Ni mti upi Hawa alitwaa tunda?

Mwanzo3:6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.”

Je ni kweli kuwa Hawa alitwaa hilo tunda kutoka mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Kama tunavyofundishwa???

Advertisements

81 thoughts on “Ni mti upi Hawa alitwaa tunda?

 1. Naomba kujibu swali lako kama ifuatavyo kwa msaada wa Yesu.
  Mti ambao Hawa alitwaa matunda yake ni “Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya”. Katika bustani ya edeni ukiachilia mbali mimea na miti mingine kulipandwa pia miti miwili maalumu ambayo ni Mti wa uzima na Mti wa ujuzi wa Mema na Mabaya Mwanzo 2:8-9. Kwa mujibu wa Maandiko matunda ya miti yote waliruhusiwa kula (pamoja na matunda ya Mti wa uzima) isipokuwa matunda ya Mti wa ujuzi wa mema na mabaya huo hawakuruhusiwa kuyala na Mungu alisisitiza sana kuwa siku watakapo shawishika kula watakufa hakika Mwanzo 2:16-17.
  Ni muhimu sana kufahamu kuwa maneno ya Mungu katika Biblia takatifu ni maneno ya Kiroho na ili mtu aweze kuelewa mambo yalivyokuwa katika uhalisia wake ni muhimu sana akitafuta kuelewa kwa tafsiri ya kiroho. Sio kila wakati Biblia inapotaja vitu mfano, miti, bahari, upepo nk inamaanisha vitu hivyo HAPANA ni lugha tu ya mfano ili kufanya mambo ya kiroho yaeleweke vizuri.
  Kwa mfano neno “UCHI” lililotumika katika mwanzo 3:7 halimaanishi uchi wa nyama kama ambavyo wengi wamekuwa wakitafsiri kwa sababu kama lingekuwa linamaanisha uchi wa nyama Mungu asingemuuliza adamu kwamba “ni nani aliyemwambia kwamba yuko uchi?” tazama Mwanzo 3:7 “Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
  Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
  Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
  Akasema, NALISIKIA SAUTI YAKO BUSTANINI, NIKAOGOPA KWA KUWA MIMI NI UCHI; nikajificha.
  Akasema, NI NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA U UCHI? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? ”
  Kila mtu anajua maana ya kuwa uchi kimwili kama adamu na hawa walivyojua kwa hiyo Mungu hakuwa na sababu ya kumuuliza adamu ni nani aliyemwambia kuwa yu uchi kama maana yake ingekuwa ni uchi wa kimwili ila kwa kuwa UCHI hapa ni katika tafsiri ya kiroho ndio maana Mungu akataka kujua sababu ya adamu kuwa uchi ndio maana alimuuliza.. JE UMEKULA WEWE MATUNDA YA MTI NILIYOKUAGIZA USIYALE?
  Mtakatifu yeyote au mtu anapookoka katika ulimwengu wa kiroho ni kwamba anakuwa kavikwa mavazi yanayojulikana kama MAVAZI YA WOKOVU Isaya 61:10 “Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu” Na mtu anapokuwa kaasi anakuwa uchi kabisa kiroho ndio maana Yesu anatoa ushauri kwa watu wenye dhambi kwamba wamwendee wanunue kwake mavazi ili AIBU YA UCHI WAO ISIONEKANE Ufunuo 3:18 “Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, NA MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
  Kilichotokea ktk Bustani ya edeni ni (copy and paste) ya kile kilichokuwa tayari kimetokea Mbinguni. Kule mbinguni Lusifer ambaye alikuwa ni malaika mkuu wa Mungu alijiinua na kujifanya yeye ni sawa na Mungu, na kwa ushawishi wake alifanikiwa kuwadanganya theluthi ya malaika wamfuate yeye na ndivyo ilivyotokea malaika wale wakaacha kumtii Mungu wakamtii shetani kwa kufuata maelekezo yake, Mungu alimtimua shetani na malaika zake na kuwatoa nje ya Mbingu.
  Ni vile vile ilivyokuwa ktk bustani ya edeni, Neno edeni maana yake ni bustani ya raha kwa mfano wa mbinguni. Mti wa ujuzi wa Mema na Mabaya ni Mfano wa “SHETANI” anaitwa mjuzi wa mema na mabaya kwa sababu anaujua utakatifu
  wa Mungu kwa viwango vyote na kauishi na tena ni mjuzi wa mabaya yote ndiye mwanzilishi wa kufuru zote duniani” Mti wa uzima ni Yesu kristo anayeitwa Yeye ndiye chemchem ya uzima, mzabibu wa kweli.
  Kwa msingi huo Matunda ni matendo fulani yanaweza kuwa mazuri au mabaya (mfano matunda ya roho, utu wema, fadhili, uaminifu nk, au matunda ya mwili uongo, kiburi, masengenyo nk)
  Mungu alijua kuwa shetani anaweza kuwashawishi adamu na hawa wasimwabudu yeye ndio maana aliwapa tahadhari mapema, na ndivyo ilivyotokea shetani kwa msingi ule ule alioutumia kuwadanganya malaika kwa kuwatamanisha kwamba wakimtii yeye na kumpinga Mungu watakuwa kama Mungu alifanya hivyo kwa adamu na hawa na matokeo yake ni yale yale yaliyowakuta shetani na malaika zake wao walifukuzwa mbinguni(shetani na malaika waasi) Adamu na Hawa walifukuzwa ktk bustani ya edeni ni (copy & paste) ya kile kilichotokea mbinguni.
  Shetani ni muongo hapendi watu wajue kweli hii ndio maana ametumia nguvu nyingi kupotosha kwa kufananisha kula matunda na kufanya uzinzi eti kwamba Adamu na Hawa walifanya uzinzi hii sio kweli. Maandiko yanasema Mtu mume na mtu mke nao walikuwa mwili mmoja na akawaagiza wazae na kuongezeka, Adamu na Hawa walikuwa ni mke na mume.
  Baada ya Uasi wa adamu na Hawa ulimwengu mzima ukawa chini ya utawala wa shetani pamoja na malaika waasi. Inamaana Mti wa ujuzi wa Mema na Mabaya ukatawala lakini Mungu aliupenda ulimwengu (Yaani wanadamu hata akamtoa mwanae wa pekee ili KILA MTU AAMINIYE asipotee bali awe na uzima wa milele.
  Kwa lugha nyingine ni kwamba tumeletewa tena Mti wa uzima (Yesu) ambaye anamuwakilisha Mungu duniani, Tunachopaswa kufanya ni kukiri kwanza kwamba Yesu ni Bwana, na Shetani si Bwana, na kufanya matendo mema au kula matunda ya mti wa uzima.
  Mbarikiwe

 2. Bwana Yesu asifiwe wapendwa. Naomba uthibitisho wa jambo hili , je ni tunda gani alilolimega hawa hata kuona yakuwa yu uchi? na pia wana wagiza wanazaliwa na nani?

 3. Mkandya umekuwa mtu wa kulalamika lalamika saana! Mara najifanya najua sana, mara sijui ninaojadiliana nao wananiita majina, ilimradi unalalamika tu! Watu wanaisogeza koma katika Maandiko, wewe unawatetea, eti kwa kuwasema kwangu najifanya najua! Hivi kuna mtu anayelijua jambo halafu akawa anajifanya? Au wasiojua ndio wenye kujifanya!

  Nimekwambia statement ya Mwa 3:3 ni ya kweli, wewe umeniambia ni uongo, nithibitishie, badala yake unanishambulia! Kwamba kwa kunishambulia unadhani Maandiko yatabadilika?

  Kama Kristo ndiye ule Mti wa Uzima, unashangaa nini mwanamke kuwa mti?

  Labda nikuulize, Uzao wa nyoka unaozungumziwa ktk Mwa 3:15 “nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Je, ni uzao kweli, au ni hadithi tu? Na kama ni Uzao kweli wako wapi huo uzao na ni akina nani? Maumbile yao huo uzao yakoje?

  Halafu hebu nisaidie ktk hili, kwanini Adamu amwite mkewe kuwa ndiye mama wa wote waishio,? 

  Baba yake Kaini ni nani?

  Majibu ya maswali haya yanaweza kutusogeza mbele katika ufahamu na kutusaidia katika kukabiliana na changamoto za ukristo, kama lilivyo kusudi la kuandikwa kwake katika Biblia!

  Asante

 4. Unajua nini Lwembe, ndio maana ndg wanaokosa uvumilivu na wewe wanajikuta wanakuita majina ambayo hayafai. Kusema kweli una vutu vyako fulani ambavyo kama si kuvumilana mtu unaweza kuamua kutofanya mjadala nawe ili kuepusha mengi.

  Unapenda mno kuona kuwa wewe ndio uko sahihi kuliko wengine bila hata kuthibitisha sawasawa kimaandiko.

  Kwa mfano hebu toa ithibati ya kimaandiko kuwa mwanamke ulikuwa mti!
  Maana angalia ulivyosema hapa: ””Basi huo ndio Mti wa Nne uliokuwamo katika bustani, ukiacha ile mitatu; ya kuliwa, wa Uzima na ule wa Ujuzi wa Mema na Mabaya. Nao mti huu wa Nne alikuwa ni mwanamke. Huyo ndiye mti wa kifo!”

  Naomba ufafauzi hapo Lwembe!

 5. Nami nakubaliana nawe Mkandya, kulingana na declaration yako, sioni tutaendelea wapi katika kujadili, maana hiyo Standard inayotakiwa kutuongoza, Biblia, sote tunamtazamo tofauti kuihusu. Ni sawa na Musa alipokuwa yungali katika hekalu la Farao, akiwa tayari amepewa uelewa wa yeye ni nani, basi wanapochungulia dirishani, Musa huwaona wana wa Israeli ni watoto wa Mungu, lakini Ramsey aliwaona watumwa wao wa milele!

  Unaona, nasi leo tunapomtazama Eve kupitia dirisha la Maandiko, mimi namuona Binti ya Mungu aliye kamili, ambaye ndani yake hakuna uasi; nawe Mkandya unamuona ni muongo aliyejiongezea maneno yake na kumsingizia Mungu!!

  Lakini juu ya hayo, ninaamini kwa kadiri tunavyoendelea katika kulitafakari Neno la Mungu, huko mbele mengi yatatufungukia!!

  Bwana akubariki, ndg yangu!

 6. Ndg Mkandya, swali nililokuuliza, kwa kadiri ninavyofahamu, wakristo wengi saana hatujafika ktk kuwa na uhakika wa kweli, kwamba ni nani anayetusimulia mambo yoote ktk Biblia; acha haya majibu yetu rahisi kwamba “Biblia ni Neno la Mungu” halafu hatua mbili mbele mtu anakomalia mafundisho ya dhehebu lao akiyafanya ndilo Neno la Mungu; kwahiyo tunabaki katika mzunguko wa mauti; maana imeandikwa mtu hataishi kwa mkate pekee bali kwa KILA NENO litokalo ktk kinywa cha Mungu! Kwahiyo kulijua Neno lipi ni la Mungu na lipi ni la Eve, jambo hilo linakudhihirishia kiwango cha uzima ulichonacho!!! Lakini jambo hilo liko wazi, 2Tim 3:16 “All scripture is given by inspiration of God, and is profitable for doctrine, for reproof, for correction, for instruction in righteousness”

  Basi, hebu yageuze mawazo yako kidogo tu hata kwa saa chache, halafu chukua mtazamo huu kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayekusimulia mambo yote kuanzia Mwa 1:1 hadi nukta ya mwisho ktk Ufu 22:21 “Amen.” Ninakuhakikishia kuwa Biblia yako itakuwa Mpya, tena utaifurahia sana, maana sasa kwako yatafunuliwa yote yaliyofichwa ambayo hufikiwa kwa imani! Hebu fikiri, iwapo Mungu anakusimulia jambo halafu wewe unasema “muongo”, kweli utaipata faida ya jambo hilo? Si rahisi, utaishia kwenye ibada nzuri na za kupendeza za akina Kaini zisizo na ufunuo!

  Kuhusu ukamilifu, labda nikukumbushe tu kuwa huwezi kukipa “Free Will” chombo ambacho ni dhaifu! Halafu, hebu tazama hapa kuhusu hiyo Free will yako uone ni wapi haswa ilikuwa applied. Hivi mtu aliyedanganywa, anakuwa ametumia hiyo free will? Biblia inasema Eve alidanganywa, kama ambavyo kanisa limedanganywa kuwa Eve aliongeza maneno yake, na WANA AMINI hivyo ktk huko kudanganywa! Lakini Adamu, yeye hakudanganywa bali alimsikiliza mkewe, katika hiyo Free will, akaamua kumsikiliza mkewe, kama ambavyo nawe Mkandya baada ya kuyapitia Maandiko ktk Mwa 3:3, sasa juu ya ufahamu huo, unayo hiari ya kuambatana na Neno kama linavyojifunua, au kuendelea na uongo uliouamini!

  Kuhusu wao kukatazwa kula kutoka Mti wa uzima, hilo sote tunafahamu kuwa halipo! Na pia Mkandya, hatutetei dini zetu, bali tunaikagua nchi tuliyopewa kuirithi – Neno! Kwahiyo ondoka ktk mentality ya dini, tazama kavukavu kile Biblia inachosema: kama inakuambia kuhusu Serpent kuwa na Uzao, physical, halafu mbele ya wakati huko ukamuona huyo aliyelizungumzia jambo hilo ktk kusanyiko la watu wawili na huyo Serpent, akiwatambua huo Uzao, halafu ni wa kidini; iwapo hutataka kujua kulikoni, utakuwa ni mtu asiyehusika na Neno la Mungu, yaani si mrithi wa hilo, thats the long and short of it!!

 7. Lakini unajua nini Lwembe? nikiangalia hoja zako za nyuma juu ya topic hii ninaona ni jinsi gani kuendelea kuijadili nawe ni kupoteza wakati, maana una mtazamo ambao kwa kifupi siwezi kukubaliana nawe.

  Hebu ona ulibyowahi kusema hapa; ”Basi huo ndio Mti wa Nne uliokuwamo katika bustani, ukiacha ile mitatu; ya kuliwa, wa Uzima na ule wa Ujuzi wa Mema na Mabaya. Nao mti huu wa Nne alikuwa ni mwanamke. Huyo ndiye mti wa kifo! Kila kizaliwacho na mwanamke shurti kife!”
  Tafadhali!!

 8. Sasa Lwembe kama ulikuwa unajua aliyeyasimulia matukio yote ni Roho mtakatifu, ulikuwa unaniuliza ili iweje?
  Na imeandikwa wapi kuwa matukio yote ya biblia yamesimuliwa na Roho mt?

  Kwamba Eva hawezi kuwa aliongeza hayo maneno ‘wala msiuguse’ kwa kuwa alikuwa katika ukamilifu asingeweza kusema uongo, kwa hiyo kilichomfanya akubali kula tunda la huo mti ni ukamilifu pia?

  Lwembe ni vema kujua kuwa ukamilifu unaosema kuwa walikuwa nao haukuwa ‘automatic’, bali lilikuwa ni suala la utashi. Mungu hakumuumba mwanadamu ili awe mkamilifu automatically, bali alikuwa na uwezo wa kuchagua(utashi) kutii au kuasi.
  Vinginevyo huo ukamilifu ungemzuia au ungemlinda asikubaliane na uongo wa shetani.

  Kwa hiyo sikubaliani na hiyo hoja yako kuwa Eva asingeweza kusema uongo kwa sababu ati alikuwa katika ukamilifu.
  Kwa hiyo bado nasisitiza kuwa hilo neno ‘msiuguse’ hakuna mahali ambapo Mungu alilisema katika maagizo yake kwa Adam.

  Na kama unataka kutumia hicho kigezo ku-justify hoja yako kuwa kulikuwa na mti mwingine, basi ni wewe utakuwa umeamua kuamini hivyo.

  Lwembe niliposema kuwa sina namna nzuri ya kuthibitisha nilimaanisha kirahis kabisa kuwa hicho kitu hakina rejea kwenye maandiko.
  Kwa hiyo wewe unaposema kuwa kipo kwa maana ya hichohicho tunachotaka kukithibitisha ati tukithibitishe kwa chenyewe, hiyo si kweli pia. Huwezi kuthibitisha kitu kwa chenyewe.

  Vinginevyo labda kama unasema kwamba hayo maagizo ambayo Eva anayanukuu kwamba Mungu aliwaagiza, basi aliwaagiza lakini hayakuandikwa kwenye biblia.

  Lwembe na kama unasema kuwa majibu ya Eva yalikuwa sahihi kabisa kwa mujibu wa Mwa 3:3, basi alimaanisha kuwa hawakutakiwa kula katika mti wa uzima, maana kwa tafsiri yako ya matumizi ya koma katika Mwa 2:9 ulisema mti wa ujuzi wa mema na mabaya hauko kwenye miti iliyokuwa katikati ya bustani.

  Maana katika Mwa 3:3 (Lakini, matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa”)

  Kwa hiyi unaposema ‘mti huo mwingine’ kwa maana ya uliokuwa katikati ya bustani unamaanisha kuwa ni mti wa uzima.

  Kwa hiyo Mungu aliwakataza wasile tunda la mti wa uzima????!!!
  Maajabu.

 9. Mkandya, nami nakubaliana nawe kwamba ni jambo zuri kwa “mtu kutokupoteza muda wake katika mambo ambayo hayawezi kuongeza thamani yoyote ya lazima katika suala zima la wokovu” bali uamuzi huo wa kipi kinaiongeza thamani, inategemea sana kuijua thamani ya kitu, hata likiwa ni Neno la Mungu!

  Pia unasema huna namna nzuri ya kuthibitisha kuwa Eva aliongeza maneno “hata tusiuguse…” Nami nakubaliana nawe kuwa ni vigumu saana kulithibitisha jambo ambalo halipo!!!

  Lakini unaposema kuwa, “Hakuna mahali Biblia imesema kuwa Mungu aliwaambia wasiuguse” na kunitaka nikusaidie iwapo najua yalipo maelezo hayo, hilo pia ni jema maana sote tupo hapa kwa ajili ya kujifunza na kushare maarifa katika Neno.

  Maelezo hayo unayosema hakuna mahali yaliponenwa hivyo, NI HAYO UNAYOYAONA katika Bilia yako hapo ktk Mwa 3:3
  “Lakini, matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa”
  Haya ndio maelezo yanayounesha mti huo mwingine! Eva hawezi kuwa ameongeza maneno maana huyo yuko katika ukamilifu kwa hiyo hawezi kuwa muongo, it is that simple! Kwahiyo tunapaswa kuwa tayari katika kulipokea neno la Mungu kwa kadiri linavyojifunua, kwa ajili ya kutusogeza mbele katika uelewa, badala ya kuling’ang’aniza li conform na mafundisho yetu!

  Kuhusu ni nani anyetusimulia habari zilizomo katika Biblia, jibu lake ni hilo jepesi ambalo sisi hulitumia katika mijadala yetu lakini hatuamini hivyo. Roho Mtakatifu ndiye anayeyasimulia matukio yote katika Biblia mpaka majibu ya Shetani, otherwise kama ni Musa au yeyote kati ya watumishi wa Mungu watakuwa ndio walioandika mambo hayo, basi they must have been gods to have traversed the element of time and thought!

  Kwahiyo, maelezo haya ktk Mwa 3:3 ni ufunuo zaidi wa yale yaliyo katika 2:17; kwa hiyo ukiyaamini hayo kama yalivyo, Mungu anawajibika kuendelea nawe katika yanayofuata, if at all itaongeza thamani; usipoyaamini hayo, ni dhahiri kuwa utabaki katika hicho unachokiamini, ambacho huwezi kukithibitisha kwa Maandiko, ambavyo sijui kithamani linasimama wapi?!

  Asante!

 10. Lwembe huwa nina tabia moja, ya kutoyapotezea muda wangu mwingi mambo ambayo hayawezi kuongeza thamani yoyote ya lazima katika suala zima la wokovu.

  Sina namna nzuri zaidi ya kuthibitisha kuwa Eva aliongeza maneno ”hata tusiuguse….”, zaidi ya kusema kuwa hakuna mahali biblia imesema kuwa Mungu aliwaambia wasiuguse. Sasa sijui Eva aliyatoa wapi haya maneno, labda wewe kuna mahali unajua yapo, nisaidie.

  Lwembe sijui wewe sanaa ya uandishi unaielewaje, ukiangalia hiyo Mwa 2:9 utaona kuwa ameanza akasema kuwa kulikuwa na miti mbalimbali kwenye bustani, lakini kwa habari ya katikati ya bustani akaeleza habari ya miti miwili (wa uzima na wa ujuzi wa mema na mabaya).

  Sijui wewe kama unaona mti wa ujuzi wa mema na mabaya hauko kwenye fungu la miti iliyokuwa katikati ya bustani sasa unaweza kutuambia ulikuwa wapi (mti) kwa mujibu wa maandiko . Lakini mimi nionavyo kwa jinsi sanaa ya uandishi ilivyokaa hapo huo mti uko kwenye fungu la miti iliyokuwa katikati ya bustani, ndio maana baada ya maelezo ya mstari wa 9a kuna semikoloni (;).

  Swali la anayetusimulia hizo habari za mwanzo sioni mantiki ya kulijibu, labda iangalie historia itakwambia nani aliandika kitabu cha Mwanzo.

  Asante ndugu yangu.

 11. Ndg Mkandya,
  Asante kwa majibu, hayajaikata kiu yangu, lakini yameipoza!
  Umesema kuwa haya maneno katika Mwa 3:3, Eva ameyaongeza, Mungu hakuyasema hayo. Kimsingi, jambo hilo la kuongeza kwenye Neno la Mungu, hilo lingemuingiza dhambini moja kwa moja kabla hata hajadanganywa na nyoka, yaani Eva alikuwa ni muongo kuliko nyoka, maana ndiye aliyeanza kumdanganya nyoka, kama nimekuelewa vizuri! Unaweza kulithibitisha jambo hili kiMaandiko?

  Pia unasema, “Lkini pia kuna maneno ambayo Eva aliyasema ambayo ni ya kweli lakini hayapo kwenye Mwa 2:17, nayo ni mti ulio katikati ya bustani. Maneno hayo yanapatikana Mwa 2;9b” Biblia yangu katika kifungu hicho inanionesha kuwa katikati ya bustani kulikuwa na mti wa uzima, na si huo wa ujuzi wa mema na mabaya kama unavyosema, “…na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” Umeiona hiyo koma baada neno bustani, ndugu yangu? Usije ukawa unatumia Biblia za kiSabato, maana hao ni mahodari wa kuhamisha koma na kuibadili maana nzima ya kifungu!

  Mwisho nikuulize, Hivi anayetusimulia habari hizo huko Mwanzo ni nani?

  Asante!

 12. Bwana Lwembe jana niliandika lakini nashangaa comment yangu haikuja, ni maswala uya mtandao.

  Ninachoweza kusema ni hiki kwamba kifungu cha Mwa 2:17 ni maneno yaliyosemwa na Mungu, na kifungu cha Mwa 3:3 ni maneno yaliyosemwa na Eva.

  Kuna maneno ambayo hayakuwa yamesemwa na Mungu katika Mwa 2:17 ambayo Eva aliyaongeza katika Mwa 3:3 akiwa anajibu swali aliloulizwa na nyoka, na wala siyaoni mahali popote.

  Mungu hakuwa amewakataza kuugusa mti wa uhjuzi wa mema na mabaya,bali aliwakataza kula matunda yake.

  Lkini pia kuna maneno ambayo Eva aliyasema ambayo ni ya kweli lakini hayapo kwenye Mwa 2:17, nayo ni mti ulio katikati ya bustani. Maneno hayo yanapatikana Mwa 2;9b

  Angalao hivyo ndivyo mimi niwezavyo kuuleza uhusiano kati ya hayo mafungu mawili,

 13. Mkandya ndg yangu,
  Nimefurahi kukuona, na ninaamini huenda kwa busara zako tukafika mahali jambo hili likaeleweka vizuri zaidi kulingana na kusudi la Maandiko, maana siamini kwamba Mungu aliyaandika hayo ili ayasome yeye, bali ni kwa ajili yetu ili kutuleta katika ufahamu wa mambo hayo!

  Basi nikuulize kuhusu jambo hili katika Mwa 3:3 “Lakini, matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa”, je, wewe unapokisoma kifungu hiki, unaona kinaoana na kile cha Mwa 2:17?? Hebu vipitie tena hivyo vifungu kwa makini halafu tuendelee sote kuanzia hapo.

  Ninakushukuru kwa kujitoa muda wako nikiamini mwisho wa jambo hili tutakuwa tumesogea mbele zaidi katika ufahamu wa Neno la Mungu!

 14. Guys, naona kama tunafanya mzaha hapa. Tafadhali naomba tukumbuke kuwa maneno tusemayo tutayatolea hesabu siku moja.

  Jaribuni kurudia kuyasoma mnayoandika.

  Lakini pia wengi wenu naona mnayarukia mambo haya bila kuwa na ujuzi nayo. Mnaongea mambo magumu sana ambayo naamini kama Mungu huwa anaweza kuchukizwa basi kuna uwezekano mkubwa mko karibu au tayari mmeshamchukiza.

  Sasa nini kigumu katika maandiko? imesema walikula mti ambao Mungu aliwaambia wasile. Bila shaka muuliza swali alitaka kujua ni mti upi. Na mti ambao Mungu aliwakataza wasile ni mti wa ujuzi wa mema na mbaya.

  Ili kuthibitisha haya ona Mwanzo 2:17a. But of the tree of the knowledge of good and evil, thou shalt not eat of it:

  Halafu ili ujue kweli kwamba huo ndio mti waliokula angalia Adam anavyojibu swali la Mungu; Mwanzo 3: 11. And he said, Who told thee that thou wast naked? Hast thou eaten of the tree, whereof I commanded thee that thou shouldest not eat? ( Kumbuka tumeona kuwa mti alioambiwa asile ni wa ujuzi wa mema na mabaya).

  Mwanzo 3:12. And the man said, The woman whom thou gavest to be with me, she gave me of the tree, and I did eat.
  Adamu hakukanusha kuwa hajala katika mti ambao Mungu alimwambia asile. Kama unajua sarufi ya Kiingereza, Adam alitumia article ”the” tree, kwa maana ya kwamba ni ule mti ambao uko kwenye tungo ya muuliza swali, yaani Mungu. Ingekuwa mti wowote tofauti na aliouliza Mungu, Adam angesema ‘a tree’. Maana yake alikubali kuwa tumekula matunda ya huo mti uliotukaza kula.

  Kwa hiyo kimsingi jibu la swali ndio hilo, mengine yote ya ngono. mti ni mwanamke, au ni Lusifa mnayoyasema sijui mnayatoa wapi wapendwa. Naomba tumwogope Mungu tuache kugoshi neno lake.

  Halaf acheni kutukanana wapendwa.

 15. Hiiiii, Lwembe,
  Rafiki yangu unatia huruma wewe!! Na sijui ni nani atakayekusaidia, maana kile ulicho nacho wewe, wadhani is right while not. Na umekomaaa weeee,kah! Mimi pengine nitakuachia maswali ya kutafakari wewe mwenyewe na pengine nitajaribu kudondoa kidogo kukujibu, na nina imani wengine watakusaidia pia.
  Jaribu kulinganisha tofauti iliyopo kati ya Mwa 3:3
  “…lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.” Na Mwa 2:17 “Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”, Je wewe unaona kuna tofauti gani hapo? Ina maana Mungu aliumba miti miwili ya Adamu akila matunda yake atakufa? Na ile dhana ya zaeni mkaongezeke, ilikuwa ni dhambi mbele za Mungu? Na kwa sababu kauli ya Mungu ya zaeni mkaongezeke ilikuwa ni ileile hata kwa wanyama, je, wanyama nao wanakomit sin? Plz, be clear and specific!!
  Nao mti huu wa Nne alikuwa ni mwanamke. Huyo ndiye mti wa kifo!, Lwembe, hivi unataka kutuambia kuwa, Mungu alipomfanyia Adamu msaidizi wa kufanana naye, alimfanyia kitu kiitwacho kifo? Na kama ni ndiyo, ni nani aliye kifo kati ya Adamu na Hawa kwa muktadha wa Biblia?
  “Leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.” Yaani siku ile ile aliyosulubiwa Kristo, mwivi yule aliingia peponi, ninaamini hicho ndicho Biblia inachotuambia., Kweli utaendelea kuishia hapahapa endapo Biblia utaisoma kama MwanaHalisi. Je, liangalie kwanza swali la mwivi pale msalabani. Mwivi alijua kile alichokuwa anakiuliza. Wewe msoamaji ndo unayechanganyikiwa bure tu. Rejea kwanza kwenye swali la huyo jamaa. Halafu usome historia ya Biblia kama iliandikwa kwa kufuata hizo punctuation marks ambazo unang’ang’ana nazo wewe. Mimi nikikwambia unahitaji maziwa, Lwembe huwa mbishi weee!!! Sasa si unaona madude unayoleta kwa wajoli wa Bwana!!! Te te tee!! Pole sana Lwembe.
  Biblia inaposema yule mwanamke mchawi alimpandisha Samweli, au Kristo kwenda kuwahubiri roho za wakati wa Nuhu zilizo kifungoni, basi kwa mpindo huu jambo hilo linakuwa haliwezekani, maana wanakiunga na kifungu cha Mhu 9:5 “..lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.” Biblia tangu mwanzo hadi ufunuo, hakuna hata sehemu yoyote ambayo imeonesha Mungu anampa utukufu ibilisi wa kufufua wafu. Hakuna. Nenda kaisome tena vizuri Biblia yako. Maeneno mengine, tumia akili tu kuelewa, Seleli alikwambia siku nyingi habari hizi but hutaki kuelewa. Ukiendelea na ibada za mizimu-kutokufa kwa roho, na roho hiyo kuwa kama nafsi iliyo hai kabisa, utapotea wewe!! Yaani acha tu. Siku ile niliwapa changamoto ya kufikiri kama ni kweli roho huwa na hadhi ya nafsi hai mara baada tu ya mtu kufa. Nikawaambia kuwa, Kama Kristo aliwaendea roho waliokuwa kifungoni, akawahubiri huko, ina maana, hata roho ya Mungu/Kristo hufa!! Usishangae, ndiyo maana ya hoja yako. Maana ukilisoma hilo fungu, linasema roho yake ikahuishwa(ikafanywa kuwa hai tena, it means ilikuwa imekufa), na kuwaendea roho wengine…. Oohh, Is this Biblical? BIG NO. Pole sana. Aya hiyo haina maana hiyo. Ndiyo maana nakwambia, acha kusoma Biblia kama the guardian. Unatia aibu na doctrines zako hizo. They are out of Christianity arena bro.
  Shetani alikwisha kufa zamani, nabii Eliya alimuua!!, Mimi hili sijui rafiki. Nijuacho ni kwamba, shetani, ambaye ndiye nyoka wa zamani, bado hajafa. Tena anachangamka sana kuwapotosha watu kama akina Lwembe maana anajua ana muda mchache tu. Mungu atamuua siku si nyingi zijazo.

  Bwana akubariki. But be keen to study the word of God.
  nzala

 16. Shalom!
  Kwanza niseme hivi kwa ajili yenu, kujifunza kunahitaji uwe na “moyo wa kujifunza” kwanza. Pia huwezi kuwa mwalimu kama huna uwezo wa kusikiliza na kutafakari unayoambiwa na mtunga somo! Unapokosa mambo haya mawili nawe ukiwa umejipachika nafasi yoyote kati ya hizo mbili, kama ni mwanafunzi basi utaishia kuwa kati ya wale watukutu, maana hao hukakikisha wanavuruga amani kwa makusudi kutokana na kuwa na uwezo finyu wa kutafakari jambo na hivyo kuhakikisha na wenzi wao hawapati kitu, na kama ni mwalimu, basi ole wao wazazi waliokuletea wanafunzi!

  Angalia kauli zenu:
  “Kuna toleo jipya la BIBLE nini? hii biblia ya kaka lwembe ni funika mbaya,..da! aisee”
  Hivi ninyi kweli mnayo hofu ya Mungu? Wengi wenu huwa nayasoma mnayoyaandika na mara nyingi mnakiri kuongozwa na Roho Mtakatifu, hivi hata RM mwenyewe mnamjua kweli? Au ndio kule kujikoki na dini na mafunuo mpaka hata Biblia zenu hamjui hata kilichoandikwa save for the few quotes mnazozitumia!?

  Biblia ninayoitumia mimi ni KJV- Scofield Study Bible 1909 Version, humo ndimo nimeyasoma haya: Mwa 3:3
  “…lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.”
  Huu ndio mti tunaouzungumzia, nao mti huu si huo mnaouzungumzia ninyi huo wa Mwa 2:17
  “Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”
  Hii ni miti miwili tofauti. Hivyo ndivyo ninavyoiona mimi kwa kadiri ninavyoisoma Biblia yangu. Kwahiyo kutokuiona kwenu yawezekana ndiko kule “kufungwa” kwa Maandiko anakokufanya Mungu kwa makusudi.

  Basi huo ndio Mti wa Nne uliokuwamo katika bustani, ukiacha ile mitatu; ya kuliwa, wa Uzima na ule wa Ujuzi wa Mema na Mabaya. Nao mti huu wa Nne alikuwa ni mwanamke. Huyo ndiye mti wa kifo! Kila kizaliwacho na mwanamke shurti kife!

  Nao mti huo ndio uliouleta Uzao wa nyoka kupitia Kaini! Yatazameni Maandiko, Adamu amemjua mkewe mara mbili halafu wamezaliwa watoto watatu! Hata Kaini hayumo katika ukoo wa Adamu. Mnadhani Mungu alikosea? Hapana, hakukosea bali aliyaficha tu hayo ili yaje yaeleweke huko mwisho. Yohana Mbatizaji akiwa ni nabii aliwaona hao wakiikimbia Hukumu, maana kati yao HAKUNA aliyeitimiza Torati yote na hivyo kuwa katika laana inayostahili Hukumu, ndipo walikuwa wanaikimbilia Neema, ambayo si yao! Mt 3:7
  “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?”
  Kwahiyo Yohana aliwatambua kwa kile walicho licha ya umaarufu wa dini zao, na heshima walizojitwika! Wao walikuwa wanaendelea katika kazi yao kubwa ya kuyapindisha Maandiko kama alivyofanya baba yao kule Edeni, nao waliipindisha Torati mpaka ikawa siyo! Hayo ndiyo matunda yao, ukiwa na macho unaweza kuyaona peupe.

  Hata leo wapindishaji ni wengi sana, wameipindisha Injili mpaka basi, ni vile tu hatujapata “Eye salve” tungewaona na kuwashangaa kama vile ukipewa uwezo wa kuwaona “wanga”! Hebu utazame mpindo huu kuhusu yule mwivi msalabani:
  “And he said unto Jesus, Lord, remember me when thou comest into thy kingdom. And Jesus said unto him, Verily I say unto thee, Today shalt thou be with me in paradise” (Luke 23:42-43).
  Hii ndiyo nukuu halisi, kama ilivyo katika Biblia, ikionesha kwamba, “Leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.” Yaani siku ile ile aliyosulubiwa Kristo, mwivi yule aliingia peponi, ninaamini hicho ndicho Biblia inachotuambia. Biblia ikisema hivyo nawe ukaiamini hivyo, Mungu atakupenda, kwahiyo ili kukuua Shetani alikwisha anzisha mafundisho ya kuua kwa kucheza na Maandiko, msingi akiuweka hapo Maandiko yanazungumzia Ufufuo kama 1Kor 15:51-54 na Danieli 12:2 nk ili akulete katika kuitilia shaka Biblia kama hapo Biblia inaposema yule mwanamke mchawi alimpandisha Samweli, au Kristo kwenda kuwahubiri roho za wakati wa Nuhu zilizo kifungoni, basi kwa mpindo huu jambo hilo linakuwa haliwezekani, maana wanakiunga na kifungu cha Mhu 9:5 “..lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.” Ambapo wao wanajua kuwa hao wanaowalisha hayo hawana RM wala uvuvio wake kwani wamewapeleka mbali sana na Injili, kwa hiyo wanayameza tu! Ndipo wanaendelea kuwanyemelea wengine!!

  Haya utazame mpindo sasa wa kifungu hicho cha Maandiko ili kukuleta katika imani tofauti na inayofunzwa na Biblia kuhusu kifo cha mkristo aliye na uzima ndani yake:
  “And Jesus said unto him, Verily I say unto thee today, thou shalt be with me in paradise.”
  Umeuona mpindo huo? Wamehamisha koma (,) kutoka pale kwenye thee, katika ile original quote, ambavyo inaleta maana ya yule mwivi kuingia peponi siku ile ile, kwa hiyo wao wameipeleka mbele kwenye today, ili kuleta maana ya kwamba mwivi huyo atakuja kuingia Paradiso huko mbele kwenye ufufuo! Itazame hata ile ‘T’ ya Today kwenye original text ambayo ni capital T iki denote kauli ya Kristo ikimhakikishia kuingia kwake leo hii, lakini wao wameiunganisha katika namna ambayo imeiondoa maana hiyo, wakiweka small ‘t’ kulingana na mpindo wao! Je, jambo hilo lina tofauti na Mwa 3:4
  “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,” ???

  Haya mwingine anakuambia Shetani alikwisha kufa zamani, nabii Eliya alimuua!! Sijui kama mnalijua chimbuko la mambo haya? Kuna wokovu mnaoweza kuupata chini mifumo hii? Zitazameni mbegu zake, zileteni katika Nuru ya Maandiko, mtayaelewa zaidi hayo, maana hakuna jambo jipya duniani, si huduma wala chochote kile, nendeni kule Mwanzo, huko ndiko mambo yote yanaanzia. Unaweza kujikuta uko katika mfumo uliopindishwa mwaka 325 au 1850 nk nawe ukajiunga tu na kuushabikia, kumbe mpindishaji, ule uzao wa nyoka unaotumiwa na mpindishaji, alisha liseti hilo dude zamani linaelekea kuzimu!

  Mbarikiwe,

  Ck Lwembe

  nb*
  Source ya “mpindo” wa punctuation: article shared kwenye groups, titled “Where did the Thief on the Cross Go?” On 23/10/2012

  *Shetani alikwisha kufa – blog

 17. Swali hilo nilimwulizaga siku nyingi sana Lwembe. Lakini hakunijibu kuwa ana aina na toleo gani la Biblia. Muziki alioucheza hadi mimi nikalala ….. ni kuwa nyoka na Hawa walizini!!! Duuuuu! Very fascinating!!! Nampendekezea toleo la KJV ya zamani. Huenda atapona.
  nzala

 18. Nzala/Mallya,Kuna toleo jipya la BIBLE nini? hii biblia ya kaka lwembe ni funika mbaya,..da! aiseePress on,Edwin Seleli

 19. Mallya ndg yangu,
  Lwembe ndiye aliyesema kuwa tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya ilikuwa ni NGONO. Ina maana kwamba, kwa kula mti huo, tungefanana na Mungu. Binafsi sijui kama Mungu ameoa ama la!! Huenda tukimwuliza Lwembe, atatupa jibu. Haya ndiyo miongoni mwa mambo mapya katika akili yangu, ninayoendelea kuyapata kutoka kwa wakristo-Lwembe. Sidhaani kama na wengine wana hii theolojia.
  nzala

 20. @ Nzala, ha haaa,””leo ukatuambia tena kwamba mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa ni NGONO. Seriously kabisa, niombee tu RM akinifunika tena na hapa””Siyo NGONO…au kwa vile ulikuwa mti wa katikati?? Tangu mwanzo alikuwepo “”UTUPU,UKIWA,na GIZA”” , Mungu alimuonya Adam asishirikiane na huyo , lakini kwa Kuwa Hawa aliamua kushirikiana na huyo na akamshirikisha na Mumewe- huyu jamaa anayeanzaga kudanganya kwa kutumia matamshi “”Eti…” Ndiyo chanzo cha hawa wazee wa kwanza kuanguka.Siyo NGONO… “”Eti alisema msile?? Hakika hamtakufa, mtafanana naye”” ni kilekile kiburi cha kutaka kufanana na MUNGU..Wapo watumishi na mapasta wengi tu wanasema “”usifuate ninachotenda bali fuata ninachofundisha, nao wanaanza na ” eti” ,wengi wameanguka kwa kujikwaa na NGONO.. Wakijitahidi sana kuikimbia NGONO… Huku wakiihubiri ni mbaya huku wakiitenda…wengine wake zao wamewakimbia kwa kuwa wameshindwa kuvumilia… Bezaleli DC

 21. Ha ha ha haa!! Nilimaanisha Lwembe. Sina mtu ninayemuuliza magumu yanaponikuta/kumbana nayo tofauti na RM. Japo huamini ktk hili, basi. Lakini hatuwezi kuzungumzia vitu viiiingi halafu tangible hivyo, leo ukatuambia tena kwamba mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa ni NGONO. Seriously kabisa, niombee tu RM akinifunika tena na hapa, nitasema kitu, otherwise, utaona kimya!! watu wengine watacementi kama wanayo na wao.
  Ubarikiwe
  nzala

 22. Nzala, “mtu wa mizimu”!

  Umenifurahisha saana safari hii, eti “Cheki tena Baba yao huyu!!” Unanipigia yowe ya Kisukuma ndg yangu!!! Halafu, hebu acha ujanja wa sokoni, eti “RM akinisukuma kufanya kitu kwa text hii, nitatoa jibu baadaye; RM akikusukuma? au ukayatafute kwenye mafundisho yenu? Usihangaike, hili waliliacha, liliwashinda!!

  Pia kulikabili Neno la Mungu huhitaji ujasiri unaoambatana na ufahamu wa uhusika. Yaani kule kujitambua kuwa wewe ni mwana katika nyumba hiyo, ndipo waweza kuingia katika vyumba vyote na kukagua vilivyomo!

  Unajua Nzala, huko nyuma, nadhani katika SG hii, mimi ni mtu wa pili kukwambia kuwa wewe si mkristo, bali ni Msabato, baada ya ndg Oguda! Umebisha saana na kulalama, uking’ang’ana kuwa wewe ndiyo hasa mkristo kuliko wengine wote wasio itunza Sabato na “sheria za maadili”, hata umetamatisha kuwa hauwezi kujazwa RM nje ya kuitunza sabato na “amri kumi za maadili”. Lakini leo nimefurahi kwamba wewe mwenyewe kwa kauli yako umelikiri jambo hilo, ukidhihirisha wazi kuwa hujui lolote kuhusu RM! Hii hapa kauli yako:

  Lwembe: “Na pia twafahamu kwamba huo Mti wa Uzima ulikuwa ni Kristo, na ule wa Mema na Mabaya ulikuwa ni Lusifa.”

  Nzala: “Kwa kauli hii Lwembe, ni vizuri zaidi ungesema kuwa unajua au baadhi yenu mnajua hivyo na siyo WOTE. Kimaandiko ktk plain writings na hata kiunabii, sijawahi kukutana nah ii kitu yako Lwembe!! This is an error!!”

  Basi hilo ni kweli, kama ulivyosema, nami napaswa niamini hivyo. Basi kwa vile Bwana yu ngali anaita, lainisha shingo yako, tayarisha pia koo lako kama mtoto mdogo, unyweshwe maziwa yasiyo ghoshiwa!

  Kristo kuwa ni Mti wa Uzima:
  Yoh 1:4 ikimzungumzia Neno, “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.”

  14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

  Rev 2:7 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.”
  Basi ndugu yangu, asili ya UZIMA ni moja tu, kama unaweza kuibaini hiyo, mafumbo mengi yataeleweka.
  Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya:
  Mti huu ulikuwa ni Lucifer ambaye sasa alikuwa adui wa Mungu. Ezk 28:13 “..ulikuwa ndani ya bustani ya Edeni (akizungumzia mfalme wa Tiro – Lucifer)’
  Isome vizuri hiyo Ezekiel, utabaini asili ya uasi na hila.

  Mwanamke kuwa ‘Mti’:
  Kuhusu hili, hebu itazame tena Mwa 3:3 “…lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa” Kama unao uwezo wa kuyaamini Maandiko, basi amini hicho unachokisoma kuwa kiko hivyo hivyo. Maana mti huu hauwezi kuwa ndio ule wa Ujuzi wa Mema na Mabaya, Mwa 2:17, kwani huu haukutakiwa hata kuguswa! Nae Hawa katika stage hii hakuwa muongo hata aongeze maelezo ambayo Mungu hakumpa, bali yalikuwa ni maelezo sahihi. Sasa jaribu kuutafuta mti huo alikuwa ni nani!!

  Kuhusu Nyoka/Serpent na Lusifa
  Nyoka ni neno la kiswahili linalo maanisha Snake au Serpent
  Snake: a long limbless reptile that has no eyelids, a short tail, and jaws that are capable of considerable extension
  Serpent: a large snake.

  Nyoka/ Serpent KiBiblia:
  Mwa 3:1 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu.”
  Kuhusu kuongea kwa Nyoka kama binadamu, hebu zirejee kauli zake hizi:
  Mwa 3:2 “Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?” Mwa 3:4-5 “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

  Kuhusu Serpent kumtongoza Hawa, hilo ndilo lililotokea. Unajua mwanamke akiguswa guswa maungo yake kinatokea nini? Sasa, hebu jaribu kulitafakari jibu la Hawa kuhusu kuguswa, unaijua ile sheria ya kumgusa mwanamke iliyopitishwa hapa Tz, hairuhusiwi hata kumkonyeza; adhabu yake nadhani ni miaka 10 au 30!! Nzala kaa chonjo na TAWLA!!!

  Kuhusu wahubiri wengi kujiaminisha katika mambo ambayo si ya kweli, ni jambo jema kuwa nawe umejitambua kuwa pamoja na hao! Maandiko yako hivyo hivyo kama ulivyo yanukuu.
  “Kaini alikuwa mkulima ardhi. Kaini alikuwa mkulima ardhi. 3Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.”
  Sioni mahali ambapo Biblia inasema sadaka hiyo ilikuwa mbovu! Ni mawazo ya watu wakijifikirisha mambo ambayo hayapo. Hawana subira ya kuyasikiliza Maandiko! Ndio maana nilisema kuna ulazima wa kuliamini Agano jipya lote ili ujazwe RM apate kukuongoza katika Maandiko. Hakuna anayeweza kwa uhakika kutoa sababu ya Mungu kuikataa sadaka ya Kaini wala kuikubali kwake ya Habili, isipokuwa kwa kupata Nuru katika Agano Jipya hapo inaposema “Kwa imani Habili alimtolea Mungu sadaka iliyo bora kuliko Kaini”

  Ndipo nikasema Imani ni mawasiliano ya siri kati ya Mungu na wanae. Umeniletea nukuu inayozungumzia imani, hilo ni jema na ndilo linalotupa uhakika wa hiyo imani kuwa ni mawasiliano ya siri au kwa lugha nyepesi UFUNUO, kama Ebr 11:1 uliyoinukuu inavyolidhihirisha jambo hilo kuwa ndio Ufunuo. Pia Rum 10:17 kwa kadiri inavyosema, “imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” basi kwa kadiri ulivyotamatisha kuwa Neno la Kristo ni Biblia ambayo ndiyo tunayoitumia kufundishana, kuonyana, kuhubiria Injili nk, hilo ni sawa kabisa. Kwahiyo kupitia Biblia, huja huko kusikia hata sisi huipata imani. Ndipo ningekuuliza, Je, Habili alikuwa na Biblia ya kusoma hata kupata imani iliyotokana na huko kuisoma au kuhubiriwa, ndipo akamtolea Mungu sadaka iliyo bora???

  Mambo haya yanataka utulivu wa moyo Nzala. Ukiutuliza moyo wako kwa Bwana, utapata usikivu na hivyo kuyaelewa maelekezo unayopewa, kuliko ukiendekeza dini! Kuwa msikivu inalipa sana. Iwapo husikilizi Instructions kwa kituo, nilikuambia utaishia porini!!

  Nikupe mfano wa mwalimu na wanafunzi akiwajaribu katika suala la usikivu:
  Asubuhi aliwaletea mtihani rahisi sana wa hesabu, somo ambalo wao huliita “mama mkwe” kwa jinsi wasivyo lipenda. Maswali yalikuwa 25. Akawaambia wasome vizuri instructions, kisha wajibu kwenye karatasi ya kujibia waliyopewa. Maelekezo yaliwaambia “wasijibu swali lolote”. Muda waliopewa ulikuwa ni nusu saa. Baada ya hapo, akakusanya makaratasi. Watoto wote walikuwa na furaha sana, “mtihani ulikuwa rahisi sana, lazima niondoke na 90 au bull!” Lakini walifeli woote kasoro mmoja tu aliyemrudishia mwalimu makaratasi yaliyoandikwa jina tu!

  Sasa wewe sidhani kama ni mwangalifu katika jambo hilo. Maana unaleta vigezo vya zamani wakati vimepitwa na wakati. Unaleta mambo ya Amri Kumi kuhalalisha kujazwa RM jambo ambalo halipo! Ni sawa tu na unavyo ng’ang’ana na maelekezo aliyopewa Nuhu kabla ya kuingia katika safina kuhusu wanyama wasio safi na walio safi ktk Mwa 7:2 halafu ukashindwa kuyafuata maelekezo mapya katika Mwa 9:1-5 ambayo yanampa Nuhu uhuru wa “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni vyote.” Sas sijui ni RM gani uliyenaye? Tazama Mt 28:19 maagizo yanakuambia, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” , umeng’ang’ana na haya hata umeshindwa kuyaona maelekezo mapya katika Mdo 2:38 yanayokutaka, “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Sasa unapozungumzia eti unamngojea RM akuongoze nawe ukiwa umeyakosa maelekezo haya mapya, utampatia wapi?

  Injili sio lele mama, hebu jaribu kuwa msikivu!!!

  Ubarikiwe,

  Ck Lwembe

 23. Hey,
  Lwembe, una theology kaka!!!
  Sijui unaziotoa wapi rafiki yangu. Duuu!!
  Hata tumeona katika wanyama wa mwitu ndiye pekee alikuwa na uwezo wa kuongea na binadamu. Kwa hiyo kwa mantiki ya maelezo yako, serpent siyo nyoka kaka (japo huko chini kuna sehemu umesema kuwa ni nyoka)??. Halafu unasema kabisa nyoka alikuwa alikuwa na uwezo wa kuongea na binadamu tangu mwanzo?? Alipewa ala za sauti kama za binadamu tangu mwanzo?? Naa kama hakuwa nyoka, alikuwa ni mnyama ndiyo but wa aina gani sasa?? Unaweza kutuambia tofauti iliyopo kati ya Surpent na Lucifer??
  Ndipo twafahamu Shetani alimvuvia na kumuongoza kumtongoza Hawa na kuishia katika tendo la ndoa lililomleta Kaini! Angalia Lwembe, unataka kutuambia kuwa Hawa alifanya mapenzi na dude lisilojulikana(lisurpent), ndipo akazaliwa Kaini?? Hey, naona kama kuna mapepo kwenye hili!! Anyway, na wengine watacementi!Ila mimi najua kuwa, hata kaini, ni uzao wa Adamu uliosi tu. Angalia, Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Mwanzo 4:1. Hili ndilo neno la Bwana. Ukisema tofauti na hapa, tunaomba utupe aya tafadhari!!!
  Wahubiri wengi hujiaminisha kwamba Kaini alimtolea Mungu sadaka mbovu, lakini si kweli Maandiko hayasemi hivyo. Si wahubiri wengi tu, hata Nzala nafahamu hivyo, maana anasoma katika neno: Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Mwanzo 4:3-5.
  Sasa, Lwembe, kati ya Maandiko haya na theolojia yako, tumwamini nani rafiki? Mungu au Lwembe??

  Jamani, tumeelewa kuhusu Imani? Sio mambo ya kukiri Amri Kumi za Mungu, sijui Sabato au kukiri wokovu au kukariri mistari ya Biblia nk. Si hayo, bali ni MAWASILIANO YA SIRI kati ya Mungu na uzao wake au wanae.. Nadhani na kwa hapa bado unahitaji msaada rafiki. Sikiliza rafiki; Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana (Waebrania 11:1) na imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo(Warumi 10:17). Neno la Kristo ni nini?
  Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. (Wakolosai 3: 16-17). Kumbe neno la Mungu ni hili tulitumialo kufundishana, kuonyana, kuhubiria injili na kwa nyimbo pia. Automaticaly, Neno la Kristo ni Biblia. Na Biblia ni jumla ya vitabu 66.

  Sasa, ndg yangu, kama unalikataa neno kama njia pekee ya kumfahamu Mungu na kufahamu tabia yake, utawasiliana naye vipi tena?? Njia hiyo ya SIRI ni njia gani?? Ukisema kwa RM, RM hutuongoza kwenye kweli yote, ambayo ndiyo Biblia!! Sasa kama imani haiji kwa neno la Kristo(yaani Biblia), nachelea kusema kuwa hiyo nayo ni imani ya kuwapeleka watu mbinguni!!
  Sikia, wengi ukiwemo na wewe Lwembe, hufikiri kuwa RM yupo kwa watu wasiyozitii na kuziishi Amri 10 za Mungu. Yesu aliwaahidi mitume wake RM kwa wale tu ambao watatii Amri za Mungu. Angali, Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu (yoh 14:15-17).
  Lwembe na wengine, RM aliahidiwa kwa wale wanaompenda Yesu tu na udhihirisho au ishara ya upendo wako kwa Yesu, ni kushika Amri zake. Nguvu ya kuihubiri injili ilitolewa kwa watu wa jinsi hiyo tu. Maana kazi ya RM ilikuwa na bado hadi leo ni kuuhukumu ulimwengu kwa habari ya dhambi. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu(yoh 16:8). Sasa wapendwa sidhani kama unaweza kuzungumzia dhambi(uvunjaji wa sheria), haki, na hukumu bila kuwepo kwa sheria. Ukisema una RM ilhali huzishiki Amri zake, huyo siyo roho wa kweli. Ni roho asiye wa Kristo. Usinulize ni roho gani!!! Mimi sijui.
  Wapendwa habari ya kuwa wafuasi wa Kristo tunaongozwa na RM ni sharti tutii, utii ambao huja kama matokeo ya upendo wetu kwake. “ …na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii…” (Ebran 5:8-9).
  Suala la utii liko palepale. Na RM, hajakuwepo tu agano la kale, alikuwepo tangu mwanzo. Yote aliyoyafanya Mungu Baba na Mwana, RM alikuwepo. Ndiyo maana hata siku moja hataongoza watu kuzikanyaga sheria za Mungu kana kwamba YEYE(RM) siyo Mungu. Kamwe haitatokea!! RM ndiye atakayetukumbusha yote… “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia…” yoh 14:26. Suala la utii lipo tu hata kwa RM. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio(Mdo 5:32).

  Jamani, tumeelewa kuhusu utii? Miongoni mwa mambo ya kukiri Amri Kumi za Mungu, ikiwemo Sabato au kukiri wokovu au kukariri mistari ya Biblia nk, ndiyo miongoni mwa vigezo muhimu sana vitakavyotufanya tuokolewe. Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu ufun 14:12
  Mungu awabariki mnapofanya maamuzi sahihi.
  nzala

 24. UZAO WA NYOKA

  Wapendwa,
  Tulipokuwa tukijadili mada ya “Ivi Tufanyeje kuhusu Ndoa Jamani…” katika maelezo yaliyotolewa, lilijitokeza jambo la Uzao wa Nyoka. .

  Ili kuweza kulipata jambo hili kwa uhakika, inatubidi turudi kwanza katika kile kitabu cha Mwanzo, maana hicho ndicho kitabu cha Mbegu, na mambo yote, huko ndiko yanakoanzia. Basi jambo la Uzao wa Nyoka kwa mara ya kwanza linaonekana katika Biblia katika, Mwa 3:15 hapo Mungu anapomwambia nyoka,
  “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.”
  Hapa ndipo suala la nyoka kuwa na uzao linapoanzia, na pia mwanamke kuwa na uzao.

  Tunapoendelea kulichunguza jambo hili, ndipo tunapoyaangalia Maandiko katika Mwa 4:1-2 tunasoma;
  “Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema nimepata mtoto mwanamume kutoka kwa Bwana. Akaongeza akamzaa ndugu yake Habili”
  Hivi ndivyo Biblia inavyotuambia; kila utakavyoisoma hakuna kinachobadilika – Adamu kamjua mkewe kama ilivyoandikwa, mkewe akapata mimba akamzaa Kaini akaongeza akamzaa Habili. Basi tuseme kwamba hawa watoto wawili waliozaliwa ndio uzao wa mwanamke? La hasha! Maandiko hayatufunzi hivyo.

  Hii ndiyo rekodi aliyoiweka Mungu tuisome siku tutakayofikia kuwa na shauku ya kujua nini kilitokea kule Mwanzo. Tumeona kuwa Adamu kamjua mkewe mara hiyo iliyoandikwa na wamezaliwa watoto wawili – kama ni mapacha wa kuongozana katika kuzaliwa au ni wa tofauti ya siku moja au mbili au wiki, sote hatujui. Labda kwa ajili ya ufahamu wa hili ni kwamba mwanamke anaweza kujifungua mapacha wanaotofautiana kwa hata siku mbili na zaidi – ukiwauliza wataalamu wa mambo ya uzazi watakujuza zaidi.

  Kuhusu Nyoka, ni kama Biblia inavyosema, nyoka (Serpent), alikuwa mnyama wa mwitu kama wanyama wengine bali yeye alikuwa juu zaidi – alikuwa mwerevu (subtil = pervasive, elusive, mysterious, magic, charm, power,…) kupita wanyama wengine. Hata tumeona katika wanyama wa mwitu ndiye pekee alikuwa na uwezo wa kuongea na binadamu.

  Wengi wetu linapofika suala la Nyoka, hukimbilia kumfanya ndiye Shetani katika ujumla wake. Lakini ukweli ni kwamba Nyoka, yule Serpent, alikuwa ni mnyama, hayawani wa mwitu, na iwapo mbele katika Biblia nyoka ameoneshwa kama Ibilisi au Shetani, basi unapaswa ufuatane nayo Biblia ili uone ni wapi yule mnyama wa mwitu amegeuka kuwa hivyo. Na iwapo utakurupuka na kusema huyo Nyoka ndiye Shetani na Ibilisi, basi Lucifer utamuweka wapi?

  Kwa bahati mbaya, kulingana na hali halisi, kamusi zetu zote hazina tafsiri ya hili neno SERPENT- wote walipotafsiri wameishia kwenye neno SNAKE ambaye ni ‘REPTILE’. Hata wabunifu nao pia wamekwama; wakikuchorea taswira ya Edeni, basi utamuona nyoka (snake), Cobra au Black Mamba anayetambaa karibu na Hawa anayelichuma lile tunda la apple! UMEONA MUNGU alivyolifumba jambo hili?

  Lakini Serpent aliyekuweko huko Edeni si huyu nyoka, (snake) tuliyenaye leo hii. Serpent hakuna anayemjua mbali na Adamu na Hawa! Mungu alimu extinct baada ya kosa alilolifanya.

  Basi kulingana na Maandiko katika Agano Jipya, huko ndiko yanakofunuliwa mambo mengi. Ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa kuliamini hilo ili tujazwe Roho Mtakatifu, huyo tuliyeahidiwa, ili kwaye tuweze kulivinjari Agano la Kale katika Nuru yake; “Lakini yeye atakapo kuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote…” Yoh 16:12

  Basi huku ndiko tunakozikuta hizo zao mbili tulizoziona huko mwanzo. Maana twafahamu kwamba uzao wa mwanamke ni Kristo, kwa uthibitisho wa Maandiko. Pia tumewaona watu wakitambulishwa kuwa ni Uzao wa Nyoka, Mt 23:33 “Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Kwahiyo wazo la kwamba eti kigezo cha kuwa uzao wa Nyoka ni kule kutokumcha Mungu, si sahihi, maana uzao ni ukoo, kwa hiyo ni lazima uwe umetokana na Nyoka; maana sheria ya Mungu isiyo badilika inasema kila kiumbe kizae kwa jinsi yake, ndipo uzao wa Serpent hauwezi kuwa kitu kingine!

  Basi Maandiko ktk Agano Jipya yanaendelea kuifunua siri ya hayo mambo yaliyotendeka huko Edeni katika 1Yoh 3:12 “si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu.” Kwahiyo kwa kadiri utakavyolitazama jambo hili, lingekuelekeza kuwa Adamu ndiye “yule mwovu” jambo ambalo lingepingana na Maandiko yote, maana hilo lingemfanya Mungu kuwa mwovu pia kwani huyo ndiye Baba wa ukoo wa Adamu, Lk 3:38-40 “wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu. Hata katika ukoo wa Adamu hayumo!!! Basi jambo hilo linatuachia jinsi moja tu, kuwa huyo alikuwa ni mtoto wa Shetani, maana huyo ndiye mwovu tumjuaye kwa kadiri ya Biblia. Basi Shetani anao uwezo wa kuumba? Hapana, hana uwezo. Lakini Maandiko yalituambia kuwa Nyoka anao uzao, naye twafahamu alifanya uovu huko Edeni hata akalaaniwa! Hata tunapojiuliza, kuwa Nyoka huyo aliyekuwa hayawani wa mwitu, tena alikuwa chini ya utawala wa Adamu, basi uasi kwake ungeanzia wapi? Ndipo twafahamu Shetani alimvuvia na kumuongoza kumtongoza Hawa na kuishia katika tendo la ndoa lililomleta Kaini! Adamu anadhihirisha jambo hilo kwa kumwita mkewe Hawa mama wa wote. Hawa alibeba mimba ya Nyoka na Adamu kwa wakati mmoja, na watoto waliozaliwa walikuwa mapacha wa baba wawili tofauti! Mapacha wa jinsi hii nadhani wanaitwa “Superfecundation”.

  Kwa hiyo Kaini ndiye Uzao wa Nyoka. Ukitaka kujua Serpent alikuwaje, basi mtazame Kaini! Huyu ndiyo Hybrid wa kwanza, damu iliyochanganywa, ya binadamu na ya Nyoka. Uzao huu ndimo Ibilisi hujidhihirisha katika namna anavyojidhihirisha Mungu katika wanawe kwa RM. Ni uzao wa kidini na ni wauaji. Hawana Ufunuo wa Neno la Mungu, ni waigizaji wazuri waliojaa nguvu za mauti!

  Ukitaka kujihakikishia jambo hili, rudi tu kule Mwanzo uwatazame hao watoto wawili, Kaini na Habili. Maandiko yanatuambia kuwa hawa walifanya ibada. Ibada ya Kaini ilikataliwa lakini ya Habili ilikubaliwa. Wahubiri wengi hujiaminisha kwamba Kaini alimtolea Mungu sadaka mbovu, lakini si kweli Maandiko hayasemi hivyo. Bali yanafunua kwamba “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini” Ebr 11:4. Basi tulipaswa kujiuliza hiyo imani iliyomuongoza Habili ilikuwa ni nini? Je, kulikuwa na Biblia? Haikuwepo, basi ilikuwaje? Sasa wahubiri wengi huchukulia “Imani” kuwa ni jambo la mwilini naye mkristo anapaswa ajitahidi kulifikia hilo. Bali unapaswa kujiuliza, yeye Habili alijuaje kuwa ile ndiyo sadaka Mungu anayoitaka itolewe? “Kwa Imani”!!! Je, ni kipi au ni Neno gani la Mungu aliloliamini hata akalitimiza kama alivyoambiwa? Maana Biblia inatufunza kuwa, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Huwezi kukurupuka kwa hisia zako ukafanya jambo, halafu ukasema ni kwa Imani, utakataliwa kama Kaini! Kwa hiyo ukweli ni kwamba “IMANI” ni mawasiliano na Mungu ya rohoni, ndipo wewe ungeweza kulifanya likupasalo kama Mungu alivyokuonesha nao ulimwengu ukabaki mdomo wazi wakishangaa nje ya matarajio yao.

  Jamani, tumeelewa kuhusu Imani? Sio mambo ya kukiri Amri Kumi za Mungu, sijui Sabato au kukiri wokovu au kukariri mistari ya Biblia nk. Si hayo, bali ni MAWASILIANO YA SIRI kati ya Mungu na uzao wake au wanae. Naye Mungu katika kulificha hilo akasema ‘Kwa imani” fulani alifanya hiki na kile, nao ulimwengu wa Dini hujitahidi kulipata hilo kwa jitihada dhahiri za mwili; kama kunajisi vyakula, nk.

  Basi Kaini hakuwa na mawasiliano na Mungu toka azaliwe, nao Adamu na Hawa walilijua hilo, walijua kuwa yule ni mnyama kwa asili!

  Iwapo kuna jambo halijaeleweka, basi wapendwa karibuni tuyatafakari Maandiko kama walivyofanya Waberoya, Mungu ni mwingi wa Rehema, atatufunulia hayo sisi watoto tupendao kujifunza Neno lake kwa ajili ya utukufu wake!

  Mbarikiwe nyote

  Ck Lwembe

 25. Mpendwa Milinga!

  Huu ni mwezi wa pili sasa toka nilipokuuliza swali, maandalizi yake ni zaidi ya kujiandaa kwa mtihani wa digrii!!!!

  Milinga upooooo???!!!

 26. Mpendwa Sam,

  Swali nimeliona. Kabla ya kulitolea maoni yangu naomba tena tujikumbushe Mwanzo 3:1-24.

  Hebu soma mstari mmoja mmoja huku ukitafakari kwa kina. Jaribu kujiondoa kwanza katika mtazamo wa kwanza ulionao na ujifanye unataka kuwa na mtazamo wa pili yaani tazama hoja kwa kutokea kona nyingine(Choose another angle of viewing the issue).

  Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

  2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;

  3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.

  4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

  5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

  6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

  7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.

  8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.

  9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?

  10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.

  11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?

  12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.

  13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.

  14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;

  15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

  16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.

  17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

  18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;

  19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

  20 Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.

  21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

  22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;

  23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.

  24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

  Mpendwa nadhani imejikumbusha aya kwa aya na umeweza kutafakari maana ya aya moja hadi nyingine.

  Majibu ya swali lako niko nayaandaa. Nitakutumia soonest.

 27. Mpendwa Milinga!

  Ukipitia bandiko langu utakuta kuna swali nimekuuliza ni vema na inapendeza ukalipitia na kujibu.

  Ubarikiwe

 28. Kwanza, mpendwa Milinga, nakushukuru kwa kunisawazishia kile kilichonichanganya. Maana ukweli ni kwamba nilishindwa kukuelewa kama unakijua unachoongea au jambo hili limekuwa gumu zaidi kwako kiasi sasa umeshindwa kujiwajibisha kwa kauli zako? Lakini asante kwa maelezo haya uliyoyatoa nadhani wengi wamekuelewa vilivyo.

  Jambo la kubadili mitazamo, ni kweli hilo litatusaidia sana kwa kutupa utayari wa kujifunza mambo mapya kadiri yanavyojifunua, lakini kubwa zaidi ni iwapo hayo mapya yanatuletea mabadiliko yoyote ya kiimani. Kwa mfano kujua kuwa sikukuu ya Krismas hiyo tarehe 25 Dec. kuwa ni uongo, hakuzaliwa siku hiyo, au kuwa sikukuu ya Pasaka inapangwa kwa mwandamo wa mwezi, yaani imesetiwa kulingana na mambo ya mizimu, na mambo mengine ya jinsi hiyo, au yanaingia sikio hili na kutokea upande wa pili!!!

  Lakini mambo hayo yanapotolewa mafichoni na kuwekwa wazi, basi mapenzi yetu kwa Neno la Mungu hupimika hapo katika namna ya Imani yetu kwake, kuwa je, twaweza kuwaacha wazazi wetu tukamfuata yeye? Mambo yote huwa ni fursa yetu kuu ya kuyalinganisha mapokeo yanayotushikilia na ukweli wa ki-Maandiko unaojifunua kwetu, nasi kufanya uamuzi ambao kwao, Mungu atahitaji hesabu yake.

  Kwa hiyo, mimi binafsi nimekuelewa ulichokisema na pia ninaheshimu uamuzi ulioufikia, nikiamini kuwa kwa kadiri ya uwezo wako hiki ulichokisema ndicho unachokiona katika Maandiko. Kwa hiyo si suala la kubahatisha, bali ni katika uhalisi wake! Ingawa nina maswali mengi ya kukuuliza, lakini nitajitahidi kuyabana ili niyalete machache yanayoweza kutuangazia zaidi sote tunaofuatilia mjadala huu.

  Kuhusu mijadala kutokumalizika kwa wazo moja, mijadala uliyoirejea kwa uchache, ni kweli inatoa mwanga huo, lakini nadhani mjadala huu ndio unaoonesha kwa nini makubaliano huwa adimu. Maana iwapo sote tunaongozwa na Roho mmoja, tofauti zingetokea wapi? Lakini ni mizao miwili tofauti, ndio maana hali iko hivyo. Wengi wetu hatuyajui hayo. Lakini ndio hivyo, uzao mmoja hutembea kwa Imani katika Neno la Mungu na uzao mwingine hutembea katika akili zake wenyewe. Hebu watazame Kaini na Habili, wote walikuwa wa kidini. Habili akienenda kwa Imani (ufunuo) na Kaini akitumia akili zake. Hata majibu yake yangekuonesha asili yake, kama uyaonavyo leo hii; unamwambia ndugu ili uwe sawa katika ukristo wako, nenda katika hatua inayofuata, kabatizwe katika Jina la Bwana Yesu Kristo kama Injili inavyotutaka ili upate vipawa halisi vya Roho Mtakatifu, kwa jeuri anakwambia, “Tumfuate nani Yesu Mwalimu au Petro mwanafunzi?” akiyapondelea mbali Maandiko katika Mdo 2:38!!

  Sadaka ya Habili aliyoitoa kwa Imani ilikubaliwa maana ililingana na hitaji la Mungu, ili Rehema yake iwafunike, yeye Habili kwa Imani alijua inahitajika Damu imwagike, kulingana na kosa walilotenda wazazi wao la kuchanganya damu. Lakini Kaini alifikiri walikula matunda, akayaleta meengi amtolee Mungu sadaka, akakataliwa! Mungu akiwa ni mwenye haki, alimpa nafasi ya kujisahihisha, Kaini ndiye mtu wa kwanza kuhubiriwa Injili na Mungu mwenyewe! AKAIKATAA Injili hiyo, akayafanya anayoyajua mwenyewe! Na mpaka leo hii uzao wake unaendeleza hayo kwa kujitungia mambo yao kinyume na Maandiko yasemavyo. Basi mizao yote miwili ikiwa ni ya kidini nayo ikijilisha toka katika shina Moja, ule Mzabibu, nayo matawi tukiwa ndio sisi, ibilisi akiwa ame graft matawi yake yatokanayo na mbegu ya hitilafu, unapaswa kuzitegemea tofauti hizo za mitazamo, si kwa uchache, bali kwa wingi!

  Kwa hiyo kimsingi, matawi yaliyokuwa grafted huzalisha mbegu za hitilafu ambazo kwa tabia huhitilafisha Injili kwa kuyaingiza mambo yaliyo kinyume na Mungu na kuyalazimisha kuwa hivyo katika wingi wao, lakini, iwapo Mzabibu huo utatoa tawi lake la asili, tawi hilo litaandika kitabu kingine cha Matendo ya Mitume!!!!

  Basi kwa leo niishie hapo nikikuomba unipe mwanga zaidi kuhusu pale walipokwisha kula hilo tunda, tumeona Nyoka akilaaniwa, na uzao wake ukitabiriwa uadui na uzao wa mwanamke; uzao wa mwanamke tumeuona katika Kristo, Je, Uzao wa Nyoka uko wapi leo hii?

  Ubarikiwe.

 29. Mpendwa Sam,

  Nashukuru Mungu kwamba ungali ukiendeleza mjadala huu. Wakati nimetoa mtazamo wangu mpya kuhusu tunda alilokula Eva na mumwe ulijikuta ukipata mkanganyiko kutokana na kwamba maoni yangu yale yalipishana na mawazo yangu ya awali. Awali nilisema kwamba Biblia wakti mwingine hutumia mafumbo na lugha yenye maana fiche (figurative language).

  Baadaye nikaja nikasema kwamba Eva na mumwe walikula matunda halisi ya kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Nikasisitiza kwamba bustani ile ilikuwa imetengenezwa kwa makusudi ya kumfanya Adam na mkewe waishi milele na kuzaa bila shida ya uchungu au utungu wala bila kutokwa jasho.

  Kutokana na mtazamo huo naona kama wewe nilikuchanganya zaidi. Naomba nikwambie kwamba hiyo ilitokana na juhudi nilizofanya zaidi za kulitafakari upya Neno. Nikazidi kuona kuwa ukweli waweza kuwa huo kwamba walikula matunda ya kawaida kabisa na wala siyo fumbo. Hadi sasa msimamo wangu bado ni huo pamoja na kwamba maelezo yako yalinipa changamoto mpya bado niliona kuwa yalifika mahali yakaacha kunishawishi nikubali kile ulichokuwa unatufundisha.

  Aidha, napenda kutaja hapa kuwa watu wanapaswa kujifunza kubadili mitizimo hasa linapokuja swala la mada ambazo zina mitazamo mbalimbali makanisani au kwa wanazuoni wa maandiko na wanatheolojia.

  Kwa mfano mada hizi hadi leo zina mitazamo mingi makanisani na kwa wanazuoni wa maandiko ya Biblia:

  1. Mada kuhusu baraka au laana miongoni mwa waliokoka. Mada hii kuna wanaoamini kwamba ukiokoka wewe huwezi kuwa chini ya laana tena. Lakini wapo waaminio kuwa inawezekana.

  2. Mada ya kuimba kwa kucheza kanisani au mikutano ya Injili. Wapo wanaopiga marufuku kucheza kanisani huku wengine wakishabikia. Wote wanayo maandiko ya kutumia kutetea msimamo wao.

  3. Mada kuhusu mwanamke au mwanaume kujichua yaani “masturbation” ina mitazamo mingi. Wapo wanaoamini kuwa ni dhambi kujichua mwanamke au punyeto mwanaume huku wengine wakiwa hawaamini kuwa ni dhambi.

  4. Mada kuhusu mavazi ya mwanamke na mwanaume hasa suruali. Wapo wanaosema ni dhambi mwanamke kuvaa suruali huku wengine wakisema siyo dhambi na wanawaacha wanawake wavae suruali siyo mtaani tu hata kanisani.

  5. Mada kuhusu TUNDA alilokula Adam na Eva bado ina mitazamo mingi. Wapo wanaosema walikula matunda ya kawaida, wapo wanaosema walifanya tendo la kuasi tu na wala siyo matunda, wapo wasemao hivi na vile………

  6. Mada kuhusu mwanamke kukaa kimywa kanisani na kwamba hapaswi hata kuhubiri wala kuwa mchungaji au kiongozi kanisani, ina mjadala sana. Ina pande nyingi za wanaounga na wasiounga mkono mwanamke kufanya huduma kanisani.

  7. Mada kuhusu uzazi wa mpango kwa kutumia sayansi ya kisasa. Wapo wanaokubali na wanaopinga. wote wanayo maandiko ya kutetea hoja zao.

  8. Mada ya kutumia dawa za asili tofauti na za hospitalini, wapo wanaosema ni dhambi kutumia dawa za asili kutibu maradhi huku wengine wakizitumia na kusema siyo dhambi. Na mada nyingine nyingi……….

  Kwa hiyo, kila inapotokea mada kama hizi kuwekwa hewani, ni vyema kujitazama vyema uko upande upi. Unashauriwa kujipima kama uko sawa. Kama utaona kuwa msimamo huo siyo sahihi mimi nakushauri ubadilishe mtazamo. Siyo dhambi kabisa kubadilisha mtazamo fulani katika maandiko. Huku ndiko kukua kiroho.

  Mada hizo zenye mitazamo mingi baina ya wakristo mara nyingi huwa haipati mwafaka kwenye mijadala na hii hutokana na kwamba wakristo wengi huwa tunadhani kuwa tumeshafahamu vyema maandiko na hivyo kudhania kuwa kile tulichokuwa tunaelewa jana kuwa ndiyo ukweli basi hakiwezi kubadilika. Wengi huendeleaa kusimamia mitazamo yao mpaka kufa. Hii nadhani ni hatari.

  Ubarikiwe.

 30. Ndugu Robert,
  Shalom!
  Kwanza, nikuhakikishie kuwa hujanikwaza kabisa, na pia ninaamini kuwa Maandiko yako kama yalivyo, kwa hiyo kwamba yako wazi au yamefungwa, hilo litategemea zaidi jinsi unavyoyaona wewe mwenyewe, kwani mwisho wa siku kila mtu huwa kile anachoamini! Ninaamini pia tupo hapa kwa ajili ya kufellowship Neno la Mungu, na si kutetea misimimamo yetu kwa kulazimisha chochote kile maana hayo ni mambo ya madhehebuni, lakini hapa tuko katika uhuru uliojikita katika mipaka ya Neno la Mungu! Kwa hiyo iwapo nilichokiona katika Maandiko kimekutatiza, na huna jibu la ki-Maandiko, kukaa kimya pia hukupa muda wa kutafakari! Mimi binafsi ninasoma humu katika blogu hii mada nyingi sana, zile ninazowiwa kuchangia nafanya hivyo kwa moyo wangu wote, katika kujifunza na kusahihishana kulingana na Maandiko, kwa hiyo nafaidika saana, nimepata views nyingi tofauti tofauti za mada mbali mbali!!

  Ninacho kushauri, usikate tamaa katika kujifunza, wala usisusie mjadala kwa vile tu mtazamo wako fulani hajaukubali, bali katika hali hizo rudi katika Maandiko uyakague tena with an open mind!
  Bwana akubariki na akutie nguvu zake!

 31. Ndugu Sam si kila andiko kwenye biblia limefumbwa mengine yako wazi kabisa.Mimi si mfungwa wa mapokeo kama unavyodhani wewe huko nimetoka muda mwingi tu baada ya kukombolewa kwa damu ya Yesu na naomba kama nimekukwaza unisamehe. Kwa faida yangu mwenyewe nakaa pembeni kama baadhi ya wenzangu hapo juu walivyoamua kujitoa katika mjadala huu. Mungu akubariki.

 32. Ndugu Robert, mimi nadhani ni vizuri kuchukua wasaa kidogo unapotaka kuchangia katika mada ili tunapojadili tuweze kupata faida ya mijadala.

  Unapozungumzia kuyabadili maana ya Maandiko katika kuyachunguza tunakokufanya, sijui nikujibu nini. Kwani nikiyatazama uliyoyaandika inanizidishia kuamini kuwa unajaribu kuzungumzia jambo usilo na ujuzi nalo! Hebu kitazame ulichokiandika: “…ndiyo maana nimesema hapo juu kuwa hii ni bustani na tunda ni tunda kweli la kuchuma na siyo kama ulivyoeleza kwamba mti mwingine ni Hawa.” Kwa hiyo iwapo tutakufuata wewe na kuisoma Biblia katika jinsi hiyo itaeleweka kweli? Yaani unatuambia kuwa tunaposoma vifungu kama hiki cha Yh 15:1 kinachosema, “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, …” tuelewe kuwa Kristo alikuwa ni mti wa mzabibu! Huo kama si upagani ni nini? Au Kristo anaposema katika Yh 6:35 “… Iam the bread of life…” kwamba Kristo ni mkate, upi, wa Bakhresa???

  Mwanzo 3:3; hapo ndipo unapopaswa kwenda kujipima kama unaamini Neno la Mungu au u mfungwa wa mapokeo!! Maana unachotueleza ni sawa na mtu anaye ukimbia Ukweli kwa kujiaminisha katika jambo lisilo na tija hasa katika Wokovu! Utasemaje kuwa wewe umempokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako wakati hata Kristo mwenyewe humfahamu! Jaribu kuwa na subira kuyatafakari kwa kina unayoelezwa ukiyakagua katika Maandiko ili kuyaona kiroho kama yanashabihiana na Injili. Vinginevyo hebu nipe jibu la kiMaandiko, Uzao wa Nyoka uko wapi leo hii?? Maana tumeuona ukitajwa katika Agano Jipya na kutabiriwa kuwepo katika Agano la Kale, na Biblia imesema Nyoka alikuwa hayawani wa mwitu!

  Wokovu sio mwisho wa vita, bali ni katika wokovu ndipo tunaposajiliwa kuipigania Imani. Kwa hiyo uaskari wako utakuwa na mashaka iwapo hata Adui humjui sawa sawa! Ndio maana makanisa yamejaa mitafaruku mashindano, kusengenyana, wivu na mambo mengine ya ajabu mengi tu lakini hakuna anayejua chanzo ni nini! Huo wokovu tunaoudai kuwa nao hata wakati mwingine tunatamani kukaa chini na kulia machozi, eti unaambiwa “Shetani alisha kufa” halafu watu wanakaa hapo na wanabarikiwa katika wokovu wa jinsi hiyo, na makundi mengine nayo kila moja na staili yake, ila kuonana wajinga mmoja kwa mwingine ndio kumetawala!! Jibu la mambo hayo utalipata wapi, kwa nabii wa kanisani kwenu? Rudi katika Maandiko, yaamini hayo, Mungu atakufunulia ndipo waweza kukaa chini na kuwaombea ndugu zako katika upendo wa kiungu na sio mambo ya kinafiki yaliyotujaa!! Mapokeo yamelivuruga kanisa na kulipa “wokovu mbadala” na “Roho Mtakatifu mbadala” kwa kuigeuza Imani yetu kutoka katika neno la Mungu na kutupeleka katika imani iliyojengeka juu ya vipawa!!

  Ubarikiwe ndugu Robert!!!

 33. Ndugu yangu Sam,vifungu nilivyoviweka hapo juu mimi naamini kwangu vinaeleweka vizuri ndiyo maana nimesema hapo juu kuwa hii ni bustani na tunda ni tunda kweli la kuchuma na siyo kama ulivyoeleza kwamba mti mwingine ni Hawa.Mimi sidhani kama kuyachunguza maandiko matakatifu ni kubadilisha maana yake.
  Mimi naamini wapo wapendwa walionielewa vizuri,hilo la wafalme na wachanga siwezi kulizungumzia. Kama sikueleweka kwa wote,uwanja uko wazi nao pia watasema wenyewe. Ubarikiwe

 34. Ndugu Robert,
  Vifungu vyote ulivyo vinukuu, ninaamini umevitoa katika Biblia. Sina uhakika kama unavielewa vina maana gani kwako, kwani kwa kauli yako mwenyewe huoni mantiki ya kuvirejea maana havikusaidii kumjua Mungu! Nimeshindwa kukielewa unachokisema maana unazungumzia kumjua Mungu halafu unaogopa kulichunguza Neno lake, sijui utamjua Mungu yupi, maana yeye ninpamoja na hilo Neno unaloliogopa kulichunguza!!

  Mungu mwenyewe unayemzungumzia anakwambia hivi: Mithali 25:2 “Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa wafalme kulichunguza jambo.” Sijajua uko katika kundi gani, la hao wafalme wenye kuyachunguza mambo au wachanga wanaosubiri kuletewa? Kwa vile huna uwezo wa kuyachunguza, ninaamini utakuwa ni mchanga, basi wasubiri wafalme watakupa majibu yatakayokupeleka mbele zaidi wakikuondolea uoga katika nafsi yako na kukuimarisha katika wokovu ulioukiri!
  Ubarikiwe

 35. Mwz 2:15-17 hapakuwa na mche wa kondeni bado,wala
  mboga ya kondeni haijachipua bado, kwa maana BWANA
  Mungu hajainyeshea nchi mvua,wala hapana mtu wa kuilima ardhi;ukungu ukapanda katika nchi,ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.
  Mwz 2:8-9 BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni,akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.BWANA akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa;na mti
  wa uzima katikati ya bustani,na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
  Mwz 15-17 BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu,akamweka katika bustani ya Edeni,ailime na kuitunza.BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu,akisema,Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,walakini matunda ya ujuzi wa mema na mabaya usile,kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
  Wapendwa katika BWANA mimi naona hii ni bustani na naona mtu anawekwa na Mungu kuilima bustani hii.Aina ya miti ndiyo hiyo imetajwa hapo na maagizo kumhusu huyu mtu wa kuilima au kuitunza bustani hii ndiyo hayo hapo yametolewa na BWANA Mungu.
  Ujumbe wangu: Ni mti upi au miti ilikuwa mingapi haitusaidii kumjua Mungu zaidi au kujua neno lake zaidi.Theolojia za nini?
  Mbarikiwe

 36. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata mjadala huu kwenye mtandao, ki ukweli nimejikuta nimenogewa mpaka nime stop kazi. Mungu awabariki wachangiaji wote

 37. Mpendwa Millinga,

  Shalom!
  Kwa kadri tunavyoendelea na mada hii, katika kuifuatilia michango inayotolewa, ile mitazamo, michango yako imenichanganya kidogo, hebu yaangalie haya mawazo uliyotuletea ili utupambanulie tupate kujua ni nini unachotaka kutuambia:

  Kwa upande mmoja unasema:
  1. Biblia imeandikwa wakati mwingine kwa kutumia lugha za picha (Figurative language) siyo kila mahala Biblia inapotaja neno fulani lina maana halisi inayotumiwa na wanadam. Kwa Mfano wasomaji wa Kitabu cha Nabii Daniel na kile cha Ufunuo wa Yohana watakubaliana na mimi. Kuna mahala Biblia inamtaja mwanamke Kahaba lakini haimaanishi mwanamke kahaba kama tuliowazoea mtaani wakijiuza miili yao. Biblia inamaana tofauti kabisa.
  2. Yesu anaposema mimi ndimi mkate wa uzima, au mimi ndimi mzabibu wa kweli, au anapotoa mfano wa Kondoo na mbuzi au wanawali kumi, nk msomaji asiyeelewa haraka anaweza akaanza kuwaza mikate tunayokula kila siku kwamba Yesu alimaanisha yeye ni mkate kama huu tunaokula. ITAKUWA AJABU SANA KUMSIKIA MHUBIRI ANAYETAFSIRI MAANDIKO HIVYO.
  3. Tunapaswa kuelewa jambo lingine kwamba Biblia iliandikwa kwa kutumia mafumbo na tamathali za semi.

  Na kwa upande wa pili unasema hivi:
  Mungu alipomwumba Adam aliotesha miti ya kila aina. Miti iliyooteshwa na Mungu ni HALISI KABISA wala siyo FUMBO linalohitaji tafsiri ya kiroho. Mungu alipoumba Jua, Mwezi, Nyota, wanyama, ndege, majani, anga, maji, nk vyote hivyo ni vitu halisi kabisa. Haihitaji mtaalam anayejua kufumbua mafumbo ya Mungu au maandiko yake aje atueleze kwamba Maandiko yasemapo Mungu aliumba Jua au Mwezi ina maana ya kitu fulani. Nadhani hapa wapendwa wote tunakubaliana.

  Tatizo kubwa limekuwa kwenye tunda alilokula Adam na Mkewe Eva. Naomba tuelewane kwamba Mungu alipoumba Miti ya kawaida na ile ya matunda Biblia inamaanisha kitu hicho wala siyo FUMBO LA IMANI. Kama matunda aliyokula Eva na Adam ni fumbo la Imani kwa nini Jua na Mwezi, wanyama na Nyota, nk hatusemi navyo kuwa ni FUMBO LA IMANI???

  Leo Biblia imeandikwa kwa Mafumbo, kesho haijaandikwa kwa Mafumbo! Basi lile ulilosema kuwa, “ITAKUWA AJABU SANA KUMSIKIA MHUBIRI ANAYETAFSIRI MAANDIKO HIVYO.” Nadhani AJABU yenyewe ndio hii tunayoiona katika haya mahubiri!!

  Mungu anatuhitaji tumtegemee yeye na si akili zetu, Mithali 3:5. Tunapojaribu kutoka na mawazo yetu, katika jambo lake, basi tufahamu kuwa tutaishia katika aibu yenye kutuvunja moyo. Mwili huongozwa na kichwa kimoja tu, tunapojibandika kichwa cha pili, yaani mawazo yetu tukiyachanganya na Neno la Mungu, hilo huzaa Fundisho ambalo kitambo kidogo hutambulika kama Mapokeo ambayo husimama badala ya Neno la Mungu. Nayo Mapokeo, kama Farao, HAYAKUBALI KUKUACHILIA UONDOKE!

  Bwana atusaidie!

 38. Millinga!

  Umenifurahisha saaana!
  Uwezo wako wa kufikiri ni mkubwa sana, yaani imagination yako!! You are so good!!

  Jambo zuri ni kwamba hauko mbali na ukweli. Kwa vile unaamini kwa moyo wako na kwa ushawishi wa Maandiko kuwa Hawa alichuma natural fruit ambalo lilikuwa na sumu iliyowaletea “health reaction” iliyowafanya wajione wako uchi, ukifanikiwa kulijua hilo tunda, utakuwa tajiri wa kupindukia! Maana wazazi wote watakukimbilia ili wawape binti zao wanao tembea nusu uchi, tunda hilo tena ili wajitambue! Ila katika mtiririko uliouleta, nina uhakika ulisahau kumalizia kuwa ule mti ulibaki Edeni kwa hiyo tutakaporudishwa huko ndipo tutaujua!

 39. Mpendwa Sam,
  Nimekupata vilivyo katika maelezo na maswali yako uliyouliza, naomba nikujibu tu kwa kifupi kwamba, ukiipitia kwa makini misitari ile niliyoinukuu kutoka katika Biblia takatifu, kwenye ile post yangu iliyotangulia, utapata majibu ya maswali yako yote. Hata hivyo, nitarudia kwa ufupi kujibu maswali yako kama ifuatavyo:-

  1.Lengo la Mungu,ilikuwa na ni kuwa, Mtu aishi kwa raha milele, ndiyo maana Mungu alimtahadharisha Adamu, akamuonya asile matunda yale ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ili apate kuishi. Mw.2:17

  2. Mungu anaendelea kumtumia Mwanadamu, katika mpango wake wote wa wokovu juu ya wanadamu ili waishi milele, Mk.16:15-16
  3.Ndivyo, Shetani aliamua kumtumia nyoka kwa welevu wake.Mw.3:1. Welevu ni busara, kama hilo halikuwa na maana yoyote Biblia isingelisema, kuwa nyoka alikuwa Mwelevu, hata kwa hekima ya kawaida tu, haiwezekani asiye na ustadi kupewa kazi inayohitaji ustadi aifanye!
  Hata Bwana Yesu, aliliona hilo, na kuwahimiza wanafunzi wake, wakati alipowatuma kazi ya injili, alisema wawe na Busara kama Nyoka. Mt.10:16
  4.Azima ya Shetani kumtumia nyoka mwelevu ni kuhakikisha kwamba anafanikiwa kuuharibu mpango wa Mungu, kumuhusu mwanadau, maana hakukubaliana nao tangu mwanzo,Mw.3:1

  5. Sijaelewa una maana gani kuuliza kuwa, mnyama ana hiari? Nyoka anayezungumziwa na Biblia ni Yule aliyekuwemo bustanini, aliyeweza kuhoji,kuzungumza na kufikiri, maana Biblia inasema alikuwa mweluvu, Mw.3:1. Kiumbe kama huyu lazima awe na hiari maana ana akili, utashi na busara!

  6.Biblia inamtaja Shetani kuwa ni Nyoka ndivyo inavyojulikana. Hilo ndilo jina lake analojulikana nalo Uf. 12:3-4, 12:9. Ambapo, Yesu (Mungu) hujulikana kama Mtu, sehemu kadhaa katika Biblia zina mtaja, kama, mzee wa siku, mwana wa adamu n.k Mt.1:23, 8:20, 12:8.

  7.Kwa lugha nyepesi, Kinyume cha Hiari ni Utumwa, Mwanadamu tangu kuumbwa kwake ni kiumbe huru, lakini mtu akiamua kwa hiari yake kumtumikia Bwana Fulani, huwa hana hiari yake mwenyewe, ispokuwa ya huyo Bwana wake, kwa kifupi huwa Mtumwa na mtumwa kamwe hana hiari yake mwenyewe, akifanya kwa hiari yake, basi amekwisha asi!. Rum.1:1, 8:14, Mith.16:1. Vivyo hivyo na kwa viumbe wengine wote. Rum.8:20-21

  Endelea kubarikiwa na BWANA Yesu.

 40. Wapendwa,

  Kama nilivowahi kusema kuwa mada hii kwangu ni ngumu au chakula kigumu naomba maoni yangu yabakie kama yalivyo endapo sitawaridhisha wengi wanaofuatilia mada hii.

  ADAM NA EVA WALIKULA MATUNDA YA KAWAIDA.

  Kwa kujifunza kwangu maandiko na uelewa wangu mdogo, nadhani na baadaye nitaweka msimamo kimantikia na kimofolojia kwamba Hawa na Adam walikula matunda ya kawaida kabisa kutoka kwenye mti wa matunda ya kawaida kama ilivyo malimao au maembe.

  Huenda kinachotuzuia kuelewa mada hii haraka ni kwa sababu Biblia haikulitaja tunda lenyewe ni aina gani.

  Kwa kutafakari zaidi mimi naona walikula tunda lenye madhara kiafya yaani tunda lenye sumu. Inaonekana kwamba kulikuwa na mti uliokuwa na matunda ya sumu. Sumu ile ndiyo iliyoingia mwilini mwao na kusababisha kinga za mwili wa Eva na Adam kupungua kabisa hadi wakaishi miaka 930 badala ya kuishi milele kama wangeendelea kula matunda yasiyo na sumu yaani matunda ya mti wa uzima.

  Najaribu kujifunza kwamba huenda mtazamo wangu ukawa sahihi kutokana na mazingira ya Bustani ya EDENI. Mungu alipomwumba Adam aliotesha miti ya kila aina. Miti iliyooteshwa na Mungu ni HALISI KABISA wala siyo FUMBO linalohitaji tafsiri ya kiroho. Mungu alipoumba Jua, Mwezi, Nyota, wanyama, ndege, majani, anga, maji, nk vyote hivyo ni vitu halisi kabisa. Haihitaji mtaalam anayejua kufumbua mafumbo ya Mungu au maandiko yake aje atueleze kwamba Maandiko yasemapo Mungu aliumba Jua au Mwezi ina maana ya kitu fulani. Nadhani hapa wapendwa wote tunakubaliana.

  Tatizo kubwa limekuwa kwenye tunda alilokula Adam na Mkewe Eva. Naomba tuelewane kwamba Mungu alipoumba Miti ya kawaida na ile ya matunda Biblia inamaanisha kitu hicho wala siyo FUMBO LA IMANI. Kama matunda aliyokula Eva na Adam ni fumbo la Imani kwa nini Jua na Mwezi, wanyama na Nyota, nk hatusemi navyo kuwa ni FUMBO LA IMANI???

  Naamini kwamba Eva na Adam walipewa Bustani nzuri yenye kila aina ya miti ya Matunda kama ambavyo watu wengi hutengeneza bustani zao nzuri kando ya makazi ya nyumba zao. Bustani ile kama tunavyoisoma ilikuwa bustani halisi (natural fruit trees gardern) na ilikuwa inazunguka makazi yao. Historia inakubaliana na maandiko kwamba mwanadamu wa kale alikula matunda tu tena bila kuyapika wala kuyatengeneza kama ilivyo leo hii.

  Kama kawaida ya mtu yeyote akienda bustanini atakutana na miti yenye matunda yafaayo kuliwa na yasiyofaa kuliwa. Lakini huwezi kujua Tunda Jema lifaalo kuliwa ni lipi kama hujaambiwa kwamba Mti fulani matunda yake ni sumu na hayafai kuliwa. Kwa nini sasa uitwe “Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya?”

  Mungu aliuita jina hilo akimaanisha kwamba UNAYO SUMU ISIYOFAA KWA AFYA YA ADAM NA MKEWE. Mfano mtoto hawezi kujua jema na baya hadi aambiwe na wazazi wake kwamba hili ni baya na hili ni zuri. Kwa Adam pia ilikuwa hivyo. Mtoto akigusa moto ukamuunguza ndipo anapotambua kwamba moto ni mbaya na unaunguza. Mtoto akililia wembe mpatie, ukimkata ndipo atajua jema na baya. Miti yenye sumu kwa afya ya mwanadamu imekuwepo tangu kale hadi sasa. Kuna miti yenye matunda yafaayo kuliwa na kuna miti haifai kabisa. Kuna makomamanga mwitu na makomamanga ya kuliwa. Mungu alimkataza Adam asile matunda yenye sumu ili asije akafa kimwili kabisa kutokana na sumu iliyokuwemo katika miti ile.

  Umewahi kutembelea Bustani yoyote yenye mchanganyiko wa miti? Unajuaje kwamba mti fulani matunda yake yanafaa kwa kuliwa au la? Nani aliyekufundisha kwamba maembe hayana sumu na kwamba yafaa kwa kuliwa? Adam aliambiwa ale matunda ya miti yote isipkuwa mti wenye matunda ya sumu yaani “ujuzi wa mema na mabaya”.

  Ukweli ni kwamba ukila matunda yenye madhara kwako ndipo utaelewa jema na baya kama ilivyo kwa mtoto. Kama unakunywa maji yasiyochemshwa kwa muda mrefu labda zaidi ya miaka 10 na hujawahi kuugua homa ya matumbo au kuhara damu, hautajua maji mabaya au maji mema hadi utakapopatwa na homa ya matumbo yaani “typhod fever” na hapo ndipo utajua jema na baya kuhusu maji ya kunywa.

  Dhambi waliyoifanya Adam na mwenzie Eva ni kula matunda yenye athari kwa afya zao ambazo Mungu alikuwa amekusudia waishi milele bila kufa wala kuugua kabisa. Adam na Eva waliasi maagizo ya Mungu kwa kula chakula chenye sumu yaani matunda yasiyofaa kwa afya ya mwanadamu. Walipokula tu wote madhara ya sumu ya matunda yale (ambayo Biblia haikuyataja) walipata “health reaction” ambayo Biblia imesema ‘wakajiona wako uchi”. Mungu Baba alipowatembelea jioni akawakuta wako hoi kiafya wakiwa wamejificha vichakani asiwaone maana walikuwa tayari wana mabadiliko ya kiafya yaliyowafanya wasikie hatia moyoni mpaka kuamua kujificha.

  Jaribu kufikiria mtu anapokula chakula chenye sumu. Mwili unaweza kutoa “reaction” hapo hapo au reaction ikawa ya muda mrefu. Matunda waliyokula Adam na mkewe yaliwasababishia madhara yafuatayo:

  1. Kutoweza kuishi tena milele wakiwa katika mwili waliopewa kwani sumu ilikuwa imeshaingia katika mfumo wote wa damu yao.

  2. Mwanamke alipata madhara ya kizazi kiasi kwamba hangeweza kuzaa watoto mpaka apate utungu. Hii inamaana kwamba kama yasingekuwa madhara ya sumu toka kwenye matunda waliyokula angezaa watoto bila uchungu wala utungu.

  3. Mwanamume kutokwa jasho awapo kazini. Kabla ya sumu ile mwanadam alikuwa hatokwi jasho mwilini hata akifanya kazi kubwa kivipi.

  4. Matunda yale yalisababisha homoni za kike za Eva kubadilika kiasi kwamba homoni zake zitaendelea kuwaka kuelekea kwa Adam tofauti na hali ya awali kabla ya kula matunda yale.

  5. Baadhi ya majukumu ya Adam yaliongezeka tofauti na awali kwani ilibidi Mungu amwambie ukweli kwamba , “ASIYEFANYA KAZI ASILE” kwani awali walikuwa wamepangiwa kuishi na kula bila kufanya kazi. Kufanya kazi ilikuwa kama njia ya kuendelea kuufanya mwili uwe unatoa sumu kadhaa zilizotokana na matunda aliyokula.

  6. Uwezo wa kukasirika na kuchukua vilianza kujitokeza. Kushutumiana na kusalitiana vilianza mara moja baada ya sumu ile ya matunda.

  Nionavyo mimi hayo ndiyo baadhi ya madhara waliyoyapata kwa kula matunda yasiyoruhusiwa kuliwa na mwanadamu.

  Shetani akiwa katika sura ya nyoka alimkuta Eva akiwa bustanini akichuma matunda yafaayo kuliwa ikiwa ni pamoja na mti wa uzima. Mti huo wa uzima wenyewe ulikuwa maalum kabisa kwa ajili ya kuongeza “body immune system” ya Adam na Eva. Mti ule ulikuwa maalum kuwa tiba ya kuwafanya waule ili waendelee kuishi milele na milele. Mti huu umefananishwa na Kristo ambaye mtu akimpata anapata Uzima wa Milele wa roho yake tu ila siyo mwili huu. Mti ule wa bustani ya Adam wenyewe ulikuwa na lengo la kuwafanya Adam na Eva na watoto wao ambao wangezaliwa baadaye waule tu kwa nia ya kupata “Endless immunity” kwenye miili yao. Mti huu unatajwa pia katika Ufunuo wa Yohana kwamba watu watakula mti huo wa uzima na hawataugua kabisa kwa kula majani/matunda ya mti huo. Huenda hoja hii ikawa na mjadala (long and hot debate) kwamba je mbinguni kutakuwa na kula tena matunda au kunywa? Naamini maandiko yanatoa majibu.

  Nyoka alipomkuta Eva bustanini alimwambia kwamba aachane na maagizo ya kwamba kama angekula yale matunda angekufa. Eva aliyatazama yale matunda akaona kwamba yanafaa kuliwa. Ni kama ambavyo unaweza kumkataza mtoto asiguse moto, lakini unamwona mtoto anazidi kuukodolea macho moto na kuuona kwamba moto huo wafaa kwa kuchezea. Mara tu anapoanza kuukamata moto huo, unamuunguza na ndipo ghafla unaona anaanza kulia kwa huzuni akijua jema na baya kuhusu moto. Hawezi kurudia tena. Nina hakika kama Adam angepewa nafasi ya kurudi kushi pale bustanini hangerudia kula matunda yenye sumu.

  Kwa hiyo naomba niondoke hewani hapa nikiendelea kuamini kwamba Eva na mumewe walikula “natural fruits” yaliyokuwa hayafai kwa afya zao na madhara yake yakawa kama nilivyoeleza hapo awali.

  Nabakia nikijifunza zaidi kutoka kwa wengine huku nikiendelea kufanya utafiti zaidi kuhusu mada hii.

 41. Katika kuiangalia Hiari au uhuru licha ya wewe kuvichanganya, bado hayo yako wazi.

  Unajua, ndugu Mabinza, huo uhuru au hiari, unao uzungumzia, nadhani ndio tatizo letu kuu. Kwanza, ili kufika katika uelewa wa jambo lolote lile, kuyajua majira au mwenendo wake ni muhimu. Kwa hiyo hata kuujua mwenendo wa kanisa kimajira, hilo lingesaidia kuweza kuukagua huo uhuru au hiari uliyonayo ili kuiona iwapo inaendana na majira ya kanisa. Katika kuyajua majira hayo itatusaidia kujua kiwango cha imani tuliyonayo.

  Israeli wakiwa ni mfano wa kanisa, basi kwa kuwaangalia wao twaweza kuyajua majira tuliyomo. Israeli, safari yao ilikuwa na sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ilikuwa ni Misri, huko utumwani, wakiwatumikia Wamisri. Kwa kanisa, huo ni ule wakati tulipokuwa huko dhambini tukitumikishwa pia. Katika hatua hiyo ya kwanza, lile kundi yaani kanisa, lilifika katika sehemu ambayo ilikuwa ni ukingoni mwa ile hatua ya kwanza, hapo ilibidi livushwe mautini ili kuingia katika hatua ya pili. Sasa tunapolitazama jambo hili la kuvushwa, huenda lingetupa mwanga zaidi juu ya hali ya hao waliovushwa. Kundi hili lilipofika ukingoni mwa bahari, ikiwakilisha KIFO, tunasoma kuwa NGUZO YA MOTO na WINGU vilirudi nyuma na kutulia katikati ya ya kundi la Israeli na Wamisri, na kisha Musa kuipiga fimbo bahari na kuwaruhusu Israeli kupita! Kanisa lilitangulia mbele!!

  Nao walipovushwa, tunawaona kusanyiko wakiwa ni wenye kushindana na hata tunawaona wengine wakiitaka nafasi ya Musa, wakiamini kuwa Mungu yuko nao! Kanisa likiwa katika nafasi hiyo, ndipo nalo tunaliona likiparaganyika na kujizalisha katika madhebu, likijiwakilisha katika kile kiwango cha kuamini kuwa kila mmoja yuko na Mungu!! Nao mparaganyiko huo hutokana na manunguniko na mwishowe kujitenga, kila mmoja akilitangulia Neno la Mungu, Musa! Hata leo hii tunaendelea katika kiwango hicho, kila kundi likija na ufunuo wake kuhusu Neno la Mungu na wakijiaminisha kuwa hayo ni mapenzi yake! Hata tunaliona kundi lote la wale waliovushwa likifia jangwani, kule kusiko na ufufuo!!! Katika ulinganishi na hali ya kanisa leo hii, hilo lingetuonesha kuwa madhehebu yetu, hayana uwezo wa kutuingiza Kaanani au mbinguni, kutokana na msingi wake kuwa dhaifu. Maana misingi hiyo imejengwa katika manung’uniko na mitafaruku, vyote vikiwa nje ya mapenzi ya Mungu. Hata sote si wageni wa usemi huu, “Dhehebu halikupeleki mbinguni!” Basi usemi kama huu ni lazima uwe umezaliwa kutokana na udhaifu wa kiimani ulioonekana katika madhehebu yetu!! Hayo yanatendeka jangwani!!!

  Sasa katika kutoka katika hatua hii ya pili na kuingia katika hatua ya mwisho, yaani Kaanani, yaani Roho Mtakatifu, hapa tunaona, baada ya lile kundi lote lililotoka Misri kufia jangwani kutokana na kumtilia shaka Mungu, sasa tunawaona watoto wao waliozaliwa jangwani, wakiwa ni wasikivu wa Neno la Mungu, Musa na kukabidhiwa kwa Joshua ambaye ni Roho Mtakatifu. Hao ndio kundi jipya lililoingia Kaanani. Ilipofika wakati wa kuingia, hao walitanguliwa mbele na Sanduku la Agano, Neno la Mungu walipovushwa Jordani – KIFO! Hilo liliashiria uongozi wa Roho Mtakatifu. Kundi lote likijiwakilisha chini ya kiongozi mmoja Joshua, katika furaha ya kuongozwa! Kundi hilo halikukubali manung’uniko wala uasi wa namna yoyote ile. Yeyote aliyejaribu kuwa tofauti aliuawa! Huo ndio ule mfano wa kifo kinachompata yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu!! Kwa hiyo imani iliyoko kwa kanisa katika hatua hii ni tofauti na ile iliyoko kwa kanisa linapokuwa katika hatua ya pili, hiyo yenye kulibishia Neno la Mungu. Unapojazwa Roho Mtakatifu, yeye kama Joshua, hukuongoza katika nchi hiyo mpya usiyoijua, unayopewa kwa ajili ya urithi wako wa Ufalme wa Mungu!

  Basi ndugu yangu Mabinza, hali ya imani kwetu iko kama hivyo, kidhehebu, na mbele kidogo tunapojitoa katika kulichukua Neno lote, hutuleta katika kiwango cha kutawaliwa kikamilifu na Roho Mtakatifu! Ndio maana nilikuambia hapo nyuma usilitangulie Neno, jaribu kulifuata, maana hatua hii tuliyomo ni ya hatari kidogo!!

  Labda nirudie tu kukuambia kuwa nimeshindwa kuendelea kukujibu, labda utakapoamua kulitariki Fundisho ulilonalo kwanza, hata kama ni taraka rejea, ndipo uyatazame vizuri niliyoyaandika na pia uyatazame Maandiko kama yanavyojifunua, ukiona umeyaelewa, basi nunua sumu ya panya ulilishe hilo fundisho ili usilirejee tena, au la basi litupilie mbali hili na kuendelea na hilo unalolijua! Uamuzi huo utayaweka maswali yoyote yale katika mtiririko unaoweza kueleweka na kujibiwa ipaswavyo!

  Ubarikiwe, ndugu yangu Mabinza!

 42. Mpendwa Mabinza,

  Kwa vile sote tunajifunza, naona ni vyema nami nikayapitia haya uliyoyaleta ili nami niweze kupata undani wa Fundisho hilo, ambalo kimsingi naamini ndilo lililopo katika makanisa yetu. Basi kwa vile naona wewe uko katika ujuzi wa hilo, naomba usinichoke katika maswali ninayoweza kukuuliza pale itakaponibidi ili kunipanua uelewa.

  Nikikunukuu maelezo yako, pale unapoielezea ‘vita’ kati ya Mungu na Shetani, umesema, “Kwa hiyo, Mungu ili kufikisha lengo lake, aliendelea kumtumia mwanadamu ambapo shetani kwa kuwa hana alichoumba ili kiwe mpango wake, huvamia kila kiumbe , hivyo akaamua amtumie Nyoka, maana Nyoka alikuwa mwelevu na hivyo angefanikisha azima ya shetani.”
  Swali:
  1. Lengo ambalo Mungu alitaka kulifikisha, ni lipi?
  2. Mungu aliendelea kumtumia mwanadamu, katika jambo lipi?
  3. Kama nimekuelewa vizuri, umesema Shetani alimchagua Nyoka kutokana na werevu wake, Ndivyo?
  4. Azma ya Shetani iliyomplelekea kumchagua Nyoka, ilikuwa ni nini?

  Pia, umeendelea kutufunza, “Kwakuwa shetani aliamua akae ndani ya nyoka, naye Nyoka pamoja na welevu wake hakuweza kukataa, akalaniwa! Mw.3:14, na tangu hapo, Shetani aliendelea kujiwakilisha kupitia umbo la Nyoka, na hujulikana hivyo kwa Lugha zote mbili ile ya kimwili na ile ya kiroho Uf.20:2, na tangu hapo Nyoka kama nyoka hana hiari! Ivyo hivyo na MUNGU tangu hapo aliendelea kujiwakilisha kupitia umbo la BINADAMU kwa Lugha zote mbili,ile ya Kimwili na ile ya Kiroho Isa.7:14-15, Mt.1:23, na katika hili Mwanadamu pia hana hiari! Mambo hayo yataendelea hivyo mpaka mwisho wa hiyo Vita! Mw.3:15 na Uf.20:2. Na hiyo historia ya Edeni itakuwa imekomea hapo!”
  Swali:
  5. Umesema Nyoka alilaaniwa kwa sababu hakumkatalia Shetani kukaa ndani yake. Je, wanyama wanayo hiari? Na iwapo wanayo hiari, nitafurahi iwapo utanionesha andiko linalothibitisha fundisho hilo, maana katika hiyo Mw 3:14 uliyonipa, nimeshindwa kulibaini hilo .
  6. Umesema, “Shetani aliendelea kujiwakilisha kupitia umbo la Nyoka.” Sasa, Shetani akiwa ni Roho na Nyoka akiwa ni mwili, Je, hawa nyoka tuwaonao wakitambaa ndimo Shetani hukaa na kujiwakilisha katika mwili kama ambavyo “MUNGU tangu hapo aliendelea kujiwakilisha kupitia umbo la BINADAMU kwa Lugha zote mbili,ile ya Kimwili na ile ya Kiroho.”??
  7. Umeonesha pia kuwa tangia Roho hizo mbili, Shetani na Mungu, zijiwakilishe katika miili, ule wa Nyoka na wa binadamu, miili hiyo miwili haina hiari tena! Katika hili pia ukinisaidia Andiko linalodhihirisha fundisho hili, litanipanua zaidi uelewa, naamini na ndugu wengine wanaofuatilia mada hii tukijifunza pamoja.

  Labda niishie hapa kwa sasa, ili itusaidie sote kuelewa tunachokizungumza kwani ninapozidi kuisoma post yako, huko mbele unapoyarejea maelezo yangu, naona mwelekeo unakuwa ni wa kutatanisha. Km hapo nyuma umesema, “…Mwanadamu pia hana hiari! Mambo hayo yataendelea hivyo mpaka mwisho wa hiyo Vita!” lakini mbele tena unatufundisha, “Mwandamu anapochagua kumtii na kumwamini Shetani anakuwa “Mtoto wa Shetani” kiroho. Vivyo hivyo, Mwanadamu akiamini na kuamua kumfuata Yesu Kristo (Mungu) anakuwa “Mtoto wa Mungu” Sasa hilo laonesha kuwa HIARI, ambayo binadamu HANA, na huo UHURU wa KUAMUA ni mambo mawili yaliyo tofauti kulingana na unachokifundisha!!!

  Kutokana na mkanganyiko unaouleta, inaniwia vigumu kupata mtiririko wa jambo unalolisema kwa hiyo nashindwa kuyaendea hayo ya mbele maana huu msingi wako nauona hata wewe mwenyewe unakupa matatizo, sembuse mimi!!!

  Ubarikiwe

 43. Mpendwa Sam,
  Namshukuru Mungu kwakuwa nimepata wasaa huu ili tuendelee kujifunza pamoja. Lakini,kama nilivyo ahidi, leo nimepata nafasi ya kuandika, baada ya kusoma somo lako la Tuesday, may 8,2012 at 9:17pm. Naomba nianzie na nukuu yako hii, “Mara nyingi kumekuwa na kuyachanganya mambo na kuyatamatisha katika hali ambayo hutuondolea udadisi, kama vile kumfanya Nyoka (Serpent) kuwa ndiye Shetani. Hebu iangalie nukuu hii kutoka katika post ya ndugu Mabinza; “Msikilize shetani alichojibu kwa mwanamke katika Mw.3:5” akimaanisha Nyoka alichojibu….” Nakubali kuwa nilimaanisha hivyo kweli! Ndg yangu, Bustanini ndipo Historia ya Ukristo wa kweli inapo anzia, yaani chanzo cha vita kati ya Mungu na Shetani, kushindwa kwa shetani na ukombozi wa Mwanadamu. Kwa hiyo,Mungu ili kufikisha lengo lake, aliendelea kumtumia mwanadamu ambapo shetani kwa kuwa hana alichoumba ili kiwe mpango wake, huvamia kila kiumbe , hivyo akaamua amtumie Nyoka, maana Nyoka alikuwa mwelevu na hivyo angefanikisha azima ya shetani. Kwa maana hiyo Shetani alikuwa akizungumza kupita uvuvio aliouweka katika yule Nyoka mwelevu. Kwakuwa shetani aliamua akae ndani ya nyoka, naye Nyoka pamoja na welevu wake hakuweza kukataa, akalaniwa! Mw.3:14, na tangu hapo, Shetani aliendelea kujiwakilisha kupitia umbo la Nyoka, na hujulikana hivyo kwa Lugha zote mbili ile ya kimwili na ile ya kiroho Uf.20:2, na tangu hapo Nyoka kama nyoka hana hiari! Ivyo hivyo na MUNGU tangu hapo aliendelea kujiwakilisha kupitia umbo la BINADAMU kwa Lugha zote mbili,ile ya Kimwili na ile ya Kiroho Isa.7:14-15, Mt.1:23, na katika hili Mwanadamu pia hana hiari! Mambo hayo yataendelea hivyo mpaka mwisho wa hiyo Vita! Mw.3:15 na Uf.20:2. Na hiyo historia ya Edeni itakuwa imekomea hapo!.

  Nimepitia Maneno yako yote uliyoyasema katka Post yako, nilivyokuelewa ni Kwmba; HAWA ndiye ule mti, Na Mwili wake ndiyo Tunda, Hawa aliruhusu na kufanya Ngono na Shetani, na hivyo kilichozaliwa ndiyo KAINI na huo ndio uzao wa Nyoka, nimeendelea kukuelewa pia kwamba, mara tu baada ya Hawa kuingiliana kimwili na Shetani kupitia Nyoka, Hawa alikwenda kurudia tendo hilo na Adamu – kwa maana hiyo,Tunda ni “Via vya uzazi” vya Hawa! Ndiyo maana Ukasema pia kwamba, nanukuu ,“….Tumesoma, pale katika Mwz 3:3 kuwa Mti huo haukutakiwa hata “kuguswa”. Basi ningependa kwanza tuliangalie suala hilo la “kuguswa” ili tuone liliashiria nini, baada ya kufahamu kuwa Mti huo ulotakiwa usiguswe alikuwa ni Hawa Hawa ndiye ule mti…..” Mwisho wa kunukuu.

  Ndg. Yangu Sam, kila nikisoma jibu la Hawa kwa Nyoka katika Mw.3:3 inasomeka hivi, “Lakini matunda ya mti ulio katikati ya Bustani Mungu amesema, Misiyale wala msiyaguse , msije mkafa ” Kwa maana hiyo, kilichozuiwa KUGUSWA kwa Mjibu wa mstari huo ni MATUNDA, na si MTI! Kama hivyo ndivyo hivyo, na iwapo Hawa ndiyo ule Mti. Basi Hawa kama Hawa, kumbe si tatizo, tatizo ni yale matunda yake! Kwa mjibu wa Biblia,Shetani ni Roho, na Mungu ni Roho – Wote hawa hawazai “Watoto wao” kimwili.KAMA ILIVYO TANGU ZAMANI Mungu ni mwenye Haki, aliumba Maraika na akawacha huru, hivyo wanaweza kuasi au kutii! Vivyo hivyo, Mungu alimuumba Mwanadamu na kumuacha Huru, anaweza kuasi au kutii! Mwandamu anapochagua kumtii na kumwamini Shetani anakuwa “Mtoto wa Shetani” kiroho. Vivyo hivyo, Mwanadamu akiamini na kuamua kumfuata Yesu Kristo (Mungu) anakuwa “Mtoto wa Mungu” Kiroho. Kwa maana hiyo Kaini ni uzao wa shetani kiroho, alichagua mwenyewe kumuasi Mungu licha ya kupewa tahadhali na Mungu mwenyewe! Yesu alikwisha sema hivyo katika Yn. 3:6 kuwa,kilichozaliwa kwa Roho ni Roho, sasa kama Shetani ni Roho, hawezi kumzaa kaini kimwili! Yesu alisema hivyo kwa sababu, mambo haya yalifanyika Duniani na yanaendelea kufanyika Duniani, hivyo huwachanganya wengi,ata Yesu alishangazwa alipoona hata wasomi hawajui hilo! Yn.3:3-12. Na yeyote yule anapo amua kuongozwa na Nguvu za Roho fulani, ni Mtoto wa mwenye Roho husika,wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni “Watoto” wa Mungu Rum.8:14. Naomba unijulishe ili nijifunze zaidi, je, nimekuelewa vizuri kuwa, UNAMAANISHA KAINI NI MTOTO WA SHETANI KIMWILI KWELI? Kama ni ndiyo kwa vipi kiumbe cha kiroho cha weza kufanya Ngono kimwili?
  Kama nilivyotangulia kusema nipo hapa kujifunza. Nimepitia maandiko mbali mbali katika Biblia, ili kuona kama Agano jipya linasema kitu Fulani, kuhusu kile kilichofanyika huko katika Bustani ya Edeni, na kuona kama kweli kile kitendo cha kuliwa tunda na wazazi wetu wa kale Adamu na Hawa ilikuwa nini hasa. Nimemsikiliza kwa makini Paulo katiika kitabu chake cha Rum.1:24-25, mistari hiyo inasema kwamba,Mungu aliwaacha katika tama za mioyo yao “…..,hata WAKAVUNJIANA HESHIMA MIILI YAO…..walibadili kweli ya Mungu kuwa uongo……….”. Naendelea kutafuta na ili kujua na hatimaye nielewe vizuri juu ya Tunda alilo chuma na kulila mama yetu Hawa na kisha kumpelekea na Baba yetu Adamu. Naomba nikili kwamba, Maneno katika post yako na andiko hili limenitoa pahala finyu zaidi na kunipeleka pahala wazi zaidi katika kuijua ile kweli ya Mungu. Hadi hapo, Ndg. Yangu Sam, ufahamu kwamba maelezo yako uliyoyatoa katika post yako niliyoitaja hapo juu, yamenisaidia sana kunifikisha hapa nilipo, na naendelea kuyachunguza kwa kuyapitia kwa taratibu, ili kuujua ukweli wa Neno la Mungu. Mpendwa, inaweza ikatokea usikubalike kwa haraka, hii si shida, Neno linsema katika Tito 2:1 “Wewe toa mafundisho yenye uzima” Nimesukumwa kutaka kujifunza zaidi juu ya hili, kwa sababu nyingi, lakini lilyo kubwa ni kwa kuwa huu ni wakati wake hasa, ambapo kanisa limefungia Nje Yesu na kukumbatia ujuzi na mafundisho ya wanadamu. Ukweli ni lazima ujulikane sasa, Neno lazima liyuweke huru,na tujue yote, ili kama Mtu kupotea apotee mwenyewe tu pasipo na kujitetea, kama yasemavyo maandiko katika Rum. 1:20 kwamba, “ Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu, yanaonekana na kufahamika kwa kazi zake….ili (Watu) wasiwe na Udhuru” Uendelee kubarikiwa.

 44. Mpendwa Haule!

  Nimeona post yako, ahsante sana , hii sio teolojia ila hii ndio teolojia original achana na hizo fake, hii ukiimaliza utawaona wote wakina Kabbalah , LILITH(babewatoto), Baali na miungu mingine kibao na utaijua ni nini.

  Kwenye Ubatizo nalipitia kwanza lile bandiko la Lwembe ila tutakutana huko.

  Ubarikiwe ndugu yangu!!

 45. Sam
  haya mafundisho umefundishwa darasani!!, maana hii ndio teologi kamil.maandiko marefu kwelikweli,Ngoja tupitie taratibu kipengele kwa kipengele.
  Asante

 46. mpendwa Sam, maelezo yangu ya hapo juu, ni kujibu maswali yaliyokuwa yamejitokeza toka kwako tar. 7/5/2012, siku ya juma tatu. kwakuwa nimechelewa kupata somo ulilolileta leo, naomba nilipitie kesho, kwani usiku umeenda sana, maana sasa ni zaidi ya saa 8 usiku!. Asante sana kwa kuwa pamoja nami. Endelea kubarikiwa na Bwana mpendwa.

 47. Mpendwa Sam,

  Nashukuru sana kwakuwa hujachoka kuwa nami katika safu hii. Sasa, naanza kuelwa kile Ndg. Yangu Mr. Juma, alichokuwa akikimaanisha katika usemi wake, kuwa “Chakula hiki ni kigumu”! Naendelea kutafuta na kujifunza kwa bidii sana ili kupata majibu ya maswali makuu MATATU; kwamba, je,miti katika bustani ilikuwa minne? kwamba, Je, Hawa ndiye aliye kuwa huo mti wa Nne? Na kwamba, je, Tunda alilokula Hawa lilikuwa nini? Kimsingi sijafikia kupata maandiko ndani ya Biblia yanyonifanya nikukubali kuwa Katikati ya Bustani kulikuwa na aina tatu za miti, na hivyo kufanya kuwa na jumla ya aina Nne za miti katika bustani. Bali naona kulikuwa na aina tatu ya miti katika Bustani yote na kati ya hiyo, miwili, yaani Mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ndiyo miti iliyokuwa katikati ya Bustani! Vile vile bado SIJAFIKIA Kupata kuwa kulikuwa na Mti wa Nne ambao ni Hawa. Lakini sitakuwa Mgumu iwapo maandiko hata kupitia wewe,yataniongoza kujua na kuelewa kuwa Hawa, ndio huo mti wa Nne! Nikiangalia ile Mw.2:16-17 naona kwamba, Mtu ATAKUFA akila matunda ya ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Lakini nikiangalia alichoeleza Hawa kama jibu lake kwa Shetani, katika Mw.3:2-3, kwamba, Matunda ya mti wa katikati wamekatazwa, kuyala wala kuyagusa. Inaonekana kama kwamba, alichojibu Hawa SI KILE kilichotamkwa na Mungu kama katazo, Mw.2:16-17; Mimi bado nakubali na kuona kuwa alichokijibu Hawa, ndicho hasa alichokimaaninsha Mungu, kwa sababu matokeo ya kula matunda yatokanayo na Mti wa ujuzi wa mema na mabaya ni sawasawa na matokeo yakula au kugusa matunda ya mti wa katikati ya bustani, yaani Mtu akila ATAKUFA! Pili, Hawa asigesema kunamti katikati ya bustani ile, iwapo kusingekuwa na mti katikati ya bustani, Biblia inasema mti huo uliokatazwa wasiyale matunda yake upo katikati ya Bustani!

  Sasa, ni matunda gani ambao mtu akila au hata kuyagusa atakufa? Na iwapo “Atathubutu” kula matunda katika ule Mti wa Uzima ataweza kuishi milele?(Mw.3:22). Katika Biblia takatifu, matunda pekee mtu akila au kuyagusa, atakufa ni DHAMBI.Hiyo ni kwa mjibu wa Rum. 6:23, ambayo inasema, mshahara wa Dhambi ni Mauti! Na wakati ukila tunda toka mti wa uzima (Yesu kristo) unapata kuishi milele, maana Lk, 5:24 inasema Yesu anao uwezo wa kusamehe Dhambi Duniani, na karama ya Mungu ni uzima wa milele, Rum.6:23! Je, Dhambi yaweza kuwa tunda la kuliwa? Ndiyo, ukisoma Hos.4:8, inasema ”Hujilisha Dhambi ya watu wangu…” Adamu na Hawa tunda walilokula lilikuwa Dhambi ndiyo maana walijificha (Mw.3:8), maana mandiko katika Isa.59:2 Yanasema, “….dhambi zimeuficha uso wa Bwana msiuone…”! Kwa hiyo, Dhambi husababisha aibu pia, ndiyo maana walijificha, Mith.14:34, inasema, Dhambi ni aibu ya watu wote!

  Sasa, iwapo dhambi ndiyo lile tunda, je, mti ni nani? Mti huo ni SHETANI, Biblia inasema katika,1Yoh. 3:8,atendaye dhambi ni wa Ibirisi! Naomba kwa leo, niishie hapo. Lakini bado najifunza,ukinielewesha vema kwa maandiko, kuwa Hawa ndiyo ule mti wa Nne na iwapo utanijulisha kupitia maandiko lile Tunda alilokula Adamu na Hawa ni lipi, nikielewa, nitakubali. Endelewa kubarikiwa na BWANA!

 48. Labda baada ya kuyajibu maswali yaliyojitokeza, sasa twaweza kuendelea mbele zaidi tukiwa tumetoka katika hatua ile ya MTI upi, kwani kulingana na Mwz 3:3 tunapaswa kuwa tumepata mwangaza zaidi.

  Basi, ninawaombeni uvumilivu na kuchukuliana nami tunapoiendea hatua ya pili ya jambo hili ili kulijua “TUNDA” lililoliwa na matokeo yake, yaani athari na kama zimetufikia na kiwango chake katika ujumla wa mahusiano yetu na Mungu.

  Tumesoma, pale katika Mwz 3:3 kuwa Mti huo haukutakiwa hata “kuguswa”. Basi ningependa kwanza tuliangalie suala hilo la “kuguswa” ili tuone liliashiria nini, baada ya kufahamu kuwa Mti huo ulotakiwa usiguswe alikuwa ni Hawa. Pia tunapolitafakari jambo hili, tuyarejee maudhui ya uumbaji katika ushahidi tunaouona leo hii. Hapa nina maana ya kuyaangalia maumbile, yaani katika viumbe vyote alivyoviumba Mungu, Dume ndilo lililoumbwa lenye kuvutia kuliko Jike! Watazame wanyama wote, utawaona hivyo kasoro binadamu tu! Basi jambo hilo lingetudhihirishia kuwa Hawa alikuwa ni mwenye kuvutia lakini pia alikuwa ni Mti wa KIFO!

  Pia Maandiko yanatuambia kuwa Nyoka (Serpent) alikuwa ni mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu, Mwz 3:1. Hata tumeona katika wanyama wa mwitu ndiye pekee alikuwa na uwezo wa kuongea na binadamu.

  Mara nyingi kumekuwa na kuyachanganya mambo na kuyatamatisha katika hali ambayo hutuondolea udadisi, kama vile kumfanya Nyoka (Serpent) kuwa ndiye Shetani. Hebu iangalie nukuu hii kutoka katika post ya ndugu Mabinza; “Msikilize shetani alichojibu kwa mwanamke katika Mw.3:5” akimaanisha Nyoka alichojibu. Lakini Maandiko yanatuambia alikuwa ni mnyama tu wa kawaida ukiacha huo werevu aliokuwa nao, kwa hiyo alikuwa chini ya Adamu kiutawala. Basi, iwapo mbele katika Biblia nyoka ameoneshwa kama Ibilisi au Shetani, basi tunapaswa tufuatane nayo Biblia ili tuone ni wapi yule mnyama wa mwitu, Mungu aliyemuumba kama wanyama wengine amegeuka kuwa hivyo. Na iwapo utakurupuka na kusema huyo nyoka ndiye Shetani na Ibilisi, basi Lucifer utamuweka wapi katika hizi falme mbili? Umeona? Inakubidi uende polepole bila jazba za kidini! Labda itakuwa vema pia tukivitazama viumbe hivi viwili kwanza, Shetani na Nyoka, ili kadiri tutakavyoendelea tusivichanganye. Shetani ni Roho (ya UASI) na Nyoka (Serpent) ni mnyama wa mwitu, nazo sifa zake zinamuonesha kuwa alikuwa juu ya wanyama wengine.

  Sasa ili kupata kulijua jambo lolote lile hutubidi kutafuta chanzo chake. Na kama jambo hilo linahusiana na Mungu, basi inatulazimu kurudi pale Mwanzo, maana kitabu cha Mwanzo ndicho kitabu cha mbegu. Hapa ndipo mambo yote yanapoanzia. Kama ni Kristo au Ibilisi au Dini au Ibada au Dhambi au Wokovu au Utakatifu au chochote kile, hapo ndipo mwanzo wa vyote. Hata Bwana wetu Yesu Kristo walipomletea suala la ndoa na talaka aliwarejesha kule Mwanzo! Pia kama nilivyosema awali, ili kuyaelewa mafumbo ya Agano la Kale inatulazimu kwanza twende katika Agano Jipya, hilo linalotuhusu sisi, tukapewe Roho Mtakatifu huko, ndipo atuongoze katika hayo mafumbo na kutufunulia!

  Basi, tukiyarejea maelezo ya mwanateologia wetu Titus Amigu, katika kile kifungu anachotusisitizia kuwa ‘Tunda’ hilo haikuwa ni tendo la ndoa, anapotuambia, “Wao walifunganishwa ndoa na Mungu mwenyewe pale aliposema katika sura 1:28. “Zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha… Jiulize kidogo tu. Wangezaaje bila kuruhusiwa na tendo la ndoa?
Basi walisharuhusiwa, hivyo kulifanya kusingekuwa haramu ya laana kubwa kama waliyopewa.”

  Maelezo haya ya kiteologia yanayopingana na Neno la Mungu, ndiyo yanayoaminika na kanisa. Kimsingi ile Mwz 1:28 licha ya wao kupewa agizo hilo, walipaswa kusubiri mwongozo zaidi wa jinsi ya kuijaza nchi. Kwa hiyo anapotufundisha hivyo, kuwa walikwisha fungishwa ndoa, kwa hiyo tendo la ndoa lilikuwa ruksa kwao, alipaswa pia atuonesha au atupe sababu ya kwanini Adamu na mkewe hawakuwa na watoto huko nyuma mpaka baada ya kuanguka ambavyo matokeo ya kujuana huko tunaona watoto wanazaliwa. Hata kama suala la kujuana hapo awali halikuandikwa, bado tungeona matunda ya jambo hilo, kwani kujuana kadiri ya mapenzi ya Mungu ni kwa ajili ya kupata watoto. Watazame wanyama wote utaliona hilo hivyo! Kwa hiyo hili fundisho si la kweli, ni akili za kibinadamu tu, wakijaribu kuweka msingi mwingine kwa kanisa. Mungu hakuwaruhusu kufanya Tendo la Ndoa!! Tena mwanateologia wetu anatamatisha kuwa kulifanya tendo hilo kusingekuwa ‘HARAMU YA LAANA KUBWA KAMA WALIYOPEWA’ yaani akimaanisha kuwa Adamu na mkewe walipewa LAANA KUBWA!!!!

  Kulingana na fundisho hili, nadhani zaidi ya asilimia 90 ya wakristo tunaamini katika fundisho hili la ‘Uzao wa Adamu kuwa ni wa nyoka uliolaaniwa’. Baada ya kuwa umelimeza fundisho hili, Sasa wanakupa glasi ya maji safi na baridi yenye kukupoza vizuri sana, kusukumia hilo pande la sumu inayoua roho taratibu, walilokupa ulimeze. Nayo glasi hiyo ya maji safi, ndizo zile habari za Yesu Kristo ziletazo wokovu na miujiza na misisimko hata unakokwenda kufia usingekujua! Maana habari zote hizo wewe zimekupatia fukuto tu, kwako hazina mahali pa kufanya makao, maana wewe mwenyewe umeikiri LAANA, nayo sasa imo ndani yako! Kristo hakuwafuata walio LAANIWA. Hakuna andiko linaloahidi wokovu kwa wale ambao Mungu mwenyewe amewalaani!! Mungu akikulaani ndio basi tena, unaondoka mbele zake kama Kaini alivyofanya, nawe unatafuta Nod yako. Kama ni dhehebu fulani, basi unakwenda huko, nawe unaendeleza vita dhidi ya Mungu kwa kulipindisha Neno lake au kufundisha kinyume na hilo. Sasa ndugu yangu, kama tumeunganishwa kwa hila na hao waliokataliwa kimbele itakuwaje?

  Nayo mafundisho ya jinsi hii, yakiwa ndio msingi uliojengwa, basi wito wa ‘Kuvunjiwa Laana’ na manabii na makanisani mwetu, pamoja na injili za utajirisho nk. vyote hivi vimejengeka juu ya msingi huo. Nasi waaminio huingizwa katika Laana hiyo kwa fundisho hilo linalojumuisha ile Dhambi ya Asili, mambo hayo huunganishwa pamoja katika laana hiyo tuliyoingizwa! Ningali najaribu kuuangalia katika Maandiko ili nione ni wapi yule aliye laaniwa alivunjiwa laana hiyo, mkipaona wapendwa tuoneshane! Lakini tunaporudi katika Biblia katika kile kitabu cha Mwanzo ili tulitazame jambo hilo la laana, ndipo hapo tunaona Mungu anazitabiria zao mbili, Uzao wa nyoka na Uzao wa mwanamke (Mw. 3:15). Hata hiyo ‘HARAMU YA LAANA KUBWA WALIYOPEWA’, tunaona aliyepewa ni Nyoka na si Adamu wala Hawa. Mwz 3:14 “Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, …” Biblia mpaka hapo imelikataa fundisho la mwanateologia wetu, kama tulivyoona, kwamba aliyelaaniwa alikuwa ni Nyoka, nao warithi wa laana hiyo watakuwa ni Uzao wake. Basi kama tunavyoona, uzao wa nyoka hauna uhusiano wowote na Adamu wala uzao wake. Laana inauhusu Uzao wa nyoka tu!

  Basi, kulingana na ukweli huu tunaouona, ya kwamba Nyoka anao Uzao ambao umelaaniwa, nao wanateologia wakatufanya sisi tunaotokana na Adamu kuwa ndio hao, hilo pekee lapaswa kutufanya tusimame kidogo na kuitafakari hali hii. Maana tumeingizwa na kudumu katika hali ya waliolaaniwa kwa ghilba, na hivyo kupita katika njia ngumu tusiyostahili. Basi hawa wenye laana yao wako wapi ?

  Vema, baada ya mambo hayo, pale katika Mwz 3:20 tunaona Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai. Mbele kidogo katika Mwz 4:1-2 tunasoma hivi; Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili.”

  Hii ndiyo rekodi aliyoiweka Mungu tuisome siku tutakayofikia kuwa na shauku ya kujua nini kilitokea kule Edeni. Kama tunavyoona, Adamu kamjua mkewe mara hiyo iliyoandikwa na wamezaliwa watoto wawili, kama ni mapacha wa kuongozana katika kuzaliwa au ni wa tofauti ya siku moja au mbili au wiki, sote hatujui. Naye Mungu asipotujulisha basi halina faida kwetu. Lakini kuhusu tuliyojulishwa, ndio hilo kama tulivyolisoma. Labda kwa ajili ya ufahamu wa hili ni kwamba mwanamke anaweza kujifungua mapacha wanaotofautiana kwa hata siku mbili na zaidi – ukiwauliza wataalamu wa mambo ya uzazi watakujuza zaidi.

  Tukiendelea mbele tunakuta ukoo wa Adamu pale katika Mwanzo 5:1-32. Katika huu, Kaini hayumo! Tukirudi tena tunaukuta ukoo wa Kaini katika Mwanzo 4:16-22. Katika Agano hili la Kale kitendawili cha Uzao wa Nyoka na Uzao wa Adamu vinabakia hivyo! Mambo haya yanafunguka au Mungu anayafunua kwa hatua katika Agano Jipya, kama Mungu mwenyewe alivyoahidi katika Kristo: “Lakini yeye atakapo kuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote…” Yoh 16:12

  Huku katika Agano Jipya, ndiko kitendawili cha Uzao wa Nyoka kinaanza kuteguliwa kwa uwazi zaidi kwa kanisa. Hebu twende katika kifungu kile cha Mathayo 3:7 pale Yohana Mbatizaji alipowakemea wale Wafarisayo na Wasadukayo waliomjia wabatizwe; “… Enyi wazao wa Nyoka!…” Sasa kumbuka ya kwamba huyo alikuwa ni nabii wa Mungu aliyekuja kwa Huduma Maalumu ihusuyo wokovu kwa Uzao wa Adamu. Kwa hiyo alipowaona lile kundi, tena wengine viongozi wa dini, wakimjia alipowatazama kwa jicho la rohoni akawajua asili yao, Uzao wa Nyoka!!!

  Kwa hiyo tunachokiona hapa ni Siri ikifichuliwa kwetu sisi kanisa tuliopo leo hii na si huko nyuma. Hawakulijua hilo, reference yoyote ya Uzao wa Nyoka, kwa maana ya kulaaniwa, kwao ilihusishwa na UASI wa kawaida kwa watu wote, uliotokana na ile laana iliyoambatanishwa kwa umahiri na ile Dhambi ya Asili (kula lile tunda), ambao ulifanywa na watu katika namna ya makosa ambayo wangeweza kuyatubia na hivyo kupokelewa na Mungu kama wana. Nao waliokithiri katika UASI, hao ndio waliohesabika kama waliolaaniwa pamoja na wale waliozivuka Sheria na kuangukia katika adhabu zake. Uelewa huu ndio umeendelea kuwepo hata sasa kulingana na ule MSINGI wa kiteologia (ulioanza kwa Nyoka kumfundisha Hawa) uliowaingiza watu wote katika laana na kuipozesha LAANA aliyoitoa Mungu kwa kuifanya inaweza kuvunjwa kwa kitubio! Bali ni katika kufunuliwa kwake hapo katika Injili, ndipo tunapata kujua kwa uhakika kuwa Uzao huo wa Nyoka upo, na ndio wenye kuhusika na LAANA hiyo!!!

  Hapa mbele kidogo tena Mungu anatudondoshea dondoo nyingine kwa ajili yetu, katika 1Yh 3:12 anasema, si kama “Kaini alivyokuwa wa yule mwovu” Sasa hakuna sehemu Biblia inamtaja Adamu kama mwovu. Mwovu yuko mmoja tu, nayo Biblia inatuambia huyo ndiye baba yake Kaini.

  Sasa, Kaini akiwa ni mtoto aliyezaliwa kwa Hawa, jambo hili la yeye kuwa mtoto wa yule mwovu, linatulazimisha kurudi tena kule Edeni ili kubaini yalikuwaje mambo hayo. Huko, yatubidi tuanzie pale Nyoka alipokutana na Hawa. Tukiyachunguza mazungumzo yao, tutaona kuwa yamechukua mwelekeo usiostahili, naye kiongozi wa mazungumzo hayo akiwa ni yule mnyama aliye chini yao, inatulazimu kujiuliza kulikoni?

  Tukiwa huko Edeni, mazingira ya huko yanatuonesha Ushirika waliokuwa nao akina Adamu na Mungu. Tena sasa tunafahamu kuwa kusudi la Mungu katika kumuumba Adamu ilikuwa Yeye akae ndani yake na kumuongoza katika furaha yote aliyomtayarishia isiyo na kikomo. Nao Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya ulikuwamo humo, ambaye ni Lusifa, ile ROHO YA UASI. Basi yale mazungumzo ya Hawa na Nyoka, kadiri ya mwelekeo yaliouchukua, huo usiostahili naye muhubiri akiwa ni Nyoka, yule mnyama aliye chini yao, nao mwelekeo wa mahubiri hayo ukiwa ni UASI, ndipo tunafika katika kiwango cha kujua kuwa Lusifa ALIMVUVIA huyo SERPENT, hata akawa katika UPAKO wa LUSIFA akiyaendesha mahubiri hayo kuyapeleka nje ya Neno la Mungu!!!

  Uasi wowote huambatana na wivu. Kama Mungu alimuumba Adamu kwa mfano wake, sioni kitu kingine kinachoweza kuinua hisia za wivu zaidi kukipata hicho kilicho juu ya vyote, au kukivuruga hicho, au kutafuta chako kilicho zaidi na kumkoga huyo uliye na wivu naye. Lusifa hana uwezo wa kuumba, kwa hiyo katika wivu wake, kwake haikuwa rahisi kumvuvia Adamu wala Hawa kwa vile walikuwa ni watoto wa Mungu. Na kama tunavyoona katika Maandiko, mbegu ya Mungu au Uzao wa Mungu hukaa ndani yao, hivyo si rahisi kuimiliki miili hiyo maana uzao wa Mungu umo ndani. Kama Biblia ilivyosema, Lucifer alikuwa karibu na Mungu katika nafasi yake aliyokuwa nayo, kwa hiyo ni dhahiri aliyajua mengi katika uumbaji hata ule mwingiliano wa damu kati ya Serpent na binadamu aliujua.

  Ndipo kukidhi haja yake akamchagua huyo Serpent na kumvuvia (kumbuka mbegu ya Mungu haikai ndani ya wanyama) ili kuitimiza azma yake hiyo ya kujipatia kiumbe atakachokaa ndani yake pia, kama Mungu kwa Adamu, ndipo akamvizia Hawa akiwa PEKE YAKE na kuanza kumtongoza! Kumbuka kwamba wanyama wote wa mwitu pamoja na huyu Serpent walikuwa chini ya utawala wa Adamu, hivyo wakiwa katika hali yao hiyo usingetegemea uasi wowote kutoka kwao, isipokuwa uasi huo uwe umevuviwa (inspired). Uvuvio huja kwa roho, nayo roho ya Ibilisi (Lucifer) ndiyo yenye kuasi. Matokeo ya mahubiri hayo tunamuona Hawa akidanganywa na kuondolewa katika NGOME aliyozungushiwa na Mungu, Neno lake. Ukishatolewa kwenye ngome unakuwa huna ulinzi tena, na ikiwa umetolewa kwa kulaghaiwa, basi hata hiari hukuondoka nawe huwa chini ya mlaghai wako kimamlaka. Basi ni katika hali hiyo ndipo Nyoka alifanya UZINZI na Hawa! Unajua pale Hawa alipokuwa amezingirwa na Neno hakujua chochote kujihusu zaidi ya kile alichoambiwa. Lakini alipotoka NJE ya NENO, alikosa vazi la ROHO Mtakatifu. naye Nyoka “alipomgusa”, tamaa ziliwaka ndani yake na wakaishia kufanya TENDO LA NDOA!! Hivyo ndivyo ile mbegu ya yule Serpent ilivyohifadhika katika tumbo la uzazi la Hawa; Nyoka akiwa ametembea na Hawa kabla ya Adamu!!!!

  Sasa ni muhimu kufahamu pia kuwa Nyoka (Snake), huyu tunayemuona leo hii si yule SERPENT aliyekuweko huko Edeni. Yule wa Edeni alikuwa mwerevu (subtil = pervasive, elusive, mysterious, magic, charm, power…), ndipo juu ya sifa hizo ongeza na UPAKO wa Ibilisi (zitazame sifa zake katika Ezk: 28:12-15), halafu ukutane naye, nawe kanisa, huna Neno, yaani kichwa, lazima ubebwe na mafuriko! Haya, huyu Serpent alikuwa na miguu na aliweza kuongea kama tulivyoona. Na pengine alikuwa mtumishi wa Adamu. Wengi wetu tunaposoma habari za nyoka huishia kumuwazia huyo nyoka tunayemjua. Kwa bahati mbaya, kulingana na hali halisi, kamusi zetu zote hazina tafsiri ya hili neno SERPENT- wote walipotafsiri wameishia kwenye neno SNAKE ambaye ni ‘REPTILE’. Hata wabunifu nao pia wamekwama; wakikuchorea taswira ya Edeni, basi utamuona nyoka (snake) anayetambaa karibu na Hawa!

  Unaona MUNGU alivyolifumba jambo hili? Yule ‘Serpent’ aliyeumbwa kule mwanzo hayupo tena duniani. Mungu alimu ’extinct’, Lakini Biblia ilisema Serpent anao uzao (seed), sasa iwapo yule Serpent wa asili leo hii hayupo ule ‘Uzao‘ wake tutauonea wapi? Kama una mawazo kuwa Biblia inapotamka nyoka (Serpent) katika maana ya Uzao, ukifikiri ya kuwa ni wale wasiotaka kuokoka au kujiunga na dhehebu lenu, basi utakuwa bado hujalielewa jambo zima, nayo Maandiko yatakuwa yamekupiga chenga! Mungu alisema Serpent, yule mnyama anao ‘uzao’: “… nami nitaweka uadui kati yako (Serpent) na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako (Serpent) na uzao wake (mwanamke)” Mungu hajasema kati ya uzao wa Ibilisi amesema Serpent yule hayawani wa mwitu!

  Sasa, kimaumbile au kitaswira alikuwaje – sote hatujui bali tunajua ndiye mnyama pekee aliyewahi kuwa na taswira mbili ile ya Serpent tusiyoijua na ya huyu nyoka (snake) wa leo atambaaye. Taswira hizo mbili hazifanani kabisa. Lakini Injili pia imetuangazia kuhusu taswira ya huyu Serpent. Maana sheria ya Mungu isiyo badilika inasema kila kiumbe kizae kwa jinsi yake, ndipo uzao wa Serpent hauwezi kuwa kitu kingine. Naye Yohana Mbatizaji akawaona wakimjia ‘fuata mkumbo’- kumbuka Yohana alikuwa ni Nabii aliyetoka uweponi mwa Mungu, Kristo anamshuhudia hivyo. Basi Yohana akawaita kile walicho, ‘Enyi wazao wa nyoka…’. Umewaona, ni binadamu katika kila namna. Usingeweza kuwatofautisha kwa namna yoyote ile isipokuwa uwe na Roho wa Mungu, maana ni Roho wa Mungu pekee anayeweza kututofautisha kwa kutuchunguza ndani yetu iwapo ule uzao (mbegu) wa Mungu upo ndani yetu. Hakuna namna nyingine ya kuutofautisha ule uzao wa nyoka, licha ya kuwa ni wa kidini, lakini Uzao wa Mungu haukai humo maana bado ni yule mnyama tu. Ndio maana nikasema Ibilisi huwatumia hao bila pingamizi lolote! Soma tena Math. 23:33, Kristo anawajua: “Enyi nyoka (serpent)…”. Usidhani hao ni wa dhehebu la ‘Kibwetere’ au walikuwa hawajaokoka au sio ‘walokole’, la hasha, angalia yale mapepo yaliyokuwa kwa yule kichaa wa Gerasi walivyomtambua Yesu kuliko pengine hata askofu mkuu wetu, hayo ni mambo ya Rohoni, zile Mbegu!

  Basi matokeo ya ule udanganyifu pale Edeni yalikuwa ni kuzaliwa kwa Kaini, naye mtoto huyu ndani yake mlikuwa na Kiini cha mbegu ya Kiroho ya Lucifer (spiritual gene) iliyopitia kwa yule Serpent. Kama Maandiko yanavyoonesha wazi kabisa ya kuwa Serpent anao uzao, basi unapaswa uliamini hilo kwanza, na pia uzao wake utatimiza yote Biblia ilichosema juu yake. Tamko la uadui kati ya uzao wa Serpent na wa mwanamke nalo sharti litimie. Sasa usingetegemea mbegu zilizo hifadhiwa, ambazo hazijapandwa au mbegu ambazo hazijakomaa zioneshane uadui moja kwa nyingine. Kwa hiyo lile tamko la Mungu katika kifungu hiki laweza kutimia pale tu mbegu hizo zilizoongelewa zikiisha kujizaa. Mbegu ya Serpent iliyopandwa kwa Hawa pale ‘alipomdanganya’ ilijizaa katika utu wa Kaini. Je kuhusu uzao wa mwanamke? Tunafahamu ya kwamba mwanamke hana mbegu bali yeye ni kitalu cha kupokea mbegu. Kwa hiyo kama alivyopokea mbegu kutoka kwa Serpent ambayo ilijizaa katika utu wa Kaini, huyo mwanamke, Mariamu, baadaye alipokea mbegu kutoka kwa Mungu ambayo ilijizaa katika utu wa Bwana Yesu Kristo. Ni mizao hii miwili tofauti iliyo katika uadui hata leo hii.

  Kama nilivyosema hapo awali mambo ya rohoni ni vigumu sana kueleweka mwilini. Lakini pale unapokuwa na shauku ya kweli ya kulijua jambo fulani katika Biblia, basi Mungu huwajibika kwa hilo moja kwa moja, ndipo angekutimizia hilo ili furaha yako iwe kamili. Lakini kwa bahati mbaya, wengi wetu huliendea Neno la Mungu katika shauku ya kudhihirisha mafundisho yetu, naye Mungu hawajibiki katika hilo, nasi huishia kuyakosa hata yaliyowazi na tukaendelea na misimamo yetu isiyo na faida yoyote kiungu.

  Hebu tazama mfano huu ili ujionee mwenyewe kwa nini mstari huu haujawahi kuamsha shauku ya kutaka kujua- ‘kulikoni’, Mwanzo 3:20- “Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye mama yao wote walio hai” Sasa, iwapo Hawa ndiye mama wa wote walio hai; je, baba wa wote walio hai yuko wapi? Na, iwapo mumewe ndio huyo Adamu, kwa nini Biblia imekataa kulikubali (to acknowledge) jambo hilo? Naye Adamu akiwa ndiye mume wa Hawa, iwapo yeye ndiye baba ya hao watoto wawili, kulikuwa na haja gani kujiondoa katika ujumuuisho wa uzazi walio ushiriki pamoja? Tena tulipoangalia ukoo wa Adamu, Kaini hatukumuona katika ukoo huo. Pia katika ukoo wa Kaini kama tulivyouona nao Adamu hayumo, hata Biblia yenyewe hakuna mahali inaposema “Kaini mwana wa Adamu”! Kumbuka Biblia ilisema Adamu hakudanganywa. Yeye alijua fika analolifanya. Naye Mungu alipowaendea na kutoa zile adhabu kwa hilo kosa, Adamu aliyasikia yote, hata pale Mungu alipoweka bayana tunda la kosa hilo kuwa kwa kuchanganya damu na huyo mnyama, sasa wamembebea uzao wake pia ambao wataishi nao tena utakuwa adui wa uzao wao; ndio maana Adamu hapa anampa mkewe jina hilo, maana ndani yake mna mizao yote miwili. Hata Kaini alipomuua nduguye Habili, bila shaka Adamu na mkewe walijua matatizo ya Kaini ni ule unyama utokanao na baba yake yule hayawani wa mwitu, Serpent, chini ya uvuvio/uongozi wa Lucifer. Hata tunapokiangalia kizazi chake pia tunamuona mjukuu wake akijisifu kuua mtu!

  Unajua, iwapo utaiweka Theologia pembeni kidogo, sisemi uiache, pengine ndiye muajiri wako, bali isogeze pembeni kidogo tu, utairudia baadae uendelee nayo ukiisha kuona ukweli wa jambo, ndipo hilo lingekusaidia zaidi katika nyendo zako na ibada. Tazama kusudi la Mungu kumuumba binadamu ni kwa yeye Mungu kuja kukaa ndani ya binadamu huyo na kumuongoza katika furaha yote Mungu aliyomtayarishia, naye amesema “…tutakuja na kufanya makao kwake”; “..kaeni ndani yangu na mimi ndani yenu” (Yoh 14:23). Hili ndilo kusudi la Mungu kwa wanae. Je, mwenye wivu na huyo Mungu mwenye mipango hiyo na wanae unadhani angefanyaje? Kwanza angevuruga ili wakose wote au angetafuta namna ya yeye pia kuwa katika nafasi hiyo. Wahubiri wengi wanajaribu kumfanya shetani bwege, lakini Biblia ilisema alikuwa mbinguni tena karibu na Mungu. Na katika ukweli huo, yeye alijua afanye nini kutimiza hilo la kuvuruga na kuabudiwa. Naye akiwa mwenye kuwajua wanyama wote, alijua pia ni yupi anayeweza kufaa katika mpango wake. Serpent ndiye aliyefaa, basi yeye naye kama Mungu akaavyo ndani ya wanae, yeye pia hukaa ndani ya uzao wa Serpent ndipo mizao yote miwili ni ya kidini nayo ungeikuta kanisani pamoja, kama ile miti miwili ilivyokuwa ndani ya bustani – ule wa uzima (Kristo) na ule wa ‘Ujuzi wa Mema na Mabaya (Lucifer), basi miti hii ingali ikiambatana hata leo. Waangalie Kristo na Yuda Iskariote, walikuwa umri mmoja (age group). Mungu akijidhihirisha katika Kristo na Shetani pia akijidhihirisha ndani ya Yuda. Wote wa kidini na wote wamo kanisani. “Je, mimi sikuwachagua ninyi thenashara na mmoja wenu ni shetani?” (Yoh 6:70). Kristo alipoondoka naye Yuda akaondoka. Kristo aliporudi kanisani katika Roho Mtakatifu, naye Yuda alirudi kanisani pia katika roho wa uasi/Mpinga Kristo. Naye roho huyo yupo hata sasa, ile miti miwili!!! Umeona Lucifer alichofanya?. Kajifanyia naye mtu kutoka kwa yule mnyama, si kwa kuumba, bali kwa kupervert kile kilichoumbwa, naye anamtawala kwa uhuru wote maana Roho Mtakatifu hakai ndani ya wanyama, naye Kaini alikuwa ni mnyama tu, Mungu anatambua hilo na Adamu pia analijua hilo ndio maana akamwita mkewe “mama wa wote walio hai” ile ‘mizao’miwili itakayoijaza nchi!

  Kumbuka, Mungu alipoumba, katika kuzaa, kila kiumbe alikifanya kizae kwa asili yake – yani zile mbegu ndizo zenye kuhifadhi asili. Udongo huzipokea mbegu zote tu na kuzihifadhi zipate kuongezeka katika kizazi. Naye Ibilisi akiwa anajua ukaribu wa maumbile ya nyoka na binadamu (Adamu/Hawa) kibailogia (kama leo hii wanavyochanganya mbegu ya farasi kwa punda na kumpata yule mnyama mule ambaye ana nguvu za punda za kubeba mizigo na kasi ya farasi katika mwendo!) Ndipo kama Biblia inavyoonesha Ibilisi alivyo muingia nyoka ili ajipatie uzao kupitia Eva. Nalo hilo likatimia ndipo wakazaliwa mapacha wawili wa baba tofauti – mmoja wa mnyama mwingine wa Adamu! Hata sayansi imethibitisha hilo la mwanamke kuzaa mapacha wawili wa baba tofauti kutokana na mwanamke huyo kutembea na wanaume wawili tofauti katika kipindi chake cha mayai kupevuka hivyo mayai yake yote mawili yakarutibishwa moja mwanaume wa nje ya ndoa na jingine mumewe. Tena mwanamke huyo alikuwa ni mzungu na akawa na hawara mweusi. Mapacha wakazaliwa hivyo mzungu, wa mume wa ndoa namwingine mweusi wa yule hawara!!

  Basi, Hawa akiwa ndiye Mti wa nne, ule Mti wa KIFO, kwa hiyo alipomshirikisha mumewe katika lile tendo, nje ya agizo la Mungu, madhara ya mti huo hayakuondolewa. Na matokeo ya kutokuondolewa kwa madhara hayo, mwanamke amebakia kuwa ni mti wa kifo hata leo! Sote tuliozaliwa na mwanamke ni lazime tufe.

  Basi kanisa likiwa ndiye mwanamke ule Mti wa Kifo, nalo limebeba mapacha! Basi vurugu zote hizi za kidini yaani madhehebu na cults, zinaashiria kifo kutokana na mbegu ya mapokeo. Sasa tutaponaje?

  Mbarikiwe nyooote!!

 49. Ndugu Mabinza,

  Nimeyaona maelezo uliyoyatoa. Labda nikukubalie hilo unalolieleza kuwa katikati ya bustani kulikuwa na hiyo miti miwili, ule wa Uzima na ule wa Ujuzi wa Mema na Mabaya kulingana na kifungu cha Mwz 2:9, kwa hiyo jumla ya miti hiyo itakuwa ni mitatu. Ambavyo wazo hilo ndilo limekuwepo katika wakati wote kuanzia hapo funzo hilo lilipoingizwa katika kanisa. Sasa ingependeza pia iwapo utatafuta jibu la Hawa, pale Mwz 3:3, kuwa ilikuwa ni nini, maana unapoongeza maarifa katika ile Mwz 2:9 na kuifanya iseme hivyo unavyotuambia, sioni ni kwa nini unashindwa kutuambia wazi wazi tafsiri ya jibu la Hawa!

  Ukiwa umeshindwa kuyaamini Maandiko katika urahisi wake kama yanavyo onekana, na kubaki unazunguka zunguka ukiondoa ‘koma hapa au nukta’ nk, labda nikushauri uchukue wasaa tena ili upate nguvu ya kukuleta katika hali itakayokufanya uyaamini Maandiko ili uyaache yakufunze kuliko kuyatangulia mbele!

  Ubarikiwe!

 50. Wapendwa,

  Nimeipenda hii ‘finetuning’ ya Sam, ukifinetune zaidi, mambo unayoyaona yanatisha! Hebu turudi hapo hapo katika Marko 16:17  hapo inaposema kuwa ishara hizi zitaambatana na waaminio; kutoa pepo wachafu, kuwawekea mikono wagonjwa nao kupona, kunena kwa lugha nk. Basi kama nimeyaelewa vizuri Maandiko haya, ni kwamba yeyote yule anayesimama kuhubiri ni lazima awe kwanza AMEAMINI, nazo ishara hizo huambatana na huyo aliye amini. Sasa unapomkuta mtu anayekataza ishara hizo kuwa zimepitwa na wakati, halafu ameshika Biblia na misalaba na amewakusanya maelfu ya watu akiwahubiria Injili ya Kristo, hivi mtu huyo atakuwa anafanya nini? Bila shaka atakuwa anawadanganya hao wote aliowakusanya, maana anawahubiria jambo asiloliamini! Hatma ya hao watu itakuwa ni nini? Naogopa hata kuliwazia hilo, labda wapendwa mlio katika Nuru zaidi mwaweza kunisaidia katika jibu la hatma ya kundi hilo kiroho kulingana na Maandiko!!

  Bwana, atuhurumie!

 51. Mpendwa Sam,

  1. Nashukuru kwa kuuona mchango wangu, kwa kuanzia,kama ulivyo eleza katika Post yako ya Saturday, may 5, 2012 at 9:54pm; naomba nikujibu kama ifuatavyo:- kama inavyo someka ile Mw.2:9, ni wazi kuwa kuna sentesi tatu zenye kushabihisha maana mbili. Sentesi ya kwanza inaanzia pale inaposomeka “BWANA……” na kuishia pale penye alama (;) na ile yapili inaanzia kwa kusomeka, “na mti wa uzima….” na kuishia penye alama ya mkato, na ile ya tatu imeanzia kwa kusomeka “…na mti wa ujuzi…” na kuishia katika alama ya kituo. Ukiusoma kwa makini mstari wote na kuugawa katikati, utasomeka hivi “9 BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa;….”(kipande au nusu ya kwanza ya mstari huo imeishia hapo) na sehemu ya pili ya mstari huo inasomeka hivi, ”….na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” (kipane cha pili, au nusu ya pili ya mstari huo imeishia hapo). Sasa hebu ona, Kipande au ile nusu ya kwanza, inajitosheleza moja kwa moja kuwa “Aina ya kwanza iliyokuwa imechipushwa katika ardhi bustanini, ni ile ya mti utamanikao na pia unafaa kwa kuliwa” – nadhani hapo nawe huna kesi. Lakini ukisoma ile nusu ya mwisho ya mstari huo utaona umegawanywa kwa alama ya mkato( ,), na kufanya ziwe sentesi mbili, lakini zikielewesha tu kuwa “Katikati ya bustani kulikuwa na mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya”. Maana yake, katikati ya bustani kulikuwa na aina mbili za miti, yaani mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na kufanya kuwepo na jumla ya aina tatu za miti katika bustani hiyo nzuri ya Bwana Mungu!
  2.

  1. Sasa, naomba tuwe pamoja hadi kwenye ile,Mw.3:22, ambayo umesema nimeiachia tu, kwakuwa nilizingatia sana theolojia, vinginevyo ningegundua kwamba kulikuwa na mti wa nne, na mti huo ndio Hawa. Nikirudi pale Mw.2:16,ili nione wakati Mungu akitoa maelekezo ya matumizi ya yale matunda toka katika ile miti iliyokuwemo Bustanini. Nimefanya hivyo nipate kuoanisha na lile tamko alilolitoa BWANA Mungu,mara tu ya kutwaliwa kwa tunda toka katika moja ya miti iliyokuwemo katika ile bustani yake nzuri! Mw.2:16-17 inasomeka,”BWANA Mungu akamwagiza huyo Mtu, akisema,matunda ya kila mti wa bustani waweza kula. Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika”. Lakini,ukisoma Mw.3:22 inasomeka hivi,”BWANA Mungu akasema, Basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;” Hadi hapo, naendelea kuona kuwa, Tunda lililoliwa ni la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ambao ni mti wa katikati kwa mjibu wa ile Mw.2:9 kama nilivyokwisha fafanua hapo juu. Uliniambia pia kuwa, nanukuu “…..Kwa hiyo suala la Kujua Mema na Mabaya si lazima uwe umekula tunda la Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya kama tunavyoona hapo katika Maandiko, Mwz 3:3!” mwisho wa kunukuu. Nimetafakari sana kauli hiyo,lakini nikili tu wazi kuwa, bado SIJAIKUBARI, maana hata ile kanuni tu ya kawaida, si lahisi mtu kula EMBE harafu akapata matokeo ya mtu aliyekula NDIMU! Mtu aliambiwa asile tunda la mti wa UJUZI WA MEMA NA MABAYA (Mw.2:16-17), na tunaendelea kuona kuwa mtoa tamko Mungu, naye anasema Mtu huyu tayari amekwishajua MEMA NA MABAYA! (Mw.3:22)Sababu hiyo ni ya kwanza kunipa ukweli kuwa, tunda lililoliwa ni kutoka mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ndiyo maana matokeo yake kwa mlaji ilikuwa ni KUJUA MEMA NA MABAYA! Lakini ushahidi wa pili naupata kutoka katika ulizo la BWANA Mungu katika Mw.3:11, inasema “…..je, umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?” Matunda ya aina ipi ya mti aliagizwa asiyale? Linganisha na Mw.2:16-17! Ushahidi wa tatu ni jibu la Adam, alijibu katika Mw.3:12 kuwa, “…..Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliye nipa matunda ya mti huo, nikala”.
  2.
  3. Lakini, kuhusu jibu la Hawa kwa nyoka kuwa, hawakuruhusiwa kula hata kuyagusa matunda ya mti wa katikati (Mw.2:16-17) Ukilinganisha na Mw.3:3) aliyapata wapi? Ni kwamba, alichojibu Hawa ndicho Mungu alichokuwa amekisema,vinginevyo Biblia ingesema kwa manufaa yetu leo! Hata hivyo,Biblia inasema si kila alilolifanya BWANA limeandikwa! Soma,Yh.21:25. Nakatika Rum.1:17, inasema,Haki ya Mungu hudhihilishwa ndani yake toka imani hata imani.Hata hivyo, hatupaswi kuamini kisichothibitishwa kwa neno, maana Neno la Mungu ndiyo kweli,Yoh. 17:17! Tafadhali Ndg, yangu Sam, hebu nipe vigezo tosha vya kimaandiko ili nielewe kama kweli Hawa ndiye ule mtii na kwa jinsi gani alijila kama tunda, na Adamu alikula tunda lipi kwa Mti Hawa! Natumaini utanirudia hivi punde. Endelea kubalikiwa na Bwana.

 52. Mpendwa wangu Orbi,

  Na wapendwa wangu wote katika Bwana, mimi hufurahi sana ninapo pita katika safu hii na kukuta maoni ya watu mbalimbali. Nahuzunika sana ninapoona Mtu au dalili ya Mtu kuonyesha “kukaa pembeni” kwa maelezo kuwa “Anasikilizia” kwanza! Katika, Ebr.10:25, inasema tusiache kukusanyika,tuonyane, na tuzidi kufanya hivyo kwa kadri tuonavyo kuwa SIKU ile ina karibia. Hakuna salama yoyote katika Roho, kwa Mtu yeyote anayetahayari wakati yeye tayari ni Mtumishi katika shamba la Bwana! Mpendwa wangu Orbi, naomba usinishushe moyo kwa kukosa michango yako, kwa sababu yeyote ile! Zaidi sana yaangalie maandiko, na uamini kuwa yapo kwa ajili yako LEO! na kwamba wewe haufanyi kazi yako mwenyewe – ETI, waweza kuiacha, kuizira kwa mda au kuibadili! Changamoto ndicho kipimo cha wazi cha kupimia kazi zetu. Gal.6:4, inatushauri tuzipime kazi zetu wenyewe! Yatupasa pia kuwakarisha kwa uvumilivu na uaminifu, wale wote wanaosababisha Mambo ambayo, hatukuyazoea “Mageni” kama inavyoshauri 3Yoh.1:8. Kwa nini? Paulo katka 1Kor.3:13 anatujurisha kwamba, kila kazi tuzifanyazo “ZITATESTIWA” kwa moto, na Kristo mwenyewe! Naomba nimalizie kuwa,Sijajua kwa nini useme hivi? Nanukuu “Hata hivyo kwa sasa nitatulia na nijifunze hao watakao kuja na hicho “chakula” kigumu kuhusu hilo Tunda…….Labda kwa wengine tunaokunywa maziwa tunaweza kupata kitu…….” Mwisho wa nukuu. Mara zote nimekuona “mla chakula kigumu!” kwa hiyo Biblia inakushauri vema, inaposema katika,2Tim,2:15 kuwa, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kuhayari, ukitumia kwa halali neon lakweli.” Asante.

 53. Ndugu Orbi,

  Kwanza nikushukuru na pia niseme kwamba lile karipio si lako bali ni la ki-Maandiko, kwa hiyo lafaa kuwepo hapo wakati wote tunapojadili chochote kile, basi hilo liwe anchor yetu! Asante kwa hilo na Mungu akubariki! Pia nikuhakikishe kuwa nami ni mtu wa mtaani tu.

  Kuhusu uhitaji wa kulijua “Tunda” katika kipindi cha Huduma ya mtume Paulo, nimezungumza hilo katika jinsi hiyo kulingana na Maandiko. Kwani Huduma ya Paul haikuwa yake binafsi bali alikuwa Kristo Mwenyewe akijenga Msingi wa kanisa lake. Naye akiwa ni Mjenzi Imara, hawezi kuchukua material ya kupaulia jengo na kuitumia katika Msingi!

  Pia umeniuliza, nanukuu kwa sehemu: “…Je kwa kulijua hilo “Tunda” ni lipi kunaweza kuleta ufahamu mpya kuhusu UASI DHIDI YA DHAMBI……Je kanisa linaweza kuulewa Wokovu kwa jinsi tofauti……..?”

  Mimi ninaamini kuwa mtu anapolijua jambo lolote lile, hilo humuongezea ufahamu zaidi wa jambo hilo na uhusiano wake kimazingira na hivyo ujuzi huo kumsaidia katika kukabiliana na changamoto za maisha, hata yakiwa ni ya Wokovu.

  Kwamba “kanisa katika miaka 2000 ya uwepo wake linatambua nini kilitokea hapo bustanini”, nadhani mwisho wa mjadala huu utakupa picha kamili iwapo uko sahihi au ulidhania tu kuwa kanisa linajua!

  Pia definition ya UASI ni kubwa ukiiangalia out of focus, lakini unapo finetune binoculars zako, utashangaa kuwaona katika kundi la waasi, hao unaodhani wameokoka! Kwa mfano hebu tulifinetune dhehebu la Katoliki; Pale linaposema ile Marko 16:17 kuhusu ishara kuambatana na waaminio, kuwa mambo hayo yalikwisha na mitume na hivyo wanaoyafanya ni wazushi, Je, huu si UASI?

  Kwa hiyo, miaka 2000 ya NURU, kutoka INJILI MOJA, na ROHO MMOJA, imezalisha makundi zaidi ya 10,000 yote yakidai kuwa wao ndio HALISI! Michezo hiyo si kwamba imekoma, bado inaendelea. Mungu akitupa miaka mingine 2000, si ajabu ukakuta katika kila nyumba ya vyumba sita, kila chumba na dhehebu lake!!!

  Hiyo ndio sababu tunarudi kule Mwanzo ili tubaini ni nini hiki? Tunamtegemea Bwana kutuongoza katika hilo katika shauku yetu ya kumfanyia Mungu wetu Ibada iliyo SAFI katikati ya vurugu hizi za kidini!!

  Ubarikiwe!

 54. Sam,

  Kwanza naomba msamaha kama maandiko yangu yametoa karipio……sina cheo cha uchungaji….hata usemashi tu wa kuwa na uwezo wa kumkaripia mcha Mungu yoyote ile….

  Lakini ndugu mimi sina woga wowote na kuyachambua Maandiko……mimi naamini pasipokuwa Mberoya utakuwa unameza chochote kile kinachotoka mimbarini…….

  Na umenishangaza mno uliposema wakati wa Paulo hakukua na uhitaji wa Kujua hilo tunda lilikuwa ni lipi……Hebu niambie kwa nini sasa kuna uhitaji wa kujua Tunda hilo…….Je kwa kulijua hilo “Tunda” ni lipi kunaweza kuleta ufahamu mpya kuhusu UASI DHIDI YA DHAMBI……Je kanisa linaweza kuulewa Wokovu kwa jinsi tofauti……..?Kanisa lina miaka 2000…. likitambua nini kilitokea pale bustanini….na Mungu alifanya nini dhidi ya UASI HUO……….Na mpaka Leo Neno la Mungu linasema SIKU YA WOKOVU NI LEO…..au NA SISI JE TUTAPATAJE KUPONA TUSOPIJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII………? Sidhani kuna “ufunuo” mpya katika kujua hilo tunda ni nini…..!!!!

  Hata hivyo kwa sasa nitatulia na nijifunze hao watakao kuja na hicho “chakula” kigumu kuhusu hilo Tunda…….Labda kwa wengine tunaokunywa maziwa tunaweza kupata kitu…….MBARIKIWE

 55. Mpendwa wangu Juma,

  Uendelee kubarikiwa,ndiyo maana ya kujifunza, asante kwa majibu yako. Neno la Mungu husema “ Hekima hulia na Ufahamu hupiga kelele” Kwa maoni yangu, ni jambo lisilo maana, iwapo Mtu ataona kuja kwetu katika Blog kama hivi, hatuvuni lolote! Binafsi nazidi kunawili kwa mafundisho na maelekezo yenu nyote myatoayo wapendwa. Najua na kuamini kuwa mahali kama hapa ni lazima shetani ajaribu naye kujihudhurisha pamoja na watoto wa Mungu, niwatoe mashaka kuwa, Neno linasema, “Nguvu za kuzimu hazitaliweza kanisa” Mungu wetu mwema ataendelea kutuondolea “Miiba” ili katika kula tusimeze kila kipikwacho! Maana amesema,Bila mimi ninyi hamuwezi Neno lolote. Inawezekana sikukuelewa vema katika maana uliyokuwa nayo katika hiyo “Statimenti” yako, ndipo kwa pupa nikashawishika kusema tu kuwa, tunapaswa kuingia kwa kujiamini na kwa “Hadhi” sawa katika ulingo huu wa mafunzo! Asante sana.

  Mpendwa Orbi,
  Nimepata nafasi ya kupitia post yako ya Saturday, May 5, 2012 at 8:25, nimefurahi kuona kuwa uko makini na umejaa tahadhari kuu. Ndg yangu, umesema hivi ”Unaweza kuja na mafundisho yoyote yale (speculations) kuhusu hilo tunda, lakini kanuni moja ya msingi ni kwamba Biblia inapokuwa Kimya unakuwa kimya, na kama unajaribu kuweka maana yako basi unafanya kwa uangalifu mkubwa mno…” Sijaelewa unachomaanisha katika usemi wako kwamba”…..Biblia ikikaa kimya unakuwa kimya, na kama unajaribu kuweka maana yako basi unafanya kwa uangalifu mkubwa mno…” Kila nikitazama katika hii habari ya Tunda,Hawa, Shetani na Bustani, sioni ni wapi na kwa lipi Biblia imekaa kimya; ninachokiona ni “Mafumbo yaliyoainishwa kwa njia ya mfano” kule kutotajwa kwa “Maana” ya mti alikochuma Tunda Hawa, ni Fumbo lililoelezwa kwa Njia ya Mfano! Kwanini iwe kwa Mifano? Mh.3:1 inasema, kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya Mbingu. Kwa nini tujihangaishe kujua kutoka katika Mifano yenye Mafumbo? Sasa ni wakati wa Mifano na Mafumbo kuwekwa wazi kwetu; Ukisoma Mk.4:11-12, Biblia inasema, sisi tumejariwa kuijua Siri ya Ufalme wa Mungu,lakini walio NJE wao yote wafanyiwe kwa Mifano. Kwa nini? Ili wakitazama wasione, na wakisikia wasikie,lakini Wasielewe; WASIJE WAKAONGOKA, NA KUSAMEHEWA; Kwa nini basi? Kwasababu wao WAPO NJE, basi hakuna maana nyingine! Kwa mtazamo huo, mimi naona, Kama yupo atakayejaliwa na Roho Mtakatifu,kutoa Maelezo ya wazi ya Ki – Biblia (Lakini Yasiwe yatokanayo na Tafsiri na mafundisho ya akili za kibinadamu) yatakayopelekea, kuujua Mfano wa Fumbo la Edeni, nadhani ni vema akaendelea kutufundisha MAANA SISI TUPO NDANI, Kuzijua Siri ni majaliwa yetu!.
  Mbalikiwe wote.

 56. @ Milinga

  Asante kwa yote, zaidi tumshukuru Bwana ambaye huitazama shauku ya mioyo yetu katika yeye ili tumjue zaidi hata tutawale pamoja naye! Ubarikiwe!!

  Nimekupata!! Bali vuta subira kidogo ili twende sote kwa pamoja nikiyajibu maswali yaliyojitokeza, kwani Changamoto huwa ni ya moto, basi lazima tuipoze kwa kuyajibu maswali!

  @ Mabinza

  Kwanza nikushukuru kwa changamoto. Pili tuirejee post yako katika mambo mawili matatu ili tuone kama tutafika katika kukipata kile kilichoandikwa. Nikinukuu ulichokiandika kinasema hivi: “Bali ule mti wa Uzima na ule wa Ujuzi wa mema na mabaya ndiyo iliyokuwa katikati ya bustani!” Lakini Maandiko yanasema hivi, “…Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya” Kwa hiyo nadhani tukibaki hapo, twaweza kuyaona mengi zaidi kuliko tukikisia kwa kuogopa yaliyo mbele!

  Pia umeandika, “Msikilize shetani alichojibu kwa mwanamke katika Mw.3:5, Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, MKIJUA MEMA NA MABAYA! Sasa baada ya kuliwa tunda hilo, Mungu alipokuja akaona tunda lililoliwa, akasema katika Mw.3: 22 kuwa, mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, KWA KUJUA MEMA NA MABAYA, na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala akaishi milele. Hadi hapo naona kuwa Tunda lililotwaliwa na Hawa ni lilokuwa katika mti wa KUJUA MEMA NA MABAYA!”

  Kimsingi, conclusion uliyoifikia ndiyo hiyo iliyopo kiteologia. Ila sijui tu katika hilo tawi lako teologia Tunda hilo mnasema nini. Lakini tunapoyaangalia Maandiko yanavyojifunua, basi hiyo Mwz 3:22 ilipaswa kuwa nuru zaidi kwetu hata tujue kuwa pia hilo tunda la huo Mti wa Nne, huo wa Mwz 3:3, likiliwa lingekufanya Ujue Mema na Mabaya! Hata hivyo Mungu alipowakataza kula mti huo hakuwambia habari ya KUJUA MEMA NA MABAYA, bali KIFO! Kwa hiyo suala la Kujua Mema na Mabaya si lazima uwe umekula tunda la Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya kama tunavyoona hapo katika Maandiko, Mwz 3:3!

  Pia nilidhani utatupa maelezo zaidi kuhusu lile tamko la Hawa kuhusu huo Mti waliokatazwa hata kuugusa, jambo ambalo hatulioni katika maagizo ya awali waliyopewa na Mungu; Je ni kwamba Hawa alikuwa anaota ndoto za mchana au ni nini basi, maana umesema uongo haukuwema ndani yake, kwa hiyo ni nini!???

  @Orbi

  Nakushukuru kwa post yako, na karipio lake!

  Lakini himizo mojawapo kwa mkristo ni kujifunza Maandiko (2Tim 2:15). Nayo Maandiko, yameandikwa! Kwa hiyo NINAAAMINI kuwa tunapoyatafakari yaliyojiri Edeni, kutoka katika yale yaliyoandikwa, HATUWI TUMEVUKA YALIYO ANDIKWA!

  Pia, ni muhimu kufahamu kuwa hakuna mwanadamu aliyeandika chochote katika Biblia katika namna ya UJUZI wake, bali Bali waliandika kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, ndio maana Biblia yote katika ujumla wake, inaitwa NENO LA MUNGU!

  Kuliogopa jambo lolote lile bila sababu ya ki Maandiko, huashiria ukosefu wa Imani katika ukiri wako wa chochote kile, hata ukiwa ni wokovu. Nao Ujasiri tunaopewa hautegemei uweza wetu, bali Nguvu zake yeye atupaye kushinda. Ndio maana tukiwa na kiu ya kuijua ILE KWELI, sisi huyaendea hayo Maandiko ambayo NDIYE YEYE na hutafuta kuzungumza naye, tukimsubiri yeye atuoneshe. Hatumfungii nje kwamba tumeridhika na hayo yaliyoandikwa nasi tukiwa hatujui ni nini, nao wanaotuambia wamepewa kazi ya kutuchunga wanazidi kutugawanya makundi kwa makundi. Kila tunapowauliza kulikoni? Majibu yao huwa ni ya mkato na ya kufisha kiu kwa vitisho vya kukufuru! Nadhani wakati wa vitisho umepita, huu ni wakati wa UWAZI na UKWELI ! Ukiona ulimwengu uko katika move yoyote ile, basi jua kuwa move hiyo imeanza katika ulimwengu wa Roho!

  Basi ndugu yangu, kama una lolote lile uliloliona katika Maandiko, njoo tujumuike pamoja! Kwani wakati mwingi wakristo, kwa uoga wao wa kudanganywa, huishia kudanganywa! Lakini ninaamini kuwa umefika wakati ambao wakristo hawapaswi kudanganywa tena. Maana Injili tumekwisha kuhubiriwa. Nazo Biblia zinagawiwa na kuuzwa kila kona, na wengi wetu tunajua kusoma, na ZAIDI YA HAYO TUNAYE ROHO MTAKATIFU. Basi tuna wajibu wa kuamini hivyo kwanza kabla hatujamsikiliza yeyote yule, vinginevyo wishful thinking ya mambo hayo, inakuacha katika Intellectual Faith ambayo ni useless when it comes to contending for the Faith! Basi twapaswa tuwe na UJASIRI wa kumsikiliza hata shetani ili tuweze kumkataa, ndiyo maana tunayavinjari Mapokeo na kuyapima katika Neno!

  Pia kujiridhisha kuwa unayajua yote yaliyo katika Biblia, nadhani huko ndiko KUYAPITA YALIYO ANDIKWA. Kwani katika Biblia kuna nabii zilizofungwa ambazo tunategemea kufunguliwa kwake. Sasa sijui itakuwaje kama tumekwisha yatamatisha Maandiko!

  Kuhusu mtume Paulo, nadhani nukuu ulizozitimia ulipaswa uende mbele zaidi ku sum up alichokuwa akikifundisha hata Roho Mtakatifu akamrejesha kule Edeni (kama alivyopelekwa Filipo kwa Toashi) kuyaona yaliyotokea na si issue ya “kunukuu vifungu”; hivyo ndivyo inavyosomwa Biblia na kueleweka katika kina kilichokusudiwa. Basi Roho asingelizungumzia habari ya Tunda katika siku za Huduma ya Paul, kwani halikuwa hitaji la wakati huo, bali leo hii tunapofika huku MWISHO! Ndiyo maana leo hii tunayapitia upya, kweupeee, mazungumzo ya Hawa na Nyoka kubaini ukweli wa Fundisho la Kiteologia, USIOGOPE!!

  @ John Haule

  Asante kwa maelezo yako.

  Ninashukuru kwa somo jipya la KABBALAH NA LILITH (babewatoto)! Nikipata wasaa nitalitazama hilo, ila kwa sasa nadhani ni vizuri tukayatazama yanayotuhusu, kwani dini ziko nyingi sana. Bali Ukristo huondoa kiu yote ya miungu mingine!!!

  Tunajaribu kuyatafakari maneno ya Hawa, ndipo tufike katika conclusion ya kubaini aina za miti iliyokuwemo humo bustanini. Je ilikuwa mitatu au minne? Kama ni mitatu, vipi kuhusu haya maneno ya Hawa? Nadhani hilo litaendana na mada, hata kama umeshindwa kufika katika uamuzi yaani umetatizika na hali hii iliyojitokeza, si kwamba eti unakuwa si wa kiroho. La hasha hata Roho, sisi hupewa kwa kipimo kulingana na Imani yetu.

  @ Wapendwa,

  Ukristo wote ni CHANGAMOTO. Hivi kufukuza pepo wachafu, nawe hujaenda hata chuo cha Biblia, au huna hata mafunzo ya uganga wa kienyeji, je si changamoto hiyo kwa wasioamini? Leo hii nimeona wachawi wengi walio okoka wakipita makanisani na kupewa fursa ya kushuhudia mambo yao ya kichawi, mpaka sasa hivi tunajua kuwa pale darajani Salenda, kuwa kuna lango la kuingilia kuzimu! Je kujua kilichotendeka pale Edeni si cha manufaa zaidi kuliko hayo ya wachawi? Kwanza, itawafaidia hata kujua mtazamo mwingine wa mambo hayo na kuwapa fursa ya kuyakagua hayo zaidi katika Maandiko. Naye Mwenye kuyaandika, akikuona katika shauku hiyo, anawajibika kwa Neno lake kukuongoza humo na kukufunulia hayo!

  Mbarikiwe nyooote!

 57. Wapendwa

  Shalom,
  Sam,tunakushukuru kwa changamoto tunapata kuitafakari vizuri biblia,Nataka twende sawa kimaandiko, Makatazo yote ya kula tunda la mti yapo Mw 2. na si Mw3.

  Mpendwa Sam,umenirudisha na kunikumbusha huko nyuma nilipata kusoma wanachoamini mason na kabbalah kuwa eti LILITH(babewatoto)””alikuwa mke wa kwanza wa Adam alikataa kuwa chini ya Adam kama msaidizi ndipo Mungu ikabidi amtwae Hawa toka ubavu kwa Adam .nao wakitumia Mw 1:27;Mw2:22 na wanakupa mistari kadhaa ili uamini,Maandiko yatuambia kuwa huyo LILITH(babewatoto)ni pepo wa roho ya jinsia isaya 34:14 ni hayawani mkubwa.

  Pia ukiwasoma KABBALAH nao mti wao TREE OF LIFE, wanasimamia maandiko na kusema kuwa ndio mti wa Mw2:19 nao wanamwamini LILITH kuwa ndiye aliyeumbwa kwanza yeye na Adan kabla ya Hawa na wanatumia mstari Mw1:27kusimamia mafundisho yao na wanakupa mistari kadhaa.unaweza kuwagagua kwenye wikipedia utawakuta huko.

  Wapendwa,Mama yetu Hawa hawezi kuwa mti wa nne, kwa sababu mwanamke na mwanaume ndio wanakamilisha neno “Adam” yaani Mtu, Mw 5:1-2,Mw1:27

  Ukisoma Mw 1: yote ni uumbaji ktk Roho,mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Mungu akastare siku ya saba.

  Mw 2;ni uumbaji ktk mwili yaani ni vitu tunavyoviona kwa macho hili hali vilishaumbwa,ndipo inaposemwa ulimwengu wa roho ni dhahiri,
  Tukumbuke habari ya talaka,Yesu aliwaambia Mafarisayo je hamkusoma maandiko.? Mathayo19:4-6 .

  Wapendwa ,
  Mungu wakati anamkataza Adam(mwanaume)asile ule mti wa ujuzi Mw2:17 Hawa(mwanamke)alikuwako pia ktk roho.

  Sam
  Luka1:42 inakamilisha maandiko ya Mw3:15

  Ninatafakari wapendwa .

 58. Mpendwa Mabinza,

  Nimebarikiwa sana na maelezo yako. Yaani sikutaka umalize ila nikashitukia umemaliza maelezo yako yamenikuna sana. Ndiyo maana nimesema watoto wachanga kimaandiko watulie kwanza wajifunze kutoka kwa wakubwa zao. Wewe ni miongoni mwa watu ambao wanakula chakula kigumu siyo maziwa tena.

  Biblia imeeleza kwamba kuna watoto wachanga ambao wamemwamini Yesu hivi karibuni hawa wanapaswa kula chakula laini kwanza kabla ya kigumu. Biblia inasema pia Roho wa Mungu atatukumbusha yote. Kwa hiyo Roho Mt. hawezi kutukumbusha kama hatujifunzi na kukua hatua kwa hatua. Paulo aliwakemea wapendwa fulani katika Korintho kuwa walipotakiwa kuwa watu wazima bado walionekana kuwa wachanga wakitakiwa kula chakula kigumu badala ya maziwa.

  Mada hii ya TUNDA alilokula ADAM na EVA ni mada ngumu ukubali usikubali. Wanatheolojia, wenye elimu ya Uzamivu na Uzamili wanaeleza kila mmoja kivyake. Hata sisi ambao hatuna elimu ya uzamivu katika maandiko tunaomtegemea Roho Mt. bado tunajifunza na tuna mitazamo tofauti juu ya tunda hilo.

  Ndugu Mabinza na wengine kama akina Sam, Kinyau, John Paul na wengineo wenye upeo wa mada hii bado tunaendelea kuomba msiache kuzidi kutupa vitu adim katika mada hii hadi utata wote uondoke.

  Naomba mjadala uendelee tujifunze zaidi. Barikiweni wote.

 59. Wapendwa,

  Sitaamini kabisa kwa mtu yoyote atakayekuja na mafundisho/Ufunuo na kusema kwamba lile tunda katika kitabu cha Mwanzo lilikua ni tunda gani…..au ni mti gani kinyume na Biblia isemavyo…!

  Unaweza kuja na mafundisho yoyote yale (speculations) kuhusu hilo tunda, lakini kanuni moja ya msingi ni kwamba Biblia inapokuwa Kimya unakuwa kimya, na kama unajaribu kuweka maana yako basi unafanya kwa uangalifu mkubwa mno… ! na kanuni nyingine ya msingi ni ile ya MAANDIKO HUTAFSRI MAANDIKO….kwa kanuni hiyo basi utaona jambo la Msingi hapo halikuwa ni tunda lipi….liliwa, bali ni ukosefu wa Utii kwa kile Mungu alichosema, na tafsri hii ya wazi ya ukosefu wa Utii kwa Mungu ndio Paulo aliyojenga mafundisho yake katika nyaraka zake. Hebu soma Maandiko yake…..kuwa ni nini kilitokea pale Bustanini….

  – Romans 5:19: Kwa sababu kama kwa KUASI KWAKE mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi kadhalika kwa Kutii kwake mmoja watu wengi wameiingizwa KATIKA hali ya wenye haki….

  – Romans 5: 12: Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia Ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo Mauti, na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi……

  Kwa hiyo kwa mistari hiyo ambayo Paulo ameaanza kuijengea hoja ya Dhambi (UASI) ilivyoingia katika kizazi cha binadamu na wokovu MKUU ulivyokuja kwa Kristo, huwezi ukasema ni mafundisho ya kitoto (Sunday school) La Msingi kilichotokea katika katika Kitabu cha Mwanzo ni UASI WA KUTOMTII MUNGU…..Biblia iko kimya mno kuhusu Tunda…..ila Biblia inapigia KELELE kwa sauti Kubwa matokeao ya UASI huo ambao ulimleta Kristo…….!

  Na labda ukiendelea mbele tena na Paulo, kila alipokuwa akizungumzia kuhusu kilichotokea katika katika kitabu cha Mwanzo alikua akizungumzia uasi…! Wala hakujaribu ku- ” spiritualize” kama wengi wanavyojaribu kufanya….angalia tena maandiko ya Paulo;

  – 1Tim 2:14: Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa Kwanza, na Hawa Baadaye, Wala Adamu Hakudanganywa ili Mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika HALI YA KUKOSA….

  Paulo hajahangaikia kabisa ni Tunda lipi…..na amefanya “literal transalation’ ( hajaweka tafsiri yake).Angalia tena katika mstari huu;

  – 2Cor.11:3; Lakini nachelea, kama yule Nyoka alivyomdanganya Nyoka Hawa kwa hila yake akawaharibu fikira zenu, mkaucha unyofu wenu….

  Paulo katika maandiko yake yote anaponukuu Kitabu cha Mwanzo hasa tukio hila anazungumzia KUDANGANYWA/KUASI/KUKOSA…..Hilo ndilo somo la Maandiko hayo katika kitabu cha Mwanzo, aina ya Tunda, aina ya mti halikuwa somo kuu….!

  Huwa siamini kwamba kuja na maana zilizofichika “mystery” ndio zinafanya uwe wa Kiroho….! Au Chakula kigumu kina maana mambo mazito yenye “deep mystery” Siamini Paulo alikuwa na maana hiyo…..! Na kama kuna mafundisho mazito yenye siri zilizofichika huwa yanatupeleka kwa Kristo tu….na Wokovu wake…..! Kwani ndivyo alivyosema katika Efeso 3:1-9. Na kama kuna siri iliyofichika katika Tunda…..biblia imeonyesha ni uasi dhidi ya Mungu…..!Hakuna jingine…!

  Kwa mtazamo wangu ni kwamba maana za kutaka kujua aina ya tunda na aina mti/miti zinaweza kuleta majadala mzuri kwetu…Lakini kwa Paulo haikuwa swala la mjadala wowote…..labda ndio maana kuna mahali pengine ameandika….”MPATE KUJIFUNZA KUPITA YALE YALIYOANDIKWA” “DO NOT GO BEYOND WHAT IS WRITTEN”

 60. Wapendwa katika Bwana,

  Ambao mpo pamoja katika kuitafutia ufumbuzi Maada iliyo mezani –Kuwa, Ni mti upi Hawa alitwaa tunda? Mimi nawashukuru wote kwa kuwa mnafanya nizidi kujifunza kwa Bidii Neno la Mungu. Napenda pia kutoa dukuduku langu kwamba, kule kusema, kama alivyosema Ndg. Yangu Milinga, ati “ Nimefuatilia mjadala huu nakuuona kuwa una changamoto sana. Yaani hapa watoto wachanga kimaandiko wanapaswa watulie kwanza. Hili jambo ni la watu wazima zaidi yaani ni chakula kigumu” Si kweli, Neno la Mungu si timu ya Mpira, kuwa kuna Simba “B” au Yanga “A” Neno la Mungu hutafasiliwa na mwenye Neno lake, yaani Mungu mwenyewe kupita Roho mtakatifu wake. Naomba, watu wasiogope kutuletea michango yao kila waonapo kuwa Roho Mtakatifu amesemanao juu ya jambo lolote, ili tujifunze. Maana Neno linasema,limefichwa kwa wenye akili na kufunuliwa kwa watoto wadogo!

  Kuhusu aina ya Mti ambao hasa Hawa alitwaa tunda, ni vema kuyarejea kwa makini , maandiko yaliyo katika Mw. Sura ya 2 na ile sura ya 3 ambayo inasema Juu ya uoteshwaji wa ile aina ya Miti na maelezo juu ya kile kilichokatazwa wasifanye na kile walichokubaliwa kukifanya wakati wote wakiwa katika bustani hiyo nzuri ya Mungu. Mw.3:16-17 tunona “ BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula. Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa MEMA na MABAYA usile……..utakufa hakika” kimsingi inaonyesha kuwa, Mungu alikuwa akimwagiza “Mtu”; Na kwa mjibu wa Biblia ni Adamu, na Hawa akiwa sehemu ya mwili wa Adamu (Ubavu) huyo ndiye Mtu aliyeumbwa na Mungu akiwa kamili, aliyeumbwa na Mungu kwa mfano wake, Mw.1:26-27. Lakini, Mungu alipokuwa akitoa agizo lake kwa huyo Mtu,hakutaja kuwa msile wala msiguse matunda ya mti wa katikati, katika ile Mw.2:16. Jibu la kutokula au kuyagusa matunda ya mti wa katikati ya bustani alilitoa Hawa katika Mw.3:2-3 alipoulizwa na shetani katika Mw.3:1. Tufahamu pia kwamba, wakati wote huo Dhambi ilikuwa haijaingia kwa kiumbe huyu “Mtu” na Mungu mwenyewe anakili na kulidhishwa na kazi yake kuwa haina kosa, Mw.1:31.

  Kama,Biblia inakubali kuwa kazi ya Mungu mpaka hapo ilikuwa ni njema. JE, Tunaweza kusema Hawa alijitungia jibu lake kwa shetani kwamba, kuna mti katikati ya bustani usiotakiwa kuliwa na hata kuguswa matunda yake, iwapo hakumsikia Mungu akielekeza hivyo? Lakini tukirudi Mw.2:9 tunaona Mungu alichipusha katika Ardhi “kila” mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa;…….na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Lakini ukisoma kwa makini katika hiyo Mw.2:9, utaoa kuwa, ile aina ya mti utamanikao kwa macho na ufaao kwa kula, ulichipushwa kote katika Ardhi iliyokuwepo bustanini. Bali ule mti wa Uzima na ule wa Ujuzi wa mema na mabaya ndiyo iliyokuwa katikati ya bustani! Sasa hebu tuone tena katika Mw.3:2-3, Mwanamke anamjibu Nyoka kuwa,wanaweza kula matunda mengine yote isipokuwa matunda ya mti wa katikati ya bustani wasiyale hata kuyagusa, kinyume chake watakufa! Msikilize shetani alichojibu kwa mwanamke katika Mw.3:5, Kwamaana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, MKIJUA MEMA NA MABAYA! Sasa baada ya kuliwa tunda hilo, Mungu alipokuja akaona tunda lililoliwa, akasema katika Mw.3:22 kuwa,mtu huyu amekuwa kama mmojawetu, KWAKUJUA MEMA NA MABAYA, na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala akaishi milele.Hadi hapo naona kuwa Tunda lililotwaliwa na Hawa ni lilokuwa katika mti wa KUJUA MEMA NA MABAYA! Kwa Mw.2:9 na Mw.3:22 inanipa kujua kuwa katika ile bustani kulikuwa na aina TATU za miti, kwanza ile inayotamanika kwa macho na kufaa kwa kula, na pili, ni ule wa uzima na tatu ni ule wa ujuzi wa mema na mabaya. Lakini hiyo miwili yaaniule wa UZIMA na ule wa UJUZI WA MEMA NA MABAYA ilikuwa katikati ya Bustani! Nitafurahi kupata ufafanuzi mzuri zaidi iwapo itaonekana kwenu wenzangu sikuelewa vizuri, nipo hapa kujifunza. Mbarikiwe na Bwana.

 61. Mpendwa Sam,

  Kwa maoni yangu nakuomba somo lako kuhusu mada hii uipost yote hapa ili tuisome kwa mtiririko mmoja.

  Nadhani wewe ni miongoni mwa walimu wa Neno wenye upana mkubwa sana. Sijawahi kuona au kukutana na mwalimu mkali kama wewe anayeweza kufafanua maandiko kwa urahisi na kwa lugha inayoeleweka kama wewe hapa.

  Hebu post maelezo yako yote kuhus mada hii wala usiogope au kusita. Hapa tunajifunza. Mimi nimevutiwa na jinsi unavyofafanua neno kwa neno.

  Ntashukuru sana kupata somo hili likiwa kwa pamoja ili nilinakiri niwe nalo mahala niwe najisomea mara kwa mara.

 62. Mpendwa Haule!

  Mstari unaokataza huo mti wa nne usiliwe ni mstari wa Mw. 3:3. Usome kwenye Biblia yako, halafu huuamini kuwa ni Neno la Mungu!!!!!

  Ubarikiwe

 63. Wapendwa,

  Nami naendelea kujifunza kwa bidii kubwa juu ya mada hii na hasa mafundisho na mafunuo yanayotolewa na ndugu yetu Sam.

  Tayari nina maswali mengi ya kuuliza lakini nataka nijifunze zaidi kwanza kabla ya kuanza kuuliza maswali hayo au kuchangia chochote kufuatana na kiwango kidogo ninachofahamu kuhusu mada hii.

  Mmmmh, kidogo imeniacha njia panda baada ya kusoma kwamba mti wa nne ndani ya Bustani ya Edeni ulikuwa ni mama yetu Hawa, kwa maana hiyo ‘alijila’ mwenyewe!! Anyway, naomba ningoje kwanza mpaka mwisho wa funzo la Ndg Sam.

  Mungu awabariki sana!

 64. Wapendwa,

  Kweli changamoto ni kubwa, haswa unapofika katika kuyaamini maandiko hapo Mwz 3:3! Naona katika kuitafakari changamoto hii, ndugu Milinga ametuvusha hadi kwenye tafakari ya tunda lililoliwa, ingawa tulikuwa bado kwenye kuuangalia kwanza uwepo wa ule MTI wa NNE uliojitokeza katika maneno aliyoyaongea Hawa hapo ktk Mwz 3:3. Kwa hiyo, ninaamini tukiujua MTI uliochumwa Tunda, basi Tunda lenyewe itakuwa rahisi kulibaini.

  Milinga umezungumzia kuhusu Biblia kuongea kwa Mafumbo na mifano au tamathali za semi; Jambo hilo ni kweli. Labda niongezee tu, kuwa Biblia yote imeandikwa hivyo, yaani ni FUMBO au barua ya wapenzi, yaani kwa kanisa; kwa hiyo ili kuyajua yaliyo katikati ya mistari, inakulazimu kuwa katika Roho ya Mwandishi ndipo hilo huwezekana!

  Basi, tukirudi katika Maandiko katika nia ya dhati ya kupata ufahamu kuhusu hilo, Mungu yu tayari kutuongoza katika mafumbo hayo hata akatuonesha mambo hayo katika urahisi uliokusudiwa kwetu, akitufichulia siri hizo kutoka katika Maandiko hayo hayo! Maana MAFUMBO hayo hatukufumbiwa sisi!!!

  Kama tulivyoona, Biblia ni kitabu cha mifano (symbols), ndipo tumeziona zile aina nne za miti iliyochipushwa bustanini. kwanza ile ya kuliwa – pili ule Mti wa Uzima (Kristo), tatu ule wa ‘Ujuzi wa Mema na Mabaya’(Lucifer) na halafu ule Mti wa Katikati. Ndipo tunapozidi kuiangalia miti hii tunaona kati ya hiyo minne miwili ilikuwa imekatazwa kwao: Mti wa “Ujuzi wa Mema na Mabaya” -Lucifer- hawakuruhusiwa kumsikiliza wala kuwa na ushirika naye katika lolote lile – Mwanzo 2:17 “… walakini matunda ya mti wa ‘Ujuzi wa Mema na Mabaya usile kwa maana …” na mti wa pili ni ule mti ‘ulio katikati ya bustani…”. Kuitambua miti hii kutatusaidia kuijua ile dhambi. Huu mti wa nne unapaswa nao uwe kiumbe (‘a personality’). Huu usingelikuwa kati ya ile miti ya matunda ya kuliwa maana hilo lingeivuruga Biblia, kwani matunda yote yamo katika ile miti ya kwanza ya kuliwa nayo hata leo hii yanaliwa kwa wingi na hayajawahi kumfanya yeyote yule ajione yu uchi! Basi tunaporudi kule bustanini na kujaribu kuwaangalia wahusika waliokuwemo humo, ili tumpate huyo kiumbe mwingine ambaye ndiye MTI WA NNE, Maandiko yanatupeleka kwa mama yetu HAWA!!! Yeye ndiye alikuwa huo “Mti huu wa Katikati ya bustani” huo waliokatazwa wasile wala kugusa!!!

  Je, mwanamke si mti wa matunda!? Je, sisi si matunda ya mama zetu?. Huo ndio MTI uliokatazwa kuliwa Tunda lake. MTI uliokatazwa alikuwa ni Hawa!! Kwa hiyo, tunaona kwamba Hawa alikuwa ndio ule mti unaoelezwa katika Mwanzo 3:3. Hivyo ndivyo Biblia inavyotufundisha; mwanamke ni mti wa matunda. Katika Luka 1:42 Elizabeti mama wa Yohana Mbatizaji alimwambia Mariamu, ”Blessed is the fruit of thy womb” umeona huo mti wa nne pale Edeni! Biblia yako inakupasa uisome kutoka mwisho kurudi mwanzo – yaani uanze Agano Jipya kwanza. Uliamini hilo katika ukamilifu wake wote ili Mungu akupatie Roho wake kwa huo utii wako kwa Neno lake, kisha baada ya hapo sasa ukirudi katika Agano la Kale, lo, yote yanakuwa wazi nawe unakuwa mwana Halisi maana yote ya Baba yako unayafahamu, sasa Shetani hana uwezo tena wa kukudanganya maana umemfukua toka ardhini’, ule mti wa ‘Ujuzi wa Mema na Mabaya’ nayo mizizi yake umeitia ‘Chumvi’ na kuianika “JUANI” katika Kristo Yesu, HALELUYA!!!.

  Bila ya kulipokea Agano Jipya katika ukamilifu wake si rahisi kuambulia chochote “..mtu hataishi kwa mkate pekee bali kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu”.

  Mbarikiwe nyoote!

 65. Wapendwa,

  Ili kuweza kupata ukweli wa maandiko ya Mw.3:3 kuhusu tunda halisi walilokula Adam na Mkewe hadi kuwapotezea utukufu wao kuna maswala kadhaa tunapaswa kuelewa. Nimefuatilia mjadala huu nakuuona kuwa una changamoto sana. Yaani hapa watoto wachanga kimaandiko wanapaswa watulie kwanza. Hili jambo ni la watu wazima zaidi yaani ni chakula kigumu.

  Naomba niyataje mambo tunayopaswa kuyafahamu ndani ya Biblia kila mara tuisomapo:

  1. Biblia imeandikwa kwa kufuata kanuni mbalimbali ikiwemo kanuni ya ‘Flashing back the story” Yaani siyo kwamba Biblia imeandikwa kwa mfuatano wa matukio ya kwanza hadi tukio la mwisho (The Bible was Not written in a chronological order).

  2. Biblia imeandikwa wakati mwingine kwa kutumia lugha za picha (Figurative language) siyo kila mahala Biblia inapotaja neno fulani lina maana halisi inayotumiwa na wanadam. Kwa Mfano wasomaji wa Kitabu cha Nabii Daniel na kile cha Ufunuo wa Yohana watakubaliana na mimi. Kuna mahala Biblia inamtaja mwanamke Kahaba lakini haimaanishi mwanamke kahaba kama tuliowazoea mtaani wakijiuza miili yao. Biblia inamaana tofauti kabisa. Sehem zingine ukisoma kile kitabu cha Daniel inatumia lugha ya picha sana. Kwa mfano soma Dan 2: 31-34 Inasema, ” 31Ee mfalme, ulitazama na mbele yako ilisimama sanamu kubwa, kubwa mno kupita kiasi, sanamu inayong’aa inayotisha kwa kuonekana kwake. 32Kichwa cha ile sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi, kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha, tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba, 33miguu yake ilikuwa ya chuma, kwa sehemu nyayo zake zilikuwa chuma na sehemu nyingine zilikuwa udongo wa mfinyanzi uliochomwa. 34Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi na kuivunja.

  Ukisoma hapo utaona kuwa Biblia hutumia sehemu kubwa lugha ya picha. Hata Yesu alipokuwa akihubiri alitumia sana mifano na picha sana. Yesu anaposema mimi ndimi mkate wa uzima, au mimi ndimi mzabibu wa kweli, au anapotoa mfano wa Kondoo na mbuzi au wanawali kumi, nk msomaji asiyeelewa haraka anaweza akaanza kuwaza mikate tunayokula kila siku kwamba Yesu alimaanisha yeye ni mkate kama huu tunaokula. Itakuwa ajabu sana kumsikia mhubiri anayetafsiri maandiko hivyo.

  3. Tunapaswa kuelewa jambo lingine kwamba Biblia iliandikwa kwa kutumia mafumbo na tamathali za semi. Kuna mahala Biblia imeandikwa kutumia mafumbo ambayo yanahitaji tafsiri ya wazi au mbele kidogo Biblia imeyatafsiri maandiko hayo. Swala la Matunda ya Mti wa Uzima, Mti wa Ujuzi wa mema na mabaya, nk inayosema Mwanzo 3;3 inaweza kutafsiriwa kwa kufuata kanuni mbili au tatu kwa mtazamo wangu,

  Kwanza, waweza kuitafsiri kwa kutumia Lugha ya picha (figurative language) kulingana na mahubiri yako ulivyoyapanga na kwa walengwa wako unaowahubiri kwa wakati huo. Kwamba Adam alikula MATUNDA kama yalivyo matunda yoyote kama vile EMBE, CHUNGWA, PAPAI, APLE, NANASI, nk. Hii inategemea wewe unataka upeleke ujumbe gani. Lakini kuweza kulijua au kufahamu matunda halisi aliyokula Adam na Eva ni vigumu hapa kwa sababu Biblia haitaji kwa wazi zaidi ya kusema Matunda ya Uzima, ujuzi wa mema na Mabaya, nk. Hivi matunda hayo waliyokula yaweza kuwa MACHUNGWA, MAEMBE, NK.? Hii bado itaendelea kuwa mitazamo ya wahubiri. Kwamba Mungu alitumia picha ya matunda akimaanisha jambo lingine.

  Pili, mtu anweza kutafsiri maandiko hayo kwa mtazamo wa mafumbo ya Mungu. Mungu anatumia lugha ya matunda akimaanisha kitu kingine ndani yake kama Yesu alivyotumia mifano ya Wanawali 10 lakini kimsingi hakumaanisha Wanawali kama tuwajuavyo kila siku mtaani bali mfano tu.

  Tatu waweza kuyatafsiri maandiko hayo kwa kueleza kuwa hakuna fumbo lolote ndani ya maandiko hayo. Hapa waswahili husema “tafsiri si sisi” yaani unatafsiri neno bila kuangalia mktadha wa mwandishi au maandiko. Kwamba neno likisema “MATUNDA” basi moja kwa moja linamaanisha “MATUNDA” Kama tunayokula kila siku yaani NDIZI, EMBE, CHUNGWA, nk.

  Kwa hiyo, katika swala la matunda aliyokula Adam na Eva wapo wenye mtazamo wa kwamba Biblia ina maana ya matunda kama tuyajuavyo matunda yanayouzwa sokoni.

  Wapo wanaojaribu kufafanua kwamba Biblia haikumaaanisha Matunda Halisi bali kuna maana nyingine iliyofichwa ndani yake. Wengi hufikia mahala husema kwamba Matunda waliyokula Eva na Adam ni “Tendo la Ndoa”. Wengine husema kwamba ni ‘UASI” walioufanya yaani KUTAMANI KUWA SAWA NA MUNGU. Kwamba kule kutamani kuwa sawa na Mungu ndiyo imefananishwa na kula Matuda ya mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya.

  Wapo wanaosema kwamba kwa kuwa mbinguni tunasoma kuwepo MTI WA UZIMA utakaozaa Matunda aina 12 na watu watakula matunda hayo ili yawe TIBA yao ya milele. wanajaribu kuufananisha Mti huo na ule uliokuwepo katika Bustani ya EDENI ambao akina Adam na Eva wakila waliweza kuendelea kuwa na uzima bila kuugua.

  Swala hili la matunda waliyokula ADAM na EVA bado linahitaji mjadala zaidi. Lakini mimi namalizia kwa kusema kwamba somo hili ni gumu bado na linahitaji sote tujifunze zaidi na zaidi.

  Naomba kuwasilisha ili mjadala uendelee zaidi.

 66. Wapendwa,

  Nafahamu kwamba Maandiko haya yanayohusiana na huo mti, tunayajua tangia utoto wetu, huko kwenye Sunday Schools zetu nk. Pia tumekuwa ndani ya ufahamu huo madhebuni kwetu kulingana na fundisho hilo katika ukristo wetu wote.

  Jambo nililotaka tulitafakari katika fundisho hilo, ni kuliangalia katika mapana ya Maandiko ili kuona kama ndivyo Biblia inavyofundisha? Ikiwa ndivyo, basi hilo ni jambo jema. Na iwapo sivyo, basi hilo litatuhakikishia kuwa fundisho hilo ni mapokeo. Na kwa tabia ya roho wa mapokeo, kutakuwa na KWELI iliyofichika kwa makusudi ya kulikosesha kanisa mwelekeo halisi. Nasi tukiwa tumefika mwisho wa safari, basi kwa ile Ahadi ya Roho Mtakatifu ya kutuweka katika KWELI yote, inapaswa kututimilia hapa duniani leo hii na si mbinguni, baada ya kunyakuliwa!

  Nimeona post ya ndugu Milinga, nakushukuru kwa kutuletea mtazamo mwingine juu ya jambo hili.

  Nilichokiona kutoka kwa mwanateologia wetu ni kwamba, kwanza, anakubaliana na mapokeo kwa kututhibitishia kuwa Mti uliochumwa hilo tunda ni ule wa Ujuzi wa Mema na Mabaya. Pili, anatuambia kuwa hilo tunda lilikuwa ni Ufalme wa Kiakili. Pia anasema kuchuma tunda ni ni kitendo cha kuupokea uzuri na ujuvi huo au uzuri wa ufalme huu wa kiakili moyoni au nafsini.

  Katika mtiririko huo wa mwanateologia wetu, labda niseme kuwa katika lile jambo la “MTI UPI?” atakuwa amenena kama sote tunavyojua, kulingana na teologia, naye akiwa ni mmoja wa hao asingenena tofauti. Kuhusu “TUNDA hilo lilikuwa lipi au ni nini?” licha ya kwamba ametupa maelezo mazuri yenye kushawishi, binafsi sioni uwiano wowote wa ‘TUNDA’ hilo kuwa ni ‘UFALME wa KIAKILI’ kadiri ya Maandiko. Naona yeye ndiye anayetumia akili zaidi katika kulielezea jambo hilo kuliko Maandiko yanavyojifunua. Kwa kifupi sijaona rejea yoyote ya kimaandiko zaidi ya hisia zake za kiteologia!

  Sehemu nyingine anasema Adamu na Hawa walikwisharuhusiwa tendo la ndoa, kwa hiyo kama kula hilo tunda ilikuwa ni kufanya tendo hilo, ‘kusinge kuwa haramu ya laana kubwa waliyopewa’ pia jambo hili sijaliona mahali waliporuhusiwa kufanya tendo la ndoa wala walipo laaniwa katika Maandiko kama anavyotufunza!

  Labda kwa sasa tuliache jambo hilo la Tunda, maana huwezi kulijua tunda bila kuujua Mti kwanza. Na kama mti huo si huu wanateologia wanaotufundisha kuwa, basi hata hilo tunda analolifundisha litakuwa silo pia!

  Jambo la msingi tunalopaswa kulikumbuka kila tunapozifungua Biblia zetu, ni umuhimu wa kuweka mawazo na mafundisho tunayoyajua pembeni kwanza, halafu kuyaaendea Maandiko kwa ‘akili isiyoghoshiwa’ yaani ‘an open mind’. Itakuwa rahisi kwa Roho Mtakatifu kutufundisha kile anachotaka tukielewe katika umbali tuliopo.

  Nafahamu kuwa wengi wananiona kama mzushi, lakini twendeni pole pole na Maandiko, tusiyatilie shaka, tuyaangalie yanavyo jifunua, tutayaona mambo mengi sana!

  Wengi wetu tunamwangalia Hawa, yule tuliyekwisha kumhukumu! Kwa hiyo sisi humshikilia Hawa aliyekwisha kuhukumiwa, katika mahusiano yake yote na Mungu, labda pale tu wake zetu wanapopewa Uchungaji, ndio humkumbuka kuwa “alikuwa sawa na Adamu katika uumbwaji”!

  Basi, Hawa alipoumbwa alikuwa ni mkamilifu. Ndani yake hamkuwemo hila wala uongo wa namna yoyote ile! Hata anapokutana na Nyoka alikuwa ni MKAMILIFU, hivyo yote aliyoyaongea yalikuwa ni kulingana na UFUNUO waliopewa na Mungu! Kwa hiyo, kauli anayoitoa Hawa inapaswa kuchukuliwa hivyo, nayo kuwa ufunuo kwetu!!! Tena hilo lingetudhihirishia kuwa yako mambo mengine waliyoyajua au kufunuliwa au kuambiwa ambayo hayajaoneshwa katika hatua hizo tulizozitegemea kuoneshwa bali yamefunuliwa mbele katika mlolongo wa matukio kama tunavyo hadithiwa na Roho Mtakatifu mwenyewe!

  Kwa hiyo Mw. 3:3 inapotuambia: “Lakini, matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa”; haya maneno hayafanani na haya yaliyopo katika Mw. 2: 17 wala yaliyo katika 3: 5 yanayoelezea ushawishi uliokifanywa na Nyoka! Wala Mwz 2:9 haielezi kuwa Mti huo wa Ujuzi wa Mema na Mabaya ulikuwa katikati ya bustani! Sisi tunayarudia Maandiko ili kuona kama walichotufundisha wanateologia ni sahihi au la, kama walivyofanya Waberoya!!! Inaweza kuwa rahisi kusoma habari ya Waberoya, lakini kukawa na ugumu katika kuwa Mberoya! Bali hilo ndilo tunalolifanya Ndugu zangu.

  Biblia yangu ninayoitumia, KJV ambayo imehaririwa na Rev. C. I. Scofield, D. D. ambayo ni Study Bible, katika Mwz 3:2 imetanguliwa na maelezo ya utangulizi (ya hao wasomi) yanayosema: “The temptation of Eve: (2) adding to the Word of God”. Kwa tafsiri rahisi inasema: ”Kishawishi kwa Hawa: (2) kuongeza katika Neno la Mungu”. Ninaamini ya kuwa wasomi wengi waliongozwa na nadharia hiyo ambayo huenda Mungu aliiacha kwa makusudi katika kipindi chote hiki ili kuyaleta mambo yote huku mwisho wa wakati ndipo ayafunue hayo kwa kutuondolea ule utando wa mapokeo na kulifunua Neno lake! Ni katika mtiririko wa jinsi hii, ndiko kulikolifanya fundisho hili lisitiliwe shaka. Lakini ukweli ndio huo kama tunavyouona.

  Labda tukifika katika uelewa huu wa Maandiko, yaweza kutusaidia kuendelea mbele ili kubaini Mti huo ni nani?

  Mbarikiwe nyoote!

 67. Wapendwa Natafakari
  Mw 2:16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,

  …Kwa kusema hivi Mungu aliwaruhusu kula matunda ya kila mti(maanisha kila mti) tuuweke na mti wan ne wa Sam…..walakini…Mw2:17… Anautaja kwa jina……

  “matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”

  Mw3:5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua “mema na mabaya.”

  Sam hapo Mw3:5 shetani anautaja mti kwa jina
  ……kwa hilo hatuna shaka na jina la mti.

  ………….Wanadamu tuliumbwa mfano na sura ya Mungu kiroho/kimwili(Utakatifu)Mwanadamu alikuwa juu ya malaika na juu ya shetani mpaka pale alipoasi, Mwanadamu aliumbwa atawale mfumo wa ulimwengu huu wa kimwili kwa mfumo wa ufalme wa mbinguni kwahiyo aliishi ktk ulimwengu wa roho wakati yupo kwenye ulimwengu wa mwili,Hivyo alijua mema na mabaya, mwanadamu aliasi(anguka) kwa kutamani kufanana na Mungu,na ndiyo alivyoasi na shetani pia . Eze 28.Mungu aliuweka huu mti kumtadharisha (ishara) binadamu kuwa huo ujuzi wa mema anaouona kuna mambo yamefichwa nyuma(evil)baba wa uasi alikuwapo asije mlaghai(hila)

  Tunajifunza
  Sam endelea kutupa tafakari yako ili tujifunze na hata mtu mwingine anaweza pia kuleta ufahamu unaofanana na wa Sam isiwe nikawazuia kwa kumtaja Sam,ila majibu yasipotoshe kiwango cha maandiko yaani tusitafakari kwa hisia kwa kudhani ni sahihi.

 68. Mpendwa Haule!

  ukipitia bandiko langu utakuta kuna swali nimekuuliza ni vema na inapendeza ukalipitia na kujibu.

  Ubarikiwe

 69. Wapendwa, niliahidi kuendeleza niliyo nayo, lakini kwa jinsi ninayoyaona ambayo ni mageni kwangu, NIMEAMUA nitulizane kwanza nijifunze. Maana Sam anasema miti iko minne na Milinga anasema tunda ni la kiakili, sijui mwingine atakuja na nini?
  Kwa hiyo ninakaa dawatini niwasikilize na pia nawaomba mniruhusu kuwauliza maswali.

  Shalom!

 70. Je, Adamu na Hawa walikula tunda gani?

  Wapendwa naomba niwashirikishe maelezo haya yaliyotolewa na mtaalam mmoja wa theolojia.
  Wengine husema ni tendo la ndoa
  MAGONJWA, DHIKI, MAHANGAIKO YA MAISHA NA KIFO NI MATOKEO YA DHAMBI WALIYOIFANYA WAZAZI WETU ADAMU NA EVA KATIKA BUSTANI YA EDENI. BIBLIA HIELEZEA DHAMBI HIYO KUWA NI KULA TUNDA LA MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA ULIOKUWA KATIKATI YA BUSTANI HIYO. WASOMAJI WENGI WA BIBLIA HUTOFAUTIANA JUU YA NINI HASA KILIKUWA TUNDA HILO, WENGINE WAKISEMA NI TENDO LA NDOA. MWANATEOLOJIA TITUS AMIGU ANACHAMBUA UTATA HUO AKIJIBU SWALI LA BW. GOTI CHIWAMBO WA S.L.P. 911 SONGEA JUU YA SUALA HILO.
  Ufalme wa kiakili ndilo tunda aliloonyeshwa Eva na Shetani kichwani na moyonimwake. Basi Eva alipofikiria juu ya manufaa ya ujuvi au ufalme huu wa kiakili moyo wake ulitamani akaona wafaa kuliwa kwa vile ulipendeza kiakili.
  Hapo akaendelea na hatua ya kuchuma tunda kile hicho ni kitendo gani? Hicho ni kitendo cha kuupokea uzuri na ujuvi huo au uzuri wa ufalme huo wa kiakili moyoni au nafsini yaani kulileta nafsini ndiko kulichuma na kulikumbatia moyoni ndiko kulila.
  Hivyo basi tangu kuliona tunda lile hadi kulichuma na kulila, mambo au vitendo vyote vinetendeka kiakili hazikuwa habari za tunda lenye kugusia kama papai , chungwa au ndimu, Tuendelee mbele.
  Baada ya kulila mwenyewe, Eva alimsimulia Adam juu ya suala hilo la kiakili pevu la ufalme na madaraka kamili ya kiakili.
  Huko kumsimulia Adam habari hiyo ndiko kunakoitwa ‘’KUMPA ADAM TUNDA’’ Naye adamu kwa upande wake alipoelewa na kutia moyoni habari hiyo ya ufalme au mamalaka kamili ya kiakili ndiko kunasemwa ‘’NAE AKALA” .
  Kwa kifupi ndugu maluli hilo tunda si tunda kama tunda ila ni zao la mti wa kiakili yaani akili peve kabisa ambalo ni ule ufalme wa kiakili au mamalka kamili ya kiakili.
  Kuliona tunda ni kule kubaini uzuri wa tunda lile la kiakili na kulichuma ni kule kuhamishia ufalme huo wa kiakili kwenye moyo binafsi.
  Kulila tunda hilo ni kule kuweka moyoni au akilini ufalme huo wa kiakili na kumpa Adam ni huko kumsimulia Adam habari za ufalme huu wa kiakili na kula kwa Adam ni huko kulipokea yeye binafsi neno hilo na kuliweka pia moyoni au nafsini mwake.
  Ndugu Kanyoto watu wengine hung’ang’ania tafsiri kwamba tunda lililoliwa ni ‘’TENDO LA NDOA’’ HII NI TAFSIRI POTOFU .Fikiria hoja au mambo matatu ambayo sasa ninataka kukuambia.
  (I)Ashakum si matusi Eva alichumaje tunda ambalo liko mwilini mwake mwenyewe? Kuchuma maana yake ni kutwaa kitu toka mahali kilipotundikwa na kuleta mahali pengine. Eva asingeweza kwa mwili wake mwenyewe
  Aidha alikulaje tunda hilo kabla ya kumshirikisha Adam hali yeye ni jinsia moja pakee yake? TUSIENDE KWENYE MATUSI hakuna heko wala misingi yoyote ya kimaendeleo.
  (II) Fikiria viungo vya uzazi utavielezeaje kama ni mti wa ujuvi wa mema na mabaya? Mbona ahera picha hiyo ingekuwa ya kichwa cha binadamu ambacho kinaweza kutambua mema na mabaya.
  (III) Zaidi ya vichekesho hivyo vyote, tendo la ndoa kati ya Adamu na Eva vilisharuhusiwa kwao kama tunavyosoma katika Mwanzo 1:28. Yaani walipata ruhusa ya kufanya kitendo hicho hata kabla ya dhambi yao katika sura ya 3:6-7; wanapoonekana wana kosa.
  Wao walifunganishwa ndoa na Mungu mwenyewe pale aliposema katika sura 1:28. “Zaeni Mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha, “Jiulize tu; ndugu Kanyoto. Jiulize kidogo tu. Wangezaaje bila kuruhusiwa na tendo la ndoa?
  Basi walisharuhusiwa, hivyo kulifanya kusingekuwa haramu ya laana kubwa kama waliyopewa.
  Basi ni wazi tunda halikuwa tendo la ndoa maana ilishakuwa halali kwao kama bibi na bwana. Basi walifanya kitu kingine, ndicho kuchuma na kula tunda ambalo nimekwisha kulieleza; NI ULE UFALME NA MADARAKA YA KIAKILI ili wawe huru zaidi au sawa na Mungu mwenyewe.
  Ndipo hao watu walitambuana kuwa ni watu wawili wa jinsia tofauti. Mwandishi hafichi; ila anasema, japokuwa walikuwa uchi, hawakuona haya yoyote. Hilo lisome kwenye Mwanzo 2:25; sura ambayo imetangulia hiyo ya 3 inayosimulia dhambi ya kula tunda lililokatazwa.
  Nimalize jibu kwa Angalia; nakufahamu tafsiri ya kwamba Adamu na Eva walifanya tendo la ndoa hali ambayo inachochewa na maelezo kwamba waliona haya; wakashona majani na kujifanyia nguo.
  Tafsiri hii iache kwani si sahihi kwa sababu haioani na maelezo yaliyotangulia; na zaidi ya hayo, inapotoshwa sababu ya akina Adamu na Eva kuona haya na kujifanyia nyuo za majani.
  Ukweli ni kwamba kutokana na kuvunja uhusiano wao na Mungu, usawa ulikuwapo kati yao ulivurungika pia. Kwa hiyo wakaona tofauti ya kijinsia kwa kiwango cha juu hali yao kuwa wadogo sana mbele ya Mungu, wanaionja kwa kipimo kingine sasa.
  Basi wanajisikia uchi wao kwa wao ndio maana wanajifanyia nguo za majani; na wanajisikia uchi mwingine mbele ya Mungu. Yaani kukosa heshima na hadhi mbele yake Mungu mwenye haki na mapendo na ndipo wanajificha kati ya miti ya bustani.
  Ndugu Kanyoto; hilo liwe wazi kuwa mkosefu hujisikia uchi mbele ya Mungu na watu.
  Mkosefu yeyote hujisikia kisaikolojia yuko uchi mbele ya wengine wasio na hatia.
  Fikiria inakuwaje baada ya mtu kushikwa wizi au mtu kwa mtu mwingine. Unaona mtu yule anaonja kabisa kwamba bila shaka watu wengine wote wanamfahamu na yeye kihadhi, ameshuka; amekuwa mtupu; hana kitu cha kumhifadhi.
  Kumbe tukirudi tena katika tatizo hilo la Adamu na Eva, hapo kabla uhusiano wao haujavurugwa; ule uhusiano na Mungu. Wao walionja usawa kamili kati yao ndiyo maana Adamu hakujisikia vibaya kuwa na jinsia nyingine tofauti palepale au Eva ndivyo alivyoweza kuhimili kujisikia vizuri mbele ya Adamu bila ya kujihifadhi kwa nguo yoyote.
  Kwa sababu hiyo, hawakuoneana haya na kuhitaji nguo yoyote. Lakini baada ya uhusiano wao kuvurugwa, wanaonja tofauti zao kwa sababu ya ubinafsi na kwa sababu ya kuteremka hadhi na jitihada za kujirejeshea usawa kati yao; zinakuwa ndiko kujishonea nguo zilizolingana na majani; lakini wapi walishakuwa wamechelewa.
  Mtengano kati ya Adamu na Eva kueleza unajidhihirisha katika jibu la Adamu na ksema kwa ubaguzi, na kwa kumtenga mkewe kwa kusema, “ni huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nani, ndiye aliyenipa matunda ya mti huo; nikala.”
  Maana yake, Adamu anamuona Eva sasa kama mtu tu; aliyeletwa pale; si mwenzi wake mshirika. Basi, uchi wa akina Adamu na Eva ndiyo hayo yanayoendela mpaka leo tunapobaguana kijinsia pale ambapo wanaume, watoto wa Adam wanapoendelea kuwaona wanawake kama watu walioletwa na kama watu ambao wamepewa tu wewe pamoja nao lakini si wenzi wao halisi,
  Haya ndugu Kanyoto tusitamani ufalme wa kiakili au madaraka halisi ya kiakili bila kumruhusu atutawale kwa enzi yake madhara yake ni makubwa kwa sasa hivi , wanaume na wanawake sisi tu sawa kwa asili yetu na kwa sababu hiyo hakuna sababu ya kubaguana .
  Maelezo haya yametolewa kutoka http://kiongozi.tripod.com/makalamc2.html

 71. Mpendwa Haule!!

  Mw 2:17 “walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika” Je mti huu ndio mti huu wa Mw3:3 “Lakini, matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa”???

  Nasubiri kutoka kwako.

  Ubarikiwe

 72. Wapendwa katika Kristo,

  Shalom!

  Katika kuliangalia swali hili, jambo la kwanza nililoliona ni Nguvu ya Mapokeo. Nikaiona jinsi ilivyotuweka kifungoni! Yaani nikaliona kanisa likisimama katika nafasi ya Hawa, nalo limekutana tena na yule Nyoka, kwa werevu na umahiri mkubwa Nyoka akalitafsiria tena kanisa, kuwa Hawa alikula kutoka ule mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya; na akaliaminisha kanisa kuwa Hawa alijiongezea maneno yake mwenyewe juu ya yale waliyoambiwa na Mungu, yaani aliongopa! Nalo kanisa limedumu katika fundisho hilo la Uongo kwa karne zote likirithishana kizazi kwenda kwa kizazi; ‘tukidumu katika fundisho hilo’!

  Lakini Maandiko yako wazi kuhusu jambo hilo. Kanisa, kama lingeondokana na tabia ya kutokumtegemea Roho Mtakatifu katika uongozi wake’ lisinge ukubali uongo huo na hivyo kuikosa maana zaidi jambo hilo!

  Nimezisoma post zilizotangulia, labda ninukuu baadhi ya vifungu kutoka humo ili kujenga msingi wa ninachotaka kuongea. Nikimnukuu Ev. Peter John Paul, yeye anasema: “Kwa hiyo jibu la kawaida bila ya kufuatilia ufunuo wa kilindi wa Neno la Mungu, ni kwamba, Mwanamke alitwaa tunda katika mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa sababu mti ambao nyoka alishikia bango na kupigia kampeni kwa nguvu na akili zake zote ili kuhakikisha mwanamke anakula ulikuwa ule wa ujuzi wa mema na mabaya.” Wazo hili ndilo linalotawala ufahamu wetu sote, lakini hii si kweli ya ki Maandiko!

  Hebu twende sote hadi pale Mwanzo 2: 9 na tuitazame ile miti tofauti iliyokuwepo mle bustanini. “…Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya” Bila shaka, ile miti ya kufaa kuliwa ilikuwa kama alivyoitaja mwinjilisti Peter John Paul. Halafu kulikuwa na Mti wa Uzima; Bwana Yesu alikuwa ndiye Mti huu wa Uzima. Ufu 22:14 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima.” Mti wa tatu ulikuwa ni ule Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya. Mti huu ulikuwa ni Lucifer ambaye sasa alikuwa adui wa Mungu. Ezk 28:13 “..ulikuwa ndani ya bustani ya Edeni (akizungumzia mfalme wa Tiro – Lucifer)’ kifungu cha 17 “..nimekutupa chini…” Pia ulikuwapo mti mwingine Edeni, kama tunavyosoma katika mwanzo 3:3 “Lakini, matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa”. Mti huu unaonekana ni tofauti na ule Mti wa Uzima (Kristo), maana mti huu ilikuwa ni kifo hata kwa kuugusa tu!.

  Ndipo sasa tumeona hiyo miti minne iliyokuwemo katika bustani ya Edeni (wengi wa wahubiri huuchukulia huu mti wa nne kuwa ndio ule wa tatu ule wa ‘Ujuzi wa Mema na Mabaya’ na hivyo kubaki na miti mitatu tu jambo ambalo si sahihi. Nenda polepole utaona iko minne; kwanza katikati ya bustani tulielezwa ule mmoja ule wa ‘Uzima’ na sasa tunaoneshwa mwingine tena katikati ya bustani hivyo miti iliyokuwa katikati ya bustani sasa twajua ni miwili.

  Hiyo ndiyo miti minne iliyochipushwa bustanini; kwanza ile ya kuliwa – pili ule Mti wa Uzima (Kristo), tatu ule wa ‘Ujuzi wa Mema na Mabaya’ (Lucifer) na nne ule Mti wa Katikati, huo usiotakiwa hata kuguswa. Hilo ndilo Fundisho la Biblia katika uwazi tuliowekewa hapo. Kwa hiyo tukiuondoa ule ‘utando wa mapokeo’ waweza kuyaona hayo kama yalivyo, na ndipo itakuwa rahisi kusonga mbele tukiuendea Wokovu Kamili. Kwani kizazi chetu, ndicho kinachosubiri kunyakuliwa, nayo NGUVU ya kutuinua juu imo ndani ya Neno lililokamili na si NENO/MAPOKEO, mchanganyiko huu hauwezi kukuinua, kwani dhamira ya roho wa mapokeo ni kutujaza mitafaruku na uzito zaidi wa dhambi!!!

  Mbarikiwe nyoote!

 73. Bwana apewe sifa kweli swali hili ni ngumu kwa kujibu.kweli maandiko matakatifu kama vile Biblia inasema usiongeze wala kupunguza wapendwa tukamate vile inapoandikwa kwa IMANI juu ya kukaza safari yetu ya kwenda Mbinguni Na zaidi tuongozwe na msaidizi wetu ndio Roho Mutakatifu. Amina

 74. Ni mti upi mwanamke alitwaa tunda?

  Halellujah! Glory to God, the Lord Jesus Christ. Amen!

  Kwa yeyote aliyetuma swali hili kwenye Mjadala, BWANA akubariki na kukulinda. Sijawahi kuingia kwenye mjadala wowote kwenye site hii, lakini sasa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia kuingia, kwa neema yake. Nimeona swali hili nikafurahi sana, lakini nikakumbuka kwamba siyo swali jepesi la kukimbilia, nisije nikanaswa katika mtego wa kutoa majibu mepesi kwa swali zito na muhimu kama hili. Kwani ninafahamu kuwa watu wengi wakiwemo wahubiri wameliendea swali hili bila ufunuo wa kiroho wa Neno la Mungu wakaishia kwenye mwisho wenye utata.

  Kiujumla, kulingana na kitabu cha Mwanzo 2:9, BWANA Mungu alichipusha katika ardhi miti ya aina tatu ambayo imenenwa kama ifuatavyo: “BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.”

  Aina ya kwanza ya miti ilikuwa ile inayotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa. Aina ya pili ni ule mti wa uzima uliokuwa katikati ya bustani. Aina ya tatu ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

  Baada ya kuchipusha miti hiyo katika bustani ya Edeni, Mungu alimfundisha Adamu aliyekuwa amemuumba kwa sura yake na kwa mfano wake, jinsi ya kutenda na kutembea katikati ya aina hizo tatu za miti aliyokuwa ameichipusha katika bustani hiyo. Akamwagiza akisema: “…Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika” (Mwanzo 3:16).

  Kwa maana hiyo Adamu alipaswa kula matunda ya kila mti wa bustani (yaani zile aina mbili ambazo ni miti ya kawaida inayofaa kwa chakula, na ule mti wa uzima). Lakini hakupaswa kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya (ile aina ya tatu) kwa sababu agizo lilikuwa kwamba siku akila matunda ya mti huo wa ujuzi wa mema na mabaya, angekufa hakika.

  Baadaye mkewe Adamu alipochomolewa ubavuni mwake alipaswa kuishi kwa kufuata maagizo hayo kwa moyo wake wote kama yalivyopokelewa na mumewe kutoka kwa BWANA Mungu.

  Kwa hiyo jibu la kawaida bila ya kufuatilia ufunuo wa kilindi wa Neno la Mungu, ni kwamba, Mwanamke alitwaa tunda katika mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa sababu mti ambao nyoka alishikia bango na kupigia kampeni kwa nguvu na akili zake zote ili kuhakikisha mwanamke anakula ulikuwa ule wa ujuzi wa mema na mabaya.

  Katika kitabu cha Mwanzo 3:1-6 tunasoma: “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke. Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.” …….

  Nisiwachoshe, kwa leo nitaishia hapa nitoe nafasi kwa wachangiaji wengine, lakini niliyonayo nitayaendeleza baadaye.

  Shalom!
  Ev. Peter John Paul

 75. Ukiangali MTI unaozungumziwa hapa , utakuta ni ule ule mti amboa katika HEZEKIEL 28 umeelezewa kama nyota ya asubuhi…yaani yule aliyeasi MBINGUNI, SHETANI.. maana alikuwapo tayari wakati MUNGU anafanya uumbaji wa NCHI na MBINGU..
  UTAONA kwamba alipomaliza uumbaji wa mwanaume na mwanamke, aliwapa mamlaka juu ya vyote Duniani…
  ila ANGALIZO lilikuwa ‘usile kati ya matunda ya MTI ULE’ maana aliwaasa wasishirikiane na YULE JAMAA ALIYEASI au moja ya matunda ya aina yake.

  IBILISI ikawa akamrubuni mwanamke washirikiane kwamba hawezi kufa, na yeye akamshirikisha mwanaume kuwa ushirika ule hauna madhara ya kifo..NDIPO WALIPOKUWA WAMEKULA LILE TUNDA….

  NADHANI INATOSHA…

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s