Mheshimiwa GeorDavie kuimba nyimbo za Injili!

Mhubiri wa kimataifa Nabii GeorDavie maarufu kwa jina la “Ngurumo ya Upako” ametambulisha nyimbo zake ziko hewani. Nabii huyu ambaye makazi yake ni Arusha Mungu amekuwa akimtumia katika Ishara na miujiza, hivi karibuni amefungua tawi la huduma yake nchini Marekani na amekuwa akienda nchi mbali mbali kwa ajili ya kuhudumia watu wenye matatizo.

Pia Geordavie Ministries wana studio ya injili N Y U FM 99.2 Kanda ya Kaskazini Arusha, ambapo wanarekodi waimbaji, TV na Vipindi vya Redio na kurusha hewani. Studio imefunguliwa mwanzoni mwaka huu.

Kwa kusikiliza nyimbo za Nabii Geordave Bonyeza hapa http://www.reverbnation.com/play_now/12946165

Advertisements

25 thoughts on “Mheshimiwa GeorDavie kuimba nyimbo za Injili!

 1. Gabriel Ayo,
  Kumbe huyu jamaa ni “msemaji wa serikali ya Mbinguni!!”
  Hili suala la Kutoa Pesa ili uombewe ni la serikali ya mbinguni pia?

 2. Mungu ashukuruwe aliye tuletea msemaji wa serikali ya ufalme wa Mbinguni. NabiiGeordevie Ni Nabii wa Mungu kabisa namuamini KAZI zake. Halafu jaribuni kusoma Biblia vizuri mtaona kwamba Manabii wote walipingwa .walijiinua watu baadhi wakawapinga manabii wa Mungu wa Kweli .ila cha kushangaza nikwamba mwanadamu wa nyakati hizi anawaamini sana wale manabii waliokufa Na kushindwa kuwaamini Manabii walio hai wanyakati hizi. Nabii Geordevie atakapo kuwa hayupo tens duniani watu wakisoma habari zake wataamini KAZI zake . bahati mbaya hauta kuwepo ili ushuudie hoyo yakitokea. Ushauri Wangu nkwamba huyu Baba Ni msemaji wa serikali ya ufalme wa Mbinguni

 3. Ni ukweli usio pingika Tumepata nabii karine yetu Tanzania na Ulimwengu.mimi nimemkubari. Mungu azidi kumbariki.wasio mwelewa’ watakuja kumwelewa’ tu. Hata wakati wa Yesu sio wote walomwelewa.Songa mbele Mh.nabii.Geordavie.

 4. Ni ukweli usio pingika Tumepata nabii karine yetu Tanzania na Ulimwengu.mimi nimemkubali. Mungu azidi kumbariki.wasiomwelewa’ watakuja kumwelewa’ tu. Hata wakati wa Yesu sio wote walomwelewa.

 5. NDUGU WACHANGIAJI

  Wagalatia 5:25 inasema “TUKIISHI KWA ROHO NA TUENENDE KWA ROHO”
  Maana yake ni kwamba kama sisi ni watu wa rohoni tuliokubali kuongozwa
  na Roho Mtakatifu ni lazima tuishi kwa kufuata KANUNI ZA KIROHO,ikiwa
  ni pamoja na kutunza na kuzungumza kwa hekima yale tunayoyaona katika
  ULIMWENGU WA ROHO.Lakini pia tusikubali mtu yeyote kwa hila yoyote
  atuingize katika majadiliano yatakayotufanya tupigane vita vya kimwili badala ya kupigana vita vya kiroho(Waefeso 6:12).

  Mtu wa rohoni hawezi kuzungumza chochote bila ya kupewa kibali na Yesu!Mtu wa rohoni hufanya utafiti wa mambo kwa kuongozwa na Roho
  Mtakatifu,kwahiyo kiuhalisia anayefanya utafiti siyo yeye bali ni Roho Mtakatifu ndani yake.1 WAKORINTHO 2:15 inaelezea SIFA YA MTU AMBAYE ANAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU kwamba “….huyatambua
  yote wala yeye hatambuliwi na mtu”.Watu wa rohoni wanawafahamu
  manabii wote wa uongo na wale wanaotumia hekima ya Yesu wako makini na zaidi ya makini katika kuleta mada,kuchangia mada na kujibu maswali wanayoulizwa!

  Ni wazi kwamba kwa kuwa hizi ni nyakati za mwisho ambazo wengi
  wamejitenga na imani,wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani(1 Timotheo 4:1),ni dhahiri kwamba ile VITA KATI YA UZAO
  WA MWANAMKE NA UZAO WA NYOKA IMEKUWA WAZI SANA(Mwanzo 3:15).Hali ilivyo sasa ni ya kusikitisha na kutisha mno kwa wateule ambao
  hawajitambui kiroho(Isaya 42:18-22).Hata hivyo unabii wa Mungu ndani
  ya Bibilia unatoa matumaini hai kwa wateule wa Yesu hasa wale watakaokataa KUOLEWA NA FEDHA.

  INASHANGAZA KUONA KUWA KUNA WANADAMU WANAOSHINDANA NA
  HEKIMA YA ROHO MTAKATIFU.HEKIMA YA MOTO WA YESU HAIPINGIKI
  WALA HAICHUNGUZIKI MILELE(1 Samweli 2:9-10).

  Binafsi hekima ya Mungu bado ninaichungulia!Ninatamani sana iwe pumzi
  ninayovuta lakini ni lazima nikubali kulipa gharama ili kuhakikisha nafsi yangu haitawaliwi na mwili huu wa udongo unaoharibika.Kweli kazi ninayo.

 6. Ndugu Kamugisha,

  Umenishtua kidogo, kwanba zaidi ya 85% ya makanisa ya kiroho yako chini ya manabii wa uongo!

  Kauli hiyo inapaswa kusemwa na mtu ambaye amesimama katika misingi miwili ifuatayo: kwanza,amefanya utafiti, na pili amefunuliwa na Mungu.

  Mimi naomba unisaidie kujua kama umefanya utafiti, na uniambie sample size yako ilikuwaje!

  Au kama umefunuliwa uniambie ulifunuliwaje!

  Maana kama hii takwimu ni ya kweli, basi tuko hatarini ikiwa ni pamoja na wewe mwenyewe.

  Nangoja.

 7. Mpendwa Wilson

  Naomba Roho Mtakatifu anipe hekima ya unyenyekevu wa MOTO ULAO(WAEBRANIA 12:29).Roho Mtakatifu naomba unipe hekima ya kufichua(LUKA 12:2).
  Lakini pia ninaomba kupitia ujumbe huu wateule wa Yesu wakajue mambo makubwa
  na magumu ambayo hawakuyajua(YEREMIA 33:3).

  SIKILIZA kwa makini Muheshimiwa mtumishi Wilson.Kumnena vibaya mtumishi
  wa Mungu aliye hai ni laana ambayo inahitaji toba ili kuiondoa.Tunatakiwa kuwategemeza kwenye maombi watumishi wa Yesu ambao wanafanya kazi ya Mungu kwa ulegevu na ufisadi na siyo kuwatukana.Pia kumnena vibaya
  mtumishi wa shetani ni kujiharibia upako wa Roho Mtakatifu ambao Yesu amekupa,
  pia unatakiwa ufanye toba ili kuituliza hasira ya Mungu kwasababu umepambana
  na mbwamwitu kimwili badala ya kupambana naye katika ulimwengu wa roho.Suala
  la kuangalia mavazi,mali,fedha(utajiri) pasipo kumchungulia Mtumishi katika
  ulimwengu wa roho na kufuata maelekezo ya Roho Mtakatifu kuhusu kile
  ulichoonyeshwa ni ZAIDI YA UPUMBAVU.

  Zaidi ya asilimia 85 ya mikisanyiko ya madhehebu na makanisa ya kiroho yako
  chini ya MANABII WA UONGO!Watumishi wote wa shetani wanajulikana na watumishi wote wa Mungu wanajulikana.Hakuna kilichojificha isipokuwa kwa wale
  VIZIWI NA VIPOFU wa kiroho(ISAYA 42:18-20).Wateule wasio na hekima ya kutunza
  kile wanachoonyeshwa katika ulimwengu wa roho kuhusu hawa manabii ndiyo
  wanaoropokaropoka onyo.Hata hivyo kuna mambo mengine Mungu anaruhusu
  yatokee kwasababu hizi ni nyakati za hatari na wateule wengi sana WAMETEKWA
  NDANI YA MADANGURO yanayoitwa makanisa ya manabii wa uongo(ISAYA 42:22,MATHAYO 24:24,25).Sasa hivi katika hizi blog kumezuka mapambano
  kati ya maagenti wa shetani na watumishi wa Mungu wasio na hekima ya Roho
  Mtakatifu.Watumishi wa shetani wanafurahi sana wanapoona wateule wameamua
  kupambana kimwili(WAEFESO 6:10-18) kwasababu wanakiuka utaratibu wa kupigana
  vita katika ulimwengu wa roho.

  YESU AFANYI BIASHARA YA REJA REJA. YESU ANAFANYA BIASHARA YA JUMLA.
  (MATHAYO 10:26-28).Manabii wa uongo ni chakula cha watu wa Mungu kama
  vile Yoshua na mwenzake walivyosema kuwa yale majitu tuliyoyaona kule KAANANI
  NI CHAKULA CHETU,tutayatafuna na kuimiliki hiyo nchi tuliyopewa na Bwana.

 8. Jamani wandugu shida kubwa minini mavazi,utajiri, au nini Geordevie ninabii WA Mungu msijitaftie mengine uamini nyamaza tupo wengi tumeuona mkono WA Mungu kupia yeye hakika Geordevi ninabii WA Mungu mavazi na anayomiliki niishara ya kuwa mungu SI maskini hii syo karne ya farasi,punda waliyotumia kina muda manabii wajao baada ya geodevi wataishi maisha yakifahari Sana coz mungu siyo maskin come on uamini nyamaza tens nyamaza tumefaidi sana

 9. Binafsi Bado nipo dilemma kuhusu
  Huyu dr. Na nabii mkuu. Kuna mengi yanasemwa.ila anajulikana kwa uchache sana kuliko mnavyodhani.Wa naomjua background yake watusaidie tafadhali.tujue historia yake na anapoishi kama ni arusha sehemu gani.asanteni

 10. Huo ndio ukweli kabisa!, kwani mungu amempa mtumishi wake vipawa vingi kadri ya unyenyekevu wake mbele za mungu songa mbele kukamilisha maono Amen.

 11. Ukweli ni kwamba MUNGU amembariki mtumishi wake kwa kila kitu na amekuwa Nabii wakipeke kwa stahili ya kipekee.

 12. May this be a blessing to all nations all over the world. A way of reaching out the gospel as promised that it will reach allover the world before the coming back of Christ. God bless all promoters of the true gospel of Christ Jesus.

 13. huu ndio ukweli wenyewe hata mimi ni balozi muhimu sana wa NYU njoo uone uweza wa mungu kuptia mtumishi wake Baba Dr Nabii Geordavie the hero of 21 cencury .

 14. tunaomba wote wenye kusikia waje wajionee kuliko kuambiwa kama akina dada. Beatrece. Dada Bety, ni lipi bora kusikia ama kujionea mwenyewe? karibu sana kwenye mahubiri ya Nabii huyu ndio utaamini baada ya kuona yanayotendeka hata mimi nilikuwa namsikia tu radioni lakini siku moja niliamua kuchukua hatua nikaenda kwenye ibada yake jumapili moja, niliyoyaona, namshukuru Mungu kwani nilikuwa nichelewe. siku hizi MIMI KILA KIPINDI NAPENDA KUWEPO LABDA NIWE NIMETINGWA NA SHUGHULI SANA. Karibu sana tunakupenda huenda ukija tu, utaweza kuuona MUUJIZA wako.

 15. Dada Beatrice si kila mchungaji aliyeitwa na Mungu ni sauti ya Mungu kwa ajili yako pengine hajaitwa kwa ajili yako. Na/au utahitaji kujionea na ukashuhudia wewe mwenyewe kuliko kuamini tu kwa kusikia na ukakubali ile taarifa iutawale moyo wako.

  La msingi kujua ni kuwa; ikiwa huna mguso kwa mtumishi anayejiita au kuitwa wa Mungu; usihukumu, we kazana kuambatana na wale ulio na mguso nao, UTAKUWA SALAMA. Usije ukakosea na kupata laana.

 16. This is the real man of God am blessed through him anoiting miracles ministries,and i fill proud to be among the ministries.

 17. Mie ni tofauti kabisa wapendwa. Sina imani na huyu mtu kama kweli anamuubiri Yesu, Mungu aliye hai. kwa taarifa nilizozipata pamoja na stori za watu waliohudhuria huduma yake sio nzuri kabisa. mie kwa upande wangu sijahudhuria huduma yake na wala sina mguso wala hanibariki. Mungu na atupe macho ya kiroho tuweze kumtambua wa mtumishi Kristo ni yupi na anaempinga Kristo ni yupi. hizi ni siku za mwisho na yatubidi tuwe macho sana wapendwa.
  Yesu Kristo awabariki.

 18. Namshukuru Mungu kwa ajili ya Mtumishi wake Baba Mhe,Nabii GEORDAVIE Kupitia vipawa na karama Mungu alivyoweka ndani yake Mnamo mwaka 2006 Alinifungua dhidi ya roho ya ukichaa kwa neno la mamlala.NAAMURU UFAHAMU WAKO UKURUDI nami nikawa mzima.Nilikuwa nikikasirika nikikushika mikono mwangu hutoki nilikuwa nawapiga watu.Pili niliponywa na Umauti nilikuwa natapika damu chungu sana sado 2 kwa siku sijui zilikuwa zinatoka wapi baadaye nikatapika mapande ya nyama,Nilijisaidia ngozi ya chura,mjusi na vitu vyeusi kama mkaana,Lakini sasa nimepona kabisa namtukuza Mungu Amen

 19. Mmi pia ni mtu ambaye naikubali sana kazi ya mtumishi huyu wa Mungu(Nabii GeoDeavie),kuanzia uimbaji hadi Huduma yake ya Ngurumo Ya Upako,kwani ishara,ajabu na miujiza huonekana kupitia huduma zake.Mungu azidi kumuinua na kumtumia zaidi.Amen

 20. Ni kweli huyu mtumishi alikua akiimba kwaya kabla.
  Kuimba na kuhubiri vyote vina lengo la kulitangaza neno la Mungu.
  Safi sana.

 21. jamaa alikuwa anaimba before nakumbuka miaka ya late 80s kuingia 90s nilikuwa na matoleo yake mawili nyimbo za mipasho ya kiinjili na tamu sana kama mtu yuko familiar nazo nyimbo kama nyakizanya, donotto was very cool bila kusahau wimbo wa ukiwa na Yesu mambo waa! Can’t wait kusikia album yake mpya ina nini.

 22. Mungu ashukuriwe sana, nilikuwa naumwa tumbo ulikuja Dar na kufanya mkutano biafra, nilipona kwa jina la Yesu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s