SHUSHO AIBUKA NA TUZO KWA MARA NYINGINE,”LISEME” WA SARAH K, NAO WABEBA TUZO YA MWAKA.


Pastor Uche Agu muongozaji wa sherehe hizo akimuombea maisha marefu na yenye baraka mwimbaji Ruben Kigame.

Christina Shusho mwimbaji nyota wa muziki wa gospel Tanzania jioni ya tarehe 28 ameibuka tena kidedea kwenye tuzo za groove zinazotolewa kila mwaka nchini Kenya kupitia kipengele cha mwanamuziki bora wa mwaka kutoka Tanzania tuzo ambayo alishinda mwaka jana akiwapita waimbaji wenzake waliopendekezwa kwenye kipengele hicho akiwemo Rose Muhando,Bahati Bukuku,Neema Mwaipopo pamoja na Boniface Mwaitege.

Sherehe za utolewaji wa tuzo hizo ziliongozwa na pastor Uche Agu mwimbaji wa Joyous pamoja na mwanadada Kambua ambao walikuwa wakiweka utani wa hapa na pale na kuchangamsha mamia ya wakazi wa Kenya waliojazana katika ukumbi wa kanisa la Baptist jijini Nairobi.wimbo ”LISEME” wa mwanamama Sara Kiarie ama Sarah K umechukua tuzo ya wimbo bora wa kuabudu wa mwaka,huku mwanadada Emmy Kosgei akiondoka na tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na wimbo wake wa Ololo ukimpatia tuzo ya wimbo bora wa mwaka kwa upande wa eneo la Rift Valley.

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa injili nchini Kenya Ruben Kigame alipewa tuzo maalumu kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki wa gospel nchini humo. Mwimbaji huyo hakuwepo kwenye tuzo hizo kwakuwa yupo safarini nchini Marekani, ingawa tuzo yake alikabidhiwa kabla hajaondoka ambapo ilionyeshwa video fupi kutoka kwake akishukuru kwa tuzo hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasifu waandaaji kwa kuzifanya tuzo hizo kuwa bora. Pia alitoa ushuhuda wake mfupi wa maisha yake kabla hajaokoka na hata alipookoka,aliweka bayana kwamba baada ya mkewe kufariki alifikiria kwamba asingeweza kuimba tena lakini Mungu ni mkuu akafanikiwa kutoa album yake ya ”TULIA”.
Baada ya video hiyo pastor Uche aliwanyanyua watu na kuongoza sala fupi juu ya Ruben Kigame akimuombea maisha marefu na baraka.

Mwanadada Neema kulia akiimba na mwenzie wimbo Wema na fadhili wa Ruben Kigame maalumu kwa ajili ya mwimbaji huyo.

Lakini kama kuna tuzo ambayo ilishangaza na kutoa kama surprise si kwa waimbaji pekee bali hata kwa umati uliohudhuria,ni baada ya mwanakaka Ekko Dydda kuibuka mwimbaji bora wa kiume wa mwaka tuzo ambayo watu walio wengi walitegemea Juliani ndiye angeshinda kwani hata mshindi mwenyewe alikiri hilo wakati wa kushukuru.Kwakuwa tuzo hiyo ndiyo ilikuwa ikikamilisha tuzo hizo ikamaanisha kwamba Juliani licha ya kuwemo kwenye category tano hakupata hata moja na kuwaachia majonzi mashabiki wake ambao wameonyesha wazi kutokukubaliana na hilo.

Ekko Dydda akiimba wimbo wake Getto unaompa jina nchini humo.

Tuzo hizo ambazo zilikuwa zikirushwa moja kwa moja na kituo cha KTN pamoja na kwenye mtandao zimesifiwa kwa kuzidisha ubora kila mwaka huku kukiwa hakuna malalamiko ya upendeleo na kuonyesha mfano wa kuigwa kwa tuzo nyinginezo ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa zawadi,pia waimbaji wa nchi hiyo waliweza kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji.pastor Uche alihitimisha ngwe hiyo kwa wimbo wake My God is good.

ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA TUKIO HILO KAMA ZILIVYOTOLEWA NA WAANDAAJI WA TUKIO HILO GROOVE AWARDS 2012.TUTAKULETEA PICHA NYINGINE ZIKIPATIKANA.

Hapa wakati jukwaa likiwekwa sawa siku ya Alhamisi.
Mambo yakiwa sawia eneo la zuria jekundu (red carpet).


Umati wa watu ukiwa eneo la Red carpet kwa viburudisho wakisubiri kuingia ukumbini hii leo.
Jukwaa likiwa sawa na tukio likiendelea.
Mwanadada Kambua akimsifu Mungu.pia alijishindia tuzo ya mtunzi bora wa nyimbo wa mwaka.
Ekko Daydda mwimbaji bora wa kiume wa mwaka akiwa haamini huku waimbaji wenzake wakifurahi pamoja naye.


Kundi la MOG wakiwajibika jukwaani.
Juliani akimsifu Mungu jukwaani.
DK na Jimmy Gait wakicheza style ya furi furi dance ambayo imewapa tuzo.

Habari na Gospel Kitaa

Advertisements

One thought on “SHUSHO AIBUKA NA TUZO KWA MARA NYINGINE,”LISEME” WA SARAH K, NAO WABEBA TUZO YA MWAKA.

  1. 2seme 2 ukweli dada Christina anawito na uwimbaji. yani nyimbo zke zinakuvuta krb na Mungu. na vilevile nyimbo zk nyingi anachukua maandiko kwenye Biblia. tofauti na waimbaji wengine wanachukua maneno ya mitaani. Mungu akubariki dada.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s