Imam wa Msikiti wa Mayaha, Kisisi apokea Uponyaji kwa Jina la Yesu!

Mchungaji Michael Peter Imani wa WAPO Mission International Tawi la Mbagala Maji Matitu akiwa amemshikia kipaza sauti Mzee Musa Hombe (Idd Hussein Seba) (73) Imam wa Msikiti wa Mayaha, Kijiji cha Kisisi, Kata ya Ekhanoda Wilaya ya Singida Vijijini.

Aliyekuwa Imam wa Msikiti wa Mayaha, akishuhudia jinsi Yesu alivyomponya baada ya kuugua kwa miaka 15 “Sasa ninatafuta wa kuninunulia Biblia, Yesu anaponya mimi nimepona, ninyi waislamu wenzangu mnapoteza muda”

Pichani ni mtoto wa aliyekuwa Imam baada ya kupokea uponyaji na kumpokea Bwana Yesu

Christopher ambaye pia ni mtoto wa Juma Kombe, akifurahia kuuona Utukufu wa Mungu baada ya kuokoka, alikuwa amepagawa mapepo na biashara zake zikawa haziendi baada ya kuokoka kwa wiki tatu akaanza kuona mabadiliko ya biashara yake kushamiri kwa kasi.  “Nilipofanyiwa maombi ya wiki 3, nikakaa sawa, nikaingia darasani kusoma, nilipojazwa Roho Mtakatifu, usiku nimelala walikuja wachawi, wakaniita jina la zamani, Abdallah, lakini sauti ya upole ikaniambia, usiitike”.

Kijana Christopher ndiye aliyesababisha baba yake Kumpokea Bwana Yesu.

Advertisements

9 thoughts on “Imam wa Msikiti wa Mayaha, Kisisi apokea Uponyaji kwa Jina la Yesu!

  1. Amen!Hakika Yesu ni mwema kwa wote. Changamoto kwa wakristo vuguvugu ambao hata hawataki kusikia habari za wokovu,WACHWA!!

  2. Asante sana mzee uliyemkiri YESU kuwa bwana na mwokozi kaza mwendo hizi ni siku za mwisho tetea nafsi yako ubarikiwe sanaaaaaaaaa.

  3. Ninamshukuru Mungu kwa Muujiza huo mkubwa.hili ni funzo kwa sisi ambao tumeokoka lakini hatuitumii neema kuwatembelea wagonjwa mahospitali,Pengine wengi wangeweza kuletwa kwa Bwana Yesu kupitia Uponyaji.Wengi tunapougua tunaomba Mungu atuponye kana Kwamba uponyaji ni kwa ajili yetu wenyewe tu,Wapendwa tubadilike tuipeleke injili na uponyaji kwa wengine na Mungu atatenda kwetu kirahisi.

  4. Hakika 2naye Mungu wa kweli, kila goti litapigwa na ulimi utakiri kwamba “YESU ni BWANA”

  5. hii ndiyo inayotakiwa, lazima mtu aone tofauti kati ya Mungu wake anayemuabudu na Mungu wa kweli. Watu wa Mungu fanyeni kazi za namna hii na sio kukaa kujibizana wenyewe kwa wenyewe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s