Nabii Malisa Kurudisha nyota zilizoibiwa PTA

Haleluya wana wa Mungu? Katika gazeti la Nyakati tole Na. 05B3 la tarehe 08-14 April, 2012. Pameandikwa somo hilo hapo juu itakuwa tarehe May 4, hadi May 6. Limetangazwa gazetini. Mtumishi awaye yote sina tatizo naye, tena huyo nabii wa Bwana Kutoka Mwanza huwa ninampenda mno. Katika ujana wake anamuishia Mungu.

Wapendwa, ninaomba msaada wenu, labda sijafundishwa jambo hili, au viwango vyangu vya Imani havijafikia kiwango!! Hili somo la kurudisha nyota zilizoibwa, kibiblia ni sahihi? na kama ni hivyo, nisaidieni references zake, nipate kujifunza zaidi kutoka kwenu, maana haya mambo magumu, pia kwa sehemu ninaamini biblia ni msitu, nisiwe mbishi sana, Mubarikiwe!

Oguda E.J

Advertisements

45 thoughts on “Nabii Malisa Kurudisha nyota zilizoibiwa PTA

 1. Hiki ni kizazi kilicho dhaifu sana katika maombi na kusoma maandiko. Wengi ni wazururaji hawana baba wa kiroho na hawana utumishi. Hivyo ni kizazi ambacho hakitaweza kutoa waamini “ma-giants” watakaoweza kusimama na injili ya Ufalme isipokuwa dwarfs-waoga na wasiojiamini katika kazi ya Mungu. Leo kukemea pepo mdogo unaitwa mchawi, wewe kweli unasehemu katika Ufalme wa Mungu mtenda miujiza?

 2. Mimi siyo mshirika wa Nabii BG Malisa lakini ukweli utabaki palepale kuwa hizi ni nyakati za uweza wa Mungu. Mtu akimtaka Mungu na uweza wake mtamwona. Matendo makuu ni fungu la wote waaminio. Nabii Malisa anamwamini Mungu ndiyo maana haya yote yanaonekana kupitia yeye. Kuwazuia watu wasimfuate tunaanza kujiuliza juu wito wako ni nini maana tunachokiona ni upako wa wivu, kazi ya Mungu isifaanyike. Nabii Malisa kama unasoma michango yetu, endelea mbele watu wafungulie waache wanaokuogopa waendelee kukutangaza kwani tangu waanze kukushambuliwa na huduma yako ndio kwanza unasonga mbele na wakosoaji ndio hao wanakimbia huduma zao. Watazamaji tunawaona!
  Keep it up till it is done.

 3. Bwana aliweka huduma tano, zote za kweli. Waelekeze watu kwa nabii wa kweli, kama unakosoa tu, na wewe tunaanza kuwa na mashaka na wewe. Ukishakosoa wakaribishe watu waje kwako au walekeze kwa nabii wa kweli! Vinginevyo na wewe ni mvurugaji tu.

  C. Kibali.

 4. Jamani Mtawajua kwa matunda yao sasa huyu askofu Mpemba amekimbia nchi. Yuko mafichoni marekani. Nabii wa kweli anasimama kama Eliya Mtishbi na kusema ijulikane leo. kwamba wewe ni Mungu wa Kweli.

 5. Jamani ni kweli manabii,wachungaji,wainjilisti,waalimu na mitume(huduma kuu 5) kuna wakweli na wa uongo,,,lkn kwa nn akiinuka mtumishi akawa na nguvu kubwa ya kuponya na kutenda miujiza anatiliwa mashaka na anasemwa kuwa ni wa uongo(wa shetani) ina maana shetani ana nguvu kuliko Mungu? kwann watu tumemtukuza shetan kuliko Mungu? Yakifanyika mambo makubwa ni ya shetani,anatumia nguvu za giza,uchawi,,,,kwa hiyo yale manyonge ndo ya Mungu? Na wanaosema kwamba watu wanakimbilia miujiza,ni nani asiyetaka miujiza? Nani ambaye yuko tayari kuteseka mpk kufa eti yy hataki miujiza? Yesu mwenyewe alidhihirishwa kusudi azivunje kazi za ibilisi,magonjwa,umaskini na mateso,dhambi hizo zote ni kazi za ibilisi,,,Yesu mwenyewe alisema amekuja kuwatangazia mateka uhuru wao,waliofungwa kufunguliwa kwao na maskini habari njema(kufanikiwa/kutajirika kwao),na km miujiza Yesu ndo mwanzilishi wa miujiza,aliitenda sana mpk kufufua waliozikwa cku 4 kaburini,na akasema yeyote aniaminiye mm kazi hz nizifanyazo atazitenda,naam hata kubwa kuliko hz atatenda.
  Miongoni mwa karama 9 za Roho mt.kuna karama ya kuponya na matendo ya miujiza,mafunuo ya utendaji ndo yanatofautiana,,,,mf Yesu wengine aliwawekea mikono,wengine alichanganya udongo na mate yake akawapaka machoni akawaambia waende wakanawe wakapata kuona,,,kivuli cha petro kiliponya wagonjwa,,,,leso ziliponya wagonjwa,,,
  Je leo mtu akipakwa tope lililochanganywa mate si ndo watasema shetani kbs huyo,,,,,kwa nn leo mtu akipata ufunuo tofautitofauti wa kuponya/kufungua waliofungwa watu wanaanza kusema ni uchawi?!
  Kila jambo tulitafakari kwanza na kumuuliza Mungu km una mashaka ksb Mungu anamtumia mtu km YY atakavyo si km mtu atakavyo. Usije kujikuta unamkufuru Roho mt. kwa kusema kazi zake ni za mapepo.
  Tahadhari ni muhimu ila tusikurupuke kunyooshea watumishi vidole,pengine tu ksb ya mapokeo tuliyopokea kwa viongoz wetu wa dini,au ksb ya uelewa wetu mdogo juu ya mambo ya kiroho.
  TAFAKARI CHUKUA HATUA!

 6. Kwa kweli nimefarijika sana na hoja za wachangiaji hapa. Mimi si msomaji sana wa Biblia lakini nina mafundisho kidogo na ni mkristo. Nachoweza kuchangia ni ushuhuda wangu binafsi na nini nimejifunza hasa katika kudhuria semina mbalimbali za wachungaji na hawa manabii. Mfano kwa Nabii Malisa nishaenda michungwani japo mimj ni Mkazi wa Dsm na pili nimeenda kwa hili kanisa lipo njia panda ya mbweni Dsm wanajiita house of prayers Kuna mtu anaitwa Yesu wa mkombo na mchungaji Musa. Naomba nijumuishe kwa kusema binafsi roho yangu inaniuma sana na hasa teyari ninapo ona sisi waumini kwel tuna uhitaji wa huduma ya kiroho lkn sasa manabii na wachungaji wote wametubadili kwa kutupeleka katika miujiza ki ukwel watu wanakimbilia miujiza. Na niseme mfano wakati naenda kwa Huyo wa kanisa la mpakani kule Bunju B wanaombea watu wengi na unajaza form unalipia elfu kumi na kuja kwako unalipia elfu thelathini wanakuja nyumbani kwako.Kwakweli nilifadhaishwa hasa huyu mvhungaji musa alipokuja nyumbani kijitonyama na kabla hajaja wakati wa maombezi ya kawaida nilimfuata mimi na mke wangu atuombee akasema nyumbani mnapokaa kuna vitu vibaya na ndipo nikalipia akaja. Sasa na alipofika alisema tusali na akatoa mistari ktk biblia sikumbuki lkn alisoma na ilisema hata Yesu alienda nyumbani kumponya lazaro hivo anasema ktk kutoa huduma ya kiroho na kumuombea mtu Yesu pia aliwatembelea watu majumbani kwao na kwahyo hilo sio jambo geni. Kilicho niudhi aliingia chumbani na kurusha maji na baadae alitoa vitu chini ya uvungu wa kitanda kuwa ni vya kichawi tulitegwa na akaondoka navyo. Kwa kwl nilimuamin sana japo moyoni ili nistua sana kwa kujiuliza mbona ni kama uganga. Nikawa muumin wao mzuri na mara kuna siku wanapika kanisani muumini unakula bure ila shart ukirud nyumban usile na basi unafunguliwa ikiwemo nyota n.k. . Mwsho mke wangu alipo tata ujauzito nilienda kama kawaida atuombee bahat mbaya mke wangu alikuwa ameteguka mguu basi huyo mchungaji Musa nilipofika na mke wangu huwa wakikuangalia wao wanasema wameotehswa so wanafanya vile vile kama waganga wa kienyeji yaani anakutajia mambo yanayo kuhusu,basi akamwangalia mke wangu akasema Hii mimba yako ina ukinzani mkubwa sana una matatizo…basi kwa kwl tulitafakar mm na mke wangu kwa pamoja na majumuisho ya mienendo yao roho ziligoma na tukasema hatutosari tena na ikawa hivo. Kuhusu malisa nilwahi sali na moja ya kivutio cku ya kwanza tulifundishwa jinsi dhambi zinavoathiri maisha ya binadam tukafundishwa chanzo cha dhambi huyo alie tufunfisha hakuwa malisa bali alikuwa kijana muhudum wa pale jina sikumbuki .Basi utaratibu wao ni kuwa huwez safishwa na kuombewa mpaka upate mafunzo basi kesho yake ilikuwa ni kwenda kutubu na kuombewa.Kinachofanyika ni kwamba kila mtu anapita mbele ya watu mnagawanywa mfano watu 30 basi unaenda mbele ya hilo kundi unaanza tubu dhambi ulizofanya.Msingi wake huyo mwalimu anasema ktk biblia sikumbuki mstari ni kwamba Yesu wakati anaponya watu alisema watubu dhambi mbele ya mashahidi kwa hyo mfano mm nilipita mbele ya hilo kundi tulilofundishwa siku ya jana yake nikatubu na huyo mwalim anasema hapo ndo unasamehewa ki kweli maaana umetubu mbele ya mashahidi. Basi kwa kweli watu walitubu sana nikiwemo na mm na wengine mambo ya pepo ndo yalitawala.Nachotaka sema sasa kulingana na mada ya nyota na uongo wa hawa watu wanaotuongoza kwa ujumla wasiwe ti manabii ni kwamba mimi kwa kwl nikampenda kbsa huyo malisa na hyo jumapili nikaenda sali nakumbuka ilikuwa mwshoni mwa 2012. Basi kukawa na sadaka ya kuomba chochote unachotaka unachukua hela unaweka ktk bahasha wengi walianzia elfu 10 na unaenda mbele wanasema ndani ya cku 7 utaona majibu na hela ikiwa kubwa basi majibu ni haraka nami nikafanya hvo nakumbuka niliweka afl 10 lkn nilichoomba sikufanikiwa . Nikajifunza kuwa kila jumapili kumbe hyo sadaka ya namna hyo wanatangaziwa na watu wengi wanajitokeza. Kwa kweli watu wa mungu ushuhuda huu mimi umenifundisha yafuatayo. Kwanza wanatuhubiria matatizo ya kila siku na hasa nyota inazungumziwa sana lkn nikirejea hoja za hapo juu na ushahidi wa kote nilipo sali kwa kwl watu hawa hawaitendei haki maneno na miongozo ya kristo ila ni kutuchanganya tu sisi waumini dhaifu na tulio wengi, Pili nashtuka kuwa kwa nini waumin wng tukienda kuombewa wote matatizo yetu ni nyota na pepo ..Nilisikitika mtu kaenda ombewa yy kaenda ili aombewe ni mgonjwa wa mguu alivunjika sasa haponi haraka mala akasukumwa kuwa ana pepo sijui jin mahaba kwa kweli naungana na wanaosema kusema tu Kwa Jina la Yesu kristo sio kwamba ndio wasionekane sio waongo kwa kweli wengi wamejificha nyuma ya Jina la bwana na Mimi pamoja na familia tumeweka msimamo wa kusoma biblia nakuomba hasa kupitia Roho mtakatifu.Mungu ni jalie mimi natuokoe watu wako tunaangamia kwa kukosa maarifa

 7. Mmekazania manabii wa uongo hamjui huo Ni ujanja wa shetani kuwasahaulisha mambo ya msingi na pia zaidi kuwatia hofu mioyoni mwenu ili mshindwe kuomba, mshindwe kwenda kanisani kwa hofu ya manabii wa uongo, mshindwe kushuhudia wanye dhambi waokoke, ili Yesu akirudi awakute hamko tayari. Haina haja ya kusikiliza mtu, Wala cd,Wala kusoma kitabu chake ili ujue Ni nabii muongo au mkweli hiyo Ni njia mojawapo tu tena ndogo, kubwa Ni Roho mtakatifu,kwani hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa roho yake Mungu mwenyewe,halikadhalika roho wa Mungu Akiwa ndani yako chochote utachosikia kwakuwa Mungu anakijua atakuambia Kama Ni ukweli au uongo na utakuwa umeokoa muda badala ya kusoma kitabu,au kusikiliza mahubiri ya mtu, au kusikiliza Cd ,Roho atakuambia na utajua na utapata mda wa kufanya mambo yako mengine ya msingi. Tatizo sasa hata huyo roho watu Hawana kwani hakai pachafu penye mwili wa dhambi bali mtakatifu Kama jina lake Roho mtakatifu, hivi inakua changamoto kwa watu wengi. Mwenye sikio na asikie.

 8. BwAna Yesu asifiwe Watu wa Mungu. Nimepitia michango yenu ila Ninachoweza kusema ni kuwa, Kama wewe unajua Kuwa unamwamini Mungu wa kweli kwa kadri ya Imani yako, piga magoti muulize juu ya Nabii huyu Kabla hujaanza kumjudge Kuwa ni wa uwongo…..mwombe Mungu akudhihirishie, aseme nawe hata katika ndoto, utapata jibu………

 9. tuweni watu wazima ki imani tujisimamie Mungu wetu wa mbinguni ndiye muhukumu mkuuuuuu

 10. ndg zangu Yesu ainuliwe.nafurahi muno kupata fursa hii ni toe mawazo yangu.nasema kinacho tusumbua ni uchanga wa kiroho na imani,kwa nininasema hivyo naamini sote tunajua kuna falme mbili ya Mungu na ya Shetani na hazijawahi kuacha kupingana na kutunishiana misuli.tujikumbusha kidogo,Eliya na manabii wa baali alijulikana wa kuabudiwa ni Mungu wa Eliya.vijana Shadraka na wenzake aliuonesha Mungu wa kweli,Paulo aliudhihilishia umma kuwa yule mama hakuwa wa upande wa Mungu wa kweli.Yesu mwenyewe alionyesha kadamnas kuwa ile ni nyumba ya ibada na si pango la wanyang’anyi.watu wakajuwa ukweli .sasa sisi na watumishi wetu wachungaji mitume nk.tunakaa kurumbana yule ni na bii wa uongo mara free mason mara tapeli,umma uamini nini kutoka kwetu vipindi vya redio na magazeti!!! au uamini naniwakuabudiwa? wazo langu,ALIYE NA UHAKIKA KUWA YULE NI NABII WA UONGO AU FREE MASON ASIMAME KAMA ELIYA ASEME AJULIKANE LEO MUNGU WA KWELI umma uone.lasivyo wote ni njaa kila mtu anavutia kwake hasa wanaohukumu wengine.tukuwe.

 11. nyota ni neema mtu aliyozaliwa nayo,aliyopewa na Mungu. sasa kama unaamini shetani anaweza kuiaribu kwa yy ni muaribifu au kuiba, basi Yesu anaweza kuirudisha labda tatizo la watu liko kwenye misingi ya dini zoa (mafundisho ) na sio Yesu Mwenye uwezo wa kugeuza kila baya kuwa jema. ukikulia kwenye huduma za kichungaji kama hauko makini huduma ya kinabii itakusumbua na hiyo haimaanishi wewe sio mwana wa Mungu

 12. Nimesoma michango iliyowekwa naomba nikubali nimejifunza sana kutokana na hoja kinzani zilizoibuliwa. Naomba binafsi niseme kwamba suala la kurejesha nyota zilizoibiwa, si la kimungu haswa miongoni mwa jamii ya waaminio. Ukiachilia fundisho la mamajusi kuona nyota, sidhani kama kuna fundisho jingine ambalo kanisa laweza kusimamia kwamba kuna sababu ya kufundisha watu wa Mungu juu ya kurejesha nyota zao zilizoibiwa na shetani. Cha msingi sasa tujilinde na haya mahubiri yanayoambatana na imani potofu maana hata sasa yameingia ndani sana ya kanisa kiasi kwamba imekuwa kazi kutenganisha baina ya ipi ni imani sahihi na ipi ni potofu. Ila walio na Roho wa Mungu haitawapa shida. Nadhani ni vema tukajikita ktk kumtafuta MUNGU na karama zake badala ya kuanza kufuatilia kurejeshewa nyota zetu. Maana tazama mtu akiokoka na kuwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya! Na siamini sana kwamba aliyeokoka kweli kweli na kushikama na Kristo anaweza kuibiwa nyota yake, labda awe mguu pande! Kwa hiyo basi YESU mwenyewe aweza kutupa (kama kweli kuna nyota kitu ambacho siamini) kila kitu cha kiroho ktk upya wake tena bora zaidi kuliko mwanzo. Ayubu baada ya kuondokewa na mali, watoto, na kuharibiwa afya ya mwili wake, baada ya kurejeshewa vilikuja vilivyo bora zaidi kuliko awali. Hatusomi kama aliombewa arudishiwe nyota bali BWANA mwenyewe alitenda! Nasi tumuangalie Kristo na kukiri nguvu zilizo katika uwezo wa jina lake siku zote! Amina!

 13. Ndugu Milinga,

  Sikutambua kwamba wakati kusafisha Nyota toka kwa Nabii Malisa umewadia……naandika nikiwa maelfu ya maili kutoka Dar es Salaam….Lakini ndugu yangu Nabii Malisa asingeweza hata kunifanya niinue mguu wangu…….Msimamo wangu katika hili umeishajikita mahali…..yaani siamini katika NYOTA YA MUUMINI…..! Kama fahamu wangu uko sahihi Muumini aliyemwamini Yesu yuko ndani ya Kristo……na yeye ni Hekalu la Mungu…..Muumini katika Kristo hayuko katika LAANA YOYOTE ILE……! Na hata kama mafundisho ya Nyota yapo….basi siku Muumini alipompokea Kristo……alipokea Nyota ing’aayo yaani Kristo……!
  Hivyo ndugu yangu Millinga sidhani ningelikuwa na muda wa kupoteza kumtafuta Nabii Malisa.

  Na kuhusu kuvuta umati….kwangu mimi hiki sio kigezo KABISA…….Umati mkubwa ulimfuata Yesu lakini alichagua wanafunzi 12 tu…..! Na huduma yake miaka 3 iliacha wafuasi 120….tu…! Kwa hiyo umati si kigezo kabisa cha udhirisho wa kazi ya Mungu, kama wengi walivyofuata mikate na miujiza enzi za Yesu na leo ni hivyo hivyo…….! Injili ya kutaka “ngekewa” za biashara…..au kupata wachumba…….visa ya Marekani…..kupanda cheo……kununua gari……..”kusafisha nyota yako” siioni kabisa katika Nyaraka za Paulo…….! Kwangu mimi ni Injili Nyingine……….!UBARIKIWE…!

 14. Leo ningekuwa Dar ningehudhuria ibada ya BG Malisa. Ila kwa kuwa niko kwetu Kigoma nategemea kusikia kutoka kwa waliohudhuria mikutano ya BG Malisa.

  Wapendwa wengi bado wana mashaka na mafundisho ya BG Malisa wa kutoka Michungwani Mwanza.

  Hapo mwanzo nimependekeza watu waende kujifunza kutoka kwake hata kama wewe unaona tayari unayo Imani na Maandiko mengi Roho wa Mungu anakuwezesha kuyaelewa, natamani kwa wale walioko maeneo ya Dar wawe na muda wa kwenda kama siyo kushangaa basi kujifunza lolote toka kwa huyu kijana Malisa.

  Hadi sasa mimi sina upande wa kuegemea. Kama mhubiri anatoa nyota chafu kwa watu au kama anawapa nyota safi nk. mimi sijawa na upande wa kusimama.

  Napenda kuwaomba watu wanaosingizia kila kitu kwamba Neno linasema au Roho Mt. yupo kutufundisha waelewe kwamba bila mwalimu wa neno hilo haiwezekani ukalielewa Neno peke yako.

  Maandiko yanasema katika Daniel,….. nao wenye hekima wavutao wengi (kwa Kristo) watang’aa milele na milele.

  Kama kuna muhubiri anayevuta watu wengi kwa ufalme wa Mungu na watu wakamwishia Mungu wao, mimi sitajali dawa au uchawi uliotumika kuwavuta watu hao. Kama mhubiri huyi=o alitumia uchawi wa Nigeria au Ghana au wa Marekani au Sumbawanga au Tanga, au Ujiji au Bagamoyo, basi uchwi huo ni kiboko.

  Kama kuna wahubiri watumiao uchawi kuvuta watu makanisani, natamani watalaam wafanye utafiti zaidi kuhusu mada hiyo na watu wapewe facts zaidi badala ya maelezo matupu.

  Hebu akina Orbi, Kinyau, John Paul, Mabinza, LWEMBE na wengineo wenye uwezo wa kufanya research juu ya “MAGIC IN CHURCHES AND HOW MAGIC BRINGS PEOPLE TO CHURCHES” Watusaidie kufanya hivyo ili tujue ukweli zaidi. Swala la kusema Biblia imeshaeleza ni sawa lakini utafiti nao waweza kuondoa mingongano ya kimtazamo makanisani.

 15. Tunatetea mapokeo ya imani tulizoaminishwa kulingana na mahali tunaabudu sote tu viungo tunaujenga mwili wa kristo tunataka tufanane haitawezekana kwa sababu paulo,napetro na apolo wote walifanyakazi lakini kila mmoja kwasehemu yake ukitaka kuijua feki lazima uijue orijino tuonyeshe kisichokuwa ktk neno wanachofanya pili wakristo baadhi walishazoea ubaya hata likifanyika zuri wanaona ubaya nakwasababu kilichotangulia kwawengi niuganga nauchawi na imani zao hazikui biblia inasema tutafanyakazi kubwa zaidi yazile alizofanya hatujaona waliotayari nawaliotayari mnawapiga mawe yesu alisema tusitupe lulu kwanguruwe kwasababu watazikanyaga aliyetumwa namungu hatishwi namaneno yawatu hushika maagizo yaaliyemtuma akisikia yawatu atakufamapema 1falme 13:1-24 ukitumwa usjadiliane nawatu naukitumwa huanzii kwa watu unapimwa na kwanza utaweza kufikisha kusudi mungu anajivunia wewe na kwashetani utatambulishwa mungu alimtambulisha ayubu na yesu alipobatizwa alipelekwa nyikani ajaribiwe na ibilisi hata musa alikaa jangwani akiandaliwa utumishi niuwanja mpana tusimwekee mungu mipaka kwaimani zetu ndogo zisizotaka kubadilika nakukua jambo gumu likimkuta mpendwa tunasema shetani kajiinua sio kwamba mungu anamuinua kiimani yesu atusaidie km paulo ktk efeso 4:7-28 ninaimani mwenye kupenda kujifunza atafanyabidii kujua neno

 16. Nimefurahi sana kuona kwamba Ndg yetu Lwembe umerudi, nilikuwa nikihitaji sana kukuona katika hii Free Site! Karibu sana. Nashukuru kuwa Mungu amekubali hilo. Unajua,Uzuri wa mjadala wowote lazima pande zote mbili yaani inayokataa na ile inayo kubali ziwe na hoja zenye nguvu ndipo MAADA hukolea. Sasa, naona kuwa, Blog yetu itasonga mbele sana katika kulifikia lengo na kusudi lililopelekea kuanzishwa kwake,Maana ugumu wa hoja ndiyo hupelekea watu kufanya udadisi na hivyo kuongezeka kwa bidii katika kulisoma na kulijifunza Neno la Mungu! Urahisi wa hoja na mtazamo wa upande mmoja huondoa udadisi na bidii ya kujifunza. kanuni moja ya sayansi husema – No friction no movement!. Roma ya kale walitumia sana njia ya ukinzani, kuwazuia watu wasisome Biblia ili wasijekuwa wadadisi na hatimaye kuugundua uongo uliojificha katika Dini yao, kitu ambacho kitaleta upinzani kwa Dini na kwa viongozi wa Dini husika! Kuna mwanamziki mmoja alipata kusema neno la uvumilivu kuwa; “unaweza kuwadanganya watu wote kwa wakati fulani, lakini huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakwati wote!” – Shetani hupingasana kauli kama hizo, lakini Ilifikia wakati watu, pamoja na vitisho, vifo na kutengwa kaika ushirika na Dini husika watu wenyebidii na waliojaa shauku, Mungu aliendelea kutia udadsi mioyoni mwao watu wadadisi na ambao hawakuwa wavivu katika kujifunza, wakajasirisha ajabu, wasikate tamaa na wasiwe na hofu ya kushindwa, Ili matokeo yaje leo hii, ili watu wajifungulie Biblia watakavyo, na hata tunawaona sasa, Shetai kaukubali uhuru huo kiana na kama kawaida yake kapenyeza “Uhuru usio na mipaka wala hofu ya Mungu!” Na kupelekea, wengine wakifungua makanisa kwa majina yao na kujijaza utukufu, bila kujua kuwa shetani amebadili nia ya Mungu iliyokuwa imewekwa, katika hayo matokeo ya watu wachache waliojitoa mhanga bila kuogopa ushindani au kuwatakia mabaya washindani wao, ndipo Demokrasia ya kuadu Mungu wa kweli. Na Shetani akalet Demokrasia yake ya uongo. Kutojiamini kunatokana na watu kutojua wapo upande upi, wenyenguvu au dhaifu? Hicho ndicho shetani hufanya,kuwatia watu mashaka na kutojiamini, ili wasikubaliwe na Mungu mwenyezi, maana Neno husema, Mungu hanahaja na mwenyekusitasita (mwenye mahaka) Shetani kwa kuwa ni Baba wa Uongo,huubadili ukweli na kuwa uongo,na kwa pupa na kutokuwa na uvumilivu kwa sisi wanadamu hujikuta tumeukubali uungo wake na kuukataa ukweli wa Mungu. Na hivyo kuvumiliana huondola, tunalaumiana na kutishana, shetani hufanya hivyo kuuficha ukweli, maana watu wasioaminiana hawawezi “BAHARINI WAKIZAMA!” Kama ujuavyo mara zote uongo, huwa mtamu masikioni mwa watu na ni rahisi kutekelezeka kuliko ulivyo ukweli, ambao haufurahishi sana masikioni na ni mgumu kuutekeleza! Kwakuwa shetani anajua wandamu ni wavivu,na si wavumilivu hujipenyeza kwa kutia fitina ili kuukimbiza ukweli! Lakini kama Neno lisemavyo “Ukweli utasimama siku zote!” Karibu sana ila TUVUMILIANE Kwa jina la Yesu Kristo – Amina.

 17. Mpendwa Mr. Millinga na woote,

  Shalooomu!

  Naona una shauku kubwa ya kuvijua vigezo vya kuwatambua Manabii wa Uongo na watumishi wengine wasiotumwa na Bwana. Ukiliamini Neno la Mungu kwa kile linachokifundisha pale linaponena, hilo ndilo Roho na Uzima, kama walivyokuambia ndugu zangu Kinyau na Orbi, liamini hilo kwanza, kama wajibu wako, halafu Mungu pia atatimiza wajibu wake kwa kukupa Roho wake atakayekuongoza zaidi katika Maandiko yake. Manabii wa Uongo hawana nguvu ya kulivuka Neno la Mungu, isipokuwa wanautegemea sana udhaifu wetu wa kuliamini Neno la Mungu na kulibishia kwetu!

  Ukitaka kumpima “Nabii huyu Mrudisha Nyota Zilizoibiwa”; nenda katika post ya “Ni ipi kazi ya Manabii” huko utayakuta mambo hayo na vigezo vya kuanzia, nadhani vinazidi hivyo kumi ulivyovitaka. Baada ya hapo unaweza kuamua kwenda kurudishiwa nyota yako au kumtafuta Mungu kwa staili nyingine ili akutimizie haja yako!

  Mbarikiwe nyoote katika Bwana mwenye Upendo nasi!

  Ck Lwembe

 18. Ndugu Mgwesa,

  Orbi amekujibu vizuri sana tena kwa kifupi. Lakini kama nisemavyo siku zote, biblia ina majibu ya kila kitu mtu anachokihitaji kukijua, ni uvivu wetu wa kuisoma na kujiweka chini ya Mwalimu Mkuu yaani Roho Mtakatifu ili atufundishe na kutufunulia kile anachotaka tukijue kutoka kwenye maandiko yake.

  Kwa mfano hilo swala la wachungaji na manabii wa uongo limeandikwa vizuri sana kwenye kitabu cha Yeremia sura yote ya 23. Lakini pia Bwana wetu Yesu Kristo alionya pia juu ya wachungaji ambao kazi yao kubwa ni kutawanya kundi la kondoo wala sio kuwachunga. Na haya tumeyaona mara nyingi sana yakitokea kwenye makusanyiko yetu, tumewaona wachungaji na maaskofu wengi ambao kwa kweli wamekuwa vikwazo vikubwa kwa kondoo wao na hasa hasa kwenye eneo la mapato na matumizi ya fedha za makusanyiko hayo.

  Leo hii si ajabu kuona wachungaji kwa wachungaji wanashitakiana mahakamani kwa ama kugombea madaraka au uonevu mwingine wowote. Wakati ninaandika haya, ninamjua mchungaji mmoja ambaye alimfukuza kazi mwinjilisti mmoja bila kufuata hata taratibu walizojiwekea wao wenyewe. Mwinjilisti huyo alipopeleka shauri lake Ofisi ya Kazi, akashinda shauri hilo na kuamuriwa kurudishwa kazini, lakini mchungaji huyo kwa kushirikiana na Askofu wake wakakataa amri halali ya mahakama na badala yake wakampa notice ya kumwachisha kazi na kumlipa mishahara yake ya mwaka mmoja. Sasa Mwinjilisti huyo amemfungulia Mchungaji huyo kesi mahakama kuu ya madai ya kuchafuliwa jina lake kwamba alipokea rushwa ya shilingi elfu kumi kama msingi wa kufukuzwa kwake kazi. Na bahati mbaya sana Mchungaji huyu hakuvishirikisha halali vinavyohusika na maswala ya rushwa kama PCCB. Watumishi hawa kuanzia Mwinjilisti, Mchungaji mpaka Askofu wao wamesahau kabisa jinsi Mungu alivyotuelekeza kupitia kwa Mtume Paulo namna ya kutunza mashauri yetu na kutopeleka mashauri hayo mahakamani. Ukipenda kujua hili soma 1 Korintho 6:1-8.

  Nimelieleza hili ambalo ninalijua, lakini yako mengi yanayotendeka kwenye makusanyiko yetu kwa sababu tu wachungaji wengi siku hizi ni wachungaji wa mishahara wala si wachungaji wa roho za watu. Wengi wao wapo kwenye huduma hii kwa ajili ya maslahi yao na wala si kwa ajili ya kumzalia Mungu matunda. Wote hawa nao ni manabii wa uongo tu kama Orbi alivyosema.

  Mungu aendelee kukupa baraka zake ndugu yetu Mgwesa.

 19. Mgwesa,

  Vyote ni sawa tu Biblia inatuonya na wote…….yoyote anayefundisha kinyume na maneno ya Mungu awe mchungaji, mwalimu, askofu maadamu anafundishi uongo hutakosea ukimwita Nabii wa Uongo……

 20. kwa nini watu wamekomaa katika manabii wa uongo. Inamaana hakuna wachungaji, maaskofu, waalimu, wainjiristi na wengine wa uongo?

 21. Millinga,

  Kwangu mimi ndugu Kinyau kamaliza yote…! Na unapotaka tutoe vigezo kumi vya kuwatambua manabii wa uongo unadhani unaweza…? Manabii wa uongo huja kwa sura nyingi na mbali mbali….Kigezo cha kumtambua huyu hakiwezi kuwa cha kumtambua yule….! Hivyo kila leo tutapima KILA AINA YA MAFUNDISHO AU MAFUNUO KWA KUTUMIA NENO LA MUNGU TU!

  Kwangu mimi mafunuo ya Malisa kuhusu nyota ni kinyume cha maneno ya Mungu…..! Sijasema ni Nabii wa Uongo bali natoa tahadhari tena kubwa kwa wapendwa…! Kwani chachu kidogo ya mafundisho huchachua donge zima…..! Anachofundisha Hakijabebwa na mafundisho ya Yesu na Mitume wake….kwa kifupi kinakwenda kinyume na mafundisho ya Biblia…..!

 22. Mpendwa ndugu Milinga,

  Ahsante kwa maoni yako ambayo inaonekana umeyawasilisha kwa nguvu kubwa sana bila sababu yoyote.

  Kabla sijasema chochote naomba urudie tena post yangu ya jana ili uniambie kama kuna mahali popote ambapo mimi nimeandika kwamba Malisa ni nabii wa uongo. Nilichokizungumza mimi ni juu ya vigezo vyako ulivyovianisha kama ndio njia ya kuwatambua manabii wa uongo. Vigezo hivyo ndugu Milinga ni vyepesi mno ukiviweka kwenye mizani ya Neno la Mungu. Kama manabii wa uongo wangetambulikana kwa vigezo hivyo ulivyovisema, basi kwa hakika hakuna ambaye angedanganywa na kupotoshwa kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyotutahadharisha. Hiyo ndiyo ilikuwa hoja yangu kuu. Sasa nakushangaa kweli kweli kuniona kwamba namhukumu Malisa bila kwenda kumhoji.

  Hata hivyo hiki kigezo cha kumhoji kila mhubiri ndipo ujue kwamba ni nabii wa kweli au wa uongo unakipata wapi katika maandiko ndugu Milinga? Hata katika hali ya kawaida isiyohusisha imani, si lazima uhojianae na mtu ana kwa ana ndipo ujue huyu anasema kweli au anasema uongo, sembuse kwa mambo ya Mungu ambayo msingi wake mkuu ni Neno lake, mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho ya Mitume? Hapo ndipo tulipojengwa wale wote tunaomwamini Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wetu.

  Vigezo vyote vya kumjua nabii wa uongo na wa kweli vipo kwenye maandiko (Neno La Mungu). Orbi amekupa mfano mmoja wa yule kijakazi aliyekuwa na pepo la uaguzi kwenye Matendo 16:16-18. Angalia, huyu binti alikuwa akifanya mambo mengi yaliyokuwa kinyume kabisa na neno la Mungu kwa siri kubwa bila wapendwa waliokuwa naye kujua mpaka Paulo alipotembelea mahali hapo. Hata maneno aliyokuwa anaongea kuhusu akina Paulo yalikuwa ya kweli kabisa kwenye masikio ya wapendwa wengi, lakini alikuwa pepo na biblia inasema kwamba alifanya hivyo kwa siku nyingi na wapendwa wa eneo hilo walijua kwamba huyo ni mwenzao na ni mtumishi mwenzao. Nadhani hata wewe Milinga ungekuwa mahali hapo ungesema hakika huyo dada amejazwa na nguvu ya Roho Mtakatifu mpaka kuwaona akina Paulo kwamba ni watumishi wa Mungu aliye juu! Hakika alijua hilo huyo dada kwa sababu yeye alikuwa mtumishi wa mungu aliye chini!!!

  Ukitaka ku-connect vizuri juu ya kijakazi huyu, hebu kasome kitabu cha Ufunuo wa Yohana 2:18-21, utamuona kijakazi huyu alikuwa kwenye kanisa la Thiatira, na Mungu analiambia kanisa hili kwamba kwa muda mrefu lilimridhia mwanamke Yezebeli anayejiita nabii kuwa miongoni mwao bila wao kutambua; lakini mwanamke huyu anawafundisha na kuwapotosha watumishi wa Mungu ili wafanye uasherati. Maana yake ni kwamba mwanamke huyu alikuwa amebeba roho ya Yezebeli, na wote tuanajua roho ya Yezebeli inafanya kazi kubwa kwenye eneo la UASHERATI NA UZINZI.

  Unapoona biblia inasema kanisa, maana yake ni watu waliookoka, lakini bado wamechangamana na hao manabii wa uongo waliobeba roho ya Yezebeli. Ndio sababu siku hizi si ajabu kusikia watumishi wa Mungu wakizini ovyo ovyo na waumini wao kwa sababu miongoni mwao wapo vijakazi wanatabiri na kutoa unabii lakini bado wamebeba roho za Yezebeli na kuzisambaza ndani ya watumishi wa Mungu (Waumini, wachungaji, Waiinjilisti, Maaskofu n.k.).

  Ukisoma tena hapo hapo kwenye Ufunuo sura hiyo hiyo ya pili utakuta Yesu analizungumza Kanisa la Pergamo. Kama nilivyosema hapo juu kanisa maana yake watu waliokoka, lakini kanisa hili la Pergamo lilikuwa linaishi mahali ambapo Shetani ana kiti chake cha enzi. Kiti cha enzi maana yake nini? Maana yake ndicho kilichokuwa kinatawala hali ya kiroho ya eneo hilo, kwa hiyo ina maana mnaweza kuwa mpo kwenye kusanyiko ambalo lipo chini ya kiti cha enzi cha Shetani. Ili kiti hiki cha enzi kiweze kufanya kazi yake sawa sawa, lazima kiwe na watu miongoni mwenu wanatekeleza matakwa ya kiti hiki, na watu hao wanaweza kuwa ni manabii, mitume n.k.

  Na ndani ya lile kanisa kulikuwa na mafundisho ya Balaamu ambaye alimfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi. Ndani ya kanisa hilo pia kulikuwa na watu washikao mafundisho ya Wanikolai. Alipoinuka Antipas kama shahidi mwaminifu wa Mungu, akauawa mara moja. Hivyo ndivyo vigezo anavyotumia Shetani kujipenyeza katikati ya watu ambao kwa midomo yao wanasema na kushangilia ‘Bwana Yesu asifiwe’ lakini nyuma yao kuna agenda nyingine kabisa. Sasa watu hao huwezi kuwatambua kwa vigezo vyako ndugu Milinga ulivyovianisha hapo juu.

  Hebu angalia pia kilichoandikwa kwenye kitabu cha Yuda 1:4 kwamba;
  “Kwa kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri katikati yenu (Kanisa), watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, waovu wapotoshao neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi wakimkana Yeye aliye Bwana wetu wa pekee, Bwana Yesu Kristo”
  Ukisoma huu mstari unaweza ukafikiri kwamba watu hawa wanamkana Bwana Wetu Yesu Kristo wazi wazi, lakini msingi wa mstari huu umejengwa kwenye neno, “waliojipenyeza kwa siri”. Kwa hiyo kama watu hawa wamejipenyeza kwa siri, basi hata operation yao itakuwa ya siri sana kwenye kanisa hilo mpaka ‘watakapokuja au watakapotokea akina Paulo’ kwenye kanisa hilo ndipo watakapomgundua au wagundua hawa vijakazi wenye pepo la uaguzi pamoja na kwamba wanatoa unabii na utabiri unaonekana machoni na kusikika masikioni mwa watu kuwa ni wa kweli.

  Kwa maana hiyo ndugu Milinga kigezo kikubwa na cha pekee katika kuwatambua manabii wa uongo na wa kweli ni kuwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu katika kila kitu na kujiweka chini ya kioo cha Neno la Mungu. Kwa vigezo ulivyovitaja wewe Milinga kamwe hutamtambua nabii wa uongo hata siku, badala yake utawaona wote ni kweli kwa sababu hutawasikia hata siku moja wakikuambia usiokoke na hutawaona hata siku moja wakiacha kutumia jina la Yesu na ndio sababu Yesu akatupa warning kwamba sio wote watakaomwita Bwana, Bwana wataokoka au watakuwa wameokoka, wengi watataja jina hilo midomoni mwao tu lakini mioyo yao iko mbali sana Naye!

  Kwa hiyo ndugu yangu Milinga unapotutaka tukupe vigezo visivyopungua kumi, sikuelewi unataka vigezo hivyo tuvitoe wapi zaidi ya hivi ambavyo neno la Mungu limeviweka wazi mbele yetu kwamba siku hizi za mwisho watakuwepo manabii wengi sana wa uongo, ili kuwatambua kipimo pekee ni neno linasemaje na hiki ndicho kipimo cha uhakika maana Neno ni Mungu mwenyewe. Sasa kama Mungu mwenyewe amekujulisha kuwa huyu ni wa uongo na huyu ni wa kweli, je unataka vigezo gani vingine?

  Hivi unafikiri Paulo alimtambuaje pepo aliyekuwa ndani ya yule kijakazi kama sio Roho Mtakatifu alimfunulia hapo hapo? Kama ndivyo kwa nini wewe unataka tuwatambue watu hawa kwa vigezo vyako ambavyo kwa hakika havina mashiko ya Neno la Mungu? Nabii gani wa uongo atakayesimama mbele yako Milinga halafu aanze kukwambia kwamba hajafunuliwa na Mungu? Nikimuona nabii wa namna hiyo, hakika nitaunga mkono vigezo vyako vyote ulivyovibainisha hapo juu.

  Halafu umenishangaza pia kwa point yako kwamba wana habari wa Uwazi walienda kwa Kakobe na kutafuta hilo sijui fuvu lililotoka Nigeria. Hivi ni kweli ndugu yangu Milinga unataka kutuambia kwamba uchawi unagunduliwa kwa namna hiyo? Uchawi ni nguvu ya kiroho ya upande wa ufalme wa giza, utaonekana na kugundulika kwa nguvu ya kiroho ya ufalme wa Nuru, fullstop! Kwa macho haya ya kawaida huwezi kuuona uchawi la sivyo uwe initiated na kuwa mmoja wao, lakini kwa macho ya rohoni ya ufalme wa Nuru unaonekana. Kama uchawi ungekuwa unaonekana kwa macho haya ya nyama na kwa namna ambayo wewe umeieleza hapo juu, basi wachawi wote tunaoishi nao mitaani wangejulikana kwa kila mtu. Ni wale tu walio na macho ya rohoni ya ufalme wa Nuru, ndio huweza kufunuliwa na kuwaona wachawi wazi wazi.

  Mungu akubariki sana ili tuendelee kulitumia Neno la Mungu kama kigezo pekee cha kuwatambua manabii wa uongo na manabii wa kweli.

  Sijaongea kuhusu ‘walokole’ walivyokuwa wakionekana hapo nyuma kwenye makanisa uliyoyataja. Lakini kwa kifupi ni kwamba tangu mwanzo wa kanisa, watu wengine waliwaona hao waliojazwa na nguvu ya Roho Mtakatifu kama watu waliopagawa na kumbuka siku ile ya Pentekoste, watu walipowaona akina Petro na wanafunzi wenzake wakisema kwa lugha mbali mbali, wakasema kwamba wamelewa kwa mvinyo (Matendo 2:13). Kwa hiyo kudharauliwa kwa ‘walokole’ kama unavyowaita wewe, hakujaanza kwenye kizazi chetu, jambo hili limetokea tangu mwanzo wa kanisa toka karne nyingi zilizopita na litaendelea kutokea mpaka Kristo atakapokuja kulichukua Kanisa lake. Kwa hao unaowaita ‘walokole’ huko kudharauliwa namna hiyo ndio nguvu yetu ya kusonga mbele!!

  Baraka nyingi kwako ndugu Millinga.

 23. Wapendwa Orb na Kinyau,

  Tatizo lenu ni kwamba mwaeleza watu wajihadhari na manabii wa uongo bila kueleza ni jinsi gani unavyoweza kuelewa fulani ni nabii wa uongo. Mimi nimetaja baadhi tu ya vigezzo ninavyoweza kutumia kumpima mtu. Nilitarajia nanyi pia mngetaja vingine badala ya maelezo marefu yasiyoeleza jambo mahsusi la kutumia kumtambua nabii wa uongo (you not mentioned specific ways/reasons of recognising false prophets). Mimi naomba watu waache kutoa mifano ya jumla tu.

  Eleza wasomaji ni vigezo gani wanavyopaswa kutumia kuwabaini manabii wa uongo zaidi ya kule kujua kwamba Yesu alisema ishara hizi zitafuatana nao waaminio…….. watafanya hivi…. itatokea hivi…….

  Hivi walokole mwaelewa kwamba Kanisa Katholiki haliwayamini makanisa ya walokole? Unaelewa kwamba kanisa linaamini kwamba walokole wamepotea? Mwaelewa kwamba hata walokole Kanisa katholiki na Warutheri au Waanglikana wameanza tu majuzi kuwakubali kwamba nanyi ni makanisa. Unaelewa kwamba miaka kadhaa iliyopita walokole wote waliitwa manabii wa uongo? Hadi sasa kuna baadhi ya wakatholiki ukiacha ngazi za juu wakati mwingine hata Maaskofu wao wanaamini Walokole ni manabii wa uongo waliotabiriwa na Yesu kwa sababu tu wanaombea watu na kutoa pepo na watu wanapona? Kinyau na Orbi hayo mwayaelewa? Mwaweza kujibu hooja hizo? Kwamba wawezaje kuwahakikishia wakatholiki, waanglikana na warutheri kwamba Maaskofu wa makanisa ya kilokole siyo manabii wa uongo?

  Wakati Askofu Kakobe ameanza huduma yake ya Maombezi na akawa gumzo jijini Dar es salaam, Walokole wote walikuja kinyume naye? Wakisema anatumia uchawi alioutoa Nigeria kwa TB Joshua wa kanisa la SCOAN. Leo hii wote wamekaa kimya hawasemi lolote tena kumhusu Mzee Kakobe? Miaka ile mimi nakumbuka mpaka nilitengwa na jamii ya walokole wenzangu kwa kuwapinga wote waliokuwa wanamsema vibaya Mzee Kakobe. Nilitengwa kabisa kanisani nisionekane kwa sababu tu nilikubaliana na mafundisho na msimamo wa baadhi ya mafundisho ya Kakobe.

  Watanzania wengi ni wasahaulifu sana. Tunasahau tulikotoka mapema. Tunasahau historia ya kanisa (Walokole) Tanzania mapema. Huku Mzee Moses Kulola akibariki wanawake kujipamba kwa nywele bandia na kukalikiti nywele Walokole wenzake wote walikuwa kinyume na mafundisho yale. Lakini leo nenda makanisa yote ya walokole, kama mwanamke hajavaa urembo na mapambo mengine mengi kichwani ikiwemo nywele bandia uniambie. Hivi leo mtu akisema walokole ni manabii wa uongo kwa kuzingatia hoja hizo walokole watajiteteaje? Tofauti ya Mlokole na Msabato asiyekubali kuvaa nywele bandia ni ipi?

  Swala lingine linaloweza kuwafanya walokole wote waonekane ni matapeli na manabii wa uongo ni swala la migawanyiko na mifarakano ya kila siku makanisani mwao. Kesi kibao mahakamani wakishitakiana, migawanyiko kibao, nk. Utaachaje kusema kuwa nasi walokole ni manabii wa Uongo?

  Kama Huyu Kijana BG Malisa wa Mwanza ni nabii wa uongo kwa sababu ya kusema atarudisha Nyota za watu zilizoibwa na Shetani kama hoja kuu ni hiyo na ndiyo inawafanya watu wasimwamini kuwa ni mtumishi halali katika shamba la Bwana, basi hapa Tanzania hatuna watumishi wa kweli kwa sababu kila mtumishi amekuwa na historia ya kutiliwa shaka na wenzake katika baadhi ya mafundisho yake au misimamo yake kuhusu maswala kadhaa ya Maandiko na mahubiri au matendo yake.

  Mwanzoni nilipendekeza kwamba natamani nipate watu kama akina Kinyau na Orbi waliokwenda kumhoji Mtuhumiwa kabla ya kumhukumu. Hivi kuna watu wamewahi kwenda kwa Mzee Kakobe kumhoji kuhusu tuhuma zake za kwamba anatumia uchawi kuponya watu wenye matatizo naa magonjwa? Mbona waandishi wa habari wa magazeti ya UWAZI wao walikwenda wakamhoji akawatembeza kanisani kote mpaka madhabahuni wakajionea na wakakosa hilo fuvu la kichwa lilosemwa kwamba lilikuwepo?

  Orbi na Kinyau na wengineo wenye msimamo kama ninyi mnashindwaje kwenda kwa BG Malisa pale Michungwani Mwanza mkajionee au mkafanye mahojiano na huyo nabii anayetyhumiwa kuwa wa uongo? Woga uko wapi? Tatizo ni nini hadi wapendwa wengi wamhukumu mtu kabla ya kwenda kufanya uchunguzi wewe binafsi? Kwa nini unatoa msimamo bila kuufanyia utafiti?

  Mwisho nawaomba mnitajie vigezo visivyopungua 10 mnavyotumia kutoa misimamo ya kwamba huyu au yule amevaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni Mbwa mwitu? Unajuaje kwamba ndani ni mbwamwitu wakati hajaanza kurarua kondoo? Yule Kibwetere wa Uganda alijulikana kuwa ni mbwamwitu baada ya kurarua kondoo. Je hawa walioko Tanzania wameshararua kondoo hadi tuwahukumu? Mimi nilidhania kwamba tunasubiri mwisho wao na siyo mwanzo wao?

  Hebu nawaomba mnitajie vigezo mnavyotumia angalau visipungue 10 kama mimi nilivyojaribu kuanisha vigezo ninavyotumia kumhukumu mhubiri yeyote ili niseme ni nabii wa kweli au wa uongo.
  Karibuni.

 24. Sasa ndugu zangu mambo Mengine usisikilize maneno ya watu. Mtumishi wa kweli au wa uongo hatambuliki kwa shuhuda za kutunga za watu au ushaidi. Biblia inasema ….”kama ni watumishi wa uongo, waacheni tuone mwisho wao. Mungu hatetewi. Huyo bishop Mpemba na shosti wake raymond wa redio mlio itaja hapi juu. Kama wenye ni wa kweli watuoneshe coz maandio yanasema kwa ishara hizo zitawafata wale waaminio. Na kama wenyewe ni wa ukweli ilikuwaje kuja kwenye mkutano wa nabii malisa mwaka jana 2011 nakuanza kurusha mawe(mch. raymond alirusha mawe na askofu mpemba alimsubiri kwa mbali kama likinuka amchukue na gari lake wakimbie tukio hilo lilitokeA MNAMO Tarehe 9.9.2011 saa 11.36 jioni(Nimetaja tukio hili coz hata mimi nilikuwa mwandishi wa habari na video clip ambazo mchungaji huyo akiwa anakimbizwa na watu pamoja na usalama wa taifa uliokuwa pale kisha akatokomea katika gari la mpemba ninazo. Je kama kweli wenyewe ni wa ukweli na wanafuata nyayo za Yesu watuonyeshe wapi Yesu alirusha mawe au alisema kuwa rusheni mawe. Ninayo mengi sana walio tenda huku Mwanza. Tena nikiongelea swala la Mali za mpemba na nabii malisa wanavyo tumia utasema mpemba ni tapeli na sio nabii wa uongo yaani yeye ni ajenti kabisa. Yote haya nimeyaondea ili kuwaasa watu kuwa tusipende kufuata isia za watu tutapotea. Manabii wa uongo wapo na wataendelea kuwepo. Ebu angalia Nabii malisa alifanya kitendo kimoja mpaka nikasema huyu ameitwa na Mungu. Fikilia wewe leo nikikutukana utakasilika na kushindwa kula, lakini yeye katukanwa na askofu huyu maneno machafu kwa muda wa mwaka mzima na hajajibu hata moja. Nadhani wadau wote wa kipindi cha saa ya ukombozi ni mashaidi hajawahi tukana mtu. Na kwa kuongezea amekua mtu anaye sisitiza sana kwa ajili ya watu kuokoka zaidi ya wahubiri wote wanao hubiri kwenye vyombo vya habari(www.nyumbanileo.blogspot.com) Ngoja kwa leo niishie hapo. Ipo siku nitawapa siri zilizo mfanya askofu mpemba kumtukana Nabii Malisa. Mpaka utacheka ni Utoto mtupu.

 25. Asante sana ndugu Kinyau,

  Aliyoyasema Millinga ni kinyume mno na Maandiko…..na hii ndio inayowapoteza wengi leo, maana utasikia mbona watu wanaponywa……..mbona mapepo yanatolewa….mbona miujiza inatendeka…..mbona watu wanaokoka….! (bila kujua anayejua kabisa kuwa nani kaokoka ni Mungu mwenyewe licha ya ukiri wetu……ambao wakati mwingine ni wa mdomoni tu ambao umesababishwa na sensationalism/emotions lakini moyoni hakuna mabadiliko yoyote).

  Kazi ya Mungu haiiangaliwi kwa miujiza tu……au wingi wa watu……ukubwa wa huduma….au Jina la Yesu linapotamkwa..! Kumbuka Paulo alimtoa pepo yule Kijakazi ambaye alikuwa muaguzi ambaye alitamka mambo ya Kweli kabisa kuhusu Paulo….lakini Paulo alijua amepagawa…..!

  Mafundisho ya Yesu na Mitume wake ni mhimili wa Imani hii….hatujaona Yesu na Mitume wakifundisha Nyota ya muumini kuchukuliwa…..Waamini wa leo wamepata mafundisho potofu kuwa mateso na shida si sehemu yao katika maisha haya ya kitambo…..hivyo kila wanapopitia adha katika na mateso wanapewa mafundisho haya potofu…..mara nyota yako imechafuka………una laana….mkosi balaa…….nk……Jamani hebu tufute vumbi Biblia zetu…….na tuusome ujumbe wake kama ulivyo….tusianze kutafuta “nyota” “mafanikio” Hebu katika kulisoma Neno la Mungu tupate kumwona Yesu kama msingi wa Maandiko na Wokovu wake ambayo unaanza katika maisha haya….na utafikia hitimisho wakati tumekizunguka kiti cha Enzi……adha….shida……mateso….ni sehemu yetu pia kama itamtelea Mungu utukufu…..Sio Kwamba Nyota imechafuka……! Mbarikiwe…!

 26. Mpendwa ndugu yangu Milinga,
  Nimesoma post yako ya leo tarehe 18 April, ikaniacha hoi kabisa!!

  Hivi ni kweli kabisa katika kuwabaini watu ambao wanatumia maandiko ya Mungu na Jina la Yesu vibaya, utajibana kwenye haya uliyoyaeleza hapo juu?

  Tahadhari ilitolewa mapema kabisa na Bwana wetu Yesu Kristo kwamba watakaowapoteza wateule wake hawatakuja kiwazi namna hiyo kama wewe Milinga unavyotaka kutuaminisha. Watakuja wakiwa wamejificha sana kwenye mavazi ya kondoo na kutumia jina hili hili la Yesu, lakini nyuma yake kuna agenda zao za siri.

  Hakuna vita iliyo rahisi kuishinda kama ya kupigana na adui yako anayekuja wazi wazi, na pia vita ngumu sana kuishinda ni ile unayopigana na adui ambaye unamuona kama rafiki yako! Shetani naye ni mjanja sana anajua kuwa akiwajia wakristo wazi wazi namna hiyo lazima atapigwa mara moja! Hivyo ili kuwateka na kuwangusha wengi, lazima aje kama malaika wa nuru.

  Miaka ya nyuma tulisikia sana habari ya mtu mmoja aliyekuwa anaitwa Kibwetere huko Uganda. Ndugu huyu alihubiri na kutabiri kila kitu kwa Jina la Yesu kiasi kwamba waumini wake wakamwamini kwa asilimia mia moja na matokeo yake tuliyasikia wote. Kama angekuja wazi wazi kama ambavyo ndugu Milinga umetuonyesha hapo juu, hakika asingepata hata mtu mmoja wa kumwangamiza.

  Neno la Mungu limehakikiwa na ni amini na kweli, halitatanguka milele. Kama Yesu alisema watakuja wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu wakali, uwe na uhakika kwamba hilo linatokea sasa na litaendelea kutokea. Kama Yesu alisema watakuja wengi kwa jina lake na kuwapoteza hata wateule, uwe na uhakika hata sasa kuna mahali Jina la Yesu linatumika visivyo ili kuwa kama kichaka chao cha kuficha mambo yao. Hebu soma hiki kilichoandikwa kwenye Injili ya Marko 13:22-23,

  “Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watafanya ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana hata wale wateule. Hivyo jihadharini, nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia”

  Kwa hiyo ndugu yangu Milinga ni muhimu sana kuchukua hatua juu ya tahadhari hii ambayo Bwana wetu Yesu Kristo alitutahadharisha mapema kabisa kwamba watakuja wengi wakidhaniwa kuwa ni watumishi wa kweli kumbe ni watumishi wa kambi ya adui.

  Mungu atubariki ili tuendelee kuwapima watumishi wote kwa kipimo pekee cha maandiko na wala si tu kwa ishara na miujiza wanayoifanya.

 27. Ndugu Millinga,

  Napenda kutoautiana na wewe kwa sababu moja tu, Yesu alisema kwamba atakayekuja kuwapoteza Wateule hatakuja kwa jinsi hiyo iliyo wazi namna hiyo…..Hebu rudia mafundisho ya Yesu tena….

  – Jihadharini na manabii wa Uongo wanaowajia wamevaa mavazi ya Kondoo….lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali……Ina maana kwa nje mafundisho yao na kila kitu kitaonekana ni safi…….lakini ndani kuna kitu kingine kabisa……..

  – Wengi watakuja kwa Jina Langu….! Nakudanganya wengi…..!Hawatakuja na jina jingine au mafundisho ambayo kwa nje yataonyesha ni mapotofu……! La hasha…….

  Je utasemaje kuhusu Paulo…..Yeye alisema wazi kuwa hujigeuza na kuwa mfano wa Nuru…….

  Mafundisho potofu lengo ni kukutoa Kwa Kristo……..si lazima yakuambie ukazini……ukaibe…..usiishi maisha matakatifu……..Soma kitabu cha Wagalatia……waliambiwa wanafuata Injili Nyingine, Yesu Mwingine si kwamba walifundishwa wasiwe watakatifu…..La hasha……! Mafundisho potofu yanakuja kwa njia nyingi mno lakini hatimaye taratibu hukutoa katika Injili ya Kristo…na haya ndio mabaya zaidi…! Mafundisho aliyopamba nayo Paulo na Mitume yalikuwa yanaongeza kitu kingine KIZURI TU JUU YA INJILI……! SHERIA…..ZA MUSA ! lakini Paulo na Mitume walipinga…..kwa sababu walijua madhara yake….kwamba hatimaye Kwa kuziingiza Sheria za Musa na kuzichanganya na INJILI utaondoa tumaini kwa Kristo……! Hivyo kusema kwamba mtu hasemi ukaibe……au usiwe mwasharati basi kabeba Injili ya Kristo inapingwa na hoja nyingi katika Matendo ya Mitume na Nyaraka za Paulo….

  Ndio haya mafundisho ya NYOTA…….taratibu kwa njia ya kujificha katika INJILI watu wataondoka katika kumtumaini Roho Mtakatifu……..!

  Hata kama unatetea kuwa hiyo ni lugha tu ya kuwavuta watu….kwa nini uitumie…..kwa nini usiseme tu kuna mkutano wa Injili…na nafasi itatatolewa ya kuombea wenye shida….! Kwa nini utumie lugha ya Sheikh Yahya na Professor Vulata au Maji Marefu…..?

 28. Wapendwa wengi hubabaishwa na lugha. Ukitaka kuwa muhubiri maarufu lazima ujue kucheza na lugha. Malisa anajua hilo. Wahubiri wote waliofanikiwa kuvuta maelfu akiwemo Yesu Kristo walijua kucheza na lugha (language twisting and playing with different words meaning the samething).

  Swala la Nyota ya mtu mbona ni somo simple tu. Mhubiri huyu akisema atakuombea ili NYOTA YAKO ILIYOIBIWA IRUDI hana tofauti na Mhubiri atakayesema atakuombea “maombi ya deliverance”. Wengine husema, kufunguliwa kutoka katika laana, wahubiri wengine utawasikia wakisema, kurudishiwa “karama” yako. Wengine hutumia neno “TALANTA” yako. Wengine husema “Kipawa chako kilichoibiwa na Shetani”. Wengine “Upako wa Utajiri”. Wengine hutumia neno “Mibaraka toka pande nne za dunia”. Wengine hutumia neno, “Kubarikiwa”. nakadhalika nakadhalika. Yote hayo ni NYOTA ya mtu. Katika ulimwengu wa roho, shetani anachokiona kwa mtu aliyeokoka ni NYOTA. cHOCHOTE ulichonacho “chema” kinachofanya maisha yako yaweze kuonekana yako juu, hiyo ni “nyota” yaani unag’aa gizani kama nyota zinavyong’aa usiku angani. Nyota ni mafanikio. Nyota ni “Talent”. Ni kipawa tupewacho na Mungu. Nyota yaweza kuwa lolote unalopaswa kulipata ili likutofautishe kutoka katika kundi la watu wengine. Watu huwa na “nyota” tofauti kama ilivyo angani kuna nyota zenye mwonekano tofauti. Nyota yaweza kuitwa kwa neno lingine, “Mkono wa Mungu juu yako” au “Neema ya Mungu”. Mariam aliambiwa, “Umebarikiwa kuliko wanawake wote….” maana yake alikuwa na “nyota” ya pekee aliyopewa na Mungu azae mwanae pekee duniani. Hiyo ndiyo maana ya nyota yako.

  Wapendwa waelewe kwamba “Somo la Nyota” katika mtazamo wa Maandiko ni tofauti sana na kule kwenda kutazama nyota kwa wachawi na waaguzi wapiga ramli. Nyota za watu wa Mungu siyo sawa na zile za kwenye magazeti au zile za bahati na sibu. Mhubiri awaye yote akija na mtazamo huo, huyo siyo mtumishi wa Bwana.

  Inashangaza watu wanapoona wahubiri fulani wanaohubiri kwa kutumia maneno ambayo hayajazoeleka, wanaanza kutiwa hofu na mashaka na kukataza watu wasiende kushiriki ibada hizo.

  Wahubiri ambao tunapaswa kuwaepuka ni hawa wenye kuendesha Ibada zifuatazo:

  1. Ibada ya kuabudu miti au vitu visivyokuwa na uhai.
  2. Ibada za kuabudu wafu au kwenda makaburini kuwaomba wafu
  3. Ibada za kutoa kafara ya wanyama au watu, epukana nazo.
  4. Ibada ya kumkana Yesu kuwa siyo mwana wa Mungu wala siyo Mungu
  5. Ibada zisizokubali kwamba Biblia ni maandiko matakatifu, epuka nazo
  6. Mhubiri asiyekemea dhambi hadharani na kwa kusisitiza sana.
  7. Mhubiri anayehubiri chuki za kijamii na kidini au kisiasa, epukana naye
  8. Muhubiri anayewataka watu wamwabudu yeye kutokana na miujiza au unabii wake anaotoa hata kama unabii huo unatimia. Epuka kabisaa
  9. Mhubiri asiyelitaja kabisa Jina pekee la Yesu Kristo anapohubiri, epuka
  10. Mhubiri anayefundisha watu kumwaasi Mungu badala ya kumcha Mungu
  11. Mhubiri asiyekubali kwamba Mungu yupo na anapaswa kuabudiwa yeye tu
  12. Mhubiri asiyehimiza watu kuwa watakatifu hapa duniani, epukana naye.

  Hayo ndiyo maeneo unayopaswa kuyatumia kabla ya kuhukumu kwamba Mhubiri fulani anahubiri uongo au anapotosha wafuasi wake.

  Hata kama (kama baadhi wanavyotaka dunia ielewe) Mhubiri fulani atakuwa anatumia uchawi kuvuta watu (kitu ambacho mimi huwa sikubali), kama ananielekeza kuishi maisha ya utakatifu, uchaji Mungu, na kumwabudu Mungu pekee, bado huyo Mhubiri, au Nabii, au Mtume vyovyote utakavyomwita mimi sitakuwa na tatizo naye.

  Kama kweli kuna uchawi unaoweza kuwatoa watu dhambini, wakaacha uzinzi, uasherati, ulevi, ufisadi, bangi, pombe, ukahaba, ufuska, ushoga, sigara, wizi, ujambazi, nk; kama kuna uchawi huo wa kuvuta watu wengi kwa Yesu wakatulia kabisa kwa Yesu bila kurudi nyuma, nadhani huo uchawi ni wa pekee sana. HATA MIMI NAUTAMANI NIUPATE NIUTUMIE KUVUTA MAELFU NA MAELFU KWENDA MBINGUNI. Kama shetani anawapa watu uchawi unaotumika kuvuruga ufalme wake yeye mwenyewe, basi shetani hana akili kabisaaa.

 29. Ndugu Millinga,

  Kwangu mimi sihitaji kununua CD/au kwenda kusilikiza mafundisho kama hayo ili kutoa uamuzi (HUKUMU) Biblia inaweza kutumiwa kufundisha chochote Kile…! Mafundisho ya kuchukuliwa nyota na kuzisafisha ni kuchukua mafundisho yaliyoko mtaani na kuyaunganisha na Maandiko kupata kusema unachotaka kusema….! Giving the Biblical texts your own meaning and understanding….!

  Inawezekana mafundisho ya Nyota kuchukuliwa yakafundishwa na wahubiri Mahiri ambayo wamejijengea majina katika Huduma Tanzania Leo…! Lakini hii haiondoa UKWELI WA MANENO YA MUNGU…..! Tuna Roho Mtakatifu anayeyaongoza Maisha ya Muumini……Tuna Neno la Mungu ambalo ni Taa ya Muumini…..!

  Waumini leo hawaongozwi tena na Maneno ya Mungu…..wamefungua mioyo yao kwa Watenda miujiza…….ambayo sana wamejenga hofu….na kutoa tafsri potofu ya Maandiko ili kuvuta Makundi makundi….Hebu angalia hofu ya Freemasons…! Hebu angalia hofu ya Misukule…..! Kila kitu hakiangaliwi tena Maandiko yanasema nini…bali Nabii/Mtume anasema nini….?

  Wakristo badala ya kuishi kwa kumtegemea Mungu….nao wanaamini katika bahati…..ngekewa……kismati…….NYOTA…..!! Haya yote ni matokea ya mafundisho ya Laana….na Injili za mafanikio kinyume na mafanikio yaliyoko katika wigo wa Maandiko.

  Maana kama umemfundisha Mkristo aliyeokoka ana LAANA…..Kwa nini usimfundishe pia Nyota yake inaweza kuchukuliwa…..?
  Injili nyingi Leo ni kinyume kabisa na Injili Ndani ya Biblia………watu hawaji Kwa Yesu kufanyika wana wa Mungu kwa kutubu dhambi….bali watapata nini toka Kwa Yesu……na zaidi ni baraka za mwili……na zisipotokea basi unaambiwa kafunguliwe….katolewe laana………karudishiwe Nyota yako…….!

  Kwa kifupi tu Kanisa la leo limekwama jangwani………linazunguka zunguka na halina mwelekeo…Tuliyaruhusu na kuyakimbilia mafundisho manyonge kutoka hizi hizi mimbari za makanisa ya Kiroho….! Na kutoka kwenye “watumishi wenye upako” bila hata kujua “upako” huo unatoka kwa nani…. na haya ndio matokeo yake……subirini hiyo siku na nendeni PTA kuuona umati wa watu wakienda kurudishiwa Nyota zao……..La kusikitisha ni kwamba Biblia itatumika……Jina la Yesu litatajwa…..”.Roho Mtakatifu” atazungumzwa…..Lakini ni Yesu yupi huyo…..? Ni Roho gani huyo….ambaye sasa anawarudishia waumini Nyota…..? Na ajabu ni kwamba wengi watatoka PTA na Shuhuda…….bila kujua ni shuhuda za kuzimu…….ambazo zitavuta hata watu wasio na kiu na Yesu aokoaye bali wanataka tu kusafishiwa Nyota wala sio kusafishwa roho zao na damu ya Yesu na kujiandaa kwa maisha yajayo…….!

 30. Nakumbuka kuliwahi kuwa na topic hapa kuhusu nyota, sikumbuki title yake lakini mwandishi alifanana sana huyu hapa chini…

  JINSI WACHAWI WANAVYOWEZA KUKUFUNGA USIFANIKIWE
  Posted by baba nyambo on December 14, 2010 at 5:36pm in Uncategorized
  View Discussions

  Salam wapendwa katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

  Leo nipo hapa kuwaletea topic mpya kabisa ambayo wachungaji wengi hawaifundishi makanisani na yamkini baadhi yao hawaijui.kama kichawa cha habari kinavyosema, leo nataka kuzungumza juu ya wachawi.kunawatu wengi sana Duniani wanalia kila wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini? nataka nikuambie leo, wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! hapa ni kwamba shetani huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. unajua kila mmoja wetu anakitu alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. ngoja nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani,soma mathayo 2:1-5.biblia inasema ‘Yesu alipozaliwa zamani za mfalme herode mamajusi wa mashariki walikwenda kumwona, na walipofika wakauliza yuko wapi aliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyita yake nasi tumekuja kumsujudia. Ukisikia mamajusi ujue si watu wema.kasome biblia ya kiingereza imesema ‘Astroggers’ yaani wabashiri au wanaanga. pia biblia ya NIV imesema Maggi, yaani washirikina, biblia nyinge imesema the Meggicians yaani wachawi.kwa tafsri hizi moja kwamoja tunatambua kwamba hawa mamajusi kuwa ni wachawi. Sasa rejea katika kauli yao walipofika kwa Yesu walisema “Yuko wapi waliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyota yake nasi tumekuja kumsujudia” mpendwa wangu sasa naomba ufungue akili yako ili Mungu akusaidie. watu hawa ni wachawi, lakini cha ajabu wanasema wameiona nyota ya Yesu wakajua ya kuwa aliyezaliwa ni mfalme. kwa hiyo tunajifunza kwamba kumbe wachawi wanauwezo wa kutazama katika ulimwengu wa roho na kutambua kwamba wewe unanyota gani katika maisha yako. si kwamba walikosea kwa yesu kusema kwamba Yesu ni mfalme walisema kweli kabisa rejea kauli za Bwana wetu alipokuwa kwa pilato aliulizwa wewe ndiye mfalme wa wayahudi hakukataa bali alijibu wewe wasema.pia akaongeza kusema kwamba ufalme wangu si dunia hii. kwa hiyo ni mfalme. pia ukirejea katika Isaya 9:6 biblia inasema “na uweza wakifalme utakuwa mabegani mwake” Hivyo basi wachawi wakishatazama katikaulimwengu wa roho na kuona nyota yako kuwa ni ya kifalme kama ya Yesus au labda nyota yako ni Biashara, au Elimu, au Ajira,nak. wanachokifanya ni kwamba wanaiba ile nyota na kuiweka kwa mtu mwingine au wakaiacha tu.

  kuna dalili za kutambua nyota yako ni ipi hasa ni rahisi sana kutambua nyota ya mtoto mdogo. kwa mfano: mtoto akiwa na nyota ya uongozi,utambua hivi watafute wanapokuwa wanacheza watoto wengi kwa pamoja, kisha angalia vizuri kaa utulie usipige kelele kisha uangalie vizuri ni lazima atakuwepo mtot atakayewadhibiti wenzake na kuwalazimisha kufanya anavyotaka yeye na lazima watafanya, kwamfano anawezakusema nyamazeni na wote kweli wakanyamaza, au twendeni na wote kweli wakamfuata.

  Pia dalili za kutambua Nyota iliyoibiwa ni hizi, kwa mfano mtoto alikuwa anafanya vizuri kabisa darasani lakini sasa hivi anazidi kudidimia wala hapendi kusoma, ukiona hivyo ujue tayari wameshachukua wanjanja! pia kwa mtu mzima unaweza kukuta kwamba unaandaa mipango lakini haitimii mipango yako.unapanga mwaka huu lazima nitafungua Duka lakini utashangaa linazuka tatizo hutafungua hilo duka mpaka mwaka utaisha. au unaandaa mpango mzuri kabisa lakini utashangaa unamwona mwenzako tayari ameshaanzisha mpango uleule kama ulivyokuwa unapanga. au kama ni biashara utaona mwingine kaanzisha vilevile kama ulivyokuwa unafikilia hapo ujue Nyota yako inatumiwa na mwingine.
  unajua nyota hizi huambatana na mawazo yako. jinsi mawazo yako yalivyo ndivyo na nyota yako ilivyo hawezi mtu akaitumia nyota yako pasipo mawazo yako.utajikuta kwamba wakati mwingine unapoteza fahamu kama hujielewi vizuri vile. hapo ujue kuna kitu.

  SASA TUNAKWENDA KURUDISHA HIYO NYOTA YAKO KUTOKA KWA WACHAWI:
  sali sala hii kwa bidii:
  Baba katika Jina la Yesu kristo nimetambua kama kunawizi wa nyota uliyonipa katika maisha yangu sasa kwa Jina lako naiamuru Nyota yangu kokote iliko irudi.katika jina la Yesu ninakuja kinyume na kila nguvu za shetani nazikata kamba zashetani nilizofungwa katika jina la yesu.asante bwana kwa kurudisha nyota yangu.

  SASA SHIKA MKONO WAKO KATIKA SCREEN YAKO NIKUOMBEE:
  Baba katika Jina la Yesu asante Mungu kwa sababu wewe ni mkuu kuliko wote.kwa Jina lako Mungu ninaamuru Nyota iliyoibiwa ya mtoto huyu, mama huyu,kijana huyu, binti huyu irudi mara moja na taabu iwapate hao waliomwibia nyota yake mtu huyu katika jina la Yesu.

  na baada ya hapo ni lazima utajiona tofauti katika mawazo yako, umekuwa na mawazo tofauti hii ni ishara kwamba nyota yakko imerudi,kama hutaona hizo dalili hizi ni ishara kwamba nyota yako haijarudi tafadhali rudia tena sala hii usichoke mpka uzione dalili hizi.

  bwana akubariki.

  Iliandikwa na Ev, Moses Mayila

 31. Bwana Yesu asifiwe sana,nawaheshimu sana watumishi wa Mungu wa kweli wote,kwa maana imeandikwa mwaminini Mungu ili mthibitike na waminini watumishi wa Mungu mpate kufanikiwa,kuhusu Malisa nilishamfuatilia kwa ufupi kwenye kipindi chake Star tv,wala cjaona kama kuna tatizo,naona kama wengi wanapata tatizo na jina Nabii.kuhusu nyota zilizoibiwa kuzirudisha inawezekana kwa mujibu wa neno la Mungu juu ya wale mamajusi toka mashariki ya mbali walivyoiona nyota ya Yesu na kuifuata kisha kuja kuisujudia,ni somo pana,so cjui kama anafundisha kwa muono upi ila haya mambo yapo na yawezekana mtu akaibiwa nyota na wachawi waganga wa kienyeji na mtu wa Mungu akaamuru kuziita na zikamludia mwenyewe,ni somo pana sana,pomoja na hayo mwenyewe nilikuwa cjui ila kuna cku pale kawe tanganyika peckes Ufufuo na uzima kawe Pastor Gwajima alifundisha kwa upana sana na watu wengi walioibiwa nyota zao kwa neema ya Mungu zilirejeshwa ktk jina la Yesu.We hujifunzi wachawi na waganga wa kienyeji wanapotangaza tunasafisha nyota?ndo haohao wanaowaibia na kuzifunika nyota za wengine ili hatma na fursa ambayo anayo huyu mtu asionekane na asiifikie hatma yake na akiifikia nikwa taabu sana,Mungu awabariki asante.Mpoki wa baba Glory.

 32. Mungu tu azidi kutusaidia na zaidi kutupa macho ya rohoni, bila hivyo wengi watadanganyika

 33. Ndugu Alfredi Katuma na wengine kama wewe, YAH: ONYO KALI !!!!!!
  Mtu yeyote anayetoa taarifa zinazoegemea upande mmoja yaani ambazo hazijathibitishwa au hakuweza kupata taarifa za kukana au kukubaliana nazo toka kwa mtuhumiwa mwenyewe naye pia ni nabii wa uongo. Yaani kama unamtuhuhu mtu yeyote kwamba siyo Nabii wa kweli na ukaeleza lolote baya kumhusu mtu huyo hata kama umepata shuhuda za watu, ukaziamini na kuanza kuzisambaza hewani kabla ya kwenda mwenyewe kuona au kumhoji huyo mtuhumiwa unayemtuhumu kwamba ni Nabii wa uongo, basi hata wewe umekuwa NABII WA UONGO.

  Kama unataka habari yako iwe ya kweli hakikisha kwamba umeisawazisha kwa kupata habari toka upande unaoutuhumu (apply a natural justice principles). Wewe ni nani hata uweze kuhukumu watu wengine bila hata kwenda kwao ukawahoji ukasikia nao wanasemaje?

  Hebu tufanye hivi: Hata kama mtu ni mbaya kiasi gani usimhukumu kwa kuzingatia ukweli unaosemwa na watu wengine tu hata kama unawaamini sana mashahihidi hao. Hebu nenda ukamhoji mtuhumiwa mwenywe naye usikie naye anasemaje? Mbona unaogopa kwenda kwake?

  Kuna kipindi Mzee Askofu Zachary Kakobe alituhumiwa saaaana kwamba ni Nabii wa uongo na anatumia uganga wa Nigeria kutenda miujiza. Watumishi wengi sana walijikwaa kwake sana. Hadi Mzee Moses Kulola alienda kwake, Mzee Gamanywa akaenda kwake kama ishara ya kuomba radhi kwa niaba ya makanisa yote kwamba sasa tuhuma zile hazikuwa za kweli na sasa waanze ukurasa mpya mpaka makanisa yote yakakubali kufanya Conference Kuuuubwa kanisani kwake Kakobe aliyekuwa anatuhumiwa kutumia uchawi kuponya wagonjwa.

  Utamaduni wa kuhukumiana hapa Tanzania sijui utaisha lini. Mtume Paulo alisema hata kama mtu natumia vibaya jina la Yesu iwe kwa hila au kwa nia njema bado Injili inasonga mbele. Kumbuka Yesu aliwaambia wafuasi wake, …hawa wakinyamaza hata mawe yatapiga kelele kumshangilia…… Kwa hiyo kama akina Malisa na Baba Gody na wengineo wanaotuhumiwa kwamba ni manabii wa uongo wanaotumia uchawi kuponya au kuokoa watu kama ni mawe au miti au wachawi, mimi sijui. Mie natazama maandiko wanayoyatumia kuhubiri watu na ninawasikiliza kwanza kabla ya kuwahukumu.

  Jitahidi kwenda kwenye mikutani yao, semina zao, makanisa yao, nunua vitabu vyao uvisome, nunua CD zao uzitazame, kaa nao kama inawezekana uwahoji maswali yako wayajibu, baada ya hapo TOA HUKUMU YAKO kama unadhani wewe ni HAKIMU au kama unayo MAMLAKA YA KUHUKUMU MANABII.

  Hebu wakristo tukue kiimani na kimaandiko, tuondoke kwenye utoto utoto wa imani na maandiko. Kumbuka naandika haya bila kuhukumu mtu yeyote hapa. Wala sijaonesha msimamo wangu kuhusu hawa wanaoitwa manabii. Naandika tu kuwataahadharisha watoa maoni hapa.

 34. watumishi mbona kama waganga wa kienyeji? asante ndugu Alfred kwa taarifa

 35. watu wa Mungu kuweni makini sana na hawa manabii! huyo malisa kwa wakazi wa mwanza nadhani hawana sababu ya kuambiwa vituko vyake hakuna mtu jijini mwanza anayefuatilia habari za mitume na manabii asiyemjua “nabii”malisa. kwa wasiojua mwaka jana jijini mwanza kulikuwa na vipindi ktk radio kwa neema fm vilivyodumu takriban miezi mitatu zikifundisha habari za mitume na manabii wa uongo pamoja na mitume na manabii wa kweli vipindi hivi viliambatana na shuhuda za watu walioabudu ktk makanisa ya manabii hawa wa uongo kwa waliobahatika kufuatilia vipindi hivyo nadhani watakubaliana na mimi kwamba iko haja ya kuwachunguza kwa makini na kuwapima watu wanaojitangaza kuwa mitume na manabii! sijasema hakuna manabii na mitume wa kweli la! maana kama ilivyo kuna noti za ukweli na pia kuna noti bandia.kama kuna kitu ilinishangaza ktk mfululizo wa vipindi hivyo ni pale alipotokea mtu mmoja kushuhudia, mtu huyu ambaye alikuwa mganga aliyeogopewa sana kutokana na alivyokuwa na uwezo ktkt mambo ya nguvu za giza. unajua huyu jamaa aliokoka ktk mojawapo ya mikutano ya bishop mpemba wa kanisa la kwa neema alishuhudia kwamba malisa na nabii mwingine ambaye huduma yake nayo ni utata mtupu anayejiita baba god mafalme mkombozi wa ulimwengu! walikuwa wateja wake wakubwa ambao walikuwa wakienda kupewa nguvu za giza ili ziweze kuwasaidia ktk huduma zao(hii ni ajabu kabisa) ni vigumu kueleza kila kitu hapa lakini maana wako walioshuhudia jinsi ambavyo watumishi hawa waivyopora mpaka nyumba za wajane na kuwaacha wajane bila makazi,wapo walioshuhudia jinsi walivyouza vitu vyao kuwapelekea manabii hawa fedha,wengine walipewa sabuni watembee nazo mifukoni kwamba zina upako wengine walipewa vitambaa vya upako wengine mafuta ya upako wengine maji ya upako na kwa mujibu wa mganga huyu aliyempokea yesu anasema maji waliyokuwa wanapewa watu ni mchanganyiko wa maji yaliyooshewa maiti na maji ya chooni. kingine kilichoshuhudiwa ni jinsi manabii hawa walivyopewa masharti ya kutokwenda kwenye msiba hata kama ni wa muumini wake yaani ni mwiko. kwa wanaotaka kujua jina la huyu mganga kabla hajaokoka alikuwa anaitwa juma rashidi na anaishi katika kijiji cha shigara wilaya ya magu na baada ya kuokoka alibatizwa na kuitwa paul. kama kuna akina tomaso wasioamini hiki nitawaombea mpaka namaba ya simu ya huyu paul. au kwa wanaotaka kupata nakala za cd za mafundisho haya na shuhuda hizo wanaweza kuwasiliana na bishop mpemba wa kanisa la kwa neema ambalo lianamiliki radio kwa neema fm, kwa no. 0767982111. au kwa wanaofahamiana na bishop maboya mnaweza kuwasiliana naye maana aliunganishwa live kwa njia ya simu kuchangia ktk mojawapo ya vipindi hivyo. nitaandika mengine naona niwaachie wengine ila jihadharini na manabii wa uongo!!!!!!!

 36. Ndugu yangu Oguda,

  Biblia si msitu mkubwa…..maana msituni utakutana na chatu…..na hata viumbe vya kufisha…Biblia ni Maneno ya Mungu…..Soma tena Zaburi yote ya 119 na Ujumbe wa Biblia uko wazi….! Angalia mwenye ujumbe mwenyewe anasema nini…” AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE AKAWAELEZA KATIKA MAANDIKO YOTE MAMBO YANAMUHUSU YEYE MWENYEWE” (Luka 24:26-27)…….Unapoona watumishi wanaleta ujumbe wa nyota zilizoibiwa hii ni Ishara tosha kabisa hawatembei tena na Mwenye Ujumbe huu….hata kama unaona pepo na Ishara mbali mbali…..Muumini Katika Kristo amejazwa Roho Mtakatifu…analindwa na Nguvu za Mungu…na UHAI WENU UMEFICHWA NA KRISTO….! Wapi na wapi na kuibiwa Nyota…..!

  Lakini kwa sababu kizazi chetu kinataka Ishara…..na maneno ya utafiti…basi Mungu ameacha tuaamini uongo….na Hakuna uongo unapoteza waumini leo kama ule unatoka Mimbarini kwa “watumishi” ambao wamekuwa kama mfano wa Nuru……!

  Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s