Mambo ya bahati nasibu

Biblia imeandikaje?

Mithali 16:25 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti”

Siku zote kuna jinsi ya kujihusisha na dhambi au kusababisha dhambi katika dunia hii, kiasi kwamba ni ngumu kutambua kwamba unajiingiza maeneo hayo!!!

Tusome haka kakipande,

Mathayo 25:14 -30 ” Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama mtu anayetaka kusafiri, akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao ili kuitunza na kuizalisha.  Mmoja akampa talanta tano mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja, kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri kwenda mbali. Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi. Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi. Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja,alikwenda akachimba shimo ardhini na kuificha ile fedha ya bwana wake. Baada ya muda mrefu yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao. Yule mtumishi aliyepokea talanta 5 akaja, akaleta nyingine zaidi. Akasema, ‘Bwana uliweka kwenye uangalizi wangu talanta tano. Tazama, nimepata faida talanta 5 zaidi. Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache, nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako. Yule mwenye talanta 2, naye akaja. Akasema, `Bwana, uliweka kwenye uangalizi wangu talanta 2. Tazama nimepata hapa faida ya talanta mbili zaidi.’ Bwana wake akajibu, Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu, umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache, nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako. Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta 1 akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unayevuna mahali usipopanda na kukusanya mahali usipotawanya. Kwa hiyo niliogopa, nikaenda, nikaificha talanta yako ardhini. Tazama, hii hapa ile iliyo mali yako. Bwana wake akajibu, Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu. Vema basi, ingekupasa kuweka fedha yangu kwa watoa riba, nirudipo, nichukue ile iliyo yangu na faida yake? Basi mnyang’anyeni hiyo talanta mkampe yule mwenye talanta kumi. Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo tele. Lakini kwa mtu yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa Nanyi mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje, kwenye giza, mahali ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Kwa maneno hayo juu japokuwa Bwana Yesu alikuwa akizungumzia juu ya hukumu ya mwisho, kutengeneza mambo, mafundisho yake pia yanatufanya tuone jinsi gani anawasiliana nasi kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kwenye karama (fedha) zilitolewa kwa watu watatu, watumwa wawili walitumia kutengeneza faida lakini Mtumwa “mbaya” na “mlegevu”  aliifukia au kuificha pesa yake, haikuzaa chochote kama alivyopewa ilirudi  vile vile, pongezi, malipo, walipewa wale wengine wawili baada ya watatu kuonekana hakufanyia kazi kile alichokuwa nacho!!

Hapa tunaona jinsi Bwana Yesu alivyo mtu wa faida, au kufanya kazi kwa bidii. Tunajifunza kutokaa tu na kusubiri vya bure bure, tunajifunza kuchagua mipango mizuri ya kutuingizia faida na mipangilio inayoeleweka. Faida siyo neno baya ila jinsi gani unaipata hiyo faida!! 

Wale watumwa wawili wametumia walichopewa na kufanya kazi yenye faida ambayo ilipokelewa vyema na bwana wao.Wewe tangu umeanza kucheza bahati nasibu umeongezewa ngapi? zaidi ya kujitabiria umaskini? hauna tofauti na yule mtumwa mwovu na mvivu!!

Wafilipi 4:19 ” Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika Utukufu ndani ya Kristo Yesu

Mwisho

Bahati nasibu ni kucheza kamari, Imani yako ijenge kwa Mungu sio kwa “kubahatisha” Mungu haitaji wewe ucheze sana bahati nasibu ili akubariki hayo mamilioni, na ndio maana siku akirudi kutuchukua hakuna cha bahati nasibu au mwenye kupata apate mwenye kukosa akose kuurithi uzima wa milele.

Tufanye kazi kwa bidii, kwa mipangilio mizuri yenye kutupa faida huku tukimsubiri Bwana atimize ahadi zake kwetu!!

Advertisements

2 thoughts on “Mambo ya bahati nasibu

  1. watu wengi bado ni wageni na huduma za kinabii kwa sababu msingi wa kanisa ulikosewa :;haukujengwa juu ya Yesu Kristo ambae ndiye jiwe kuu bali ulijengwa. juu y dini ; ujio wa Bwana Yesu uliwachanganya watu wa dini YHN 10:19-21; kuna vitu ambavyo watu wa dini hawakuwai kuviona(kama za kipindi pia)ambavyo Yesu alivitenda ili kudhihirisha uweza MUNGU ndani ya kanisa LUKA 13:10-13.Watu wengi leo hawajui kuwa Yesu alitembea na hudum zote tano mfn YHN 4:15-19 hii ni huduma ya kinabii;
    Unapowaambia watu mimi nimeitwa kubeba kusudi la Mungu, watu ambao msingi wao ni Yesu wanajua Mungu hakutuma mtu akampa maneno matupu kama watu wa dini wanavyoaminisha watu, Mtume Paulo, ansema hivi , warumi 15:17-19, watu watatii na kumfuata Yesu kwa neno lake Yesu linalo hubiriwa kwa utimilifu kwa nguvu za ishara na maaajabu ktk nguvu za Roho Mtakatifu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s