Polisi wavamia waumini wa EFATHA na kuwapiga!

Usiku wa kuamkia jumatatu ya Pasaka waumini wa Efatha Mwenge walivamiwa kwenye Ibada ya Morning Glory wakapigwa na hata kupelekwa polisi kwa madai ya kuchoma kiwanda, kuvamia walinzi wa Afro Plus na kuwapiga!

Je, kuna uhalali wa polisi kuvamia sehemu ya Ibada na kupiga waumini au kurusha risasi?

Advertisements

5 thoughts on “Polisi wavamia waumini wa EFATHA na kuwapiga!

 1. Shalom,

  Hakuna laana kubwa kama kushambulia kanisa.

  Hakuna nchi yoyote duniani inayoshambulia nyumba ya Ibada kama walivyofanya polisi wetu.
  Mamlaka ya serikali inatoka kwa Mungu na Mungu ndiye anayezipa serikali uhalali. Lakini Mamlaka hiyo (Serikali) inapoanza kushambulia mamlaka ya Mungu (Kanisa) ni laana kubwa sana.

  Kanisa ni mwakilishi (ubalozi) wa Mungu duniani na Mungu. Kushambulia Kanisa ni kumshambulia Mungu moja kwa moja. Hii ina Maana serikali yetu ndiye imekwisha kabisa.

  Wangefahamu siri hii wangeenda kuomba msamaha wa hadharani na kutafuta amani na Mungu. La sivyo kupiga mabomu kanisani itaigharimu serikali na watakatifu tunapaswa kuomba Mungu atusaidie.

  Kumwaga Damu kanisani kwa waumini waliokuwa wanaabudu ni Laana isiyo na mpaka.

  Mimi nakwambia kuna kitu kisicho kuwa cha kawaida kitakachotokea.

  Polisi walipaswa kuzingira kanisa na kutumia uongozi wa kanisa wangewakamata watuhumiwa wao na si kupiga kanisa na waumini kwa mabomu, risasi za moto.

  Tena tumeona walikuwa wanawapiga waumini waliokwisha kuwakamata, mateke na ngumi kwa jazba kweli kweli. Sasa polisi ana piga watu aliokwisha wakamata kwa nini? Tulifikiri polisi ni mwamuzi kumbe polisi walikuwa wametumwa na Afro Plus.

  Hichi ni kitendo cha kufuru iliyopitiliza.

 2. Shalom
  napenda kuwapa pole watu wa Mungu kwa mikasa hii iliyowapata, mjipe moyo mtashinda.
  Lakini pia naomba kuhoji hizi biashara kama saccos na benki kukaa ktk nyumba za ibada, Sikatai makanisa kumiliki hizo huduma muhimu tena napenda tumiliki zaidi ya hapa ila tu ziwekwe mbali na nyumba za ibada.
  Nasema hivi kwasababu biashara zinalindwa na nguvu na busara za kibanadamu mara nyingi, na zina wezakuadhiri utulivu na amani inayohitajika ktk kuabudu kama ilivyotokea hapa.
  Mungu azidi kulinda kanisa lake.

 3. KANISA la Efatha Foundation lililopo Mwenge, Dar es Salaam, limelalamikia kitendo cha Polisi Mkoa wa Kinondoni, kuvamia na kuwakamata waumini wake 53 waliokuwa wakihudhuria ibada Jumatatu ya Pasaka.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kulikuwa na vurugu zilizosababishwa na waumini wa kanisa hilo waliokutwa na mapanga, nondo na sime kwa lengo la kubomoa majengo ya Kampuni ya Uchapaji ya Afro Plus, jambo ambalo liliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia.
  Efatha Foundation na Afro Plus wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu, kila mmoja akidai kuwa mmiliki halali wa eneo hilo na suala lao lipo mahakamani.
  Kenyela alisema polisi ilipokea taarifa za kuwapo moto katika Kiwanda cha Afro Plus, askari wake na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji walifika eneo la tukio, lakini walizuiwa na walinzi wa Efatha kuuzima.

  Hata hivyo, watumishi wa kanisa hilo linaloongozwa na Mtume na Nabii Josephat Mwingira, jana walikanusha madai ya polisi na kwamba, polisi ndiyo walivamia waumini wake waliokuwa kwenye ibada.

  “Jumatatu ya Pasaka saa 12:00 asubuhi, waumini wa Efatha walikuwa katika ibada ya Morning glory, ghafla walivamiwa kutoka nje na watu ambao baadaye walitambuliwa kuwa ni polisi,” alisema Natu Shilla, Katibu Mkuu wa Ephata Foundation. Shilla alisema kutokana na kitendo hicho ibada ilisimama hasa baada ya mabomu ya machozi na risasi za moto kupigwa kanisani humo.
  “Kilichofuata ni vurugu huku waumini wakikimbia na polisi wakiwapiga kwa virungu na vitako vya bunduki na mateke. Baadhi ya waumini walijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili na ukumbi wa kanisa ukatapakaa damu,” alisema Shilla. Shilla alikiri kukamatwa kwa waumini 53 na kwamba, kulikuwa na idadi ya waumini na wachungaji kati ya 60 na 70 na kuongeza kuwa, magari yaliyokuwa yameegeshwa nje ya kanisa yalivutwa.

  “Kwetu sisi inaonyesha kuwa tukio hilo liliandaliwa kwa makusudi ili litekelezwe Kanisa la Efatha. Hii inatupa hisia kuwa kuna chuki kubwa kwa huduma ya Efatha,” alisema Shilla. Naye Godson Mmari ambaye ni mchungaji wa kanisa hilo, alisema vurugu zilianzia kiwanja namba 90, baada ya polisi kuvamia wakidai kuwa kulikuwa na moto unaowaka. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Efatha, Gothalm Mbele, alikiri walinzi wa eneo hilo kujibishana risasi na polisi kwa sababu walikuwa wakilinda fedha.

  “Benki ni eneo nyeti linalohifadhi fedha za wananchi, kwa hiyo walinzi walihisi wamevamiwa na watu waliotaka kuhatarisha usalama wa fedha,” alisema Mbele.

  Source: Mwananchi.

 4. Shalomu,
  Mimi naamini kuwa hakuna uhalali wa Polisi kuvamia maeneo ya Ibada. Lakini swali la msingi zaidi ni je ni halali kwa nyumba za Ibada kutumika kama kichaka cha kuficha wahalifu? Watu wafanye uhalifu halafu wakimbilie Kanisani/Msikitini kwa lengo la kujikinga wasikamatwe na dola na dola iwaachie tu? Inahitajika Busara zaidi.

  Swali la Pili, kwa nini nyumba ya Ibada itumike kuvunja sheria za Nchi?

  Shalomu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s