Lugha yako ya maombi ni ipi?

Maombi ya muhitaji yananoga. Wakati wa shida hata wasiofuatilia Mungu watamkumkubuka na kuita jina lake. Kuna lugha nyingi kwenye maombi, mfano wengine wanaimba, wengine husikiliza muziki wa kuabudu, wengine hunena kwa lugha, wengine wanaenda sehemu iliyotulia nje kwenye fukwe za bahari, vijito, milima ili tu waweze kuongea na Mungu hiyo yote ni jinsi ya kuingia, jinsi ya kutaka kusikika na Mungu ni Lugha ya maombi.

Kuna mambo ambayo hatuwezi kwa nguvu zetu, hatuwezi kufanya lolote, Mtunzi wa zaburi aliandika “Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu” Zaburi 42:8

Siku ya Mateso yangu nitakuita, kwa maana utaniitikia” Zaburi 86:7

Unapokuwa huna tumaini, umechoka sana ndio wakati wa kupaza sauti yako kwa Mungu na kumuita akusaidie. Imani yako itakuwa na kuendelea na Mungu atatengeneza nafasi kwako ya kukutana na nguvu zake zitakazokutana na tatizo lako kwa jinsi ambavyo hukutegemea.

Kama watoto wa Mungu wetu aliye hai, inabidi maombi yawe ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, Maombi ni mahusiano yako na Mungu, Maombi ni yanakupa nguvu ya kuingia na kupita mahali ambapo ni pagumu kwa akili za mwanadamu. Maombi ni daraja, Maombi yana faida kwetu.

Una jambo gani linalokushinda? Ni gumu kiasi gani? Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu.


Advertisements

12 thoughts on “Lugha yako ya maombi ni ipi?

 1. Ubarikiwe dada Mary,

  Kama ulivyosema, maombi ni maisha Muumini, na la msingi katika hilo ni kuwasiliana na Muumba wako.Njia ya kuwasiliana naye inaweza kutofuatiana mno kwa kila mtoto wa Mungu, kama vile watoto wa familia moja ambavyo wanaweza kuwasiliana na wazazi wao kwa lugha tofauti tofauti kutoka na umri wao na jinsi walivyouumbwa na wazazi wao wakaelewa wanasema nini, ndivyo wana Mungu wanavyoweza kuwasiliana na Baba yao wa Mbinguni kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
  Katika maisha yangu ya kutembea na Bwana nimekua na lugha na njia mbali za kuzungumza na Bwana, nyakati ziliponiruhusu nilikuwa ni mtu wa maombi alfajiri na mapema….na nilinunua saa ya alarm kuniamsha, kuna nyakati pia nilikuwa mtu wa usiku…..! Muda mzuri ulikuwa ni baada ya wanafamilia kulala niliiigia katika kipindi cha kusoma maneno ya Mungu ambayo yaliishia katika maombi….na maombi haya yalikuwa si ya kukaa mahali pamoja tu bali kutembea tembea na kuzunguka kwa kutembea nikizungumza na Bwana….Kuna nyakati pia vyote vilishindikana muda wangu mzuri ulikuwa ndani ya gari……foleni kwangu mimi ilitumika mno kuwa maombini……..na sasa hivi muda wangu mzuri mahali nilipo ni kwenda Park…..na Makatba….mahali penye utulivu ili Kusema na Bwana…..

  Lugha za maombi Je? Nazo zimekuwa zibadilika kutoka na maombi yenyewe……Nimelia mbele za Bwana……Nimepiga Kelele mbele yake……Nimelalamika nilipoona kama mambo yananiendea kombo…..Nimekuwa kimya kwa kutafakari nikizungumza naye……Nimenena kwa Lugha…….Nimecheka na kufurahi kwa maombi kwa kuzikumbuka ahadi zake zilizo katika Biblia kwa yale…….Hivyo lugha yangu ya maombi imekuwa ikibadilikabadilika kutokana maombi yenyewe na nyakati za Kiroho nazopitia…….La msingi ni kutopoteza tu yale Mawasiliano yenu ya ajabu ambayo tumepewa kuwasiliana na Muumba wetu…..!

 2. MPONDA TAG CHURCH
  MAOMBI MAALUMU-TAREHE 02 MPAKA 05 MAY 2012
  1. MUNGU ALIONGEZE KUSANYIKO LAKE HAPA MPONDA
  A. KIROHO
  B. KIIDADI
  C. KIUCHUMI

  2. MUNGU AFUNGUE MILANGO KUPATA SHILINGI MILIONI MIA MOJA NA ISHIRINI KWA AJILI YA GHARAMA ZA UJENZI WA JENGO KUBWA LA KANISA

  3. NEEMA YA WOKOVU IWAFIKIE WAKAZI WA HAPA MPONDA –MAJIRANI NA NDUGU ZETU NAO WAOKOLEWE NA KUMJIA KRISTO KATIKA MAISHA YAO

  4. MUNGU AWASAIDIE WASHIRIKA WOTE WAENDELEE KUSIMAMA KATIKA NEEMA YA WOKOVU MPAKA SIKU YA BWANA ILIYOKARIBU KUUJILIA ULIMWENGU WOTE

  5. ROHO WA MUNGU ATAWALE NA KUATAMIA KUSANYIKO LAKE LOTE ILI KARAMA –TALANTA NA VIPAWA MBALI MBALI VIFANYE KAZI KWA UTUKUFU WAKE

 3. MAOMBI NI UHAI KWA KILA ANAYEMWAMINI MUNGU NA PIA JAMBO LA ZIADA NI KUJUA KUWA TUNAPOFUNGA NI KUJINYENYEKEZA MBELE YA MUNGU AHUSIKE NA MAOMBI YETU NA SIYO KUMLAZIMISHA ATENDE KAMA TUPENDAVYO SISI KWANI HAJA ZETU ZINATAKIWA ZIMRUDISHIE MUNGU UTUKUFU NA SIO MATAKWA YETU WANADAMU

 4. Mungu awabariki jamani. Namshukuru Mungu kwa ajili yenu, Dinam, ni vizuri kuwa na kiu ya maombi, ni vizuri zaidi kama maombi yakiwa chakula chetu, kila wakati unapojisikia hata usipojisikia unaomba tu. Wakati mwingine ukiwa kwa gari unaendesha au daladala kwenye foleni unaweza kujiunganisha kwenye maombi kama dada Amina ulivyosema unapenda nyimbo za kuabudu unaweza kusikiliza wakati wowote hauchoki ila zinakufanya kuwa karibu na uwepo wa Mungu.

  Siyo lazima utumie nguvu, kawaida tu kama unaburudika. Siyo wakati wa shida tu, hata wakati wa amani.

  Kuna somo niliwahi kuliweka hapa kwa ufupi https://strictlygospel.wordpress.com/2009/05/08/maombi-ya-asubuhi-na-faida-zake-i/

  NItaweka part 2 yake nikimaliza kutype. Mungu awabariki, Julian salam kwa Mchungaji ninawakumbuka. Barikiweni sana!

 5. mie hw napenda sn nyimbo za kuabudu, hazinichoshi. wkt natafuta uwepo wa Mungu. mi naona hayo maombi ya alfajiri angepanga cku aweke 2 ili 2nufaike wote. au cyo dada Mary

 6. Bwana Yesu asifiwe dada Mary naomba na mimi unitumie faida ya maombi ya alfajiri tafadhali nina kiu na hayo maombi. Mungu akubariki

 7. Mimi nikiamka asubuhi ninazunguka nyumba yangu na kunena kwa lugha, lakini nasikia uwepo wa Mungu zaidi nikiwa nje ya nyumbani, uwani na nikitembea barabarani huku naomba.

 8. Dada Mary kuna siku ulifundisha faida ya maombi ya Alfajiri ulipokuja kwenye huduma Kisii. Napenda kusema yamenijenga sana naomba unitumie mafundisho mengine kuhusu maombi. Mungu akubariki

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s