke wa Christ for all Nations!!
  Kitu ambacho nakuomba ukizingatie ni hiki “Wokovu hutokana na neema ya Mungu tu kwa njia ya Yesu Kristo.” Kama umekwisha okolewa kwa neema hiyo, basi shika sana ulichonacho, asije mwingine akakupokonya.
  Ningelifurahi sana kujua ni wapi unakoishi pengine tupo nchi moja!!!!!!
  Baraka ziwe kwako.

 6. Mimi nakubaliana nawe kabisa mtumishi kwa yote uliyoyasema,kitu kinachokuwaga kinanishangaza hasa huko nyumbani kwanini sisi watu tuliomjua Yesu wengi wetu tunapenda kunyooshea wengine vidole?sikatai kuonyana na kufundishana pia kumwonyesha mtu(mpendwa)njia iliyo njema,lkn not in a way that unakuwa unamjudge.

  Dhanbi lazima ikemewe,lkn je unaweza kumqualify mtu aliyeimba nyimbo ya injili kwenye nightclub, harusi ya watu wasiomjua Yesu or sherehe yoyote ile isiyo ya kikristo kuwa ametenda dhambi?
  To me hao ndio hasa wanaotakiwa hasa kusikia neno ili wamjue Yesu wetu na kumpokea,hata ukimpata mmoja ktk elfu mmoja au usipate kabisa lkn utaacha umepanda mbegu mengine tumwachie Mungu yeye afanye kazi ktk mioyo ya watu kwa namna yake.
  Mimi nimezaliwa kukulia Tz,wakati naondoka watu walikuwa wananiambia unakoelekea watu hawamjui Mungu imani yako itadorola na then nilikuwa mromani wa kawaida tu na huwezi kuamini nilikuwa naenda kwenye mikutano ya injili mingi na makanisa ya kiroho na sikuwahi kuokoka nimeokoka hukuhuku ughaibuni ambako ndio wengine walioniwahi walisema nitadorola kiroho wakati then nilikuwa just a church goer,kwahiyo naweza kusema nilipokuwa naenda kwenye mikutano ya bhonke,or big november crusade japo sikuokoka lkn kuna mbegu ilipandwa ndani yangu ikamea na kuchanua,sikuwahi kufikiria kuokoka i dont know why may be God knows,ingawa nilikuwa napenda kusikiliza neno la Mungu.

  Ndio mana nasema tusipende kujudge wana Mungu

 7. Mpendwa Lulu: Wewe umenibariki kwa kukubaliana nami katika hili. Kama nilivyotangula kusema “mgonjwa ndiye ahitajiye daktari” na pia ni vema kujua ya kwamba daktari anamihaji mgonjwa pia ili aweze kutibu. Tena tujue ya kwamba hata daktari naye anaweza kuugua na kuhitaji daktari mwingine ili aweze kumtibu. Kwa ilani ya kazi ya Udaktari; daktari haruhusiwi kujiandikia dawa mwenyewe. Basi hata katika mambo ya kiroho mtumishi wa Mungu anahitaji pia kuhudumiwa. Wengi wetu hujaribu sana kuona ya kwamba sisi kazi yetu ni kuwasaidia wengine (yaani kutoa tu, kutoa tu pasi ya kupokea) na mwisho wake huwa ni mgumu. Mimi ninahitaji kila mara kukaa na kumsikiliza mwingine ili anilishe nami nishibe. Kwa ajili hiyo basi kama wote tayari wanamjua Yesu na wamempokea wote tunahitaji si kuhubiriwa tu bali kufundishwa, kulishwa, kukumbushwa, kuimarishwa ili tuweze kuukulia wokovu wetu. Hapa napenda kusema ya kwamba kumjua na kumpokea Yesu ni safari ndefu hadi mtu afikiapo mwisho wa maisha yake ya hapa duniani. Mtume Paulo anasema: “Ama kweli ndugu zangu, sidhani kuwa nimekwisha pata tuzo hilo, lakini jambo moja nafanya: nayasahau yale yaliyopita na kufanya bidii, kuyazingatia yaliyo mbele. Basi nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu” (Wafilipi 3:13-14)
  Ninapoisoma mistari hii ya Mtume Paulo ninajifunza ya kwamba: hata kama mtu anamjua na tayari amempokea Yesu yampasa mtu huyo kujua ya kwamba safari yake haijafikia mwisho wake. Na hata ya kwangu mimi haijafikia mwisho.
  Kwa wale tunamjua na tulikwisha mpoke YESU “tufundishane na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na TENZI ZA ROHONI: huku tukimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwetu” (soma Wakolosai 3:16)

 8. Nakubaliana na wewe kabisa mtumishi wa Mungu,wagonjwa ndio wanahitaji Daktari,na Yesu alikuja kwa jili ya wenye dhambi,Injili itatangazwa vipi km wanaohubiriwa wote tayari wanamjua Yesu na wamempokea?

 9. Bwana Yesu asifiwe, hivi karibuni kumeibuka mjadala wa kanisa, jijini Kampala. Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Judith Babirye ambaye hapo awali hakuwa akienda kwenye kumbi za starehe kuimba hivi sasa anakubali mialiko hata kuimba kwenye kumbi zinazopiga nyimbo ambazo sio za kikristo. Wachungaji wameonekana kukerwa na tabia hii mpaka kuibua mjadala huo kwenye vyombo vya habari za Kikristo. Kazi ya uimbaji ni kuhubiri pia, je Kwanini wanaona si sawa kwa yeye kuhubiri kwenye kumbi hizo? hii haina tofauti na waimbaji wanaoalikwa kuimba kwenye harusi zisizo za kikristo na pia Ma MC waliookoka.

  Kama nilivyosoma hapo kuhusu mada hii: Dada huyu amealikwa kwenda kuimba kwenye kumbi za starehe. Ukumbi wa starehe ni upi? Starehe ni nini? Starehe ina maana mbili kimsingi: Moja ni ile hali ya kuishi bila shida au usumbufu na pia kuwa na raha; pili kufanya au kuwa na mambo ya anasa. Watu waliokombolewa na kuokoka wanaishi kwa starehe ( hapa nina maana ya kujiepusha na anasa za dunia hii) ndani ya Masihi waksterehe katika neema yake. Japo wana shida mbali mbali za hapa na pale wana matumaini katika maisha yao. Sasa nirudi kwenye huduma ya Waimbaji na tena niseme si waimbaji tu bali wahudumu wa kazi ya Mungu (Wakristo na hasa wale waliokoka); ni wajibu wetu kuwafuata na kuwatafuta waliopotea maana roho moja ya mkosaji ikikombolewa mahali popote malaika wa mbinguni hushangilia na kumpa utukufu Mungu. Walo wazima hawahitaji daktari bali wagonjwa. Kama hawaji hospitali watafutwe huko waliko.
  Nina wimbo wangu naukumbuka sana ukisema:
  Bwana Mungu alisema, Bwana Mungu alisema,
  Nimtume nani aende kuokoa ulimwengu:
  Kwa sababu aliyaona matendo yao wanadamu
  alisikitika kuona ulimwengu unakwisha.
  Bwana Yesu akajibu, unitume mimi niende kuokoa ulimwengu
  Kwa sababu aliyaona matendo yao wanadamu
  alisikitika kuona ulimwengu unakwisha.
  Yesu auliza leo nimtume nani aende kwao hao wakimbiliao anasa za dunia hii?
  Inatubidi kuwafuata; si kwa ajili ya kufanya biashara bali kwa ajili ya kuwapelekea UJUMBE ULIO HAI. Yesu alishuka duniani ili aukombee ulimwengu.

 10. Binafsi naona zipo njia nyingi sana za kuwafikia watu hao zaidi ya kuwafuata huko kwenye Night Clubs,tatizo ni kwamba hao watu tunaowalenga wapo hapo kwa dhumuni gani,wengi wao ni walevi na wazinzi ambao wote hao wana style zao na miondoko yao wanayopenda iwe perfomed wanapokuwa ndani ya Clubs,Na mara nyingi ustaarabu maeneo hayo huwa ni mdogo sana they can do anything to you na kwao ikawa ni kawaida,na always huwa wanapenda siku zote wafanyiwe vile wanavyotaka wao kwa kuwa hawaingii bure.Je utaweza?.Kwa hivyo unaposema unawafuata hukohuko,USIPORUDI JE? Hao watu baadhi yao wanatoka katika maeneo tunayoishi.Have you ever talk to them about salvation?,inawezekana hata hatujawahi sasa why tosiwahubirie kwanza huku huku mtaani.Nowadays anyone can sing gospel music kwasababu ni deal,sio kitu cha ajabu tena ndo maana inapigwa mpaka Bar na sasa watu wengi wana access ya kuusikiiliza hata majumbani kama muziki mwingine wowote na wanaendelea na maisha yao kama kawaida.Tusidanganyane hapa inawezekana mioyo yetu bado inatamani yale mambo ya Misri ambayo tulikwisha yaacha.Kumbuka ni rahisi mno kilicho najisi kukinajisi kilicho kitakatifu kuliko kilicho kitakatifu kukibadili kilicho najisi.Hizo nyimbo za injili wanaweza kuzisikia kwa njia njingi mfano Radio ,Tv nk kama haitoshi basi kuna maeneo maalum ama nafasi nyingi za kuweza kutoa hiyo huduma ya uimbaji mf, Makanisani,semina na mikutano na kama hawatazisikia huko na kubadirika basi Night Clubs ni zaidi.

  Thats my comment!

  MBARIKIWE!!!

 11. Jamani embu tuache kuhukumu,tumuache Bwana hiyo ndiyo kazi yake.

  Tatizo ni kwamba binadamu tupo wepesi sana kuhukumu wengine,mtu km anaimba sehemu za starehe ni sehemu ya huduma km huduma zingine,wewe km umeshaokoka huitaji hiyo injili hata km hao watu hawamsikilizi,hatujui km wanapanda mbegu na ipo siku itamea na kuzaa matunda.

  Yesu alikuwa kwajili ya wenye dhambi na si watakatifu.
  Sijawahi kusikia mtu anaimba injili kwenye night club km wengine walivyosema hapo juu lkn,hata km itatokea ni sawa kwasababu tumeamuliwa tukahubiri Injili ulimwenguni kote hakuna mipaka,iwe kazini,hospitalini,misibani,harusini,nightclubs and the list goes on and on.

  Mungu wetu ni wa ajabu hamtokei kila mtu kwastyle moja,tuelimike na tumwangalie Mungu wetu jinsi anavyotenda kazi juu yetu na si kuangalia macho ya binadamu ambae maranyingi anaangalia umekosea wapi.

  Muendelee kubarikiwa tunapoendelea kujifunza

 12. Kila jambo lifanyike kwa hekima na kiasi (mipaka)… kama ni kuhubiri jamani andaeni mikutano ya ijnili as many as possible mkaimbe huko, hapo ni mahali sahihi pa kupanda mbegu yako kwa njia ya uimbaji (neno la Mungu) Mimi nadhani kwenda night club kuimba ni kutumia vibaya mbegu zako maana ovious zitaanguka katika miiba na michongoma au hata barabarani…. Mtu kalewa chakari halafu unamuhubiria je ataamua maamuzi sahihi katika hali ile?

  Pili kuna nyimbo zinazolenga kumpa Mungu utukufu kama Usifiwe Jehova, I wanna Praise You Lord, Nakupa sifa Na shukrani, Uinuliwe….. zikiimbwa kwenye kumbi hizo zinaleta maana kweli? unamsifu Mungu kwa kipi Hapo?

  Tukija kwenye swala la proffesional na kwamba ndo kazi yao ya kuwaingizia kipato labda nishauri japo si busara sana basi watunge nyimbo za kijamii zaidi, kuelimisha jamii katika maswala mbali mbali kama elimu, afya, haki za binabamu n.k ili wakaziimbe huko wapate hizo pesa…. lakini Biblia inasemaje, anayetumika Madhabahuni hula madhabahuni na kama ndege wanalishwa je wewe si zaidi ya ndege? sasa ni vyema ukajua madhabahu sahihi ya kuitumikia kama ni club ama wapi….

  Siku za Mwisho hizi tuwe macho “DO NOT COMPROMIZE DA WORD OF GOD”

 13. Sikubaliani kabisa na huyo muimbaji labda uniambie ameacha imani yake.Hata hivyo ni nani ajuaye kama ameiacha! Naomba waimbaji wa muziki wa injili wabadilike wamekuwa na skendo nyingi na inaonekana sasa kama wanautumia muziki huo kama kufunika mienendo yao.Sehemu kama hiyo utamuubiria nani akusikie tena kwa nyimbo! mara nyingi watu maeneo hayo wapo kwa ajili ya kucheza tu na kujiburudisha na si kusikia na kutafakari kinachoimbwa na kufanyia kazi.Zaidi utasababisha na wazinzi wakutamani na wewe na walevi wakiwa wamelewa wakutuze na kukushikashika! TUACHE MIZAHA!

 14. nyimbo za injili kupigwa kumbi za starehe,kitaalam tunaita incompatibility, kumbi za starehe zinapigwa nyimbo za starehe na kumbi za injili nymbo za injili,, kama we ni muimbaj wa injili afu una mashabiki wanakuita kwenye kumbi za sherehe,nakupa pole labda unihakikishie kuwa injili ni starehe la sivyo wenye hekima watakuombea tu walau upate macho ya kuona! hamjiulizi kwa nini wahubiri wa injil hawaitwi huko??? moto usio na moshi utawaka!!

 15. Ndugu yangu uliyechangia hapo juu kuwa hata Yesu aliketi pamoja na wenye dhambi, ninachojua mimi Bwana Yesu hakuwahi kwenda bar wala club kama nitakuwa nimekosea mtanisahihisha.Mambo yanayofanywa night clubs yanatisha!Mimi nadhani hata kama ni kupeleka injili kuwepo mipaka kuhusu mahali.Utaweza kuhubiri injili kwa mlevi akakuelewa?au unahubiri injili huku watu wengine wanafanya mambo ya ajabu(siwezi kuyataja hapa).Hapa badala ya kuimba watu wasikie ujumbe ili wachukue hatua ya kumfuata Bwana Yesu unawaburudisha tu maana wengi wanachokifuata huko ni burudani. Hivyo mwisho wake hakuna matokeo yanayotarajiwa.Tunaimba nyimbo ili kumsifu Bwana sasa kwenye kumbi za starehe na clubs huko tunamsifu Bwana kweli? huyu anazini,huyu anavuta sigara au bangi,huyu anakunywa pombe kali hivi hawa watakuwa kwenye hali ya kupokea ujumbe na kutafakari kweli? mlevi anaweza kulia na kutoa machozi lakini kumbe dhamira/nia yake siyo kulia unayemtazama unaona kama analia kweli!

 16. Bw asifiwe
  Mimi naona Uimbaji ni huduma km huduma zingine,hivyo km watakuwa wanawaimbia waliookoka tu wataitangaza vipi injili?halafu ndugu zangu mnaosema wamwimbie Bwana na si pesa,kusema kweli hiyo haiwezi kuwa practical km hiyo ndio kazi ya mtu anayofanya.
  Mungu awepata watumishi wake huduma tofauti kuna watu wanataka kuwafikia watu hospitalini,nightclubs,mashuleni,harusini n.k na Mungu anamgusa kila mtu kwa namna anavyojua yeye na tusimlimit wala hatuna haki ya kuhumu.
  Mbarikiwe

 17. Ni kweili uimbaji ni profession.Lakini kama ni profession na wanahitaji kipato,tuseme kuwa wanaenda kujipatia kipato na si kumuimbia Bwana. Swala linalo wagusa wengi ni ile hali ya mtu kwenda sehemu kama kumbi za starehe na kuperfom huku akiimba nyimbo za injili.

  Lakini kuna vitu kadhaa vya kujiuliza lakini kabla ya yote tujue hili,ULIMWENGU WA KIROHO NA ULIMWENGU WA KIDUNIA vimepingana kama ilivyo anga na ardhi kamwe havita changamana.Kwa hilo dogo utajiuliza maswali yafuatayo:

  Ikiwa kwenye kumbi za starehe watu wamekusanyika kwa ajili ya furaha ya kidunia,je watapenda muimbaji aimbe nyimbo zenye ujumbe upi,mavazi na stepu zipi?Je, naye atakubali kuwa kinyume na wao na aikose ajira kwa siku nyingine au atakubaliana nao ili kukuza uteja nao?

  Mtazamo wa kusema ni ajira kama kweli tunataka kuwafunza na kuwatunza wana injili wetu naona ni potofu.Aidha tuone ya kuwa kuna mengi yanayojiri hapa duniani awali tunaona ni mageni ya kukemewa lakini baada ya muda twazoea na kuona ni kawaida.

  Ombi:TUSIENDE KWA MAZOEA YA DUNIA HII TUTAANGUKA KIROHO!

 18. as long as watu wanapata injili na waimbaji wanakwenda kwa mzigo na sincerity mioyoni mwao wakiangaishwa na mimba ya Yesu ya kutaka roho ziingizwe mbinguni na as long as hawachichakachui wala kuchakachachuliwa, no p kabisa, kwa kila njia, kila namna na kwa gharama yeyote ile tutasaka roho wa wanadmau mpaka waokoke, huko huko club kuna waimbaji kwaya wakutisha, mapastor, wainjilisti, mawaziri, madaktari, maprofs, wakulima, wafanyabiashara, waume, wake, wanafamjilia, mafundi uashi,seremala nk na watu wengine wa maana ikiwa pepo pombe zitwatimka na wakaokoka, utashanga what potentialities God had invested in them for the betterment of the society and heaven but unfortunately devo akawataimu tu.

 19. Jamani, tuwe wakweli tu: Uimbaji wa waimbaji wengi wa nyimbo ‘za injili’ hivi leo wanafanya hivyo kama kazi (profession), hivyo wanahitaji kupata mapato kwa kazi zao. Kwa mantiki hiyo, sioni tabu wakienda kupiga miziki yao katika hizo kumbi za starehe, maana tangu hapo tayari wanashindana kwenye tuzo za muziki sambamba na wanamuziki ‘wa kidunia’.

  Ila kwa wale waimbaji ambao wanaimba kama sehemu ya ibada (na hawa ni wachache sana na hawatafuti kupata faida na utajiri kutokana na uimbaji wao), hao hawawezi hata kufikiri kwenda kwenye kumbi hizo maana wao wanamwimbia Mungu na si kufurahisha (kutumbuiza/kuburudisha) wanadamu.

 20. Yesu mwenyewe aliketi na wenye dhambi jamani,huko huko watu waweza kubadilika ili mradi haimbi za dunia anaimba za injili ni moja ya injilisti kama ule unaofanyika na watumishi masokoni,mitaani,stend kwenye madaladala ili mradi anapeleka injili jamani watasikiaje wasipohubiriwa?songa mbele dada Mungu akuzidishie mafuta.

 21. Kwa kweli inashangaza, lakini sasa sijui tunaelekea wapi? Tusipokuwa makini, Ukristo utakuwa kama utamaduni hali ni Imani Iliyo hai. Kinachoshangaza ni juhudi kubwa ya watoto wa Mungu kuiga dunia badala huku kanisani ndio kuwe kwa kuigwa! Kingine ni kupenda pesa!Hata Paulo alisema,shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha! Waimbaji, acheni kupenda pesa!Kumbukeni waimbaji wa zamani kama wa Shangilieni, Ulyankulu, Nkinga, Mapigano n.k, tujifunze kwao!!!Lakini sisi pia, tukumbuke kuwaombea hawa watumishi maana huduma yao ni muhimu sana.

 22. Wana wa Israel waligoma kuziimba nyimbo za BWANA Mungu katika nchi ya ugenini! Wakatundika vinubi vyao juu ya miti, kando ya mito ya Babeli. Tatizo ni kuwa nyimbo za sasa nyingi ni kwa ajili ya WATU na si kwa ajili ya BWANA. Ndiyo maana hata ambapo BWANA hayupo zinaweza kuimbwa tu! Zinaimbwa si kwa ajili ya BWANA bali kwa ajili ya KUWABURUDISHA WATU!

  Anayeimba nyimbo kwa BWANA hawezi kuziimba kuburudishia walevi na wazinzi na wasiojitakasa! Kama mtu ataandaa tukio na kulifanyia ukumbi public, hilo ni jambo jingine. Lakini hawa wanaandaa na wanamuita muimbaji kisha kupatana kiasi watakachomlipa kwa ajili ya show yake…! Hapo kuna tofauti kubwa sana. Jambo la pili waimbaji wengi sasa wanaimba kupata pesa. Kwa hiyo hatajali nani amesikia au hajasikiliza ule wimbo ili mradi tu yeye apate pesa! Tuko nyakati za hatari.

  natamani ningekuwa na PC yangu nichangie kwa kirefu. Lakini hata haya machache yanatosha kwa sasa!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s