Kujiengua kwa James Millya, Mungu amejibu maombi ya Godbless Lema?

MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, kwa miaka mitano, James Millya,ametangaza kujiuzuru nafasi zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai kuwa CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania. Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini Arusha. Alisema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe. Alitaja nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.

Wakazi wa Arusha hawajaamini ukweli huu, kutokana na Ndugu James Millya alivyokuwa mchapa kazi na mwenye mapenzi na Chama cha CCM kabla ya kukihama chama hicho.

Leo Jumatatu, Tarehe 16 April 2012 ni siku ya saba ya maombi ya kufunga kwa Mbunge aliyevuliwa madaraka Arusha kupitia chama cha CHADEMA, Godbless Lema, alipotangaza mfungo wa siku saba tangu  jumanne iliyopita.

Advertisements

10 thoughts on “Kujiengua kwa James Millya, Mungu amejibu maombi ya Godbless Lema?

 1. Ni kweli kwamba Mungu ni wa watu wote, habagui dini wala kabila na inabidi watantzania tuwe makini tusije tukajikuta tunaamini Mungu atajibu maombi ya chama kimoja na kutojibu ya chama kingine. Huwezi jua kilichomtoa Milya CCM, undani halisi anaujua Milya na interest zake mwenyewe kwani hivi karibuni nimesikia kuwa anajihusisha na genge la wahalifu kuwadhulumu wanyonge wapiga kura akiwa ndani ya chadema. Mungu Ibariki Tanzania. —-

  JAMES OLE MILYA ADAIWA KUMILIKI GENGE HATARI LA VIJANA WAHALIFU.

  Ni Yule aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Arusha kabla ya kutimkia CHADEMA

  Adaiwa kulitumia kutapeli watu kujiingizia kipato kwa maslahi yake binafsi

  Mama aliyekumbana na genge hilo atoboa siri nzito baada ya kutapeliwa gari aina ya fuso

  Apanga kumuona Rais amsaidie, amtaka kusambaratisha genge hilo hatari hapa nchini.

  Na Victor Bariety,Mwanza

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha (UVCCM), kabla ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), James Ole Milya anadaiwa kutumia taaluma yake vibaya na kwa maslahi yake binafsi kwa kumiliki genge la wahalifu anaowatumia kutapeli mali za watu yakiwemo magari na baadaye kuwakingia kifua punde wanapokamatwa na vyombo vya dola.

  Imeelezwa kuwa, Ole Milya ambaye kitaaluma ni mwanasheria amekuwa akifanya hivyo kwa lengo la kujiongezea kipato ambapo imedaiwa kuwa vijana anaowatumia kwa utapeli huo ni wale wazoefu kwenye kazi hiyo na tayari kwa kutumia mgongo wake wamekwisha fanikiwa kuwatapeli watu kadha wa kadha ndani na nje ya Mkoa wa Arusha yalipo makazi ya Genge hilo.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya gazeti hili,vimemueleza Ole Milya kama mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuwafundisha vijana wake mbinu kali za kutapeli pasipo mwenye mali kughutuka na inapotokea kutiwa mbaroni Ole Milya amekuwa mstari wa mbele kuwatetea vijana hao wadogo kiumri wanaojihusisha katika shughuli zake hizo za kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu(Utapeli).

  Akizungumza na gazeti hili Jijini Mwanza, mmoja wa watu waliokumbana na matapeli hao wanaodaiwa ni vijana wa Ole Milya, Mlalamikaji ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kimnyak katika kata ya Kimnyak Wilaya ya Arusha alidai kuwa alikumbana na matapeli hao Januari mwaka jana 2012 na bila kujua anatapeliwa alijikuta akikabidhi gari lake,ambapo hakulipata tena.

  Alidai kuwa,Chanzo cha yeye kukabidhi gari hilo ni baada ya mmoja wa vijana hao kumfuata akidai kuwa yeye ni msimamizi wa Camp ya ZARA inayojengwa katika kijiji cha Esirwa Endulen Ngorongoro hivyo alihitaji magari kwa ajili ya kubeba vifaa vya ujenzi katika camp hiyo bila kujua ulikuwa ni mpango kabambe uliosukwa na kundi hilo ili kumtapeli.

  “Nilimpatia magari mawili moja aina ya tipa isuzu na nyingine Fuso ambapo alikuwa akiyatumia kupeleka vifaa vya ujenzi katika eneo la camp ya Zara Tours iliyoko Endulen Ngorongoro”
  “Baada ya muda alikuja kunirubuni na kuniambia kuwa,kadi halisi ya gari inahitajika katika ofisi za hifadhi ya Ngorongoro kwa kuwa gari hilo litahitajika kupita getini mara kwa mara kwenda kuchukua vifaa karatu nami nilimkubalia na kumkabidhi kadi hiyo bila kujua ni mpango wao na Ole Milya kutaka kunitapeli gari yangu na baadaye aliliuza bila mimi kujua”.

  “Baadaye nilipata taarifa kuwa gari yangu aina ya fuso haipo site taarifa ambazo nilipewa na kijana mmoja aitwae Emanuel.”alisema na kuongeza.

  “Nilipomuuliza Richard gari langu lilipo alidai amelipeleka garage huko Karatu iitwayo Sule…. Nilifunga safari hadi karatu na kukuta hakuna garage yenye jina hilo na ndipo nikampigia dereva aitwae Edward simu akaniambia yuko njiro mjini Arusha”.

  “Nilipomuuliza gari lilipo alidai liko garage ila hajui ni garage gani na linatengenezwa nini kwa kuwa yeye alifikisha gari Arusha na kumkabidhi funguo ndugu Richard kwa makubaliano kuwa wataonana siku inayofuata kwa ajili ya kwenda garage. kesho yake alipofika Richard alimjulisha kuwa amekwisha peleka gari hilo garage hivyo aendelee kupumzika likiwa tayari atamjulisha. Nikaamua kumwambia nimeanza kuwa na wasiwasi juu ya gari kutokana na taarifa tofauti za gari anazonipatia kila ninapompigia simu na tangia siku hiyo Mawasiliano yalianza kuwa magumu baada ya Richard kuwa hapokei simu yangu”aliongea kwa masikitiko mwanamke huyo huku akibubujikwa na machozi.

  Baadaye akiwa anatafakari asijue la kufanya anasema,alipata taarifa kuwa,Richard Birikaa amekamatwa na yuko katika kituo cha polisi makao akiwa ameshtakiwa kwa makosa mengine ya utapeli likiwemo la kumtapeli ndugu Petei jumla ya wastani wa Tshs. 16m.

  “Bila kuchelewa..nilienda mpaka Endulen na kumkuta akiwa amepatiwa dhamana… niliongea na Familia ya Richard na ndipo mbele ya mama yake mzazi, baba yake mdogo ndugu John Kereto, dada yake Mosipa na mdogo wake aitwae Makaai alikiri kuwa gari hilo ameliuza mjini Arusha. Nilifika kituo cha polisi Endulen nikaandika maelezo katika kituo hicho na nikaruhusiwa kuondoka na ndugu Richard ambaye alikiri kunitapeli gari na aliahidi akifika Arusha atanionyesha alikouza gari langu”.alisema bi Mollel.

  Hata hivyo katika hali ya kushangaza,Baada ya kufika Arusha kijana huyo alimgeuka na kudai asingeweza kumuonyesha wala kumtaja aliyeemuuzia gari hilo kwa madai hamkumbuki na hata akimkumbuka hawezi kumtaja kwa kuwa anahofia kupoteza maisha.
  Baada ya vuta nikuvute kijana huyo alikubali, kumkabidhi mwanamke huyo eneo lake la ardhi lililoko Ukerewe kufidia gari alilouza.

  Mkataba huo ulisainiwa mbele ya baba yake mdogo anayeitwa ndugu John Kereto (Mwalimu mstaafu), kaka yake Richard ndugu Sakara Birikaa na mwanasheria Emanuel Kinabo ikiwa ni pamoja na nakala ya power of attoney ya kukabidhiwa eneo hilo ikiambatanishwa katika makubaliano hayo.

  Mkataba huo(tunao)Ndugu Richard Ndorosi Birikaa alisaini akikubali kulipa ndani ya siku kumi kuanzia tarehe 26 Machi 2012 hadi tarehe 5 Aprili 2012 atakuwa amelipa fedha za Kitanzania jumla ya 62,730,000 Milioni. ikiwa ni thamani ya gari na malipo ya kazi zilizofanywa na gari hilo alilojipatia kwa njia ya udanganyifu(kitapeli) na kuliuza bila ridhaa ya mmiliki au kulirejesha gari hilo.

  Hata hivyo alisema,baada ya kukabidhiwa eneo hilo baba mdogo wa kijana huyo,John Kereto na Sakara Birikaa waliomba kupewa siku kumi yaani kuanzia tarehe 26/3.2012 hadi tarehe tarehe 5/4/2012 ili watumie muda huo kumshawishi Richard iwapo atakuwa tayari kumtaja aliyemuuzia gari hilo.
  “Hata baada ya muda huo kuisha bado Richard alishikilia msimamo uleule kuwa hawezi kumtaja aliyemmuzia gari langu kwa kuwa anaweza kupoteza maisha hivyo yuko tayari kukabidhi eneo hilo hamyebe lililoko katika kisiwa cha ukerewe Mkoani Mwanza na mnamo Tarehe 14/4/2012 Richard alisaini mkataba kwa mara nyingine tena kuwa amenikabidhi eneo hilo badala ya gari langu”.

  Januari 2013 nilisikia kuwa ndugu Richard anataka kuliuza eneo hilo kwa mara nyingine. Ndipo nikaamua kumpeleka ndugu Abraham kwa ajili ya kuliendeleza eneo hilo.
  “Cha ajabu tarehe 5/2/2013 Richard Ndorosi Birikaa akifuatana na ndugu James Ole Milya akidai hakuwahi kunimilikisha eneo hilo”
  “Baada ya kuonyesha mikataba katika ofisi ya OCD wilaya ya ukerewe mwenye namba 0754 392719 Richard kwa ujasiri alidai kuwa saini inayoonekana katika mkataba huo si yake ila imegushiwa”.

  “Alipoulizwa na OCD kuhusu power of attoney inayoonekana imeambatanishwa alidai nyaraka hiyo ni sahihi ila hajui imepatikanaje”.alisema.

  Kufuatia hali hiyo.alilazimika kufungua mashitaka kituo cha polisi na kupewa namba ya jalada kumbukumbu PMB/RB/364/2013 “WIZI WA KUAMINIWA”mkoani mwanza na baadaye Richard alitiwa mbaroni na kuwekwa Lockup katika kituo cha polisi ukerewe na kisha kusafirishwa hadi Mwanza tarehe 9/2/2013.

  Hata hivyo alisema,katika hali ya kusikitisha na inayodhihirisha Ole Milya anamiliki genge la wahalifu,James Ole Milya na ndugu Loomu Ojare ambaye ni wakili maarufu jijini Arusha walimshauri ndugu Richard Birikaa kukana saini zilizo katika mkataba huo mbele ya OCD wilaya ya ukerewe.

  “Ndipo nilipogundua na kuamini kwamba Ole Milya siyo mtu mwema na hastahili kuwa kiongozi wa watu katika Taifa letu..maana ameshasuka mpango huu vema na kuieleza familia nzima ya ndugu Richard Birikaa kukana saini katika mkataba huo”.

  “Maana hata majuzi tu 11/2/2013 John Kereto ambaye ni ndugu wa kijana huyo alipoitwa katika kituo kidogo cha polisi endulen kuhojiwa iwapo anajua kitu chochote juu ya mkataba wa Richard na mimi mmiliki wa gari lililouzwa na kijana huyo alinikana na kusema hakuna mkataba wowote aliowahi kushuhudia namuomba Rais Kikwete anisaidie kupata haki zangu na kusambaratisha mtandao mzima wa Ole Milya”.alisema mama huyo huku kwikwi za kilio zikiwa zimemkaba.
  Harakati za

  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini pia kuwa,kuna mpango umesukwa na ndugu Ole Milya na wenzake wa kutafuta uwezekano wa kuondoa kumbukumbu za tuhuma zilizowahi kuripotiwa katika kituo cha polisi makao na endulen wilayani ngorongoro ili kumwezesha mtuhumiwa ndugu Richard kukana utapeli wa gari hilo.

  Uchungzi pia umebaini kuwa,ili kuhakikisha mpango wao wa kutapeli eneo hilo unafanikiwa,Ole Milya na wenzake hivi karibuni waliweka kambi kwenye Kisiwa Cha Ukelewe kuanzia tarehe 5 Februari 2013 hadi tarehe 9 Februari 2013 akimfua mtuhumiwa Richard Ndorosi Birikaa jinsi ya kulikwepa shitaka hilo.
  MWISHO.

  NAMBA KWA AJILI YA KUTHIBITISHA MADAI YA MLALAMIKAJI BI MOLLEL.

  Namba za Richard Birikaa 0757 057 011, 0717 182 530, 0789 803 000.
  Namba ya mkuu wa kituo Endulen 0754612017 wilayani Ngorongoro.
  Polisi Makao namba mkuu wa kituo makao 0755843026
  Namba ya mlalamikaji 0767 427 405.

 2. Naungana na Ndugu Kinyau Haggai na Ndugu Orbi.
  Pengine ni vema tusichanganye mambo na kuona ya kwamba Mungu yupo ndani ya Chama fulani. Hii inakuwa sawa na kusema ya kwamba Mungu ni wa dini fulani au kwa mapanuzi zaidi wa dhehebu fulani. Mtu yeyote ahamapo kutoka Chama fulani cha Siasa; bila shaka ana sababu zake na pia kimsingi anaitumia haki yake katika kujiamlia apendalo.
  Jambo hili halitofautiani na lile la Mkristo wa dhehebu fulani kuhamia dhehebu jingine na pia hata mgawanyiko na mipasuko ya makundi.
  Mimi sina shida kumwunga mkono mtu asimamaye katika kweli kwa manufaa ya wote. Ninapoomba nawaombea viongozi wote waliopo madarakani bila kujali ni kutoka chama kipi, kabila lipi, ukoo upi, dini ipi nk. Nikijua ya na tena kuwa na uhakika ya kwamba hakuna mtu aliyemkamilifu katika yote; hata huko alikohamia Millya wapo vilevile wanaofanana na kule alikotoka. La msingi ni kuliombea Taifa letu sote tuneemeke.

 3. Huu ni mwanzo tu wa ishara ya mambo ambayo Mungu anakwenda kutenda katika taifa hili kwa kuwa mkono wake ni wenye uweza na nguvu hakuna awezaye kuuzuia.Watanzania wote wanaopenda mabadiriko tunapaswa kumuunga mkono Godbless Lema na kuomba juu ya taifa letu.MAMBO MENGI YAJA HUU NI MWANZO.

 4. Ndugu Kinyau,

  Nakupongeza mno kwa mawazo yako…….Hivi Mungu ni mpenzi wa chama Kipi Tanzania….? Hata kama ndugu Lema alifunga kwa ajili ya hili, hilo ni swala binafsi kabisa kati yake yeye na Mungu……na halikutakiwa hata kuletwa hadharani…..? Maana inawezekana hata ndani ya CCM kuna wengi wanafunga na kuomba ili wasio na mapenzi ya kweli na CCM waondoke…….utasemaje hapo……?

  Mada hii kwangu mimi ni sawa na ile ya Nabii Joshua kuhusu kufa kwa Raisi wa Malawi….au Lowasa kuwa Raisi…….Kuna Marais wengi duniani…….wanakufa….wanapinduliwa …….Kwa nini Malawi tu…….?Au alipotabiri kuhusu Zambia kunyakua kombe la Africa……! Kuna hata wengine wameandika kwamba wale wanaompinga Nabii Joshua sasa wafunge vinywa…!!!!Niliposoma Nilibakia kutabasamu tu na kusema kweli wakristo tunasafari ndefu mno ya kujua utendaji wa Mungu….!

  Kwa hiyo hata hili la Lema….ni vigumu kutoa majibu…..maana naona si muda mrefu tutasema Mungu yuko upande wa Chadema………au Mungu ni wa CCM…..!!!

 5. NADHANI NI WAKATI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KUJIPIMA UPYA KABLA YA 2015, KWANI UKIONA VIJANA WANAANZA KUJIENGUA KIJUE KUNA ANGUKO KUMBWA MBELE YAKE! VIONGOZI WAKE PIA WAMRUDIE MUNGU KWANI ILANI YA CHAMA HIKI KIMEWEKA WAZI NI NINI KITAWALETEA WANA NCHI WA TANZANIA,HUYU JAMAA NAMJUA ALIKUWA MWENYEKITI WANGU WA UVCCM MKOA WA ARUSHA NIKISOMA MAKUMIRA UNIVERSITY! TATIZO LIPO KWA WATENDAJI NDANI YA CHAMA! OTHERWISE, WANA NCHI SANA SANA WA ARUSHA WATAANGALIA, KAMA HAWAJAANGALIA NI CHAMA KIPI KINAWALETEA, KITAWALETEA MAENDELEO! KWELI TUNAHITAJI WACHA MUNGU KATIKA UONGOZI JAMANI! HIVYO CCM IJIPIME UPYA!

 6. Wapendwa,
  Kabla ya mtu kusema chochote, nadhani wachangiaji wangejibu swali lililoulizwa hapo juu kwamba je, Mungu amejibu maombi ya Godbless Lema?

  Kwangu mimi swali hili lipo too general na sidhani kama ni rahisi sana kulijibu!! Nasema swali hili ni gumu kulijibu kwa sababu muuliza swali hajatueleza agenda gani za mfungo wa siku saba alioendelea nao Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini alikuwa nazo moyoni. Mimi ninachojua ni kwamba huwezi kufunga na kuomba bila kuwa na agenda unazotaka Mungu ashughulike nazo kwa ajili yako au jamii unayoishi.

  Hivi kweli muuliza swali unataka kutuambia kwamba moja ya agenda za kufunga kwa Lema kwa siku saba ilikuwa ndugu Millya ahame CCM na kujiunga na CHADEMA? Mbona tunataka kuipeleka blog hii kusikukuwa na manufaa yalikusudiwa?

  Kitu gani cha ajabu kwa mwanasiasa wa Tanzania kuhama chama kimoja na kujiunga na chama kingine? Hivi ni kweli tunahitaji kufunga kwa siku saba ili mwanasiasa mmoja ahame toka chama kimoja kwenda chama kingine na tuseme kwa hakika kwamba Mungu amejibu maombi yetu?

  Nimelitafakari sana swali hilo hapo juu kweli sikuona mantiki yake, mtanisamehe kwa wale watakaoona nimewakwaza kwa tafakuri hii.

  Mungu awabariki sana.

 7. Huyu bwana amefanya uamuzi wa kidemokrasia. Kila mtu ana uhuru wa kuabudu dini anayoitaka. Hali kadhalika kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama anachoona kitafaa kwake.

  Haina maana kuendelea kutumikia chama ambacho unaona kinatenda mambo yasiyoubariki moyo wako na kila siku moyo wako umejaa kuhukumiwa nafsi yako.

  Kila mtu aelewwe kwamba HAKUNA CHAMA PENDWA MILELE. Kama mke na mume waliokuwa wanapendana saaana huwa wanafikia hitimisho la kuachana sembuse kuachana na chama ambacho siyo mke wako au mumeo?

 8. Hakika huu ni mfano wa kuigwa. Yeyote atakayeona sera za chama chake hazina manufaa ahame upesi.

 9. Anaona mbali sana huyu!Ni hasara kuendelea kupigania vita upande unaoona utashindwa vibaya karibuni!tuwaache wenye fikra hafifu waendelee kutarajia miujiza ya shetani!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s